Mali ya Dunia na Ulimbikizaji kwa Uroho.
935. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk. 173:
“Kwa yeyote yule ambaye siku zake mbili za maisha zikawa sawa (hakuna maendeleo ya kiroho) kwa hakika yupo katika hasara.”
936. Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 311:
“Mfano wa dunia hii ni sawa na maji ya bahari. Kiasi chochote kile anywacho mwenye kiu kutoka bahari, kiu chake kitaendelea kuongezeka hadi kika kumuua.”
937. Al Imam Muhammad at-Taqi a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 368:
“Watu wanaheshimiwa humu duniani kwa kuwa na mali na Akhera watu wataheshimiwa kwa kuwa na matendo mema.”
938. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Makusanyo ya Waram:
“Maangamizo ya wanawake wangu yako katika mambo mawili:
• Dhahabu na mavazi yasiyo ya heshima;
Na maangamizo ya wanaume wafuasi wangu yapo katika kuiacha elimu na kukusanya na kulimbikiza mali.”