read

Matamanio na Tamaa Zisizo Halali.

928. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Kafi, J. 2, Uk. 79:

“Baada yangu mimi, ninawahofia umma wangu katika vitu vitatu:
1. Upotofu baada ya kuelimika,

2. matamanio yanayo potosha na

3. Tamaa ya tumbo na sehemu za siri.”

929. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Al-Kafi, J. 2, Uk. 80:

“Hakuna ‘ibada ya Allah swt iliyo na thamani zaidi kuliko usafi, uhalisi wa tumbo la mtu na sehemu zake za siri kutokana na matamanio au tamaa.”

930. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Makarim-ul- Akhlaq, 429 :

“Kwa mtu ambaye anakuwa na matamanio na maovu yanapokuwa daima yako tayari na yeye anayaepukana nayo kwa sababu ya hofu ya Allah swt, basi Allah swt atamharamishia moto wa Jahannam na atamhakikishia kuwa hatakuwa na tishio kubwa ….”

931. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: Al-Muhajjat-ul-Baidha

“Yeyote yule anayejinusuru na maovu ya tumbo, ulimi, na sehemu zake za siri basi kwa hakika amejinusuru kutoka madhambi.”

932. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha U. 553:

“Kumbuka (wakati wa kutenda dhambi), kuwa raha zinapotea, wakati matokeo (maovu na mateso) yake yanabakia.”

933. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 5, Uk. 548:

“Yeyote yule anayembusu kijana wa kiume kwa matamanio ya kitamaa, basi Allah swt atamuadhidhibisha na kumchapa kwa miale ya moto.”

934. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 79:

“Je kuna jitihada gani iliyo afadhali kuliko usahihi wa tumbo na wa sehemu za siri.”