read

Mtarajiwa Al-Mahdii A.S. aa Utawala Wake wa Haki.

970. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Sunan Abi Daud, J. 4, Uk. 107;

“Al Mahdi anatokana na kizazi changu kutokea kwa wana wa Fatma Bi Zahra a.s.1

971. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 129:

“Mwenye furaha ni yule ambaye ataweza kumfikia Al-Qaim a.s. wa Ahlul Bayt a.s. na kumfuata kabla ya kudhihiri kwake. Mtu huyu atawapenda wapenzi wa Imam Al Mahdi a.s. na atawachukia maadui wake, na atakubalia uongozi wa Maimam a.s. kabla ya kudhihiri kwake. Na hawa ndio marafiki zangu, na kwa hakika hawa ni watu halisi katika umma wangu ambao mimi ninawatukuza sana.”

972. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Musannif, J. 11 Uk. 371:

“Allah swt atamwinua mtu mmoja kutokana na kizazi changu, kutokea Ahlul Bayt a.s. yangu, kwa kuja kwake ardhi hii itajazwa kwa uadilifu kama vile ilivyojaa sasa hivi kwa dhuluma na kukosekana kwa haki.”

973. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Musnad Ahmad ibn Hanbal, J. 2, Uk. 83 na J. 3, Uk. 446 na J. 4, Uk. 96; Sahih Bukhari, J. 5, Uk. 13 na Sahih Muslim, J. 6, Uk. 21, na No. 1849 ya Riwaya–25 na Marajeo mengine ambayo yameelezwa na Wanazuoni wa Kisunni:

“Mtu yeyote atakayekufa bila kumjua Imam wa Zama zake (Imam wa zama zetu hizi ni Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s.) Basi atakuwa amekufa kama vile walivyo kuwa wakifa katika zama za Ujahiliyyah.”

974. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 316:

“Atakapo dhihiri Al Qaim a.s., basi mbingu itanyesha mvua, ardhi itaotesha miti yake, uadui utakwisha kutoka mioyo ya waja (ili kwamba wote waweze kuishi kwa amani na mapenzi ya kindugu), na wawindaji na wanyama wataendelea kuishi kwa amani kwa pamoja…………”

975. Abil Jarudi amesema, Al-Kafi, J. 1, Uk. 34:

“ Mimi nilimwuliza Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. iwapo yeye alikuwa akijua kuhusu mapenzi yangu na utiifu wangu kwake, naye alinijibu kuwa alikuwa akijua. Nami nikamwambia kuwa nilikuwa na swala nililokuwa nikitaka kumwuliza ili aweze kunijibu, kwa sababu mimi nilikuwa kipofu na nilikua nikitembea kwa uchache sana, na hivyo nilikuwa siwezi kumtembelea kila mara. Naye alinitaka mimi nimwulize swala nililokuwa nikitaka kumwuliza. Hivyo mimi nilimwomba anijulishe dini au madhehebu yeye na Ahlul Bayt a.s. wanayoifuata na ambayo inapendwa na Allah swt, ili nami niweze kufanya ‘ibada ya Allah swt kwa mujibu wa madhehebu hayo.”

Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. alinijibu:
“Kwa hakika wewe umeniuliza swala kubwa sana, ingawaje umeniuliza kwa kifupi sana. Kwa kiapo cha Allah swt mimi ninakujibu kuhusu dini yangu na dini ya mababu zangu kupitia huyo tunavyomwabudu Allah swt. Nayo ni:
‘Kwa kukiri imani yetu kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa ni Allah swt, na kwamba Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume wa Allah swt, na kusadiki kuwa chochote kile kilichomteremkia yeye (Qur'an Tukufu) ni kutoka kwa Allah swt, na kuwa na mapenzi (yetu) ya wapenzi wetu na watiifu kwetu (Ahlul Bayt a.s.) na kuwachukia maadui wetu, kujisalimisha kwa njia yetu, na kumsuburi Al Qaim a.s. (Imam wa kumi na mbili ambaye atadhihiri pale itakapotokea amri ya Allah swt), na kutaka (kudumisha yale yaliyofaradhishwa na mambo yaliyo halalishwa) na kwa kuwa mcha Allah swt halisi (kwa kujiepusha na yale yote ambayo ni haramu).

976. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Yaumul-Khalas, Uk. 269:

“Atakapo dhihiri Al Qaim a.s., basi mikono yake itakuwa juu ya vichwa vya waumini, naye atawapa maendeleo ya kiakili na kukamilisha subira yao na kile wanacho kiangalia mbele. Baada ya hapo Allah swt ataongezea nuru yao macho na uwezo mkubwa wa kusikiliza ili kwamba kamwe kusitokezee vizuizi baina yao na Al Qaim a.s. pale atakapo amua kuongea nao, na watakapomsikiliza, wataweza kumwona ilhali atakuwa mahala pake.”

977. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 391:

“Wakati wa Al Qaim a.s. muumin atakaye kuwa mashariki ataweza kumwona muumin mwenzake aliye magharibi, na vivyo hivyo muumin aliye magharibi ataweza kumwona muumini aliye mashariki.

Tanbih.
Ndugu msomaji ! Kwa hakika sasa hivi tunayo ala za mawasiliano mbalimbali kama vile Satellite, Television yafuatayo ambayo yanaweza kuwa yenye manufaa makubwa kwetu ili kuwaza kuangalia vyema na kuelewa hiyo riwaya vitu ambavyo havikuwapo wakati maneno matukufu ya riwaya hiyo yalipokuwa yakisemwa.

978. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk. 7:

“Huyu Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. atakuwapo mahala ambapo ni karibu na Al Ka’aba Tukufu baina ya nguzo na nafasi ya kusimamia ya Mtume Ibahim a.s. na atatoa mwito, atakapo kuwa akisema:
‘Enyi watu wangu hasa ambao Allah swt amewawekeni kwa kuwatayarisha nyinyi kwa furaha ya kudhihiri kwangu juu ya ardhi hii ! Njooni kwangu kwa utiifu. Na kwa hakika kauli hii itawafikia wale wote watakapokuwa na hata kama watakuwa vitandani wakiwa mashariki ya ardhi au magharibi yake. Na watamsikiliza kwa mwito wake huo mmoja tu ambao utafikia kila sikio la kila mtu, nao watajitayarisha kwa ajili ya kuja kwake. Kwa hakika haitawachukua muda wowote isipokuwa pumzi tu kiasi kidogo kukusanyika hapo baina ya mlingoti na nafasi ya kusimama ya Mtume Mtume Ibahim a.s., wakimwitikia Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s.’”

979. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimwambia mfuasi wake aliyekuwa halisi, Mufadhdhal, mambo fulani kutokea kisa cha Al Imam Muhammad al-Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. na kudhihiri kwake,

“Ewe Mufadhdhal ! Waambie wafuasi wetu habari za Al-Mahdi ili wasiwe na shaka katika Dini yao.” Bihar-ul-Anwaar, J. 53, Uk. 6.

980. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s., amesema Kamal-ud-Din, Uk. 445:

“Mimi ni Al Mahdi na mimi ni yule ambaye bado nipo hai na ambaye nitaijaza ulimwengu kwa haki na uadilifu kama vile ilivyojazwa kwa maovu na dhuluma.

Kwa hakika ardhi haitabakia bila ya kuwa na mbashiri, na watu kamwe hawataisha bila ya kuwa na kiongozi. Na hii ni amana na hivyo msiwaambie wote wale Waislam wenzenu isipokuwa wawe ni watu wa Allah swt (wawe katika haki).”

981. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. amesema, Kamal-ud-Din, Uk. 484:

“Kwa mambo yanayotokea kwa Waislam, murejee katika riwaya zetu, ( yaani Wanazuoni au Ma’ulamaa), kwa sababu wao ndio wawakilishi wangu kwenu na mimi ni Hujjatullah juu yao.”

982. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. alimwandikia barua Sheikh Al Mufid, Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk. 175:

“Sisi tunaelewa hali yako na mazingara yako na hakuna jambo lolote lako lililojificha kwetu sisi.”

983. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. alimwandikia barua Sheikh Al Mufid, Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk. 175:

“Si kwamba sisi hatukujali wewe au tumekusahau, kwa sababu kama ingekuwa hivyo, matatizo na balaa zingekuwa zimekuondokea wewe na maadui wako wangekuwa wameisha kumaliza. Hivyo, muogope Allah swt na uwe mtiifu kwake, asifiwe Allah Jalli Jalalahu.”

Dua :
Tunamwomba Allah swt aharakishe kudhihiri kwa Imam wetu wa kumi na mbili Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. ili aweze kudumisha usawa, ukweli, na haki katika ulimwengu mzima. Amina.

  • 1. Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s. yeye ni Imam wa kumi na mbili katika mfululizo wa Imam ambao wanaaminiwa na Mashi’a. Kwa hakika Imam sio kwamba ni Mashi’a tu wanafuata Mashi’a ndio wanamfuata kweli kwa sababu wao ndio wanafuata kauli na Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwani Imam Mahdi a.s. yeye ametajwa katika vitabu vyote vya Masunni na Mashi’a na dalili zake zote na maisha yake na dalili za Kudhihiri yametajwa katika vitabu vyote hakuna madhehebu ya katika Islam iwe katika upande wa Masunni au Mashi’a wanaoweza kukana kuwapo kwa Imam Al Mahdi a.s. habari zaidi zinapatikana katika vitabu vya Tarikh vile vile mimi nimekikusanya na kukitarjumu kitabu kimoja kinacho zungumzia Dalili za Qiyamah na kudhihiri kwa Imam Al Mahdi a.s. hivyo msomaji unaweza kutafuta kitabu hicho kikakusaidia na ukajua dalili za Qiyamah na dalili za kudhihiri kwa Imam Al Mahdi a.s. kuhusu maswala ya Imam Mahdi a.s. katika vitabu vya Waislam utavipata usiache kufanya utafiti.