read

Mukhtasari wa Dalili

1. Baghdad itateketezwa kabisa.

2. Basra itazama.

3. Waarabu watatawaliwa na mfalme wa ukoo mmoja tu kwa nguvu.

4. Msikiti wa Borasa (baina ya Baghdad na Kazmain) utadhoofika.

5. Kutakuwa na nchi nyingi za Kiislamu na kutakuwa na soko la kawaida

6. Qum itakuwa ni kitovu cha mafunzo ya Kiislamu, kitakuwa ni kituo kipya kuliko kile cha Najaf (Iraq ). Na hapo ndipo kutakuwa kukitolewa ahkamu za dini.

7. Kutakuwapo na reli kupitia katika nchi za Kiislamu.

8. Azarbaijan itakumbwa na vita.

9. Wanawake watakosa heshima kabisa.

10. Duniani kote kutaenea sheria za kidemokrasia.

11. Kutakithiri kizazi cha wanaharamu.

12. Kutakithiri riba na rushwa.

13. Kuzaliwa kwa wanawake waovu katika familia nzuri.

14. Watu wenye hali ya chini wataweza kujenga majumba makubwa.

15. Watu wema na waaminifu watakuwa wakiomba mauti ili waepukane na maudhi wanayoyapata.

16. Watoto na majahili watapanda juu ya Mimbar, na watajulikana kama khatib.

17. Wanazuoni watajiingiza katika mambo ya dunia.

18. Madhumuni ya kutafuta Elimu itakuwa ni kutaka kutafuta pesa.

19. Badala ya kusalimiana matusi ndiyo yatakayo kuwa yakitumika watu watakapokuwa wakikutana.

20. Watu watatoka katika dini zao kwa sababu ya ulafi wa vitu.

21. Dini ya Kiislamu itakuwa dhaifu.

22. Mambo ya kuingiliana yatakuwa yakifanyika kidhahiri kama vile wafanyavyo wanyama.

23. Wanawake watasuka nywele zao kama nundu za ngamia.

24. Kupatwa kwa mwezi na jua na mitetemeko vitatokea Mashariki na Magharibi na baadaye katika Bara la Arabia

25. Kutakuwa na ongezeko katika kuzaliwa watoto wa kike.

26. Ulawiti na pombe vitakuwa ni vitu vya kawaida.

27. Mitetemeko ya kila mara itaongezeka.

28. Wanawake watakuwa na taasisi zao.

29. Wanawake watafanya kazi pamoja na wanaumme katika kutafuta maisha yao.

30. Usafiri utakuwa wa haraka sana.

31. Kutakuwa na muongezeko wa ajali za njiani.

32. Mavazi yatakuwa mafupi.

33. Mwanamme na Mwanamke watajaribu kuonana sawa kijinsia

34. Kutakuwa na ndoa za kuoa jinsia yake yaani mwanamme atamuoa mwanamme mwenzake na mwanamke atamuoa mwanamke mwenzake (na mambo haya hasa yanatokea katika nchi za Ulaya).

35. Wakazi wa Kufa na Najaf watakuwa wamekaribiana sana.

36. Wakazi wa Makkah na Madina wataongezeka.

37. Hijab itakuwa imepotea (hijab, bubui).

38. Maji yataanza kujaa katika ziwa Sawa.

39. Kutakuwapo na nyota yenye mkia karibu na Capricorn.

40. Watu wengi sana watakufa kwa sababu ya kuenea kwa vita

41. Misikiti na Qur’an itarembeshwa kwa dhahabu.

42. Kutatokea na moto mkubwa sana katika mashariki na utaendelea kuwaka kwa siku saba.Na moto huo utatia khofu kubwa sana kwa mioyo ya watu.

43. Kutakusanyika bendera tofauti tofauti huko Kufa na kusababisha mifarakano mikubwa.

44. Utawala wa Kifalme utakwisha huko Iran

45. Kutatokea na mivurugo katika nchi za Kiaarabu. Kila nyumba ya mwarabu na nchi zote za Kiislamu zitahusishwa humo.

46. Kukosa Imani kutaenea kote.

47. Waislamu wataiga tamaduni na mila za maadui zao.

48. Vifo vya ajali vitaongezeka.

49. Ala za muziki zitaenea kiasi kwamba hakutakuwa na mtu hata mmoja atakayesalimika kwa sauti zao.

50. Watu wataanza kukataa kuwapo kwa Imam Mahdi a.s.

51. Kutaonekana sura katika jua, na sauti zao zitasikika duniani kote.

52. Mwanadamu atafika mwezini.

53. Sufiani atatokezea na kueneza utawala wake wa vitisho.

54. Sayyed Hassan atatokezea huko Iran. Na yeye atafika Multan kwa kupitia Kirman huku akiteka sehemu zote. Yeye atamfikia Imam Mahdi a.s. na kujisalimisha mbele yake.

55. Kutatokezea wazushi wa mtume sitini.

56. Mtume Issa a.s.atateremka kutoka mbinguni.

57. Maafa magonjwa ya kuambukiza na ukame utaenea kote.

58. Nafsi ibn Zakia atauawa katika al- Kaaba (mtu mcha Mungu atauawa katika al-Kaaba

59. Jua litachomoza kutoka Magharibi kwa siku moja.

60. Warusi wataingia Bara la Arabia na watu weupe wataingia Bara la Palestina.Nao baadaye watapambana.

61. Wachina wataingia Bara la Arabia na kusababisha maangamio na maafa ambayo yatakuwa ni mambo ya kawaida.

62. Baadhi ya miji itateketezwa kwa sababu ya maafa na misukosuko.

63. Sauti ya kutisha itasikika kutoka mbinguni.

64. Kutokezea kwa Dajjal.

65. Moto na moshi itakuwa kawaida duniani.

66. Mvua zitatokezea pasipo na misimu yake.

67. Kuongezeka kwa joto katika anga za juu.

68. Kulipuka kwa moto mkubwa katika Aden.

69. Baadhi ya makundi ya wanaume yatakuwa yamegeuka maumbo.

70. Kutatokea na mabadiliko ya ajabu katika sayari ya Capricorn

71. Mkuu wa Dola ya Misri atauawa.

72. Kutakuwapo na mvua ya mfululizo kwa muda wa siku ishirini na nne(24).Dunia nzima itakuwa imejaa michafuko, maafa na maangamizo n.k.

1659. Hadith hii ifuatayo inatuonyesha dhahiri kuwa kuna haja ya kuwapo kwa Imam wa zama na kumtii yeye ni faradhi kwetu sisi,kama vile wanavyoinakili Maimamu wa Kishiah na vile vile Wanazuoni wa Ahli Sunna pia wananakili vivyo hivyo katika vitabu vyao. Hadithi mashuhuri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. inayopokelewa na madhehbu yote ni kama ifuatavyo:

"yeyote yule atakayekufa bila ya kumtambua na kumjua Imam wa zama zake basi mtu huyo atakufa mauti ya ujahili (yaani atakufa kifo cha ukafiri)."

1660. Hadith ya Pili

Madhehebu yote ya Islam kwa pamoja yanaelezea Hadith ifuatayo na ambayo ni uthibitisho wa ukweli wa Kiislamu na vile vile Sahih Bukhari na vitabu vingine vyote vya Hadith pia vinaelezea kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisema:
"Baada yangu watakuwapo Maimamu kumi na wawili ambao watatokana na Maqureish."

1661. Hadith ya Tatu

‘Allamah Syed Jamal ud-Din Muhaddath ambaye ni mwachuoni mkubwa wa Ahli Sunna, anaandika katika kitabu chake Rawdhat ul-Ahbaab kwa kumnakili Sahaba Ja'abir ibn ‘Abdullahi Ansari wakati Allah swt alimfunulia Aya hii Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.:-
"Enyi mlioleta Imani! Mtiini Allah swt na Mtume wake na vile vile mumtiini 'ulil Amr'."

"Basi mimi (anaendelea Bwana Ja’abir) niliuliza "Ewe Mtume wa Allah swt! Sisi tunaelewa Allah swt pamoja na Mtume wake.Lakini jee ni wakina nani hao ambao wanajulikana kama 'ulil Amr" ambao utiifu wao umefaradhishwa kwetu sisi?"

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alitoa majibu haya yafuatayo:
"Wao watakuwa Makhalifa baada yangu na wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib na amfuataye atakuwa ni mwanae Hasan na atamfuatia Hussein na baadaye atafuatia Ali ibn al-Hussein na baadaye Mohammad ibn Ali na anatambulika katika Tawrati kwa umashuhuri wa jina la Baqir na ewe Jaabir! Karibu utafikia zama zake na hapo tafadhali naomba unifikishie salamu zangu. Baada yake atakuja Ja'afer as-Sadiq bin Mohammad na baadaye Musa ibn Ja'afer na baadaye Ali ibn Musa na baadaye Muhammad ibn Ali na baadaye Ali ibn Mohammad na baadaye Hasan ibn Ali na baadaye Muhammad ibn al-Hasan ambaye atakuwa juu ya ardhi hii kama hujjatillah na bakiyallah katika wamchao Allah swt. Huyo ndiye atakayepata ushindi wa mashariki hadi wa magharibi wa dunia hii. Na yeye mwenyewe ambaye atakuwa hayupo mbele ya wafuasi (Mashiah) wake na wale wampendaye hadi kwamba hao hawatabakia katika itikadi ya Uimamu illa wale tu ambao Allah swt ameshawachukulia mitihani ya nyoyo zao."

Ja’abir r.a. anaelezea kuwa: Mimi sikusita kumwuliza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
"Ewe Mtume wa Allah swt! Je katika zama za Ghaibat, wafuasi (Mashiah) wake wataweza kufaidika naye?"

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu:
"Naam ! Kwa kiapo cha Allah swt ambaye amenituma nikiwa Mtume wake,kuwa katika zama zake za Ghaibat ,Mashiah wake watang'arika kwa nuru yake na kufaidika kwa Ukhalifa wake kama vile watu wanavyofaidika na jua hata kama litakuwa limejificha katika mawingu."

1662. Hadith ya Nne

Imam Abu Dawud ameandika katika kitabu chake Sunan na Imam Tirmidhi anaandika katika Sahih Tirmidhi kwa kumnakili Abu Said Khudhri,kuwa: “Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:
Mahdi anatokana nami na mwenye uso unaong'aa na pua yake iliyo ndefu ataijaza ardhi kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imeshajaa kwa dhuluma na ufisadi, na atatawala kwa kipindi cha miaka saba.' "

1663. Hadith ya Tano

Imam Abu Dawuud katika Sunan amendika kwa kumnakili Sayyidina Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.:
"Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa iwapo kwisha kwa dunia hata kama ni siku moja itakayobakia,hivyo pia Allah swt atamtuma mtu mmoja kutokana na Ahlul Bayt yangu (kizazi changu) humu duniani ambaye ataijaza dunia kwa uadilifu na haki kama vile itakavyokuwa imejaa kwa dhuluma na ufisadi."

1664. Hadith ya Sita

Imam Abu Dawud amemnakili Ummul Moominiina kufuatilia mfululizo huo wake kuwa:
Mtume Mtukufu s.a.w.w amesema kuwa
'Mahdi atatokana na Itrati (kizazi) yangu, yaani atatokana na kizazi cha Fatimah az-Zahra a.s.'

1665. Hadith ya Saba

Imam Bukhari katika Sahih Bukhari , Imam Muslim katika Sahih Muslim na Kadhi ibn Mas'ud Baghawi katika Tasnif Sharh al-Sunnah. Wote wanamnakili Abu Hurayrah akisema: "Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

'Je hali yenu itakuwaje wakati Mtume Issa a.s. atakapoteremka kwenu na Imam wenu atakuwapo ametokea miongoni mwenu?'"

1666. Hadith ya Nane

Imam Tirmidhi katika Sahih Tirmidhi na Imam Abu Dawud katika Sunan Abu Dawud wanamnakili Abdullah Ibn Mas'ud akinakili riwaya: Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.
“Kuwa dunia haitakwisha hadi hapo mfalme wa Kiarabu atatokea kutokana na kizazi changu,na ambaye jila lake litakuwa kama jina langu."

1667. Hadith ya Tisa

Imenakiliwa na Maimamu wa Ahli Sunna katika Sahih zao, riwaya ifuatayo: Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.
"Atatokezea mtu mmoja katika Ahlul Bayt yangu,atakayetawala na jina lake litakuwa kama jina langu."

1668. Hadith Ya Kumi

Imam Abu Is-haq Tha'alabi katika tafsir yake anamnakili Anas bin Malik kuwa: Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema kuwa
"Sisi wana wa Abdul Muttalib ni viongozi wa watu wa Jannah, yaani mimi , Hamza, Ja'afer na Ali na Hasan , Hussein na Mahdi

1669. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. :

“Hakuna watu wanaopoteza utajiri wao isipokuwa kwa kutokana na madhambi yao, kwani Allah swt kamwe hawadhulumu viumbe vyake.”

1670. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Wale wote wanaotukuzwa na kuheshimiwa kwa woga wa maovu yao, kwa hakika wao watakuwa miongoni mwa watu waovu kabisa siku ya Qiyama.”

1671. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Hamaki huziba (nuru ya) moyo wa mwenye hekima. Asiyeweza kudhibiti hamaki yake hawezi kuitawala akili yake.”

1672. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Mwenye kuiacha hamaki yake ipande, huharakisha mauti yake.”

1673. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Jihadhari na hamaki, kwani mwanzo wake ni wendawazimu na mwisho wake ni majuto.”

1674. Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Hamaki ni moto uliokokwa, mwenye kuipoza hamaki huuzima (moto wake); na mwenye kuiachilia huwa ni wa kwanza kuungua humo.”

1675. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Jilindeni kutokana na ukali wa hamaki na jiandaeni kupambana nao kwa kuvunja hamaki na kwa kuvumilia.”

1676. Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Kujidhibiti wakati wa kushikwa na hasira humsalimisha mtu wakati wa maangamizo.”

1677. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Kitu gani kilicho kiovu zaidi kuliko hamaki wakati mtu aliyepandwa na hamaki hutoa roho iliyoharamishwa na Allah swt.”

1678. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Ikiwa mmoja wenu atapandwa na hamaki, kama amesimama akae chini, na kama amekaa alale. Na kama hamaki haikupoa baada ya kufanya hivyo, basi atawadhe kwa maji baridi au aoge, kwani moto hauzimiki ila kwa maji.”

1679. Mtu mmoja alimwambia Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na kusema:

“Mimi mpaka hivi punde tu nilikuwa nikiamini kwamba wewe na baba yako ni watu wabaya kabisa, lakini sasa ninahisi kwamba huo moyo wangu uliokuwa umejaa chuki na uadui dhidi yenu, sasa umejaa mapenzi na ikhlasi. Hakika hakuna mwingine anayestahiki cheo hiki kitukufu isipokuwa wewe tu.

1680. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Jiepusheni na ghadhabu, kwani huleta mashaka.”