read

Mwanamke Kumridhisha Mume Wake

869. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema , Bihar al-Anwaar, j.81, uk 385

“Siku ya Qiyamah mwanamke hataokolewa na hatapata uokovu wowote kutoka kwa Allah swt bila ya idhini ya bwana wake.”

870. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. ameripoti kutoka kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambaye amesema, Al-kafi, j5, uk.324 :

“Bora wa wanawake miongoni mwenu ni yule ambaye ana sifa tano
1. Mwanamke asiye na matatizo, Mtiifu, Mnyenyekevu, Mwenye matumizi madogo

2. Mvumilivu wakati bwana wake anapokasirika

3. Mshiriki mwema na msaidizi wakati wa shida,

4. Mpaji wa hima kwa bwanake anapokuwa amezongwa na mawazo na shida

5. Mtunzaji wa mhifadhi wa nyumba ya bwana wake anapokuwa hayupo.

Kwa hivyo mwanamke kama huyo ni wakala katika mawakala wa Allah swt na kwa hivyo mawakala wa Allah swt hawatakuwa wenye hasara (yeye anapata matumaini sahihi).

871. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J.5, Uk.507

“Mwanamke yeyote yule anayepitisha usiku ambapo mume wake amemkasirikia na kumghadhibikia, ibada zake hazikubali hadi pale huyo mwanamke atakuwa amemridhisha bwana wake.”

872. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Makarim-ul-Akhlaq,J.2, Uk. 246 :

“Haki za bwana kwa mke wake ni kuziwasha taa, kutayarisha na kupika chakula na kumpokea mume wake anapokuja mlangoni kwa maneno mazuri na kamwe asimkatalie mume wake anapomhitaji yeye binafsi ( kujamiiana) isipokuwa anapokuwa sababu zake.1

873. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.,Mustadrak-Al-Wasa'il-ush-Shiah, J.14, Uk. 257 :

“Mwanamke kamwe hatatekeleza haki za Allah swt hadi yeye ametekeleza haki za mume wake.”

874. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s.,Wasa'il ush-Shi'ah, J.10, Uk. 527

“Siku moja mwanamke mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwambia: ‘Ewe Mtume wa Allah swt ! Je bwana ana haki gani kwa mke wake ?’

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimjibu: “Mwanamke amtii mume wake na wala asimuasi.’”

  • 1. Mara nyingi tunaona kuwa mwanamke hafikirii wala haoni umuhimu wowote katika masuala kama hayo. Mume anapobisha hodi tu na kukaribia mlangoni, basi mwanamke anapoufungua mlango tu anaanza mashambulio yake kwa kila aina ya silaha alizonazo. Kwa hakika hii ni tabia mbaya mno kwani mume wake ametoka wapi na ameyapitia yapi hayajui. Hivyo inatakiwa kumkaribisha vyema na kumpa angalau bilauri moja ya maji. Lakini iwapo mwanamke atakuwa na tabia kama hii basi ugomvi utaweza kuzuka baina yao na hata mwanamke kuchapwa kibao kwa kutokana na hasira za mume wake.