read

Mwanamke na Mahari.

833. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 58, Uk. 321:

“Ubashiri mbaya wa mwanamke ni kuwa mahari yake ya juu kabisa na ghadhabu zake.”

834. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. a.s Amesema,

“Waizi huwa wa makundi matatu:
1. La kwanza wale wanaozuia kutoa sadaka;

2. pili wale wanao jiwekea mahari ya mwanamke na kujihalalishia kwa ajili yao wenyewe;

3. tatu wale wanaochukua mikopo na hawajaamua kurudisha mikopo hiyo kwa ajili ya kulipa madeni yao.”

835. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 387:

“Kwa hakika moja ya baraka za Allah swt kwa mwanamke ni mahari yake kutokuwa juu, na moja ya maovu ya mwanamke ni kuwa na mahari kubwa.”

836. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 21, Uk. 253:

“Msifanye mahari ya wanawake ikawa nzito, kwa sababu hiyo inaleta uhasama na uadui.”

837. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar, J. 64, Uk. 268:

“Kuna madhambi maovu kabisa ya aina tatu:
1. Kuwatesa wanyama wakati wa kuwachinja,

2. Kuchelewesha na kutokulipa mahari ya mwanamka, na

3. Kutokulipa mishahara ya wafanyakazi.”