Ndoa kwa Kujali Imani na Uaminifu.
843. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. bila kujali daraja la kizazi cha mtu, amesisitiza na kusema, At-Tahdhib, J. 7, Uk. 394:
“Mtu yeyote anapokuletea habari za kutaka kukuoa na wewe kwa kuridhika unakubali, kwa adabu zake na dini yake, basi ungana naye kwa ndoa. Na iwapo hutafanya hivyo, basi wewe utakuwa umesababisha fitina na ufisadi mkubwa kabisa juu ya ardhi.”
844. Imam Jawad a.s. ameandika katika barua, Al-Kafi J. 5, Uk. 347 na Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 393 na At-Tahdhib, J. , Uk. 394:
“Mtu yeyote akutakaye wewe katika ndoa anayetaka kukuoa na wewe unakuwa umeridhika na dini na uadilifu wake, basi ungana naye kwa ndoa.”
845. Siku moja mtu mmoja alimwambia Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa, Al-Mustadrak, J. 2, Uk. 218:
“Yeye alikuwa na binti wake na alimwuliza Imam a.s. kuwa yeye amwoze binti wake kwa nani, kwa hayo Imam a.s. alimjibu: Muoze binti wako kwa yule ambaye ana imani na ni mcha Allah swt: Kwa sababu atampenda na kumheshimu huyo binti wako, na iwapo yeye atakuwa mkali juu ya binti yako, basi hatamdhuru.”
846. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al- Muhajjat-ul-Baidha, J. 3, Uk. 94:
“Yeyote yule atakaye muoza binti wake kwa mtu ambaye si mcha Allah swt basi kwa hakika amevunja uhusiano wake pamoja naye.”