read

Neema Nne za Allah Swt

1019. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema kuwa kila asubuhi, kila Mwislamu anatakiwa azikumbuke neema nne za Allah swt. Hofu yangu ni kwamba asipozikumbuka, kuna hatari ya kuzipoteza neema hizo:

1. Namshukuru Allah swt ambaye amenisaidia kumtambua Yeye na hakuuacha moyo wangu gizani.

2. Namshukuru Allah swt ambaye ameniweka pamoja na wafuasi wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

3. Namshukuru Allah swt ambaye ameiweka riziki yangu kwake Yeye na si mikononi mwa watu.

4. Namshukuru Allah swt ambaye amezifunika dhambi zangu na aibu zangu na hakunidhalilisha mbele ya watu.

1020. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.,Nur al-Absaar Shablanji.

“Mwovu wa watu ni yule anayewawekea pingamizi na anakuwa mkali kwa watu wake wa nyumbani.”

1021. Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu :

“Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, wala msifuate vyayo za Shaytani; kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri.”