read

Riba

1359. Dhambi la riba ni miongoni mwa Madhambi Makuu.

1360. Kwa mujibu wa Qur’an tukufu, kuchukua riba ni dhambi ambayo inasababisha adhabu kali kabisa kutoka kwa Allah swt. Adhabu za kuchukua na kutoza riba ni kali kabisa kuliko madhambi mengine. Kama ilivyoelezwa katika Surah Aali Imran, 3, : 130 - 131:

‘Enyi Mlioamini! Msile riba, mkizidisha mara dufu kwa mara dufu; na mcheni Allah ili muweze kuwa na ufanisi’ ‘Na ogopeni moto wa Jahannam ambao umetayarishiwa makafiri.’

1361. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah al Baqarah, 2, Ayah 275 :

‘Wale wanaokula riba, hawasimami ila kama anavyosimama yule ambaye Shaitani kamzuga kwa kumsawaa; na haya ni kwa sababu wamesema, ‘biashara ni kama riba’, Allah ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba. N a aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kishaakajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) aliyoipata; na hukumu yake iko kwa Allah. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.’

1362. Ayah hiyo inatuthibitishia kuwa wale wanaochukua riba watabakia kwa milele katika Jahannam (Motoni) na kamwe hakutakuwa na uwokovu kwa ajili yao. Allamah Muhammad Husain Tabatabai (a.r.) katika Tafsiri ya Al-Mizan , anasema:

“Adhabu aliyoiweka Allah swt kwa ajili ya mla riba ni kali kabisa kwani hakuna mahala pengine palipozungumzwa kwa ajili ya wale wavunjao kutoka Furu-i-Diin. Kosa lingine ni lile la kulea urafiki pamoja na maadui wa Islam. Athari za riba zipodhahiri na bayana kwetu sote. Kukusanya na kuficha mali ndiko kunako ongezea tofauti kati ya tabaka la masikini na tajiri. Umasikini ni ugonjwa ambao unamdhalilisha na kumshusha hadhi mgonjwa wake, unateketeza uthamini wake na kuharibu maadili yake. Na haya yanaelekeza katika mutenda maovu, uizi, ubakaji na mauaji. Walanguzi ndio watu wanaowajibika kwa kuteketea kwa usawa wa kijamii, ambao wamejilimbikizia mali kupita kiasi kwamba haiwafikii wanao hitaji na wenye dharura. Kwa kuvunjika kikamilifu kwa mshikamano wa kijamii unaweza kuzua na kukuza vita vya wenyewe kwa wenyewe au vita vya ndani na kuendelea hadi kuzuka kwa vita vya dunia ambavyo hatima yake itakuwa ni mauaji na maangamizo. Katika ulimwengu wa sasa ikiwa na silaha za kisasa za teknolojia ya hali ya juu na ya maafa makubwa katika nuklia na kemikali, vita vinapozuka si kwamba vinaleta mauaji ya wanaadamu tu bali humgeuza yeye kuwa ni picha tu, mgonjwa na asiye na uwezo wowote na ameharibika kimwili kwa vizazi na vizazi vijavyo.

1363. Katika kitabu ‘Islam and World Peace’ imeandikwa:

“Islam inasema kuwa mapato ya mtu yatokane na kiwango cha juhudi na kazi iliyofanyika.” Kwa sababu uwekezaji wenyewe haufanyi kazi wala jitihada ya aina yoyote ile. Hivyo, mali ya matajiri haitakiwi kamwe kuongezeka kwa kutokana na riba.”

1364. Mtume Muhammad s.a.w.w. anasema katika Hadith moja, katika Wasa’il al-Shiah :

“Ibada inayo sehemu sabini. Na muhimu kabisa ni mtu kujipatia kipato chake kilicho halali.”

1365. Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika Muhajjatul Baidha :

“Mfanyabiashara mwaminifu atahesabiwa pamoja na Mitume a.s. Siku ya Qiyama. Uso wake utakuwa uking’ara kama mbalamwezi.”

1366. Qur’an Tukufu inarejea kutuambia katika Qur'an Tukufu, Surah al-Baqarah, 2 Ayah 275:

‘‘Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kishaakajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) aliyoipata; na hukumu yake iko kwa Allah. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.’

1367. Ayah ya hapo juu ya Qur’an inaendelea Qur'an Tukufu, Surah al-Baqarah, 2 Ayah 276 :

‘Allah huyafutia (baraka mali ya ) riba: na huyatia baraka (mali yanayotolewa) sadaqa . Na Allah hampendi kila kafiri (na) afanyaye dhambi.’

1368. Qur’an Takatifu inatuambia Surah al-Baqarah, 2, Ayah 278 :

‘Enyi Mlioamini ! Mcheni Allah, na acheni yaliyobakia katika riba, ikiwa mmeamini.’

1369. Ushahidi wa imani ya mtu katika utiifu wa Hukumu za Allah swt, ayah hiyo hiyo inaendelea : Qur'an Tukufu, Al-Baqarah, 2, Ayah 279

‘Na kama hamtafanya hivyo, basi fahamuni mtakuwa na vita na Allah na Mtume Wake….Na mkiwa mmetubu, basi matapata rasilimali zenu; msidhulumu wala msidhulumiane.’

1370. Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amezungumzi katika hotuba yake huko Makkah :

“Muelewe kuwa riba iliyokuwa imekusanywa katika zama za ujahiliyya sasa imesamehewa kabisa. Kwanza kabisa mimi binafsi nina wasameheni ile riba (iliyopo shingoni mwenu) ya (mjombangu) '‘Abbas ibn Abdul Muttalib."

1371. Imeripotiwa kutoka Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. kuwa, katika Al-Kafi :

“Kuchukua Dirham (au pesa moja) kama riba ni vibaya sana machoni mwa Allah swt kuliko kuingiliana na mwanamke aliyeharamishwa kwako.”

1372. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Wasa’il al-Shiah :

“Mtume Muhammad s.a.w.w. amemlaani vikali yule ambaye anayekubali riba, anayelipa riba, aneyeinunua riba, anayeiuza riba, yule anayeandika mikataba ya riba na yule anayekuwa shahidi wa mikataba hiyo.”

1373. Ibn Baqir anaripoti kuwa Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. alijulishwa kuhusu mtu mmoja aliyekuwa akitoza na kupokea riba kama ndiyo halali kama vile ilivyo halali maziwa ya mama. Kwa hayo, alisema Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. katikaAl-Kafi :

“Iwapo Allah swt atanipa uwezo mimi juu ya mtu huyu, basi nitamkata kichwa.”

1374. Sama’a anasema kuwa yeye alimwuliza Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. je ni kwa nini Allah swt ametaja kuharamishwa kwa riba mahala pengi katika Qur’an.

Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. alimjibu, Wasa’il al-Shiah :
‘Ili kwamba watu wasiache tendo la kutoa misaada (kama vile kutoa mikopo bila ya riba).”

1375. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Shughuli mbaya kabisa ni ile ambayo inahusisha riba.”

1376. Zurarah anasema kuwa yeye alimwuliza Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. kuhusu Ayah ya Qur’an isemayo katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Baqarah,2, Ayah 276:

‘‘Allah huyafutia (baraka mali ya) riba: na huyatia baraka (mali yanayotolewa) sadaqa .’

1377. Na akaongezea kusema :

“Lakini mimi ninaona kuwa mali na utajiri wa watoza riba inaendelea kuongezeka tu kila siku.”

1378. Amesema Al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Loh ! hasara inawezekana kuwa kubwa sana ? Kwa merejeo ya Dirham moja yeye anaipoteza Dini yake. Na iwapo yeye atafanya Tawba humu duniani basi kutafikia mwisho kwa mali aliyoichuma humu duniani kwa njia iliyo haramu na hivyo kuwa fukara.”

1379. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika Mustadrakul Wasa'il :

“Yule anayechukua riba basi Allah swt atalijazatumbo tumbo lake kwa moto kiasi hicho hicho. Iwapo yeye amechuma zaidi kwa kutokana na mapato ya riba, basi Allah swt hatakubalia matendo yake mema. Hadi kwamba kiasi cha punje moja kama kitabakia ambacho kimepatikana kwa njia ya riba. Allah swt pamoja na Malaika Wake wataendelea kumlaani huyu mtu.”

1380. Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :

“Usiku wa Mi’raj Mimi niliwaona baadhi ya watu waliokuwa wakijaribu kusimama lakini hawakuweza kufanikiwa kwa sababu ya matumbo yao makubwa, niliuliza, ‘Ewe Jibraili ! Je ni watu gani hawa ?’

Jibraili alijibu :
“Hawa ndio wale waliokuwa wakichukua riba. Sasa wao wanaweza kusimama tu kama wale waliokamatwa na Mashetani.”

1381. Mtume Muhammad s.a.w.w. aliendelea,

“Na hapo nikawaona wao wakikusanywa katika njia za wafuasi wa Firauni. Kwa kuona uchungu wa joto la Moto mkali, wao walipiga kelele : ‘Ewe Allah swt ! Je Qiyama itakuwa lini ?’
(Hivyo imekuwa dhahiri kuwa Moto unaozungumziwa katika riwaya hii ni adhabu katika Barzakh ).

1382. Imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema, katika Mustadrakul Wasa'il :

“Wakati zinaa na riba vitakapokuwa ni vitu vya kawaida katika mji wowote basi Allah swt huwapa ruhusa Malaika kuwaangamiza wakazi wake.”

1383. Ipo riwaya nyingine isemayo kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, katika Mustadrakul Wasa'il kuwa :

“Utakapofika wakati Ummah wangu utaanza kutoza na kupokea riba, basi mitikisiko na mitetemeko ya ardhi yatakuwa yakitokea mara kwa mara.”

1384. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema, Wasa’il al-Shiah :

“Iwapo mtu atazini pamoja na mama yake katika Al-Ka’aba tukufu, basi dhambi hili litakuwa hafifu mara sabini kuliko tendo la kutoza na kupokea riba.”

1385. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Katika macho ya Allah swt, kuchukua Dirham moja ya riba ni mbaya kabisa hata kuliko matendo thelathini ya kuzini pamoja na maharimu wake yaani baba kuzini pamoja na binti yake.”