Semi za Imam Ali Ibn Abi Talib A.S.
Uadilifu.
1032. Taji la mfalme ni uadilifu wake mwenyewe.
1033. Utatawala iwapo nawe utakuwa mwadilifu.
1034. Uadilifu huangamiza ulafi , uroho na tamaa.
1035. Ngome ya Utukufu (ya Allah swt) huikinga nchi yenye mtawala mwadilifu.
Shurutisho na shari
1036. Kulazimisha/Kushurutisha kunaifanya akili iwe kipofu.
1037. Shari kunamfanya mtu awe mwoga wa uadilifu (ataiongopea)
1038. Uchokozi ni hatua ya kukaribia maangamizi.
1039. Kinachodhulumu haki ni kule kusaidia vilivyo batilifu.
1040. Udhalimu kwa mwenye dhiki ni dhuluma kubwa kuliko zote zile.
1041. Allah swt huharakisha kuanguka kwa wachokozi.
1042. Ushidi wa mshari ni kushindwa kwa nafsi yake.
1043. Kustarehe humu duniani kwa fidia ya akhera ni kujidhulumu nafsi yako.
1044. Kuwakandamiza yatima na wajane kunaleta magonjwa na kupotea kwa ne’ema.
Ulimi na usemi:
1045. Mtu amehifadhika chini ya ulimi wake.
1046. Ulimi mtamu/mzuri hupata marafiki wengi.
1047. Ulimi wako utasema kile kilichozoeshwa. (Kwa hivyo jihadhari kabla ya kusema).
1048. Akili ni busara. Akili ya mpumbavu ipo chini ya ulimi wake(anasema kabla ya kufikiri).
1049. Ulimi ni mkalimani wa akili.
1050. Ulimi wa mtu ni uzani wake mwenyewe.
1051. Ulimi unaathari za kuchoma zaidi ya mkuki.
1052. Usemi wa kweli ni ulimi mtukufu.
1053. Jihadhari na ulimi, kwani ni sawa na mshale unaoweza kufyatuka kutoka upinde.
1054. Mtu bila kusema (ulimi useme mema na kukataza mabaya) ni ama sanamu au mnyama.
1055. Ulimi wa mwenye busara upo akilini mwake (huongea na akili yake na hufikiria zaidi na kusema kwa uchache kwani ni yenye manufaa).
1056. Kuujaribu (kucheki) ulimi ni afadhali kuliko kulitazama tumbo.
1057. Yeyote yule asiye uhifadhi ulimi wake basi ataujutia mbeleni.
Ukimya naKusema.
1058. Kila vile busara ya mtu iongezekavyo ndivyo vivyo hivyo maneno yake hupunguavyo.
1059. Ukimya ni majibu ya maswali mengi sana.
1060. Ukimya ni jibu bora kabisa kwa mpumbavu.
1061. Mazungumzo bora ni yale yaliyo mafupi na yenye manufaa.
1062. Bora ya misemo ni ile iliyochujwa na kuhakikishwa.
1063. Ukae kimya ili ukae salama.
1064. Kusema kupita kiasi kunamdharaulisha mtu.
1065. Urefu wa mazungumzo huidhoofisha hotuba.
1066. Hotuba ni kama dawa; kiasi kidogo kinaponya na kwa kuzidi kiasi kunaweza kumwua mgonjwa.
1067. Usimpuuzie yule asemaye bali wewe uyatilie maanani yale ayasemayo.
1068. Kusema kidogo ndivyo kukosewa kidogo.
Kifo (Mauti).
1069. Watu wako wamelala hali wako hai na huwa macho baada tu ya kufa.
1070. Kujielekeza kwa mabaki ya matamanio ya mtu ndiko kujiuwa haraka.
1071. Ufe kabla ya kifo kukuijia.
1072. Mauti inaidhihaki tamaa.
1073. Mauti ni kutenganisha toka kitakachoisha na kuelekea kule pasipokwisha.
1074. Kuikumbuka mauti kila mara kutampunguzia mtu tamaa za duniani.
1075. Wale watembeao juu ya ardhi siku moja watazikwamo.
1076. Tamaa hukuongoza katika njia ya upotofu.
1077. Wakati hatuna matumaini huwa hatuhuzuniki.
1078. Kufadhaika huwa pamoja na tamaa.
1079. Kinachoipatia madhara na hasara dini ni tamaa.
1080. Waroho ni watumwa wa matilaba(matamanio) yao.
1081. Kutokuwa na mategemeo kunaituliza na kuipumzisha roho.
1082. Uroho huuangamiza uadilifu
1083. Ubinadamu ni wa aina mbili; wale wenye matamanio matupu na wale watakao kuja kuwa wasioridhika.
1084. Tamaa huingamiza hadhi ya mtu bila ya kuongezeka kwa bahati yake.
1085. Hata kama wakiwa uchi na wenye njaa, hao walioridhika huwa ni wenye furaha.
1086. Kuridhika ni hazina isiyo na kifani.
1087. Kuridhika ni hadhi na heshima isiyodidimia milele.
1088. Mwenye kuridhika tu ndiye aishiee kwa amani na usalama.
Ustahimilivu, Uvumilivu Na Utulivu.
1089. Kutokuwa na saburi ya akili ni yenye madhara kuliko ustahimilivu.
1090. Chifu ya sababu ya Islam ni utulivu kwa Allah swt
1091. Ustahimilivu ni matunda ya Imani.
1092. Ujue kuwa utulivu ni hatua ya awali katika dini halisi na uaminifu ni mwili
1093. Kwa ustahimilivu, bahati mbaya huwa siyo tena bahati mbaya.
1094. Ule uwezo wa uvumilivu wa ghadhabu (hasira) ni bora kuliko kuchukua kisasi.
Mali (Utajiri).
1095. Mapenzi ya mali inachochea tamaa na kuharibu wema.
1096. Usia unawafariji warithi
1097. Mali ni chanzo cha hamaki.
1098. Bora ya akiba ni pale ambapo kazi zinatawanywa vyema.
1099. Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo anapotengana nayo.
Akili na Upumbavu.
1100. Uadui ni kazi ya wapumbavu.
1101. Dhana ya mwenye akili ni mafumbo.
1102. Kwa kumtii Allah swt ni sawa kwa hisa ya akili na hekima ya mtu.
1103. Kupigana vita dhidi ya matakwa yake mtu ni jihad kubwa kabisa.
1104. Sababu ya busara na akili ni kukubalia ujinga wake mwenyewe.
1105. Mwerevu hulenga pale na thabiti.
1106. Mpumbavu hulenga pale penye mali.
1107. Dhana ya mtu inategemea akili yake ilivyo.
1108. Dhana ya mwenye busara na hekima ni sahihi kabisa kuliko kithibitisho cha mpumbavu
1109. Kwa kujitenganisha na vitu vya muda na kujiweka tayari kwa maisha ya kudumu ndiko kunako busara na hekima hisa kubwa.
1110. Mtu huyo ni mwenye busara ambaye matendo yake yanathibitisha aliyoyasema.
1111. Mtu mwenye busara hasemi ila pale penye dharura au penye sababu.
1112. Kila mtu aliye mwenye busara na hekima huwa yuko masikitikoni.
1113. Mwenye busara ni mwenye faida hata kama akiwa katika hali gani ile.
1114. Kujihusisha na wapumbavu ni kuitesa Roho.
1115. Mpumbavu yupo peke yake hata kama akiwa katika jamii.
1116. Kutoka kupata hekima (matakwa yake) hayawezi kufidiwa na fedha.
1117. Hakuna ugojwa ulio mbaya kabisa kuliko kutokwa kwa hekima.
Uwema na Matendo Mema.
1118. Kwa uwema mtu anaweza kumteka mtu aliye huru.
1119. Wema haufi kamwe.
1120. Kazi iliyo bora zote ni kujijumuisha pamoja na walio wema.
1121. Kuwa mwema kwa mema ni uwema na hii ndiyo fahamu ya mtu ya hali ya juu.
1122. Thamani ya mtu inategemea uzani wa uadilifu wake.
1123. Angukia ndani kwa wema na uangukie nje kwa matakwa.
Tamaa
1124. Mapenzi ya mali (utajiri) yanachochea tamaa na kuupoteza uwema.
1125. Tamaa haielewi mipaka yake.
1126. Kuwa na imani ya Allah swt ni jitihada iliyo bora kabisa.
1127. Tamaa iliyo kuu kabisa ya wanyama ni kule kushibisha tumbo lao wenyewe.
1128. Tamaa iliyo kuu ya wanyama porini kule kuwanyanyasa wengineo.
1129. Tamaa kuu ya mwanamke ni kuivutia dunia kwake na kuchochea fujo humo.
1130. Jitihada kuu kabisa ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.humu duniani ni kuiongoza dunia.
1131. Tamaa yako iwe ni ile kwa ajili ya akhera na hapo utajirekebisha.
1132. Thamani ya mtu inategemea utukufu wa jitihada zake.
1133. Ukuu na ufahari wa mtu unategemea utukufu wa jitihada zake na wala sio pale penye kuozapo mifupa ya mababu zetu.
Rehehma na Msamaha:
1134. Kusamehe ni taji la ukubwa na fahari.
1135. Rehema inaitukuza nguvu.
1136. Itakuwa ni vyema iwapo rehema itashirikishwa pamoja na ukubwa.
1137. Itakuwa ni adhabu kubwa itakayotolewa mbali na kuombwa msamaha.
1138. Unyenyekevu inatangaza ukubwa.
1139. Unyenyekevu ni matunda ya elimu na hekima.
1140. Unyenyekevu bila ya kutazama panapostahili ni sawa na huna uwezo.
1141. Majivuno huangamiza na kumharibia sifa mtu.
1142. Kwa kuwa na majivuno au kiburi ni sawa na kuipa akili sumu.
1143. Kiburi hukandamiza mwenendo wa maendeleo.
1144. Majivuno huua na kuudhalilisha ukubwa.
1145. Unyenyekevu ni sawa na wavu uliotandwa kwa ukubwa.
1146. Kujivuna na kule kujideka ni matokeo ya wale wenye akili kasoro.
Ulimwengu:
1147. Ulimwengu huu ni sawa na daraja ituvushayo kwenda akhera.
1148. Dunia hii ni sawa na duka la maovu.
1149. Mapenzi ya dunia ni chanzo (mizizi) cha matatizo na maovu yote.
1150. Ufahari wa wapumbavu na walio wajinga ni mapenzi ya dunia.
1151. Dunia ni chungu mno zaidi kuliko ule utamu wake ulio nao.
1152. Kuipatia dunia hii talaka ni sawa na kupanga harusi na Akhera.
1153. Dunia hii ni sumu na wale wailao sumu ni majahili.
1154. Uishi kwa kiwiliwili chako humu duniani na uifanyishe kazi nafsi (imani) yako kwa ajili ya akhera.
Watu
1155. Watu ni zaidi ya vile walivyokuwa awali na huishi zaidi ya walivyokuwa wakiishi mababu zao.
1156. Mtu aliye jasiri kuliko wengine, atulizaye matamanio yake (subira).
1157. Itakuwa ni jambo la upuuzi iwapo nafsi itakuwa imedhoofika hali mwili wa mtu bado ana siha nzuri na iliyo njema.
1158. Yule aijuaye na kuelewa ubinadamu huchagua upweke.
1159. Yule ampendae Allah swt hupigana na aibu za watu.
1160. Yeyote yule asiyejifikiria na kujithamini mwenyewe basi amepotoka.
Matakwa ya Subira
1161. Hekima iliyo kuu kabisa ni kule kupingana na matakwa na matamanio ya mtu.
1162. Atakuwa ni mtu mwenye furaha kuu iwapo ataishinda nafsi yake mwenyewe.
1163. Adui wa kupindukia wa mtu ni yale matakwa yake.
1164. Vita vilivyo bora kuliko vyote ni vile vita dhidi ya nafsi ya mtu.
1165. Ulafi wa sehemu zetu za siri ndizo nyavu zilizo tegwa na Shaytani.
Madhambi.
1166. Kuishi kwako hapa (mbali na utukufu) na dhambi isiloweza kusamehewa.
1167. Usiogopeshwe na chochote kile isipokuwa madhambi yako mwenyewe.
1168. Madhambi yanaharibu ibada ya Allah swt.
1169. Uharibifu ni matunda ya madhambi.
1170. Madhambi yanampotezea mtu utukufu wake.
1171. Kujiepusha na madhambi ni afadhali kuliko kutenda mema .
1172. Kutenda madhambi ni ugonjwa na dawa yake ni kujiepusha nayo na kufanya tawaba
Mafunzo ya Tahadhari.
1173. Kila mtazamo wako wa fahamu ni fundisho kwako
1174. Walio kufa wamewachia mafunzo kwa ajili ya walio hai.
1175. Njia walizozipitia wale waliokufa na waliotutangulia ni zenye kutufunza na kututahadharisha sisi tuzifuatazo.
1176. Uhakika wa mambo ni mkufunzi wa kutosha kabisa.
1177. Umri mkubwa ni mkufunzi aliye bora kabisa .
Shauri
1178. Kutoa onyo la upole katika umati wa watu ni jambo lililo bure.
1179. Mtoa mashauri asiye na uwema ni sawa na vile upinde unavyokuwa bila uzi.
1180. Mshauri aliye bora kuliko wengine ni yule akuelezeaye makosa na dosari zako.
Uaminifu, Uadilifu
1181. Ulimi mtukufu ni ule ulio adilifu.
1182. Kwa kutimiza ahadi ni mfano ulio bora kabisa wa uaminifu na uadilfu.
1183. Ukweli ina maana ya kwamba ulinganifu wa matamko kwa mujibu ya maamrisho ya Allah swt atakavyo.
Udanganyifu na Khiana
1184. Urafiki haupo kamwe katika uongo.
1185. Kwa kubadilisha maana halisi ya jambo kuna haribu asili yake.
1186. Kusema uongo kunaharibu habari.
1187. Kusema uongo panapostahili, kutamlindia heshima za mtu.
1188. Kusema uongo na unafiki kunadhalilisha nidhamu na heshima ya mtu.
Ukiasi na Ufujaji.
1189. Aliyebarikiwa ni yule ambaye anaelewaye vyema thamani yake na asiyevuka mipaka
1190. Kwa kupima kiasi ni nusu ya hifadhi
1191. Ufujaji unapotea kabla ya njaa
1192. Ufujaji unapoteza uwema na sadaka
1193. Tamaa ya mali kunaharibu ukiasi alionao mtu
1194. Kiasi kwa uangalifu kinabakia zaidi ya kile kilicho fujwa
1195. Hakuna ufahari katika ufujaji
1196. Kupima kiasi ni njia ya usalama na ya amani
Uwema ( Hisani )
1197. Heshima na ukukuzi hauwezi kamwe kulinganiswa na ubaya, sio yenye wema
1198. Mwenendo wa mtu ni diraja ya akili yake
1199. Urithi ulio bora kabisa ni uungwana wa mtu
1200. Hakuna chochote kile chenye thamani dhidi ya uungwana
Kuwaheshimu Wazazi
1201. Kuwatazama wazazi ni fardhi iliyo kuu kabisa
1202. Kuwatunza na kuwastahi wazazi wako (kuwalea) na malezi ya watoto wako, ndiyo yatakayo kulea wewe na kukustahi
Pupa
1203. Hakuna ushindi uliopo katika pupa
1204. Lawama huwa ni daima kwa yeyote aendeleae kwa pupa
Husuda
1205. Husuda humwibia mtu raha zake
1206. Silaha ya husuda ni malalamiko na mapingamizi
1207. Husuda huitafuna uwema kama vile moto iharibuavyo mbao
Kazi
1208. Matendo ndiyo matokeo ya nia
1209. Uwe mwaminifu katika kazi zako, kwami majaribio ya Allah swt yako macho sana juu yako
1210. Siku ya mwisho ni siku ya Qiyamah na wala si siku ya kufanya kazi
1211. Shauku ya uaminifu ni uharibifu mambo mema
1212. Upande ulio mgumu wa tendo, ni kuhifadhi utukufu wa jambo
1213. Bila ya uaminifu , kazi zote hazitakuwa na thamani yeyote ile
1214. Itakuwa ni wema iwapo mambo mema yawe rafiki yako na matilaba, adui yako
1215. Elimu kiasi kidogo huharibu mienendo na tabia
1216. Kazi nyingi zenye tamaa, zitaharibu zingine zote
1217. Hakuna aheshimiwaye zaidi kuliko wengine ila ni yule mwenye kufanya ibada
1218. Hakuna usalama ulio bora kuliko ibada
1219. Kumtii Allah swt ni sehemu ya busara ya mtu
1220. Ibadi ni pahala palipobora pa kujihifadhia
1221. Kujionesha au kujidai kunaharibu na pia kuighasi ibada
Kufanya Ghiba
1222. Hakuna uwema au uamnifu katika kufanya ghiba
1223. Yeyote yule asikilizaye ghiba basi ndiye mfanya ghiba mwenyewe
1224. Yeyote yule awasemae wengineo kwako, ndivyo vivyo hivyo ujue wazi wazi kuwa ndivyo akusemaye wewe kwa wengineo