read

Talaka na Athari Zake.

875. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi, J. 6, Uk. 54:

“Kwa hakika Allah swt hapendi kabisa au humlaani mwanamme au mwanamke yeyote ambaye anakuwa na nia ya talaka au anaoa kwa ajili ya kustarehe tu.”

Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameirejea kauli hii mara tatu kusisitiza kuwa mwanamme yeyote yule anayempa mke wake talaka kwa ajili ya kuoa mwanamke mwingine na kutaka kustarehe starehe za ndoa na mwanamke mpya na vile vile mwanamke yeyote yule anayeomba talaka kwa sababu kama hizo hizo na kuolewa na mwanamme mwingine, basi wote hawa wanajitumbukiza katika laana za Allah swt.1

876. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 104, Uk. 107:

“Wanawake katika umma wangu ambao wanafuata sunnah nne (mambo mema manne) basi wataingizwa Jannah:
1. Iwapo yeye atalinda utukufu wake,

2. Anamtii mme wake,

3. Anatimiza sala zake tano, na

4. Anafunga saumu katika mwezi wa Ramadhani.”

  • 1. Leo dunia imekuwa ya uwazi zaidi. Mwanamme anapokuwa na mali na hivyo wanawake wanapoona kuwa mwanamme huyo ana mali na utajiri basi wengi huanza kumtemelea huyo mwanamme na wanaanza kutamaniana. Hivyo kama nilivyoelezea hapo nyuma kuwa wanawake wanakuwa na tabia ya kujiweka kiovyo wanapokuwa nyumbani yaani hawavai vizuri wala kuwavutia wanaume zao na hujiweka kama vijakazi, hivyo mwanamme anapowaona wasichana na wanawake nje ya nyumba yake wamevaa vizuri na kuvutia basi hutumbukia katika mitego ya mapenzi ambavyo tumeona mara nyingi huwapokonya waume wengine. Hatimaye utasikia kuwa bwana anataka kumpa talaka mke wake au mke anataka kumpa talaka mume wake si kwa sababu nyingine bali ni kutaka kuolewa na mwanamme au mwanamke mwingine kwa sababu ya urembo au mapesa. Talaka na ndoa zinamasharti yake. Kuwepo na uadilifu. Lakini talaka na ndoa kama hizo katika Islam zimeharamishwa kabisa.