read

Ubashiri wa Imam Jaafer As-Sadiq A.S.

Mazungumzo yafuatayo yamefanywa na Imam Jaafer as-Sadiq a.s. ambamo ameripoti ubashiri wa siku za mwisho wa dunia hii. Yametolewa kutoka Darul Islam, Bihar-ul-Anwar na Raudhat-ul-Kafi. Wanaoripoti habari hizo ni Allamah Naraqi na Sheikh Kulaini r.a. kutokea kwa Himran.
Imam a.s. alisema:
1. "Haki itakuwa imetokomezwa na watu walio katika haki hawatapatikana.

2. Dhulma na uonevu utaenea katika miji yote.

3. Kufuata Qur’an kimatendo itajulikana kama tabia ya kizamani.

4. Zitatolewa maana ya Aya za Qur’ankwa mujibu wa matakwa ya watu, hivyo mafhum ya Qur’an itakuwa imebadilishwa na kupotoshwa.

5. Wadhalimu watakuwa wakiwa kandamiza wale walio katika haki.

6. Uchokozi na uchochezi utatokea kutoka kila pande na pembe.

7. Matendo maovu na kukosa aibu vitaenea na kuzagaa kila mahala.

8. Ulawiti utakuwa ni jambo la kawaida.

9. Muumin atakuwa akionekana kama mtu dhalili ilhali waovu watakuwa wakiheshimiwa

10. Vijana hawatakuwa wakiwaheshimu wakubwa wao.

11. Huruma itakuwa imepotea kabisa.

12. Waovu watakuwa wakitukuzwa kwa udhalimu wao na hakutakuwapo na mtu yeyote wa kuwapinga.

13. Wanaume watafurahishwa mno kwa kuingiliana na wanaume wenzao.

14. Wanawake watawaoa wanawake wenzao.

15. Mapesa yatatumika kwa ajili ya matumizi yale yaliyo haramishwa na Allah swt.

16. Starehe, anasa na zinaazitashamiri.

17. Zinaa itajulikana kama maadili yaliyopitwa na muda.

18. Muumin atatengwa kwa sababu ya kufanya ibada za Allah swt.

19. Jirani mmoja atafurahi mno kwa kumuudhi na kumbughudhi jirani mwenzake.

20. Wazushi (kama Salman Rushdie wa Uingereza) watatukuzwa na kusifiwa katika kueneza fitina na yale wanayozusha.

21. Ushauri mzuri utakanwa.

22. Milango ya wema itafungwa wakati milango ya maovu itafunguliwa.

23. Al-Kaaba haitatumika au haitafikika kwa sababu ya vikwazo na ugumu utakao wekewa mahujaji.

24. Watu watalazimishwa kuacha kwenda Makkah kuhiji.

25. Watu hawatakuwa wakitimiza ahadi zao watakazokuwa wakizitoa.

26. Wanaume watakuwa wakitumia dawa za kuamsha tamaa za kiume kwa ajili kulawiti na wanawake watakuwa wakitumia vyakula vya mafuta ili kujitayarisha kwayo.

27. Baadhi ya wanaume watakuwa wakiishi kwa kujipatia mapesa kwa kuuza mikundu yao.

28. Na wanawake watakuwa wakijipatia mapesa kwa kufanyisha biashara ya zinaa.

29. Wanawake wataunda vilabu vyao, mashirika na umoja wao.

30. Wanaume atajigeuza kama wanawake na watavutia na wanawake.

31. Wanaume watajirembesha kama wanawake.

32. Ulawiti utachukuliwa kama ndiyo ustaarabu na starehe ya kweli.
Na Banu Abbas watalipia ulawiti.

33. Wanawake wataona fakhari kwa kuwa na waume nje ya mume mmoja wa ndoa na vivyo hivyo wanaume watakuwa hivyo hivyo.

34. Heshima itakuwa ikitolewa kwa utajiri wa mtu na wala si ucha Mungu.

35. Riba ndiyo itakayokuwa biashara ya kila siku.

36. Ushahidi wa uongo utakuwa ukisadikiwa mno.

37. Kile alicho kiharamisha Allah swt kitachukuliwa ni halali na chochote kile alicho kihalalisha Allah swt kitachukuliwa ni haramu.

38. Maamrisho ya Dini yatageuzwa kwa mujibu wa matakwa yao.

39. Wachokozi na waovu watatenda maovu kwa udhahiri bila ya khofu yoyote ile na Muumin hawataweza kuwazuia vyovyote vile.

40. Watawala watawapenda mno Makafiri kuliko Muumiin.

41. Rushwa ndiyo itakuwa njia ya kujitimizia kazi kutoka maofisa wanaohusika.

42. Wanaume wata walawiti wake zao.

43. Watu watakuwa wakiuawa kwa visingizio vidogo vidogo na magomvi madogo madogo.

44. Wanawake watawafanyia wanaume dhihaka, nao wata shawishiwa kufanya uhusiano na wanawake

45. Wanaume wataishi kwa mapato ya wake zao zitakazopatikana kwa zinaa

46. Wanawake watakuwa wakiendesha hukumu majumbani huku wanaume wakiwatii wake zao kwa sababu wanawake hao ndio watakuwa wenye mapato.

47. Wanawake watatumiwa katika kupatikana huduma mbalimbali.

48. Kula kiapo kwa jina la Allah swt litakuwa ni jambo lililowekwa ulimini.

49. Pombena kamari vitapatikana kila mahala na vitakuwa vimezagaa.

50. Wanawake wa Kiislamu wataingiliana na Makafiri, ambapo Waislamu hawataweza kuwazuia na wala hawatakuwa na uwezo kama huo.

51. Maadui wetu watasaidiwa na watawala na marafiki zetu watadhalilishwa kiasi kwamba hata kiapo chao hakitakubaliwa.

52. Udanganyifu na hila ndizo zitakuwa desturi miongoni mwa watu.

53. Usomaji na usikilizaji wa Qur’an utakuwa ni bughudha kwa watu.

54. Kusikiliza mambo fidhuli ndiyo itakuwa ikipendelewa na watu.

55. Jirani hatamstahi jirani mwenzake illa kwa khofu ya ulimi mkali na mchafu.

56. Sheria na kanuni za Allah swt hazitatambuliwa na waovu hawataadhibiwa kwa maamrisho hayo.

57. Ghiba na kulaghaiana ndivyo vitakuwa vitu vya kawaida.

58. Madhumuni ya Hajj na Jihad yatakuwa mbali na yale ya Kiislamu.

59. Misikiti itarembeshwa kwa dhahabu.

60. Watawala watawataka ushauri Makafiri.

61. Litakuwa ni jambo la kawaida kuibia katika uzani na vipimo vya biashara.

62. Kumwaga damuya watu wegine litakuwa ni jambo la kawaida.

63. Watu watajigamba kwa ndimi zao chafu zenye matusi mabaya ili kuwatishia watu wengine.

Imam a.s. aliendelea kusema:
64. "Watu watakuwa wakipuuzia sala na kutojali.

65. Watu hawatakuwa wakilipa zaka ingawaje watakuwa na utajiri mkubwa.

66. Sanda za maiti zitakuwa zikiibiwa na kuuzwa tena.

67. Mauaji yatakithiri mno kiasi kwamba hata wanyama pia wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.

68. Watu watakuwa wakisali katika mavazi ya kiajabu.

69. Macho na mioyo itapoteza nuru zao za heshima na huruma.

70. Watu watakuwa wamejishughulisha na maswala ya kutafuta mali na mapesa tu.

71. Watu watasali kwa kuonyesha tu.

72. Watu watatafuta ilimu ya Dini kwa ajili ya kujipatia mali ya dunia.

73. Ushirika katika makundi yatakuwa ndiyo mambo ya maisha.

74. Wale watakaojipatia riziki kwa njia ya halali, watasifiwa kwa midomo tu.

75. Matendo maovu na machafu yataenea hata Makkah na Madina

76. Watu waliokufa watafanyiwa mizaha na vichekesho.

77. Mwaka hadi mwaka hali itakuwa ikiendelea kuharibika kuwa mbaya zaidi.

78. Matajiri wataigwa.

79. Masikini, mafukara watafanyiwa dhihaka na kufedheheshwa.

80. Matukio ya kudura kama yale ya mitetemeko, maporomoko n.k. yatakuwapo lakini watu watakuwa hawaviogopi.

81. Matendo maovu yatakuwa yakitendwa kiwaziwazi.

82. Wazazi watatupa watoto wao na watoto watawatusi wazazi wao na daima watakuwa wakitaka mali na utajiri wa wazazi wao.

83. Wanawake hawatawatii na kuwafuata waume wao.

84. Siku itakayopita bila ya mtu kutenda madhambi, basi itachukuliwa ni siku yenye nuksi.

85. Watu wenye uwezo wataficha mali muhimu na kuviuza kwa bei ya ulanguzi.

86. Waombaji na walaghai watajumuika katika kucheza kamari na kulewa.

87. Pombe itatumika kama ni kitu chenye kuponya i.e.dawa.

88. Makafiri watatukuzwa juu ya watu wengine na Muumin watadhalilishwa na kupuuzwa.

89. Kutafanywa malipo kwa ajili ya kutoa Adhan na sala

90. Misikiti itajaa kwa watu wasiokuwa na khofu ya Allah swt.

91. Watu wenye fahamu na akili kasoro ndio watakaokuwa wakiongoza sala za jamaa' na watu kama hao kamwe hawatashutumiwa au kusutwa na badili yake wataheshimiwa."

Vifo Vyeupe na Vyekundu:

1655. Kuhusu kifo cheupe na chekundu, Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: "Kabla ya kudhihiri kwa al-Qaim a.s. kutatokezea kwa aina mbili za vifo- nyekundu na nyeupe.

Kwa nyekundu kunamaanisha damu yaani kumwagika kwa damu nyingi mno kwa sababu za vita na mauaji ya aina mbalimbali. Na kifo cheupe kinamaanisha kuzuka kwa maafaya magonjwa ambayo yatakuwa daima yakienea na kuzuka kila mahala."

Tanbihi: Kwa vifo vyekundu hapo juu tunaelewa kuwa kutakuwapo na vita vya kutisha mno ambapo damu itakuwa ikimwagika kutoka kila pembe ya dunia.Tunasikia kila siku katika maredio na televisheni vile dunia yetu hii ilivyokumbwa na mauaji kila pande. Na ama kuhusiana na kifo cheupe, tunasikia vile magonjwa mbalimbali ya saratani, ukimwi n.k. yanavyoua watu kwa mamilioni.

Ubashiri wa Imam ‘Ali

1656. Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake,

1. Watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa.

2. Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi.

3. Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi.

4. Waislamu wataanza kuchukua riba.

5. Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida.

6. Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa.

7. Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia.

8. Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao.1

9. Wanaume watawataka wanawakeushauri na uongozi.

10. Hakutapatikana huruma kokote pale, dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu.

11. Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida.2

12. Mauaji na umwagaji wa damu utachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe.

13. Watu wenye ilimu watakuwa wadhaifu na wadhalimu watakuwa wenye nguvu.

14. Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu.

15. Wasufi na wasomaji wa Qur’an watakuwa wapumbavu.

16. Kutakuwa kukitolewa ushahidi wa kughushiwa (wa uwongo).

17. Qur’an Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu.

18. Misikiti itakuwa ikijengewa minara mirefu.

19. Watu waovu watakuwa wakiheshimwa.

20. Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao.

21. Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale.

22. Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaume wao kwa uroho wa mali.

23. Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana.

24. Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu

25. Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa.

26. Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji.

27. Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi.

28. Wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.

29. Kuiga hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke (ajifanye mwanamke na mwanamke atapenda ajifanye kama mwanamme3.)

30. Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea.

31. Mbwamwitu watakuwa wengi, katika makundi ya kondoo.

32. Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia .

33. Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko kitu chochote kile.

34. Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem. Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem.

Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema:
"Ewe Bwana, naomba utwambie Dajjal atakuwa ni mtu wa aina gani?"

Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed. Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia Dajjal na atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal.

35. Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia. Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyota ya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damu. Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.

36. Jua litakuwa pamoja naye.

37. Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.

38. Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,

39. Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.

40. Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye Dajjal yatakauka hadi siku ya Qiyama

41. Baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema "Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri, mimi ndiye niliyewaumba, na niliyewafanya nyie mkawa wazuri. Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana."

42. Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.

43. Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaa

44. Wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,

45. Huyo Dajjal atauawa mahala panapoitwa Aqba huko Syria atauawa siku ya Ijumaa mchana,

46. Mtume Issa a.s. atasali nyuma ya Imam Mahdi a.s.

47. Na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.

  • 1. Mambo kama haya ndivyo yanavyotokea katika kupiga kura za kidemokrasia!
  • 2. Kwa utumwa hapa kunamaanisha mbinu za kumfanya mtu asiweze kusema dhidi ya mambo ya mfadhili wake kama vile tunavyoona na kusikia kuhusu masharti ya misaada itolewayo na nchi na watu wafadhili.
  • 3. Nimesikia katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC mnamo tarehe 17 Novemba 1995 saa 6.30 jioni kuwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar University cha huko Misri kimetoa fatwa kuwa mwanamme anaweza kujigeuza k,uwa mwanamke na vile vile mwanamke anaweza kugeuzwa kuwa mwanamme kwa njia za operesheni ati kwa sababu ni maumbile yake ndivyo yalivyo.
    Vile vile nimesikia katika idhaa ya Kiingereza ya BBC hivi majuzi (wiki moja kabla ya Fatwa kutoka Al-Azhar) kuwa kumefanywa uchunguzi na utafiti huko Amerika na kutolewa ripoti kuwa mtu khanisi na anayelawiti na kulawitiwa aachwe awe hivyo na wala asilaumiwe na jamii kwa sababu ndivyo yalivyo maumbile yake.