read

Ulawiti.

893. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi :

“Kuingiza (uume) mwanzoni mwa nafasi ya haja kubwa ni dhambi kubwa kabisa hata kuliko kuingizia katika sehemu ya mbele ya siri ya mwanamke. Kwa hakika Allah swt ameangamiza ummah mzima wa Mtume Lut1 a.s. kwa sababu wao walijiingiza katika laana ya ulawiti. Allah swt kamwe hakumteketeza hata mtu mmoja kwa dhambi za zinaa.”

894. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. ,Wasa’il al-Shiah :

“Mtu yeyote anayetenda ulawiti pamoja na kijana wa kiume atapatwa na janabah (uchafu) ambao hautaweza kutakasishwa hata kwa maji ya dunia nzima. Allah swt atamghadhabikia na kumlaani vikali. (Yaani Allah swt atazichukua rehema na baraka kutoka kwake na kumlipa Motoni i.e. Jahannam). Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa ! Pepo (Jannah) zitakuwa zimemkasirikia mno. Na mtu ambaye anakubali kulawitiwa kwa nyuma, basi Allah swt humweka ukingoni mwa Jahannam (motoni penye moto mkali kabisa) na atamweka huko hadi hapo atakapo maliza kuwahoji watu wote. Hapo ndipo atakapo mwamrisha kuwekwa Motoni. Atapitia adhabu moja baada ya pili hadi kuzimaliza adhabu zote za Jahannam na hadi atakapofikia daraja la chini kabisa. Na kamwe hataweza kutoka hapo.”

895. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi

“Ulawiti ni moja ya Madhambi Makuu na inaadhibu pale mtu mmoja anapompanda mtu bila ya kumwingilia. Na iwapo atamwingilia kwa nyuma basi hiyo itakuwa ni kufr (ukafiri).”

896. Hudhaifa ibn Mansur anasema: “Mimi nilimwuliza al-Imam as- Sadique a.s. kuhusu Dhambi Kuu. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Kubana kwa sehemu za kiume baina ya mapaja mawili kwa njia isiyoruhusiwa.”

Nikamwuliza tena,
“Je ni mtu gani anayetenda dhambi la ulawiti ?”

Al-Imam as- Sadique a.s. alinijibu :
“Yule ambaye amekufuru kwa Allah swt kwa yale aliyoteremshiwa Mtume Muhammad s.a.w.w. (Qur’an tukufu ).”

897. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa kumjibu Abu Basir kuhusu Qur’an Tukufu, Surah Hud, 11, Ayah 82, isemayo :

فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِنْ سِجِّيلٍ مَنْضُودٍ

‘Basi ilipofika amri yetu, Sisi tuliibinua (mji) juu chinii, na kuwateremshia mvua ya mawe magumu ya udongo uliopikwa, tabaka juu ya tabaka.’

Al-Imam as- Sadique a.s. alimjibu:
“Kama mtu ataiaga hii dunia huku akisadiki kuwa ulawiti ni halali, hakika Allah swt atampiga kwa jiwe moja ambalo liliwadondokea watu wa Mtume Lut a.s.2

Walivyoadhibiwa Umma wa Mtume Lut a.s.

898. Qur’an tukufu imeelezea aina tatu za adhabu zilizoteremshiwa umma wa Mtume Lut a.s. .

Sauti kubwa ya kutisha na mayowe ya kusikitisha na makubwa mno

Kupigwa kwa kutupiwa mawe juu yao

Kupindua ardhi juu chini

899. Baada ya kutaja adhabu hiyo ya tatu, imeelezwa katika Sura Hud, 11 : 83

مُسَوَّمَةً عِنْدَ رَبِّكَ ۖ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ

‘(Mawe hayo ya udongo uliopikwa) yalikuwa yametiwa alama (za adhabu) za Mola wako; Na wala haipo (maangamizo ya miji) mbali kutoka wadhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya)’

900. Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. amesema : katika Fiqh-i-Ridha

“Jiepusheni na ulawiti na zinaa, na huu ulawiti ni chafu na mbaya kabisa kuliko zinaa. Madhambi haya mawili ndiyo vyanzo vya mabaya sabini na mbili ya humu duniani na Aakhera.”

901. Qur’an tukufu imetumia neno ‘utovu wa adabu, uchafu’ kwa ajili ya zinaa kwa njia ambayo imetumika vile vile kwa ajili ya ulawiti. Twaambiwa katika Surah A’araf, 7, : Ayah 80 – 81

وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُمْ بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِنَ الْعَالَمِينَ

‘Na (Sisi tulimpeleka) Lut, wakati alipowaambia watu wake:”Je ! Mwatenda jambo chafu ambalo halikutendwa na yeyote kabla yenu katika ulimwengu.’

إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِنْ دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنْتُمْ قَوْمٌ مُسْرِفُونَ

“Nyinyi mnawaendea wanaume kwa hamu (ya kufanyiana uchimvi) badala ya wanawake; Ama nyinyi ni watu wafujaji.’

902. Kumtazama kijana mdogo wa kiume kwa macho ya ashiki au uzinifu ni Haraam kabisa, hususan kijana ambaye bado hajaota nywele za usoni mwake. Madhara na adhabu za mtazamo wa ashiki au uzinifu vinazungumziwa kwa mapana na marefu katika maudhui yanayozungumzia zanaa. Vile vile Mtume Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Wasa’il al-Shiah

“Jiepusheni na kuwatazama kwa macho ya ashiki au uzinifu vijana wa matajiri na watumwa, hususan wale ambao hawajaota hata ndevu. Kwa sababu uchokozi unaofanywa kwa mitazamo ya aina hiyo ni mbaya kabisa kuliko uchokozi wa kuwatazama hivyo wasichana wadogo walio katika hijabu.”

903. Ni haraam kumbusu kijana wa kiume kwa kuashiki. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi kwa kumnakili Mtume Muhammad s.a.w.w. :

“Iwapo mtu atambusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki, basi Siku ya Hukumu (Siku ya Qiyama) , Allah swt atamfunga mdomoni mwa mtu huyo hatamu ya moto.”

904. Al-Imam ar-Ridha a.s. amesema katika Fiqh-i-Ridha :

“Wakati mtu anapombusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki (mapenzi au nyege) basi Malaika wa mbinguni na Malaika ardhini , Malaika wa Rehema na Malaika wa adhabu wote kwa pamoja humlaani huyo mtu. Na allah swt humtolea hukumu yake kwenda Motoni (Jahannam). Loh ! mahala pakutisha mno.”

905. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Mustadrakul Wasail :

“Allah swt atamwadhibu Motoni (Jahannam) kwa maelfu ya miaka mtu ambaye anambusu kijana wa kiume kwa ashiki au matamanio ya mapenzi.”

906. Wanazuoni wanasema kuwa wanaume wawili kulala pamoja chini ya blanketi au shuka moja bila mavazi kunawapa adhabu kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, navyo pia ni miongoni mwa madhambi makuu.

907. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. ,Wasa’il al-Shiah :

“Tengenezeni vitanda vya kulalia tofauti kwa ajili ya watoto wenu wanaozidi umri wa miaka kumi. Ndugu wawili wa kiume au ndugu wawili wasichana au ndugu na dada yake wasilazwe pamoja katika kitanda kimoja."

908. Kwa mujibu wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.,

“Mtu aliyetenda dhambi kama hili, mwili wake uchomwe moto hata baada ya kuuawa kwa njia nyingine. Yaani akishauawa kwa adhabu atakayoiamua Qadhi, basi baada ya kuuawa mwili wake uchomwe moto.

909. Tunakuleteeni hadith ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliyoisema :

“Mtu yeyote anayestahili kuuawa mara mbili kwa kupigwa mawe basi huyo ni mlawiti.”

910. Ni lazima ujilikane wazi wazi kuwa mwanamme yeyote anayemlawiti kijana wa kiume (anamwingilia sehemu za haja kubwa), basi wafuatao watakuwa wame haramishwa kwake :

1. mama wa kijana huyo,

2. dada na

3. binti yake huyo kijana kwa maisha yake yote.

4. Yaani, mtu huyu (mlawiti) kamwe hataweza kumwoa mama yake, au dada au binti ya huyo kijana.

911. Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:

"Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera.
Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni:-
    • Wanapoteza nuru

    • Wanakuwa maskini

    • Maisha yao yanakuwa mafupi.

Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:-
    • Allah swt atakuwa amewakasirikia mno

    • Watahesabiwa siku ya Qiyama kwa Sharia kali

    • Wataishi milele Jahannam.

912. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

"Manukato ya Jannah yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannah."

913. Taudhihul Masail ya Ayatullah Sistani:

                    (2413) Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake. Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti ni kijana ambaye hajabaleghe. Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme kimeingia katika sehemu za haja kubwa au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake.

                    (2414) Iwapo mwanamme atamuoa mama au dada wa kijana mvulana, na akamlawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.

  • 1. Kipo kitabu kimoja nilichokitarjumu ambacho kinazungumzia visa katika Qur'an, na kisa hiki pia kipo kimezungumziwa kwa marefu.
  • 2. Msomaji anashauriwa kukisoma vyema kijitabu nilichokitayarisha mimi kinachozungumzia Ummah wa Mtume Lut a.s. kwa makini kwani kinazungumzia vyema juu ya hali ilivyokuwa na ilivyokuja kuharibika na mafunzo tuyapatayo kwa kukisoma kisa hicho. Kama hukipati basi wasiliana kwa anwani yangu iliniweze kukusaidia.