read

Umri Wetu Tuutumie Vyema.

988. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Abu Dhar, Bihar al-Anwaar, J. 77, Uk. 77:

“Ewe Aba Dhar ! Faidi vitu vitano kabla ya vitu vitano:
1. Ujana kabla ya uzee,

2. Siha yako kabla ya magonjwa,

3. Utajiri wako kabla ya umaskini,

4. Ufaragha wako kabla hujawa mashughuli, na

5. maisha yako kabla ya kifo chako.”

989. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 257:

“Itakapofika siku ya Qiyamah, kikundi cha watu kitasimama na kuja kubisha hodi katika mlango wa Jannah. Nao wataulizwa ni nani wao, nao watajibu: Sisi ni watu wa subira na kwa hayo wataulizwa ni kitu gani walichokifanyia subira, nao watajibu sisi tumefanya subira kwa ajili ya Allah swt dhidi ya kumwasi Allah swt. Kwa hivyo Allah swt atasema kuwa hao ni wasema ukweli na atawaruhusu waingie Jannah. Kwani Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu:
Sura Az-Zumar, 39, Ayah 10:

قُلْ يَا عِبَادِ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۗ وَأَرْضُ اللَّهِ وَاسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُمْ بِغَيْرِ حِسَابٍ

‘Sema: Enyi waja wangu mlio amini ! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Allah swt ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.’”

990. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 206:

“Aliye na furaha ni yule ambaye hana matamanio na matarajio makubwa katika maisha yake na anafaidi kila fursa anayoipata.”