read

Zinaa na Athari Zake Mbaya.

886. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi, J. 5, Uk. 554:

“Imeandika katika Tawrat: Mimi ni Allah swt, muuaji wa wauaji na muadhibu wa wazinifu.”

887. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 5, Uk. 541:

“Ziko athari sita za zinaa, tatu ambazo zinapatikana humu duniani na tatu zitapatikana huko akhera. Zile zitakazoonekana duniani:
1. Itaondao heshima ya mtu na kumdhalilisha;

2. Itamfanya mtu awe maskini; na

3. Itafupisha umri wa maisha yake (yaani atakufa haraka).

Na zile zitakazo patikana Akhera ni:
1. Adhabu za Allah swt,

2. Hali ngumu kabisa katika utoaji wa hesabu, na

3. Kutumbukizwa katika Jahannam kwa ajili ya milele.”

888. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Kutokea Tawrat, Al-Kafi, J. 5, 554:

“Kuwa enyi watu msizini kwa sababu mkifanya hivyo wake zenu pia watafanya vivyo hivyo. Kile mkipandacho ndicho mtakacho kivuna. (kila ufanyavyo na wewe utafanyiwa hivyo).”

889. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 14:

“… yeyote yule amkumbatiaye mwanamke, ambaye ameharamishiwa kwake, basi atafungwa kwa minyororo ya mioto pamoja na Shaytani na wote kwa pamoja watatupwa katika Jahannam.”

890. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. wakati mmoja aliulizwa naAmar ibn Mussa kuhusu kufanya tendo la kujamiiana pamoja na wanyama au kujitoa manii kwa mkono au kwa kutumia sehemu zinginezo za mtu mwenyewe, na Imam a.s. alimjibu, Al-Kafi, J. 5, Uk. 541:

“Hali yoyote katika hizi na vyovyote vile ambavyo mwanamme humwaga maji yake, inachukuliwa kuwa ni zinaa (na imeharamishwa).”

891. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi, J. 2, Uk. 270:

“Amelaaniwa! Amelaaniwa yule mtu ambaye anafanya tendo la kuwaingilia wanyama.”

892. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-'Ummal, J. 5, Uk. 316 ;

“(Zinaa miongoni mwa jamii moja) mwanamme kwa mwanamme au mwanamke kwa mwanamke (ni zinaa).”