Utumwa

Mtazamo Wa Ki Islamu Na Qa Nchi Za Magharibi
Author(s): 
Publisher(s): 

Kitabu hiki kimerudiwa kimechapishwa tena kwa ruhusa ya waandishi, ili kuafikiana na Kongamano la Kilimwengu la Umoja wa Mataifa dhidi ya Ubagazi wa Rangi, (United Nations World Conference against Racism) ambalo lilitegemewa kufanyika katika jiji la Durban, Afrika ya Kusini, mwezi Augosti, 2001. Mada mbili zilizo pendekezwa kuwepo kwenye agenda zilisababisha migongano ya kimataifa. Agenda hizi zilikuwa: Malipo ya fidia kwa utumwa na biashara yake ambayo ilifanywa na mataifa ya Ulaya na Marekani (U.S.A) hapa Afrika na nyingine ilikuwa kulinganisha Uzayuni (Zionism) na ubaguzi wa rangi.

Translator(s): 
Category: 
Topic Tags: 
Person Tags: 

Neno La Mchapishaji Wa Kwanza Toleo La Kiingereza

Kitabu hiki kimerudiwa kimechapishwa tena kwa ruhusa ya waandishi, ili kuafikiana na Kongamano la Kilimwengu la Umoja wa Mataifa dhidi ya Ubagazi wa Rangi, (United Nations World Conference against Racism) ambalo lilitegemewa kufanyika katika jiji la Durban, Afrika ya Kusini, mwezi Augosti, 2001. Mada mbili zilizo pendekezwa kuwepo kwenye agenda zilisababisha migongano ya kimataifa. Agenda hizi zilikuwa: Malipo ya fidia kwa utumwa na biashara yake ambayo ilifanywa na mataifa ya Ulaya na Marekani (U.S.A) hapa Afrika na nyingine ilikuwa kulinganisha Uzayuni (Zionism) na ubaguzi wa rangi.

Suala la malipo ya fidia kwa Afrika kutoka kwa mataifa yaliyojihusisha na utumwa limeachwa kushugulikiwa kwa muda kwa makubaliano baina ya mataifa yanayodaiwa na Afrika, kuweka nguvu na msukumo mkubwa katika kuisaidia Afrika kuendeleza mpango wake wa kurejesha hali nzuri ya uchu mi. Mpango mmoja wapo unaojulikana sana ni ule wa: Millenium Africa Recovery Plan, ambao unasimamiwa na Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini. Msaada unaozungumziwa hapa bila shaka unaeleweka kwamba ni aina ya ukandamizaji wa kiuchumi kwa kuendeleza utumwa wa kiuchumi hapa Afrika daima milele.

Wayahudi wapatao milioni tatu (3) waliuawa wakati wa vita kuu ya Pili ya Dunia ambapo zaidi ya Waafrika milioni kumi (10) walichukuliwa kuwa watumwa. Malipo ya fidia kwa ajili ya mauaji ya Halaiki ya Wayahudi yanaendelea hadi leo. Msaada wa ruzuku kwa serikali ya Uyahudi (Israeli) kutoka Marekani ambao ulianza kutolewa tanga 1948 sasa umefika kiwango cha dola za Kimarekani billion 18. Utafutaji wa watu watuhumiwa wa “makosa ya kivita” ambao yasemekana ndio walio husika kuwaua Wayahudi tangu 1939 hadi 1943 unaendelea hadi leo. Kwa mara ya kwanza Wayahudi walidai fidia mnamo mwaka wa 1951 kiasi cha dola za Kimarekani bilioni (1.5) moja na nusu. Madai haya yalifanyika miaka sita baada ya kukoma Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Ni takribani miaka 140 tangu kupigwa marufuku utumwa katika nchi za Magharibi. Makubaliano yalisainiwa na Chansela akiwakilisha Ujerumani mnamo tarehe 10 Septemba, 1952.

Je uhai wa Mwafrika hauna thamani ya kutosha ili ulipiwe fidia? Majumba ya makumbusho na makaburi makubwa yanajengwa kwa madhumuni ya kuhuisha kumbukumbu ya wale wanaodaiwa “kuuawa kikatili na Manazi wa Kijerumani.” Dunia inalazimishwa kutubu dhambi zake dhidi ya Wayahudi, na pamoja na kisingizio hiki bandia, hakuna uhalali wa hata kidogo unoifanya Israeli kulundika silaha nyingi kiasi hicho kisicho linganishwa. Yeshayahou Lebowtz (Israel and Judaism, Jerusalem, 1987) ameandika kwa ufupi: “Israeli si dola yenye kumiliki jeshi, bali ni jeshi lenye kumiliki dola.”

Utumwa Mambo Leo:

Uendelezaji wa wazi wa aina za utumwa unaweza kufanikiwa kwa njia ya kusaidia Mipango kama vile “Millenium African Recovery Plan.” Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za uzalishaji unaofanywa na “Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba” (Multi Ntional Cartels) tayari upo. Mfumo huu hupenya kwenye kila tabaka la uchumi wa dunia, iwe ni bidhaa zinazo zalishwa, kama sukari, silaha za kivita, madawa ya tiba au biashara ya dhahabu na madini ya platinamu. Utumwa wa kiuchumi kupitia udhibiti mkali wa mtiririko wa mitaji ulimwenguni uko imara mikononi mwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Uharibifu kwa Afrika ulitokea kwa njia ya utawala wa mabavu wa kikoloni wa moja kwa moja, uliofanywa na Uingereza, Udachi, Ufaransa, Ureno na Ubeligiji. Hii ilifu atiwa na udhibiti wa nje ya Afrika, kwa kuanzisha serikali kidhalimu ili kuendelea kudhibiti kwa njia za hila zaidi. Kwa kufichuliwa vibaraka hawa kwa ajili ya ulimwengu kuwaona, ikawa vigumu zaidi kuendelea kwa uwazi kusaidia vitendo vyao viovu dhidi ya jamaa zao. Vurugu zilidhibitiwa ili kuhakikisha kuendelea uingiaji kwenye hakiba kubwa za madini.

Njia changamano ilikuwepo kazini kwa zaidi ya miaka 30, ambayo ni kulitumbukiza bara hili (la Afrika) kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyo na maana yoyote. Ahadi za “kusamehe madeni” zinatolewa kwa lengo la kuendeleza utumwa kwa Waafrika. Huu “Utumwa Mpya” unaweza kuonekana tofauti kwa nje na ule wa West African Slave Trade” (Biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi), lakini misingi yake inafanana. Kwa kuanzishwa kwa mfumo wa makao makuu ya fedha (Benki ya Dunia na shirika la Fedha la Kimaraifa), Polisi wa Dunia (North Atlantic Treaty Organization), imewarahisishia wakoloni kazi ya kuwa na mamlaka ya kuitawala Afrika. Mfano wa wazi unaoonyeshwa na nguvu hizi za wakoloni na washirika wake, ni kuunda taifa la Israeli katikati ya Rasi ya Arabia. Kwa hiyo ni muhimu sisi kuchambua na kuonye sha ulinganifu huu baina ya Uzayuni (Zionism) na washiri ka wake na ukubwa na vipimo vya utumwa unaoendelezwa na nguvu za wanyonyaji.

Kwa hiyo, tumeona ni muhimu kukichapisha kitabu hiki, kiitwacho: “Utumwa, kwa Mtazamo wa Kiislamu na Usio wa Kiisilamu”, kilichoandikwa na Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (ambacho kilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1972).

Kwa madhumuni ya: Kuwataarifu kwa mara nyingine washiriki kwenye Kongamano hili kuujua uovu halisi wa utumwa ambao umekuwa unaendelea kwa karne tano zilizopita.

Kupanua akili za wasomaji na hivyo kutambua jinsi utumwa ulivyogeuzwa na kuwa kama ulivyo sasa katika hali yake ya udanganyifu zaidi, na njama za nchi ya Israeli na Marekani zenye sera za kuuendeleza ili ziweze kutimiza malengo yao ya siri.

“Ahlul Bait (A.S) Foundation of South Africa” inaona fahari kuitambulisha kazi hii rasmi yenye thamani na wanayo matumaini kwamba usiri unaogubika akili zetu utaondolewa na kuamsha akili za watu wote wenye msimamo unaostahili.

Kwa kweli sisi ni wadeni kwa Muadhama Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (Dar es salaam, Tanzania) na kwa unyenyekevu tunashukuru juhudi zake za miongo michache katika kueneza mafundisho ya Uislamu hapa Afrika. Tabia yake ya kisomi imeonekana kwenye mfululizo wa mada nyingi zilizo chapishwa zikijumuisha maelekezo ya jumla kama vile “Haja ya Dini”, hadi kufikia kazi za kisomi kama hii. Bilal Muslim Mission of Tanzania, imefanya kazi kubwa ya kueneza kazi hii na zingine nyingi za maandishi na akawatia moyo Waislamu na wasio Waislamu duniani kote pamoja na Afrika ya Kusini katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Mwenyezi Mungu amzidishie neema hapa duniani na akhera, na tunamwomba Muweza wa yote amjaalie nafasi kubwa zaidi ya kutunufaisha kwa kutumia kalamu yake, Insha-Allah.

Syed Aftab Haider
Ahlul Bait Foundation of South Africa
August 2001.

Neno La Mchapishaji Toleo La Kiswahili

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la “Slavery – Islamic & Western Perspectives kilichoandikwa na Mwanachuoni mkubwa Marhum Allamah Sayyid Sa’eed Akhtar Rizvi.

Kitabu hiki kwa ufupi kinaelezea juu ya biashara ya utumwa ilivyokuwa ikiendeshwa na wazungu hapa Afrika, wakisaidiwa na Kanisa Katoloki na Makinisa mengine yaliyofu-atia. Mwandishi kwa kutumia elimu, akili, mantiki na utafiti wa kina, amefichua ukweli wote uliokuwa umejificha nyuma ya biashara hii ya udhalilishaji wa binadamu. Hapa Afrika na duniani kote, watu wangali wanaamini kwamba biashara ya utumwa hapa Afrika (hususan Afrika ya Mashariki) ilianzishwa na kuendeshwa na Waraabu wakiungwa mkono na Uislamu. Kwa hiyo mbele za watu Uislamu ulionekana kama dini isiyojali ubinadamu, iliyowaswaga mababu zetu kama wanyama na kuwafanya watumwa kwenye nchi zao. Mwandishi anayakanusha yote haya, na kuonyesha jinsi gani Uislamu ulivyokuwa dhidi ya biashara hii ya tumwa, na ulivyofanya ili kukomesha biashara hii. Na kuonyesha jinsi gani Wazungu walivyoing’ang’ania biashara hii, na jinsi Mapadre na Maaskofu walivyozibariki meli zilizokuwa zimebeba watumwa.

Tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu (na wasio kuwa Waislamu) wazungumzaji wa Kiswahili, na hili likiwa ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya ‘Al`Itrah Foundation’ katika kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akh Salman Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu, na kuondokana na dhana hii potofu juu ya biashara ya utumwa.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 1017
Dar-es-Salaam
Tanzania.

Utangulizi Wa Mchapishaji Kwa Toleo La Kwanza La Kiingereza

Utumwa ni moja wapo ya maovu ambayo yamekuwepo katika jamii tangu kuwepo kwa mwanadamu hapa duniani na jitihada za wanamageuzi kujaribu kuuzuia zimeshindwa kwa karne nyingi sana. Ustaarabu wa kale haukuweza kuondoa utumwa, kwa hiyo jamii za wakati huo ziliafiki kuwa nao. Baadhi ya jamii hizo za kistaarabu ziliulea utumwa. Makanisa ya Kikristo yalishiriki katika biashara ya utumwa. Mapadri wao walizibariki meli zilizokuwa zinabeba shehena za binadamu na waliwaonya watumwa kuwa watiifu, lakini hawakuwasihi mabwana wenye kumiliki watumwa kuwa wapole kwa shehena hizo za watu. Hivi karibuni mnamo mwaka 1970 Kanisa Katoliki lilinunua wasichana 1500 kutoka India, eti kwa sababu wasichana wa kizungu huko Ulaya hawakutaka kuishi maisha ya kitawa (usista). Miongoni mwa dini zote ni Uislamu tu ndio ulioharibu misingi yote ya uovu huu. Lakini, ni kejeli ya histo ria kwamba watu walio rutubisha utumwa wakasaidia uendeleaji wake na walifaidika nao, baadaye ndio wakawa mabingwa wa kuukomesha.

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Missioni of Tanzania, amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafi- ti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upendeleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur’ani, hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislamu.

Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi.

Peermahomed Ebrahim Trust kwa fahari kubwa wanakileta kitabu hiki kwa wasomaji na wana matumaini kitakubaliwa na jamii.

Wadhamini,
Peermahomed Ebrahim Trust Karachi, Pakistan
15 Jamadi, 1392
27 June, 1972.

Utangulizi Wa Mwandishi Kwa Toleo La Pili

Kitabu hiki kiliandikwa kwa ombi la marehemu Haji Hasanali P. Ebrahim, ambaye ndiye aliye kichapisha kutoka kwa Peermahomed Ebrahim Trust, Karachi, mnamo mwaka 1972. Mara baada ya kuchapishwa, nakala zote zilinunuliwa, lakini mahitaji yakawa bado yanaendelea.

Kwa kukidhi mahitaji hayo, mwanangu, Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Rizvi sasa ametayarisha toleo la pili.

Baadhi ya mabadiliko madogo madogo yamefanywa katika mpangilio wa Sura; ibara zimeongezwa hapa na pale; na mwanangu ametayarisha maelezo ya ufafanuzi chini ya kurasa, ambayo yameongeza ubora wa kitaaluma wa kitabu hiki. Mwenyezi Mungu na amrefushie maisha na amwongeze nguvu za kuendelea kuutumikia Uislamu wa kweli kwa uaminifu. Pia ninawashukuru marafiki ambao wamenisaidia kwa namna yoyote ile katika kufanikisha kuchapishwa toleo hili:

S.S. A. Rizvi
Gopalpur (India)
28 Novemba 1987.

Utumwa Katika Zama Za Kale

"Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na wanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari." (Qur'an 49:13).

Utumwa sio taasisi iliyoanzishwa na Ukristo au Uislamu. Ni Utumwa ulikuwepo kwa muda mrefu hata kabla ya kuanzishwa hizi dini mbili. Kwa mtazamo wa haraka kuhusu utumwa wa kale, ninamnukuu Jaji Ameer Ali:

“Shughuli ya Utumwa ina rika moja sawa na kuwepo kwa binadamu. Kihistoria dalili zake zinaonekana katika kila zama na kila taifa…Wayahudi, Wayunani, Warumi na Wajerumani wa kale, watu ambao taasisi zao za kisheria na za kijamii zilizoathiriwa mno na tabia na desturi za kisasa, walizitambua na kuzifanya aina zote za utumwa, utumwa wa kazi za kiuchumi na wa kazi za nyumbani. Baada ya kuanzishwa kwa makundi ya washenzi wa Magharibi na Kaskazini katika mabaki ya dola ya Warumi, zaidi ya utumwa wa mtu binafsi, utumwa wa taifa moja kulifanya taifa lingine kuwa mtumwa, ambao haukujulikana sana kwa Warumi, ukashamiri kwenye nchi zote mpya zilizo kaliwa… kanuni za kishenzi, kama zile za Warumi, ziliona utumwa kama hali ya kawaida ya binadamu; na kama mtumwa alipewa ulinzi, ilikuwa kwa sababu mtumwa alikuwa mali inayo milikiwa na bwana wake, ambaye ni yeye peke yake baada ya nchi, alikuwa na mamlaka juu ya uhai na kifo kwa mtumwa.1
Katika nchi ya Uajemi (Persia) ikulu ya Mfalme ilikuwa na watumwa wanawake elfu kumi na mbili. Wakati Mfalme wa Byzantine anaketi kwenye kiti chake cha enzi, maelfu ya watumwa walikuwa tayari kutoa huduma kamili na mamia ya watumwa waliinama kuonyesha heshima wakati mfalme anainama kuvaa viatu. Huko Ugiriki au Uyunani, idadi ya watumwa ilikuwa kubwa zaidi ya watu walio kuwa huru, licha ya kwamba Ugiriki ilitoa watetezi wakubwa wa ubinadamu na haki.

Kila jeshi la Kiyunani ambalo lilirudi nyumbani na salamu za ushindi, lilifuatwa na kuindi la watumwa. Aristotle, mwanasalsafa maarufu wa zamani, alipokuwa anazungumzia suala la iwapo kila mtu alikusudiwa na maumbile kuwa mtumwa au la, anasema: “Hakuna ugumu katika kujibu swali hili, katika misingi yote miwili, ya akili na kweli.

Ya kwamba watu baadhi fulani watawale na wengine watawaliwe si tu kwamba ni jambo muhimu bali ni kitu chenye manufaa kuanzia saa ya kuzaliwa kwao, watu wengine wameumbwa ili wawe watumwa, wako kwa ajili ya kutii tu, na wengine wameumbwa kwa ajili ya kutawala.” Halafu anahitimisha; “…watu wengine kwa asili wako huru, na wengine ni watumwa, na kwa utumwa huu (uliotajwa) wa mwisho, wote ni wenye manufaa na haki.”2 Katika utawala wa Rumi, utumwa wa kale ulifika kilele chake, lakini Dola ya Kirumi ilipoanza kuanguka, watumwa wengi wakaanza kuwa na hali nzuri kwa kiwango kidogo.

Lakini uovu wa utumwa ulionekana wazi kabisa. Uovu huu ulishinda ujuzi wa uhalali wa Kiyunani kama ambavyo imeshinda falasfa stadi ya Kigriki.

Kuonyesha mapenzi kwa watumwa lilionekana si tendo la hisia za kawaida lakini ilikuwa tabia pekee ya mtu mwenyewe binafsi. Mtumwa hakuonekana kama binadamu, hakuwa na haki, hakuwa na roho.3 Wakati huo wa ujio wa Uislamu (mnamo karne ya 7 CE) utumwa ulikwisha enea kote kote huko India, Ajemi, Rumi, Rasi ya Arabia, Romania na Ugiriki. Watu waliokuwa na hali nzuri na nafasi nzuri na wasomi wa nchi hizi hawakuwatilia maanani watumwa kustahiki kupatiwa hata angalao pia haki za msingi za kibinadamu.

Mtumwa alikuwa anaonekana kama bidhaa isiyo na thamani zaidi kuliko hata ya ng’ombe.4 Mara nyingi mtumwa aliuzwa kwa bei rahisi kuliko kondoo na mbuzi. Kwenye hafla maalum za kijamii wageni waheshimiwa wa nchi walikuwa na tabia ya kukusanyika pamoja na Kiongozi wa Nchi kutazama michezo ya kupigana watu na katika michezo hii watumwa walifanywa wapigane kwa kutumia mapanga na mikuki kama vile maonyesho ya mapigano ya jongoo wawili na kware katika kipindi cha zamani cha jamii ya kikabaila. Watu walishangilia kwa kupiga makofi hadi mtu mmoja miongoni mwa wapiganaji aliuawa. Watazamaji walimshangilia sana mshindi.5

Kwa upande mwingine, Rasi ya Arabia ilizunguukwa na nchi ambazo bado zilikuwa na dalili za ufahari wa ustaaraabu wa Kirumi na Kiyunani uliokuwa unaporomoka, na kwa upande mwingine, ilizunguukwa na nchi zilizogubikwa na imani za dini za “Zoroastria” na “Uhindi.” Kama ilivyo tajwa hapo juu, kwenye nchi zote hizi utumwa ni taasisi iliyo tambuliwa.

Vibao kumi na mbili vya maandiko (ya sheria zao) vilitoa mhuri wake rasmi kuithibitisha taasisi hii. Ukali usiopunguka wa matatizo na ukatili ambao watumwa walifanyiwa, haukupungua, lakini, kwa namna yoyote ile, watumwa sasa walikubaliwa kama wanyama (hayawani) ambao hatima yao ilikuwa ni kufanya kazi na kufa tu kwa manufaa ya hao walio wamiliki.

Sina nia ya kukifanya kitabu hiki kuwa historia ya unyama waliofanyiwa watumwa lakini itoshe tu kusema kwamba mtu lazima siku zote abebe hatia katika dhamira yake kwamba wakati fulani alijiingiza kwenye uovu wa utumwa.

 • 1. Ameer Ali, Spirit of Islam (London: University paper back, 1965), PP. 259-261; pia
  angalia Will Duratnt, The Story ofa Civilisation, juzuu ya III (New York, 1944), P.397.
 • 2. Aristotle, Politics, Book one, Sura ya 5 (New York: Modern Library, 1943), uk. 58-60.
 • 3. Durant, W., op.cit., Juzuu ya III uk. 397, Juzuu IV (New York), uk. 29).
 • 4. Ibid
 • 5. Ibid.

Ukristo Na Utumwa

Ingawaje utumwa ulikuwa taasisi ya kale ambayo ilianza kabla ya historia ya binadamu haijaanza kuandikwa, ni salama kusema kwamba ukubwa wa biashara hii ulifika kilele chake kwa kuendelezwa na mataifa ya Kikristo ya Ulaya na Amerika ambao kama ilivyo kawaida yao, waliigeuza kuwa biashara yenye utaratibu uliopangwa kwa uangalifu sana na wakaanza kuwakamata watumwa kwa maelfu. Kabla hatujaanza kutoa maelezo ya biashara hii mbaya sana ya utumwa ambayo ilianzishwa na Wareno, Wahispania na mamlaka zingine za kiubaharia za Kikristo kutoka Magharibi kwa ajili ya makoloni yao mapya, hebu tuangalie kwanza tuone kama Ukristo, kama mfumo na imani, ulifanya lolote wakati wa siku za mwanzo sana kupunguza ukali wa mateso kwa wengi wa watumwa. Jaji Ameer Ali anaandika kuhusu Ukristo:

Ukristo uliona utumwa kuwa ni taasisi iliyo tambuliwa na himaya (dola); na wenyewe ukakubali mfumo huu bila ya hata kujaribu kupunguza uovu wake, au kuahidi kukomesha polepole, au kuboresha hadhi ya watumwa.

Chini ya sheria ya nchi, watumwa walikuwa kama mali inayo hamishika. Waliendelea kuwa hivyo chini ya utawala wa Kikristo.

Utumwa ulishamiri miongoni mwa Warumi tangu zama za kale. Watumwa hao ama wamezaliwa wazalendo au wamezaliwa kutoka nje, ama walipatikana kutokana na ushindi wa vita au kununuliwa, walijulikana kama mali tu ya kuhamishika. Mabwana zao walikuwa na mamlaka na uwezo wa kuamua juu ya uhai au kifo kwao. Ukristo ulishindwa kabisa kukomesha utumwa au kupunguza uovu wake.1

Will Durant anatoa maelezo kuhusu nafasi ya Kanisa kama ifuatavyo. Kanisa halikulaani utumwa. Kanisa la Orthodox na waasi, Kanisa la Rumi na washenzi wote walidhani taasisi hii ilikuwa ya kawaida na haingeharibiwa. Sheria za kipagani zilimwingiza utumwani mwanamke yeyote aliye huru ambaye aliolewa na mtumwa; sheria za Mfalme Constantine (Mfalme Mkristo) ziliamuru mwanamke wa aina hiyo kuuawa kwa kukatwa kichwa, na mtumwa mwanamume kuchomwa moto akiwa bado yu hai.

Mfalme Gratian alitoa amri kwamba mtumwa yeyote aliye mshitaki bwana wake kuhusu kosa lolote isipokuwa uhaini dhidi ya serikali, lazima achomwe moto akiwa bado yu hai mara moja bila hata kufanya uchunguzi ili kupata uhalali wa shitaka.2

Rekebisho moja tu lililoagizwa na Ukristo linaonekana katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa mtu fulani aitwaye Filemoni alipomrudisha mtumwa wake, aliyeitwa Onesimo, na kupendekeza amfanyie wema. Hakuna zaidi ya hapo. Inavutia kuona kwamba neno “slave” (“mtumwa”) la asili ya lugha ya Kiebrania limebadilishwa na kuwa “mtumishi wa nyumbani” kwenye toleo la Biblia liitwalo “Authorised Version of the Bible,” na likabadilishwa kuwa “mtumwa mtumishi” katika toleo liitwalo “Revised Standard Version,” kwa sababu, katika maneno ya “The Concise Bible Commentary,” neno hili (yaani mtumwa) limeachwa kutumiwa kwa sababu ya maana yake.3 Mtu hushanga iwapo mtarjumi anayo haki ya kubadilisha asili ya neno kwa sababu tu ya maana zake au ukumbusho wake?”

Itavutia kuona hapa kwamba neno “slave” (“mtumwa”) ni la asili ya Wazungu. Lilianza kuwapo na kutumika wakati Wajerumani (Franks) walipokuwa wanajishughulisha na kulipatia “Washenzi” soko la watumwa la Wahispania, na mateka hao walio wengi walikuwa Waturuki kutoka jimbo la Slovakia (sasa ni sehemu ya Czecoslovakia).

Watu hawa huitwa “Slav” na kwa hiyo mateka wote wakaitwa “slaves.”

Nukuu ifuatayo inaonyesha dhahiri mtazamo wa Uislamu na Ukristo kuhusu suala la utumwa na rangi ya ngozi: “Mwondoshe mtu mweusi! Siwezi kuzungumza naye,” alisema Archbishop Mkristo aliyeitwa Cyrus wakati Waarabu walioshinda walipowatuma wawakilishi wao wenye uwezo mkubwa ili wazungumze kuhusu makubaliano ya kusalimu amri mji mkuu wa Misri, ujumbe huu wa wawakilishi hawa uliongozwa na mtu mweusi aliyeitwa Ubaydah kama mtu mwenye uwezo mkubwa sana kuliko wote. Archbishop, alishangaa alipoambiwa kwamba mtu huyo mweusi alipewa ukubwa na maelekezo na Generali Amr, na kwamba Waislamu huwapa watu weusi na weupe heshima na daraja sawa na huwahukumia watu kwa tabia na si kwa rangi.4

Tukio hili linakupa tu maelezo kwa ufupi kile ninachotaka kueleza kwa urefu zaidi katika kitabu hiki.

 • 1. Ameer Ali, op. cit., uk. 260-261
 • 2. leeky, W.E. History of European Morals, Juzuu ya II ( New Yolk,
  1926), kama ilivyonukuliwa na Will Durant, op. cit., juzuu ya IV, uik. 77.
 • 3. Clarke, Rev. W. K. L, The Concise Commentary (London: S.P.C.K,
  1952) uk. 976.
 • 4. Leeder, S.S., Veild Mysteries, of Egypt (London, 1912), Uk. 332.

Uislamu Unashambulia Utumwa

Uislamu mara nyingi umeelezwa na waandishi wa Kristo kwamba ni dini ambayo si tu kwamba ilifumbia macho utumwa bali pia iliuhimiza. Hii ni shutuma nzito sana iliyoelekezwa dhidi ya Uislamu, na kwenye kitabu hiki nakusudia kuonyesha uwongo wake. Kama ingewezekana, ningechukua mtizamo wenye huruma kwamba shutuma dhidi ya Uislamu zinatokana na kutokujua ukweli, lakini nahuzunika kuona kwamba wakosoaji wengi wanaonyesha kuwa na mwelekeo wa chuki na uovu. Tumeeleza kwa ufupi msimamo wa Ukristo kuhusu utumwa, na maelezo mengi zaidi yatatolewa baadaye. Hapa, kwa kuanzia ngoja tuuan- galie Uislamu na mfumo wa kanuni zake.

Kwa kadiri utumwa ulivyohusika, Waarabu katika siku za kabla ya Uislamu walikuwa wakosaji wabaya kama majirani zao. Watumwa walikuwa bidhaa ya biashara na utumwa ulikuwa ni asasi iliyokwisha anzishwa. Utumwa ulikuwa chanzo cha kupatia maisha kwa maelfu ya watu na chanzo cha kazi kwa maelfu ya wengi. Kwa watu wenye nafasi nzuri ya maisha idadi ya watumwa ndani ya kaya moja ilikuwa ni alama ya hadhi ya kaya hiyo.

Hii ndio hali iliyo kuwa wakati wa ujio wa Uislamu. Utumwa ulipinga msimamo wa Uisilamu kwa kiasi kikubwa kama ambavyo ibada ya masanamu inavyofanya. Lakini ambapo ibada ya masanamu ina mizizi yake katika mambo ya kiroho na kwa hiyo kuweza kukabiliwa na akili, utumwa mizizi yake ilikuwa katika biashara, katika muundo wa kijamii, katika miradi ya kilimo, na akili peke yake ilikuwa silaha dhaifu ya adui mwenye madhara mno na aliye jikita mizizi yake kwa ndani sana. Ni vipi basi utumwa ungeweza kukomeshwa?

Watu waliofahamishwa vibaya wanaweza kushauri kwamba Mtume wa Uislamu angeliweza kutumia nguvu. Lakini udhaifu wa nguvu kwa madhumuni haya unatambulika vizuri sana kwa wanafunzi wote wa elimu ya jamii wasio na upendeleo. Nguvu inaweza kufanikisha kusalimu amri, lakini bila kuepuka hufanikisha uadui. na mara nyingi uadui ni mkali sana kiasi kwamba mambo mengi mazuri yamepotea wakati nguvu ilipotumika kwa ajili ya maendeleo yake. Hali mbaya ya kusikitisha inayowapata watu weusi wa Marekani, ni mfano mmoja unaoonyesha jinsi gani matumizi ya nguvu yanavyoweza kuwa dhaifu wakati ikiwa lengo ni kupata mageuzi ya kijamii. Ukombozi wa watumwa haukubadilisha msimamo wa watu weupe kwa watumwa wao waliokombolewa, na uchungu ulioje wa urithi wa uhasama wa ubaguzi wa rangi ulioachwa katika jamii! Toynbee ameandika, “Watu weusi ambao walikomolewa kisheria kutoka kwenye utumwa huko Marekani (U.S.A) mnamo mwaka 1862, pamoja na sababu nzuri sasa wanayojisikia kwamba bado, zaidi ya karne moja baadaye, wananyimwa haki kamili za kibinadamu na raia wenzao walio wengi ambao ni Waamerika weupe. 1

Vita vya Uislamu dhidi vya utumwa vililenga kubadili, msimamo na fikira kwa jamii yote, ili kwamba baada ya kukombolewa, watumwa wangekuwa wafuasi wake waliofunzwa na wenye uzoefu wa muda mrefu, bila ya kuwepo na haja yoyote ile ya kufanya maandamano, migomo, maasi ya kijamii na ghasia au fujo za ubaguzi wa rangi.
Na Uislamu ulilipata lengo hili lilioonekana haliwezekani (kupatikana) bila vita yoyote ile kupiganwa. Kusema kwamba Uislamu haukupigana vita kwa sababu ya kukomesha utumwa itakuwa si maelezo sahihi.

Uislamu ulipigana vita kwa sababu ya kuondoa utumwa, lakini, ni vita ambayo ilipiganwa si kwa kutumia upanga, wala hakuna damu iliyomwagika. Uislamu ulilenga vita yake kwenye chimbuko la adui yake (yaani utumwa) na kuunda washirika wake kwa kuamsha hisia zilizo bora zaidi za wafuasi wake. Mashambulizi dhidi ya utumwa yaliendeshwa kwa kulenga pande tatu.

Kwanza, Uislamu ulikataza kununua watumwa na kuwamiliki. Kabla ya kuja kwa Uislamu, utumwa uliendeshwa kiholela. Watu waliokuwa wanadaiwa walifanywa watumwa, mateka wa kivita, ama waliuawa. Kwenye mataifa yaliyo kuwa dhaifu, watu waliwindwa kama wanyama, wakauawa au kutekwa na kufanywa watumwa. Uislamu katika hali isiyo ya utatanishi, uliwakataza wafuasi wake kuwafanya binadamu wenzao watumwa kwa kisingizio chochote kile. Isipokuwa tu kwa yule adui mwabudu sanamu ambaye ametekwa kwenye vita ambayo ilipiganwa ikawa ama ya kujitetea au kwa ruhusa ya Mtume au warithi wake halali. Tofauti hii ilikuwa, kama anavyoieleza Jaji Ameer Ali: “Ili iwe kama dhamana kwa kulinda maisha ya mateka.”2

Kama Allamah Tabatabai alivyokwisha eleza kwa undani na urefu zaidi, kabla ya Uislamu, watu wenye nguvu, na wapendao kutawala wengine kuwa watumwa, walikuwa na desturi ya kuwafanya watumwa binadamu wenzao waliod- haifu bila kusita. Sababu muhimu miongoni mwa sababu nyingi za kuwafanya watu wengine kuwa watumwa ni hizi zifuatazo:

Vita: Mshindi aliweza kufanya chochote anachotaka kwa adui aliye mshinda. Angeweza kuwauwa wapiganaji waliokamatwa mateka, angefanya kuwa watumwa au pengine kuwaweka chini ya mamlaka yake au makucha yake.

Utawala: Mkuu au mtawala angeweza kumtia utumwani, kutegemeana na hiari yake ipendavyo, mtu yeyote aishiye katika himaya yake.

Ulezi: Baba au babu alikuwa na mamlaka yote kwa kizazi chake. Angeweza kumuuza au kumtoa zawadi; angeweza kumwazimisha kwa mtu mwingine, au kubadilishana na mtoto mwingine mvulana au msichana.

Uislamu ulipotokeza, ulibatilisha na kutangulia sababu mbili za mwisho kabisa. Hakuna mtawala au mlezi aliye ruhusiwa kuwafanya raia wake au watoto wake kuwa watumwa wake. kila mtu alipewa haki zake kikamilifu; mtawala na mtawaliwa, mzazi na mtoto walitakiwa kuishi katika mipaka iliyowekwa na dini; hakuna mtu aliye ruhusi- wa kuchupa mipaka hiyo.

Na Uislamu ulikataza kwa ukali sababu ya kwanza, yaani, vita, kwa kuruhusu kuwafanya watumwa wale tu waliotekwa kwenye vita iliyopiganwa dhidi ya adui aliye kafiri. Hapakuwepo na njia nyingine yoyote ambayo mtu angefanywa mtumwa. Wakati huo huo, Uislamu ulinyanyua hadhi ya utumwa na kunfikishia mtumwa hali ya kuwa mtu aliye huru na ukafungua njia nyingi za kuwakomboa watumwa.3

Kabla biashara ya utumwa haijaanza kufanywa katika kiwango kikubwa na watu wa Magharibi (wakati ukoloni ulipoanza), ilikuwa ni katika kupigana vita tu ndipo watu walifanywa mateka. Lakini Uislamu haukuruhusu vita vya uvamizi. Vita vyote vilivyo fanyika wakati wa uhai wa Mtume, vilikuwa vya kujitetea. Si hivyo tu, mbadala ulianzishwa na kuanza kutekelezwa: “Kuwaacha mateka kuwa huru, ama kwa fidia yoyote au bila ya fidia yoyote.” (Qur’ani 47:4)
Kwenye vita vilivyolazimishwa kwa Waislamu, Mtume aliamuru mateka walioangukia kwenye mikono ya Waislamu wafanyiwe wema wa kibinadamu.

Wenye uwezo waliruhusiwa kununua uhuru wao kwa kulipa fedha kidogo, na baadhi yao waliachwa huru bila malipo yoyote.

Yote yalitegemea uamuzi wa Mtume au warithi wake halali, kwa kuzingatia usalama wa Waislamu na ukubwa wa hatari kutoka kwa adui. Mateka wa vita ya kwanza ya Kiislamu, yaani vita ya Badr, walipewa uhuru kwa malipo ya fidia (malipo yalikuwa fedha au kazi ya kufundisha watoto kumi wa Kiislamu kusoma na kuandika), ambapo mateka wa kabila la Tay waliachwa huru bila malipo yoyote yale ya fidia. 4

Hata kwenye utumwa wa aina hiyo palikuwepo na sharti lililoambatanishwa kwamba mama asitenganishwe na mwanae, wala ndugu asitenganishwe na ndugu yake wala mume na mkewe wala mtu na ukoo fulani asitenganishwe na watu wa ukoo wake. Mtume na Imamu wa kwanza wa madhehebu ya Shia, Ali bin Abi Talib, walipitisha adhabu zilizokuwa kali sana kwa mtu yeyote yule aliyemfanya mtu huru kuwa mtumwa: adhabu hiyo ilikuwa kukata mkono wa mhalifu. Ameer Ali anaandika katika kitabu chake kiitwacho “Mohammedan Law:

“Kumiliki mtumwa kwa mujibu wa sheria za Qur’ani ilitegemea na sharti la aina ya vita ambayo Waislamu walipigana, iliyo halisi, halali yaani vita ya kujitetea dhidi ya maadui waabudu masanamu; na iliruhusiwa kwa sababu ya kudhamini ulinzi wa maisha ya mateka… Muhammad aliikuta desturi hiyo ipo miongoni mwa Waarabu wapagani; alipunguza ubaya wa uovu huo, na wakati huo huo akaweka sheria kali kwamba isipokuwa kwa ukaidi wa wafuasi wake, utumwa kama anzisho la kijamii ungekoma kuwepo kwa kusitishwa vita ambazo taifa la Kiislamu lilihusika mwanzoni.

Kukata mwili wa mtu vipande vidogo vidogo pia ilikatazwa kwa dhahiri na Muhammad, na taasisi ambayo ilisitawi huko katika falme ya Ajemi na falme ya Byzantine ilipigwa marufuku na iliwekewa masharti makali sana. Biashara ya utumwa haikujulikana wakati wa utawala wa makhalifa wanne wa mwanzo, “makhalifa waongofu,” kama wanavyoitwa na madhehebu ya Sunni. Hakuna ushahidi hata kidogo, wa kuaminika kimaandishi kwamba kuna mtumwa yeyote alimilikiwa kwa kununuliwa wakati wa utawala wa makhalifa hao.

Lakini baada ya ukoo wa Umayya kuchukua utawala wa ukhalifa, mabadiliko yaliingizwa kwenye msimamo wa Uislamu. Muawiyah ndiye aliyekuwa mtawala wa kwanza Mwislamu ambaye aliingiza katika ulimwengu wa Muhammad (wa Kiislamu) mpango wa kuwapata watumwa kwa njia ya kuwanunua. Pia Muawiyah alikuwa khalifa wa kwanza kutumia mila ya Byzantine ya kuwalinda wanawake zake kwa kutumia watu walio hasiwa. Wakati wa utawala wa ukoo wa Abbas, Imamu wa madhehebu ya Shia, Jafar al- Sadiq alihubiri dhidi ya utumwa, na fikira zake zilikubaliwa na Mutazila. Karmath, ambaye alisitawi wakati wa karne ya tisa kwa kalenda ya Kikristo… anaonyesha aliuona utumwa kuwa kinyume cha sheria.5

Hivyo tunaona kwamba bidii ya Uislamu kujaribu kuwazuia wafuasi wake kupatana na kumiliki watumwa ilikwamishwa na Banu Umayyah. Na lazima niweke kwenye kumbukum- bu kuonyesha fedheha inayo endelea na kugusa idadi kubwa ya Waislamu, hawakujali kabisa maagizo ya Mtume na amri za makatazo za Qur’ani, na Waarabu pia walishirikiana na Wakristo wa Ulaya kwenye biashara inayo chukiza mno ya watumwa ya Afrika ya Mashariki. Biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi, yote ilikuwa katika mikono ya Wakristo wa Ulaya.

Pili, Uislamu ulianzisha kampeni kabambe ya kuwakomboa watumwa. Ukombozi wa watumwa ulitangazwa kuwa fidia ya kulipia dhambi kadhaa. Suala hili linahusiana na sheria za Uislamu lakini, tutaorodhesha chache miongoni mwao ili kuonyesha jinsi gani dhambi ndogo zilisamehewa kwa adhabu ya fidia ya kumwacha mtumwa huru.

Mathalani, kama mtu alishindwa kufunga saumu bila sababu ya maana wakati wa mwezi wa Ramadhani, au kama alishindwa kufunga saumu ya itikafu au kiapo cha nadhiri, na kadhalika, fidia yake ilikuwa kumpa uhuru mtumwa mmoja kila siku aliyokosa kufunga, pamoja na kulipa kwa kufunga saumu baadaye.

Vivyo hivyo, kwa kila kosa la nadhiri, mtumwa mmoja aliachwa huru kama fidia; au kosa la kuchana mtu nguo zake kama kuonyesha huzuni yake mtu kwa kufiwa na mke au mtoto; au kama mwanamke anajipigapiga au kujikata au kuvuta nywele zake kuonyesha huzuni ya kufiwa na yeyote; au kujiua kwa ajali na; wakati mwingine hata kwa sababu ya kumuua Mwislamu kwa kukusudia; au kama mume alimwambia mkewe kwamba alikuwa kwake kama mama yake, na kwa makosa mengine mengi.6

Kutoka kwenye mifano hii, mingine haina uzito lakini ilipenya kwa kina kwenye utamaduni wa Waarabu, mtu anaweza kuona jinsi gani sheria za kidini zilivyofungwa kwa lengo la kuwakomboa watumwa, na hatimaye kukomesha kabisa laana ya utumwa katika jamii.

Inawezekana pia ikahojiwa kwamba kwa kuamrisha ukombozi wa watumwa kama kafara ya dhambi, Uislamu ulikuwa unaruhusu taasisi ya utumwa iendelee kudumu. Hii haikuwa hivyo. Kwa kila namna ya ukombozi wa mtumwa kulikofanywa kama kafara, aina nyingine vile vile ya kafara ilielekezwa badala yake-ikionyeshwa wazi kwamba lengo la Uislamu lilikuwa katika wakati muafaka wa kujenga jamii iliyo huru kutokana na taasisi hii yenye madhara.7

Pia Uisilamu ulitangaza kwamba mwanamke yeyote mtumwa ambaye anazaa mtoto na bwana wake anayemmili- ki, ilikuwa si ruhusa kumuuza, na kama mzazi mwenzake (mmiliki wake) akifa, mwanamke huyo anakuwa huru moja kwa moja.8 Aidha, kinyume na mila zingine zote za huko nyuma, Uislamu uliamuru kwamba mtoto aliyezaliwa na mama mtumwa kutokana na bwana wake anayemmiliki, basi lazima mtoto afuate hadhi ya baba yake.

9Watumwa walipewa haki ya kujikomboa wenyewe ama kwa malipo ya fedha au kufanya kazi kwa mapatano ya kipindi cha makubaliano. Kauli ya makubaliano ya kisheria huitwa mkataba.

Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

الَّذِينَ يَبْتَغُونَ الْكِتَابَ مِمَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ فَكَاتِبُوهُمْ إِنْ عَلِمْتُمْ فِيهِمْ خَيْرًا ۖ وَآتُوهُمْ مِنْ مَالِ اللَّهِ الَّذِي آتَاكُمْ ۚ{33}

“Na wanaotaka kuandikiwa wapate uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni….” (Quran 24:33)

Neno kitab kwenye maana yake ni makubaliano ya maandishi baina ya mtumwa na mmiliki wake unaojulikana kama “Mukatabah – hati ya mkataba.” Jambo la muhimu kwenye mukatabah ni kwamba pale ambapo mtumwa anataka kufanya makubaliano ya maandishi ya aina hii, bwana wake lazima akubali.10 Kwenye aya iliyonukuliwa hapo juu, Mungu amefanya wajibu kwa Waislamu kuwasaidia watumwa katika kujikomboa.

Mtumwa anapotaka kujikomboa, bwana wa mtumwa si tu kwamba akubali, lakini pia anatakiwa amsaidie mtumwa kiasi fulani kutoka kwenye utajiri wake mwenyewe,11 kiasi tu cha utoaji wa kuridhisha katika hali ambayo mtumwa ataweza kuishi maisha ya kuheshimika baada ya kupewa uhuru wake
Hivyo, miaka 1400 iliyopita, Uislamu ulishughulika katika njia ya ufanisi zaidi kuangamiza utumwa. Pia Uisilamu ulielekeza kwamba watumwa waliokuwa wanataka kujikomboa, kuwa uhuru lazima wapewe msaada kutoka hazina ya taifa (baytul mal).12

Hivyo, kama tegemeo la mwisho, Mtume na warithi wake wa haki walitoa fidia ya kuwapa uhuru watumwa kutoka kwenye hazina ya taifa. Qur’ani inatambua ukombozi wa watumwa kama ni njia moja wapo ya ruhusa ya matumizi ya sadaka na misaada. (Angalia (Qur’ani 9: 60, 2:177)

Na inafaa kukumbuka kwamba mtumwa anakuwa uhuru moja kwa moja kama bwana wake akimkata sikio lake au kumpofua jicho lake.13 Pia kama watumwa anayeishi kwenye nchi ya Kiislamu, wakikubali Uislamu mbele ya wamiliki wao, basi, watakuwa huru moja kwa moja.

Kama mtumwa akiwa kipofu au akipata kilema chochote ataachwa huru.14 kwa mujibu wa Imamu Jafar al-Sadiq (amani iwe juu yake.), kama mtumwa ni Mwisilamu na amefanya kazi kwa miaka saba, basi alistahili kupewa uhuru wake.

Kumlazimisha mtumwa huyo kuendelea kufanya kazi hairuhusiwi.15 Ni kwa sababu ya hadithi hii kwamba wanachuoni wa kidini wana maoni kwamba kumpa uhuru mtumwa baada ya kufanya kazi kwa miaka saba ilikuwa ni tendo la wema linalopendekezwa sana.

Kwa nyongeza katika njia hizi za lazima, na za hiyari za kuwakopmboa watumwa, ilitajwa kama muundo safi sana wa sadaka.

Imamu Ali aliwakomboa watumwa elfu moja, aliwanunua kwa fedha yake mwenyewe.16 Imamu wa saba–Musa al-Kazim naye aliwakomboa watumwa elfu moja. Imamu wa nne, Ali bin Al-Husein, alikuwa na tabia ya kumpa uhuru kila mtumwa aliyekuwa chini ya miliki yake kila Sikukuu ya Iddi (adhimisho la kila mwaka la Waislamu.) Ni muhimu kuzingatia kwamba katika matukio yote yaliyotajwa hapo juu, watumwa wote waliopewa uhuru walipatiwa njia za kutosha za kuwawezesha kujipatia riziki katika hali ya kuheshimika.

Uislamu ni ya kwanza na ndio tu dini ambayo iliagiza ukombozi wa watumwa kama jambo jema na likiwa ni sharti la mtu kutambulika kuwa ana imani ya kweli katika kumwamini Mungu. Hakuna dini nyingine zaidi ya Uislamu ambayo ilihubiri na kuamuru kwa njia ipi iliyo bora kabisa kuliko zote ya kuonyesha mapenzi kwa binadamu wenzetu walioko kwenye utumwa. Kwenye sura ya 90 ya Qur’ani, kumwacha mtumwa huru imeagizwa kama msingi mwema na ulio mkuu kabisa wa imani:

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي كَبَدٍ {4}

أَيَحْسَبُ أَنْ لَنْ يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ {5}

يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُبَدًا {6}

أَيَحْسَبُ أَنْ لَمْ يَرَهُ أَحَدٌ {7}

أَلَمْ نَجْعَلْ لَهُ عَيْنَيْنِ {8}

وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ {9}

وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ {10}

فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ {11}

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ {12}

فَكُّ رَقَبَةٍ {13}

“Hakika tumemuumba mtu katika taabu. Je, anahani kwamba hapana yeyote mwenye uwezo juu yake? anasema: Nimeharibu mali nyingi (bure) je, anadhani kwamba hapana yeyote anayemuona? Je, hatukumpa macho mawili? Na ulimi na midomo miwili. Na tuka- muongoza njia mbili Lakini hakupita njia nzito Na nini kitakujulisha njia nzito ni nini! Ni kumwacha huru mtumwa: (Qur’an 90:4-13)

Ni lazima ielezwe kwamba uachaji uhuru mtumwa ni jambo ambalo limependekezwa sana. Uislamu ulidhibiti utumwa kwa njia nzuri, yenye upendo na inayotekelezeka, hivyo kwamba ilifanya kumtunza mtumwa ilikuwa ni wajibu mkubwa sana kwa bwana wake, na wakati huo huo uliamuru kuwajali na kuwatendea wema mkubwa watumwa, hivyo kwamba mara nyingi watumwa walipoachwa huru hawakutaka kuondoka na kutengana na wale walio wamiliki.

Tatu, Uislamu uliwarejeshea watumwa heshima na kunyanyua hadhi zao kijamii. Uislamu haukutofautisha baina ya mtumwa na mtu aliye huru, na wote walitendewa kwa usawa, bila ubaguzi. Ulikuwa ukweli huu kwamba ndiyo siku zote ulivyo wavuta watumwa kwenye Uislamu. Inasikitisha na inaumiza moyo kuona kwamba wale wasioacha makelele yao yasiyo ya haki ya kuukosoa Uisilamu hawataki kuona msimamo huu wa usawa, ambapo hata wakati huu wa kipindi cha kuelimika zipo nchi zenye kutunga sheria zinazobagua umati wa walio wengi, na kuwaweka kwenye hali halisi ya utumwa.

Uislamu hautambui tofauti ya taifa au rangi ya ngozi, nyeusi au nyeupe, raia au wanajeshi, watawala au watawaliwa; wote hawa wapo sawa, si tu kinadharia bali katika hali halisi. Muadhini wa kwanza (mpiga mbiu wa mwito wa Sala) wa Uislamu, mfuasi mtiifu (mpenzi) wa Mtume na sahaba aliyeheshimika sana, alikuwa mtumwa mweusi (Mhabeshi).

Qur’ani inaweka kipimo cha ubora wa mtu kwenye Aya ya 13 Sura ya 49. Maneno haya yameelekezwa kwa binadamu, umati wote wa dunia yote, na yanahubiri undugu asilia wa mwanadamu bila kutofautisha kabila, ukoo, taifa au rangi ya ngozi. Inasema:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ {13}

“Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamune na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa mbali mbali na makabila mbali mbali ili mpate kujuana tu. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari.” (Qur’an 49:13)

Aya hii inaweka wazi mtazamo wa Uislamu kuhusu maisha ya binadamu hapa duniani. Inaweka kigezo kimoja tu cha ubora au hadhi na hicho ni uchaji Mungu, chenye maana ya utiii na unyenyekevu kamili kwa ayapendayo Mwenyezi Mungu. Aya hii inateketeza na kuangamiza kabisa tofauti zote zilizotengenezwa na binadamu na zilizo za bandia kuhusu taifa na rangi ya ngozi, ambazo tunaziona kila mahali duniani kote hadi sasa. Kuelzea ubora wa uchamungu, ngoja tuangalie Mwenyezi Mungu anavyosema:

لَيْسَ الْبِرَّ أَنْ تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ {177}

“Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anayemuami- ni Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao na katika kuwakomboa watumwa na akawa ana shika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita hawa ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.” (Qur’ani 2:177)

Aya hii kwa wazi kabisa inaonyesha kwamba kwa yenyewe, hakuna wema maalum katika kuelekea upande wowote mahususi wakati wa Sala. (Umoja wa Qibla unaonyesha umoja wa imani ambayo hupelekea kwenye umoja wa kiro- ho na kufikia kilele cha ulinganifu wa kimwili.) Imani na ibada iliyoamrishwa katika aya hii ndio wema halisi, na mbali ya kuamriwa na Mungu, zinavutia kwenye fikra za mwanadamu.

Tafadhali zingatia kwamba, “kutoa mali kwa upendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili… wale walioko kwenye utumwa,” ni mojawapo ya wema huo. Katika hadithi ya Imamu Muhammad al-Baqir, inasemekana kwamba mtu anapompiga mtumwa wake (mwanamume au mwanamke), bila ya sababu yoyote ile ya halali, ipo njia moja tu ya fidia ya kosa hilo nayo ni kumpa uhuru hata kama tendo hilo la kupiga lipo katika mipaka iliyowekwa na Mungu.

Katika hadithi nyingine, Zurarah alimuuliza Imamu huyo huyo kuhusu msimamo wa bwana kwa watumwa. Imamu akamjibu kwamba; “kitendo kinachofanywa na watumwa bila kukusudia hakistahili adhabu lakini watumwa wakikataa kumtii bwana wao mfululizo na kwa kukusudia, basi hapo ndipo wanapostahili kuadhibiwa.” Itakuwa ni jambo la kuvutia kwamba, mtumwa alipewa haki ya kumshitaki bwana wake. Hadithi ya tatu kutoka kwa Imamu huyo huyo inasema kwamba mtu mwenye tabia nne zifuatazo atasamehewa dhambi zake na atapandishwa na kuwekwa juu sana katika mazuri ya himaya za Peponi.

(1) Mtu anayempa hifadhi yatima na kumtimizia mahitaji na kumwondolea matatizo yake na anakuwa mwema kwake kama baba yake, anampa mapenzi ya wazazi wake;

(2) mtu aliye mwema na mwenye huruma na anawasaidia wasio na uwezo;

(3) mtu anaye toa matumizi kwa wazazi wake na ni mwenye huruma, mwenye kuwafikiria na kuwaangalia;

(4) na mwisho, mtu ambaye hamkasirikii mtumishi au mtumwa wake na humsaidia kazi ambayo ameamriwa kuifanya na hampi kazi ambazo zipo nje ya uwezo wake kuzifanya.

“Uisilamu umeagiza kwamba bwana amfanyie mtumwa wake kama mmoja wa jamaa ya familia yake, mtumwa lazima apate mahitaji yote ya muhimu katika maisha yake, kama anavyopata mtu mwingine katika familia hiyo. Mtume alikuwa na tabia ya kula pamoja na watumwa na wafanyakazi wake, na kuketi na kuzungumza nao, yeye mwenyewe Mtume hakula chakula kizuri zaidi kuliko wao wala hakuvaa nguo nzuri zaidi kuliko wao, wala hakuwabagua kwa namna yoyote ile.

“Wamiliki wa watumwa walilazimishwa wasiwape shida watumwa wao, ilikuwa si ruhusa kuwatesa, kuwatukana au kutowatendea haki watumwa. Watumwa walipewa fursa ya kuoana wao kwa wao (kwa ruhusa ya wamiliki wao), au na wanamume walio huru au wanawake walio huru. Watumwa waliruhusiwa kutao ushahidi, na kushiriki katika mambo yote pamoja na watu walio huru. Wengi katika wao wali- teuliwa kuwa magavana, makamanda wa jeshi na watawala.

“Mbele ya macho ya Uisilamu, mtumwa mcha Mungu anapewa nafasi ya juu zaidi kuliko mtu aliye huru lakini si mcha Mungu.”17

Imeelezwa kwenye hadithi za kuaminika kutoka kwa Mtume kwamba, bwana ni lazima amlishe mtumwa wake chakula anachokula yeye na amvishe mavazi anayovaa yeye.

Kwenye hotuba yake maarufu aliyo hutubia huko Arafat tarehe 9 Dhul-Hijjah 9 A.H. wakati wa hija yake ya mwisho, Mtume alisema; “…na watumwa wenu, zingatieni kwamba mnawapa chakula mnachokula nyinyi na muwav- ishe nguo ambazo nyinyi mnavaa.

Na kama wakifanya kosa ambalo hungependa kusamehe basi wauzeni, kwani wao ni watumishi wa Mwenyezi Mungu na si vema kuwatesa…” 18

Kusema kwamba Uisilamu uliwatendea watumwa wema kwa mujibu wa msingi wa usawa ni kutokusema ukweli wote.

Kwa sababu, kwa kweli, kwa idadi fulani ya makosa, adhabu inayotolewa kwa mtumwa ilikuwa nusu ya ile iliyotolewa kwa wengine.19 Hii ilikuwa tofauti na jinsi mataifa mengine yalivyo wapa adhabu kali zaidi watumwa kuliko watu wengine.

Profesa Davis anaandika; “Sheria ya makosa ya jinai takriban kila mahali ilikuwa kali zaidi kwa watumwa kuliko watu huru.” 20

Mtume wa Uislamu kila mara aliwasihi wafuasi wake kuwatendea wema watumwa wao kama jamaa wa familia zao. Yeye na familia yake mara kwa mara waliwatendea wema watumishi wao.

Mtumishi mwanamke katika familia ya Fatimah, binti yake Mtume, anasadikisha kwamba, bimkubwa wake (Fatuma) alikuwa na desturi ya kugawana naye kazi zote ngumu za nyumbani na alisisitiza kwamba mtumishi lazima apumzike kila baada ya siku moja ambapo yeye, Fatimah, angefanya kazi zote. Hivyo, palikuwepo na mgawanyo sawa wa kazi baina ya bimkubwa na mfanyakazi wa ndani.

Pia imetaarifiwa kwamba siku moja Ali na mtumishi wake wa kiume Qambar walikwenda dukani ambapo Ali alich- agua nguo mbili, moja ilikuwa nguo ya bei ya chini na hafifu na nyingine nzuri na ghali. Ali alimpa Qambar ile nguo nzuri.

Qambar akashtuka: “Ewe Bwana wangu!” Alisema: “Nguo hii ni nzuri zaidi na wewe ni mtawala wa Waislamu. Chukua wewe nguo hii.”

Ali akajibu, “Hapana, Qambar, wewe ni kijana na vijana sharti wavae nguo nzuri.” Je? kitendo cha namna hii kingemfanya mtumishi ajihisi kuwa yeye ni mtu duni miogoni mwa watumwa?
Wamiliki wa watumwa hawakuruhusiwa kuwapa watumwa wao kazi nyingi kuzidi uwezo wao.

Waliagizwa kamwe wasiwaite watumwa wao wanaume na wanawake kwa majina ya kudhalilisha, lakini badala yake walitakiwa wawaite majina yenye huba zaidi kama: “kijana wangu,” au “msichana wangu wa kazi” iliamriwa pia kwamba watumwa wote lazima wavae nguo na wale chakula sawa na wamiliki wao wa kiume na wa kike.

Iliagizwa pia kwamba katika hali yoyote ile mama asitenganishwe na mtoto wake, wala kaka kutenganishwa na kaka yake, wala baba kutenganishwa na mtoto wake, wala mume kutenganishwa na mkewe, wala ndugu kutenganishwa na ndugu yake.

Sasa ngoja turejee kwenye Qur’an:

وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنْبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ مَنْ كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا {36}

“Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili, na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia (msafiri) aliyeharibikiwa, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi mwenye kiburi, ajivunaye.” (Qur’an 4:36)

Mtukufu Mtume alimpa mtumwa Abu Dharr al-Ghifari kama zawadi yake na akamwambia amtunze katika hali iliyo bora kabisa, ampe chakula kile anachokula yeye, amnunulie nguo zozote zile anazozipenda yeye.

Abu Dharr alikuwa na joho ambalo kwa haraka alilikata vipande viwili, na akampa kipande kimoja mtumwa. Mtume akasema: “vizuri sana!” Abu Dharr akamchukua mtumwa huyo hadi nyumbani kwake na akampa uhuru. Mtume akafurahi sana kwa kiten- do cha Abu Dharr na akasema: “Mungu atakulipa kwa hilo.” Jinsi Imamu wa nne, Zaynul Abidin alivyomtendea – msichana wake mtumwa inajulikana sana katika historia ya Kiisilamu. Wakati fulani ilitokea mtumwa huyo msichana alikuwa anamtengea chakula Imamu, kwa bahati mbaya, akaangusha bakuli lenye mchuzi wa moto na ukamwagika juu yake. Mtumwa huyo wa kike alitambua dhara na mau- mivu aliyomsababishia Imamu. Mtumwa huyo alikuwa anajua tabia ya mtukufu Imamu na akaanza kukariri aya ya Qur’an:

“… Na wazuiao ghadhabu.”
Imamu akajibu:
“Nimejizuia ghadhabu yangu,”
Mtumwa akaendelea:
“Na wanaosamehe watu;”
Imamu akasema:
“Nimekusamhe,”
Hatimaye, mtumwa huyo msichana akasema:
“Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani;”
Imamu akajibu:
“Nimekuacha huru ili nitafute radhi ya Mungu.”

Mtumwa huyo msichana alinukuu maneno hayo kutoka aya ya 134 Sura ya 3 ya Qur’an. Aya hii inasomeka ifuavyo: “Ambao hutoa katika (hali ya) wasaa na katika (hali ya) dhiki, na wajizuiyao ghadhabu na wanaowasamehe watu (na wawafanyiao ihsani); na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani.”

Wakati fulani mtu mmoja alisema kwamba watumwa wa Imamu Zaynul Abidin huambizana wao wakisema kwa wao kwamba walikuwa hawamwogopi bwana wao. Aliposikia habari hii, Imamu alisujudu kwa Mungu kumshukuru na akasema: “Ninamshukuru Mungu kwamba viumbe wake hawaniogopi.” Kutokana na yale ambayo tumeyasema hapo juu lazima ieleweke dhahiri jinsi gani watumwa walivyopendwa na kutendewa wema na Mtukufu Mtume na Maimamu wa Ahlul Bait, na wale waliofuata maamrisho ya Qur’an na mifano iliyowekwa na Mtume na Maimamu.

Kuhusu msimamo wa bwana Mwislamu anaye miliki mtumwa na watumwa wake, Will Durant anasema: “…. Aliwatendea katika hali ya ubinadamu mchangamfu na wa huruma hali iliyowafanya wajione wanafuraha na labda pengine salama zaidi kuliko mfanyakazi wa kiwandani katika kipindi cha karne ya 19 huko Ulaya.” 21

Mwishoni mwa karne ya 18, Mouradgead’ Ohsson (chanzo kikuu cha taarifa cha waandishi wa Magharibi kuhusu ufalme wa Ottoman) alitamka: “Labda pengine hakuna taifa ambalo mateka, watumwa, wavuja jasho katika manchani wana kirimiwa vizuri zaidi au kutendewa wema zaidi ya vile watendewavyo miongoni mwa wafuasi wa Muhammad.” 22

P. L. Rwiere anaandika: “Bwana mwenye kumiliki mtumwa aliamuriwa kumgawia mtumwa wake riziki aliyopewa na Mungu. Lazima itambuliwe kwamba, kwa hili, mafundisho ya Kiisilamu yaliafiki heshima ya namna hiyo kwa utu wa mwanadamu na kuonyesha maana hasa ya usawa ambao ulitafutwa bila kupatikana katika kipindi cha ustaarabu wa kale.”23

Na si katika ustaarabu wa kale tu; hata pia wakati huu wa sasa wa ustaarabu wa Kikristo, imani iliyojengeka ya mam- laka ya juu sana ya kimbari bado ingali inajionyesha kila siku. A.J. Toynbee anasema kwenye kitabu kiitwacho “Civilazation on Trial,” “Kufutika kwa tofauti katika msingi wa kiambari (kitaifa) miongoni mwa Waisilamu ni moja ya mafanikio makubwa kabisa ya Uislamu, na katika dunia ya leo, kama inavyotokea kuna kilio cha haja, kwa ajili kuutangaza na kuueneza wema wa Kiisilamu…”

Halafu anasema kwamba “katika jambo hili la hatari la kuendekeza kujihisi tofauti ya kiambari (kitaifa) hakuwezi hata kidogo kukataliwa kwamba (ushindi wa watu wanaosema Kiingereza) kumekuwa ni balaa.” 24

Napoleon Bonaparte amenukuliwa akisema kuhusu hali ya watumwa kwenye nchi za Kiisilamu: “Mtumwa hurithi mali ya bwana wake na anaweza kumuoa binti yake. Wengi wa watu wa vyeo juu waliwahi kuwa watumwa. Wengi wa Mawaziri Wakuu, wamameluke wote, Ali Ben Mourad Beg, walikuwa watumwa! Walianza maisha yao kwa kufanya kazi za mikono nyumbani kwa wamiliki wao na baadaye walipandishwa katika daraja kwa sifa zao au kwa upendeleo.

Katika nchi za Magharibi, kinyume chake, wakati wote mtumwa wa nyumbani; nafasi yake ni ile ya chini kabisa. Warumi waliwaacha huru watumwa wao, lakini kamwe watumwa walioachwa huru hawakulinganishwa na wazawa. Fikira za watu wa Mashariki na Magharibi zinato fautiana sana hivyo kwamba ilichukuwa kipindi kirefu kuwafanya Wamisri kuelewa kwamba jeshi lote lilijumuisha watumwa walio milikiwa na Sultan al-Kabir.25

 • 1. Toynbee A.J. Mankind and Mother Earth, (N.Y.: Oxford University Press, 1976), uk. 12.
 • 2. Ameer Ali, Muhammadan Law, j. 2, uk. 31.
 • 3. Al-Tabataba’i Sayyid Muhammad Husein, al-Mizan fi Tafsir'l Qur'an, j. 16, toleo la
  pili (Beirut, 1390/1971), uk. 338-358.
 • 4. Al-Waqid, Muhammad bin Umar, Kitabul Maghazi, toleo la M. Jones, j. 1. (London:
  Oxford University Press, 1966), uk. 129; Ibn Sa'd, al-Tabaqatul Kabir, j. 11: 1
  (Leiden: E. j. Brill, 1912), uk. 11, 14.
 • 5. Ameer Ali Muhammadan Law, j. 2, uk. 31-2.
 • 6. Al-Khu'i, Sayyid Abu'l Qasim, Minhajus-Salihin, toleo la tatu, j. 11 (Najaf, 1974), uk.
  328-331, vile vile tazama Qur'an: 4:92, 5:89 na 58:3.
 • 7. Ibid.
 • 8. al-Amili, Hurr, Wasa'ilu'sh-Shi'ah, j. 16 (Tehran, 1983), uk. 128.
 • 9. Ibid.
 • 10. al-Amili, op. cit., j. 16, uk. 101
 • 11. Ibid.
 • 12. Ibid, uk. 121-2
 • 13. Al-Hilli, Muhaqqiq, Sharaya'ul Islam, (kitabul-'Itqad), vile vile tazama Encyclopaedia of
  Islam, j. 1. (Leiden: E. J. Brill, 1960), uk. 31.
 • 14. Ibid., uk.31-3
 • 15. Ibid, uk. 43-4.
 • 16. Ibid., uk. 3.
 • 17. at-Tabataba'i, op, cit, j. 338-358.
 • 18. Ibn Sa'd, op, cit, j. 11:1, p. 133; al-Amili, op. cit., j. 16, 21.
 • 19. al-Amili, op. cit., j. 18, uk. 401f. 527-8, 586-7; j. 19, uk. 73, 154f.
 • 20. Davis, D.B., The problem of Slavery in Western Culture (N. Y: 1969), uk. 60.
 • 21. Hurgronje C.,Muhammedanism, (N.Y., 1916), uk. 128, kama ilivy- onukuliwa na W.
  Durant, the story of Civilization, j. 4. (N.Y., 1960)
 • 22. Kama ilivyonukuliwa katika The Encyclopaedia of Islam, j. 1 uk. 35
 • 23. Riviere P.L., Revue Bleaue (June 1939).
 • 24. Tonbee, A.J., Civilization on Trial (New York, 1948), uk. 205.
 • 25. Cherfils, Banaparte, et l'Islam (Paris, 1914).

Watumwa Katika Historia Ya Uisilamu

Kutoa mfano kuonyesha namna gani Uislamu umenyanyua hali na hadhi ya watumwa na kuwatendea wema kama binadamu badala ya kuwafanya mzigo wa mhayawani (ambavyo ndivyo walivyo fanyiwa kabla ya Uisilamu), hadithi ifuatayo ni yenye mvuto maalum.

Siku moja Mtume aliketi mahali akiwa na Salman, Bilal, Ammar, Shuhayb, Khabbab (wote walikuwa watumwa kabla ya hapo) na kundi la Waisilamu fukara, ambapo watu fulani wasio Waisilamu walipita karibu na hapo.

Walipowaona hawa watu “duni” wapo pamoja na Mtume, walisema, “Umewachagua watu hawa kutoka miongoni mwa watu wako? Unataka sisi tuwafuate wao? Je, Mwenyezi Mungu amewaneemesha wao, hivyo kwamba wao wameamini na sio sisi?

Ni vizuri zaidi utokane nao na usishirikiane nao; ukifanya hivyo, basi labda tunaweza kukufuata wewe.” Mtume hakukubaliana na matakwa yao, na Mwenyezi Mungu akateremsha aya ifuatayo kuhusu suala hili:

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِمْ مِنْ شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِمْ مِنْ شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ {52}

وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُمْ بِبَعْضٍ لِيَقُولُوا أَهَٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنْ بَيْنِنَا ۗ أَلَيْسَ اللَّهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ {53}

وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنْكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِنْ بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ {54}

Wala usiwafukuze wanaomwabudu Mola wao Mlezi asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, (hata uwafukuze). Ukiwafukuza utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu wao kwa wao, ili waseme: Je, hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Je, Mwenyezi Mungu hawajui wanao mshukuru?
Na wanapokujia wanaoziamini ishara zetu waambie: “Asalamu alaikum! Amani iwe juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema…” (Qur’an 6:52 –54)

Salman, Bilal, Ammar na masahaba wao wanasema:

“Wakati Mwenyezi Mungu alipo teremsha aya hizi, Mtume alituelekea sisi, akatuita twende karibu zaidi naye, na akasema; ‘Mola wenu amejiamrishia rehema juu Yake.’ Halafu tulikuwa na kawaida ya kukaa pamoja naye, na alipotaka kusimama (na kuondoka hapo) alifanya hivyo. Halafu Mwenyezi Mungu akateremsha aya:

وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ{28}

“Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni hali ya kuwa wanataka radhi Yake. Wala macho yako yasiwaruke…” (Qur’an 18:28)

“Ulipoteremshwa ufunuo kama huu, Mtume alikuwa na mazoea ya kututaka tuketi karibu naye sana hivyo kwamba mapaja yetu yalikaribia sana kuguuza mapaja yake; na hakusimama kabla yetu. Tulipo hisi muda wake wa kusimama umefika, tulimuomba ruhusa yake kuondoka; na hala- fu alisimama baada ya sisi kwisha kuondoka. Na alikuwa na desturi ya kutuambia; Nina mshukuru Mungu ambaye hakuniondoa hapa duniani mpaka Aliponiamuru kuwa na subira na kikundi cha ummah wangu. Nitakuwa na nyinyi katika maisha yangu, na, baada ya kufariki, nitaendelea kuwa na nyinyi.”1

Ninaorodhesha kwa ufupi majina ya baadhi ya watumwa ambao daraja lao la kiroho limenyanyuliwa juu sana katika Uisilamu na katika jamii ya Kiisilamu, tangu hapo Uisilamu ulipoanza kuwepo:

1. Salman, Muajemi:

Wa kwanza na wa mbele kabisa ni Salman al Farsi (Muajemi). Alikuwa mtoto wa mchungaji wa dini ya Zoroasta katika jimbo la Fars. Tokea mwanzo kabisa, alikuwa na shauku ya kuwa mfuasi wa dini isiyokuwa na nyongeza au pungufu zilizofanywa na binadamu.

Hali hii alikuwa nayo siku nyingi hata kabla ya ujio wa Uislamu.

Akabadili dini ya uzoroasta akaingia kwenye Ukristo, na akawa mtumishi wa mchungaji maarufu mmoja baada ya mwingine akiwa katika harakati ya uchunguzi wa elimu ya kidini. Baada ya kupata matatizo na shida kwa muda mrefu alijihusisha na mtawa mmoja huko Antiokia, ambaye wakati wa kufa kwake, alimpa ushauri kwamba muda muafaka ulikwisha fika wa kuja kwa Mtume wa mwisho hapa duniani.
Akamwambia afanye safari ya kwenda Hijaz, jimbo la Arabuni ambalo ndani yake mna miji ya Makka na Madina. Alipokuwa njiani anaelekea huko, alikamatwa na kuwa mateka na kikundi cha wapiganaji, na akauzwa kutoka bwana mmoja hadi mwingine, hadi akafikisha wamiliki kumi. Hatimaye, alinunuliwa na mwanamke wa Kiyahudi huko Madina. Si rahisi kutoa maelezo ya kina kuhusu mate- so aliyofanyiwa wakati akiwa mateka kwa kipindi kirefu.

Hata hivyo ilionyesha kwamba hatima yake hiyo ilikuwa inamsogeza karibu na lengo lake, kwa sababu ilikuwa kati- ka mji wa Madina alikutana na Mtukufu Mtume wa Uisilamu. Baada ya majaribu magumu Salman alidhihirikiwa ndani ya nafsi yake na “Mtume” yule ambaye alikuwa anangojewa kwa muda mrefu kama ilivyotabiriwa katika Agano Jipya, (Yohana 1: 19-25) akakubali kuwa Mwisilamu.2 Mtukufu Mtume wa Uisilamu akamnunua kutoka kwa bimkubwa wake wa Kiyahudi na akamwacha huru. Ilikuwa ni baada ya vita ya Badr, vita ya kwanza ya Uisilamu, na kabla ya vita ya Uhud.3

Imani, ujuzi na uchaji Mungu wa Salman na mafanikio yake yasiyo na mfano wa kulinganisha, ilimuweka juu ya masahaba wengine wote wa Mtukufu Mtume. Yeye ni mmo- jawapo wa nguzo nne za Waisilamu wa kweli katika dini (pamoja na Abu Dharr al-Ghifari, Miqdad na Ammar.)

Salman anayo sifa pekee ya kujumuishwa kwenye Ahlul Bayt (Nyumba ya Mtume) kwa sababu ya imani na uchaji Mungu wake. Hadithi zinazoonyesha ubora na uadilifu na wema wake haziwezi kuorodheshwa kwenye kitabu hiki kidogo. Hata hivyo, ninazinukuu baadhi ya hadithi hizo ili msomaji apate picha ya haraka ya hadhi yake mbele ya Mtume na warithi wake.

Ingawaje alikwisha ukubali Uislam, Salman hakushiriki kwenye vita ya Badr kwa sababu wakati huo alikuwa bado mateka. Baada ya Badr, alishirki kikamilifu kwenye vita vya kutetea Uisilamu na Waisilamu.

Wakati Quraysh wa Makka na makabila mengine mengi pamoja na Wayahudi wa Madina, walipozingira Madina, Salman ndiye aliye mshauri Mtume kuchimba handaki kuzunguuka mji wa Madina ili liwe kizuizi kwa adui asi- weze kushambulia sehemu dhaifu za jiji. Na ikawa ni kwa sababu hii vita hiyo ikapewa jina la “Vita vya Handaki.”4

Ilikuwa ni kwenye vita hivi ambapo mahojiano ya kirafiki yalipoanza baina ya Muhajirina wa Makka na Ansari wa Madina. Mada ilikuwa: Je, Salman alikuwa Muhajirina au Ansari?

Ansari walidai kwamba kwa kuwa Salman alikwenda kwa Mtume huko Madina, alikuwa kwenye kundi la Ansari; Muhajirina wakadia kwamba kwa sababu Salman aliacha maskani na familia yake; alikuwa Muhajirina.

Ubishi huu wa kirafiki pia unaonyesha jinsi gani daraja la Salman lilikuwa kubwa katika kipindi kifupi cha miaka mitatu ambapo kila kundi lilikuwa linadai kuwa ni mtu wa kundi lao. Vyovyote vile, mgongano huo ulifikishwa kwenye mamlaka ya juu – kwa Mtume, ambaye aliamua kwamba Salman kamwe hakutokana na makundi hayo mawili Muhajirina au Ansari, akasema:

“Salman anatoka kwetu (Nyumba ya Mtume).”5 Ilikuwa heshima kubwa ya aina hiyo ambayo imeendelea kutajwa kwenye hadithi na mashairi. Mshairi anasema:

Moyo wa ibada na utii wa Salman ilikuwa ni jadi yake, ambapo hapakuwepo na uhusiano baina ya Nuhu na mtoto wake.

Mtukufu Mtume pia alisema, “Salman ni bahari isiyokauka na hazina isiyo kwisha. Salman anatoka kwetu, familia (Nyumba ya Mtume), amepewa hekima, na amejaaliwa akili.”6 Imam Ali anasema; “Salman alikuwa kama Luqman, Mtu mwenye Hekima.”7 Wasomi wengi wa Kiisilamu wanafikiri Luqman alikuwa Nabii. Imamu Jafar as-Sadiq alisema Salman ni bora zaidi kuliko Luqman.8 Imamu Muhammad al-Baqir alisema kwamba Salman alitoka kwa watu (Mutawassiman) watu wanaotambua tabia za ndani za watu.)9 Hadithi nyingi zinasema kwamba Salman alikuwa anajua al-Ismul a’dham (jina kuu kabisa la Mwenyezi Mungu);10 na kwamba alitoka kwa Muhaddathin (wale watu ambao malaika huwasemesha.) 11

Kuonyesha ukuu wa Salman, inatosha kwamba Mtume alisema: “Imani ina madaraja kumi, na Salman yupo kwenye daraja la kumi (yaani daraja la juu zaidi), Abu Dharr yupo kwenye daraja la tisa, na Miqdad yupo kwenye daraja la nane.” Wakati wowote malaika Jibril alipomtokea Mtume, alikuwa na kawaida ya kumwomba afikishe salamu za Mwenyezi Mungu kwa Salman na amfundishe elimu ya mambo yajayo. 12

Kwa mujibu wa hali hiyo, Salman alikuwa na desturi ya kumtembelea Mtume wakati wa usiku, ambapo Mtume na Amiri wa Waumini Ali walimfundisha elimu ya siri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo kamwe hakufundishwa mtu mwingine kwa sababu hakuna mtu ambaye angeihimili.

Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Imamu Ali alisema, “Salman alipata ujuzi wa watu wa kwanza na ujuzi wa watu wa mwisho, yeye ni bahari isiyokauka kamwe na anatoka
kwetu Nyumba ya Mtume.”13

Allama Majlisi anaandika kwenye kitabu kiitwacho Aynul l- Hayat kwamba inaeleweka kutoka kwenye hadithi za Shia na Sunni kwamba baada ya masumin hakuna mtu aliye kuwa sawa na Salman, Abu Dharr na Miqdad, miongoni mwa masahaba wa Mtume. Imamu Musa al-Kazim alisema, siku ya ufufuo kuna mtu ataita kwa niaba ya Mwenyezi Mungu kwamba wako wapi hawariyyin na waumini wa Muhammad bin Abdullah, ambao walidumu bila kutetereka kwenye njia waliyoonyeshwa naye na kamwe hawakuvunja mila yake?’ Halafu watafufuka Salman, Miqdad na Abu Dharr.14

Mtukufu Mtume alisema, “Mwenyezi Mungu ameniamuru kuwapenda masahaba wanne miongoni mwa masahaba wangu.” Watu wakauliza ni nani hao masahaba wanne. Mtukufu Mtume akasema, Ali bin Abi Talib, Salman, Miqdad na Abu Dharr.”15

Kwa mujibu wa hadithi, Mwenyezi Mungu alimpelekea Salman makarama na zawadi kutoka Peponi; na Pepo ilim- ngojea kufika kwake kwa shauku kubwa.16

Wakati mmoja Mansur bin Buzurq, yeye mwenyewe akiwa Muajemi alimuuliza Imamu Jafar al-Sadiq kwa nini alikuwa anamkumbuka sana Salman al-Farsi. Imamu akasema: “Usiseme Salman al-Farsi (Muajemi). Sema, Salman wa Muhammad. Sharti ujue kwamba sababu ya mim kumkumbuka sana mtu huyu ni kutokana na tabia zake jema kuu tatu: Kwanza, aliacha matamanio yake binafsi kwanza, na kuzin- gatia yale ya Amiri wa Waumini, Ali.
Pili, aliwapenda fukara na aliwapendelea wao kuliko matajiri. Tatu, alipenda ujuzi na aliwapenda watu wenye elimu. Hakika Salman alikuwa mtumishi mzuri wa Mungu, Mwisilamu safi na hakutokana miongoni mwa washirikina.” 17

Wakati fulani masahaba wa Mtume walikuwa wanasimulia juu ya wahenga wao, wakionyesha fahari kwa nasaba za familia zao. Salman alikuwa miongoni mwao. Umar, ambaye baadaye alikuwa Khalifa wa pili, alimgeukia na kumuuliza aeleze kuhusu jadi yake na nasaba yake.

Salman akasema: “Mimi ni Salman, mtoto wa mtumishi wa Mwenyezi Mungu, nilikuwa fukara na Mwenyezi Mungu akanipa utajiri kupitia kwa Muhammad (s.a.w.), nilikuwa mtumwa, na Mwenyezi Mungu akanipa uhuru kupitia kwa Muhammad (s.a.w.). Hii ndio jadi yangu na daraja langu, Ewe Umar!”18

Kama ambavyo imekwishaelezwa huko nyuma kwamba Abu Dharr mwenyewe alikuwa mmoja wapo wa nguzo kuu nne za dini (imani) na alikuwa kwenye daraja la tisa la imani. Lakini hata Abu Dharr hakuweza kumwelewa Salman sawasawa.

Wakati fulani Abu Dharr alikwenda nyumbani kwa Salman. Salman aliweka chungu cha kupikia chenye maji katika moto. Wakaendelea na mazungumzo lakini kufumba na kufumbua chungu kilianguka chini na kujifunika.

Lakini ajabu ya majabu, hakuna hata tone moja la maji lililodondoka kutoka kwenye chungu, na Salman akakirejesha chungu kile motoni tena. Baada ya muda tukio hilo likajirudia tena. Hakuna tone la maji lililodondoka, na Salman akakirejesha chungu kwenye moto bila papara.

Abu Dharr akaduwaa. Kwa haraka akatoka nje na akaku- tana na Imamu Ali njiani. Alimsimulia yale aliyoyaona. Ali akasema” “Ewe Abu Dharr, kama Salman atakujulisha mambo yote anayo yajua, utashangaa. Ewe Abu Dharr, Salman ni lango la kuingia kuelekea kwa Mwenyezi Mungu hapa duniani. Yeyote anaye mkubali Salman ni muumini, yeyote anaye mkataa ni kafiri. Salman anatoka kwetu – Nyumba ya Mtume.”19

Nadhani hadithi hizi chache na za kuaminika zinatosha kuonyesha daraja la juu sana la Salman mbele ya Mwenyezi Mungu, mbele ya Mtume, Imamu Ali na warithi wake.

Salman akateuliwa kuwa gavana wa Iran, alikwenda Madain, makao makuu ya serikali ya wakati huo. Watu wa Madain, kwa kipindi kirefu walizoea kuona fahari na utukufu wa baraza la wafalme wa Iran, walikuwa wanangojea msafara wa kifahari. Lakini hakuna msafara uliotokea. Badala yake, mzee mmoja, alikuwa amebeba vitu begani anatembea kwa mguu anawaelekea wao.

Wakamuuliza huyo mgeni kama aliuona msafara wa gavana. Mgeni huyo akasema: “Mimi ndiyo gavana wenu.” Na huyo gavana mwenye moyo mkunjufu wa Madain alitawala kwa aina yake ya ujuzi, huruma, haki na umadhubuti hivyo kwamba mnamo kipindi kifupi, Madain yote ilikuwa chini ya mamlaka yake. Ushindi huo haukufanywa na polisi au jeshi la wapiganaji, bali kwa uwezo wa ukamilifu wake wa kiroho, uchaji Mungu na ustahamilivu.

Salman alifariki dunia mnamo mwaka wa 36 A.H. huko Madain (Madyan). Imamu Ali alisafiri kutoka Madina kwenda Madain (Madyan) kwa muda wa nusu siku kimiujiza ili aweze kutekeleza ibada ya mazishi ya sahaba na ndugu yake wa kuaminika.20

Hii ilikuwa heshima ya pekee ya Salman. Kaburi la Salman huko Madain (Madyan- Iraq) hutembelewa na mamia ya mahujaji kila siku. Hija (ziyara) iliyowekwa inaonyesha ukuu wake kwa Mwenyezi Mungu.

2. Zayd Bin Harithah

Zayd bin Harithah bin Sharahil al-Kalbi, mvulana wa Kiarabu, alitekwa nyara wakati wa utoto wake na akauzwa kama mtumwa.

Jambo hili lililotokea kabla ya kuja kwa Uisilamu. Hakim bin Hizam bin Khuwaylid ndiye aliye mnunua kwenye soko la Ukaz, na akampeleka kwa shangazi yake, Khadijah binti Khuwaylid, ambaye naye alimpa Mtukufu Mtume.21

Baba yake Zayd alikuwa anamtafuta mwanae. Baada ya muda mrefu akagundua kwamba Zayd alikuwa Makka. Alikwenda Makka na akaamua kutoa fidia kwa ajili ya kumkomboa mwanae Zayd. Mtume alisema kwamba kama Zayd anataka kuungana na familia yake, hakuna haja ya kulipa fidia yoyote. Alikuwa huru kuondoka. Lakini Zayd hakutaka kwenda na baba yake na akapendelea kubaki na Muhammad. Harithah, baba yake Zayd, alisikitika sana na akasema; “Ewe mwanangu, wewe unapenda kuendelea kumwacha baba yako na mama yako kwa ajili ya Muhammad?” Zayd akasema: “Yale ambayo nimeyaona katika maisha ya Muhammad ndio yanayo nilazimisha kwamba nisimwache kwa ajili ya mtu mwingine yeyote.”

Msimamo wa aina hiyo wa mapenzi kwa Mtukufu Mtume uligusa nyoyo za wote wale waliomjua baadaye. Na ilikuwa tabia hii ya pekee ya kutenda wema ambayo ilifanya takriban bara Arabu yote kuukubali Uisilamu katika kipindi kifupi cha miaka ishirini na tatu.

Vyovyote vile, Harithah alishangazwa na akatangaza kwenye Kaabah kwamba tangu hapo na kuendelea wala yeye hakuwa baba yake Zayd ama Zayd kuwa mwanae.

Ni hapo ambapo Mtume Muhammad akatangaza kwenye hijr Ismail (pembeni mwa Kaabah) kwamba: “Ninatangaza kwamba tangu sasa na kuendelea Zayd ni mwanangu.” Harithah, aliposikia taarifa hii, akarudi nyumbani kwake bila huzuni. 22

Zayd bin Harithah sasa aliitwa Zayd bin Muhammad. Ubini huu uliendelea hadi mwaka 5 A.H. ambapo aya ifuatayo iliteremshwa:

مَا جَعَلَ اللَّهُ لِرَجُلٍ مِنْ قَلْبَيْنِ فِي جَوْفِهِ ۚ وَمَا جَعَلَ أَزْوَاجَكُمُ اللَّائِي تُظَاهِرُونَ مِنْهُنَّ أُمَّهَاتِكُمْ ۚ وَمَا جَعَلَ أَدْعِيَاءَكُمْ أَبْنَاءَكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ قَوْلُكُمْ بِأَفْوَاهِكُمْ ۖ وَاللَّهُ يَقُولُ الْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِي السَّبِيلَ {4}

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ ۚ فَإِنْ لَمْ تَعْلَمُوا آبَاءَهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ وَمَوَالِيكُمْ ۚ وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُمْ بِهِ وَلَٰكِنْ مَا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا {5}

“Mwenyezi Mungu hakumwekea mwanadamu nyoyo mbili kifuani mwake. Wala hakuwafanya wake zenu ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayesema kweli, naye ndiye anaye ongoza njia. Waiteni kwa (ubini wa) baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu…” (Qur’an 33:4-5)

Halafu Zayd kwa mara nyingine akaitwa Zayd bin Harithah23 Mtume alikwisha muoza Zayd kwa binamu yake Zainab binti Jahash, ambaye alikuwa bint wa shangazi yake Umaymah.24 Wana ndoa hawa wawili walianza kugombana, na Zayd akamtaliki Zainab, kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Mtume akamuoa Zainab yeye mwenyewe.

(Wakati huo Zainab alikuwa na umri wa zaidi ya miaka hamsini.25 Ukweli huu peke yake unatosha kusafisha utando mnene wa hadithi zenye nia mbaya ambazo maadui wa Mtume wamesingizia kuhusu ndoa hii takatifu.)

Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qur’an:

فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ إِذَا قَضَوْا مِنْهُنَّ وَطَرًا ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّهِ مَفْعُولًا {37}

“…Basi Zayd alipokwisha haja naye alikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watakapokuwa wamekwisha timiza nao shuruti za talaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.” (Qur’an 33:37)

Kwa hizi ndoa mbili za Zainab bin Jahash, kanuni mbili za kipagani ziliondolewa:

Kwa ndoa ya kwanza, fikira ya imani ya kuwa taifa fulani ni bora kuliko nyingine au imani kwamba kuwa mtumwa au mtumwa aliyeachiwa huru ilikuwa fedheha kuhusu hadhi ya watu, ilifutwa.26

Na kuhusu ndoa ya pili, imani ya kwamba mtoto wa kiume wa kupanga alikuwa mtoto halisi, ilisitishwa. Mtume mwenyewe alimuoa mwanamke aliyetalikiwa na mwanae wa kiume wa kupanga, sasa ni vipi liwepo dai la kusema kwamba mtoto wa kupanga alikuwa mtoto halisi wa kuzaa? Kwa hiyo, desturi ya Kiarabu ambayo ilimtambua mtoto wa kupanga kama mtoto halisi iliondolewa kabisa. 27

Zayd ni mtu mmoja tu miongoni mwa masahaba wa Mtume ambaye ametajwa kwa jina ndani ya Qur’ani. Alikuwa mtu wa tatu kuingia katika Uisilamu baada ya Khadija binti Khuwaylid na Ali bin Abi Talib. Zayd alikuwa kamanda wa jeshi la Kiisilamu lililopelekwa kupigana na majeshi ya Kikristo huko Muta. Baada ya kifo cha kishahidi cha Zayd, Jafar, binamu yake Mtume, akashika nafasi ya kamanda badala ya Zayd, naye pia alikutana na kifo cha aina hiyo hiyo.28
.
Zayd alikuwa na mtoto, Usamah, aliyemzaa na mke wake wa kwanza, Umm Ayman. Usamah alikuwa na umri wa miaka 19 alipoteuliwa kuwa kamanda wa jeshi ambalo lilijumuisha masahaba wote mashuhuri wa Mtume, pamoja na Abu Bakr, Umari na Uthman.

Masahaba wengine walipodharau uteuzi wake, Mtume aliwakaripia kwa kusema: “Zayd alikuwa mbora zaidi yenu, na mwanae Usamah pia ni mbora zaidi kuliko nyinyi wote.” Usamah aliamuriwa na Mtume kwenda na jeshi kulipa kisasi cha kifo cha baba yake huko Muta. 29

3. Ammar Bin Yasir:

Alikuwa mmoja wapo wa masahaba walio heshimiwa mno wa Mtume na mfuasi mwaminifu wa Imam Ali. Ammar alikuwa miongoni mwa wale walio teswa kikatili kwa ajili ya Uisilamu. Alihama kwenda Ethiopia30 mara mbili na Madina, alisali kuelekea qibla mbili yaani Baytul Maqdis na Ka’ba. Alishiriki kwenye vita zote za Kiisilamu tangu mwanzo,31 na aliuawa kishahidi kwenye vita ya Siffin mnamo tarehe 9. Safar, mwaka wa 3 A.H. Ammar na wazazi wake walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwa Waisilamu.
Baba yake, Yasir alikuwa mtu wa kabila la Qahtan kutoka Yemen. Yeye pamoja na kaka zake wawili, walikwenda Makka kwa madhumuni ya kumtafuta kaka yao aliyepotea. Kaka zake walirudi kwao Yemen lakini Yasir akakaa Makka ambapo alifanya mkataba na Abu Hudhayfah (wa kabila la Bani Makhzum), na akamuoa mtumwa wake msichana, Sumayyah binti Khayyat. Yasir na Sumayyah walizaa watoto wawili, Abdulah na Ammar, ambao kwa mujibu wa mila za Kiarabu waliwekwa katika daraja la watumwa wa Abu Hudhayfah. 32

Baada ya kuingia kwenye Uisilamu, Abu Jahl, akisaidiwa na wapagani wengine, akaanza kuitesa familia yote kikatili.

Misumari ya chuma iliwekwa kwenye miili yao na wakalazimishwa kulala chini kwenye mchanga wa jangawani wenye joto kali. Joto la jua na mchanga wa jangwa lilisababisha misumari ya chuma kuwa na joto kama moto; ngozi zao ziliungua. Mateso haya kwa kawaida yaliendelezwa hadi wahusika kupoteza fahamu. Halafu misumari ya chuma iliondolewa na wakamwagiwa maji. 33

Mtume alisikitishwa sana na mateso ya familia hiyo; lakini alikuwa hana uwezo wa kuwasaidia. Hata hivyo alikuwa na desturi ya kwenda karibu nao na kuwapa moyo wa kustahamili uonevu wa watesaji wao. Aliwapa salamu nzuri sana za Peponi na kusema: “Kuwemi wavumilivu, Enyi familia ya Yasir, kwa sababu mnayo nafasi nzuri iliyotayarishwa kwa ajili yenu Peponi. 34

Yasir na Sumayyah waliuawa kikatili na wapagani wa kabi- la la Quraysh, waliongozwa na Abu Jahl. Hii ni sifa kubwa ya familia hii ya kuheshimiwa kwa ajili ya Uisilamu. Sumayyah alikuwa mchamungu sana na mwanamke aliye muogopa Mungu; alikuwa mwanamke wa kwanza kufa kishahidi kwa ajili ya Uisilamu.

Wazazi wa Ammar, walipouawa, Ammar alijifanya kukana Uisilamu, na kitendo hicho kilimwokoa. Halafu akaenda kwa Mtume huku analia kwa uchungu kwamba alilazimika kutamka maneno ya kufuru ili aweze kutoroka kutoka mikononi mwa makafiri.

Mtume alimwambia asiwe na wasiwasi, kwani hakusema maneno hayo kwa dhati ya moyoni mwake. Kwa mujibu wa tukio hili aya ifuatayo iliteremka:

مَنْ كَفَرَ بِاللَّهِ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَٰكِنْ مَنْ شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِنَ اللَّهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ {106}

“Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake – isipokuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa.” (Qur’an 16:106)35

Ammar aliposimulia maovu aliyofanyiwa Sumayyah aliye rehemewa, Mtume akasema, uvumilivu, “Ewe Abu Yaqzan; Ewe Mwenyezi Mungu, usimghadhibikie na kumwadhibu kwa moto wa jahanamu yeyote kutoka katika familia ya Yasir.” (Mtume alipokwenda Madina, na msikiti wake (Mtume) ulikuwa unajengwa, Ammar alikuwa anabeba mizigo ya mawe mara mbili zaidi ya kawaida kwa shauku kubwa.

Wakati huo huo alikuwa anakariri beti fulani za mashairi, ujumbe uliomo kwenye beti hizo ulimfikia Uthman (ambaye baadaye aliteuliwa kuwa khalifa wa tatu) ambaye alidhani kwamba Ammar alikuwa ana mdhihaki. Uthman alipozidiwa na kutokuelewa kwake, alimpiga Ammar usoni hadi damu ikatoka kwa kasi na akakinga ili damu isitoke kwa wingi.

Ammar akalalamika kwa Mtume, ambaye mwenyewe alilisafisha na kulifunga jeraha na akasema: “Ammar ni ngozi baina ya macho yangu na pua yangu.”

Halafu akasema: “Sawa, Ewe Ammar, utauawa na kundi la waasi, wewe utakuwa unawaita watu hao waje Peponi na wao watakuwa wanakuita uende Jahanamu.” 36

Umashuhuri na heshima ya Ammar inaweza pia kufuatiliwa kutoka kwenye matamko yafuatayo ya Mtume: “Ammar yuko pamoja na ukweli, na ukweli upo pamoja na Ammar popote pale atakapokuwa.

Ammar ni ngozi baina ya macho yangu na pua yangu; na atauawa na kundi la waasi.”37 Pia Mtume alisema; “Ammar amejaa imani kutoka utosini hadi unyayoni (miguuni).”38 Zipo hadithi nyingine nyingi za Mtume na Maimamu kuhusu Ammar.

Ammar alikuwa mmojawapo wa masahaba wenye imani ambaye siku zote alimfuata Imamu Ali. Mnamo mwaka wa 35 A.H. wakati Ammar na wengine wengi, walipinga sera ya Uthman bin Affan (Khalifa wa tatu) kuhusu mgawo wa hazina ya taifa, Khalifa Uthman aliagiza apigwe, akapigwa sana bila huruma hivyo kwamba mishipa ya tumbo lake ilipasukana ikasabaisha ugonjwa wa chango la ngiri (henia).39

Kama alivyo kuwa baba yake, Yasir alikuwa mshiriki wa Banu Makhzum, kwa hiyo wakamchukua Ammar nyumbani kwao (akiwa bado hana fahamu) na wakasema kwamba kama Ammar akifa wangelipa kisasi chake kwa Uthman. Kama ambavyo imekwishaelezwa hapo juu, Mtume alikwisha sema kwamba Ammar angeuawa na kundi lililoasi; na ndivyo ilivyotokea.

Ammar aliuawa mnamo 37 A.H. na jeshi la Muawiyah bin Abu Sufyan. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 90 au 91. Siku hiyo alipouawa kifo cha kishahidi, alikuwa anapi- gana kijasiri kabisa dhidi ya jeshi la Muawiyah, wakati mtu mmoja kutoka Syria, Abu Ghandiyah al-Muzani, alimjeruhi vibaya kiunoni; marafiki zake wakambeba na kumpeleka mahali pa salama. Akaomba maji; mtu mmoja akampa kikombe cha maziwa. Ammar akasema: “Usemi wa Mtume ulikuwa wa kweli.” Watu wakamwomba awaeleze. Akajibu, “Mtume aliniaarifu kwamba riziki yangu ya mwisho hapa duniani ni maziwa.” Basi akanywa maziwa na baadaye akafa.40

Amiri wa Waumini Ali alipata taarifa hiyo kuhusu msiba huo. Alitoka nje haraka na akakiegemeza kichwa cha Ammar kwenye mapaja yake. Na akakariri wasifu ufuatao kwa ajili ya sahaba wake mwaminifu:

Ee kifo, ambacho kinakuja kwangu kwa vyovyote;
Afadhali unipumzishe haraka;
Kwa sababu umewamaliza marafiki zangu wote;
Ninaona kwamba wewe unawatambua marafiki zangu wapendwa wote,
Kama vile mtu anakuongoza kwao kwa lengo maalum.”

Kisha baada ya kukariri: “Hakika sisi tumetoka kwa Mungu na tutarudi kwa Mungu,” akasema: “Mtu yeyote ambaye hakuhuzunishwa sana kutokana na kifo cha Ammar hana fungu katika Uisilamu. Mungu na amrehemu Ammar.” Amiri wa Waumini aliisalia maiti yake na akamzika kwa mikono yake. 41

Kifo cha kishahidi cha Ammar, kilimsababishia matatizo Muawiyah kwa sababu watu wengi katika jeshi lake walikumbuka usemi wa Mtume, na wakatambua kwamba kifo cha Ammar, kilionyesha kwamba Muawiyah na jeshi lake walikuwa waasi na hawakuwa katika njia iliyo sahihi. Akiwa katika jitihada za kutuliza jeshi lake, Muawiyah akasema kwamba Ali ndiye aliye sababisha kifo cha Ammar kwa sababu yeye ndiye aliyempeleka kwenye uwanja wa vita. Amiri wa Waumini aliposikia taarifa hii ya ujanja wa Muawiyah, akasema: “Basi, ni Mtume mwenyewe ndiye aliye muua Hamzah kwa kumpeleka kwenye uwanja wa vita wa Uhud!” 42

4. Miytham Al-Tammar:

Miytham al-Tammar (muuza tende), mtoto wa kiume wa Yahya, alikuwa mtumwa aliyenunuliwa na Imamu Ali. Lakini watu wachache sana walijua kwamba alikuwa mtumwa kwa sababu Ali alimpa uhuru na akawa rafiki mkubwa na wa karibu sana wa bwana wake wa zamani. Miytham alijumuishwa kwenye kundi la hawariyyun. Maana yake “Mwanafunzi” kama ilivyokuwa kwa wanafun- zi kumi na mbili wa Isa.

Imamu Ali alimfundisha Miytham elimu ya siri ya Allah, na akampa utambuzi wa mambo yajayo. Miytham akajua undani wa kifo, mateso ya wakati ujao, ambayo nyakati nyingine alikuwa anawaelezea watu na watu walimcheka, lakini matukio yaliyotokea baadaye yalithibitisha kuwa alikuwa sahihi.

Ali alipomnunua. Miytham, alikuwa anaitwa Salim. Ali akamwambia kwamba alisikia kutoka kwa Mtume kwamba “baba yako alikwita Miytham huko Ajemi (Iran).” Miytham alishangaa kwa sababu hakuna mtu aliyejua jina hilo hapo Arabuni. Halafu Ali akamwambia aendelee kutumia jina lake la mwanzo; hivyo akaanza kuitwa Miytham tena, na akampanga mtu aitwaye Abu Salim43

Miytham alikuwa mchamungu sana. Imeandikwa kwamba; “…yeye (Miytham) Mweneyzi Mungu na amwie radhi, alikuwa miongoni mwa watu wachajimungu sana na ngozi yake ilikaukia mwilini mwake (kwa sababu ya kufunga saumu na sala za mfululizo.)”

Abu Khalid al-Tammar anasema kwamba siku moja ya Ijumaa walikuwa wanasafiri kwa mashua katika mto wa Frati (Euphrates), ambao dharuba ilizidi kuwa kubwa, Miytham alitazama juu na akawaambia wateremshe nanga na kuisalimisha mashua kwa sababu dalili zilionyesha kwamba dharuba ingekuwa na nguvu sana. Halafu akasema kwamba takriban katika muda huo huo Muawiyah alifariki dunia. Watu waliandika tarehe hiyo, ambayo baadaye ilithibitika kuwa sahihi. 44

Shaykh Kashshi anasimulia kwamba siku moja Miytham al- Tamar alikuwa anapita karibu na kundi la watu wa kabila la Asad, wakati Habib bin Muzahir alifika hapo.

Wakasimama na kuanza kuzungumza. Habib akasema: “Imekuwa kama vile ninamtazama mzee (ambaye anakipara na ambaye ana tumbo kubwa, na anauza tende na matikiti maji) kwamba amekamatwa, na maadui zake wamemsulubu kwa sababu ya kuipenda familia ya Mtume halafu wameto- boa tumbo lake.’ Sifa zote hizo zilikuwa zalengwa kwa Miytham, ni sifa zake.”

Miytham akajibu: “Mimi pia ninamtazama mtu (ambaye uso wake ni mwekundu) ambaye atakuja kumsaidia mtoto wa Mtume na atauawa kishahidi na kichwa chake kitapelek- wa Kufah.” Alimaanisha Habib bin Muzahir.

Halafu kila mmoja wao alielekea njia yake. Watu waliosikia mazungumzo haya wakasema kwamba walikuwa hawajapata kuona mtu yeyote muongo zaidi kama hao wawili (Miytham na Habib.)

Wakati huo huo Rushayd al-Hujri (ambaye pia alikuwa miongoni mwa marafiki wa karibu sana wa Imamu Ali na alipewa ujuzi wa mambo yajayo) alifika hapo na akauliza kama walimuona Habib kwa dhihaka. Rushayd akasema “Mwenyezi Mungu na amwie radhi Miytham! Alisahau kusema kwamba mtu ambaye angekipata kichwa cha huyo mtu mwenye uso mwekundu angepata dinari mia moja zaidi ya wengine kama zawadi.” Rushayd alipoondoka watu wakasema kwamba yeye alikuwa muongo zaidi ya wale wawili.45 Baada ya muda mfupi utabiri wote ulitimia kikamilifu: Miytham alisulubishwa, Habib aliuawa kishahidi huko Karbala, na mtu aliyepeleka kichwa cha Habib, Kufah alizawadiwa dinari mia moja zaidi.

Amiri wa Waumini Ali alikwisha mwambia Miytham: “Baada yangu, utakamatwa na watakusulubu na wataku- choma kwa mkuki siku ya tatu damu itatokea puani na mdomoni na ndevu zako zitakuwa nyekundu kwa sababu ya kudondokewa na damu yako.

Sharti ungoje rangi hiyo ya nywele. Watakusulubu mlango- ni kwa Amr bin Hurayth na wenzako tisa; na msalaba wako utakuwa mfupi kuliko mingine lakini hadhi yako kwa Mwenyezi Mungu itakuwa ya juu zaidi. Njoo; nikuonyeshe mti ambao utatumika kukusulubu wewe.” Halafu akam- wonyesha Miytham mti huo.46

Hadithi nyingine inasema kwamba Ali bin Abi Talib alimuuliza Miytham; “Utakuwa na msimamo gani hapo wakati mwanaharamu katili wa Bani Umayyah (yaani Ubaydullah bin Ziyad) atakulazimisha kunilaani na kunitukana mimi?”

Miytham akasema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kamwe sitafanya hivyo.” Ali akasema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu usipokubali kufanya hivyo watakuua na kukusulubu.” Miytham akasema kwamba angevumilia maovu yote hayo, na kwamba mateso ya aina hiyo hayawi chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu. Halafu Ali akampa biashara zenye kheri: “Ewe Miytham, utakuwa pamoja nami kwenye daraja langu huko peponi.”47

Baada ya Ali kuuawa kishahidi, Miytham alifanya tabia ya kwenda karibu na mti huo na kusali hapo. Alikuwa akisema, “Mwenyezi Mungu na akuneemeshe wewe, Ewe mti; nimeumbwa kwa ajili yako, na wewe unakua kwa ajili yangu.” Kila alipokutana na Amr bin Hurayth, alimwambia: “Ninapotembelea jirani na kwako, lazima ukumbuke haki yangu kwamba mimi ni jirani yako.” 48

Mnamo mwaka wa 60 A.H. Miytham alikwenda Umrah (hija ndogo). Kule Madina alitembelea nyumba ya Umm Salamah, mke wa Mtume.Alipojitambulisha, Umm Salamah akasema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mara nyingi nilimsikia Mtume anakupendekeza wewe kwa Ali bin Abi Talib usiku wa manane.”

Miytham alikuwa na haraka hivyo alimwambia Umm Salamah afikishe salamu zake kwa Imamu Husein na amwambie kwamba baada ya muda mfupi “tutakutana kwa Mwenyezi Mungu.”

Umm Salamah akamwambia mfanyakazi wake kupaka mafuta uzuri kwenye ndevu za Miytham. Kupaka mafuta uzuri kwenye ndevu ilikuwa alama ya kuonyesha heshima ya juu kwa mhusika katika mila za Kiarabu.

Baada ya hapo Miytham akasema: “Ewe Mama wa Waaminio, umepaka mafuta uzuri kwenye ndevu zangu; lakini muda mfupi ujao zitapakwa rangi ya damu yangu kwa ajili ya kuwapenda nyinyi, Ahlul Bayt.” Umm Salamah akasema kwamba Imamu Husein alikuwa anamkubuka yeye sana. Miytham akasema: “Mimi pia nina mkumbuka kila mara; lakini sasa hivi nina haraka,a na kuna hatima inayotungojea mimi na yeye, na wote tutafika hapo.”

Alipotoka nje, Miytham akakutana na Abdullah bin Abbas na akamwambia amuulize chochote kila alichotaka kujua kutoka kwenye tafsiri ya Qur’ani, kwani “Nimesoma Qur’an kutoka kwa Amiri wa Waaminio na ninajua sehemu mbili kuteremka kwake (tanzil) na tafsiri (tawil).” Bin Abbas akaomba karatasi na wino na akaanza kuandika imla ya Miytham. Kwamba mtu wa daraja la Abdullah bin Abbas hakudharau kuandika imla ya Miytham inaonyesha heshima kubwa aliyopewa katika kundi la wenye elimu ndani ya jamii ya Kiisilamu49

Halafu Miytham akasema: “Hisia zako zitakuwaje, Ewe Bin Abbas, utakaponiona mimi ninauawa kishahidi na wenzangu tisa?”

Bin Abbas aliposikia taarifa hii, akaanza kuchana karatasi, huku akisema kwamba Miytham amekuwa mchawi. Miytham akasema, Usipasue karatasi hiyo. Endapo utona kwamba yale niliyokwambia hayajatokea, basi utakuwa na muda mwingi sana wa kupasua karatasi hiyo50

Baada ya umrah, Miytham akarudi Kufah. Wakati alipokuwa safarini, Ubaydullah bin Ziyad aliteuliwa kuwa gavana wa Kufah. Siku moja Ubaydullah akamuuliza mpasha habari wa kitongoji jijini Kufah kuhusu Miytham. Alipoambiwa kwamba Miytham alikwenda umrah, akamwambia mpasha habari huyo kwamba kama angeshindwa kumleta (kumtoa) Miytham, angeuawa yeye badala yake. kwa hiyo, mpasha habari alikwenda Qadisiyyah kumngoja Miytham. Alipofika Qadisiyyah, Miytham akakamatwa na kufikishwa kwa Bin Ziyad. Watu wakamwambia Bin Ziyad kwamba Miytham alikuwa karibu sana na Ali bin Abi Talib kuliko wote. Bin Ziyad akashangaa: “Hivi Ali alikuwa anamwamini huyu Mwajemi (asiye Mwarabu) sana?” Halafu mazungumzo yaliendelea ifuatavyo:

Bin Ziyad: “Yu wapi mlinzi wako?”
Miytham: “Anawangojea waovu, na wewe ni mmoja wao.”
Bin Ziyad: “Unadiriki kusema hivyo mbele yangu? Sasa unayo njia moja tu ya kuokoa maisha yako: lazima umlaani Abu Turab.”
Miytham: “Simjui Abu Turab ni nani.”
Bin Ziyad: “Mtukane na umlaani Ali bin Abi Talib.” Miytham: “Utafanya nini nikikataa?”
Bin Ziyad: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu nitakuua.”
Miytham: “Bwana wangu (yaani Ali) aliwahi kunitaarifu kwamba wewe ungeniua na kunifanya mimi na wengine tisa kuwa mashahidi, pale kwenye mlango wa nyumba ya Amr bin Hurayth.”
Bin Ziyad: “Sitafanya hivyo kuthibitisha kwamba bwana wako ni muongo.”
Miytham: “Bwana wangu hakusema uongo wowote. Chochote kile alichosema, alisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume, ambaye naye alisikia kutoka kwa malaika Jibril, ambaye naye alisikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Jinsi gani wewe utathibitisha uongo wao? Si hivi tu, hata ninajua jinsi utakavyoniua na mahali utakapo nifanya mimi shahidi. Na ninajua kwamba nitakuwa mtu wa kwanza katika Uislamu ambaye atafungwa hatamu mdomoni ili nisiongee na mtu wa kwanza ambaye ulimi wake utakatwa.”

Bin Ziyad akamfunga jela Miytham na Mukhtar bin Abu Ubaydah al-Thaqafi. Miytham akamtaarifu Mukhtar kwam- ba yeye angeachiwa huru na kwamba angelipa kisasi cha damu ya Imamu Husein na angemuua mtu huyu (yaani Bin Ziyad.) Na ilitokea kwamba Mukhtar alipochukuliwa kwenda kuuawa, mjumbe alifika hapo kutoka kwa Yazid akiwa na amri ya kumwachia huru Mukhtar.

Halafu Miytham akatolewa nje na akasulubiwa kwenye mti uliokuwa mlangoni kwa Amr bin Hurayth. Sasa ndipo Amr akaelewa nini ilikuwa maana ya ombi lakeMiytham, na kwa hiyo, alimuamuru mtumishi wake kuchoma ubani kwenye msalaba wake na kufagia ardhi chini yake.

Miytham akaugeuza msalaba kuwa mimbari. Akaanza kusimulia hadithi za Mtukufu Mtume akizikweza sifa na ubora wa Ahlul Bait, na pia hadithi kuhusu uovu wa Banu Umayyah na kulaaniwa kwao katika Qur’an na hadithi, na jinsi watakavyo angamizwa.

Bin Ziyad aliarifiwa kuhusu ujasiri huu usio wa kawaida na moyo wa kujitolea wa Miytham. Alihofu isije mihadhara ya Miytham ikawafanya umma kuwapinga Banu Umayya na kuwafedhehesha mbele ya watu. Kwa hiyo aliamuru kwamba mdomo wa Miytham ufungwe hatamu ili asiongee. Baada ya muda, ulimi wake ulikatwa.

Siku ya tatu, mtu mmoja akamjeruhi Miytham kwa mkuki akisema: “Ninakujeruhi licha ya kwamba ninatambua kwamba kila mara ulifunga saumu wakati wa mchana na unasimama usiku kucha ukisali.”

Jioni ya siku hiyo damu ilitokea puani na mdomoni, ikafanya uso na kifua chake kuwa na rangi nyekundu, na akafariki dunia. Miytham aliuawa kishahidi kwa ajili ya Uislamu, siku kumi kabla ya Imamu Husein hajafika Karbala. Maana yake ni kwamba Miytham alikufa tarehe 21 au 22 Dhul hijjah, 60 A.H. Wakati wa usiku wauza tende saba waliuchukua mwili wake kwa siri na kumzika kwenye ukingo wa mfereji na kufuta alama za kaburi.51

Baadaye wakati hapakuwepo na hatari, kaburi lilidhihirishwa kwa watu. Leo hii imekuwa ni sehemu ya heshima kubwa ambapo wafuasi wa dini huenda kuhiji.

Neema mojawapo ya Mwenyezi Mungu aliyopewa Miytham ilikuwa kwamba elimu na uchajimungu ilibakia kwa dhuria wake, kizazi hata kizazi. Watoto wake, wajukuu zake na vitukuu vyake walikuwa miongoni mwa masahaba wa kuheshimiwa na Maimamu wa Kishia. Miytham alikuwa na watoto sita: Muhammad, Shuayb, Salih, Ali, Imran na Hamzah. Wote walikuwa miongoni mwa masaha- ba wa Imamu wa nne, tano na sita.

Miongoni mwa wajukuu zake, Ismail, Yaqub na Ibrahim (wote watoto wa Shuayb) walikuwa masahaba wa Imamu wa tano, sita na saba. Ali bin Ismail bin Shuayb bin Miytham anahesabiwa miongoni mwa wana theolojia mashuhuri wa madhehebu ya Shia. Mazungumzo yake na maadui zake yanaonyesha ujuzi, akili yake na uimara wa akili yake. Zaidi ya hayo tunaona majina mengine mengi miongoni mwa dhuria wa Miytham yametajwa kwenye vitabu vya hadithi na wasifu.

5. Bilal Al-Habashi:

Bilal al-Habashi (mtu wa Ethiopia) alikuwa muadhini wa kwanza wa Mtume. Baba yake alikuwa Riyah, na mama yake Jumanah, na lakabu yake ni Abu Abdillah na Abu Umar. Alikuwa mmojawapo wa kundi la watu waliosilimu mwanzoni kabisa. Alishiriki katika vita ya Badr, Uhud, Khandaq na zingine.52

Bilal alikuwa mtumwa wa kwanza wa Safwan bin Umayyah. Wakati wa utumwa wake, aliteswa kinyama kwa sababu ya imani yake. Aliamuriwa kulala chini kwenye mchanga wa jangwa la Arabia unaounguza akiwa uchi, jiwe zito liliwekwa juu ya kifua chake na kumfanya asipumue kwa urahisi. Na kama vile hiyo haikutosha, watu wane sana walitumia kuruka juu ya jiwe hilo, katika jaribio la kutaka kumuua kwa njia hiyo. Hata hivyo, sauti moja tu ilisikika kutoka kwa Bilal nayo ni (Mungu Mmoja! Mungu Mmoja!)Ahad! Ahad! 53

Mtume alipoona ukatili aliokuwa anafanyiwa Bilal, alisikitika sana. Abu Bakr akamnunua na kumwachia huru Bilal. Mnamo mwaka wa 2 A.H. wakati adhana (wito wa kwenda kusali) ilipoamriwa, Bilal alipewa heshima ya kuadhini.54

Baadaye, watu fulani walishauri kwamba heshima hii angepewa mtu mwingine, kwa sababu Bilal hakuweza kutamka herufi ya Kiarabu “shin” kwa lafudhi ya Kiarabu. Mtume akasema; “Hii ‘sin’ ya Bilal ni ‘shin’ inayosikika kwa Mungu.” Mwenyezi Mungu hatazami umbile lilivyo, Yeye hupendezwa na utakatifu wa moyo.

Wakati mmoja Bilal alikwenda kwa Mtukufu Mtume na akakariri beti ya shairi kwa lugha yake akimsifu Mtume. Mtume akamtaka Hassan bin Thabit al-Ansari kutafsiri katika lugha ya Kiarabu.

Hassan akasema:
“Tabia bora zinapoelezwa nchini kwetu,
Wewe unaonekana kuwa kigezo chetu.”

Ni ukweli unaojulikana sana kwamba Mtume alikuwa na tabia ya ucheshi inayopendeza licha ya kwamba hata kwenye misemo ya uchekeshaji alikuwa mkweli. Siku moja bimkubwa mmoja hapo Madina alimwomba amwombee kwa Mwenyezi Mungu ampatie sehemu ya makazi huko Peponi. Mtume akasema; “Wanawake wazee (vikongwe) hawataingia Peponi.” Bi kizee huyo aliondoka akiwa analia. Bilal akamwona na akamuuliza kwa nini alikuwa analia. Bimkubwa huyo akasimulia mkasa wote. Bilal akaenda naye kwa Mtume, na akasema: “Mwanamke huyu ames- imulia hivi na hivi kutoka kwako?” Mtume akasema: “Hata watu weusi hawataingia Peponi.”

Sasa hata Bilal akaanza kulia. Halafu Abbas, mjomba wake Mtume akafika hapo na alipoelewa kuhusu mkasa huo, akajaribu kuingilia kati kwa kuzungumza na Mtume, ambaye alimwambia kwamba hata mzee mwanamume hataingia peponi. Abbas naye alipojumuika katika kundi la wenye kulia, Mtume akawaambia wawe na furaha kwa sababu Mwenyezi Mungu atawaumba kuwa vijana tena na wenye nyuso zinazo ng’ara na halafu wataingia peponi.55

Bilal alikuwa mpenzi wa Ahlul Bayt. Imamu Jafar al-Sadiq amenukuliwa kusema: “Mungu na amneemeshe Bilal! Alitupenda sisi, watu wa Nyumba ya Mtume, na alikuwa mchaji Mungu bora sana miongoni mwa waja wake Mwenyezi Mungu.”

Imeandikwa katika Kamil Bahai kwamba Bilal hakuadhini au kukimu sala wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr,56 na hakutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr kama Khalifa. Shaykh Abu Jafar al-Tusi amesimulia kwenye Ikhtiyar al-Rijal taarifa isemayo kwamba Bilal alikataa kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr; na Umari alikamata vazi lake lililotengenezwa kwa ngozi na akasema: “Hii ni zawadi ya Abu Bakr; alikuachia huru na sasa unakataa kutoa kiapo cha utii kwake?”

Bilal akasema: “Kama Abu Bakr alinikomboa kwenye utumwa kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu, basi na aniachie niendelee na kumcha Mwenyezi Mungu; na kama aliniachia huru kwa sababu ya kumtumikia yeye, basi nipo tayari kumpatia huduma zihitajikazo. Lakini sitatoa kiapo cha utii kwa mtu ambaye Mjumbe wa Mungu hakum- teua kuwa Khalifa wake.” Umari akamkaripia sana akasema:

“Hutakiwi kuwa na sisi hapa.” Hii ndio sababu baada ya kutawafu Mtume, Bilal
akahamia Syria.
Baadhi ya mashairi yake kuhusu mada hii ni kama ifuatavyo:
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Sikumgeukia Abu Bakr,
Kama Mwenyezi Mungu hangenilinda, fisi wangesimama miguuni mwangu.
Mwenyezi Mungu amenipa wema na Ameniheshimu,
Hakika kuna wema mwingi sana kwa Mwenyezi Mungu.
Hutaniona nina mfuata mtu wa bidaa,
Kwa sababu mimi siendekezi bidaa kama wao.”

Mwandishi wa Istiab anaandika, “Alipo tawafu Mtume, Bilal alitaka kwenda Syria. Abu Bakr akamwambia abaki Madina ili amtumikie yeye (binafsi).

Bilal akasema: “Kama umenipa uhuru kwa ajili ya kukutumikia wewe, basi nikamate niwe mateka tena; lakini kama uliniondoa kwenye utumwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi niache niende katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Abu Bakr akamwacha aendelee na mipango yake.”57

Bilal alifariki dunia huko Dameski kwa ugonjwa wa tauni mnamo mwaka wa 18 A.H. au 20 A.H. na akazikwa huko Bab Saghir.58 Kaburi lake huko Dameski hutembelewa na maelfu ya Waisilamu waaminifu kila mwaka.

Fizzah:

Fizzah al-Nubiyyah (kutoka Nuba, sasa iko ndani ya nchi ya Sudan) pia amepata sifa njema ya milele kwa ajili ya kuji- tolea kwake katika Uislamu na kuwapenda Ahlul Bayt. Mwanzoni, alimtumikia Fatimah, binti yake Mtume.

Ilipangwa na Mtume kwamba siku moja Fatimah angefanya kazi za ndani wakati Fizzah angepumzika, na siku iliyofuata Fizzah afanye kazi ambapo Fatima naye anapumzika.

Baada ya kifo cha Fatimah, Ali akamuoza Fizzah kwa Abu Thalabah al-Habashi. Akazaa naye mtoto wa kiume, na halafu Abu Thalabah akafariki dunia. Baadaye Fizzah akaolewa na Malik al-Ghatathan. Siku moja Malik akalalamika kwa Umari kuhusu Fizzah.

Umari akasema; “Unywele ambao chimbuko lake ni familia ya Abu Talib unayo elimu zaidi kuliko Adi.”59(Adi lilikuwa kabila la Umari)

Fizzah alikuza familia yake mwenyewe; lakini aliendelea kuwapenda Ahlul Bayt. Yeye, kwa hiyari yake mwenyewe, alikwenda na Husein hadi Karbala naye akapata masum- buko makali na mateso yaliyo wapata familia ya Imamu Husein.

Elimu yake ya Kitabu Kitukufu, cha Qur’an, anasifiwa kati- ka dunia ya Kiisilamu. Imetaarifiwa kwamba angalau kwa miaka yake ishirini ya mwisho wa uhai wake, hakutamka neno lingine lolote isipokuwa Qur’an; na kila mara alizungumza kwa kukariri aya za Qur’an.

Kipande kimoja cha kuvutia cha mazungumzo kinanukuliwa hapa kwa lengo la kuonyesha ujuzi wake wa pekee.

Abul Qasim al-Qushayri anamnukuu mtu wa kuaminika kwamba wakati mmoja aliachwa nyuma na msafara wake na akawa anasafiri peke yake. Katika jangwa, alimwona mwanamke na akamuuliza yeye alikuwa nani. Mwanamke akakariri aya ya Qur’an:

فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ {89}

“Basi wasamehe na uwaambie (maneno ya) Amani: Hivi karibuni watajua. (Qur’an 43:89)

Akagundua kosa lake, na halafu akauliza: Unafanya nini hapa?
Mwanamke:

وَمَنْ يَهْدِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ مُضِلٍّ ۗ{37}

“Na wale ambao Mungu huwaongoza hakuna atakaye wapotosha.” (Qur’an 39:37)

Mwanamume: “Wewe ni jini au mwanadamu?” Mwanamke:

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ{31}

“Enyi wana wa Adamu! Vaeni mavazi yenu mazuri kila wakati wa sala na mahali pa sala.” (Qur’an 7: 31)

Mwanamume: “Unatoka wapi?” Mwanamke:

“Hao wanaitwa na hali ya kuwa wako mbali kabisa” (41:44) Mwanamume: “Unakwenda wapi?”

Mwanamke:

وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ{97}

“Na Mwenyezi Mungu, amewajibishia watu wafanye Hija katika Nyumba hiyo, kwa wale wenye uwezo wa kugharamia safari.” (Qur’an 3:97)

Mwanamume: “Siku ngapi zimepita tangu uachwe na msa- fara?”

Mwanamke:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ{38}

“Na kwa hakika tuliumba mbingu na dunia na vyote viliv yomo ndani humokwa muda wa siku sita.” (Qur’an 50:38)

Mwanamume: “Unataka chakula?” Mwanamke:

وَمَا جَعَلْنَاهُمْ جَسَدًا لَا يَأْكُلُونَ{8}

Wala hakuwapa wao miili ambayo haikuhitaji chakula.” (Qur’an 21:8)

Hivyo mwanamume akampa mwanamke huyo chakula. Baada ya hapo mwanamume akamwambia mwanamke akimbie haraka. Mwanamke akasema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ{286}

“Mungu haibebeshi nafsi yoyote mzigo isiyoweza kuubeba.” (Qur’an 2:286)

Hivyo mwanamume akamwambia mwanamke aketi kwenye ngamia nyuma yake. Lilikuwa jibu lililotoka kwa mwanamke huyo:

لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّهُ لَفَسَدَتَا ۚ{22}

“Kama pangekuwepo, miungu wengine (mbinguni na ardhini), zaidi ya Mungu Mmoja, pangekuwepo machafuko pande zote mbili. (Qur’an 21:22)

Aliposikia hivi alishuka chini kutoka kwenye ngamia na akamwomba mwanamke apande juu ya ngamia, na amwendeshe yeye. Alipoketi juu ya ngamia, mwanamke huyo akakariri aya hii:

وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ {13}

“Utukufu uwe kwake Yeye ambaye amemtiisha kiumbe huyu ili tumtumie, kwani hatungeweza kusafiri mwendo mrefu sisi wenyewe.” (Qur’an 43:13)

Baada ya muda si mrefu, wakaungana na msafara. Mwanamume akamuuliza mwanamke kama alikuwa na ndugu miongoni mwa wasafiri kwenye msafara huo. Mwanamke akasema: “Ewe Dawud! Hakika tumekufanya wewe uwe khalifa hapa duniani; Muhammad ni Mtume tu; Ewe Yahya kishike kitabu kwa nguvu zote; Ewe Musa, Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi!” (38:26, 3:144, 19:21, 20:11-12.)

Mwanamke akaita majina haya, na akawaona vijana wanne wanakimbia kuelekea kwake. Hapo hapo akamuuliza mwanamke huyo uhusiano wake na vijana hao. Mwanamke huyo alisoma aya hii:

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ{46}

“Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia hii.” (Qur’an 18:46)

Wakati huo watoto hao wakafika hapo; mama akawaambia watoto wake:

يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ {26}

“Ewe baba yangu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumua- jiri ni mwenye nguvu na mwaminifu.” (Qur’an 28:26).

Watoto wa mama huyo wakampa mwanamume aliyekuja hapo na mama yao ujira kwa ajili ya usumbufu na huduma. Lakini mama wa watoto hao akaona ujira huo ulikuwa mdogo, kwa hiyo akasema:

وَاللَّهُ يُضَاعِفُ لِمَنْ يَشَاءُ ۗ{261}

“Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye.” (Qur’an 2:261).

Kwa hiyo, wanawe wakaongeza ujira wa mwanamume. (Upo uwezekano mkubwa sana kwamba watoto hawa wa kiume baba yao ni mume wa pili wa Fizzah, Malik al Ghatathani.)

Mwanamume huyo akawauliza watoto hao wa kiume mama huyo alikuwa nani. Wakamwambia kwamba alikuwa Fizah, mtumishi wa Fatimah, binti yake Mtume na kwamba tangu miaka ishirini iliyopita alikuwa hajasema neno lolo isipokuwa Qur’an 60

7. Qambar:

Mara nyingi jina la Qambar limetajwa kwenye hadithi. Na amepewa sifa za daima na beti za shairi lifuatalo la Imamu Ali: “Nilipoona jambo ambalo ni kinyume cha sheria, Niliwasha moto na kumwita Qambar.

Mtu mmoja alimuuliza Qambar bwana wake alikuwa nani. Qambar alielezea sifa za Imamu Ali bin Abi Talib kwa namna ya dhahiri na ya kupendeza hivyo kwamba limenakiliwa na muhadithin bila kubadili hata kidogo.61.
Kwa sababu haki haiwezi kutendeka kwayo katika kulitafsiri, ninaiacha hotuba hiyo. Nimekwisha sema jinsi Qambar alivyokuwa anatendewa wema kwa mapenzi na Imamu Ali. Baada ya kifo cha Imamu, Qambar alikuwa na desturi ya kusimulia kwamba alikuwa ana mtumikia bwana wake mara chache sana kwa sababu Imamu Ali alikuwa akifanya kazi zake yeye mwenyewe; alikuwa anachota maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku, alikuwa anafua nguo zake mwenyewe, alikuwa hata anashona nguo zake mwenyewe wakati ihitajikapo; alikuwa anachota maji kisimani yeye mwenyewe kwa matumizi yake ya kila siku; alikuwa anawalisha chakula kizuri na nguo nzuri lakini yeye mwenyewe alikuwa anavaa na kula kama mtu fukara. Mara nyingi alitumia usemi wa: “jihisi upo nyumbani mtoto.”

Qambar alikuwa na desturi ya kusema: “Ni katika siku moja tu alinikasirikia. Ilikuwa wakati nilipomwonyesha fedha nilizoziweka kama akiba yangu ya matumizi ya baadaye. Fedha hiyo ilikuwa mafungu ya kipato nilichopewa na watu wengine na zawadi nilizopewa na watu wa familia yake. Nilikuwa nimekusanya dinari mia moja. Nilipo mwonyesha kiasi hicho cha fedha, alionekana kukasirika, na kilicho niumiza mimi zaidi, Ali alionekana na huzuni.”

Qambar akamuuliza kwa nini alikuwa na huzuni hivyo. Ali akajibu ‘Qambar, kama ulikuwa huna utumizi na fedha, je, hakuna watu jirani yako ambao wana hitaji fedha?

Baadhi yao pengine wanakufa njaa, wengine pengine ni wagonjwa na walio dhaifu. Je, usingeweza kuwasaidia (kwa fedha hiyo?). Sikufikiria kama ungekuwa huna huruma kiasi hicho na unapenda utajiri kwa ajili ya kuwa tajiri.

Qambar nina hofu hufanyi jitihada ya kujaribu kupata faida kutoka kwenye Uislamu; jaribu sana kwa dhamira hasa na kwa moyo safi. Ziondoe sarafu hizo nyumbani mwangu.” Qambar akagawa fedha hizo kwa masikini haraka sana na kwa wahitaji, Qambar alikwisha achwa huru na Imamu Ali, lakini aliamua kuendelea kubaki naye.

Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi, gavana aliyeteuliwa na Abdul Malik bin Marwan kutawala Iraq, alikuwa katili aliyekuwa na tabia ya kujivuna kwamba, “Kitu kitamu kuliko vyote hapa duniani ninacho kitamani ni kuua.” Jina lake limekuwa methali kwenye uovu. Aliua watu 120,000 ambao kosa lao lilikuwa kumpenda Ali bin Abi Talib na Ahlu Bayt. Idadi hii haijumuishi wale watu walio uawa na yeye kwenye vita. Alijaribu sana kuwamaliza Shia wa Ali kutoka Iraq. Said bin Jubayr na Kumayl bin Ziyad ni waathirika wake wawili.

Wakati fulani Hajjaj aliuliza, “Yupo aliye bakia miongoni mwa wafuasi wa Abu Turab (yaani Ali) ili niweze kumrid- hisha Mwenyezi Mungu kwa kumuua?” Akajibiwa kwa kuambiwa kwamba alikuwepo Qambar, mtumwa wake.

Hivyo Qambar, aliye mtu mzee sana, alikamatwa na akafik- ishwa kwake. Halafu mazungumzo yalikuwa kama ifu- atavyo baina ya Hajjaj na Qambar:

Hajja: “Wewe ni mtumwa wa Ali?”
Qambar: “Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na Ali ni mfadhili wangu.”
Hajjaj: “Kazi yako ilikuwa nini ulipokuwa unamtumikia Ali.”
Qambar: “Kazi yangu ilikuwa kumpa maji ya kutawadha ili apate udhu.”
Hajjaj: “Ali alikuwa akikariri nini baada ya kutawadha?” Qambar: “Ali alikuwa na tabia ya kukariri aya hii: “Basi walipo sahau walio kumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipo furahia yale waliyo pewa tuli- washika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa.” (6:44)
Hajjaj: “Nadhani ni sisi alio maanisha kujumuishwa kwenye aya hii?”
Qambar: “Ndio.”
Hajjaj: “Ni vema uache dini ya Ali.”
Qambar: “Kabla sijaacha dini hii, niambieni dini gani ni nzuri zaidi kuliko yake.”
Hajjaj: “Utafanya nini kama nikikukata kichwa chako?” Qambar: “Basi itakuwa ni bahati njema kwangu na bahati mbaya kwako.”
Kwenye hadithi nyingine swali hili la mwisho na jibu lake limenukuliwa tofatui.
Hajjaj: “Hakika nina taka kukuua. Ni vema uchague namna yako mwenyewe ya kufa.”
Qambar: “Ni juu yako. Niue kwa namna yoyote unayotaka, kwa sababu nitakuua kwa njia hiyo hiyo Siku ya Hukumu. Na, ni jambo la ukweli kwamba bwana wangu alikwisha niambia kwamba ungeniua kwa kunikata kichwa.”

Hajjaj akaamuru akatwe kichwa Qambar aliuawa kifo cha kishahidi kwa ajili ya imani yake. Leo hii kaburi lake huko Baghdad ni mahali panapotembelewa na maelfu ya mahujaji62

8. Said:

Said, mtumwa mwingine wa Ali bin Abi Talib, anasema kwamba ilikuwa siku moja ya joto kali, Ali alikuwa na shughuli ya kuandika barua. Akataka kumtuma Said aende kuwaita baadhi ya maofisa wake. Akamwita mara ya kwan- za, pili, tatu, na kila mara alipoitwa Said alinyamaza kimya kwa kukusudia.

Imamu alisimama mwenyewe na akamuona Said amekaa mahali ambapo si mbali na alipokaa. Akamuuliza kwa nini haitiki wito wake. Saidi akajibu, “Bwana, nilitaka kujua ni mahali gani, wakati gani na kwa jinsi gani ungeweza kukasirika.” Ali akatabasamu na akamwambia Said kwamba hangeweza kuamsha hisia za kukasirisha na hivyo kumkasirisha kwa kutumia hila hizo za kitoto. Imamu Ali akamwachia huru, lakini akaendelea kumsaidia hadi kifo chake.

9. Watumwa: Wasaidizi Wa Imani.

Kama ambavyo Mtume wa Uislamu alileta ujumbe wa undugu ulimwengu mzima, ilikuwa ni dhahiri kwamba ujumbe huu wa kuikomboa roho ya mwanadamu ungewavutia na kuwapendezesha watu wa mataifa yote na imani; lakini hususan yale makundi yenye kuonewa na kudhulumiwa. Ilikuwa kawaida kwamba sehemu kubwa zaidi ya wafuasi wake wa mwanzo ilikuwa ya watumwa.

Wapinzani walihofu; katika hali ya kukata tamaa, wakaanza kuwatesa watu walioingia kwenye Uislamu mwanzoni. Zaidi ya hayo majina ambayo maelezo yake yamekwisha tolewa hapo juu, yafuatayo ni majina yanayohitaji kuangali- wa kwa makini.

Suhayb bin Sinan wa Roma alikuwa mtumwa aliyesilimu na kuwa Mwisilamu wakati wa siku za mwanzo wa Uislamu. Mtu huyu alikuwa mfua chuma stadi, akitengeneza deraya na panga. Kwa hiyo, alikusanya akiba kubwa ya fedha. Baada ya kuwa Mwisilamu, pia alikutana na mateso ya kikatili aliyofanyiwa na makafiri.63

Alipotaka kuhamia Madina, makafiri wakamkamata na wakamnyang’anya fedha yake yote. Kwa hiyo, alifika Madina akiwa fukara. Umari, Khalifa wa pili, alimpa dhamana ya kuongoza sala ya jamaa, baada ya kifo chake hadi hapo Khalifa mwingine atakapochaguliwa.64

Khabbab bin al-Arrat alikuwa sahaba maarufu wa Mtume. Alikuwa mtu wa sita kukubali Uislamu. Alitoka bara la Afrika; na akateswa kwa sababu ya ukweli.65

Alikuwa miongoni mwa wale walioitwa “Shia (wafuasi wenye ari) wa Ali.” Mtoto wake wa kiume, Abdullah pamoja na watu wote wa familia yake, waliuawa kishahidi na Makhariji mwaka wa 40 A.H.66

Kujitolea mhanga kukubwa kabisa kw ajili ya Uislamu kuli- fanyika huko Karbala mnamo mwaka wa 61 A.H. kuliko- fanywa na Imamu Husein na masahaba wake.
Kundi la roho 120-lilikabiliana na jeshi la Yazid bin Muawiyah (wapiganaji wasiopungua 30,000.) Ni jambo la kuzingatia kwam- ba kwenye kundi hilo la waumini 120, takriban watu 16 walikuwa watumwa au watumwa walioachiwa huru. Walikuwa kama ifuatavyo:

Shawadhab – Mwafrika aliyekufa kishahidi, alikuwa mmoja wapo wa wasomi walio heshimiwa sana wa sheria za Kiisilamu na hadithi. Watu walikuwa na kawaida ya kusafiri kutoka mbali kumsikiliza yeye.67

Aliposikia taabu ya Husein, Shawadhab na bwana wake wa zamani (na sasa ni sabaha) Abis Shakiri waliungana pamoja na wakaingia kwenye uwanja wa vita wa Karbala na wakafia humo.

Jonh (Yahya) bin Huwai, – Wa kutoka Ethiopia, inawezekana alisilimu kutoka dini ya Kikristo kama jina lake linavyoonyesha. Alikuwa mtumwa wa Abu Dharr al- Ghifari, sahaba maarufu wa Mtume. Baada ya kifo cha Abu Dharr, aliambatana na Ahlul Bayt ambao walikuwa wanamwangalia. Akafuatana na Imamu Husein huko Karbala, na mbali ya kwamba kwa wakati huo alikuwa mtu mzee, alijaribu kwenda kuingia kwenye uwanja wa vita kupigana.

Imam Hussein kwanza alikata; lakini John aling’ang’ania na mwishowe Imam alimruhusu kwenda kwenye uwanja wa mapambano. Alipoanguka Imamu Husein alikwenda kwenye maiti yake, akaweka paji la uso wake kwenye mapaja yake, na akamwomba Mungu ang’arishe uso wa John. Watu wa kabila la Asad walipofika hapo baada ya siku tatu kuwazika mashahidi, walishangaa kuona maiti iliyokuwa inang’aa kwa nuru ya peponi na kufunikwa na mafuta mazuri ya peponi. Hii ilikuwa maiti ya John.

Salim, Zahir bin Amr, Qarib bin Abdullah Du Ali, Mumjih bin Sahm, Sa’d bin Harth, Nasr bin Abi Naizar, Aslam bin Amr na Sulayman walikuwa miongoni mwa waathirika wa “shambulio la kwanza” jaribio lililofanywa na kikosi cha Yazid kukimaliza kikundi kidogo cha Imamu Husein kwa kuwazidi nguvu kwa uwingi, uwezo, uwepesi na mashambulizi ya kushtua. Jeshi la Yazid lilishindwa katika jaribio lake la kwanza kwa sababu ya ubora wa mbinu za kundi la Husein na utii kamili kwake. Kikosi cha Yazid kilirudi nyuma, na kuacha nyuma, wapiganaji wengi waliouawa.

Lakini ushindi huu wa wafuasi wa Imamu Husein uli- patikana kwa gharama kubwa. Masahaba wa Imam Hussein walikuwa wamelala katika uwanja wa mapambano, miongoni mwao wakiwemo mashahidi sita waliotajwa hapo juu ambao walikuwa watumwa. Pia palikuwepo na watumwa wengine sita waliokufa kishahidi hapo Karbala. Majina yao ni: Harith bin Nabhan, Said, Nafi, Salim, Shabib na Wadih. Maelezo pia yanapatikana kwenye historia za mtumwa wa Kituruki wa Imamu Zaynul Abidin ambaye alipigana na jeshi la Yazid na akajitoa mhanga kwa ajili ya Uislamu. 68

Aqabah bin Saman, – pia ni mtumwa, alikuwa miongoni mwa masahaba walioaminiwa sana wa Imamu Husein. Imamu alimwachia sahaba huyu nyaraka zake muhimu zote azitunze yeye. Kwa istilahi ya kisasa, tunaweza kusema kwamba alikuwa katibu wa Imamu Husein. Sahaba huyu alijeruhiwa kwenye uwanja wa vita wa Karbala na akatekwa na kuwa mfungwa wa kivita pamoja na familia ya Imamu Husein. Akiwa mmoja wapo wa mashahidi walioona kwa macho wenyewe mauaji ya halaiki ya watu huko Karbala, maandiko ya Aqabah bin Samem ni chanzo muhimu sana cha historia. Bin Jarir al-Tabari, mwanahistoria maarufu Mwisilamu, ameandika maelezo ya Aqabah kwenye kitabu chake kiitwacho Tarikh al-umam wa al-muluk. Orodha hiyo ya matukio ilitenganishwa kutoka kwenye orodha ya matukio ya al-Tabari na kuchapishwa huko India pamoja na maelezo kutoka kwa marhum Mujtaba Husein Kamunpuri wa Aligarh Muslim University.

Waisilamu wakati wote wamekuwa na fahari kwa mihanga ilyotolewa na mashahidi wa Karbala kwa ajili ya Uislamu. Dhuria wa Imamu Husein wakati wote wamekuwa wana wapa salaam mashahidi hao, wakati mwingine wanawataja mmoja baada ya mwingine, wakati mwingine wanawataja kwa pamoja.
Shia Ithna Asharia, wakiongozwa na Maimamu wao, kila mara huwapa salaamu mashahidi hawa kwa tamko lifuatalo, Karibuni siku zote:-
Salaamu kwenu, Enyi watakatifu wa Allah na mlio wapendwa wake; Salaamu kwenu, Enyi wateule wa Allah na wapenzi wake;

Salaamu kwenu, Enyi wasaidizi wa Dini (imani) Wazazi wangu nawafidie maisha kwa ajili yenu, Mlio tohara na safi, na imekuwa tohara na safi ardhi mliyozikiwa; kwa hakika mumepata mafanikio (ushindi) makubwa kabisa;

Ningependa kwa Mwenyezi Mungu kwamba ningekuwa pamoja nanyi katika kushiriki mafanikio hayo.69

10. Watoto Wa Watumwa:

Maimamu na Makhalifa Tangu ujilio wake hadi kipindi cha ukoo wa Umayya, Uislamu ulipata ushindi wa kiwango cha mafanikio katika vita yake ya wema dhidi ya utumwa.

Watumwa hawakuwa tena binadamu wa daraja la kudharauliwa kama wanyama, bali walikuwa watu wanaume na wanawake wenye hadhi na heshima. Watumwa wengi walioachiwa na kuwa huru, waliweza kupata kazi za juu na kupata vyeo vikubwa. Dhuria wa Mtume na wafuasi wao waliendeleza msimamo wa Kiisilamu kwa utumwa.

Maimamu kadhaa walioa wanawake watumwa ambao baadaye wakawa mama wa Maimamu.

Madhehebu ya Kaysaniyyah yaliamini Muhammad al- Hanafiyyah (mtoto wa Imamu Ali) kuwa ndivyo Imamu baada ya Imamu Husein. Mama yake Muhammad al- Hanafiyyah, Khawla bint Jafar bin Qays alikuwa mateka ambaye Ali alimuoa. Lakini hapana mtu alitoa ushauri kwamba kuzaliwa na mama aliyekuwa mateka, ilikua dosari katika imani ya madhehebu ya Kaysaniyyah.

Vivyo hivyo, Madhehebu ya Zaydiyyah wana amini kwam- ba Imamu, baada ya Imamu Zaynul Abidin, alikuwa ni mwanae Zayd ambaye alizaliwa na mama msichana mtumwa kutoka Sindhi, jina lake Huriya.

Hata Shahr Banu, binti yake Yazd Jurd (mfalme wa mwisho wa Iran) ambaye aliolewa na Imamu Husein na akamzaa Imamu Zaynul Abidin, alifika Arabuni akiwa mateka. Hata hivyo sifa zake binafsi zilimpa fursa ya kupewa cheo cha “Mkuu wa wanawake.”

Hamidah Khatun, mama yake Imamu Musa al-Kazim alikuwa msichana mtumwa kutoka Berber. Anasifiwa kwa elimu yake na uchamungu wake. Akawa anaitwa Hamidah mtakatifu. Imamu Jafar al-Sadiq alikuwa na desturi ya kuwapeleka wanawake kujifunza kanuni za dini kutoka kwa Hamidah na alikuwa na tabia ya kusema kwamba, “Hamidah ni mtakatifu kutokana na uchafu wote kama kipande cha dhabahu.”

Mama yake Imamu Ali al-Riza pia alikuwa msichana mtumwa kutoka Afrika Magharibi Kaskazini. Jina lake Taktum (au Najma) na alijulikana kama Tahirah, aliye takaswa. Alijulikana kwa elimu yake na uchamungu wake. Imamu Muhammad al-Taqi alikuwa mtoto wa Sabikah, aliyejulikana zaidi kama Khayzurah, mtumwa msichana kutoka Nuba. Imamu Musa al-Kazim alimwambia Yazid bin Sabt kupeleka salam zake kwa Sabikah. Kwenye hadithi anaitwa Tayyibah.

Mama yake Imamu Ali al-Naqi, Sammanah, wa Maghrib, alikuwa mtumwa, lakini alikuwa anaitwa Sayyidah (mkuu wa wanawake) hakuwa na mtu wa kulingana naye kwa uchaji Mungu, mapenzi na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Alikuwa akifunga saumu karibu mwaka wote. Imamu Ali al-Naqi alimwambia kwamba alikuwa analindwa na Mwenyezi Mungu na alikuwa wa kwanza miongoni mwa wakweli na waadilifu.
Imamu Hasan al-Askari pia alizaliwa na mama ambaye alikuwa mtumwa msichana, Hudayth (au Salil.) Katika kumwonyesha hadhi yake ya juu miongoni mwa Shia, inatosha kusema kwamba baada ya kifo cha Imamu Hasan al-Akari yeye alikuwa mtu wa katikati kabisa ndani ya Ushia na jamii yote ilikusanyika kumzunguuka yeye na aliwaongoza katika njia iliyo bora kabisa. Shia walikuwa wakimwita “Jaddah,” bimkubwa.

Narjis Khatun, mama yake Imamu wetu wa 12 ambaye yupo hai mpaka sasa, alikuwa mtoto wa mfalme wa himaya ya Byzantine. Lakini pia alifika kwa Imamu Hasan al-Askari kama mtumwa.
Kiasi hiki kitatosha kwa upande wa kiroho.

Tukiangalia upande wa siasa, tunaona watumwa wasio hesabika waliofika katika kazi za vyeo vya juu sana vya uwajibikaji, ukijumlisha na makamanda wa majeshi, kufanya kazi ya ugavana, na uhakimu. Si tu kwenye utawala, pia tunawaona wataalam wa theolojia (elimu ya dini), wafasiri wa Qur’an, muhadithi, wana sheria na waandishi, ambao ama walikuwa watumwa au watoto wa watumwa, au watumwa walio achwa huru.

Ukiwaondoa khalifa wa kwanza, tatu, nne na tano, makhalifa wote wa ukoo Abbas walizaliwa na wanawake watumwa. Al-Mansur (khalifa wa pili wa ukoo wa Abbas) maarufu, alikuwa ndiye khalifa wa kwanza kuzaliwa na mama aliyekuwa mtumwa, Salamah, aliyetoka Berber. Kuanzia kwa Mamun al-Rashid (khalifa wa sita wa Banu Abbas) hadi wa mwisho wote walikuwa watoto wa wasichana watumwa. Yafuatayo ni majina ya makhalifa na mama zao watumwa:

Mamun al-Rashid: Murajil, mtumwa msichana mweusi
Mutasim Billah: Mtumwa msichana kutoka Kufah, jina lake aliitwa Maridah
Wathiq Billah: Mrumi, jina lake ni Qaratis
Mutawakkil Allallah: Mtoto wa Shuja
Muntasir Billah: Mrumi, jina lake ni Habashiyyah
Mustin Billah: Mukhariq
Mutazz Billah: Mrumi, jina lake ni Qabihah
Muhtadi Billah; Wards au Qurb.
Mutamid Allallah: Mrumi, jina lake ni Fityan.
Mutazid Billah: Sawab (au Hirz au Dhirar)
Muktafi Billah: Mturuki mtumwa msichana, jina lake ni Jyaq au Khudi.
Muqtadir Billah: Mrumi au Mturuki, mtumwa msichana, Gharib au Shaghab
Qahir Billah: Fitnah
Radhi Billah: Mrumi, jina lake ni Zalum.
Muttaqi Lillah: Khalub au Zuhra
Mustakfi Billah: Awjahun Naa au Ghusm.
Muti Lillah: Mashalah
Attai Lillah: Hazar au Atab.
Qadir Billah: Dumanah au Tamami
Qaim Billah: Kutoka Armenia, jina lake ni, Badrudduja au Qatrunnada
Muqtadi Bi Amrillah: Arjwan
Mustazhir Billah: Mtumwa (jina halikuandikwa)
Mustarshid Billah: Mtumwa (jina halikuandikwa)
Rashid Billah: Mtumwa (jina halikuandikwa)
Muqtafi Li Amrillah: Kutoka Ethiopia, mtumwa msichana
Mustanjid Billah: Kutoka Karjiyya, mtumwa, jina lake ni Taus
Mustadi Bi Amrillah: Kutoka Armenia, jina lake ni Dhaddha
Nasir Li Dinillah: Mturuki, mtumwa, jina lake ni, Zamurrad
Zahir Bi Amrillah: Jina halikuandikwa.
Munstansir Billah: Mturuki mtumwa (jina halikuandikwa)
Mustasim Billah: Hajir70

Hata wakati wa karibu sana wa falme ya Ottoman ya Uturuki, familia ya Kifalme inaweza kujumuishwa katika familia ya kitumwa kwa sababu mama wa watoto wa hao masultani walikuwa watumwa.

Muda mrefu kabisa kabla ya utawala wa Sulayman, Sultani ama alikwisha acha kuchukua mke kutoka kwenye familia za Kisultani au alimpa daraja la mke kwa mama wa watoto wao. Mfumo wa utawala wa Ottoman kwa makusudi ulichukua watumwa na kuwafanya mawaziri wa nchi.

Ufalme huo ulichukua wato- to wa kiume kutoka kwenye zizi la kondoo shambani na kuwafanya washauri wa Sultani na kuwaoza mabinti wa kifalme, waliwachukua wanaume vijana wa nhi ambayo wahenga wao walikuwa na majina ya Kikristo kwa karne nyingi, na kuwafanya watumwa wa nchi kubwa kabisa za Kiislam.

Katika kipindi chote cha historia ya Kiislamu, tunaona watumwa wakipanda siyo tu katika nyadhifa za utawala bali hata katika Ufalme pia. Katika maneno ya Will Durant, “Inashangaza ni watoto wangapi wa watumwa wamepanda katika nafasi za juu katika usomi (kitaaluma) na Kisiasa, katika ulimwengu wa Kiislamu; ni wangapi, kama vile Mahmud na wale Mamelik wa mwanzo, walikuja kuwa Wafalme.”71

Subktagin wa Ghazni na mtoto wake, Mahmud (mfalme mpiganaji maarufu ambaye aliishambulia India mara kumi na saba) walikuwa watumwa na watoto wa watumwa mtawalia. Utawala wa kwanza wa Kinasaba wa Kiislamu wa nchini India nao pia uliundwa na utawala wa kinasaba wa watumwa.

Kabla ya kuifunga sura hii, ni lazima nisisitize nukta moja: Wale wafungwa wote au watoto wa wafungwa ambao wali- fika kilele cha heshima kiroho au Kisiasa hawakufanywa hivyo kamwe kwa sababu ya kuwa watumwa au watoto wa watumwa; bali walifikia daraja hizo kwa sababu walikuwa Waislamu waliokuwa na uwezo.

Daraja zao za kiutumwa au kuachiwa huru kamwe halikuongezeka au kupunguza nafasi za mafanikio yao; kamwe haukurahisisha wala kuzuia kufikia lengo lao la maisha. Jamii ya Kiislamu, shukurani kwa sheria madhubuti za Uislamu na Mtume Muhammad, walikuwa vipofu–kirangi na vipofukihadhi (yaani Uislamu haufadhilishi rangi au hadhi ya mtu).

Jambo moja tu lililohusika lilikuwa ni uwezo wa kufanya jambo au kitu ambao mwanamume au mwanamke alikuwa nao.

Mafanikio haya, yaliyo patikana miaka 1400 iliyopita, ni kilio cha tofauti sana kutokaka na kushindwa kwa dhahiri kwa Ukristo katika miaka hii ya 1960 ambako, katika nchi ya Kikristo ya Amerika (U.S.A) kama mtu mweusi (Mnegro) anakuwa Meya (wa Jiji) inaonekana ni habari kubwa; na wakati ambapo katika mwaka 1971 serikali ilipanga kumpandisha cheo mwanajeshi wake wa kwanza mtu mweusi kuwa admiral (mkuu wa jeshi la wana maji), aliyeitwa Kapteni Samwel Lee Granely.

Unaona kidokezi cha habari hizi. Mtu fulani kutoka jamii ya watu weusi (Manegro) anachaguliwa na kupandishwa cheo kwa misingi ya kisiasa kwa sababu ni mtu mweusi (Mnegro). Lakini ingekuwa hasa hasa ni sifa zake tu za kibinafsi, jina hili lisingekuwa ni jambo la kutangazwa na kuenezwa kila mahali!

Aina kama hiyo ya ubaguzi wa rangi na kujiona ilikuwa, na hata sasa haifikiriki katika Uislamu.

Hivyo basi, ni dhahiri kwamba Uislamu ulifanikiwa mahali ambapo kila dini nyingine na mifumo imeshindwa mpaka sasa. Uislamu uliwachanganisha watumwa katika jamii ya Waislamu bila kujali rangi zao au asili. Kuamua kutokana nakumbu kumbu zake zenyewe (zilizo za kweli), hatuwezi ila kushanga mafanikio makubwa ya Uislamu katika uwanja wa nyanja hii.

 • 1. Al-Majalisi, M.B., Hayatul Qulub, j. 11 (Tehran: Kitabfurushi-e- Islamia, 1371 A.H.), uk.
  562-3; Abu Na'im Ahmad al-Isfahani, Hilyatul Awliya, j. 1 (Beirut, 1967), uk. 146-7.
 • 2. Ibn Sa'd, op. cit., j. 4:1, uk. 58.
 • 3. al-Majilisi, Bihar al-Anwar, j. 22 (Tehren, n.d.), uk. 355; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 193-
  5; Ibn Hajar al-Asqalani, al-Isabah fi Tamyiz's- Sahabah, j. 3 (Calcutta: Asiatic Society of
  Bengal, 1853-88), uk. 224.
 • 4. Ibn Sa'id, op. cit., j. 11:1, uk. 47.
 • 5. al-Majilisi, Bihar, j. 20, uk. 189, 198; Ibn Sa'id, op. cit., j. 4:1, j. 7:2, uk. 65.
 • 6. al-Majilisi, Bihar; j. 22, uk. 348.
 • 7. al-Majilisi, op. cit., j. 22,uk. 330, 391; Ibn Sa'id, op. cit., 4:1, uk. 61; Abu Na'im, op.
  cit., j. 1, uk. 187.
 • 8. al-Majilisi, op. cit., j. 22 uk. 331.
 • 9. Ibid, uk. 349.
 • 10. Ibid, uk. 346.
 • 11. Ibid, uk. 327, 349.
 • 12. Ibid, uk. 347.
 • 13. Ibid, uk. 319; Ibn Sa'id, op. cit., j. 4:1, uk. 61; Abu Naim, op. cit., j. 1, uk.187.
 • 14. al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 342.
 • 15. Ibid, Uk. 321.
 • 16. Ibid, uk. 325; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 190.
 • 17. al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 327.
 • 18. Ibid, uk. 381
 • 19. Ibid, uk.374.
 • 20. Ibid, uk. 372,380.
 • 21. Ibn Hajar, op. cit., j. 2, uk. 45.
 • 22. al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 314, 318; Ibn Sa'd, op. cit., j.3: 1, uk. 28; Ibn Hajar, op. cit.,
  j.2, uk. 45-6.
 • 23. al-Majilisi, op. cit., j. 3 uk. 29; Ibn Hajar, op. cit., j. 7, uk. 600.
 • 24. Ibn Sa’d, op. cit, 8, uk. 31; Ibn Hajar, op. cit, 2, uk. 46, j. 7, uk. 600
 • 25. Al-Tabataba’i, al-Mizan, toleo la tatu, j. 4 (Beirut: 1974), uk. 195.
 • 26. Al-Amili, op. cit., j. 14, uk. 43; Ibn Sa'd, op. cit., j. 8:1, uk. 71
 • 27. Al-Majilisi, op. cit., j. 22, uk. 187; Ibn Hajar, op. cit., j. 7, uk.600
 • 28. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 32; Ibn Hajar, op. cit., j. 2, uk. 47.
 • 29. Ibn Sa'd, op. cit., j. 2:2, uk. 41-2; j. 4:1, uk. 46-7.
 • 30. Ibn Sa'd, op. cit. j.3:1, uk. 179; Ibn Athir, Usdlu'l-Ghabah fi Ma'rifat's-Sahabah, j. 4 (Egypt, n.d.).
 • 31. Ibid.
 • 32. Ibid, j. 3:1, uk. 176.
 • 33. Ibid, j. 3:1, uk.177; Abu Na'imi, op. cit., j. 140.
 • 34. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 178; Abu Naimi, op. cit., j. 1 uk. 140; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk.1219.
 • 35. Ibn S a'd , op. cit., j. 3:1, uk. 177, 180; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 1220;
 • 36. Ibn S a'd , op. cit., j. 3:1, uk. 177, 180; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 1220; al-Bukhari, al-Sahih, j. 8. (Chapa ya Misr) uk. 185-186; al- Trimidhi, al-Jami' al- Sahih, j. 5 (Chapa ya Misir) uk.669; Ahmad bin Hanbal, al-Musnad, j.2 Chapa ya Misir) uk. 161, 164, 206, j. 3, uk. 5, 22, 28, 91, j. 4, uk. 197, 199, j. 5, uk. 215, 301, 307, j. 6, uk. 289, 300, 311, 315; Ibn 'Abdi'l-Barr, al-Isti'ab fi Ma'rifat'l-Ashab, j. 3, uk. 1140.
 • 37. Ibn Sa'd op. cit.,j. 3:1, uk. 187; Hakim, al-Mustadrak'ala's-Sahihayn, j. 3, (chapa ya Hyderabad) uk. 392; Ibn Hisham, al-Sirah j. 2, (chapa ya Misir Toleo jipya) uk. 143; Ibn Kathir, al-Tarikh, j. 7. uk. 268, 270.
 • 38. Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 139; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 1219; Ibn Majah, al-Sunan, j. 1 (chapa ya Misir toleo jipya) uk. 65; al- Haythami, Majma'al-Zawa'id,j. 9 (chapa ya Misir toleo jipya) uk. 295; Ibn 'Abdu'l-Barr, op. cit., j. 3, uk. 1137.
 • 39. al-Baladhuri, Ansabu'l-Ashraf, j. 5, uk. 48, 54,88; Ibn Abi'l-Hadid, Sharh Nahj'al- Balagha, j. 3, uk. 47; Ibn Qutaybah, al-Imamah wa 's- Siyasah, j. 1, uk. 35-6; Ibn 'Abd Rabbih, al-Iqdu 'l-Farid, j. 4 (chapa ya Misir) uk. 307; Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 185; al-Diyarbakri; Tarikhu'l- Khmis, j. 2, uk. 271.
 • 40. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 184-5; Abu Na'im, op. cit., j. 1 uk. 141.
 • 41. Qummi, Abbas, Muntaha'l-Amal, j. 1 (Tehran:1381 AH) uk.92.
 • 42. Al-Tabari, al-Ta'rikh, j. 1, uk 3316,-3322; j. 3, uk. 2314-2319; Ibn Athir, al-Kamil, j. 3,
  uk. 308-312; IObn Kathir, al-Ta'rikh, j. 7, uk. 267-272.
 • 43. Al-Mufid, Kitab al-Irshad, Tarjuma ya I.K.A. Howard (London:Muhammad Trust) uk.
  243-244; na Rijal ya al-Kashshi kama ilivyonukuliwa na Qummi, op. cit., j. 1, uk. 157.
 • 44. Qummi, op. cit., j.1, uk. 157
 • 45. Kashshi, Rijal kama ilivyonukuliwa na Qummi, op. cit., j. 1, uk.143-4.
 • 46. Qummi, op. cit., j. uk. 157; al-Mufid, op. cit., uk. 244.
 • 47. Ibid
 • 48. Ibid
 • 49. Ibid
 • 50. Ibid
 • 51. Ibid. uk. 158-9.
 • 52. Ibn Sa'd, op. cit., j.3:1, uk. 170; Ibn Hajar, op. cit., j. 1, uk. 336.
 • 53. Ibn Sa'd, op. cit., j. 166; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 336.
 • 54. Ibid, uk. 167.
 • 55. al-Majilisi, Hayatu'l-Qulub, uk. 129-130; Biihar, j. 16, uk. 295.
 • 56. Shustari, Nurullah, Majalisu'l-Mu'minin (Tehran, 1268 AH.) uk. 54; na vile vile angalia
  Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 169
 • 57. Shushtari, op. cit., j. 1, uk. 150.
 • 58. Shushtari, op. cit., uk. 54; vile vile tazama Ibn Sa'd, 0p. cit., j.3:1, uk. 170; Ibn Hajar, op.
  cit., j. 1, uk. 336-337.
 • 59. Shubar, S. 'Abdullah, Masabihul Anwar, j. 2 (Najaf: Matba'ah al 'Ilmiyyah, 1952/1371)
  uk. 425-6 akinukuu Manaqib ya Ibn Shahr Ashub.
 • 60. Majilisi, Bihar, j.43 (Beirut, 1983/1403) uk. 86-7; Ibn Shahr Ashub, Manaqib Aal
  Abi Talib, j. 4 (Bombay, 1313 AH.) uk. 15
 • 61. Kashshi, Rijal kama ilvyonukuliwa na Qummi, op. cit., j. 1, uk. 153
 • 62. Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk. 153; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 514.
 • 63. Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 514
 • 64. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk.161-4; Ibn Hajar, op. cit., j. 3, uk. 516.
 • 65. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 116-7; Abu Na'im, op. cit., j. 1, uk.144.
 • 66. Ibn Sa'd, op. cit., j. 3:1, uk. 21; Ibn Hajar, op. cit., j. 4, uk. 739.
 • 67. Qummi, op. cit., j. I, uk. 266.
 • 68. Kwa maelezo zaidi juu ya Imamu Husein na Karbala, tazama Rizvi, S.M., Imam Husayn,
  the Saviour of Islam, (Vancouver: 1984).
 • 69. Qummi, Mafatihu'l-Jinan ( Tehran, n.d.) uk. 427.
 • 70. Tizama sura zinazohusika za kitabu Rawdatu’s-Safa cha Muhammad Khawind Shah; vile vile Ibn Rabbih al-Undulusi, al- 'Iqdu'l-Farid, j. 5 (Beirut: 1983) uk. 113-131.
 • 71. Durant, W., The Story of Civilization, j. 4, uk. 209.

Chimbuko La Watumwa Weusi

Sasa tumeona msimamo wa Uislamu kuhusu utumwa, hebu ngoja tuuangalie Ukristo na wafuasi wake, na tuone wali- fanya nini kuhusu suala hili. Inashangaza kuona kwamba Wakristo, ambao kwa sababu wanazo zijua wao, siku hizi wanajifanya kama mabingwa wa uhuru wa mwanadamu, kumbe wao ndiyo mawakala wa dhahiri na watetezi wakubwa wa mfumo huu wa utumwa. Walivumbua falsafa na uthibitisho wa kimaadili, kama sababu za kuwafanya watumwa watu “wasio staarabika.” Mojawapo ya hoja zao ni kwamba walikuwa wana waokoa watu hao (watumwa) kutoka kwa majirani zao wanaokula watu hapa duniani, na kutoka kwenye fedheha ya daima milele baada ya uhai wa hapa duniani.

Uislam na wafuasi wake kamwe hawakuwa na fikira kama hizo. Wingi mno wa maandiko ya Kiisilamu hauna kitu kama hicho, kutokana na aina hii ya jitihada ya uadilishi wa kusikitisha. Lakini waandishi wa Kikiristo kila mara hutaja biashara ya utumwa kama vile wao hawakuhusika kwa vyovyote vile na tatizo hili, na kwamba ni Uislam ndio ambao “ulihimiza na kuhalalisha utumwa” ambapo wao, Wakristo, kila mara walijaribu kukomesha mpango huu mbaya sana! Haya ndiyo maelezo ya waandishi wa Kikristo.

Ni jambo la kuvutia kuona kwamba wakati wanapo zungumzia kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika ya Magharibi ambayo ilifanywa kikamilifu na Wakristo peke yao, waandishi na wanahistoria wa Kikristo, wameipa biashara hii jina la “West African Slave trade,” Yaani biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi au “Atlantic Slave – Trade” yaani biashara ya utumwa ya Atlantic, lakini wanapotoa maelezo kuhusu suala hili kwa upande wa Afrika ya Mashariki, hubadili maneno na kuandika “Arab Slave Trade” yaani biashara ya utumwa ya Waarabu.

Ukristo, kwa kutumia propanganda ya udanganyifu wa jinsi hii, umefaulu kwa kiwango kikubwa kupanua uwanja wa athari zake miongoni mwa Waafrika ambao humo umeweka mkakati wa propaganda yake na wanafurahi sana lakini hawatambui ukweli kwamba makanisa ya Kikristo yalikuwa washiriki wenye bidii sana kwenye “African Slave Trade” (biashara ya utumwa ya Kiafrika). Sura zifuatazo zitaonye- sha picha ya kweli kwa wasomaji.

Mnamo mwaka wa 1492, ambapo Columbus, akiwakilisha ufalme wa Hispania aligundua “New World” (Dunia mpya), alianzisha mfululizo mrefu na mchungu wa ushindani wa kimataifa katika kujipatia makoloni, ambao hadi sasa baada ya karne nne na nusu, hakuna suluhu iliyopatikana. Ureno, ambayo ndio iliasisi kitendo cha kujipanua kimataifa, ilidai hizo nchi mpya kwa hoja ya kwamba zilikuwa kwenye eneo la madaraka ya amri ya baba mtakatifu (papal bull) wa 1455 inayowaruhusu wareno (ambao ni Wakristo) kuwafanya watumwa wapagani wote.

Katika kujaribu kuepuka ubishani, mamlaka hizi mbili, zilitafuta suluhisho, na kwa sababu zote zilikuwa katika madhehebu ya Ukatoliki, zilimwelekea Baba Mtakatifu – hatua ambayo ilikuwa ya kawaida na ya mantiki katika kipindi ambapo madai ya wakati wote ya Kipapa yalikuwa bado hayana upinzani ama kutoka kwa mtu binafsi au serikali ya nchi. Baada ya kuchunguza kwa makini madai ya washindani, Baba Mtakatifu, katika mwaka 1493, alitoa mfululizo wa amri za kipapa ambazo ziliweka mipaka ya kuaua kati ya makoloni yanayomilikiwa na dola hizo mbili za Ulaya: Mashariki ilichukuliwa na Ureno na Magharibi ilichukuliwa na Hispania. Mgawanyo huo, hata hivyo, haukukidhi matege- meo ya Ureno na mwaka uliofuata washindani hao wawili walifanikiwa kuhitimisha mwafaka wa maridhiano zaidi kwenye Mkataba wa Tordesillas ambao ulirekebisha uamuzi wa Baba Mtakatifu kuiruhusu Ureno kumiliki Brazili1 kama koloni lake.

Lakini maamuzi haya hayakuweza kuzifunga mamlaka zingine ambazo zilikuwa zina wania kunyakua makoloni mengi iwezekanavyo; Uingereza, Ufaransa, na hata Uholanzi zilianza kudai sehemu zao (makoloni) hapa duni- ani. Mtu mweusi, pia, alikuwa apate sehemu yake, licha ya kwamba hakuomba; ilikuwa uanzishwaji na upanukaji wa mashamba makubwa ya miwa, tumbaku na pamba ya ulimwengu Mpya.

“Kwa mujibu wa Adam Smith, maendeleo ya koloni jipya yalitegemea jambo moja rahisi la kiuchumi- ‘ardhi pana yenye rutuba.’ Hata hivyo, umiliki wa makoloni wa Uingereza hadi 1776, kwa ujumla unaweza kugawanywa katika aina mbili. Aina ya kwanza ni wakulima wadogo wanao jitosheleza na kushughulika na uchumi wa bidhaa mbalimbali.

Aina ya pili ni koloni ambalo limesheheni hali iwezeshayo mtu kuzalisha bidhaa kuu mbali mbali kwa wingi kwa madhumuni ya kuuza nje. Katika aina ya kwan- za, yalikuwemo makoloni ya Kaskazini ya bara la Marekani; katika aina ya pili, yalikuwepo makoloni ya tumbaku na visiwa vya miwa vya Caribbean. Kwenye makoloni; ardhi na mtaji havikuwa na manufaa bila ya kuwepo nguvu kazi ya musuli. Kibarua, lazima awepo wakati wote na lazima afanye kazi, au ahimizwe kufanya kazi, katika kundi moja.

Bila ya sharti hili, kibarua angeamua kuwa na mwelekeo wake binafsi na kufanya kazi katika ardhi yake mwenyewe. Hadithi moja inasimuliwa mara nyingi kuhusu kabaila mmoja wa Uingereza, Bwana Pell, ambaye alichukua pauni za Kiingereza elfu hamsini (50,000) na vibarua mia tatu akaenda nao kwenye koloni la Swan River huko Australia.

Mpango wake ulikuwa kwamba vibarua hao wangefanya kazi kwake, kama iliyvokuwa Uingereza. Bwana Pell akawasili Australia ambapo ardhi ilikuwa pana sana vibarua wakapendelea kufanya kazi kwenye mashamba yao madogo kwa manufaa yao kama wamiliki wadogo, badala ya kufanya kazi chini ya kabaila kwa kulipwa ujira. Austaralia haikuwa Uingereza, na kabaila huyo alibaki hana mtumishi wa kumtandikia kitanda au wa kumchotea maji.”2

 • 1. Williams, Dk. Eric, Capitalism and Slavery (London, 1964) P. 4.
 • 2. Ibid uk. 4-5

Kwa Hiyo Ufumbuzi Unaofaa Ni Utumwa

“Ni njia ya kuchukiza,” ingawa inaweza kuwa hivyo, kama Merivalle alivyoiita, utumwa ulikuwa taasisi ya kiuchumi yenye muhimu wa kwanza. Utumwa ulikuwa ndiyo msingi wa uchumi wa Ugiriki na ukajenga Ufalme wa Kirumi.

Katika zama hizi utumwa ulizalisha sukari kwa ajili ya chai, na vikombe vya kahawa vya dunia ya Magharibi. Ulizalisha pamba ikiwa ndiyo msingi wa Ukabaila mambo leo. Utumwa ulijenga Marekani (US) ya Kusini na visiwa vya Caribbean.”1

“Ulaya ikiwa na watu wachache katika karne ya kumi na sita, hivyo kwamba, vibarua wa kulima bidhaa muhimu kama miwa, tumbaku na pamba katika Dunia Mpya hawangepatikana kwa idadi ya kutosheleza kuruhusu uzalishaji wa kiwango kikubwa. Utumwa ulikuwa muhimu kwa lengo hili na ili kuweza kuwapata watumwa, wazungu walianza kwanza kuwatumia Waaborigine kama watuma.”2

Lakini utumwa wa Kihindi kamwe haukuwa mkubwa kwenye makoloni ya Uingereza…Kwa upande wa Wahindi… utumwa ulionekana kama jambo lilotokealo mara chache, kama kinga ya adhabu na si kama ndiyo hali ya kawaida na ya kudumu.

Katika makoloni ya New England, utumwa wa Wahindi haukuwa na faida, kwani utumwa wa aina yoyote ulikuwa hauna faida kwa sababu haukustahili kwenye kilimo cha mazao mbalimbali ya makoloni haya. Juu ya haya, mtumwa wa Kihindi alikuwa hawezi kufanya kazi kwa bidii. Wahispania waligundua kwamba mtumwa mweusi mmoja alikuwa sawa na watumwa wanne wa Kihindi. Afisa mmoja mashuhuri wa Hispaniola alisisitiza mnamo mwaka 1581 kwamba itolewe ruhusa ya kuwaleta watu weusi, jamii iliyo kakamavu kwa kazi badala ya wazawa ambao ni dhaifu sana hivyo kwamba wanaweza kuajiriwa kwenye kazi ndogo zisizo hitaji matumizi ya nguvu nyingi kama vile kutunza mashamba ya mahindi….

Bidhaa za siku za usoni za “New World,” yaani miwa na pamba, zilihitaji nguvu ambazo watumwa wa Kihindi walipungukiwa na wakataka “mtu mweusi wa pamba” aliye mkakamavu kama ambavyo miwa inahitaji nyumbu wenye nguvu ambao hupatikana Louisiana, wenye kisifa cha jina la ‘nyumbu wa sukari.’ Kwa mujibu wa Lauber, inapolinganishwa kiasi cha malipo kilichotolewa kwa mtu mweusi (Mnegro) kwa wakati huo huo na kwa mahali hapo hapo, utaona kwamba bei za watumwa wa Kihindi zinaonekana kuwa za chini mno.

Wingi wa nguvu kazi ya Kihindi, pia, ilikuwa ndogo, ambapo vibarua wa Kiafrika walikuwa hawaishi. Kwa hiyo, watu weusi (Manegro) waliibiwa kutoka hapa Afrika kwen- da kufanya kazi kwenye ardhi, iliiyoporwa (na kuibiwa) kutoka kwa wazalendo wa Kihindi (Wahindi wekundu) huko Marekani. Misafara ya baharini ya Prince Henry the Navigator (Mfalme Henry Baharia mvumbuzi) ilikamilisha ile ya Columbus, historia ya Afrika ya Magharibi ikawa kamilisho la historia ya West Indians.” (Wahundi wa Magharibi)3

 • 1. Ibid
 • 2. Ibid, uk. 6
 • 3. Ibid, UK. 8-9

Wakristo Wanapanga Biashara Ya Utumwa

Watumwa walikuwa wanachukuliwa kutoka hata katika wakati wa Ufalme wa Kirumi, lakini “biashara halisi ya Utumwa” ilianza mnamo karne ya 16 baada ya ujio wa mataifa ya Kikristo ya Ulaya. Edward A. Alpers wa Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam, anaandika kwamba; “kama tunavyoleta utofautisho baina ya biashara inayoambatana katika watumwa ambayo ilichuruzika katika sahara kutoka magharibi mpaka kaskazini ya Afrika kuanzia siku za nyuma sana za wakati wa utawala wa Ufalme wa Kirumi, kwa upande mmoja, na kioja tunacho kiita The West African Slave Trade kwa upande mwingine, kwa hiyo lazima tulete tofauti hiyo hiyo kwa Afrika ya Mashariki.”1

Walter Rodney pia wa Chuo, Kikuu cha Dar es Salaam, anaanza kuandika kijitabu chake “West Africa and the Atlantic Slave-Trade kwa maneno yafuatayo: - Wakati wote lazima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa iliyo;fanyi- ka katika bahari ya Atlantiki” lilikuwa ni tukio katika histo- ria ya dunia, iliyo husisha mabara matatu – Ulaya, Afrika na Marekani.

Watu walio toka kwa dhamira ya kutafuta watumwa walikuwa Wazungu waliotoka katika kila nchi kati ya Sweeden kwa upande wa Kaskazini na Ureno kwa upande wa magharibi. Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya kuingia nusu karne ya kumi na tano. Mara moja na kwa haraka sana walianza kukamata (watumwa) Waafrika na kuwapeleka kufanya kazi Ulaya kama watumwa, hususan katika Ureno na Hispania. Lakini maendeleo muhimu sana kwa biashara hii ya utumwa yalikuwa katika karne ya kumi na sita, ambapo mabepari wa Kizungu walitambua kwamba wangepata faida kubwa sana kwa kutumia nguvukazi ya Waafrika kuujenga na kuuendeleza utajiri wa nchi zote za Amerika.

Matokeo yake, Waafrika walipelekwa Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati, Amerika ya kusini na Visiwa vya Caribbean kwa ajili ya kukidhi haja ya nguvukazi ya watumwa kwenye machimbo ya dhahabu na shaba, na kwenye mashamba ya kilimo cha mazao ya miwa, pamba na tumbaku. Biashara hii mbaya ya kununua na kuuza binadamu ilidumu kwa kipindi cha miaka (400) mia nne, kwani Atlantic slave-Trade (Biashara ya Utumwa wa kupitia bahari ya Atlantiki) ilikoma mwishoni mwa miaka ya 1870.

“Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu jinsi Biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilivyopangwa huko Ulaya, na kuhusu faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama Uingereza na Ufaransa. Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu safari za kutisha kutoka Afrika hadi Marekani kuvu- ka bahari ya Atlantic. Waafrika walipangwa kama dagaa kwenye meli za kubeba watumwa, na matokeo yake walikufa wengi sana.”2

Na dagaa walioje! Kwa maelezo zaidi kuhusu upakiaji huu wa watumwa kwenye meli, soma taarifa ifuatayo: - Moja ya hati yenye kuuvunja moyo sana katika nyaraka zote zinazotisha ni “Plan of the Brookes,” mpango mbaya sana wa karne ya kumi na nane wa kupanga watumwa kwenye meli ya kubeba watumwa ‘Brookes’… Kwa mahesabu sahi- hi, teknolojia ya kushtua ilitengenezwa - futi na inchi, chumba cha kusimama na nafasi ya kupumua iliwekwa kwa matumaini ya faida kubwa. Mtu mmoja Bwana Jones anapendekeza kwamba wanawake watano wahesabiwe kama wanaume wanne, na wavulana watatu au wasichana watatu wafanywe kuwa sawa na watu wazima wawili … kila mtumwa mwanaume aruhusiwe futi sita kwa futi moja na inchi nne (1’4”x6’) kama nafasi ya chumba chake, kila mwanamke alipewa nafasi ya upana wa futi tano na inchi kumi na futi moja na inchi nne…. (5’10”x1’4”); na inaendelea hivyo mpaka kila mtu anapata nafasi – watumwa 451.

Lakini Muswada wa Bunge unaruhusu watumwa 454. Kwa hiyo hati hiyo inahitimisha kwamba kama watumwa watatu zaidi wangeweza kuwekwa kwa kubanwa katikati ya wale waliotamkwa kwenye mpango, mpango huu ungeweza kuchukua idadi ile ile ambayo imeelekezwa kwenye muswada.3

Mara Waafrika walipofikishwa upande mwingine wa bahari ya Atlantic, kwa hakika walikuwa katika “Dunia Mpya”, iliyojaa ukandamizaji na ukatili. Taarifa ifuatayo inaweza kusaidia kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo. Rodney anaandika:

“Kuanzia wakati walipofika (Wakristo) Wazungu hadi 1600, takriban Waafrika milioni moja (1, 000,000) walichukuliwa kwenye meli za kubeba watumwa. Wakati wa kipindi hicho, Wareno walikuwa ndio wafanya biashara wakuu wa biashara ya watumwa huko Afrika ya Magharibi. Ama wali- wapeleka Waafrika huko Brazil, ambayo nchi hiyo ilikuwa koloni lao, au vinginevyo waliwauza kwa waloezi wa Kihispania huko Mexico, Amerika ya kati, Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean. Mnamo karne ya kumi na saba, kiasi cha Waafrika wapatao milioni saba hadi nane kutoka Afrika ya magharibi walivushwa bahari ya Atlantic.

Wadachi walijumuika na Wareno kama wafanya biashara wakuu wa biashara ya utumwa mnamo karne ya kumi na saba, na karne iliyofuata Waingereza wakawa wafanya biashara wakubwa kushinda wote wa biashara ya utumwa. Wakati biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilipofikia kileleni mnamo karne ya kumi na nane, meli za Kiingereza zilikuwa zinachukua zaidi ya nusu ya jumla yote ya watumwa na idadi iliyobaki iligawanywa baina ya Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadane (Danish).

“Ilipofika karne ya kumi na tisa, palikuwepo na mabadiliko mengine ya watu ambao walishika nafasi mbele katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikushiriki kikamilifu kwenye biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu ambao waliloea Brazil, Cuba, na Amerika ya Kaskazini ndio ambao walipanga sehemu kubwa ya biashara. Waamerika (U.S.A) ndiyo katika kipindi hicho hicho tu walipata uhuru kutoka kwa Waingereza, hili lilikuwa taifa jipya (U.S.A.) ambalo lilikuwa na mgawo mkubwa kabisa kuliko wote katika biashara ya watumwa katika biashara ya Atlantiki katika kipindi cha miaka hamsi- ni ya mwisho, kwa kuchukua kiwango kikubwa zaidi cha watumwa kuliko ambavyo imewahi kufanya huko nyuma.

“Ilipoanza “biashara ya watumwa ya Atlantiki kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi, ilichukua utaratibu wa kutu- mia nguvu moja kwa moja wa Wazungu kuwashambulia Waafrika waliokuwa wanaishi karibu na pwani. Mabaharia wa kwanza wa Kireno walipofika kwenye pwani inayoju- likana leo kama Mauritania, waliacha meli zao na kuanza kuwawinda watu waitwao, Moors watu walioishi katika jimbo hilo. Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo – ilikuwa uvamizi wa nguvu. Hata hivyo, baada ya mashambulizi kadhaa ya kushtukizwa, Waafrika wa pwani wakawa na kawaida ya kulinda kwa zamu na walijilinda kwa nguvu dhidi ya washambuliaji wao Wazungu.

Katika kipindi kifupi tu, Wareno walitambua kwamba uvamizi haikuwa mbinu inayofaa na iliyo salama katika kujaribu kuwapata watumwa. Zaidi ya hayo, pia walitaka dhahabu na bidhaa zingine za Kiafrika, ambazo wangeweza tu kuzipata kwa njia ya kununuliana na kuuziana kwa amani. Kwa hiyo badala ya kuvamia, Wareno waliona afadhali kutumia bidhaa zilizo tengenezwa kiwandani ili kuwatia moyo Waafrika kubadilishana na bidhaa zao na hata kuweza kuwafikisha mateka wa Kiafrika kwenye meli za Wazungu kwa urahisi. Mpango huu haukufanywa na Wareno pekee, lakini hata wazungu wengine wote walitambua na kukubali kwamba huo ulikuwa mpango mzuri zaidi wa kupata bidhaa hapa Afrika; na ilikuwa kwa njia hii waliweza kupata mamilioni mengi ya Waafrika.”4

Akifafanua juu ya kipengele hiki cha biashara ya watumwa, mwandishi anasema: “Moja ya vitu muhimu sana ni kutambua jambo liumalo sana na lisilo pendeza kwamba walikuwepo Waafrika ambao waliwasaidia na kushirikiana na Wazungu katika kuwafanya Waafrika wenzao kuwa watumwa. Maana yake ni kwamba hatuwezi kuchukua msimamo dhaifu na kusema kwamba watu weupe walikuwa wabaya sana na watu weusi walikuwa waathirika (katika kuangamia). Mfano unaofaa na sambamba ambao ungeweza kusaidia kuelewa yale yaliyotokea katika Afrika ya Magharibi wakati wa kipindi cha karne za biashara za watumwa unaweza kuonekana hapa Afrika leo, ambapo viongozi wengi wanashirikiana na mabeberu wa Ulaya na Marekani (U. S. A.) kwa lengo la kuwanyonya na kuwakan- damiza Waafrika walio wengi.

Hatimaye, Waafrika wa Afrika ya Magharibi walifikishwa kwenye hali ya “uza au uuzwe.” Hapa suala la bunduki lilikuwa na umuhimu maalum. Kuwa na nguvu, serikali ili- hitaji bunduki, lakini ili kupata bunduki kutoka kwa wazungu, Waafrika ilibidi kuwapa Wazungu watumwa na wao kupewa bunduki. Watawala wa Kiafrika walijikuta wenyewe wanawauza watumwa ili wapate bunduki ambazo ziliwawezesha kuwakamata raia wao na kuwauza kama watumwa ili wanunue bunduki nyingi zaidi. Hali hii inaweza kuelezewa, kama “ubaya juu ya ubaya (mzunguuko unaoashiria kukwama).” Watawala wa Kiafrika ambao waliwasaidia wazungu hawasameheki moja kwa moja, lakini inafafanua jinsi gani mwishoni hawakuwa washirika halisi wa Wazungu bali walikuwa watumishi au vibaraka wa Wazungu.” 5

Na kanisa lilikuwa linafanya nini wakati wote huo? Msikilize mwandishi huyu huyu anasema; “Kwa sababu faida kubwa sana ilikuwa inapatikana kwa kuwachukua watumwa kutoka Afrika, Wazungu walikataa kuzisikiliza dhamiri zao. Walifahamu kuhusu mateso yaliyo wapata watu katika Afrika, ndani ya meli za kubebea watumwa na kwenye mashamba yaliyokuwa yanalimwa na watumwa ya Waamerika, na walitambua kwamba kuwauza binadamu wenzao ni jambo ambalo halingethibitishwa kimaadili. Hata hivyo kanisa la Kikristo lilijitokeza na kutoa sababu nyingi likijitetea kuingia kwake katika biashara ya watumwa.

Wachungaji wengi walifanya biashara ya watumwa, hasa katika Angola, na wengine wengi walimiliki watumwa, katika nchi za Amerika. Sababu moja tu ambayo ilitolewa na kanisa Katoliki kuhusu vitendo vyake ilikuwa kwamba lilikuwa kinajaribu kuziokoa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa wabaya zaidi, kwani wala hawakuweka wazi kwamba walikubali kwamba Waafrika walikuwa na roho.

Badala yake, walikubaliana na fikira kwamba mtumwa wa Kiafrika alikuwa sehemu ya rasilimali kama fenicha au hayawani wa kufugwa. Hakuna sehemu ya historia ya Kanisa la Kikristo ambayo inafedhehesha zaidi kuliko kusaidia “Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki.”6

Kwa mujibu wa orodha ya Lloyd, iliamuliwa kwamba watumwa walikuwa ni bidhaa, na wenye thamani sana. Hati za bima zilizochukuliwa kutoka Lloyd waliwakatia watumwa hati za bima hadi kufika kiasi cha pauni za Kiingereza 45 kila mtumwa kiasi hicho cha fedha ni kikubwa katika kipindi hichi cha mwanzoni mwa karne ya 18 huko Uingereza.
Ili kuwazuia watumwa wasitoroke, au kuwaadhibu, nyenzo zisizo za kawaida kama zilivyoorodheshwa hapa zilitumiwa katika Afrika ya Magharibi na katika visiwa vya West Indies.7

Siku zote kulikuwepo watu wachache ambao walipinga Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki. tangu mwanzo; lakini serikali mbalimbali na wafanya biashara hawakuwajali, wakati wa karne ya kumi na tano, kumi na sita na kumi na saba. Haikuwa hivyo, hadi mwishoni mwa karne ya kumi na nane wakati majaribio ya dhati yalifanywa kwa lengo la kukomesha biashara hii.

James Boswell, akijaribu kukana hoja za watu waliotaka biashara ya watumwa ikomeshwe, anaandika katika kitabu chake kiitwacho “Life of Johnson.” Kwamba: Jaribio la kinyama na la hatari ambalo kwa muda fulani limeendelea kuwepo kwa lengo la kupata sheria ya bunge letu, ili kukomesha tawi la maana sana na muhimu la faida kibiashara, lazima lingekwisha amuliwa mara moja, kama isin- gelikuwa kundi lisilo na maana la washabiki waliokuwa msitari wa mbele kwalo bila kufaulu, ndilo ambalo linaunda kundi kubwa la Wakulima, Wafanya biashara na wengineo ambao rasilimali yao imetumbukizwa na kuhusishwa kwenye biashara hiyo, kwa sababu zao kujikinaisha, hufikiria kwamba hapangekuwepo na hatari.

Ujasiri ambao jaribio hilo limepata msisimko mshangao wangu na hasira, na ingawa watu fulani wenye uwezo mkubwa wameliunga mkono, ama kwa sababu ya kutaka umaarufu wa muda mfupi, wakati wanao utajiri, au kupenda kujumuika kwenye fitina, wakati hawana kitu, maoni yangu hayatetereki.

Kukomesha hali ya kuwepo utumwa ambayo katika zama zote, MUNGU ameruhusu, na binadamu akaendeleza, haingekuwa unyang’anyi tu kwa tabaka la raia wetu wasio hesabika; lakini pia ingekuwa ukatili mno kwa Washenzi wa Kiafrika, ambao sehemu kutoka miongoni mwao inaokolewa kutoka kwenye mauaji ya kinyama, au kutoka kwenye utumwa isiyovumilika katika nchi yao wenyewe, na huwaingiza kwenye maisha ya hali ya furaha zaidi, hasa zaidi sasa kupita kwao kwenda katika visiwa vya West-Indies na wanavyotendewa huko katika hali ya udhibiti wa kibinadamu. Kukomesha biashara hiyo itakuwa sawa na kufunga milango ya huruma kwa binadamu.”8Marekebisho ya takrima ya kibinadamu wanayofanyiwa na huruma, hujionyesha yenyewe kwenye maelezo ya kina na picha iliyoonyeshwa hapo juu!

 • 1. Alpers, Edward A., East Africa Slave-Trade (Dar-es-Salaam: The Historical
  Association of Tanzania, 1967)
 • 2. Rodney, Walter., West African and the Atlantic slave-trade (Dar- es-Salaam: The
  Historical Association of Tanzania, 1967)
 • 3. Newsweek (March 15, 1965) uk. 106
 • 4. Rodney, op. cit., uk.4-5
 • 5. Ibid, uk. 7f.
 • 6. Ibid uk.22.
 • 7. Lloyd’s list, 250th Anniversary (1734-1984) April 17, 1984, London, uk. 149.
 • 8. Boswell, J, Life of Johnson (N.Y. Modern Library Edition, 1965) Uk. 365

Biashara Ya Watumwa Ya Afrika Ya Mashariki

Kama ilivyokuwa Afrika ya Magharibi, biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki ilikuwa mashuhuri na ilianzishwa kikamilifu na kutokana na maendeleo na jitihada za nchi za Kikristo za Ulaya. Bwana E. A. Alpers anaandika kwenye “African Slave-Trade (Biashara ya Utumwa ya Afrika):

Ushahidi zaidi kwamba biashara ya watumwa kwa vyovyote vile ilikuwa mashuhuri katika Afrika ya Mashariki kabla ya karne ya kumi na nane, imeletwa na Wareno. Hakika Wareno, wakiwa ndiyo waasisi (waanzilishi) wa Atlantic Slave-Trade, wangejaribu kuendeleza biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki kama wangeikuta tayari ipo na imekwisha shamiri. Lakini maandiko ya mwanzo ya Wareno yanataja tu biashara ya watumwa kwa kupitia tu.

Lililokuwa muhimu zaidi ni wale wafanyabiashara za dhahabu na pembe za ndovu walizipeleka Arabuni na India. Wavamizi wa Kireno walielekeza juhudi zao kwenye bidhaa hizo wakati wa karne ya kumi na sita na kumi na saba, sio tu kwenye pwani ya Kenya na Tanzania, bali pia katika Msumbiji na Zimbabwe. Hata nta na ambari zinaonyesha zilikuwa bidhaa muhimu zaidi kuzidi watumwa wakati mrefu sana wa kipindi hiki. Kwani tofauti na wakoloni katika nchi ya Amerika, Wareno kamwe hawakuanzisha uchumi wowote wa kilimo huko India.
Biashara ya watumwa ya Wareno kutoka Msumbiji kwenda India kwa nadra sana ili- fika idadi ya watu elfu moja katika kipindi cha mwaka mmoja wowote ule, na kwa kawaida ilikuwa chini ya nusu ya idadi hiyo. Huko Brazil ilikuwa haramu kufanya biashara ya watumwa hadi mwaka 1645, na kamwe haikulitiliwa maanani hadi mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa. Hadi mwaka wa 1753, wakati misingi ya biashara mpya ya watumwa ilikuwa inawekwa Afrika ya Mashariki, palikuwepo na jumla ya watumwa 4399 tu wa Kiafrika katika India yote ya Wareno.

“Misingi hii ni ipi? Licha ya mahusiano ya muda mrefu baina ya Waarabu na Afrika ya Mashariki, biashara ya watumwa haikutiliwa matumaini na Wafaransa. Kwa mujibu wa tarakimu rasimi, zaidi ya watumwa 1,000 walikuwa wanasafirishwa kila mwaka. Wafaransa, wakifanya magendo kwa ajili ya kukwepa kodi ambazo zilitozwa Msumbiji, labda waliongeza idadi na kufika angalau 1,500. Inawezekana ni idadi ile ile ilichukuliwa kutoka Ibo wakati wa muongo huu. Kwa hiyo Wareno kule Msumbiji na Ibo (na baadaye Quelimane, karibu na mdomo wa mto Zambezi unapoingilia baharini) walijishughulisha na sera ya biashara ya watumwa na hawakurudi nyuma, wakaendelea nayo hadi kukomeshwa kwake.

Biashara ya watumwa ilizidi kupamba moto mnamo miaka ya themanini, hasa zaidi baada ya kumalizika vita ya uhuru wan chi ya Amerika.

Katika miaka ya sabini, wafanya biashara ya utumwa wachache wa Kifaransa walichukua mizigo kutoka Msumbiji kwenda visiwa vya West-Indies, kwa sababu waliiona hasara ilikuwa inaongezeka katika wakati wa kutafuta bidhaa zao zinazohamashika kwenye pwani ya Guinea. Sasa, wakati wa amani, kwa mashindano makubwa zaidi ya kutafuta watumwa katika Afrika ya Magharibi, ilifunguliwa njia kwa ajili ya upanuzi mkubwa wa biashara ya watumwa ya Waamerika kutoka Afrika ya Mashariki.

Wakati huo huo meli za Wareno pia zilianza sehemu ya kufaa (ingawa ilikuwa bado ni ya kufuata) katika biashara ya watumwa kwenda kisiwa cha Mascarene. Tarakimu rasimi kutoka Msumbiji peke yake zinaonyesha kwamba tangu 1781 hadi 1794 jumla ya watumwa 46,461 walipakiwa kwenye meli za Kireno na za kigeni, ambazo karibu zote zilikuwa za Wafaransa. Ikijumlishwa na idadi ndogo ya magendo, angalau watumwa 4,000 lazima walikuwa wanaondoka Msumbiji wakati wa kipindi hiki kila mwaka.” 1

Ilikuwa katika hali hii ambayo Waarabu walipanua msaada wao kuwasaidia hawa wafanyabiashara ya utumwa wa Kikristo. Mwandishi huyo huyo anasema: “Baada ya Waarabu wa Oman kuitika wito wa baadhi ya watawala wa Kiswahili wa miji ya pwani na kwa msaada wao waliwatoa Wareno kutoka Mombasa mnamo 1698 na sehemu zingine muhimu za mbali, wao wenyewe walikuwa wanyonge sana kushughulika na jambo lingine zaidi ya kuwasumbua na kuwaibia watu hao hao waliowaomba msaada wao; lakini baada ya familia ya Busaid ilipowapindua Yarubi na kuanzisha utawala wao katika Oman mnamo 1744, wali- weza kuanza unyonyaji wa kiuchumi wenye faida kutoka kwa watu wa Afrika ya Mashariki. Kama walivyofanya wafanya biashara wote wa zamani sehemu ya pwani, lengo lao kubwa na la msingi ni kupata pembe za ndovu, lakini kuanzia hapo pia tunaweza kuona ongezeko katika biashara ya watumwa.

“Hata hivyo, hakuna takwimu sahihi zozote zile zenye kuonyesha kuhusu ukubwa wa biashara ya utumwa iliyofanywa na Waarabu katika karne ya kumi na nane. Dalili ya kwanza iliopo inatoka kwa mfanya biashara ya watumwa wa Kifaransa aitwaye Jean Vincent Morice, ambaye alifanya biashara Zanzibar na Kilwa, ambayo ilikuwa bandari muhimu ya watumwa katika pwani, mnamo miaka ya 1770. Mnamo tarehe 14, September, 1776, Morice alifanya mkataba na Sultani wa Kilwa kwa ununuzi wa angalau watumwa
1,000 kwa mwaka. Katika misafara mitatu kabla ya kuutia sahihi mkataba huu, Morice alikwisha nunua watumwa 2325 kwa ajili ya kuwasafirisha nje. Morice hatuambii Waarabu walikuwa wakiwachukua watumwa wangapi kutoka pwani kila mwaka, lakini kwa wazi aliona kuwa ilikuwa biashara kubwa kwa viwango vya Kifaransa.

Inaonekana ni sawa kusema kwamba angalau watumwa 2000 walikuwa wanachukuliwa kwa mwaka katika kipindi hicho. Kwa hiyo, licha ya kwamba Wafaransa hawakutawala biashara ya watumwa hapa kama walivyofanya Msumbiji, walikuwa kichocheo kwa mahitaji ya soko la watumwa katika kipindi ambacho biashara ya Waarabu ilikuwa bado ndiyo inakua katika uchanga wake. Juhudi za Ufaransa ziliendelea hadi miaka ya 1780, lakini mnamo mwishoni mwa karne hiyo, juhudi hizi zilionyesha zilikwisha pungua sana umuhimu wake kuliko biashara ya Waarabu.

Mambo kadhaa mapya yalisababisha kuongezeka mahitaji ya watumwa kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya kumi na tisa. Katika eneo la mamlaka la pwani ya Ureno, palikuwepo na ongezeko la juu sana katika biashara ya utumwa kwenda Brazil. Hii ilisababishwa na kuondolewa kwa familia ya kifalme ya Kireno kutoka Lisbon kupelekwa Brazil wakati wa Vita za Napoleon. Ruhusa maalum zilitolewa kwa Wabrazil na mara biashara inayoshamiri katika watumwa ikawa inaendeshwa kupitia Rasi ya Tumaini Jema huko Afrika ya kusini.2

“Sasa ni ukweli unaokubalika miongoni mwa wataalam wa historia makini wa Afrika ya Mashariki kwamba njia ndefu za biashara kati ya bara na pwani zilianzishwa hasa zaidi kwa kutumia ujasiri na moyo wa kujituma wa Waafrika. Kwa maneno mengine njia za biashara zilibuniwa na Waafrika kutoka bara kwenda pwani, wala si Waarabu, au Waswahili, ambao walisafiri kutoka pwani kwenda bara kupitia sehemu zisizojulikana.

Wafanya biashara wa Kiswahili walianza tu kutelekeza usalama wa pwani mnamo nusu ya pili ya karne ya kumi na nane, na walisafiri kufuata njia safi ambazo ziliendelezwa kwa miongo mingi kabla yake. Ni baada tu kuanza karne ya kumi na tisa ndipo wafanya biashara wa Kiarabu walijasiri kufuata njia hiyo.” 3

Wayao ambao walikuja kuwa wafanya biashara makini sana wa Kiafrika wa biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki, hivyo walikuwa na desturi ya muda mrefu ya kubeba pembe za ndovu na bidhaa zingine halali kwenda pwani miongo mingi kabla ya mahitaji ya pamoja ya Wafaransa na Waarabu kutaka watumwa yalipoeleweka.”4

“Katika Afrika Magharibi njia hizi ziliendeshwa kwenda bara kutoka pwani na Waafrika ambao kazi yao hasa ilikuwa kutafuta watumwa. Watumwa walitawala biashara ya Afrika ya Magharibi tangu mwanzo. Katika Afrika ya Mashariki wala hapakuwepo na hali zilizolingana na hiyo. Biashara ya watumwa lazima ionekane kuwepo katika mazingira ya mapema zaidi, iliyokwishajengeka kwa umakini, na biashara yenye faida ya masafa marefu ambayo chimbuko lake ilikuwa ubebaji wa pembe za ndovu. Hii ni muhimu kukumbuka hasa kwa mikoa ya kusini ambalo kila mara ilikuwa hazina kuu ya “Biashara ya Utumwa katika Afrikamashariki.”5

Bwana Alpers anahitimisha, “lazima iwe wazi sasa kwamba fikira ya zamani inayotamkwa kiholela kwamba wengi wa watumwa walikamatwa na wafanya biashara wanyang’anyi wa Kiarabu na Kiswahili ni moja wapo ya mambo ya kubuniwa na ngano tu ambazo zimekuzwa kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika mashariki. Lakini lazima tuwe waangalifu tusifanye kosa la kutoa tathmini potofu kuhusu mchango waliotoa watu hawa kwenye biashara hii.” 6

Kwa mara nyingine, lazima nisisitize kwamba lengo langu si kudhihaki juhudi za kundi dogo la waadilifu ambao walikuwa wanashughulika na propaganda dhidi ya utumwa. Ninachotaka kuonyesha ni kwamba juhudi zao hazikufaulu (na hazingefaulu) hadi pale shinikizo la kiuchumi lilipoilaz- imisha kwanza Uingereza ilipolazimika kufuatana na matatizo ya kiuchumi kuanza kuzuia utumwa, biashara ya utumwa na halafu kukomesha utumwa.

Kwa kweli, Uingereza ilipojitokeza kwa ajili ya kutaka kukomesha utumwa haikusimama kwenye mapaa ya nyumba na kutangaza kwamba ilikuwa inakomesha utumwa kushindana dhidi ya wenye viwanda wa Kifaransa. Uingereza ililigeuza jambo hili kuwa suala la kimaadili na kiunyofu kabla haijatumainia kushinikiza serikali zingine kufuata mpango wake. Na ilifanya hivyo. Tunatambua jinsi Uingereza ilivyoanzisha vita si kwa lengo la kulinda maslahi ya himaya yake kiuchumi na kisiasa, lakini ilifanya hivyo ili “kulinda Uhuru wa Watu.”

Ndivyo ilivyokuwa kuhusu vita yake dhidi ya utumwa. Murua na maadili mema lilikuwa suala la waadilifu wachache tu ambao hawakuwa na uwezo. Suala halisi, kama serikali mbali mbali na walowezi na wakoloni walivyohusika, lilikuwa kuhusu uchumi.

 • 1. Alpers, op. cit., uk. 5-6
 • 2. Ibid uk. 7-8.
 • 3. Ibid, uk. 13.
 • 4. Bid, uk. 14.
 • 5. Ibid uk. 15.
 • 6. Ibid uk. 24.

Mateso Ya Watumwa

Tumekwisha ona Uislam ulichofanikiwa katika kupunguza ukali wa maumivu ya taabu ya watumwa na jinsi gani, kwa mara ya kwanza na mara ya mwisho katika historia, watumwa walivyopewa hadhi ya ubinadamu wakiwa na haki juu ya wamiliki wao. Sasa hebu tuangalie jinsi Wakristo walivyo watendea watumwa wao. Kabla ya kutoa maelezo, lazima niweke jambo moja wazi. Maelezo haya ni ya kuhusu taabu za watumwa katika kipindi cha karne tano zilizopita ambapo, kama ilivyoelezwa mapema, Wakristo walianza biashara ya watumwa ya huko nyuma katika kiwango kisichoeleweka. Kama nilivyoonyesha kwenye sura iliyo pita, Waarabu pia waliwapa Wakristo msaada katika jambo hili kwa hiyari yao katika kipindi cha robo ya mwisho ya karne ya kumi na nane.

Kwa kuwa maelezo mengi mno ya nchi za Ulaya kuhusu biashara ya utumwa katika bara la Afrika, huanza kwenye kipindi hiki, kwa hiyo yapo maelezo mengi yaliyo wazi kabisa kuhusu yale yaliyoonekana na watu huko. Hivyo, Wakristo lazima wabebe uzito wa kuhusika na machukizo haya kwa kiwango kikubwa. Wakristo walikuwa wanawapa mateso haya kwa kipindi cha karne nne ikilinganishwa na karne moja ambayo ndicho kipindi ambacho Waarabu waliungana nao katika kuwashawishi ingawaje walihiyari kufanya hivyo.

Waathirika hao walikuwa Waafrika masikini wasiokuwa na ulinzi, watu wewusi (manegro) wa pwani ya magharibi na Mashariki ya Afrika na pia waliotoka katikati ya bara hilo. Waafrika walifanywa kama mali inayohamishika tu na vitendea kazi au viliyo vibaya zaidiya hapo. Ilibidi wafanye kazi, au pengine walilazimishwa kufanyakazi katika masharti yaliyo magumu sana kwenye mashamba mapya yaliyomilikiwa na mabwana zao, mataifa yenye nguvu yaliyo ya Kikristo ya nchi za Magharibi, ambao walichukua na kuvimiliki visiwa vyote kuvuka bahari ya Atlantic na katika ulimwengu mpya na vile vile hata nyumbani nchini Ureno na Hispania na nchi za Ulaya ya kati ya Ufalme Mtakatifu wa Kirumi chini ya miliki ya mapapa wa Kanisa Katoliki.

Mateso ya biashara ya utumwa yalijitokeza zaidi wakati wa robo ya mwisho ya karne ya kumi na tisa. Popote pale uvamizi ulipofanyika kijijini, vifo na uharibifu vilifuatia (vilitokea). Watu wengi zaidi walikufa wakilinda nyumba na familia zao, au kutokana na matokeo ya njaa na magonjwa ambayo kwa kawaida yalitokea baada ya vurugu kama hizo kuzidi, basi watu wengi waliofanywa kuwa watumwa, achilia mbali na wale waliouzwa huko pwani.

Mtu anaweza kutetemeka anapofikiria njia mbaya sana na za kikatili mno zilizotumika kuwakamata wazalendo masikini wa Afrika, walitenganishwa na ndugu zao, walichukuliwa na kutendewa vibaya zaidi kuliko hayawani. Sasa tutatoa maelezo mafupi kutoka kwenye vitabu vyao wenyewe, vya waandishi wa nchi za magharibi ili tuonyesha jinsi gani watumwa walivyoteswa na mbinu zipi za kikatili zilizotumiwa na wawindaji wa watumwa. Mbinu zao wakati fulani zilitekelezwa kiholela, na ziliingiza hasara, kwa sababu walikuwa wezi, si wapiganaji. “Utendaji wao ulikuwa kuzunguuka vijiji kadhaa ambavyo waliviteua kuvivamia, walinyemelea kimya kimya wakati wa usiku. Kwa kawaida kijiji kilikuwa kimejengeka kwa vibanda vilivyojengwa kwa tope ya kawaida na kuezekwa kwa mianzi na majani ya mchikichi, vyote hivi vikiwa vinashika moto na kuungua kwa urahisi sana, kwa hiyo, wavamizi walichoma moto vibanda hivyo bila aibu wala haya, na mara nyingi wali- fanya hivyo wakati wa alfajiri.

Wakazi wa vibanda hivyo walipoamka kutokana na mngurumo wa moto unaowaka kwa ukali walijikuta hawana la kufanya isipokuwa kukim- bilia nje, ambako huko walizingirwa na kukamatwa. Yeyote miongoni mwao aliyejaribu kuleta upinzani, aliuawa, kwani wawindaji wa watumwa hawakuwa na huruma.

Wazee na wasiojiweza na watoto wachanga waliuawa hapo papo kwani hawakuwa na shida nao, na ni wale tu wanaume na wanawake wenye nguvu, na wavulana na wasichana, waliachwa hai, ili wapelekwe utumwani, huku nyuma wakiacha maiti tu na majivu ya nyumba zilizoungua, mahali ambapo hapo mwanzo palikuwepo familia zenye furaha na makazi yaliyokuwa yanashamiri. Hasara ilikuwa kubwa mno kuzidi hiyo zawadi. Lakini uharibifu, mkubwa mno ilikuwa kama alama ya utumwa wa watu weusi, tangu nyakati zake za mwanzo, hadi mwisho. Popote pale utumwa ulipotokeza hali iliyofuata, ni vifo, magonjwa na maangamizi.

Watu waliokamatwa kutoka katikati ya mikoa ya bara walikuwa na bahati mbaya kidogo, walilazimika kutembea kwa miguu yao hadi pwani – mwendo mrefu wa kuchosha na kutia huzuni wa maili nyingi na msitu mnene na jangwa baya. Walitembea bila kuwa na nguo za kutosha, bila ya kinga yoyote dhidi ya miba mikaliu na mawe yenye ncha chonge na yenye kukeketa. Ili kuwazuia watumwa wasitoroke, walivishwa kongwa shingoni, wale waliokuwa wasumbufu, mikono yao iliingizwa kwenye ubao unao kwaruza wenye matundu, visigino vya miguu yao ilifungwa kwa minyororo.

Misitari mirefu iliyojulikana kwa jina la watumwa, iliunganishwa kwa kamba, walisafiri mwendo, mrefu kwa taabu kuelekea kwenye hatima yao ya kutisha, kwani Waafrika wote walikuwa wakielewa kwamba wazun- gu walikuwa wanakula nyama ya watu weusi ambao waliwanunua kutoka kwenye boma. Wamiliki wao waliwaswaga mbele kwa mateso makali na bila kupumzika, bila kujali majeraha na mikwaruzo ya ngozi, waliishiwa na nguvu kwa sababu ya kuchapwa mijeledi mingi. Kama kuna yeyote aliyeelemewa na mateso hayo na akashindwa kabisa kuendelea mbele, alitupwa pembeni mwa njia, na kama kuna mmoja wao alizidiwa na maradhi, aliachwa afe au kwa kuhurumiwa zaidi aligongwa kichwa ili afe haraka.” 1

“…Kwenye hali ya hewa nzuri au mbaya, pamoja na magonjwa na vifo, na kwa maasi yote na kujiua wenyewe, kila mwaka meli zilileta maelfu ya watumwa Marekani na katika visiwa vya West Indies. Walikuja kwa meli za mataifa mengi: Ufaransa, Udachi, Ureno, na Danmark – lakini zaidi ya nusu waliletwa na meli za Kiingereza ambazo zilisafiri kutoka Bristol, London, au Liver pool. Kila mwaka, walifikishwa pwani katika hali ya kuugua au wazi- ma wa afya, wakiwa wamekubali matokeo ya maisha au kukata tamaa na daima milele hawakurudi tena walikozaliwa… Matumizi ya watumwa, kama ilivyo matumizi yake mabaya, kamwe hayabadiliki; yalifanana kote duniani na kutoka kipindi kimoja hadi kingine.

Huko Marekani na katika visiwa vya West-Indies, kama ilivyokuwa wakati wa Rumi ya kale, au Ugiriki au mwanzo wa historia isiyo dhahiri, utumwa uligawanywa kwenye aina mbili pana utumwa wa kutumika ndani ya nyumba na utumwa wa kutumika mashambani.” 2

Sasa ngoja tuoneshe nukuu zingine zaidi kutoka kwenye kitabu hicho hicho “Freedom from Fear or the Slave and his Emancipation” kilicho andikwa na O.A. Sherrard, kuonye- sha jinsi gani na kwa kiwango gani mataifa ya mwanzo kabisa ya Kikristo kutoka Magharibi yalivyowatesa kinya- ma mno bila ya huruma watu Weusi ambao hawakuwa na namna yoyte ya kujilinda. Pia msomaji ataona imani na fiki- ra zao duni kuhusu binadamu ambao walitofautiana nao kwa rangi na taifa.

“Tukiangalia historia kwa mapana yake, walipita katika hatua mbili: katika hatua ya kwanza uvumilivu mabegani mwao, kama Atlas mstahamilivu, utukufu wa mamlaka nyingi zilizostaarabika zilizokufa zamani; na hatua ya pili yenye kudhalilisha zaidi kuliko ya kwanza, walipoteza hata ile heshima ya uwakilishi, na kuanguka kwenye hali ya unyonge ambamo mchango wao ulikuwa kutumikia uroho wa watu binafsi.
Hali yao, hasa zaidi katika hatua ya pili, wangeweza kuiogopesha dhamiri mbaya ya dunia ya Kikristo kwa jina, lakini jambo la kushangaza ni kwamba waliiacha hivi hivi bila yenyewe kusisimka. Wazo la utumwa lilikolea sana hivyo kwamba hakuna mtu aliye hoji usahihi wake. Mataifa yote ama yalifumbia macho au yalifurahia jambo hilo.” 3

Watumwa wengi waliofanya kazi kwenye mashamba, kazi yao ilikuwa ngumu sana, kazi aliyopewa, kwa mawazo yake ilikuwa kazi ya kifundi; alitakiwa kulima zao ambalo lilikuwa geni kwake – kwa sehemu kubwa miwa katika visiwa vya West Indies, pamba na tumbaku huko Marekani na kwamba kazi yake ilikuwa mpya alistahamili mzigo mzito zaidi kuliko mwenzake huko Ugiriki au Rumi au miongoni mwa watwa na wajakazi wa Ulaya… Kila kitu kilikuwa kipya na kigeni kwake; kwa hiyo, alivunjwa vun- jwa moyo humo; alitakiwa afundishwe kazi zake mpya; ali- zoneshwa kama usemi ulivyokuwa.

‘Kuzoesha’ ilikuwa neno lililotumika badala ya nidhamu kali, ambayo ilifikiriwa na wapinzani wa utumwa kubeba si chini ya asilimia ishirini ya wale waliopitia humo. Inawezekana hiyo inazidi kiwango halisi, lakini hata hivyo lazima ikubalike kwamba idadi kubwa walikufa. Nidhamu ilikuwa chungu, hapakuwe- po na nafasi ya kurekebisha kwa kuifanya kuwa nzuri zaidi na asili mia sabini hawakufika mwisho.4

Watumwa walipita kwenye hatua ngumu za mateso ya kuo- gofya na kutisha hasa. Limbikizo la athari za mateso yote zilikuwa msiba mkubwa. Tunamnukuu Sherrard tena, “hii ilikuwa kweli zaidi kwenye mpito wa ‘nidhamu’, kwani bila shaka yoyote sehemu kubwa ya watumwa waliokufa kwenye nidhamu yake wangekufa katika tukio lolote kutokana na athari za mpito wa kati. Uzoefu ulionyesha kwamba idadi kubwa zaidi ya watumwa waliokuwa dhaifu au kukonda wakati walipowasili, walikufa muda mfupi baadaye kutokana na jambo lolote walilofanya. Mamlaka za tiba zilitoa taarifa kwamba hali hiyo ilisababishwa na kufungiwa kwenye nyumba za watumwa kwa muda mrefu kabla ya kupanda meli, haja ya usafi na hewa wakati wapo ndani ya meli, kubadilisha nguo, chakula na tabia, na hasa zaidi mabadiliko ya hewa (Buxton, uk. 188).

Lakini walikubali kwamba palikuwepo na jambo lingine zaidi ya hilo-hujuma ya kisaikolojia au kiroho, ambayo waliielezea, labla kwa namna ya ajabu, kama ‘masikitiko ya kukumbuka ndugu na urafiki, uvunjaji sheria wa kifidhuli wa yale yote yaliyokuwa yanaheshimiwa sana na mapenzi ya kijamii ya nchi na undugu, na matumaini yasiyo na mwisho ya kushushwa daraja ya utumwa kamili.’ Hili likijumlishwa kwenye mateso ya kimwili pia lilivunja utashi wa kuishi na mtumwa alifanya hivyo haraka sana pindi alipopata nafasi ya kwanza, au kwa urahisi zaidi, alijibana na kufa.”

Kwa uchache, walikuwepo wamiliki wa aina tano na sura tano za utumwa wa watu weusi – Kihispania, Kifaransa, Kidachi, Kidenishi na Kiingereza bila kuhesabu Marekani, ambayo mwanzoni ilikuwa Kiingereza. Waamerika ndani ya U.S.A., hadi sasa, karne hii ya ishirini, wanavunja sheria zao wenyewe na mtu mweusi bado hajafuzu kupata haki kamili za uraia, na yapo matatizo kwa Mtu Mweusi (Mnegro) nchini kwake mwenyewe kama dunia ijuavyo fika (vema).

Hatima ya kuogofya ya mtumwa wa shamba ni mbaya – jinsi alivyopigwa chapa kwa chuma chenye moto, alivyolazimishwa kushughulikia minyororo mizito, mgongo wake ulichanika na kuwekwa alama za kuchapwa kwa kiboko, jinsi alivyofungiwa jela w

akati wa usiku, makazi na malazi yake, mara nyingi yamejengwa chini ya ardhi na ni machafu.” Wareno walijenga msululu wa ngome, katika pwani ya Guinea, ambamo Waafrika wanyonge waliwekwa baada ya kukamatwa hadi idadi ilipotimia kustahili kusafirishwa kwenda Hispania, kwenye utumwa na baadaye Marekani na Ulimwengu Mpya…

roho zao zilihukumiwa kwenye mateso ya milele; miili yao ilikuwa mali ya taifa la Kikristo ambao wangekalia nchi yao.”5
Mwandishi anaelezea jinsi utumwa ulivyoanzishwa kwenye makoloni ya Uingereza ndani ya Marekani: “Meli ya Kidachi ilikuwa inaingia kwenye Mto Jame huko Virginia na kupakuwa watumwa weusi ishirini wa kuuzwa. Wakoloni waliwanunua haraka sana na hivyo utumwa wa Mtu Mweusi ukaanzishwa huko kwenye makoloni ya Uingereza yaliyokuwa Marekani.” Kwa kipindi kifupi,” Uingereza ilipata nafasi ya kwanza ya shehena za siri za watumwa, nafasi ambayo ilishikilia kwa kipindi cha zaidi ya miaka tisini.”

Watumwa waliuzwa kwenye minada, walinunuliwa wakiwa uchi wa mnyama, wanaume kwa wanawake wote namna moja, na mtumwa alikalishwa kwenye kiti, ambapo wanunuzi (wazabuni) walimkagua na kushika shika misuli yake na kukagua meno na kumfanya aruke na kunyoosha mikono, ili kuthibitisha kwamba hawakununua mtumwa mgonjwa au asiye jiweza. Kwa kuwa watumwa walinunuli- wa mmoja mmoja, kilichofuata ni kwamba mume na mke, watoto na wazazi walikwenda kwa wamiliki tofauti; na hasara ya ndugu na jamaa na yote yale ambayo watumwa walikuwa wanayapenda yalijumlishwa kwenye hasara ya kukosa uhuru, kwa hiyo mtumwa aliondoka kwenye chum- ba cha mnada, akiwa amenyang’anywa kila kitu, kuanza maisha mapya yalio duni, ya kukata tamaa na utumwa wa kuangamiza.”6

 • 1. Sherrad, B. A., Freedom from Fear (London, 1959) uk. 61-62.
 • 2. Ibid. uk. 67f.
 • 3. Ibid uk. 11.
 • 4. Ibid. uk. 69.
 • 5. Ibid. uk. 26.
 • 6. Ibid uk. 67

Makanisa Yashiriki Biashara Ya Watumwa

Kanisa la Kikristo lilikuwa na msimamo gani kuhusu biashara ya utumwa wa mtu Mweusi? Tangu mwanzo wake, Ukristo ulifumbia macho hali mbaya ya watumwa. Kama ambavyo imeelezwa huko mwanzoni, ni katika rejea moja tu kuhusu utumwa ndipo inapatikana kwenye waraka wa Mt. Paulo, akimrudisha mtumwa kwa Filimoni kwa mmiliki wake. Basi, ni hiyo tu basi. Ameer Ali anafafanua kwa usahihi kwamba: “Ukristo ulikuta utumwa ni taasisi inayotambuliwa na ufalme; ulikubali mpango huo bila kujaribu kupunguza ukali wa tabia yake ya uovu; au kuendeleza kuukomesha pole pole, au kunyanyua hadhi ya watumwa.”1

Ili kutambua nini Makanisa ya Kikristo yalifanya kwenye biashara ya watumwa ni vema mtu asome tena maneno ya Bwana Alpers ambaye anaandika, pamoja na mambo mengineyo, kwamba: “Wakristo walitambua kwamba kuuza binadamu wenzao hakungehalalishwa na kuthibitishwa kimaadili. Hata hivyo, kanisa la Kikristo lili- jitokeza na visingizio kuhusu biashara ya watumwa. Wachungaji wenyewe wengi walifanya biashara ya watumwa, hasa zaidi katika nchi ya Angola, na wengine wengi walimiliki watumwa huko Amerika ya Kusini na Kaskazini.

Sababu moja tu ambayo ilitolewa na Kanisa Katoliki kuhusu kuwepo kwake kwenye biashara ya watumwa ni kwamba lilikuwa linajaribu kukomboa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa ndiyo wabaya zaidi, kwani wao hawakukubali hata angalao kusema wazi kwamba wanakubali kwamba Waafrika wana roho.

Badala yake waliunga mkono wazo kwamba mtumwa wa Kiafrika alikuwa sehemu ya rasilimali kama fenicha au mnyama wa kufugwa.

Hakuna sehemu ya historia ya kanisa la Kikristo ambayo ilikuwa ya kufedhehesha zaidi kuliko kujihusisha kwake na “Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki.” 2

Hoja za James Boswell zimekwisha nukuliwa ambamo ame- sisitiza kwamba utumwa ni taasisi ambayo iliruhusiwa na Mungu katika vipindi vyote na kwamba kuikomesha ingekuwa sawa na kufunga lango kuu la huruma kwa wanadmau!

Sasa ninanukuu kutoka kwenye “Capitalism and Slavery” maandishi ya Dk. Eric Williams, ambaye alikuwa mtaalam wa historia aliyetambuliwa na pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago. Anaadika: “Pia Kanisa liliunga mkono biashara ya watumwa.

Wahispania waliona fursa ya kuwageuza imani wapagani ndani ya biashara hiyo, na (madhehebu ya Kikristo ya) “the Jesuits”, “Dominicans” na “Franciscans” walijihusisha mno na kilimo cha miwa, ambacho kilisababisha umilikaji wa watumwa muhimu. Hadithi imesimuliwa kuhusu mzee wa Kanisa huko Newport ambaye kila wakati, Jumapili iliyofuata baada ya kuwasili watumwa kutoka pwani, alikuwa anamshukuru Mungu kwamba mzigo mwingine wa viumbe washenzi uliletwa mahali ambapo wangeweza kupata manufaa ya neno la Injili.’

Lakini kwa ujumla wakulima wa Kiingereza walipinga Ukristo (kufundishwa) kwa watumwa wao. Ukristo uliwafanya watumwa kuwa wapotovu zaidi, kutokuwa watiifu na kwa hiyo wanakuwa hawana thamani. Pia ilikuwa na maana pia kutoa maelekezo kwa lugha ya Kiingereza, jambo ambalo liliruhusu makabila mbali mbali kukutana pamoja na kupanga njama za uasi… Gavana wa Barbados mnamo mwaka wa 1695 alilihusisha hilo na wakulima kukataa kuwapa watumwa mapumziko siku ya Jumapili na sikukuu, na mwishoni mwa 1832 maoni ya umma wa Uingereza (Britsh public opinion) yalishtushwa na wakulima walipokataa pendekezo la kuwapa Watu Weusi siku moja ya kupumzika ili kuruhusu kukomesha soko la Jumapili la Watu Weusi.

Kanisa lilitii. “Society for the Propagation of the Gospel” (chama cha kuitangaza Injili) kilikataza mafundisho ya Kikristo kwa watumwa wake huko Barbados, na kuwapiga chapa ya ‘Society’ (chama) watumwa wake wapya kuwatofautisha na wale waliomilikiwa na watu wa kawaida; watumwa wa mwanzo walikuwa urithi wa Christoper Codrington. Sherlock, baadaye akawa Bishop wa London, aliwahakikishia wakulima kwamba ‘Ukristo na kuikumbali Injili hakuleti hata cheme ya tofauti kuhusu mali za raia.’ Wala haukuwekwa vikwazo katika shughuli za kikanisa. Kwa kazi zake kuhusu Asiento ambazo zilisaidia kumfanya kama muwakilishi (Balozi) mwenye mamlaka kamili wa Uingereza huko Utrecht, Bishop Robinson wa Bristol alipandishwa cheo na kuwa Askofu wa dayosisi ya London.

Kengele za makanisa ya Bristol zililia kushangilia kuhusu taarifa ya kukataliwa na Bunge muswada wa Wilberforce uliotaka kukomeshwa kwa biashara ya watumwa. Mfanyabiashara wa biashara ya watumwa, John Newton, aliyashukuru makanisa ya Liverpool kwa ushindi wa jaribio hili la mwisho kabla hajabadilika na akaomba baraka za Mungu zimjie yeye. Alianzisha ibada ya hadhara mara mbili kwa siku kwa uchu wake, akihubiri yeye mwenyewe, na alitenga siku moja ya kufunga saumu na kusali, si kwa ajili ya watumwa bali kwa ajili ya wafanyakazi wa meli. ‘Sikujua,’ aliungama, ‘utamu au saa zaidi za sakramenti takatifu ziwe mara nyingi zaidi kuliko kwenye safari mbili za baharini za kwenda Guinea.’

Kadinali Manning maarufu wa karne ya kumi na tisa alikuwa mtoto wa mfanya biashara tajiri wa visiwa vya West Indies aliye kuwa anashughulika na bidhaa zilizo limwa na watumwa.Wamisionari wengi waliona ni faida kubwa kumfukuza Beelzebub kwa Beelzebub (yaani, kumfukuza shetani kwa kumtumia shetani). Kwa mujibu wa mwandishi wa siku hizi za karibuni sana wa Uingereza kuhusu biashara ya watumwa, walifikiri kwamba njia nzuri zaidi ya kurekebisha matumizi mabaya ya watumwa Weusi ilikuwa kumfanya mwenye shamba kuwa mfano mzuri kwa kuwatunza watumwa na mashamba wao weneywe, ili kutimiza katika utekelezaji wa aina hii ukombozi wa wamiliki wa mashamba na kuendeleza misingi yao.’

Wamisionari wa Kanisa la Moravian kisiwani hapo walimiliki watumwa bila kusita; Wamissionari wa Kanisa la, mwandishi mmoja wa historia anaandika kwa mtiririko wa mvuto kwamba Baptists (yaani, Wakristo wa madhehebu ya Baptst) hawakuruhusu wami- sionari wao wa mwanzo kupinga kumiliki watumwa. Hadi mwisho kabisa, Askofu wa Exeter aliendelea kuwa na watumwa wake 655, na mnamo mwaka wa 1833 alilipwa pauni za Kiingereza 12,700 kama fidia ya watumwa hao.

Wataalam wa historia wa Kanisa waliomba msamaha wa kufedhehesha, kwamba dhamiri ilizinduka polepole sana kutathmini uovu ulioletwa na utumwa na kwamba utetezi wa utumwa uliofanywa na watu wa kanisa ‘ulitokana na utashi wa uzuri wa utambuzi wa maadili.’ Hakuna haja ya kuomba msamaha wa aina hii. Msimamo wa watu wa kanisa ulikuwa ndio msimamo wa mtu wa kawaida. Karne ya kumi na nane kama nyingine yoyote, haingeweza kuvuka mipaka ya uchumi wake. Kama alivyo hoji Whitefield alipokuwa anatetea kusomwa tena kila kipengele cha mkataba wa Georgia uliositisha utumwa, ‘Ni rahisi kuonyesha kwamba nchi za joto haziwezi kulimwa bila Watu Weusi.’

Quaker (kundi la Wakirsto ambalo halipendelei mikutano rasmi na halipendelei ghasia au vita) - wasiofuata kanuni, hawakukubali kuacha biashsra ya watumwa. Mwaka wa 1756 walikuwepo Quaker themanini na nne waliorodhesh- wa kama wanachama wa kampuni ifanyayo biashara kwenda Afrika, miongoni mwao ni “the Barclay”: na “Baring families.” Shughuli ya watumwa ilikuwa moja wapo ya uwekezaji wenye faida kubwa wa Quaker wa Uingereza halikadhalika na wale wa Marekani na jina la mfanya biashara ya watumwa, The Willing Quaker, aliarifu kutoka Boston – Siera Leone mwaka wa 1793, inaashiria uthibitisho ambao ulisababisha biashara ya watumwa kuheshimiwa katika jamii ya Quaker.

Jamii ya Quaker ilifanya upinzani dhidi ya biashara ya watumwa kwanza kutoka Marekani na kutoka kwenye vijiji vya jamii ndogo vya kaskazini, ambavyo havikujihusisha na nguvu kazi ya watumwa. ‘Ni vigumu’, anaandika Dk. Gray, ‘kukwepa dhana kwamba upinzani huo dhidi ya mpango wa watumwa kwanza uliwekewa mipaka kwa kundi ambalo halikupata manufaa ya moja kwa moja kutoka kwenye biashara hiyo, kwa hiyo walikuwa wapinzani.’

Utumwa ulikuwepo wakati wa Mwingereza wa karne ya kumi na nane. Na sarafu ya Kiingereza, guinea, ingawaje ilipatikana kwa nadra, chanzo chake ilikuwa biashara ya Africa. Mhunzi wa dhahabu wa Westminster alitengeneza kufuli kwa ajili ya Watu Weusi na mbwa. Sanamu za watu weusi na tembo, ishara ya biashara ya watumwa zilipamba ukumbi wa Liverpool Town Hall. Alama za cheo na vifaa vya wafanya biashara ya watumwa vilionyeshwa wazi ili vinunuliwe kwenye maduka na kutangazwa kwenye magazeti.

Watumwa waliuzwa kwenye minada ya wazi. Watumwa wakiwa rasilimali isiyo na thamani, na wanaotambulikana kidogo sana kisheria, posta masta alikuwa wakala aliyetumiwa mara nyingi kuwakamata watumwa wanaokimbia na matangazo yalichapishwa kwenye vyombo vya habari vya kiserikali. Watumishi Weusi walionekana sehemu mbalimbali. Wavulana weusi wadogo walikuwa wasaidizi wa makapteni wa watumwa, wanawake wa mitindo au wanawake waadilifu. Mashujaa wanawake wa Hograrth, ‘The Harlots Progress’ kinahudumiwa na mvulana Mweusi, na Orabella Burmester ya Mar’guerito steen anaonyesha maoni yake ya kupenda mvulana mweusi mdogo ambaye angempenda kama mtoto wake wa paka mwenye manyoya marefu. Watumwa Weusi walioachwa huru walionekana miongoni mwa ombaomba wa London na walijulikana kama ndege weusi wa Mtakatifu Giles.

Walikuwa wengi mno hivyo kwamba iliundwa kamati ya bunge mwaka 1786 kwa lengo la kuwasaidia masikini weusi. Mshairi Cowper aliandika: “Watumwa hawawezi kupumua Uingereza.’ Hii ilikuwa leseni ya mashairi.

Mwaka 1677 iliaminika kwamba ‘Watu Weusi kwa kuwa ni kawaida kwamba hununuliwa na kuuzwa miongoni mwa wafanyabi- ashara, kwa hiyo wao ni bidhaa, na pia kwa kuwa kwao makafiri, inaweza kuwepo mali kwao. Mwaka 1726 Mwana sheria Mkuu alitangaza kwamba ubatizo haukumpa mtumwa uhuru au kufanya mabadiliko yoyote katika hali ya mpito ya mtumwa; juu ya hayo mtumwa hakuwa huru kwa kuletwa Uingereza, na mara afikapo Uingereza mmiliki wake angeweza kulazimishwa kisheria mtumwa husika kurudi mashambani. Hiyo mamlaka adhimu kama Sir William Blackstone aliamini kwamba kuhusu haki yoyote mmiliki wa mtumwa anaweza kupata uhalali kamili kwa ajili ya utumishi wa kuendelea wa John na Thomas (yaani watumwa waliobatizwa), watabaki katika hali ileile ya kutawaliwa maisha yote; hapa Uingereza au penginepopopote.” 3

Wakati meli zilizobeba watumwa kutoka nchi za Kikristo kwenda katika nchi za magharibi za Amerika ya Kaskazini na Kusini, wachungaji, wa Kikristo walikuwa na desturi ya kuzibariki meli hizo kwa jina la Mweza Mwenye nguvu zote na kuwaonya watumwa wawe watiifu. Kamwe haikupata kuingia akilini mwao hao wachungaji kuwaonya wamiliki wa watumwa kuwa na huruma kwa watumwa.

Ni vigumu kuamini lakini inaonyesha kwamba Kanisa Katoliki linafikiri ni sahihi kabisa na inaafikiana na mafundisho ya kanisa lao kununua watumwa hata katika kipindi hiki cha miaka ya 1970. Mwezi Augosti, 1970 dunia ilishtushwa kusikia kwamba Kanisa Katoliki lilimnunua, kwa bei ya kuanzia pauni za Kiingereza 250 hadi 300 kila mmoja, kiasi cha wasichana wa Kihindi 1500 na kuwafun- gia kwenye mabweni ya kidini kwa sababu wasichana wa Kizungu hawataki kuishi maisha ya usista. 4

Palitokea kilio kikubwa hapa duniani hivyo kwamba Vatican ililazimika kuunda tume ya kuchunguza jambo hili. Lakini hata kabla ya tume kuanza kazi yake ya uchunguzi, msemaji wa Vatican alikubali kuwepo kwa “ukweli” kwenye taari- fa hiyo, ingawaje katika kutimiza wajibu wa kazi yake alilaumu gazeti la Sunday Times kwa uchuuzaji wake wa hisia za watu.

 • 1. Ameer Ali, Spirit of Islam (London: University Paper-backs,1965) uk. 260.
 • 2. Alpers, op. cit., uk 22.
 • 3. Williams, op. cit., uk. 42-5
 • 4. Sunday Times (London,) kama ilivyonukuliwa katika East African Standard (Nairobi)
  Augast, 1970.

Kwa Nini Utumwa Ulikomeshwa.

Mtu anaweza akasema: “Hivi haikuwa Uingereza ya Kikristo hatimaye ndio iliyo komesha utumwa? Vema, kama mtu anafanya udhalimu si yeye ndiye anayetakiwa kuendeleza udhalimu huo? Kama ambavyo imekwisha elezewa, Uingereza ilikuwa ndio mfanya bishara ya watumwa mkub- wa zaidi ya wote, na nguvu za kiuchumi zilipoilazimisha kukomesha biashara ya watumwa, ilifanya hivyo. Je! ni Uingereza inayostahili au Ukristo ndiyo unastahili kupewa shukurani zozote kwa tukio hilo? Kwa nini tusizishukuru nguvu za uchumi ambazo ndizo zililazimisha Uingereza kutokuendelea na biashara hiyo?

Ukweli ni kwamba harakati dhidi ya utumwa hazikuongozwa na makanisa; kazi hiyo ilifanywa na watu waadilifu wachache ambao vilio vyao vilikuwa havisikilizwi hadi pale umuhimu wa kiuchumi ulipolazimisha Bunge kupitisha muswada mnamo mwaka wa 1870 dhidi ya biashara ya watumwa. Baada ya miaka 26, muswada mwingine ulipitishwa kukomesha utumwa katika makoloni ya Uingereza mnamo mwaka 1833. Kama Profesa D.W. Brogan alivyoandika kwenye utangulizi wa kitabu cha Dk. Eric Williams ambacho ni kizuri, kiitwacho “Capitalism and Slavery”,

“Kukomeshwa kwa biashara ya utumwa halafu kusitishwa kwa utumwa, hayakuwa tu matokeo ya kuboreka kwa kiwango cha mfumo wa maadili ya kisiasa humo Uingereza (ingawaje Dk. Williams hadharau kazi ya watu kama Clarkson kuwa ina umuhimu) lakini ilikuwa namna ya kupunguza hasara.

Ukiritimba wa kilimo cha miwa cha visiwa vya West Indies haukuvumilika kulinganishwa na jamii ya viwanda iliyokuwa inastawi haraka, yenye kujiamini kwa usahihi katika nafasi yake ya ushindani isio tetereka mnamo siku za mwanzo za mageuzi ya viwanda. “Kufupisha, kwa maneno ya Profesa Brogan, mpango wa utumwa ulikuwa “unavumiliwa, unatetewa, unasifiwa almuradi ulikuwa na faida.”

“Mpango wa mtumwa ulikuwa na faida sana na kwa kipindi kirefu. Mafanikio ya Bristol na Liverpool na kwa kiwan- go fulani, ya Glasgow yalitegemea faida ya mashamba ya miwa ya visiwa vya West Indies. Mkulima wa West Indies alikuwa mshindani wa ufahari wa tajiri mpenda anasa wa East Indies. Ilikuwa kama kupoteza muda kwa waadilifu kuonyesha kwamba kila tofali lililojenga maghala makubwa ya Bristol na Liverpool lilitokana na damu ya Mtu Mweusi. Lakini sauti ya waadilifu ilisikika mara chache sana miongoni mwa mlio wa sarafu ya Uingereza Guine (jina hilo hilo linakumbusha biashara ya pembetatu baina ya Uingereza, Afrika na makoloni ya transatlantic).”

“Biashara ya pembe tatu” maana yake ni nini? Kutoka Uingereza, bidhaa mchanganyiko “mfano halisi wa mzigo wa mfanya biashara ya watumwa” ulipelekwa Africa. Mavazi mazuri na umalidadi kwa Waafrika, vyombo vya nyumbani, nguo za kila aina, chuma na metali, pamoja na bunduki, pingu na minyororo.” Kutoka Afrika mzigo wa binadamu ulichukuliwa kupelekwa visiwa vya West Indies na nchi za Amerika.
Kutoka West Indes na makoloni mengine; sukari, tumbaku na rangi ya buluu, pamba, kahawa na malighafi zingine zilipelekwa nchi mama (yaani Uingereza) ambako yalitengenezwa kwenye viwanda na halafu yakaingizwa tena kwenye makoloni.1

Mashamba yalianzishwa kwa sababu ya kuwepo nguvu kazi ya utumwa na yakalindwa na ukiritimba. Halafu ukaja mtengano wa makoloni 13 ya Marekani ambayo yalifunga soko kubwa dhidi ya nchi iliyohuru makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West Indies. Athari yake nyingine ilikuwa kwamba nchi iliyo huru sasa, ya Marekani (U.S.A.) iligeuka kwenye makoloni ya Ufaransa yaani Visiwa vya Saint Domingue (Haiti), Cuba na Brazil. Dk. Williams anaandika, “Ubora wa makoloni ya sukari ya Ufaransa ulikuwa kwa ajili ya wakulima wa Kiingereza, kubwa miongoni mwa maovu mengi ambayo yalijitokeza nje kutoka kwenye Pandora’s box**. (sanduku la Pandora) ilikuwa ni mapinduzi ya Marekani. Kati ya mwaka 1783 na 1789 maendeleo ya sukari ya visiwa hususan vya Ufaransa, vya Saint Domingo (Haiti), hususan lilikuwa jambo la kushangaza katika maendeleo ya kikoloni. Rutuba ya udongo wa makoloni ya Ufaransa ilikuwa ni ya wazi mno, sukari ya Ufaransa iligharimu moja ya tano (1/5) chini zaidi ya ile ya Uingereza, mavuno ya wastani huko Saint Domingo na Jamaica yalikuwa tano kwa moja.”2

Athari iliyosababisha maafa kwenye makoloni ya Uingereza ya West Indies inaweza kuamuliwa na ukweli kwamba “mwaka 1775 Jamaica ilikuwa na mashamba 775; hadi kufika 1791, katika kila mashamba mia moja, mashamba ishirini na tatu yaliuzwa kwa ajili ya kulipa, kumi na mbili yalikuwa kwenye miliki ya wafilisi, wakati saba yaliachwa; na wakulima wa West Indies, wakiwa na deni la kiasi cha pauni milioni ishirini.”

Polepole, wakulima wa Kiingereza walipoteza moja kwa moja mamlaka yao ambayo waliyafurahia kwa kipindi kirefu katika soko la Ulaya. “Uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Ufaransa, uliingiza pauni za Kiingereza zaidi ya milioni nane, na Uingizaji bidhaa ndani ya nchi, zaidi ya pauni milioni nne, tani zilizo shughulikiwa 164,000 na wafanya kazi wa meli 33,600; uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Uingereza uliingiza pauni za Kiingereza milioni tano, na uingizaji bidhaa ndani ya nchi chini ya milioni mbili, tani zilizo shughulikiwa, 148,000 na wafanya kazi wa meli 14,000. Katika hali zote makoloni ya sukari yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Ufaransa kuliko yalivyokuwa kwa Uingereza.”3

Hivyo, gharama ya sukari (na hivyo hivyo kwa bidhaa zingine zote.) ilianza kwenda juu sana. Dk. Williams anaeleza, “Ukiritimba wa mkulima wa West Indies haukuwa tu jambo lisilofaa kinadharia, haukuwa na faida katika hali halisi. Mnamo mwaka 1828 ilikisiwa kwamba iliwagharimu raia wa Uingereza zaidi ya pauni milioni moja na nusu kwa mwaka. Mnamo mwaka 1844, ulikuwa unagharimu nchi pauni 70,000 kwa juma moja na jiji la London peke yake pauni 6,000. Uingereza ilikuwa inalipa zaidi ya pauni milioni tano kwa ajili ya sukari yake kwa mwaka kuliko Bara lota la Ulaya… Mbili ya tano (2/5) ya bei ya ratili moja ya sukari iliyotumiwa Uingereza iliwaisha gharama ya uzalishaji, Mbili ya tano (2/5) ilichukuliwa kama ushuru wa serikali, moja ya tano (1/5) shukurani kwa mkulia wa West-Indies…4

Pole pole, Saint Domingue (Haiti) koloni la Ufaransa, lili- ibuka kama mzalishaji muhimu sana wa sukari. Kwa mtazamo wa Waziri Mkuu wa Uingereza, William Pitt, hili lilikuwa jambo lenye uamuzi. Umri wa visiwa vya Uingereza vya sukari ulifika mwisho. Mpango wa West- Indian haukuwa na faida, na biashara ya watumwa ambayo ndio ilikuwa tegemeo lake, badala ya kuwa na manufaa kwa Great Britain… ni ya uharibifu mno ikilinganishwa na dhana ya maslahi.5
Kwa hiyo, Pitt aligeukia India kulima na kuzalisha sukari. Mpango wa Pitt ulikuwa na sehemu mbili: kurejesha soko la Ulaya kwa msaada wa sukari kutoka India, na kupata fursa ya kukomesha biasharra ya watumwa kimataifa tukio ambalo lingeiangamiza Saint Domingue. Kama haingekuwa ukomeshaji wa Uingereza. Wafaransa waliwategemea sana wafanyabiashara ya watumwa wa kimataifa, basi ingekuwa ukomeshaji wa Uingereza hivyo kwamba hata kama Uingereza peke yake ingepiga marukufu biashara ya watumwa, uchumi wa makoloni ya Ufaransa ungetetereka.

“Mpango wa Pitt ulishindwa kwa sababu mbili. Umuhimi wa sukari ya kutoka India ya Mashariki, kwa kiwango kilichopangwa, haingewezekana kwa sabahu ya kodi ya ushuru kuwa juu iliyowekwa kwa sukari yote isipokuwa ile iliyozalishwa kwenye makoloni ya Uingereza ya West-Indies… Pili, Wafaransa, Wadachi na Wahispania walikataa kukomesha biashara ya utumwa.

Ilikuwa rahisi kuona malengo halisi ya kisiasa yaliyoko nyuma ya pazia la ubinadamu la Pitt. Gaston-Martin, Mfaransa maarufu mwenye taaluma ya historia ya biashara ya watumwa na makoloni ya Caribbean, anamlaumu Pitt kwa kutaka kuwapa uhuru watumwa kwa kutumia propaganda, hapan shaka kwa kutumia jina la ubinadamu. lakini pia kuharibu biashara ya Ufaransa. Na anahitimisha kwamba kwenye propaganda hii ya kiihsani na kiubinadamu palikuwepo na malengo ya kiuchumi.

Halafu pakatokea tukio moja kubwa. Wakulima wa Kifaransa huko Saint Domingo, mwaka 1791, wakihofia matokeo ya Mapinduzi ya Ufaransa, waliwapa Uingereza visiwa hivyo; muda si mrefu Windward Island ilifuata mtindo huo; Pitt alikubali kuvichukua visiwa hivyo mwaka wa 1793. Vikosi vya jeshi la Ufaransa vilipelekwa kimoja baada ya kingine mara kadhaa lakini havikufanikiwa kuvirejesha visiwa hivyo kwenye miliki ya Ufaransa.

Dk. William anafafanua: “Hii ni zaidi ya manufaa ya kiso- mi. Pitt hangeweza kumiliki Saint Domingo na kukomesha biashara ya watumwa wakati huo huo. Bila ya kawaida yake ya kuingiza watumwa 40.000 kwa mwaka, Saint Domingo ingekwisha filisika. Kitendo cha Pitt kukubalia kuchukua kisiwa hicho kimantiki kilikuwa na maana kwamba hangeendelea na mpango wake wa kukomesha biashara ya watumwa. Kwa wazi hakusema hivyo. Pitt alikwisha fika mbali sana katika kuwaahidi raia wa Uingereza.

Aliendelea kuzungumza kuhusu kukomesha biashara ya watumwa hata hapo alipokuwa anaitumainisha biashara ya watumwa katika hali halisi… Sababu za Pitt zilikuwa za kisiasa na kwa kiwango kidogo kibinafsi. Pitt alipendelea biashara ya sukari: Ama ilikuwa lazima aivuruge Saint Domingo kwa kuingiza sukari nyingi sana Ulaya na ya bei rahisi kutoka India au kwa kukomesha biashara ya watumwa; au aichukue Saint Domingo iwe yake binafsi.”6

Hali hii ingeipatia Uingereza ukiritimba wa sukari, rangi ya buluu, pamba na kahawa… Lakini kama Pitt angeikamata Saint Domingo, biashara ya watumwa lazima ingeendelea. Wakati Saint Domingo ilipochukuliwa na Ufaransa, biashara ya watumwa ilichukua sura mpya ya kuwa kama vile suala la ubinadamu tu…

Lakini kuharibika kwa Saint Domingo haikuwa na maana ya ukombozi kwa makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West- Indies. Walijitokeza maadui wawili wapya kwenye uwanja. Cuba ilisonga mbele na kuziba pengo lililoachwa kwenye soko la dunia baada ya kutoweka Saint Domingo.”7

Wakati ule ule, chini ya mamlaka ya Marekani, sukari ya Cuba na wazalishaji wengine waliokuwa na msimamo wa kati, bado ilipata soko Ulaya, na sukari ya ziada kutoka British West Indian ililundikana Uingereza. Kufilisika kwa wakulima ilikuwa hali ya kawaida. Kati ya 1799 hadi 1807, mashamba 65 ya Jamaica yaliachwa, 32 yaliuzwa kufuta madeni, na malalamiko 1807 ya madai yalikuwa yana ngoja uamuzi dhidi ya 115. Mada zilizokuwa zinazungumziwa hapo kisiwani ni madeni, maradhi na vifo.
Kamati ya bunge iliyoundwa mwaka 1807 iligundua kwamba mkulima wa British Indian alikuwa anazalisha kwa hasara. Mwaka wa1800 faida ya mkulima ilikuwa asilimia 2.5 (2 ½ %), mwaka wa 1807 hakuna faida. Mwaka wa 1787 mkulima alipata 19/6d. Faida kwa kila ratili mia na kumi na mbili; mwaka 1799, 10/9d; mwaka wa 1803, 18/6d; 1805, 12/-; katika kwaka 1809, hasara. Kamati ilidhani sababu kubwa ilikuwa hali mbaya ya soko la nje. Mwaka 1809 sukari ya ziada ya Uingereza ilikuwa tani 6,000. Uzalishaji ukasitishwa. Kuwekea mipaka uzalishaji, biashara ya watumwa lazima ikomeshwe.” 8

Kwa hiyo, kwa maneno ya Dk. Williams, “Kukomeshwa kwa biashara ya watumwa moja kwa moja ilisababishwa na kuvurugika kwa uchumi huo.”9

 • 1. Williams, Dr. Eric. Capitalism and Slavery uk. 65.
  ** Pandora box ni maneno ya methali, maana yake ni mpango ambao ukihamasishwa
  huzalisha matatizo mengi yasiyodhibitika.
 • 2. Ibid, uk. 122.
 • 3. Ibid, uk. 123
 • 4. Ibid, uk. 138-9.
 • 5. Ibid, uk. 146.
 • 6. Ibid uk. 146 -7, Ibid uk. 1487- 8.
 • 7. Ibid, uk. 148-9.
 • 8. Ibid, uk 149.
 • 9. Ibid, uk 150.

Unafiki Wa Wakomeshaji Wa Biashara Ya Watumwa

Kama mtu yeyote anataka kudhani kwamba sababu ya kukomeshwa kwa utumwa ni maendeleo ya unyofu wa maadili, basi anashauriwa kuangalia msimamo wa watu waliokuwa wanashughulikia suala la kukomesha biashara ya watumwa katika mfumo wa malengo yao ya kiuchumi. Hivyo tunaona kwamba wale wale washikiliaji wa maslahi ya West Indies ambao kabla ya tatizo lililotajwa, walikuwa ni waungaji mkono motomoto wa biashara ya watumwa sasa waligeuka kuwa “waungwana wenye huruma na shauku ya kuukomesha utumwa”. Dk. Williams anasema, kwa kejeli kabisa, ilikuwa ni wamiliki wa watumwa wa siku za nyuma wa West Indies ambao sasa walishikilia tochi ya kuwahurumia binadamu.

Wale ambao, katika mwaka wa 1807, kwa majonzi walikuwa wanatabiri kwamba kukomesha biashara ya watumwa ya Uingereza “ingesababisha kupungua kwa biashara, kupungua kwa ushuru wa kodi, na kupungua kwa safari za baharini; na hatimaye kudhoofisha na kuondoa kabisa msingi mkuu wa ustawi wa Uingereza, walikuwa, baada ya 1807, watu wale wale waliokataa ‘mpango wa mtu’ kuwaiba watu masikini na ambao hawana jinsi ya kujitetea.”

Manufaa ya West India katika mwaka wa 1830 yaliweka azimio la “kuchukua hatua madhubuti zaidi kusitisha biashara ya watumwa ya nje; kushughulikia suala la ukan- damizaji uliokwisha fanywa ambao kwamba ustawi wa makoloni ya Uingereza ya West Indes… hatimaye yali- utegemea. Wajumbe kutoka Jamaica, walopelekwa Uingereza mwaka 1823, walitangaza kwamba makoloni yangepatanishwa kwa urahisi kuhusu kukomeshwa kwa biashara ya kishenzi na ya kinyama, ambayo ustaarabu ulioendelea wa wakati huu hukuiruhusu tena kuwepo… Kundi kubwa la kukomesha biashara ya watumwa lilijidhihirisha nchini Jamaica katika mwaka 1849.

Auj claplo, vyama na madhehebu viliunganishwa kuhusu suala la Africa kutendewa haki. Walilaani biashara ya watumwa na utumwa kama ni “kinyume cha ubinadamu iliyozalisha maovu mabaya sana Afrika - kuwadhalilisha wote waliohusika katika biashara hiyo, na kudhuru maadili na utashi wa kiroho wa watumwa, na kusihi kwamba neno la kuchuk- iza ‘mtumwa’ liondolewe kwenye msamiati duniani pote. UTUMWA LAZIMA UANGUKE, na utakapoanguka, JAMAICA ITASTAWI! Walitamka kwa ukali, iliingia kwenye vita nyingi bila ya sababu zilizo halali.” 1

Na palikuwepo na manufaa gani ya vifungu vya maneno vilivyo vikali na ambavyo vinaweza kuamuliwa kutokana na ukweli kwamba ubepari wa Uingereza, hata baada ya kuvuruga utumwa wa West Indian, “Uliendelea kustawi kutokana na utumwa uliokuwa unaendelea huko Brazil, Cuba na utumwa wa Amerika ya Kaskazini na Kusini.” Kwa hiyo, kwa maneno ya Profesa Brogan, “tunapata mafumbo ya wajibu uliogeuzwa. Ilikuwa sawa kabisa kwa watetezi wa hoja ya kukomeshwa utumwa, kulaani matumizi ya sukari iliyo zalishwa na watumwa kutoka West Indes, lakini hakuna aliyependekeza kusimamisha matumizi ya pamba iliyozalishwa kutoka Marekani (U.S.A.). Hakika, hakuna mtu aliyependekeza kwa dhati kuacha kutumia sukari iliyozalishwa na watumwa kutoka Brazil au Cuba. Fedha sio hisia, hisia za uovu za uzuri, husokota na kupotosha njama.”
Dk. Williams anaandika, “Baada ya India, Brazil na Cuba, bila ya dhana yoyote. Je, muungwana yeyote angeweza kuhalalisha pendekezo lolote lililopangwa kuimarisha minyororo ya utumwa ambayo bado imewafunga Watu Weusi wa Brazil na Cuba. Kwa usahihi hiyo ndio ilikuwa maana ya biashara huru ya sukari.

Kwani baada ya mwaka 1807 British West Indians walikataliwa na kunyimwa kuendesha biashara ya watumwa, na baada ya 1833 wakanyimwa nguvu kazi ya watumwa. Kama watetezi wa kukomesha utumwa walipendekeza sukari ya kutoka India, kwa makosa, kwa misingi ya ubinadamu kwamba ni sukari iliyolimwa na watumwa huru, ilikuwa ni wajibu wao kwa kanuni zao na dini yao kususia sukari iliyolimwa na watu wa Brazil na Cuba. Katika kuanguka kufanya hivi isiamuliwe kwamba hawakuwa sahihi, lakini si jambo la kukanusha kwamba kushindwa kwao kutumia njia hiyo ilivuruga hoja ya ubinadamu. Baada ya 1833, watetezi wa kukomesha utumwa, waliendelea kumpinga mkulima wa West Indian ambaye sasa aliajiri wafanya kazi huru. Ambapo, kabla ya hapo 1833, waliwagomea wamiliki wa watumwa wa Uingereza, baada ya 1833 waliunga mkono sababu ya wamiliki wa watumwa wa Brazil.”2

Kuondolewa kwa Watu Weusi kishenzi kutoka Afrika ni shughuli iliyoendelea kwa karibu miaka 25 tangu 1833, ambao walipelekwa kwenye mashamba ya miwa ya Brazil na Cuba. Uchumi wa Brazil na Cuba ulitegemea biashara ya watumwa. Msisitizo peke yake ulidai kwamba watetezi wa kukomesha utumwa wa Uingereza walipinga biashara hii. Lakini jambo hilo lingerudisha nyuma maendeleo ya Brazil na Cuba na matokeo yake kuzuia biashara ya Uingereza. Haja ya kupata sukari ya gharama ya chini baada ya 1833 ilishinda chuki yote ya utumwa. Tishio ambalo hapo mwan- zo lilichochewa na fikira ya mswaga watumwa wa Uingereza wa West Indies mwenye mjeledi; mswaga watumwa wa Cuba mwenye mjeledi, panga, jambia,. kisu na bastola na kufuatwa na mbwa mwitu, haikuamsha hata maoni ya watetezi wa kuzuia biashara ya watumwa.”3

Hivyo ni wazi kwamba sababu halisi yaubinadamu na uungwana wa Uingereza wala haikuwa usawa wa kiunyofu au mwamko wa kimaadili bali ilikuwa ni kwa sababu ya shinikizo la kiuchumi na kuwaumiza washindani wao wa biashara. Kwa maneno ya Profesa Brogan, somo la Ubepari na Utumwa linavunja moyo na kufadhaisha kama si jipya. “Pale ilipo hazina yako ndipo moyo wako unapo lala.’

 • 1. Ibid, uk 175-6.
 • 2. Ibid, uk 188.
 • 3. Ibid, uk. 192.

Ilikuwa Ni Vita Ya Wenyewe Kwa Wenyewe Ya Marekani

Je, Ni Ya Kuwakomboa Watumwa?

Nadhani itakuwa kwa manufaa ya wasomaji kutizama kwa umakini hadithi isemayo kwamba vita ya Marekani ya wenyewe kwa wenyewe ilitokea kwa lengo la kuwakomboa watumwa. Ni ngano ambayo iliyobuniwa na haina uhusiano wowote na hali halisi ya ukweli. Nina nukuu hapa kutoka kwenye sura ya 22 ya “Lincoln, the Unkown” kilichoandikwa na mwandishi wake maarufu Dale Carnegie.1 Anaanza na maneno haya: - “Muulize raia wa kawaida wa Kimarekani leo kwa nini Waamerika walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe, atakacho kuambia ni kwamba, ‘Kuwakomboa watumwa.’ “Ni kweli hivyo?”

“Hebu tuangalie. Hapa ni sentenso ambayo imechukuliwa kutoka kwenye hotuba ya kwanza ya Lincoln ya kuzindua urais wake. ‘Sikusudii kuingilia kati, taasisi ya utumwa, moja kwa moja au kuzunguuka kwenye majimbo ambayo utumwa bado upo. Nina amini sina haki ya kisheria kufanya hivyo, na sipendelei kufanya hivyo.”

Ukweli ni kwamba mzinga ulikuwa unanguruma na majeruhi wanatoa sauti ya kulemewa kwa takribani miezi kumi na nane kabla Lincoln hajatoa tangazo la “Ukombozi wa watumwa.”
Wakati wote huo watu wenye msimamo Mkali na Watetezi wa kukomesha utumwa walimsihi achukue hatua haraka, walimshambulia kupitia kwenye magazeti na kumshutumu kwenye majukwaa ya mikutano.

“Wakati mmoja ujumbe wa mawaziri wa Chicago ulikwenda Ikulu ya Marekani na kile walichokitangaza kwamba ilikuwa ni amri ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu Mweza wa Yote kuwaachia watumwa kuwa huru haraka sana. Lincoln aliwaambia kwamba alidhani kwamba kama Mweza wa Yote alikuwa na ushauri wowote wa kutoa, Angekuja moja kwa moja makao makuu na ushauri huo, badala ya kuwasilisha kwa mzunguuko wa kupitia Chicago.”

Zaidi ya hayo, Dale Carnegic anaendelea kunukuu kutoka kwenye jibu la Lincoln alipojibu makala ya Greedy, ‘The Prayer of Twenty million.’(‘Sala ya milioni ishirini).

“Kusudio langu kubwa katika mapambano haya ni kuokoa Muungano, na wala si kuokoa au kukomesha utumwa. Kama ningeokoa Muungano bila kumpa uhuru mtumwa hata mmoja, ningefanya hivyo; na kama ningeokoa Muungano kwa kuwapa uhuru wa watumwa wote ningefanya hivyo, na kama ningeuokoa Mungano kwa kuwapa uhuru baadhi yao na kuwaacha wengine, pia ningefanya hivyo.

Ninachofanya kuhusu watumwa na machotara, ninafanya hivyo kwa sababu ninaamini inasaidia kuokoa Muungano, na kile ninachovumilia, ninavumilia kwa sababu siamini kama ingesaidia kuokoa Muungano. Sitafanya yote wakati wowote nitakapoamini kile ninachokifanya kitadhu- ru lengo; na nitazidisha juhudi nitakapoamini kufanya hivyo itasaidia lengo.”

Akifafanua jibu hilo Dale Carngie anaandika: “Majimbo manne yamebakia na watumwa pamoja na Kaskazini, na Lincoln alitambua kwamba kama angetoa tangazo la “ukombozi wa watumwa” mapema mno katika mzozo huu, angewafukuzia kwenye Shirikisho, kuimarisha kusini, na pengine kuvunja Muungano daima milele. Palikuwepo na methali wakati huo ambayo Lincholn angependa kuwa na Mungu Mweza wa Yote upande wake, lakini lazima aipate Kentucky.

“Hivyo alisubiri wakati mzuri, na kufanya mambo kwa tahadhari”

“Lincoln mwenyewe alioa kwenye familia yenye kumiliki watumwa, ya Jimbo la mpakani. Sehemu fulani ya fedha ambayo mke wake Lincoln alipokea ilitoka kwenye urithi wa shamba la baba yake ambayo ilitokana na mauzo ya watumwa. Na rafiki mmoja tu wa karibu sana na wa kweli ambaye Lincoln alikuwa naye, alikuwa Joshua Speed ambaye alitoka kwenya familia yenye watumwa. Lincoln aliwahurumia watu wa Kusini kwa maoni yao. Kwa upande mwingine, alikuwa na desturi ya kumshehimu mwanasheria Mkuu kuhusu Katiba na sheria na rasilimali. Hakutaka kusababisha shida kwa mtu yeyote. (ila kwa watumwa)

“Lincoln aliamini kwamba majimbo ya kaskazini yalistahili kulaumiwa sana kwa kuendelea kuwepo kwa utumwa “Marekani (U.S.A)” kama ilivyo huko kwenye majimbo ya Kusini; na kwamba kuliondoa tatizo hilo, sehemu zote lazima zivumilie mzigo sawa kwa sawa. Kwa hiyo hatimaye alitengeneza mpango ambao ulikuwa karibu sana na moyo wake. Kwa mujibu wa mpango huo, wamiliki wa watumwa waliokuwa kwenye mipaka ya majimbo yenye uaminifu walipewa dola mia nne kwa kila Mtu Mweusi. Watumwa walitakiwa kuachiwa huru polepole, polepole sana.

Mlolongo wa mambo haya haukutakiwa kumalizika kikamilifu hadi Januari 1, 1900. Lincoln aliwaita wawakilishi kutoka kwenye Majimbo ya mipaka wamuone huko Ikulu White House, akawasihi wakubali pendekezo lake.

“Lincoln alihoji na kusema, mabadiliko yaliyomo kwenye pendekezo lake, yanakusudiwa kuja polepole kama umande unavyo dondoka kutoka mbinguni, bila kupokonya au kuvunja matarajio ya watu. Kwa nini msikubali pendekezo hili? Mambo mengi sana mazuri bado hayajafanyika kwa jitihada moja, katika wakati wote uliopita, kama ilivyo katika upaji wa Mungu sasa hivi ni upendeleo wenu wa juu kutekeleza. Muda mwingi ujao na upana wake usije ukalalamika kwamba ulipuuzia jambo hili.”

Msomaji angekumbuka kwamba mpango huu wa kuwapa watumwa uhuru “kwamba ulikuwa karibu mno na moyo wake Lincoln” ulikuwa sawa na mpango ambao tayari ulik- wisha wekwa na kutekelezwa miaka 1300 iliyopita katika Uislam na ambao ulitoa matokeo ya kushangaza katika ulimwengu wa Kiisilamu. Kama mpango huo ungekubaliwa na ndugu zake Lincoln, hapange kuwepo na chuki kubwa baina ya mataifa, migongano ya ndani, mageuzi ya kijamii na udhaifu wa hisia ambao bado unaendelea kuwepo nchini Marekani (U.S.A.) karne moja baada ya kile kilichoitwa Ukombozi wa watu weusi (Emancipation of Negroes).

Bahati mbaya, wawakilishi wa Majimbo hayo yaliyokuwa yanapakana walikataa mpango huo. Carnegie anasema, “Lincoln mara moja alikasirika sana. Lazima niiokoe serikali hii, kama inawezekana, alisema na inaweza ikaeleweka, kwa mara zote, kwamba sitakubali kuacha mchezo huu, na kuacha kadi yoyote ile ipatikanayo iwe haijachezwa….Ninaamini kwamba kuwapa uhuru watumwa na kuwapa silaha watu weusi sasa imekuwa jambo la msingi na muhimu kivita. Nimesukumwa kwenye uchaguzi ama kutekeleza hilo au kuuwachia) Muungano (usambaratike).

“Ilibidi Lincoln ashughulike haraka, kwani Ufaransa na Uingereza walibakia kidogo watambue Shirikisho. Kwanini? Sababu zilikuwa rahisi. Tuchukue mfano wa Ufaransa kwanza.”

Napoleon wa III alikuwa mfalme wa Ufaransa. Alikuwa na shauku kubwa ya kutaka utukufu wa mamlaka ya utawala, kama alivyokuwa ami yake mtukufu, Napoleon Bonaparte, alivyo fanya. Kwa hiyo, alipoona majimbo yanapigana, na alitambua kwamba walikuwa na shughuli nyingi mno kuweza kufikiria kuhusu utekelezaji wa sheria ya “Momoe Doctrine,” aliamuru jeshi kwenda Mexico, huko likaua wazalendo elfu kadhaa, likashinda nchi, ikaitwa Mexico iliyo chini ya himaya ya Ufaransa, na likamweka Archduke Maximilian kukalia kiti cha enzi.

“Napoleon aliamini na si bila sababu, kwamba kama kundi linalotaka shirikisho lingeshinda, lingependelea ufalme wake mpya; lakini kama kundi linalotaka shirikisho lingeshinda, United States ingechukua hatua za haraka za kuifukuza Ufaransa huko Mexico. Kwa hiyo, ulikuwa ni upendeleo wake Napoleon, kwamba Kusini ifaulu kujitenga, na alitaka kuisaidia kutekeleza kujitenga huko kwa kadiri ya uwezo wake.

Mwanzoni mwa vita, jeshi la majini la Kaskazini lilifunga bandari zote za Kusini, bandari 189 zikawa chini ya ulinzi wao na walifanya doria kwenye eneo la maili 9,614 za uwanda wa pwani, njia nyembamba za maji zinazounganisha bahari na zinazounganisha bahari na maziwa, vinamasi na mito. Hiki kilikuwa kizuizi kikubwa mno ambacho ulimwengu haujapata kuona. Kundi lililotaka Muungano lilikuwa lina haha.

Halikuweza kuuza pamba yake, wala kuweza kununua bunduki, risasi, viatu, madawa au chakula. Watu hawa walianza kuchemsha karanga na mbegu za pamba kuwa mbadala wa kahawa, na walianza kuchemsha majani ya miti ya matunda mithili ya mibuni na kuchuja maji yake na kuwa mbadala chai. Magazeti yalianza kuchapishwa kuwekwa kwenye matangazo. Nyumba zenye sakafu za udongo na zenye kufuka moshi, zililoweshwa dabwa dabwa kwa mafuta ya wanyama, zikachimbuliwa na kuchemshwa ili kupata chumvi.

Kengele za makanisa ziliyeyushwa na kutiwa katika mizinga. Reli za magari madogo mitaani katika mji wa Richmond zilikatwa katwa na kufanywa silaha katika mashua za kivita zenye bunduki.

Watu wa Muungano hawakuweza kuzifanyia matengenezo reli zao au kununua vifaa vipya, kwa hiyo usafiri ulibakia kidogo sana; nafaka ambayo ilinunuliwa kwa dola mbili, pishi tisa huko Geogia, ilinunuliwa kwa dola kumi na tano Richmond. Watu waishio Virgini walikuwa wanashinda na njaa.

Ilibidi utaratibu fulani ufanywe haraka sana. Kwa hiyo, Kusini walikubali kumpa Napoleon wa III dola milioni 12 kama angeutambua Muungano na atumie meli za Kifaransa kuondoa kizuizi. Kwa upande mwingine, waliahidi kumzidishia nguvu kwa amri ambayo ingeanzisha moshi kwenye kila kiwanda huko Ufaransa usiku na mchana.

Kwa hiyo Napoleon akazisihi Urusi na Uingereza kuungana naye katika kuutambua Muungano. Utawala wa makabaila uliokuwa madarakani, wahusika wake waliweka sawa miwani zao, wakanywa toti kadhaa za Scotch Whisky, na wakasikiliza kwa hamu kubwa mazungumzo ya awali ya Napoleon. Marekani (U.S.A.) ilianza kutajirika sana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwaridhisha, Walitaka kuona taifa linagawanyika, Muungano unavunjika. Kwa upande mwingine, walitaka pamba ya Kusini. Viwanda kadhaa vya Uingereza vilifungwa, na watu milioni moja hawakuwa tu hawana kazi, bali pia kuwa fukara na kushuka chini kuwa omba omba halisi.

Watoto walikuwa wanalia njaa, mamia ya watu walikuwa wanakufa kwa sababu ya njaa. Michango ya raia kwa ajili ya kununua chakula cha wafanya kazi wa Uingereza ilichukuliwa na kupelekwa kwenye vijiji vya ndani kabisa ya dunia hata India ilioko mbali sana na China ambayo ilibanwa na umasikini. Palikuwepo na njia moja, na njia moja tu, kwamba Uingereza ingeweza kupata pamba na hiyo ilimaanisha waungane na Napoleon III katika kuutambua Muungano na kuondoa kizuizi.

“Kama hilo lingefanyika, nini kingetokea Marekani? Kusini wangepata bunduki, baruti, mkopo, chakula vifaa vya njia ya reli, na msaada mkubwa sana wa hali na mali.

“Na Kaskazini wangepata nini? Wangepata maadui wawili wapya na wenye nguvu. Hali hiyo kuwa mbaya kiasi hicho sasa, hapangekuwepo na matumaini.

“Hakuna aliyejua hilo vizuri zaidi kumzidi Abraham Lincoln. “Ni kama vile tumecheza kadi yetu ya mwisho’, aliungama hivyo katika mwaka 1892. Ama lazima tubadili mbinu zetu au tukubali kushindwa mchezo.’

Kama ilivyoona Uingereza, makoloni yote yalikwisha jitoa kutoka kwenye utawala wake tangu mwanzo. Sasa makoloni ya Kusini nayo yamekwishajitoa kutoka makoloni ya Kaskazini; na Kaskazini ilikuwa inapigana kuilazimisha na kuitiisha Kusini. Je, pangekuwa na tofauti gani kwa mtu wa kawaida huko London au mwana mfalme huko Paris kama Tenessee na Texas zingetawaliwa kutoka Washington au Richmond? Hakuna. Kwao vita haikuwa na maana yoyote na yenye kuleta hatari bila madhumuni ya maana.

‘Nilikuwa sijapata kuona vita imepamba moto kama hiyo katika uhai wangu’, aliandika Carlyle, ‘iliyokuwa inaonekana zaidi kama ya kipumbavu.

Lincoln aliona kwamba msimamo wa Ulaya kuhusu vita hiyo lazima ubadilike, na alijua jinsi ya kufanya. Watu milioni moja huko Ulaya walikwisha soma “Uncle Toms Cabin” walikisoma kisa hicho na wakalia na wakajifunza kuchukia michomo ya moyo na udhalimu wa utumwa. Kwa hiyo Abraham Lincoln alitambua kwamba kama angetoa tangazo lake la “ukombozi wa watumwa”, watu wa Ulaya wangeiona vita kwa namna tofauti. Haingekuwa tena ugomvi wa kumwaga damu kwa sababu ya kudumisha Muungano ambao haukuwa na maana yoyote kwao. Badala yake, ingetukuzwa kuwa vita takatifu ya kutokomeza utumwa. Serikali za Ulaya hazingeitambua Kusini. Maoni ya watu hayangestahamili kuwasaidia watu ambao wanapi- gana kwa lengo la kuendeleza utumwa wa kibinadamu.

Hatimaye, kwa hiyo, mnamo Julai, 1862, Lincoln akiwa amedhamiria kutoa tangazo lake, lakini McClellan na Papa mnamo siku chache za nyuma waliliongoza jeshi la Kusini kwenye fedheha ya kushindwa mara kadhaa. Seward alimwambia Rais kwamba muda huo haukuwa mwafaka, hivyo angelazimika kungoja na kutoa tangazo kwenye kilele cha ushindi wao.

“Ushauri huo ulionekana wa hekima. Kwa hiyo Lincoln akangojea na miezi miwili baadaye ushindi ukapatikana.”

Na kwa hiyo, kuendeleza Vita ya Muungano, tangazo la “Ukombozi wa Watumwa” lilichapishwa mnamo Septemba 1862, ambalo lilitakiwa lianze kutekelezwa tarehe Moja, Januari 1863.

Ninampa Abraham Lincoln heshima ya juu sana na amekuwa mmoja wapo wa mashujaa ninao wapenda tangu nilipokuwa mdogo. Lakini heshima hiyo msingi wake ni kwenye ukweli na hali halisi, si kwenye mambo ya kubuniwa. Lincoln alikuwa na ubinadamuna, na yeye, kutoka ndani ya moyo wake alikuwa dhidi ya utumwa. Lakini haina maana kwamba tumtukuze kwa propaganda za uwongo. Uhalisi wa jambo hili ni kwamba hakupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa lengo la kuwapa watumwa uhuru, kwa usahihi zaidi aliwapa watumwa uhuru kwa lengo la kushinda vita na kuokoa Muungano.

 • 1. Carnegie, Dale, Lincoln: The Unknwown (Surrey, U.K.: The World Work Ltd. 1948) Sura ya 22

Utumwa Wa Kimajimbo

Hadi sasa tumechambua aina moja tu ya utumwa, yaani utumwa wa utumishi wa nyumbani kwa mtu. Lakini ilitajwa kwenye sura ya kwanza kwamba utumwa ni wa aina mbili, aina ya pili ni Utumwa wa Kimajimbo au taifa moja kutumikisha taifa lingine. Licha ya kwamba utumwa wa nyumbani sasa hivi unajulikana kwamba ulikomeshwa, utumwa wa kitaifa bado upo unaendelea. Moyo ukiwa umejaa huzuni mtu anaona uharibifu wa maisha ya binadamu kwa mpango maalum na hadhi ya binadamu inaendelezwa na ustaarabu wa Kikristo karibu katika kila nchi hapa duniani.

Wahindi Wekundu walikuwa wakazi wa mwanzo wa Nchi mpya. Wapo wapi sasa? Walitolewa polepole kutoka kwenye ardhi yao na wamelazimishwa kuishi kwenye ardhi yenye rutuba hafifu ambayo haiwezi kuzalisha mazao, vishamba vilivyoko ndani ya Marekani (U.S.A). Waaborigine wa Australia walipitishwa kwenye uonevu wa aina hiyo hiyo. Wahindi Wekundu na Waaborigine walikuwa wanawindwa kama wanyama pori: yaani, nyati na kadhalika na sasa hivi idadi yao inakaribia kufutika kabisa katika uso wa dunia hii. Dk. Eric Williams ananukuu maelezo ya Mkuu wa wahindi wekundu, Hatuey, ambaye alipewa adhabu ya kifo kwa kuwawekea pingamizi wavamizi, alikuwa imara katika kukataa imani ya Kikristo kama njia ya kwenda kwenye wokovu alipotambua kwamba wauaji wake, nao pia walikuwa na matumaini ya kwenda Peponi. 1

Lakuhuzunisha zaidi ni hatima ya Waafrika wa Afrika ya Kusini. Wareno wakiwa na tangazo la Papa Walazimisheni makafiri kuwa watumwa” wanang’ang’ania kuiweka Angola na Msumbiji chini ya nira ya Utumwa wa kitaifa.

Ni jambo la kushangaza kweli kuona Papa Paulo wa VI mara nyingi hutoa matamshi kuhusu matatizo ya kisiasa ya dunia; akini kamwe hata siku moja hajaona umuhimu wa kuishauri Ureno kuzungumza na “raia” wake hapa Afrika na kwingineko. Badala yake Mapapa wamekuwa wakien- deleza uhusiano maalum na Ureno na Hispania, nchi hizi mbili za Kanisa Katoliki ambazo zinakataa kuyaacha huru makoloni yake ya Afrika. Katika mwezi wa July, 1970, Papa Paulo VI aliwapokea viongozi fulani wa wapigania uhuru wa makoloni ya Ureno katika Afrika. Mkutano huu uli- ikasirisha sana Ureno, ambayo ilitoa tamko la pingamizi; Vatican katika hali ya wasi wasi ilitoa maelezo. Akieleza kuhusu jambo hili, barua ifuatayo yenye kichwa cha habari “Muhtasari wa Papa ni Faraja: ilichapishwa katika gazeti la “Standard Dar es Salaam (Tanzania) na muunini mweusi wa Roman Katoliki, aliposema: “Kipengee cha habari; ‘Muhtasari wa Papa waifariji Ureno’ (Standard, July 11) yahusika. Ninanukuu sentenso muhimu:

Muhtasari wa Vatican … ulisema kwamba Papa alipowapokea (yaani viongozi wa vyama vya ukombozi katika Afrika walioko chini ya utawala wa Kireno) wakiwa kama Wakatoliki na Wakristo, bila ya kuangalia shughuli zao za kisiasa. Aliwakumbusha kuhusu mafundisho ya Kanisa kwamba njia za amani siku zote zitumike hata katika kutafuta kile mtu akionacho kuwa ni haki yake mtu.

“Habari za mapema zaidi kwamba Baba Mtakatifu amepokea viongozi hao waliosemwa, zimenisumbua na kunitia wasi wasi sana. Sasa ufafanuzi huu umefanya wasi wasi wangu kutulia. Ngoja nieleze kwa nini.

Lilikuwa Kanisa la Roman Katoliki ambalo ndilo lililoleta ukoloni wa Kimagharibi kwa kuigawa ardhi yote na nchi zote mpya zilizogunduliwa hivi karibuni katika mafungu mawili; kuwapa Wahispania nusu ya Magharibi (kama nchi za Amerika) na kuwapa Wareno nusu ya Mashariki (kama nchi ya Afrika na India).

Makoloni ya Ureno katika Afrika yameundwa imara sana juu ya lile Agizo la Papa. Niliposoma mapema kwamba Papa Paulo VI aliwapokea viongozi wa vyama vya Ukombozi, nilishangaa iliwezekana vipi. Kwa mujibu wa imani yetu ya kutokukosea kwa Papa, Paulo VI analazimika kuchukua na kuhalalisha kila kitu kilichoamriwa na kuagizwa na wale watakatifu waliokwisha mtangulia. Kwa hiyo, kwa mujibu wa kufikiria kwangu asingewatia moyo viongozi hao.

“Sasa ufafanuzi wake umenifariji mimi sana kiroho. Sasa naweza kulala kwa amani na kuwa ujuzi wa uhakika kwamba Kanisa halikujilaumu lenyewe kwa kuonyesha kwamba Mapapa walikosea katika kuuweka na kuunga mkono “mwanga” wa bara hili jeusi chini ya Ubepari wa Kireno.

“Pia ushauri wake kwa hawa waitwao ‘Waathirika kutokana na Ukoloni’ kubakia katika amani (yaani kuvinyang’anya silaha vikundi vya wapigania uhuru) ni sawa na mvinyo wa zamani ndani ya chupa mpya. Inanikumbusha maombi ya mapadre wa Kanisa la Romani Katoliki wakati wa kuendeshwa meli zenye watumwa kutoka bandari za Ureno kwenda katika visiwa vya West Indes.
Waliomba kwa Mola Mwenye Uwezo na nguvu zote kuhakikisha usalama wa meli hizo na siku zote waliwaamuru watumwa weusi wawe na tabia za kiungwana na utii.

Kwa hakika, hawakufikiria kwamba ni lazima kuwashauri mabwana (wamiliki ) wa watumwa kuwafikiria nao kuwa ni wanaadamu. Nina furaha kwamba Kanisa langu halijabadilika katika kipindi chote hiki cha karne ndefu.”

Sera ya Afrika ya Kusuni ya Ubaguzi wa rangi inalaumiwa ulimwenguni pote na Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) na kila mahali. Lakini Makanisa siku zote yalifuata mstari huo huo. Ilikuwa baada tu ya “mabadiliko ya Upepo”

Katika Afrika na kutokea kwa haraka uhuru wa nchi za Kiafrika kwamba makanisa yalitambua haja ya kuupinga mfumo ulio mbaya kabisa ambao hukatilia wenyeji wa asili (wazawa) wa nchi husika haki ya kufanya kazi, kutembea, kukaa, kupanda vipando vya kusafiria, kuchuma au kulala katika ardhi yao wenyewe. Na hata pia wakati Makanisa mengine yote, yalipolazimishwa na haja muhimu za Kisiasa, walionyesha upinzani wao kwa aina hii ya utumwa, Kanisa la Kidini la Mageuzi-‘The Dutch Reforned Church’ bado linaunga mkono mfumo huu wa kinyama.

Rhodesia inafuata nyayo za Afrika ya Kusini. Msemo ulio- zoeleka na maarufu wa kuchekesha wa Kiafrika katika sehe- mu hizi za dunia unaelezea kuhusu Mwafrika mmoja akiumwambia (rafiki yake) Mzungu: “Ulipokuja ulikuwa na Biblia na sisi tulikuwa na ardhi. Sasa hivi sisi tunayo Biblia na wewe una ardhi, (unaimiliki).

Mbali na utumikishaji huu wa kijeuri na dhahiri, bado upo udanganyifu mwingine ambao biashara ya utumwa wa Kitaifa hudhihirisha uso wake. Ukiwa kama kinyonga, hubadilisha rangi yake kwa kutegemea mazingira. Ukoloni wa dhahiri sasa umebadilika na kuwa ukoloni mamboleo; lakini inafikia pale pale kwenye utumikishaji na watu na yale mataifa makubwa yenye nguvu kwa kutumia mbinu zenye utata zaidi au zisizokuwa na utata sana.

Tumekwisha ona nini kilitokea kuhusu league of Nations (Shirikisho la Mataifa). Imeondolewa na badala yake ni UNO, lakini wakati mataifa dhaifu yanapolia na kuomba kuwepo na haki, usawa na uadilifu, shinikizo la kidiplomasia hutumika na madai yao ya haki kuhusu haki zao za msingi huondolewa na kuwekwa kando au huahirishwa. Kuna usaliti wa kisiasa, na rangi ya ngozi bado ndio kiumacho. Kwa kweli nchi zitawalazo au zile ambazo zina nguvu na zimejizatiti vyema kwa vyombo na uwezo wa kuleta maangamizi makubwa na uharibifu, bado zinashikilia utawala wao
Aina hii ya utumwa inafanywa leo hii siyo tu na mataifa bepari ya Kikristo bali na Wakomonist pia, na itaendelea hivi kwa kipindi kirefu maadam jamii ya kibinadamu inabakia katika kugawanyika katika makundi ya walio na mguvu na walio dhaifu au mpaka kuwepo na kutambuliwa kwa Mwenye Kudra na Mwenye Nguvu zote, Mwenyezi Mungu (atambuliwe), na Himaya (Enzi) yake katika Ulimwengu wote iwe imeaminiwa kabisa na kupokewa.

Hata sasa wakati Karne ya ishirini inaelekea kufika mwisho wake na Waamerika wakiwa wanajifaharisha wenyewe katika yale waliyoyapata, suala la “Watu Weusi-Manegro” liko mbele kabisa na bado halijapatiwa ufumbuzi. Kwa kukata tama, O.A Sherrad anasema: Utumwa umekuwepo kutoka mwanzo na utamalizika katika mfumo mmoja au mwingine, kwa kadiri ambavyo mwanadamu ana tamaa ya madaraka.

Matokeo yake yamekuwa katika taabu zaidi, mauaji zaidi, kushuka heshima zaidi, huzuni zaidi, mateso zaidi na dhambi kuliko asasi yoyote nyingine ya mwanadamu. Inaangamiza mtu mmoja mmoja na jamii nzima ya mwanadamu. Hutia chachu katika maingiliano ya mwanadamu, kwani alama aonekanayo mtu ni hofu… imeshughulika na wakati uliopita katika hali ya kiovu na iliyojaa makosa, na pengine ni yenye uovu zaidi na makosa zaidi katika wakati wa sasa. Utumwa kama si wa dhahiri sana lakini ni wenye kutapakaa zaidi na hofu yake ni yenye kuenea kote.

Hofu ya kinyonge, dhalili na ya kitumwa ijitokezayo miongoni mwa vibaraka vyake inaitembelea na kuyaandama Makao ya Utawala wa Urusi; hofu ya maangamizi ya mtumwa mnyonge huzidisha uhasama kati ya Mashariki na Magharibi; hofu ya lipizo la mnyonge hujizalisha katika Afrika ya Kusini na kuyafunika majimbo; hofu ya mafedhuli kutia kasumba mateso, vifo vya ghafula, hunyonyesha makundi makubwa ya watu ulimwenguni pote.2

Lakini hatushirikiani katika mtazamo huu ulio mbaya kabisa. Tunatambua kwamba tatizo lenyewe ni kubwa kabisa, lakini tunajua pia kwamba Uislam ni Dini iliyoletwa na Allah, Aliye Muweza juu ya kila kitu. Uislam, miaka 1400 ulileta mpango wa sura tatu (three sided programme) kwa ajili ya kuondoa utumwa.

Kuzuia njia za kupatia watumwa wapya, kukomboa watumwa, na kuirudisha na kuiweka heshima ya kibi nadamu kwa watumwa. Na ukweli ni kwamba ingawa Banu Ummayya waliuhujumu upande mmoja wa mpango huo kwa kuingiza utumwa kwa njia ya kuwanunua, hawakuweza kupunguza athari ya pande hizo nyingine mbili zilizobaki. Na watumwa katika ulimwengu wa Kiislamu walipata tena heshima yao ya kibinadamu iliyopotea.

Mfumo ambao umeonyesha manufaa yake, na ambao umepata mafanikio katika nyanja, ambako mifumo mingine imeshindwa kabisa, kwa hakika utapata ukomeshaji wa jumla wa kila aina ya mgawanyiko, mtengano, tofauti na dhuluma kama utapewa nafasi. Ameer Ali anaandika:

“Inabakia kwa Waislamu (sic.–japo kwa makosa) kuonyesha uwongo wa kashifa juu kumbukumbu za Mtume mkubwa na Mtukufu (zinazofanywa na wazushi na maadui wa Uislam) kwa kutamka kwa maneno ya wazi kwamba Utumwa (utumwa katika sura ya aina yoyote ile na tofauti za mataifa na rangi) unachukiwa na dini yao, na umekatazwa na sheria yao.”3 Na tuna uhakika kwamba Uislam utapewa fursa na Allah ili kuleta haki yote na kamili katika ulimwengu.

Maimamu wa Kishia, Viongozi waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu, waliiendeleza kazi ya Mtukufu Mtume na waliingiza katika wafuasi wao ile roho ya kweli ya Uislam. Wao kwa mifano yao na kwa kupitia kwenye dua, wameuhifadhi Uislam asilia (wenyewe) kwa ajili ya wafuasi wao.

Na Imamu wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Imamu Muhammad al-Mahd (amani iwe juu yake) Anayengojewa, atadhihiri tena wakati ulimwengu huu utakapokuwa umejaa dhuluma, ukatili na kutokuaminika.
Wakati yeye Anayengojewa atakapotokea kutoka katika Ghaibati (Alikofichwa na Allah) ataujaza ulimwengu na Haki, Uadilifu, Uaminifu na Rehema. Tumeamini katika ulimwengu ulio bora zaidi (wa kesho–Akhera) na tunajua kwamba katika hali yoyote ile utumwa utavyojitokeza katika kujificha kwake katika wakati wa kudhihiri tena kwa Imamu wa Kumi na mbili, yeye anayengojewa, (utumwa huo) utalazimika kutoweka na kuicha nafasi yake kwenye undugu na heshima ya kibinadamu kwa watu wote.

 • 1. Williams, op. cit., uk. 8.
 • 2. Sherrard, op. cit., uk. 188-189.
 • 3. Ameer Ali, Spirit of Islam, uk. 267

Maelezo Ya Nyongeza (Post Script)

Mheshimiwa Mwandishi (wa kitabu hiki) aliandika nyongeza ya maelezo katika mwaka wa 1987 wakati Afrika ya Kusini ilikuwa bado ni Taifa la kibaguzi (ubaguzi wa rangi) na shirikisho la Urusi (Sovieti Union) ilikuwa bado ni taifa lenye nguvu sana.

Licha ya mabadiliko haya muhimu katika uwanja wa kisiasa ulimwenguni, maelezo ya mwandishi kuhusu utumwa wa kitaifa (taifa moja kutumikishwa na lingine) bado ni halali wakati huu wa mwanzo wa karne mpya.

Ukoloni mambo leo bado upo katika mifumo mbalimbali tofauti na sasa Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO) linatumiwa kama mhuri wa kibali cha kuendelezwa zaidi shabaha na malengo ya mataifa yenye nguvu sana yaliyobaki katika ulimwengu huu.

Nchi ya Marekani (USA) na washirika wake wa Ulaya walitumia “Kadi ya demokrasia,” demokrasi ya kuteuliwa katika Ulimwengu wa Tatu inavumilika tu kama itahakikisha faida na maslahi ya nchi za Magaribi, kama ilivyoonekana katika suala la Algeria na Uturuki.

Baraza la Usalama, Baraza pekee lishughulikalo na maamuzi ya Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO), linaendesha shughuli zake katika misimamo isiyokuwa ya kidemokrasia. Inatumika kwa kuchaguliwa tu au kuteuliwa katika kuhalalisha maslahi ya matajiri na wenye nguvu juu ya mataifa yaliyo dhaifu ya ulimwengu.

Nchi ambayo iko ndani ya ‘vitabu vibaya’ vya nchi za Magharibi kamwe nchi hiyo haiwezi kupatiwa uamuzi ulio sawa na haki wakati nchi ya Iraq ilipoivamia Iran, hakukuwepo na dhoruba kali la jangwani, lakini wakati nchi hiyo hiyo, yaani Iraq ilipoivamia Kuwait na kuitishia Saudia (Saudi Arabia) na washirika wengine katika eneo hilo. “majeshi ya ushirika huo” yaliungana kwa kibali cha ridhaa ya Umoja wa Mataifa (UNO).

Jinai hiyo katika hali zote lilikuwa sawasawa na kutendwa na mhalifu yule yule, lakini bado hali iliyooneshwa kwa mhalifu ilikuwa tofauti kwa sababu tu muathirika wa pili (yaani Kuwait) alikuwa mshirika wa upande wa nchi za Magharibi wakati ambapo huyo muathirika a kwanza (Iran) hakuwemo ndani ya vitabu vizuri vya nchi ya Marekani (USA).

The New World Order (mpango wa Marikani) kwa hakika ni zama ya unafiki: Mataifa yenye nguvu za kijeshi bado yanaendelea kulundika na kutengeneza zaidi silaha za kisasa zenye maangamizi makubwa na wakati huo huo wanaendelea kuhubiri kwa mataifa dhaifu kuhusu kujizuia wasitengeneze silaha kama hizo!

Wakiwa mbele kwa masuala ya mazingira; wachafuzi wakubwa kabisa wa mazingira ni mataifa yenye viwanda vingi: lakini bado ni nchi ya Marekani (USA) ambayo ndiyo inakataa kutia sahihi mkataba wa kuzuia momonyoko wa ukanda wa hewa safi katika angahewa.

Kanuni ya uadilifu ya haki kwa wote siyo kawaida katika mpango huu wa Marikani (New World Order). Maslahi binafsi ya matajiri na nchi zenye nguvu, katika istilahi yake zaidi ya kistaarabu ya “maslahi ya kitaifa” bado ndio ufunguo unaofanya kazi katika mchezo huu. Pengo lililopo kati ya nchi za Kaskazini na Kusini linakuwa kwa haraka sana. Serikali za nchi masikini haziko huru kutekeleza sera zao wenyewe; ni Benki ya Ulimwengu, chombo kingine cha Ukoloni mambo leo, ambayo ndiyo inayowaundia sera za kiuchumi watu wan chi hizo. Sera hizi haziboreshi wengi wa watu katika nchi za Afrika na Asia.
Kwa masikitiko sana, hata katika suala la utambuzi wa misiba ya watu inaonyesha kunakuwepo na ubaguzi; msiba wa kundi moja la watu ambao waliteseka katika mikono ya Wanazi unafahamika kwa mapana sana (na Pia wakazawadiwa kuwa na “Nchi ya kuishi” ambayo baadaye inageuka kuwa “taifa”) wakati ambapo utambuzi wa msiba wa mamilioni ya Waafrika ambao walichukuliwa na kupelekwa katika nchi za Amerika na kunyang’anywa jina lao, utambulisho, dini, lugha na haki za msingi za kibinadamu bado ni jambo lilioko katika kujadiliwa.

Na tukiwa pamoja na mwandishi, tunamwomba Muumba Mwenye Nguvu Zote aharakishe kudhihiri kwa Mahdi, aliye Masihi, ambaye atauondolea ulimwengu na uonevu na kuieneza haki na amani katika ulimwengu.

Amin.

Back cover

“Enyi watu! Hakika Adamu hakuzaa mtumwa mwanaume au mtumwa mwanamke, wanadamu wote wako huru.” Imamu Ali (as)

Maoni ya watu kuhusu utumwa ni kwamba umetupwa kwenye mapipa ya takataka ya historia, wakati bado athari za ushenzi huu wa kuchukiza ambao mwanzo wake ulikuwa dhidi ya Waafrika, unajitokeza wenyewe kwa sura mpya na mbaya zaidi kwenye karne ya 21. Tangu kupigwa marufuku kwake rasmi katika mwaka wa 1863, utumwa umechukuwa sura ya uovu na ya kuchukiza zaidi, katika muundo wa utumwa uliopakazwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za kuzalisha unaofanywa na “Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba” (Multi National Cartels) ni muundo mpya wa utumwa.

Allamah Rizvi anaelezea suala hili la biashara ya utumwa kwa muktadha wake halisi. Allamah Sayyid Saeed Akhtar amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafiti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upendeleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur’an, Hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislam. Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha na kujigamba. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi.

Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640/ 2127555
Barua Pepe: alitrah@raha.com
Tovuti: www.ibn-tv.com