Ukweli Wa Shia Ithna Ashariyyah

Author(s): 
Publisher(s): 

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Haqiqat Shi’a Ithna-Asahariyyah kilichoandikwa na, Dr. ‘Asad Wahid Al-Qaasim.

Kitabu hiki ni utafiti wa kina uliofanywa na mwanachuoni huyu mahiri, kuhusu mitafaruku iliyotokea katika Uislamu na baina ya Waislamu, kuanzia wakati wa Mtukufu Mtume (saww), na mara tu baada ya kufariki kwake hadi sasa. Katika utafiti wake huu, ameiangalia sana historia ya Kiislamu kama ilivyohifadhiwa katika vitabu vya historia vilivyo andikwa na wanachuoni wa Kiislamu wa kuaminika wa madhehebu zote za Kiislamu zijulikanazo. Katika kujadili masuala mbali mbali yenye utata, huwa ametumia dalili, hoja, akili na elimu.

Translator(s): 
Category: 
Topic Tags: 
Person Tags: 

Kuhusu Mtungaji

Mtungaji ni mtafiti katika misingi ya ukweli, mwenye kujitahidi jitihada kubwa kabisa katika njia ya kuufikia, hadi Allah (s.w.t.) akamwongoa katika njia ya sawa, “Na wale ambao wamejitahidi katika njia yetu. tutawaongoa katika njia zetu.”

Amezaliwa katika kijiji cha Dairul-Ghusun katika ukingo wa Magharibi, katika nchi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Amehitimu masomo yake ya Sekondari, kisha akaenda Jordan Na akapata Diploma ya Uhandisi, kisha akaenda Ufilipino na akapata Shahada ya kwanza ya Uhandisi kisha akapata Shahada ya pili katika Idara ya ujenzi. Na hivi sasa amepata shahada ya Udaktari katika Idara ya utawala wa serikali baada ya kumaliza utafiti wake (wa “Islamic public Administration” “Mfumo wa utawala wa Kiislam”).

Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Haqiqat Shi’a Ithna-Asahariyyah kilichoandikwa na, Dr. Asad Wahid Al-Qaasim.

Kitabu hiki ni utafiti wa kina uliofanywa na mwanachuoni huyu mahiri, kuhusu mitafaruku iliyotokea katika Uislamu na baina ya Waislamu, kuanzia wakati wa Mtukufu Mtume (saww), na mara tu baada ya kufariki kwake hadi sasa. Katika utafiti wake huu, ameiangalia sana historia ya Kiislamu kama ilivyohifadhiwa katika vitabu vya historia vilivyo andikwa na wanachuoni wa Kiislamu wa kuaminika wa madhehebu zote za Kiislamu zijulikanazo. Katika kujadili masuala mbali mbali yenye utata, huwa ametumia dalili, hoja, akili na elimu.

Pia katika jitihada yake hii, amejaribu kuelezea kwa urahisi kabisa njia za kupunguza (kama si kuondoa kabisa) misuguano iliyopo baina ya Waislamu na baina ya madhehebu.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo watu hawakubali kitu mpaka kwa hoja na dalili za wazi. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeona ikitoe kitabu hiki kwa luhga ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Abdul Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 1017
Dar-es-Salaam.

Dibaji Ya Mtarjum

Mtunzi wa kitabu hiki Haqiqat Shi’a Ithna-’Ashariyyah amejitahidi sana kutoa ushahidi wa hoja zake katika Kitabu cha Sahih Al-Bukhari na hiyo ni kutokana na uzito na umuhimu wa Kitabu hicho ambacho kinazingatiwa na ndugu zetu Ahl as-Sunnah wal Jama’a kuwa ni Kitabu Sahih zaidi baada ya Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Na yaonyesha kuwa Mtunzi amenukuu ushahidi wake kutoka Sahih Al-Bukhari (Arabic- English) cha Dr. Muhammad Muhsin Khan-chapa ya Dar al-Arabia Beirut.

Ama kuhusu Sahih zingine kama vile Sahih Muslim na nyinginezo, Mtunzi ametaja ni mlango na maudhui gani amenukuu ushahidi wake jambo ambalo halitamwia vigumu msomaji kufuatilia pindi atakapopenda kufanya hivyo.

Ni matumaini yetu kuwa - wasomaji wetu watavutiwa na mtiririko wa Kitabu hiki; pili, watakuwa ni wadadisi, waadilifu na wapambanuao haki na batili. Hivyo hawatakanusha au kukubali jambo bila ya ushahidi wowote.

Tunamwomba Allah (s.w.t.) atuonyeshe njia ya haki na atujaalie kuifuata na atuonyeshe njia ya mfarakano na atujaalie kuiepuka.

Wabillaahi Taufiq.
Abdul Karim J. Nkusui
27/11/2001

Kwa Kila Mwenye Kutafuta Ukweli…

Natoa Zawadi Ya Kitabu Hiki

Ulimwengu wa Kiislamu siku hizi unashuhudia majaribio mengi ya kuchochea fitina na kuleta mparaganyiko baina ya Madhehebu ya Kiislamu na kuyachongea baadhi yake kwa mengine, na unashuhudia mashambulizi makali yanayo elekezwa kwa Shi’a Al-Imamiah Al-Ithna- ’Ashariyah kwa kuitukana itikadi yao ya Kiislamu na kuishambulia bila ya adabu au huruma.

Na ulimwengu wa Ki-Islamu umegharikishwa kwa mamilioni ya nakala za vitabu ambavyo vinatukana itikadi ya madhehebu hii. Na ambacho hakifichikani kwa yeyote ni kwamba vingi kati ya vitabu hivyo vinatungwa kwa msukumo unaotoka kwa Mawahhabi, na misaada kutoka kwao inaendelea kwa madai ya kutetea Ahl as-Sunnah wal- Jama’a.

Na majarabio yao haya si kingine isipokuwa ni kutaka kutimiza malengo ya wakubwa wao ambao wanaenda mbio kuwagonganisha Waislam wao kwa wao, na wanashutumu dhehebu la Shi’a kwa ukafiri, ushirikina, umajusi, kuritadi na tuhuma za mazushi mengine.

Na haikuwa kuandika kwetu maudhui haya isipokuwa ni kuuzindua ‘Ummah kuhusu ukweli wa dhehebu hili linalo singiziwa, ambalo mizizi ya itikadi yake na fikira zake ni kutoka ndani ya Kitabu Kitukufu na Sunnah Tukufu za Nabii, na utaona katika kurasa za utafiti huu, hoja na dalili zinazounga mkono hayo kutoka katika Qur’an Tukufu na vitabu Sahih vya Hadith kutoka kwa Ahl as-Sunnah, na hasa kitabu cha Al- Bukhari ambacho wanakizingatia kuwa ni kitabu Sahih baada ya Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Na Mwandishi wa maudhui haya ni mmoja tu miongoni mwa wengi walioona haki na wakaifuata baada ya kuwa amekumbwa na fitina, lakini akakataa kujiingiza humo isipokuwa baada ya utafiti na uchunguzi kama alivyoamrisha Allah (s.w.t.):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ {6}

Enyi mlioamini kama Fasiq akikujieni na habari: (yeyote ile, msikubali tu) bali pelelezeni (kwanza) msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mlio yatenda. (49:6)

Mwanzo ulikuwa ni pale nilipopata vitabu vya Ihsan Ilahi Dhahiri, Musa Al-Musawi na wengineo katika Waandishi ambao wanadai kuwa Shi’a ni makafiri na wala hawaamini Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na kwamba wana Qur’an nyingine na wananasibisha kwenye misingi isiokuwa ya Ki-Islamu kabisa. Mwanzo sikuwa natilia maanani kauli zote hizo, na hiyo ni kwa sababu ya elimu yangu ya mwanzo kwa misingi ya vitabu hivyo vyenye sumu na ambavyo havina malengo isipokuwa kuchochea fitina na mparaganyiko, tukiachilia mbali kutia chumvi mno na kukuza mambo kupita kiasi.

Haikuwa rahisi kuviamini, hasa kwa kuwa sikuwa na shaka kabla ya hapo ya kwamba Shi’a ni Waislamu kama wengine miongoni mwa Ahl as-Sunnah, na hiyo ni pamoja na kuwa na elimu ya kuwepo baadhi ya hitilafu ambazo haziafikiani na fujo hilo la kutia shaka na kukufurishana.

Lakini kutokuwa kwangu na elimu ya uhakika wa itikadi ya Kishia kwa undani, na kutosheka kwangu kwa mwanzo, hakukuwa kunastahimili mbele ya mawimbi makubwa ya kuwa na shaka. Mawimbi ambayo yalikuwa yanaletwa na watu ambao wametumbukia na kuwa mateka wa baadhi ya vitabu vyenye sumu, baada ya kuamini kila kilichopo humo bila ya kudadisi wala kujaribu kujua rai ya Shi’a katika hilo kama kwamba watunzi wa vitabu hivyo ni ma’asum (wasio na madhambi), ambao haijuzu kufikiri juu ya kauli zao au kuzijadili au kuhakikisha upeo wa usahihi wake.

Na kwa masikitiko makubwa miongoni mwa hawa mateka kuna mwenye nia nzuri, na kwa mashambulizi yake dhidi ya Shi’a hataki chochote isipokuwa kutetea itikadi Sahih ya ki-Islamu kama anavyoona yeye.

Lakini Ta’assub ya upofu wenye kuchukiza na ujahili ni udhuru ambao haukubaliki baada ya kutimia njia za utafiti na uchunguzi. Mu’umin ni mwerevu na wala haamini kila kinachosikiwa na kusemwa, kwani kuna wapiga debe wa masultan na maulamaa waovu, jambo ambalo linatulazimu kuchukua kinga na tahadhari katika anga lenye kufunikwa na mawingu ya fitina na kugubikwa na giza lake.

Na mbele ya nyenzo hizi nilikuta nafsi yangu inasukumwa kwenye utafiti na uchunguzi ili kujua ukweli wa hawa Mashi’a, na nimetazama maoni ya pande mbili, na hoja zao kimaudhui na akili timamu. niliepusha nafsi yangu kutokana na Ta’assub ya kimadhehebu ya upofu ambayo haisaidii chochote katika haki, hasa katika utafiti wa masuala ya hitilafu baina ya Shi’a na Sunni unazingatiwa kwamba ni utafiti ambao uko katika duru la Uislamu kwa dalili zitokazo katika Qur’an Tukufu na Hadith tukufu za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.)

Hapa naleta mukhtasari wa utafiti wangu kwa msomaji mtukufu, ambaye namuomba afikirie katika yale anayoyasoma, kwa hakika katika utafiti huu tumetegemea sana Hadith kutoka katika vitabu Sahih vya Ahl as-Sunnah na hasa Sahih Bukhari ambayo wameizingatia kuwa Hadith zake ni sahih haziguswi na shaka wala haiwezekani kuwatuhumu wapokezi wake 1mpaka ikawa daraja ya Sahih Bukhari kwao inafuatia Kitabu cha Allah (s.w.t.). Na katika uchunguzi huu tutaeleza nukta muhimu za Ikhtilafu baina ya Sunni na Shi’a, mfano; Uimamu, msimamo wa Mashi’a kwa Masahaba, Qur’an na Sunnah tukufu za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) tukiongezea baadhi ya maudhui ambayo ni mashuhuri kwa Mashi’a kama vile ndoa ya Muta’ (ndoa ya muda maalum) na Taqiyah …. Kwa dalili na hoja kutoka katika Kitabu Kitukufu cha Allah (s.w.t.) na Hadith sahih kutoka kwa Ahl as-Sunnah. Na hapa tunaashiria misingi tulioitegemea katika utafiti wetu na tunaitakidi kuwa ni salama zaidi katika kufikia ukweli.
Nayo ni kwamba, tumezingatia kwamba mwongozo wetu katika kutoa dalili uwe ni katika yale yote yanayoafikiana na mafuhumu ya Kitabu Kitukufu, na ambao utangulizi wake ni salama kwa sababu tunaweza kuitakidi dalili zinazoonekana kuwa ni Sahih lakini bila ya kuangalia utangulizi wake kiakili ambao huenda haukuafikiana na kinachotolewa ushahidi, na hili ni jambo ambalo limewatumbukiza wengi kwenye dimbwi la kuchanganyikiwa katika kujua ukweli na kuwapeleka mbali na ukweli.

Anayeamini tangu mwanzo kwamba Masahaba wote ni katika wale ambao hawaguswi na masharti ya kukosolewa na kurekebishwa, anaweza kukubali baadhi ya uwongo kuwa ni kweli, kwa matokeo ya nyendo za baadhi ya Masahaba ambao hawaendi sambamba na ubainifu wa Kitab na Hadith tukufu. Kisha hakuna budi tueleze baadhi ya nukta za makala ya daktari Muhammad Ar-Ramihi chini ya maudhui yenye anuani:

Je, tunahitaji kujifunza namna ya kufikiria? kutokana na faida inayopatikana humo, tumeonelea katika kumfumbua macho msomaji mtukufu kwa misingi ya fikira Sahih ya kielimu, na misingi yake huenda itamsaidia katika kusoma kwake utafiti huu katika upande mmoja bila ya mwingine.

Hii ni pamoja na kuongezea kwamba ushahidi wa Shi’a kwa Hadith zinazotoka katika vitabu Sahih vya Ahl as-Sunnah haimaanishi kwa hali yeyote ile kuamini kwao usahihi wa yote yaliopokelewa humo bali ni kwa kusimamisha hoja na dalili kwa wanao wapinga kwa yale yaliokuja kwa njia yao na kuwalazimisha kwa yale walio jilazimisha nafsi zao na huu ndiyo usawa na uadilifu halisi kwa watu wa mantiki na uadilifu.

Na kuhusu manhaji (njia) sahihi ya kufikiria au utafiti sahihi wa kielimu tumeonelea kwamba tuelezee baadhi ya nukta za makala ya daktari Muhammad Al-Ramihi Mhariri wa Jarida la Kiarabu la Kuwait:

Je, Tunahitaji Kujifunza Namna Ya Kufikiri?

“Moja ya mambo ambayo yamekuwa ni muhimu katika akili ya Mwarabu (binadamu) wa leo ni jambo la fikra sahihi au kufikiria kielimu - tukitaka ukweli halisi - nalo ni jambo ambalo lipo katika mifumo yetu ya malezi na katika jamii zetu kwa upana zaidi, na bila ya kuwepo mapito mema kwa mkabala wa kufahamu jambo hili tutabaki tunasikia, kusoma na kusema mambo ambayo Allah (s.w.t.) hakuyateremshia dalili, yanayoonekana mazuri kwa mandhari yake, lakini yana kila madhara kwa jamii yetu ya Kiarabu (Kiislamu) kwa sasa na kwa wakati ujao, na hatua za awali za fikra sahihi ni kutojisalimisha kwa kila kinachosemwa na kuandikwa na kukichukua kijuujuu, ikiwa hakina tegemeo la dhahiri la kiakili.

Mwanadamu ni kiumbe hai anapatwa na mambo, anapatia na kukosea, na sio lazima kila anachokisema ndiyo mwisho na kikomo kama ile kauli isemayo “kauli ya zamani tu ndio Sahihi kwa sababu waliotangulia wamekwishaisema,” haimanishi kikomo cha usahihi wake.

Rai ya zamani kuhusu jambo miongoni mwa mambo imekwisha semwa na kizazi kilichoishi katika wakati ambao binadamu walikuwa bado hawajapata maarifa waliyo nayo hivi sasa, na kwa kiasi vizazi vinavyokuja vitapata maarifa makubwa na mapana zaidi kuliko tuliyo nayo leo, kwa sababu elimu na maarifa ni kitu kipana na sio mazoea yanayobadilika kila siku kulingana na matamanio ya baadhi yetu au kutokana na ufinyo wa fahamu zao.

Hakika ubaya ambao unaenea baina yetu kwa wingi unatutishia kubaki mateka wa kutokuwa na maendeleo hali ya kuwa tunaghariki katika vita bila ya lengo, tunapigana na kuzozana kwa matamanio na kujisababishia matatizo ya kipuuzi, na tunazozana baina ya hitilafu bila ya kufikiria fikra ya kielimu ambayo ndiyo alama ya leo na ni kigezo cha kubaki hai” 2

Dhana Nzuri Ya Moja Kwa Moja Kwa Maulamaa Walio Tangulia Mara Nyingine Inamwongoza Mtafiti Kwenye Upotovu

Na ushahidi ni kwamba, fikra potofu zimekuwa nyingi baina yetu. Ametoa Fatwa hata yule ambaye usahihi hana hata chembe ya kuweza kutoa Fatwa katika siasa, dini, utamaduni na uchumi, na tukashangilia (kuwa ni wenye kujitahidi). Upeo wa elimu yao ni ton lililodondoka kutoka kwenye maandishi ya waliotangulia, na waliokuja baada yao au kuyasoma katika zama na nyakati zinazo tofautiana sana na zama zetu na hali zetu, wao katika hali zote - ni wenye kujitahidi au kunukuu - hawafikirii kwa yale yalioandikwa au kusemwa katika wanayo yatolea Fatwa katika mambo ya dunia na dini.

Hakika ni kwa ajili ya kupenda kutoa fatwa bila ya elimu katika mambo kumewafanya watu wawe na wasiwasi katika mambo yao ya msingi, mambo ya dini na dunia yao. Ni kweli elimu mpya za kijamii zinatuambia: “Hakuna kisomo kisicho fungamana na dalili, kwani wewe unaposoma dalili unasoma kwa maarifa yako ya kielimu, kisiasa, kiutamaduni … lakini ni kweli vile vile kuna dalili ambazo kuna uwezekano wa kuwepo Ikhtilaf (tofauti) ndogo ndogo na kuna dalili zinazo gongana na akili kwa mara ya kwanza.

Na kabla hatujaingia katika maudhui ya Kitabu hiki ambacho msomaji atapata humo ukweli wenye kuathiri na hoja zenye nguvu, ni vema tuelezee baadhi ya kauli chache za maulamaa wa Ahl as-Sunnah ambazo zinathibitisha na kukiri Uislamu wa Mashi’a na ambazo bila shaka zinaweka wazi uongo wa kauli za wale ambao wanawakufurisha, na wana watuhumu kwa mengi yasiokuwa hayo na ambayo hawanayo.

Imam Shahid Hassan Al-Banna alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya kuleta uelewano kati ya pande mbili za Sunni na Shi’a. Na ustadh Saalim Al-Bahnasaawi anasema juu yake “Tangu ilipoanzishwa ‘Jamaatut-taqribi’ baina ya Madhehebu ya Kiislamu na ambayo Imam Hassan Al-Banna alitoa mchango wake na Al-Qummi, ushirikiano unaendelea baina ya Ikhwanul-Muslimin na Shi’a”.3

Na huyu Al-’Allamah Al-Sheikh Muhammad Al-Ghazaali anasema: “… hakika pande mbili zinasimamisha uhusiano wao kwa Uislamu kwa kuamini Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na wanaafikiana maafikiano ya moja kwa moja juu ya misingi ya jumla katika dini hii,4 vile vile anasema: “Hakika kila kilichobaki katika wakati wetu huu miongoni mwa Ikhtilaf ni fitina iliyozuliwa baina ya Sunni na Shi’a! Nayo ni fitina inayoenezwa na ukoloni na kwa uchache wanataka kuibakisha ili iwe ni utambi daima baina yao kisha watekeleze malengo yao kupitia utambi huo.5

Na ustadhi Anwar Al-Jundi anasema: “Ukweli ni kwamba tofauti kati ya Sunni na Shi’a haizidi tofauti zilizopo tofauti baina ya madhehebu manne”6

Na anasema Sheikh Hassan Ayyub katika maneno yake ya kusifu Shi’a al-Imamiah Al-Ithna-’Ashariyah: “Huenda kundi la Imamia kwa ujumla liko mbali sana na ghuluu (kusifu kupita kiasi) na lililo kubaliana na akili katika dini yake, na ni katika makundi ya Kishi’a yaliyo karibu sana na Ahl as-Sunnah …”, dhehebu lao ni ya Tawhid halisi katika sifa za Allah (s.w.t.) na kumtakasa Muumba kutokana na kufanana na viumbe …7

Sheikh wa Al-Azhar Muhammad Shaltut anatoa Fatwa ya kujuzu kufanya ‘ibada kulingana na madhehebu ya Shi’a Ithna- ‘Ashariyah. Na anayetaka ziada ya kauli za maulamaa wa Ahl as-Sunnah ambazo zinashuhudia Uislamu na itikadi ya Kishi’a basi arejee Kitabu cha As- sunnatu wa Shi’a dhajatu muftailah au Kitabu cha Araul-Ulamaai l- Muslimina Fi Shiati wa Thawrahtil-Islamiyah vya Dr. Izzudin Ibrahim.
Ikiwa Maulamaa watukufu mfano wa Al-Banna, Kishki, Al-Maududi, Anwar Al-Jundi Al-Ghazaali na Hawway, Hassan Ayyub, Fatihi Yakun, Atilimisani, Abu Zahra, Shaltut na wengineo wengi ambao nafasi haitoshi kuwataja - wanaona kuwa Shi’a ni Waislamu wenye kumpwekesha Allah (s.w.t.), je, ni mantiki na akili kuacha kauli zao na kuchukuliwa kauli za Dhahiriy, Al-Khatib Al-Jazairi, Al-Gharib, na wengineo miongoni mwa waandishi wanaowakufurisha Shi’a na ambao hawakumsikia yeyote isipokuwa kupitia katika vile vitabu vyao vyenye sumu?

Wako wapi wao kati ya Maulamaa wajuzi ambao wametoa Fatwa juu ya Uislamu mzuri wa Shi’a?

Na ni nani Musa Al-Musawi ambaye baadhi wanakitolea ushahidi Kitabu chake dhaifu, na kukizingatia kuwa ni msingi wa hukumu yao juu ya Shi’a isipokuwa ni kati ya watu waovu waajiriwa (mamluki) aliye tayarishwa na maadui wa Uislamu baada ya kufaulu mapinduzi ya Kiislamu ili kufanya mambo maovu wakamvalisha kilemba cha Maulamaa wa Kishi’a ili atukane itikadi yao kwa jina la Ushi’a baada ya kujazwa mifuko yake kwa kile kitakacho fikisha paji lake motoni siku ambayo haitofaa mali wala watoto isipokuwa yule atakayemwendea Allah (s.w.t.) kwa moyo safi, na watajua wale ambao wamedhulumu ni mwisho gani wataishilia.

 • 1. Rejea Jarida la Al Mujtamaul Kuwaitiyyah No:920 la juni 13/1989 ambapo utaona jinsi ulivyokuwa ukali wa kumjibu sheikh Muhammad Al Ghazali naye ni katika maulamaa wakubwa wa Ahl as- Sunnah kwa sababu ya kutia shaka baadhi ya ushahidi wa Hadith zilizopo katika Sahih Bukhari, pia rejea ukurasa wa kitabu hiki utaona riwAyah za kisa cha Malaika wa mauti pamoja na Mtume Musa (a.s.) ambazo sheikh huyu alizitilia shaka.
 • 2. Jarida la Kiarabu No 372 la Novemba 1989.
 • 3. Kitabu cha As-Sunnatul- muftaraa alayha uk. 57.
 • 4. Kitabu cha Kaifa nafhamul Islam uk. 144 -145.
 • 5. Kitabu cha Difaun ‘anil- ‘aqidati wa-sh-Shariah.
 • 6. Kitabu cha Al-Islamu waharakatu-t-taarikh Uk. 421.
 • 7. Kitabu cha Tabsitul-aqaidi-l-Islamiyyah uk. 429 na uk. 430 kilichochapishwa 1980.

Utangulizi: Ni Nani Shi’a Ithna-’Ashariyyah?

Tunaeleza katika mwanzo wa utafiti huu nini makusudio ya neno Shi’ah, vipi limeanza, na kuenea kwa Ushi’a . Tunakuta katika kamusi za lugha kuwa neno Shi’a lina maana ya “Kufuata na wafuasi, na aghlabu limetumika jina hili kwa wafuasi wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na watoto wake mpaka likawa ni maalum kwao”.

Na wa mwanzo aliepanda mbegu ya Ushi’a katika Uislamu ni Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) naye ni wa kwanza kutamka jina la Shi’a kwa wafuasi wa Ahlul Bayt (a.s.) kama alivyopokea hayo As-Suyuti katika tafsiri yake Durrul-Manthur katika Ayah tukufu (Hao ni viumbe bora). Amesema: Amepokea Ibn Asakir katika Sanad yake kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillah amesema: Tulikuwa kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na akaingia Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) basi akasema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.): “Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika huyu na wafuasi wake wao ni wenye kufaulu siku ya Qiyamah na kwake imeteremka! “Hakika walioamini na kufanya vitendo vyema hao ndiyo viumbe bora.”1

Hivyo Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alilingania Manhaj (njia) hii na akawafanyia Ahlul-Bayt (a.s.) wapenzi na wafuasi. Na utapata juu ya hayo katika sehemu ya kwanza ya utafiti huu, dalili zinazothibitisha wosia wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.)kwa Ahlul-Bayt (a.s.) wake kwa Uimamu katika ‘Ummah huu baada yake, kuanzia kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na kuishia kwa Al Imam Muhammad Mahdi Sahibu-z- Zamaan (a.s.) ambaye atadhihiri mwisho wa zama ili kujaza dunia kwa haki na uadilifu kama ilivyojaa dhuluma na ujeuri.

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alipoaga dunia, kundi katika Masahaba, walionelea ukhalifa usiende kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), na Imam (a.s.) alikwishasema kwa kupinga kwake juu ya hilo kwa kukataa kwake kumbai Abubakr kwa kipindi cha miezi sita kama alivyopokea hayo Bukhari katika Sahih yake ambayo maelezo yake yatakuja katika sehemu ya kwanza kwa idhini ya Allah (s.w.t.). Na walikataa kumbai pamoja naye kundi la Masahaba wakubwa, mfano wa Zuber, ‘Ammar, Salman, Abudhar na wengineo.

Kisha Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alipoona kukataa kwake kunasababisha mbomoko usiotengenezeka katika Uislamu, na sote tunajua kuwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) hakuwa akitaka Ukhalifa wala hakutaka kutawala wala kupupia Ufalme na kushinda - alikubali na akayafumbia macho yale anayo yaona kuwa ni haki yake kwa kuunusuru Uislamu kutokana na kubomoka na kuparaganyika. Wafuasi wake walibaki chini ya uongozi wake, na Ushi’a haukuwa na nafasi ya kudhihiri katika zama za Makhalifa wa kwanza, kwa sababu Uislamu ulikuwa unapita katika manhaj yake iliyo sawa sawa.
Na alipopewa Bai’a Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), Mu’awiyah bin Abi Sufian alikataa kumbai na akampiga vita katika sehemu ya Siffin, na alimtangulia kwa hilo ‘Aisha bint Abubakr as- Siddiq.

Alitoka akiongoza jeshi linalompiga vita Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika vita vinavyojulikana kama vita vya Jamal. Masahaba wengi walijiunga pamoja na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika vita vya Siffin hadi wengi wao wakauliwa chini ya uongozi wake, kama vile ‘Ammar bin Yaasir, Khuzaimatu Dhi Shahadatain, Abu Ayyubil-Ansari na wengineo.

Na baada ya mambo kumnyookea Mu’awiyah bin Abi Sufian na kumalizika kwa duru ya Makhalifa, Mu’awiyah bin Abi Sufian alifuata sera ya madikteta, akawakandamiza Waislam na kuchukua Bai’a ya mwanae Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa, ‘Ummah kwa mabavu, na akazikhalifu Ayah za Allah (s.w.t.) zilizo wazi, kama vile kumnasibisha Ubaydullah bin Ziyad kwa baba yake na kupanua meza za vyakula, kujenga mahekalu makubwa na mengineyo katika israf na upuuzi, yote hayo kwa mali za ‘‘Ummah na pato la Waislamu.

Haya yote na watu bado wako karibu na zama za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na makhalifa, na namna walivyokuwa wakiyapanyongo mambo ya dunia na matamanio yake.

Kisha akamtilia sumu Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na akamuua baada ya kutengua ahadi na masharti yote aliyomuahidi, kisha akachukua bayi’a kwa mwanae Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa mabavu na hali yake inajulikana kwa ‘Ummah bila ya kuwa na ikhtilafu - Waislamu walishamjua kuwa ni mtu wa dunia hana uhusiano na dini… mpaka yakatokea mapinduzi ya Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) Karbala, na kuuawa kwake Shahid pamoja na wafuasi wake wasiopungua sabini na mbili miongoni mwa Aali zake na wafuasi wake, baada ya kukataa kumbai Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian.

Vivyo hivyo ulikuwa ni mwendo wa watawala wa Bani Ummayyah na Bani Abbas, katika kuwakandamiza Ahlul-Bayt (a.s.). Ukandamizaji kwa Ahlul Bayt (a.s.), ulikuwa kwa muda wote huo, na waliyapata (matatizo) mengi, miongoni mwayo ni kuuliwa, kufungwa jela na kuadhibiwa.

Ukiuchunguza mwendo wa watoto wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kwa ujumla, na ukaulinganisha na mwendo wa wafalme wa Bani Umayyah na Bani ‘Abbas, utagundua kuwa ndio umesababisha kuenea kwa Ushi’a ambao ndio Uislamu wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na si vinginevyo, na wala si kama walivyosema wapumbavu ambao walikuwa wakikariri wanayo yaeneza watawala wa Bani Umayyah na Bani ‘Abbas kuwa Ushi’a ni upuuzi wa ‘Abdillah bin Saba’ au mengineyo yasiyokuwa hayo miongoni mwa uongo ambao unasambaratika mbele ya macho ya anayesoma Itikadi hata kwa uchache tu.

Katika kipindi cha kwanza cha Bani Abbas, Al Imam Ja’afar as-Sadiq (a.s.) ambaye ni Imam wa Sita wa Mashi’a - kutokana na siasa yake ya hekima, aliweza kushirikiana na watawala na watu.

Na kwa sababu ya watawala kushughulika na kuimarisha utawala wao - alianza kueneza hukumu na kusambaza Hadith ambazo alizichukua kwa baba yake Al Imam Muhammad Al-Baqir (a.s.) kutoka kwa baba yake Al Imam Zaynul ‘Abidiin (a.s.) kutoka kwa Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), Bwana wa Mashahid (na Imamu Hasan as), kutoka kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.).

Ushi’a ukadhihirika bila ya kuwa na mfano katika zama hizo, kupanuka Madrasah ya Al Imam Ja’afar as-Sadiq (a.s.) katika zama hizo na umashuhuri wake ndiyo sababu ya kuitwa madhehebu ya Ja’afariyyah katika manhaji (njia) ambayo Shi’a Imamiyyah Ithna-’Ashariyyah wanaiamini tangu wakati huo hadi leo hii, na ambayo si kingine isipokuwa ni madhehebu ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na ambayo ndiyo dhehebu la ki-Islamu la asili.

Miongoni mwa waliokuwa wanafunzi wake wakubwa ni kama vile Hassan Al-Basriy na Abu Hanifa An-Nu’uman ambaye amesema katika kauli yake mashuhuri. “Kama sio miaka miwili angeangamia Nu’uman” alikuwa na maana ya miaka miwili ambayo alikuwa mwanafunzi katika darasa la Imam Jaafar bin Muhammad bin Ali bin Hussein bin Ali bin Abu Talib (a.s.), na ambaye amepewa laqab ya As-Sadiq.
Abu Hanifa aliuawa kwa sumu katika jela ya Abu Ja’afar Al-Mansur kwa sababu ya mapenzi na ufuasi wake kwa Ahlul Bayt (a.s.), na kumpinga kwake Mansur, na kwa sababu alikataa cheo cha Qadhi katika utawala wake. (rejea chochote ukitakacho katika vitabu vya historia juu ya hilo) Mansur alimkataza kutoa Fatwa hali yuko ndani ya jela.

Ama aliye eneza yanayojulikana kama madhehebu ya Hanafi ni Qadhi Abu Yusuf ambaye alikuwa mwanafunzi wa Abu Hanifa, Haruna Rashid alimpa uqadhi, jambo ambalo lilimsaidia katika kueneza madhehebu hayo.

Ni maarufu katika tarikh kuwa madhehebu manne yamechipukia kwa Al Imam Ja’afar as-Sadiq (a.s.), Imam Malik amechukua elimu yake kutoka kwenye vitabu vya Abu Hanifa ambaye amesoma miaka miwili kwa Al Imam Ja’afar as-Sadiq (a.s.) kama tulivyo bainisha juu, kisha Shaf’i akachukua kutoka kwa Malik, kisha Imam Ahmad akasoma kwa Shaf’i. Hivyo kinacho patikana katika vitabu vya madhehebu manne na kikaafikiana na madhebu ya Al Imam Ja’afar as-Sadiq (a.s.), basi kimetoka kwa Al Imam Ja’afar as-Sadiq (a.s.); na kinacho tofautiana ni Ijtihad yao.

Hakika Shi’a al-Imamiyyah Ithna-’Ashariyyah ni dhehebu ambalo limeepukana na Shub-ha na shaka, kwa sababu chini ya jina la Ushi’a yamechipuka makundi mengi sio katika Shi’a wala Shi’a sio miongoni mwa hayo na wala sio katika Uislamu hata chembe, Shi’a wako mbali nayo kama vile mbwa mwitu na damu ya Yusuf. Mfano wa baadhi ya madhehebu ambayo yamesema juu ya uungu wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), wakidai kuwa sehemu ya uungu ipo kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na imeungana na mwili wake, na baadhi yake yanasema kuwa Maimam ni Manabii wakidai kuwa wao ni waungu. Al Imam Ja’afar as-Sadiq (a.s.) alipojua Itikadi yao akawa mbali nao akawalaani na akawaambia wafuasi wake wawe mbali nao, na akatoa kauli kali juu ya hilo.

Na sijui ni kwa nini tunaona baadhi wanAyahesabu makundi haya na mfano wake katika Ushi’a pamoja na kujulikana kwake kuwa yako nje ya Uislamu na Mashi’a wako mbali nayo.

 • 1. Durrul - Manthuur ya Suyuti na Sawaiqul - Muhriqah ya Ibnu Hajar.

Sehemu Ya Kwanza: Uimamu

Kauli ya Uimamu sio bida’a iliyozuliwa na Shi’a kwani makundi yote ya Kiislamu yanasema kuwa Uimamu ni wajib, bali ni dharura ya kimaumbile kwa watu wote. Pamoja na kwamba Shi’a wana maoni maalumu, yaliyo muhimu zaidi ni kwamba, Uimamu ni maalumu kwa Maimamu kumi na mbili kutoka katika Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na utaona hoja zenye nguvu juu ya hili kutoka katika vitabu Sahih vya Hadith vya Ahl as-Sunnah.

Na kama Uimamu usingekuwa faradhi kwa Waislamu wote basi wasingekuwa chini ya uongozi wa Makhalifa na kuwafuata wafalme ambao walichukua utawala kwa jina la Ukhalifa kama vile Banu Umayyah, Banu Abbas na wengineo, na kukataza kuwakhalifu na kutoka katika utawala wao, kwa sababu wao ni Makhalifa na Ulul-’Amr. kwa hiyo Uimamu ni dharura ya kimaumbile, akili ina hukumu hivyo kwa ajili ya kulinda Shariah kutopuuzwa na kuchezewa. Hivyo ilikuwa ni dhuluma kuwatukana Shi’a kwa kauli yao juu ya Uimamu. Amma kuhusu itikadi yao ya kuwa Uimamu ni maalumu kwa Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) kumi na mbili, kuna dhambi gani kwa hilo? Je siyo vyema kwetu kuwauliza Shi’a ni dalili gani waliyo nayo juu ya hilo? Tutafupisha hoja na dalili zetu katika majibu yetu juu ya swali hili kwa utaratibu ufuatao:-

Kwanza - Hoja Za Kuthibitisha Uimamu Wa Ahlul- Bayt (A.S.)

Dalili zilizopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) juu ya Uimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) katika ‘Ummah baada yake ni nyingi. Tunaorodhesha zilizo mashuhuri kati ya hizo:

*Katika Sahih Muslim kwa Isnad yake kutoka kwa Zaid bin Arqam amesema: “Hakika Mtume alisimama akahutubia katika Ghadir Khum (baina ya Makkah na Madina), akasema: “Enyi watu hakika mimi ni binadamu, anaweza kunijia Mjumbe wa Mola wangu (Malaika wa Mauti) basi nikamwitikia, hakika mimi nawaachieni vizito viwili cha kwanza ni Kitabu cha Allah (s.w.t.) humo kuna uongofu na Nuru, basi chukueni (uongofu) katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) na shikamaneni nacho, na Ahlul Bayt wangu”.1

*Na katika Sahih At-Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa Ja’bir bin ‘Abdullah amesema: “Nilimwona Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) katika Joho lake siku ya ‘Arafa naye yuko juu ya ngamia wake anahutubia, basi nilimsikia anasema: “Enyi watu hakika mimi nimekwisha kuachieni ambayo kama mtashikamana nayo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Allah (s.w.t.) na kizazi changu, Ahlul Bayt wangu2

Tanbihi

Pia imepokewa kwamba Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi ninawaachieni ambacho kama mtashikamana nacho hamtapotea kamwe, Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Sunnah zangu”.

Tukikadiria usahihi wa Hadith hii basi haipingani na Hadith mbili zilizo Sahih hapo juu, kwa sababu Ahlul-Bayt (a.s.) wao ndiyo njia zinazoaminika zaidi katika kupokea Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.). Isipokuwa neno wa sunnatiy peke yake kama ilivyo katika Hadith ya mwisho halitoshelezi kujua (hiyo sunnah), kwa sababu madhehebu zote za Kiislamu zinadai kuwa zinafuata Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) pamoja na kuwepo hitilafu nyingi baina ya madhehebu. Kwa kutazama hitilafu zao katika Hadith iliyopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), basi ni Sunnah ipi tutafuata?

Bila shaka Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni moja lakini njia za kuipokea ni nyingi. Hivyo Sunnah imetofautiana kwa kutofautiana mapokezi ya wanaopokea, hivyo Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ikawa ni nyingi, na matokeo ya hayo Waislamu wamekuwa madhehebu mengi. Imepokewa kwamba idadi yake ni makundi sabini na tatu, kila kundi linasema kuwa linafuata Sunnah Sahih ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na kushikamana na kundi lolote kati ya haya hakuleti uongofu unaotakiwa kupatikana kama ilivyokuja katika Hadith.

Hivyo ikawa kuamini Hadith inayosema kushikamana na Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Ahlul-Bayt (a.s.) inakubalika zaidi katika akili na mantiki, kwa sababu kuna yanayotufanya tujue na yanaondosha shaka na Ikhtilaf kwa kujulikana kutakaswa kwa Ahlul Bayt (a.s.) kutokana na uchafu kama utakavyoona katika yanayofuata. Katika Sahih Muslim hakika Mtume amebainisha kuwa Ahlul-Bayt (a.s.) wake ni Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), Bi.Fatimah az- Zahra (a.s.) na watoto wao Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na Al-Imam Hussain ibn Ali ibn Abi Talib na kwamba wao ndiyo ambao imeteremka kwao Ayah ya Tat-hiir (kutakaswa) kama anavyopokea Muslim kwa isnad yake.

“Kutoka kwa Swafiyyah bint Shaibah amesema: ‘Aisha amesema: “Alitoka Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ana Kisa’(amejifunika shuka), basi alikuja Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akamuingiza pamoja naye (chini ya shuka), kisha alikuja Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akamuingiza pamoja naye, kisha akaja Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) akamuingiza pamoja naye, kisha akaja Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akamwingiza, kisha akasema: Hakika Allah (s.w.t.) anataka kukuondoleeni uchafu nyinyi Ahlul Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa3

Na katika Sahih At-Tirmidhi inabainika kwa hoja zilizo wazi kuwa wake wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) sio waliokusudiwa katika Ayah ya Tat-hiir kama baadhi ya watu wanavyodai ambapo At-Tirmidhi amepokea kwa isnad yake. Kutoka kwa ‘Amr bin Abi Salamah, mtoto wa kulelewa wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kwamba amesema: “Imeteremka Ayah hii ‘Hakika Allah (s.w.t.) anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa” Katika nyumba ya ‘Umm Salamah, basi akamwita Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.),Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na akawafunika kwa Kisa’ (shuka), na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) yuko nyuma ya mgongo wake akawafunika kwa Kisa’ kisha akasema: ‘Ee Allah (s.w.t.) hawa ni Ahlul Bayt wangu basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’

‘Umm Salamah akasema: ‘Na mimi niko pamoja nao ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.)?’ Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) akasema: ‘Wewe uko mahala pako na uko katika kheri.’ “4

Na katika Musnad ya Ahmad amepokea kwa Isnad yake kutoka kwa ‘Umm Salamah: “Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimwambia Bi Fatimah az-Zahra (a.s.): ‘Niitie mume wako na watoto wako’, basi akaja nao, hivyo akawafunika kwa Kisa’, kisha akaweka mkono wake juu yao akasema: ‘Ewe Allah; hakika hawa ni Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) basi jaalia rehema zako na baraka zako kwa Muhammad na Aali wa Muhammad, hakika wewe ni Mwenye kuhimidiwa mtukufu’. ‘Umm Salamah akasema basi nikanyanyua Kisa’ ili niingie pamoja nao akakivuta kutoka kwenye mkono wangu na akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri.’ “5

Hadith Ya ‘Umm Salamah Katika Mapokezi Ya Bukhari

Katika Mustadrak As-Sahihain amepokea Al-Hakim kwa isnad yake kutoka kwa Hanashi Al-Kinaani, amesema: “Nilisikia Abu Dhar anasema akiwa ameshika mlango wa Ka’aba: Enyi watu anaenijua basi mimi ni yule mnaemjua na asienijua basi mimi ni Abu-Dhar, nimemsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akiwa amesema; ‘mfano wa Ahlul Bayt wangu kwenu ni kama mfano wa Jahazi la Nabii Nuh (a.s.), atakayelipanda amenusurika na atakayeacha kulipanda ameghariki na kuteketea”6

Vilevile katika Mustadrak As-Sahihain kwa isnad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas: Amesema Mtume wa Allah (s.a.w.w.) “Nyota ni tumaini kwa watu wa ardhini kutokana na kughariki, na Ahlul Bayt wangu ni tumaini kwa ‘Ummah wangu kutokana na ikhtilaf, kama kabila katika Waarabu litawakhalifu basi watakhitilafiana na kuwa kundi la Iblis “7

Na kwa kufafanua zaidi na kuongezea katika yaliyopita miongoni mwa dalili katika kuthibitisha kuwa Ahlul Bayt (a.s.) ndio wenye vyeo hivyo vitukufu kwa kutakaswa, wamefanywa kuwa ni maalumu kwa kupewa sifa ya tamshi la Alayhi Salaam (katika vitabu, kunatumika vifupisho vya hivyo kama (a.s.) bila ya Masahaba wengine wote na wake wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na hiyo ni kutokana na vyeo vyao vitukufu na kwa yale aliyo yafanya Allah (s.w.t.) kuwa ni maalumu kwao kwa kuwatakasa kutokana na uchafu na makosa madogo kwa makubwa kama yanavyo dhihirika katika sehemu nyingi katika Sahih Bukhari: “‘Ali alayhi-s-salaam amesema:’Nilikuwa na ngamia katika hisa yangu ya ngawira na Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amenipa sehemu katika (mali ya) Khums, basi nilipotaka kumwoa Fatimah alayha-s-salaam binti wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.)…“.8

Katika mlango wa kuhimiza Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) Sala ya usiku na Sunnah bila ya kuifanya kuwa ni wajib, akasema “Mtume (s.a.w.w.) aliwagongea mlango Fatimah na ‘Ali alayhima-s-salaam usiku kwa ajili ya Sala “9

Na katika riwaya nyingine: amesema: “Nilimwona Mtume (s.a.w.w.) na Hasan ibn ‘Ali alayhima-s-salaam alikuwa anafanana naye…”10 Na vilevile: kutoka kwa Ali ibn Hussein alayhima-s-salaam alimwambia11 “Hakika Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) amemwambia kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) amemwambia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimgongea mlango usiku yeye na Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) binti wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.), akawaambia je, hamsali?”

Na ni mashuhuri kwamba sifa hii ya (Alayhi Salaam) hakupewa asiye kuwa Ahlul Bayt isipokuwa Manabii tu.

Na ameamrisha Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ya kwamba kuwasalia Ahli bayt wake kuambatane na kumsalia yeye, katika hadith ya Bukhari kupitia kwa Abdul-Rahman bin Abi Layla, amesema: “Alinikuta Kaab bin ‘Ujrah akasema: Je, nikupe zawadi? Hakika Mtume (s.a.w.w.) alitujia (siku moja) basi tukasema: “Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.), tumeshafahamu namna ya kukusalimia, basi ni namna gani tutakusalia?” akasema: “Semeni: Allahumma Salli alaa Muhammadin wa Aali Muhammadin kamaa Sallayta alaa Ibrahima wa aali Ibrahima Innaka Hamidum Majid”.12

Hiyo ni kwa sababu Ibrahim alikuwa ni mtume na ahlul-bayt wake walikuwa ni manabii na wenye kulinda Shariah baada yake, vivyo hivyo walikuwa Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) lakini tofauti ni kwamba wao wamekuja ili wawe Maimamu na wala sio Manabii kama alivyobainisha hayo Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alipomwambia Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) “Nafasi yako kwangu ni kama nafasi ya Harun kwa Mtume Musa (a.s.) isipokuwa hakuna Nabii baada yangu”13 kama yatakavyokuja hayo baadaye. inafahamika katika yote yaliotangulia miongoni mwa Hadith kwamba Allah (s.w.t.) Mtukufu kama alivyomfanya Mtume Wake kuwa ni maalumu anayeteremshiwa wahyi - Kwa Uma’asum na kutakaswa kwa kuwa sifa yake ni kufikisha ujumbe na dhamana ya usalama wa tablighi yake vinginevyo watu wasingeamini maneno yake na wala wasingekuwa na uhakika wa ujumbe wake. vile vile amewafanya Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) kuwa ni maalumu kwa Uma’asum na kutakaswa kwa dalili ya Ayah:

إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا {33}

“Hakika Allah anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa
(Al-Azhab 33:33)

Na kwa sifa yao ya kujaza nafasi ambayo ameiacha Mtume. Na hiyo ni kwa kubeba Shariah ya Allah (s.w.t.) kwa vizazi vijavyo kwa ajili ya kuihifadhi dini kutokana na upotovu wa wapotoshaji, uongo wa wadanganyifu na shaka za wenye shaka. Kwani kitu kibaya mno kilichokumba Shariah zilizotangulia ni kwamba wafuasi wake walikuwa wanachukua hukumu za Manabii wao baada ya kuondoka kwao kwa kila mtu. Basi upotovu ukawa kama ilivyosema Qur’an Tukufu basi wakapotoka na kupotea:

أَفَتَطْمَعُونَ أَنْ يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِنْ بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ {75}

“Mnatumaini ya kwamba watakuaminini (hao WAyahudi) na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Allah kisha wanayabadilisha baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua” (Surah Al-Baqarah 2:75)

Na kwa hiyo Uimamu unazingatiwa kuwa ni mlolongo wa Unabii katika jumla ya kazi zake isipokuwa kinachohusiana na Wahyi kwani huo ni maalumu kwa Manabii, na makusudio ya kuwa Uimamu ni mlolongo wa Unabii ni kule kuhifadhi Shariah kinadharia na kivitendo. Hivyo ikawa ni wajib Maimamu wawe Ma’asum kutokana na uwajib wa kunukuu Shariah ya Allah (s.w.t.) - ambayo alikuja nayo Mtume wa Allah (s.a.w.w.) - Kwa vizazi vijavyo kupitia katika njia safi, na ya asili ambayo imepitia kwa Maimamu kumi na wawili wa Ahlul Bayt (a.s.).Na kuna dalili za Qur’an zinazoashiria kuwa Uimamu ni cheo kitukufu hakipati mtu, dhalimu au fasiki, amesema Allah (s.w.t.):

قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِنْ ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ {124}

Hakika mimi nitakufanya kuwa Imam kwa watu”; akasema (Ibrahim): “Je na katika kizazi changu?”; (Allah) akasema: “(ndiyo, lakini) ahadi yangu haitawafikia madhalimu.
(Al Baqarah 2:124)

Hivyo makosa madogo na makubwa yanamfanya anayeyatenda kuwa ni dhalimu, hivyo ikawa hakuna budi ya Imam kuwa ni Ma’asum kutokana na makosa yeyote au dhambi kama ilivyoonyesha Ayah iliyotangulia.

Uchunguzi Juu Ya Ayah Ya “Tat-Hiir”

Hakuna shaka kwamba Ayah ya “Hakika Allah anataka kukuondoleeni Uchafu Ahlul-Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa” inaonyesha Uma’asum wa wale iliyo teremshwa kwa ajili yao, kwa sababu rijsi katika lugha ina maana ya uchafu (na uchafu ni kinyume cha usafi), na tohara katika lugha ina maana ya utakaso na usafi.

Rijsi ni dalili ya dhambi na tohara ni dalili ya uchamungu, hivyo mradi wa Allah (s.w.t.) Mtukufu kuwaondolea rijisi (uchafu) ni kuwaepusha na kuwaweka mbali na mambo yanayo sababisha upungufu kwao, hii haina maana nyingine isipokuwa ni Uma’asum na utakaso ambao Ayah imeteremka kwa ajili yao nao ni Ahlul Bayt (a.s.) “Muhammad, Ali, Fatwimah, Hassan na Hussein” kama zilivyo onyesha hayo kwa uwazi Hadith zilizotangulia.

Pamoja na hayo, kuna baadhi ya wanaosema kwamba Ayah hii siyo maalumu kwa Ahlul Bayt wa Nabii (s.a.w.w.), (Ali, Fatwimah, Hassan na Hussein) tu, bali inawahusu wake zake pia kwa hoja ya kuja Ayah ya Tat- hiir katikati ya Ayah nyingi (Katika sura ya Al-Ahzab) zinazohusu wake wa Nabii.

Lakini Ushahidi huu haukubaliwi, kwa kuongezea tuliyoyaeleza kuhusu Hadith ya ‘Umm Salamah kuwa Ayah hii ni maalumu kwa waliobainishwa majina yao miongoni mwa Ahlul Bayt (a.s.).

Hakika Ayah inaonyesha kwa dalili ya wazi juu ya Uma’asum wa ambao imeteremka kwa ajili yao kama tulivyotangulia kubainisha na wanawake wa Nabii sio Maasumu na hakusema yeyote juu ya hilo, na kutishiwa kwao talaka kama ilivyokuja katika Ayah zilizo tangulia Ayah ya Tat-hiir inatosha kuthibitisha ukweli huu, tukiachilia mbali kutoka kwa ‘Aisha bint Abubakr ibn Abu Quhafa na kuongoza jeshi lenye kumpiga vita Khalifa wa Waislamu na Imam wao ambaye ni wajib kumtii, na mengineyo mengi utakayoyaona kwa ufafanuzi zaidi huko mbele. Na yanayotilia nguvu pia, kutoingia wake wa Nabii katika makusudio ya Ayah ya Tat-hiir ni dhamira ya wenye kusemeshwa katika Ayah zilizotangulia Ayah hizo, ni dhamiri ya wingi wa wanawake zitazame Ayah:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ إِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا {28}

وَإِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنْكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا {29}

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَنْ يَأْتِ مِنْكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرًا {30}

وَمَنْ يَقْنُتْ مِنْكُنَّ لِلَّهِ وَرَسُولِهِ وَتَعْمَلْ صَالِحًا نُؤْتِهَا أَجْرَهَا مَرَّتَيْنِ وَأَعْتَدْنَا لَهَا رِزْقًا كَرِيمًا {31}

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَعْرُوفًا {32}

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا {33}

“Yaa ayyuha Nnabiyyu qul-liaz’waajika in kuntunna turidnal-hayata- d-dun’yaa waziynatahaa fataalayna....umatti’ikunna wa usarrihkunna saraahan jamilan wain kuntunna… minkunna … ya nisaa Nnabiyi man yya’ti minkunna bifaahishatin… lastunna… falaa takhdha’na... waqarna fiy buyuutikunna walaa tabarrajna...” (Al Azhab 33:28-33)

Na maneno yalipoanza kuhusu jambo la Tat-hiir, dhamiri ya mwenye kusemeshwa ikabadilika kwenda katika dhamiri ya wingi wa wanaume Innamaa yuriydullahu liyudhhiba ankumu-r-rijsa ahlal-bayti wa yutwahhirakum tathiyra, na hakika kuteremka Ayah za Qur’an kwa kuwahofisha wanawake wa Nabii kwa talaka, na Allah (s.w.t.) kutaka kuwataka Ahlul Bayt (a.s) kuja kwa kufutana, haina maana ya ulazima wa makusudio ya minasaba miwili kuwa ni wanawake wa Nabii, hiyo ni kwa sababu kuna Ayah nyingi za aina hii katika Qur’an zinazo zungumzia kuhusu mambo mawili tofauti, na huenda sababu ya kuja pamoja katika Ayah hiyo hiyo ni kuafikiana kwa kutokea minasaba miwili kama amabavyo Qur’an Tukufu haikupangwa kulingana na mfuatano wa Ayah kama zilivyoteremka, na hii inajulikana.

Hivyo basi hakuna ushahidi wowote kuwa sehemu ya Ayah ya Tat-hirr ni katika kipande ambacho kipo katika Qur’an iliyokusanywa.

Mwisho, katika yanayothibitisha kutoteremka Ayah ya Tat-hiir kwa wake wa Nabii ni Hadith ya Thaqalain (vizito viwili) ambayo inaamrisha kushikamana na Kitabu na Ahlul Bayt (a.s.). Kama makusudio ya Ahlul- Bayt (a.s.) ni wake zake, je kunapatikana Hadith tukufu kwa Waislamu inayosema tufuate wanawake na kushikamana nao baada ya kufa kwa Nabii sambamba na kushikamana na Kitabu cha Allah (s.w.t.)? Bila shaka hakuna. Namna gani itakuwa hivyo hali wamekwisha amrishwa kujilazimisha kubaki katika nyumba zao tukiachilia mbali kuwa wote walikuwa katika wakati mmoja, na kama itasemwa kwamba kushikamana nao ni kufuata walioyapokea, miongoni mwao katika Hadith za Nabii tunasema; kuna miongoni mwao ambaye hakupokea hata Hadith moja.

Pili -Dalili Za Kuthibitisha Idadi Ya Maimamu Wa Ahlul Bayt (A.S.)

Ni Kumi Na Mbili

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ameeleza kwamba Idadi ya Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) ambao wanafuata baada yake ni kumi na mbili. Imekuja katika Kitabul-Ahkam katika Sahih Bukhari: “Amesema: nimemsikia Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) anasema: ‘Watakuwa Maimamu kumi na mbili’, akasema neno sikulisikia, baba yangu akasema amesema kwamba wote ni kutoka katika Maquraish.”14

Na katika Sahih Muslim: “Dini haitaacha kuwa imesimama hadi siku ya Qiyamah na watakuwepo kwenu Makhalifa kumi na mbili wote ni katika Maquraish”.15

Na “mambo ya watu hayataacha kutengemaa maadam wataongozwa na Maimamu kumi na mbili.16

Na katika Musnad ya Ahmad kwa isnad yake kutoka kwa Abdallah bin Mas’ud kwamba amesema “Aliulizwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuhusu jambo la Makhalifa, akasema ni kumi na mbili kama vile idadi ya viongozi wa Bani Israil.”17

Na katika Taurati ya Ahlul-Kitab (kuna aya) ambayo madhumuni yake ni: “Hakika Allah (s.w.t.) Mtukufu alimbashiria Mtume Ibrahim kuhusu Ismail kwamba atamkuza, atampa kizazi na atamjaalia katika kizazi chake viongozi kumi na wawili na ‘‘Ummah mkubwa. Na tamko la neno kwa neno kama ilivyokuja katika (Taurati) kutoka katika Kitabu kitakatifu: “Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu”.18

Hakika Hadith za hapo juu baadhi yake zinabainisha kwamba utukufu wa Uislamu umejaaliwa katika Makhalifa kumi na mbili, na baadhi yake zinaonyesha kuwa uhai wa dini na kubaki kwake hadi siku ya Qiyamah umeegemezwa kwao na kwamba wao wote ni katika Maquraish. Na katika mapokezi mengine wote ni katika Bani Hashim, mapokezi haya hayaafikiani na madhehebu yeyote isipokuwa madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s.) - Madhehebu ya Shi’a Al-Imamiah Al-Ithna ‘Ashariyyah - na hiyo ni kwa kuafikiana idadi hii pamoja na idadi ya Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) kumi na mbili, wakati ambapo Maulamaa wa Ahl as-Sunnah katika kufasiri Hadith hii wamefikia katika njia yenye kikomo. Je makusudio yake ni Makhalifa wanne kwa kuongezea na makhalifa wa Bani Umayyah na Bani ‘Abbas?

Sisi tunajua kwamba Makhalifa wa mwanzo hawakuwa kumi na mbili, na wala kuwajumuisha kwao Bani Umayyah na Bani Abbas idadi hii haipatikani kwao na wala maulamaa wa Kisunni hawatatofautiana katika jambo kama walivyo tofautiana katika kufasiri kwao Hadith hii. Tunatoa mfano mmoja ili uone mgongano wao katika tafsiri ya Hadith hii, nayo ni rai ya As-Suyuti, anataja katika Kitabu chake cha tarekhe:
“Na walishapatikana Makhalifa kumi na mbili, Makhalifa wanne, Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), Mu’awiyah bin Abi Sufian, Zuber na ‘Umar bin ‘Abdul-Azizi, hawa ni nane, na inakisiwa anaweza kuunganishwa nao Al-Mahdi Al-Abbas kwa sababu yeye katika Bani ‘Abbas ni kama vile Abdul-azizi katika Bani Umayyah, na Tahir Al-’Abbas vile vile, kwa kile alichopewa miongoni mwa uadilifu, wanabaki wawili wanaosubiriwa mmoja wao ni Al-Mahdi kwa sababu yeye ni katika Ahlul Bayt (a.s.).”19

Na idadi ya kumi na mbili haitopatikana katika kundi lolote isipokuwa katika Maimamu wa Shi’a Ithna-’Ashariyyah. Na Hadith zilizo pokelewa maalumu kwa jambo hili katika njia za Kishi’a ni nyingi zinapita mpaka wa Tawatur ambapo humo kumetajwa majina ya Maimamu kumi na mbili kwa ufafanuzi zaidi kiasi ambacho haikubaliki shaka wala Ikhtilaf.

Basi ni kipi kinachotufanya tuache tafsiri ya Hadith iliyo wazi inayoafikiana na mfuatano wa Maimamu kumi na mbili wa Kishi’a na tunatupia nafsi zetu wenyewe katika matatizo ambayo hakuna pa kutokea.

Ni mashuhuri kwamba bwana wetu Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na Ahlul- Bayt (a.s.) na kizazi chao kimetokana na Mtume Ismail (a.s.) na viongozi kumi na mbili ni maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) na ‘Ummah mkubwa ni ‘Ummah wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na hii inafaa kuwa hoja kwa Ahlul-Kitab kuhusu ukweli wa bwana wetu Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.).

Tatu-Hoja Za Kuthibitisha Kupewa Ukhalifa Al Imam ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.)

Tumekwisha tanguliza hoja za Uimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) na kwamba Maimamu wao kumi na mbili ndiyo Makhalifa wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.). Na katika yafuatayo tunabainisha Hadith zinazoonyesha Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kumfanya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kuwa Khalifa katika ‘Ummah baada yake, na Imam wa kwanza (katika Maimamu kumi na mbili). Hadith hizi ni Mutawattir katika pande mbili isipokuwa Ikhtilaf baina yao imepatikana katika ushahidi wake, Hadith zilizo muhimu zaidi kuhusu hili ni ile inayojulikana kama hotuba ya Ghadiir, tunaitaja kwa muhtasari.

Katika Sahih Tirmidhi katika sanad yake kutoka kwa Zaidi bin Arqam kwamba Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) amesema:” (yeyote) ambaye Mimi ni kiongozi wake, basi ‘Ali (pia) ni Kiongozi wake.”20

Na katika Sunan Ibn-Maajah kwa isnad yake kutoka kwa Al-baraa’ bin ‘Aazib amesema: “Tulirejea pamoja na Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kutoka kwenye Hijja ambayo alihiji akateremka katika baadhi ya njia akaamuru Sala ya Jama’a, basi akashika mkono wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akasema: “Je, mimi si bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Wakasema: “Ndiyo!! Wewe ni bora”, Akasema: “Je, mimi si bora zaidi kuliko kila mumini kwa nafsi yake?” Wakasema: “Ndiyo”, Akasema: “Basi huyu ni kiongozi wa (yule) ambaye mimi ni kiongozi wake; Ewe Allah, mpende atakayemfanya kuwa kiongozi, Ewe Allah mfanye adui atakaye mfanyia uadui.”21

Na katika Musnad Ahmad bin Hambal kwa isnad yake kutoka kwa Al-Barra’ bin Aazib amesema “ Tulikuwa pamoja na Mtume kutoka kwa Al-Barra’ bin Aazib amesema “Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allah (s.a.w.w.) katika safari tukateremka Ghadir Khum, tukalinganiwa Sala ya Jama’a, pakasafishwa kwa ajili ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) chini ya miti miwili basi akasali Adhuhuri na akamshika Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) mkono akasema: “Je, si mnajua kuwa mimi ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Wakasema: “Ndiyo.” Akasema: “Je, si mnajua kuwa mimi ni bora zaidi kwa kila Muumin kuliko nafsi yake?” Wakasema: “Ndiyo.” Basi akashika mkono wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na akasema: “Ambaye nilikuwa kiongozi wake basi ‘Ali ni kiongozi wake! Ee Allah, mpende atakayempenda na mfanyie uadui atakayemfanyia uadui.”
Baada ya hapo ‘Umar bin Al-Khattab akasema: “Pongezi ewe mtoto wa Abu Talib, umekuwa kiongozi wa kila Muumin mwanamume na mwanamke.”22

Hadith hii imekuwa ni Mashuhuri kwa jina la Al-Ghadir kwa kutokea katika sehemu ya Ghadir al-Khum, nayo ni miongoni mwa dalili za Shariah zenye nguvu na iliyo wazi zaidi juu ya Ukhalifa wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na Uimamu wake baada ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.).
Na Hadith hii inazingatiwa ni katika daraja la juu la usahihi na yenye nguvu kwa sababu ni Mutawatir kwa Waislamu wote Sunni na Shi’a.

Baadhi katika wale ambao hawakuweza kuutilia shaka usahihi wa sanad ya Hadith hii wamejaribu kutilia shaka ushahidi wake juu ya Uimamu na Ukhalifa kwa kuchukulia kuwa neno mawla: lina maana ya Urafiki au Mpenzi na sio kiongozi, lakini neno Maula kama lilivyo katika Hadith ifuatayo kwa mfano limekuja kwa maana ya kiongozi au M-bora zaidi kwa uongozi au uwakala.

Kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) amesema: Hakuna Muumini (yeyote) isipokuwa mimi ni bora kwake zaidi kuliko watu (wote) katika dunia na akhera.

Mkipenda someni: “Annabiy awla bil-muminina min anfusihim, Fa ayyumaa Muumin taraka maalan falyarithuhu as-habuhu man kanuu, fa in taraka dainan au dhiyaa’n falyaatini wa anaa mawlaahu.23

Tukiangalia mazingira ya Hadith ya Ghadir, wakati wake na sehemu ambayo imeizunguka na vielelezo vingine, vyote hivyo vinaonyesha kweli kwamba makusudio hayakuwa isipokuwa Uimamu na utawala ambao una maana ya uongozi kwa maana zake zote na kati ya vielelezo hivyo ni: -

1. Hakika Ayatu-t-Tablighi “(Ewe Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako na kama hutofikisha basi utakuwa hujafikisha Ujumbe wake, na Allah (s.w.t.) atakulinda na watu),”24 ambayo ilishuka kabla ya tukio la Ghadiri kwa tamko lake kali na vielelezo vilivyopo, inaonyesha kuwa mazungumzo hayakuwa ni juu ya urafiki wa kawaida, kwa sababu haya hayawajibishi umuhimu wote huo na mkazo, kwani Allah (s.w.t.) amefanya jambo la kufikisha kuwa ni lenye kutegemea kuthibiti kwa Ukhalifa baada yake kwa sababu ni kwa Ukhalifa tu na wala sio jambo lingine Allah (s.w.t.) na Mtume wake watausalimisha ‘Ummah huu na dini yao kwa wale waliorithi elimu ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) baada kufariki kwake.

Kama ilivyo Ayah maalumu kwa kukamilisha dini: (“Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema zangu na nimekuridhieni Uislamu kuwa ni dini yenu”)25 ambayo iliteremka baada tu ya kumalizika hotuba ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), ambapo alimtawaza Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kuwa Khalifa na Imam kwa ‘Ummah. Inaonyesha kwa dalili ya wazi kwamba maudhui yalikuwa ni muhimu mno kama vile maudhui ya uongozi na Ukhalifa baada ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na kwamba alikuwa katika mnasaba wa kumteua Imam baada yake. Huyu atakayekuwa Imam baada yake si mwingine ila ni Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), na makusudio ya Hadith sio (“Ambaye nilikuwa kipenzi chake na msaidizi wake basi Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni kipenzi chake na msaidizi wake).

2. Njia ambayo Hadith imeelezwa kwa hali zake zote, jangwa lenye joto kali, ambapo hotuba ilitolewa hapo na kuchukua muafaka wa watu katika hali hiyo na sehemu hiyo yote, haya yanaonyesha usahihi wa mwelekeo tulio uchukua wa kumtawalisha Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika nafasi ya Uimamu na wala sio jambo lingine, kwa sababu ni jambo muhimu na ni wajibu lijulikane kabla ya kufika mauti ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), ambayo yeye mwenyewe hakuwa anajua itakuwa ni lini kwani yanaweza yakamfika kabla ya kufika kwake Madina. Hivyo ni wajibu wake kutangaza jina la kiongozi baada yake wakati huu, kwani kutangaza jina la kiongozi kuna athari za kivitendo kwa Waislamu baada yake na kwa dunia yao.

Ama kujua kwao kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni kipenzi cha waumini - kwa mfano - ni jambo ambalo halina athari katika maisha ya watu na kutojua kwao hakubadilishi kitu katika maisha yao na taratibu zao.

3. Na katika Sahih Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa Imran bin Huswayn amesema: “Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alituma jeshi na akampa uongozi wake Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) wakaenda katika sariya (kikosi) akampata msichana akamchukua, wakamkataza, na wanne katika Masahaba wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) wakakubaliana wakasema tutakapokutana na Mtume wa Allah (s.a.w.w.) tutamweleza aliyo yafanya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), basi Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuja na ghadhabu inaonekana katika uso wake na akasema: “Mnataka nini kwa ‘Ali? Hakika ‘Ali ametokana na mimi na mimi nimetokana na yeye, naye ni kiongozi wa kila muumini baada yangu.”26

Na kauli ya Allah (s.w.t.):

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ {55}

Hakika kiongozi wenu ni Allah, Mtume wake na walioamini ambao wanasimamisha sala na wanatoa zaka hali wakirukuu. (Al Maidah 5:55)

Imeshuka kwa ajili ya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), kama inavyofafanuliwa katika tafsiri za wafasiri wengi27 alipotoa sadaka pete yake kwa maskini aliyemjia akiwa katika sala hali akirukuu.

Na katika Hadith zingine ambazo zinaashiria Ukhalifa wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni Hadith ya Manzilah (Cheo), kutoka kwa Mus’ab bin Sa’ad kutoka kwa baba yake: ‘Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alitoka kwenda Tabuk, na akamwacha ‘Ali (a.s.).

Ambaye alisema: “Unaniacha pamoja na watoto na wanawake?” Mtume akasema: “Je, huridhii kuwa cheo chako kwangu ni kama cheo cha Harun kwa Musa, isipokuwa hakuna Nabii baada yangu?”28

Hadith hii inaonyesha kuwa vyeo vyote alivyokuwa navyo Harun kwa Bani Israil katika upande wa Mtume Musa (a.s.) kwa kuondoa Unabii. - Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa navyo, kwa sababu Hadith haina kizuizi chochote au sharti, na kwa hivyo yanafahamika kutoka ndani ya hadith hiyo yafuatayo:-

1. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa ni waziri wa Mtume na msaidizi wake maalumu na mshirika wake katika uongozi wa ‘Ummah kwa sababu vielelezo vimethibitsha vyeo hivyo kwa Haruna. Qur’an Tukufu inasema:

وَاجْعَلْ لِي وَزِيرًا مِنْ أَهْلِي {29}

هَارُونَ أَخِي {30}

اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي {31}

وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي {32}

كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا {33}

وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا {34}

إِنَّكَ كُنْتَ بِنَا بَصِيرًا {35}

قَالَ قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَىٰ {36}

Na nijaalie waziri katika jamaa zangu, Ndugu yangu Haruna (mfanye awe ndiye waziri wangu), nitie nguvu kwa (ndugu yangu) huyu, na umshirikishe katika kazi yangu (hii)…” (Allah) Akasema: Hakika umepewa maombi yako (yote haya uliyoyataka)., ewe Musa!
(Twaha 20:29-36)

2. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), alikuwa ni bora zaidi katika ‘Ummah baada ya Mtume kama alivyokuwa Harun katika Bani Israil.

Na yanayotilia nguvu kustahiki Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika cheo hiki kitukufu na kuwa kwake Khalifa wa ‘Ummah baada ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni kwamba yeye alikuwa ni mjuzi kati ya Masahaba wote. Katika kutambua hili walio mashuhuri kati yao ni hawa wafuatao:-

Kutoka kwa Said Bin Jubeir kutoka kwa Ibn ‘Abbas: “Amesema ‘Umar:’ Msomaji wetu mzuri ni Ubay na hakimu wetu ni Ali’.”29 Hiyo ni kwa sababu mwenye kuhukumu zaidi ndiyo mjuzi zaidi wa hukumu na kanuni, na hilo liko wazi,na inatosha kuthibitisha ujuzi wake mkubwa kule kuwa kwake mlango wa mji wa elimu ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na hekima yake, kama ilivyo katika Sahih Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas amesema: ‘Amesema Mtume (s.a.w.w.): “Mimi ni mji wa hekima na ‘Ali ni mlango wake.”30

Na katika Mustadrak As-Sahihain kwa sanadi yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas (r.a.) amesema: “Mimi ni mji wa elimu na ‘Ali ni mlango wake, basi anayetaka elimu apitie mlangoni.”31 Al-Hakim amesema isnad ya Hadith hii ni Sahih. Na katika Mustadrak As-Sahihain vilevile Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimwambia ‘Ali: “Wewe utaubainishia ‘Ummah wangu yale waliyo hitilafiana baada yangu.”32

Tujaalie kwamba Nabii wa Uislamu hakutaka yeyote kushika nafasi ya Ukhalifa baada yake; na tujaalie kwamba uchaguzi wa ukhalifa ulikuwa ni jukumu la ‘Ummah. Je, inajuzu katika uchaguzi kumwacha mjuzi zaidi na mchamungu zaidi na mwenye sifa nyingi zaidi katika pande zote kama tulivyobainisha? Kwani Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa ni mjuzi zaidi kati ya Masahaba wote na walikuwa wakirejea kwake wanapopatwa na mushkeli mgumu wa kidini.

Ama kuhusu juhudi yake na uchaMungu wake, amekwisha julikana kwamba ni Imam wa wenye juhudi. Na kuhusu ushujaa wake na ujasiri wake wa kipekee, alikuwa ni wa kwanza kujitolea muhanga katika Uislamu na alikuwa na nafasi muhimu katika kila tukio, katika vita vya Badr ameua kwa upanga wake Dhul-fiqar mashujaa thelathini katika mashujaa wa Kiquraish, na katika Uhud na Hunain alisimama msimamo wa kihistoria wa kufa na kupona akimtetea Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) baada ya wengi katika Masahaba kukimbia. Na katika Khandaq alijitokeza kupambana na shujaa mkubwa wa washirikina ‘Amr bin ‘Abdiwud Al-’Amiri, wakati ambapo hakujaribu yeyote kujitokeza miongoni mwa Masahaba waliobaki.

Na katika Khaibar Allah (s.w.t.) kupitia kwake alifungua mlango wa ngome baada ya kuwashinda, na lilishindwa kufungua kundi kubwa la Masahaba wakiwa pamoja. Vilevile ametafautiana na Masahaba wengine kwa kutomgusa ukafiri hata chembe, alipata malezi yake ya kipekee chini ya mwalimu wa kwanza wa binadamu, Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ambapo hakumwacha hata punde moja katika uhai wake wote mpaka alipoaga dunia akiwa mikononi mwake.

Katika uhai wake wote alikuwa anachukua elimu na hekima kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.), hivyo akastahiki kwa jitihada yake kuwa ni mlango wa mji wa elimu ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na mlango wa hekima yake na ndugu yake.

Na katika Sahih Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa ‘Umar amesema: ‘Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alifanya udugu baina ya Masahaba wake, basi alikuja Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akilia, akasema: ‘Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) umefanya udugu baina ya Masahaba wako na hukufanya udugu baina yangu na yeyote, Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akasema: ‘Wewe ni ndugu yangu duniani na akhera’33

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alimwambia Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.): ‘Wewe umetokana na mimi na mimi nimetokana na wewe’34 Pia ametofautiana na Masahaba wengine kwa kuwa ana fadhail nyingi zaidi. Imekuja katika Mustadrak As-Sahihain kutoka kwa Ahmad bin Hanbal, amepokea kwamba: “Haikupokewa kwa yeyote katika Masahaba wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) katika fadhail kama ilivyopokewa kwa ‘Ali”35 Na katika Kanzul-’Ummal: Amesema Mtume wa Allah (s.a.w.w.) ‘Hakika Allah ameniamrisha kumwozesha Fatimah kwa ‘Ali’36

Na hiyo ni baada ya kukataa kumwozesha kwa baadhi ya Masahaba waliokwenda kumposa kwa kujaribu kupata utukufu huu mkubwa kwa kuoa mtoto wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.),bibi wa wanawake waumini wa watu wa peponi, ambaye Allah (s.w.t.) anaghadhibika kwa ghadhabu yake; Na ni mkweli aliyesema: ‘kama ‘Ali asingeumbwa Bi.Fatimah asingepata mtu anayemfaa’.37

Na baada ya hayo yote kama tukijaalia kuwa uchaguzi wa ukhalifa uliachiwa watu wenyewe basi kwa hakika Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa ni bora wa waliokuwepo na anayefaa zaidi kwa ukhalifa.

Kukhalifu Kwa Jamhuri Ya Waislamu Nasi (Pokezi) Za Uimamu

Baada ya kueleza hoja na dalili zilizotangulia juu ya Nabii kumteua Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kwa amri ya Allah (s.w.t.), kuwa Imam wa Waislamu baada yake kwa kuanzia na Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) kumi na mbili kwa ujumla, baadhi ya watu wanaweza kuuliza kwa kusema: Ikiwa ni kweli nasi (pokezi) zote hizo ni za Uimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) basi kwa nini na vipi ukhalifa umeenda kwa wengine?

Kwa kujibu swali hili tutaeleza baadhi ya matukio muhimu ya kihistoria ambayo yalikuwa na athari kubwa katika kubadilisha mwelekeo wa historia ya ki-Islamu tukianzia na ijtihad ya makhalifa wa mwanzo katika ukhalifa na mengineyo mbele ya Hadith zilizo thabiti za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na kumalizia kwa Bani Umayyah kuuteka ukhalifa kwa nguvu na kutishia kwa upanga, kwa yanayopatikana humo miongoni mwa neema za kidunia na ukubwa, ambao ndiyo ndoto waliyokuwa wakiiota mara nyingi. Miongoni mwa matukio hayo ni: -

1. Baadhi ya Masahaba kumzuia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuandika wosia.

2. Baadhi ya Masahaba kukhalifu jeshi la Usamah na kukosoa kupewa kwake uongozi.

3. Matukio ya Saqifah na Bai’a ya Abubakr.

4. Ukhalifa wa ‘Umar na Bai’a yake.

5. Shura na Bai’a ya Uthman.

6. Tukio la Jamal na kutoka ‘Aishah.

7. Tukio la Siffin na uasi wa Mu’awiyah bin Abi Sufian.

8. Kufa Shahidi Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.).

9. Kufa shahidi kwa Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.).

10 Mapinduzi ya Karbala na kuawa shahidi kwa Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.).
Na katika yafuatayo tutayaelezea matukio haya kila moja kwa kirefu:-

Kwanza- Baadhi Ya Masahaba Kumkataza Mtume Wa Allah (S.A.W.W.)

Kuandika Wosia

Mtume alipotaka kuandika wosia mbele ya Masahaba wakubwa akiwa katika hali ya mwisho ya uhai wake, na kuzidiwa na maradhi, baadhi yao walimtuhumu kwa neno ambalo lilizua zogo kubwa, na Mtume akakasirika kwa athari yake, hivyo akawafukuza katika majilisi yake na akaacha kuandika wosia. Tukio hili lilitokea siku ya Alhamisi, kabla ya kufa kwake kwa siku chache, na tukio hili limejulikana kama; ‘Huzuni ya siku ya Al-hamisi’. Kama yanavyo dhihirika hayo katika Hadith zifuatazo:-

Amesema Ibn ‘Abbas: “Siku ya Al-khamisi, ni ipi siku ya Al-khamisi, Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alizidiwa na maumivu akasema: ‘Njooni nikuandikieni wosia, hamtapotea kamwe baada yangu’, wakazozana, na haifai kuzozona mbele ya Nabii, wakasema: “Ana nini? Anaweweseka?” Wakataka kumwuliza, basi wakampinga: Akasema: “Niacheni kwani ambayo niko nayo ni bora kuliko hayo mnayoniitia”38

Ibn ‘Abbas amesema: ‘Alipozidiwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na katika nyumba (yake) kuna wanaume, Nabii akasema: “Njooni nikuandikieni wosia hamtapotea kamwe baada yake”; Baadhi yao wakasema: “Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amezidiwa na maumivu, na mnayo Qur’an, na kinatutosha Kitabu cha Allah (s.w.t.). Walio kuwepo walikhitalafiana na kuzozana, baadhi yao wakasema karibieni akuandikieni, na baadhi yao wakasema yasiokuwa hayo. Walipozidi kukhitalifiana, Mtume wa Allah (s.a.w.w.) Akasema: “Ondokeni.” ‘Ubaidullah akasema: Ibn ‘Abbas alikuwa akisema, “Hakika huzuni iliyo kubwa kabisa ni ile ambayo ilitokea baina ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na kuwaandikia wosia huo kwa kule kuhitalifiana kwao na kupaza kwao sauti zao’.39

Kutoka kwa Ibn ‘Abbas Amesema: ‘Alipozidiwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na katika nyumba kuna wanaume kati yao ni ‘Umar bin Al-Khattab, Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) akasema njooni nikuandikieni maandiko hamtapotea baada yake,” ‘Umar akasema, “Hakika Nabii amezidiwa na mnayo Qur’an.

Kinatutosha Kitabu cha Allah (s.w.t.); walio kuwepo wakakhitalifiana na kuzozana kati yao, kuna wanao sema sogeeni Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) awaandikie maandiko hamtapotea baada yake na kati yao kuna wanaosema aliyo sema ‘Umar, walipozidi kuzozana na kukhitalafiana mbele ya Nabii, Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akasema: “Ondokeeni.”

‘Ubaidullah akasema: Na Ibn ‘Abbas alikuwa akisema: “Hakika huzuni kubwa kabisa ni ile iliyotokea baina ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na baina ya kuwaandikia maandiko hayo kutokana na Ikhtilaf yao na mzozo wao.”40

Na katika Sahih Muslim majibu yao yalikuwa: ‘Wakasema: “Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anaweweseka.”41 Ibara hii ya mwisho ambayo inamtuhumu Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kwa sifa ambayo inagusa Uma’asum wake na utukufu wake, inafahamika wazi kwamba wasemaji wake wanataka kuwazuia Waislamu wasiandikiwe mandiko na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na kutaja jina la khalifa wake wazi wazi, isije ikazuia wenye tamaa kufanya mikakati na kubadilisha mwelekeo wa ukhalifa wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ili upitie wanakotaka wao. Abubakr Ahmad bin Abdul-azizi Al-Jauhari amejaribu katika Kitabu chake As-Saqifah kuficha jambo hili akasema: “Basi ‘Umar akasema neno ambalo maana yake ni kwamba maumivu yamemzidia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kisha akasema tuna Qur’an Kitabu cha Allah (s.w.t.)’.42

Ni wazi neno “Yahjur, (anaweweseka) halina maana ya “Yatawajaa” (anaumwa) ambalo ametaka huyu aliyechelewa kulibadilisha, ili kuficha ubaya wa neno la kwanza kwa Nabii.

Na kila anayefikiria katika Hadith hizi anapata yakini kuwa wa kwanza kusema: “Yahjuru Rasulu Ilahi siku hiyo ni ‘Umar bin Al-Khattab kisha likasambaa kwa waliokuwepo ambao walikuwa na rai kama yake, na kwa sababu hiyo Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akakasirika na kuwafukuza kwa kuwaambia: “Niondokeeni”.

Na ukifikiria katika kauli ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.): ‘Njooni nikuandikieni maandiko hamtapotea kamwe baada yake,’ na kauli yake katika Hadith ya Thaqalain- ‘Hakika mimi nimekuachieni vitu viwili vilivyo vizito miongoni mwenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea,- Kitabu cha Allah (s.w.t.) na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu,43 unajua kuwa lengo la Hadith mbili hizi ni moja, ambapo Mtume katika maradhi yake alitaka kuwaandikia ufafanuzi wa aliyoyafanya kuwa ni wajibu kwao katika Hadith ya Thaqalain.

Lakini akaacha kuandika baada ya neno lao hilo ambalo walimshtusha kwalo na ambalo lilimlazimisha kuacha ili baadhi yao wasifungue mlango katika kumtuhumu Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) – ambapo haikubakia athari ya kuandika maandiko isipokuwa fitina na Ikhtilaf baada yake, ya kwamba je, aliweweseka katika aliyoyaandika? Allah (s.w.t.) atuepushe mbali - au hakuweweseka, kama walivyo khitalifiana katika hilo mbele yake, kama ilivyodhihirika katika Hadith zilizotangulia, ambapo wao walitosheka kwa waliyo nayo miongoni mwa Qur’an na wakajawazisha wenyewe kuacha maneno ya Nabii naye yuko katika hali ya maradhi, kana kwamba wamesahau aliyoyasema Allah (s.w.t.) juu ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.)

وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ {3}

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ {4}

عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ {5}

“Hasemi kwa matamanio yake isipokuwa wahyi unaofunuliwa, amemfundisha Mwenye nguvu sana, (An-Najm 53:3-5)

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ{7}

Aliyo kuleteeni Mtume yachukueni na aliyokukatazeni yaacheni” (Al-Hashr 59:7)

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ {19}

ذِي قُوَّةٍ عِنْدَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ {20}

مُطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ {21}

وَمَا صَاحِبُكُمْ بِمَجْنُونٍ {22}

“Hakika hiyo ni kauli ya Mjumbe Mtukufu mwenye nguvu, mwenye cheo cha heshima kwa Allah (s.w.t.), anayetiiwa huko (mbinguni na malaika wenzake). Kisha mwaminifu na Mtume wenu sio kichaa” (At-Tak’wiyr; 81:19:22)

Ibn ‘Abbas ameueleza msimamo huo kwa maelezo mazuri aliposema: “Hakika ni huzuni kubwa kabisa iliyo tokea baina ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na baina ya kuandika usia kwa sababu ya khitilafu yao na sauti zao,” yote hayo yalitokea mbele ya Mtume, sasa ni mangapi yatatokea kwa kuondoka kwake na baada ya kufa kwake?

Pili- Baadhi Ya Masahaba Kukhalifu Jeshi La Usamah Na Kukosoa Kupewa Kwake Uongozi

Ni maarufu kwa Waislamu wote kwamba Mtume aliandaa sariya (kikosi) kwenda kupigana Roma na akampa uongozi Usamah bin Zaid, naye ni kijana wa miaka kumi na saba, na hiyo ni sariya ya mwisho katika zama za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na hakubaki yeyote katika wakuu wa Muharjirin na Ansar, kama vile Abubakr, ‘Umar, Abu ‘Ubaidah, Sa’ad na mfano wao isipokuwa aliwaingiza katika jeshi”44 Na kuna ijma’ juu ya uhakika huu, na kwa watu wa sira na historia ni jambo la kawaida.

Akamwamuru ‘Usamah kuondoka lakini waliona uzito kwa hilo na baadhi yao wakatuhumu kufanywa kwake kiongozi mpaka Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) akakasirika sana kwa kutuhumu kwao, akatoka akiwa amefunga kitambaa kichwani (kwa maumivu), na hiyo ilikuwa ni wakati wa maradhi yake, na kabla ya kufariki kwake kwa muda wa siku mbili, akapanda mimbar na akasema; kama alivyopokea Bukhari kwa isnad yake kutoka kwa ‘Umar.

Kutoka kwa Ibn ‘Umar amesema: “Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimwamuru ‘Usamah kuongoza watu basi wakatuhumu katika uongozi wake. Mtume akasema: ‘Kama mtatuhumu katika uongozi wake, basi mlikwisha tuhumu katika uongozi baba yake, naapa Wallahi hakika alikuwa ni katika watu wanaopendeza sana kwangu, na hakika huyu ni katika watu ninaowapenda sana baada yake”45 Kisha akawahimiza kuondoka naye na kufanya haraka, isipokuwa walizembea kwa mara nyingine na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alifariki kabla hawajaanza kuondoka. Katika tukio hili tunajifunza yafuatayo:-

1. Ijtihadi ya baadhi ya Masahaba katika kauli ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ambapo walipinga uteuzi wa Usamah kuwa kiongozi wao kutokana na umri wake mdogo, pamoja na kuwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alikabidhi bendera yake kwake. Tukilifahamu hili basi haitakuwa vigumu kwetu kufahamu namna na sababu katika ijtihadi yao mbele ya kauli ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) katika mambo makubwa zaidi, kama vile kumteua Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kuwa Khalifa na Uimamu wake.

2. Hakika Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kumfanya Usamah kuwa kiongozi wao naye ni kijana wa miaka kumi na saba tu, amelifanya hilo ili iwe funzo la kivitendo katika kukubali uongozi wa ambaye ni mdogo kuliko wao kiumri na hivyo Mtume alidhihirisha ghadhabu yake walipo tuhumu huo uongozi wa Usamah.

3. Mtume alipompa Usamah bendera alikuwa anajua kwamba wakati wa kwenda kwa Mola wake umeshakaribia, na bila shaka alikuwa anafikiria yale yatakayotokea baada yake katika kugombania ukhalifa. Hekima yake kubwa ya kuwaweka wakuu wa Muhajirin na Ansar katika sariya hiyo ambayo aliiamuru kuondoka kabla ya kufa kwa siku chache, ni ili pasiwe na nafasi ya kugombania uongozi, tukiachilia mbali kufanyika kwa ijtihadi.

Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa anaandamana na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) muda wote huo, na wala hakuachana naye hata mara moja wakati wa maradhi yake, na baada ya kufariki kwake alishughulika na kumwosha, na Muhajirin na Ansar wakaenda kugombania uongozi katika Saqifah ya Bani Sa’ada baada ya kuona uzito wa kwenda katika jeshi la Usamah ambalo wao walikuwa ni askari wake, na hivyo ndivyo ilivyokuwa ijtihadi yao kwa kuogopa yatakayotokea baada ya kufariki Mtume wa Allah (s.a.w.w.) katika hali ya kutokuwepo kwao.

Tatu -Matukio Ya Saqifah Na Bay’ia Ya Abubakr

Katika wakati ambao Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) pamoja na aliokuwa nao wanashughulika na mazishi ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), ‘Umar alikuwa anatangaza kupinga kwake kufariki kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na anatishia kumuua kila anayesema hilo, na wala hakuwa anaamini kufariki kwa Mtume mpaka aliporejea Abubakr kutoka sehemu iliyo nje ya Madina inayoitwa Al-Sunh, kama ilivyo pokewa kutoka kwa ‘Aisha (r.a.):
“Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alifariki na Abubakr yuko (sehemu iitwayo) Sun’hi.” Isma’il akasema: ‘Akimaanisha (Aisha sehemu iitwayo) Aliyah.’

Basi ‘Umar alisimama na akasema: “Naapa Wallahi kuwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) hakufariki. Wallahi sikuwa nawaza moyoni mwangu isipokuwa hilo na Allah (s.w.t.) atamfufua, na atakata mikono na miguu ya wanaume.”

Akaja Abubakr akamfunua Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akambusu na akasema: “Kwa Baba yangu na mama yangu, ulikuwa mwema wakati ulipokuwa hai na ukiwa maiti, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, Allah (s.w.t.) hatakufisha mara mbili, kisha akatoka na akasema: ‘Ewe mwenye kuapa tulizana.’46

Lakini Ansar walikwisha jikusanya katika Saqifah ya Bani Sa’ada na wakampendekeza Sa’ad bin ‘Ubadah ili awe khalifa wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na wakuu wa Muhajirin (Abubakr, ‘Umar na Abu ‘Ubaidah) walipojua hilo waliwaendea haraka, na wakatangaza kuwa wao wana haki zaidi katika jambo hilo.

Pakatokea mjadala baina ya Muhajirin na Ansar, mjadala na mzozo ukazidi, akasimama kiongozi wa Ansar Sa’ad bin ‘Ubadah kisha akasema: ‘Amma baad, sisi ni Ansar wa Allah (s.w.t.) na Jeshi la Kiislamu na nyinyi Muhajirin ni kundi, na lilikuja kundi katika kaumu yenu, hivyo wakawa wanataka kutung’oa katika asili yetu na kutupakata katika jambo (hili).’47

Abubakr akasimama na akatoa hutoba, akataja humo fadhail za Muhajirin na akatoa hoja ya Uquraish wao katika kustahiki kwao ukhalifa. Abubakr, ‘Umar Al-Khattab na Abu ‘Ubaidah bin Al-Jarah wakawaendea. ‘Umar akawa anazungumza, Abubakr akamnyamazisha48 Abubakr akasema: ‘Hapana, lakini sisi ni viongozi na nyinyi ni mawaziri, wao (Maquraish) ni Waarabu wa nyumba ya kati na ni ukoo bora.49 Nimewaridhia mmoja kati ya hawa wanaume wawili50 mpeni bay’ia ‘Umar Al-Khattab au Abu ‘Ubaidah bin Al-Jarah.’51

Mmoja wa wakuu wa Ansar akajibu, naye ni Habab bin Al-Mundhar, akasema: ‘Hapana hatufanyi kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi.’52

Na jibu la Ansar lilikuwa katika Hadith nyingine: “akasema msemaji wa Ansar: ‘Mimi ni asili yake isiyo tingishika na tawi lake lenye nguvu, kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi enyi Maquraish.’ Fujo ikazidi na kelele zikawa nyingi mpaka nikaudhika kutokana na Ikhtilaf’.53

Hali ilipokuwa mbaya kiasi hiki, ikaja duru ya ‘Umar Al-Khatib akasema: ‘Haiwezekani kuingia panga mbili katika ala moja, Wallahi Waarabu hawaridhii kuwafanya nyinyi viongozi na Nabii wake hajatoka kwenu na sisi tuna hoja juu ya hilo kwa anayekataa.’ Habab bin Al-Mudhir akamjibu kwa kusema:’

Enyi Ansar shikamaneni na jambo lenu na wala msisikie maneno ya huyu na wenzake, kwani ninyi mna haki zaidi na jambo hili kuliko wao’.

Lakini safari hii Ansar waligawanyika, ‘Usaid bin Hudhair kiongozi wa Aus ambaye alikuwa mpinzani wa Sa’ad bin ‘‘Ubadah, kiongozi wa Khazraji akatangaza kuwaunga kwake mkono Muhajirin na akaahidi kuwapa bay’ia. Basi ‘Umar alisimama akamwambia Abubakr: ‘Nyoosha mkono nikupe bay’ia’. ‘Umar akamba’yi na baadhi ya Muhajirin’.

Ansar, kama alivyopokea Bukhari kwa isnad yake kutoka kwa ‘Aisha kwamba ‘Umar alichukua bay’ia kwa Abubakr kwa kuwatishia na kuwaogopesha.

‘Aisha amesema: ‘basi haikuwa hotuba yao miongoni mwa hutoba isipokuwa Allah (s.w.t.) aliwanufaisha kwayo, kwani ‘Umar aliwatisha watu na kulikuwa na unafiki kwao, basi Allah (s.w.t.) akawajibu kwa hilo’.54

‘Umar alimwambia kiongozi wa Ansar Sa’ad bin ‘Ubadah ambaye alikataa kubay’i: “Tulimrukia Sa’ad bin ‘Ubadah”, basi akasema msemaji miongoni mwao:’ Mnamuua Sa’ad bin ‘Ubaadah’ ‘Umar akasema:’Allah (s.w.t) amuue’55

Mpaka hapa tunafunga pazia la maigizo ya matukio ya Saqifah ambayo yalimalizika kwa kumbay’i Abubakr baada ya ugomvi ulio shuhudiwa baina ya Muhajirin na Ansar juu ya ukhalifa, na ‘Umar Al-Khattab amekiri kwamba bay’a ya Abubakr ilikuwa ya ghafla, lakini - kwa rai yake - Allah (s.w.t.) ameepusha shari. “Basi asidanganyike mtu kusema kwamba bay’ia ya Abubakr ilikuwa ghafla na ikatimia, ndiyo ilikuwa hivyo kweli, lakini Allah (s.w.t.) ameepusha shari yake.”56

Na wote wanajua kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na wengine katika Bani Hashim na wengineo katika Masahaba mfano Zuber, Twalha, ‘Ammar, Salman, Miqdad, Abu Dhar, Khuzaima dhi-Shahadatain, Khalid bin Sa’ad, ‘Ubay bin Ka’ab, Abu Ayyub Ansari na wengineo - hawakushuhudia bay’ia hiyo, wala hawakuingia Saqifah siku hiyo kwa sababu wao walikuwa wanashughulika na tukio kubwa la kifo cha Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na kufanya wajibu wa kuandaa mazishi yake na kuzika mwili wake mtukufu kwenye kaburi lake.

Watu wa Saqifah walimpa Abubakr bay’ia, hivyo hapakuwa na njia kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) pamoja na aliokuwa nao isipokuwa kukataa kumbay’i kama yanavyo dhihirika hayo katika maneno ya ‘Umar: “Allah (s.w.t.) alipomfisha Nabii wake tulikuwa tuna habari, isipokuwa Ansar walikhalifu na wakakusanyika katika Saqifah ya Bani Sa’adah, na akatukhalifu sisi ‘Ali, Zubeir na waliokuwa pamoja nao”57

Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) hakuona athari ya kujadiliana isipokuwa ni fitina ambayo aliona ni bora kupoteza haki yake kuliko kuipata katika hali hiyo, kwa sababu ya fitina mbaya ambayo iliuzunguka Uislamu kwa kila upande.

Hatari ya wanafiki na wale walio pembezoni mwake miongoni mwa mabedui waliobobea katika unafiki - kama zilivyosema Ayah za Qur’an - na nguvu zao ziliongezeka kwa kuondoka Mtume, ukiongozea hatari ya Musailamah al-Kadh-dhaab, Twaliyhat bin khuwailid mwongo, Sajaah Ad-Dajalah, Warumi, Kisra, Qaisar na wengineo miongoni mwa wanao watakia shari Waislamu. Na hatari nyingine zisizokuwa hizo zilizokuwa zinautishia Uislamu na kubaki kwake, hivyo ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kutoa muhanga haki yake, lakini bila ya kufuta hoja zake katika ukhalifa.

Alitaka kuhifadhi haki yake katika ukhalifa na kumjadili aliyefanya jitihadi humo kwa njia ambayo haitaleta fitina itakayowapa mwanya maadui wa Uislamu. Alibaki nyumbani kwake na akakataa kumbay’i yeye pamoja na aliokuwa nao kwa muda wa miezi sita, na alipoona kumbay’i ni kuepukana na fitina alituma ujumbe kwa Abubakr.58 “Njoo na wala asije yeyote pamoja nawe” kwa kuchukia asije akahudhuria ‘Umar.

Na kama angefanya haraka kumbay’i isingetimia hoja yake wala wafuasi wake wasingepata hoja, lakini kwa aliyoyafanya alikusanya baina ya kuhifadhi dini na kuhifadhi haki yake ya Ukhalifa kwa Waislamu; wakati huo hali haikuruhusu kupigana kwa upanga wala kushinda kwa hoja, na ukweli unadhihirika wazi alipojaribu Abu Sufian kumwendea Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) zaidi ya mara moja alimhimiza kushikilia haki yake ya ukhalifa kwa kusema: “Ukitaka, tutakupa farasi na watu wa kupigana nao na nitawanyima wao katika sehemu yao”.59

Lakini Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikataa aina hii ya msaada mara zote kwa sababu alikuwa anajua kuwa makusudio ya Abu Sufian ni kuchochea cheche ya fitina na kuanzisha vita ambavyo Uislamu hautasimama tena baada ya hapo.

Hasira (Ghadhabu) Ya Bibi Fatimah Az-Zahra (A.S.)

Bi Fatimah az-Zahra (a.s.) alifariki akiwa na hasira juu ya Abubakr, kwa sababu ya kumkataza mirathi yake kutoka kwa Mtume. “Hakika Bi Fatimah az-Zahra (a.s.) binti wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimtaka Abubakr baada ya kufariki Mtume wa Allah (s.a.w.w.), amgawie mirathi yake katika alioyaacha Mtume wa Allah (s.a.w.w.) katika aliyo mpa Allah (s.w.t.). Abubakr akamwambia: ‘Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema: “Haturithiwi, bali tuliyoyaacha ni sadaka”.

Binti wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akakasirika na akamhama Abubakr na hakuacha kufanya hivyo mpaka akafariki, na aliishi miezi sita baada ya kufariki Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Alikuwa anamwomba Abubakr fungu lake kati ya aliyo yaacha Mtume wa Allah (s.a.w.w.) miongoni mwa mali ya Khaibar, Fadak na sadaka zake za Madina, Abubakr akamkatalia na akasema, si kuwa ni mwenye kuacha kitu alicho kifanya Mtume wa Allah (s.a.w.w.).60

Na hasira yake kwa Abubakr ilikuwa kubwa kiasi ilimfanya amuusie Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kuwa Abubakr asimsalie wala kusindikiza jeneza lake, na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alizika mwili wake kwa siri usiku. Bukhari amesema katika Kitabul-Maghazi “Abubakr alikataa kumpa kitu chochote, basi akamkasirikia Abubakr kwa ajili hiyo na akamhama na hakumsemesha mpaka akafariki, na ameishi miezi sita baada ya kufariki Nabii, na alipofariki, mume wake Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alimsalia na akamzika usiku na hakumruhusu Abubakr kumsalia”.61

Ardhi hiyo ya Fadak ni kijiji katika Hijaz walikuwa wakiishi humo wAyahudi, na Mtume (s.a.w.w.) alipoiteka Khaibar, Allah (s.w.t.) alitia hofu katika nyoyo zao wakafanya suluhu na Mtume kwa kumpa Fadak. Ikawa ni miliki ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa sababu ni katika vitu ambavyo havikupatikana kwa vita si kwa wapanda farasi wala kwa wanaokwenda kwa miguu, kisha akampa binti yake Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) Tukiongezea yale aliyo miliki Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) katika mali ya khums ya Khaibar na sadaka za Nabii haya yote yalikuwa ni milki ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) khasa, na hakuna yeyote mwenye haki isipokuwa yeye.

Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) alikuwa - kulingana na rai ya Abubakr - ametaka asiyokuwa na haki nayo, hivyo ni moja kati ya mambo mawili wala hakuna la tatu, ima alikuwa ni jahili hajui hukumu ya mirathi ya Nabii au alikuwa mwongo ana tamaa ya kuchukua kisichokuwa haki yake. Mambo yote mawili ni mustahili kwa Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) ambaye Allah (s.w.t.) alikuwa akikasirika kwa hasira yake, naye ni bibi wa wanawake waumini wa peponi, na Allah (s.w.t.) amemtakasa kutokana na kila dhambi na uchafu kama ilivyotangulia, na ambaye Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema juu yake ni “Kipande (cha nyama) kinachotokana na mimi basi atakaemkasirisha amenikasirisha.”62

Na amemwambia: “Ewe Fatmah je, huridhii kuwa ni bora wa wanawake wa ‘Ummah huu?”63 Vile vile amesema “Ni bibi wa wanawake wa watu wa peponi”.64 Na hata kama tukisema Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) alikuwa ni kama wanawake wengine na wala hana sifa zote hizo kama ilivyo katika Hadith hapo juu - basi kuwa kwake binti wa mwalimu wa binadamu na mke wa Amirul-Mu’uminiina Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ambaye wameshuhudia kuwa ni hakimu wao yaani mjuzi wao, zinapinga dhana yeyote ya kuwa mjinga, hiyo ni kwa sababu kama Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) alikuwa ametaka haki isiyokuwa yake - kama alivyoona Abubakr na kwamba Mitume (a.s.) hawarithiwi, basi yeyote kati ya baba yake na mume wake angekuwa ni bora zaidi kumfahamisha hayo, ilihali mume wake Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ndiyo hakimu wao kwa kutambua hayo, angemkataza kutaka mirathi hiyo kama isingekuwa ni haki yake.

Lakini tusijaalie hivyo na tunajilinda kwa Allah (s.w.t.) kuwa hivyo, kwani ilipomfikia habari ya kuwa Abubakr amekataza haki yake katika Fadak, na mali nyingine aliompa Allah (s.w.t.) baba yake Madina, na khums ya Khaibar, alimwendea akiwa na kundi la Muhajirin na Ansar na akawahutubia hotuba iliyo waliza watu. Na katika jumla ya aliyo yasema (bi. Fatimah) ni haya: “...na ninyi sasa mnadai kwamba hatuna mirathi wala cheo, je wanataka hukumu ya kijahili, je nani ni mbora wa kuhukumu kuliko Allah (s.w.t.) kwa watu wenye yakini.

Ole wenu enyi Waislamu, katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) unamrithi baba yako na mimi simrithi baba yangu? Hakika umeleta kitu kibaya kabisa, kisha akawasomea Ayah “Muhammad hakuwa isipokuwa ni mtume na walishapita kabla yake mitume, je, akifa au akiuliwa mtarudi kwenye ukafiri? na atakae rudi kwenye ukafiri basi hamdhuru Allah (s.w.t.) chochote na Allah (s.w.t.) atawalipa wenye kushukuru. Enyi watu! Nadhulumiwa mirathi ya baba yangu na ninyi mnaniona na kunisikia...? Hadi mwisho wa hotuba hiyo.65

Hakika maana ya kauli ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) “Haturithiwi” haina maana ya kuzuia hukumu ya mirathi katika mali ya Manabii na milki zao za kidunia kama alivyofanya ijtihad Abubakr - kwani Nabii Suleiman alimrithi Daud kama inavyosema Qur’an juu ya hilo katika kauli yake Allah (s.w.t.) Mtukufu:

وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ ۖ{16}

“Na akamrithi Suleiman Daud.”(An-Naml 27:16)

يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ ۖ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا {6}

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَلْ لَهُ مِنْ قَبْلُ سَمِيًّا {7}

“Anirithi mimi na arithi watu wa Yaaqubu na mjaalie ewe Mola awe ni mwenye kuridhiwa,ewe Zakaria, hakika sisi tunakubashiria mtoto jina lake ni Yahya.
(Maryam 19: 6-7)

Na maana ya anirithi katika Ayah iliyotangulia haina maana ya kurithi Unabii kwa Sababu Unabii sio wa kurithiana hivyo maana ya kauli ya Mtume-haturithiwi - tukifaradhisha kuwepo kwake ni kwamba Manabii hawatakusanya au kulimbikiza dhahabu na fedha ili iwe ni mirathi baada yao kama wanavyofanya wale wanaotaka dunia.

Tanbih

Hakuna budi kueleza jambo muhimu nalo ni kwamba Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kuacha kumbay’i Abubakr ilikuwa ni kwa sababu ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kumuusia Uimamu na Ukhalifa na sio kwa sababu ya Abubakr kumkataza Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) mirathi yake, kama ambavyo wengine wanavyosingizia kuacha kwake hilo, vinginevyo ni sababu ipi iliyofanya kundi la Masahaba wakubwa kukataa kumbay’i vile vile, na hali walisha mfuata Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), na nini maana ya kauli ya ‘Aisha - kama ilivyo tangulia hapo mwanzo.

Ni kuchukia kuhudhuria kwa ‘Umar? ‘Umar hakuingilia chochote katika hitilafu ya mas’ala ya mirathi ya Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) wakati ambapo tumeona namna gani alikuwa na nafasi muhimu katika maslahi ya Abubakr tukiachilia mbali kuwa mas’ala ya mirathi hayawezi kuchukuliwa kuwa ni kipingamizi cha Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kutompa bai’a Abubakr isipokuwa kama ataona kwamba yeye sio Khalifa wa kisheria, na kama si hivyo ingekuwa ni wajibu kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kubay’i mara moja bila ya kuacha hata kwa siku moja, sasa itakuwaje kama ataacha kwa muda wa miezi sita?

Je, Mtume Muhammad Mustafa (S.A.W.W.) Alidokeza Juu Ya Abubakr Kupewa Ukhalifa?

Baadhi ya watu wanatoa hoja juu ya haki ya Abubakr kuwa Khalifa, na kudokezewa na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) juu ya suala hilo, katika Hadith aliyopokea Ibnul-Jauzi kwa Isnad yake kutoka kwa ‘Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) amesema: “Alipofariki Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na alikwisha mtanguliza Abubakr katika sala basi tukaridhia kwa dunia yetu kwa aliyeridhiwa na Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa ajili ya dini yetu, hivyo tukamtanguliza Abubakr.”66

Hadith hii ina uongo uliowazi ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ambaye wanadai amepokea Hadith hii ndiye aliye mkhalifu Abubakr, na hakumbay’i isipokuwa baada ya miezi sita, na walishamfuata katika kukhalifu Masahaba wakubwa - kama ilivyotangulia - na tukikadiria usahihi wa Hadith hii basi inalazimu Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) awe ndiyo wa kwanza kubay’i.

Lakini riwayah inapingana kabisa na hotuba maarufu za ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ambazo ziko wazi juu ya malalamiko ya Ukhalifu wa Abubakr na kuunyakua kwake. Kwa kuongezea kukhalifu kwa ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kumbay’i Abubakr ambako peke yake kunatosha kutengua Hadith hiyo, hapa kuna dalili nyingine zinazotilia mkazo uongo wa Hadith hiyo:-

a.) Jeshi la ‘Usamah bin Zaid ambalo Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimkabidhi bendera mikononi mwake na akawahimiza Masahaba kuondoka naye yuko katika pumzi za mwisho katika umri wake mtukufu, na walikuwepo katika sariya hiyo wakubwa wa Muhajirin mfano, Abubakr, ‘Umar na Abu ‘Ubaidah - kama Mtume angetaka kumfanya Abubakr kuwa Khalifa asingemweka katika sariya hiyo.

b.) Kama Hadith ya juu ingekuwa sahihi basi Abubakr angeitolea hoja mwenyewe siku ya Saqifa kwa walio mkhalifu, wakati ambapo alikuwa na haja sana ya hoja ili kumaliza ugomvi, lakini siku hiyo tulimwona anatoa hoja kwamba kabila la Maquraish ni bora zaidi kama ilivyo tangulia.

c.) Na juu ya yote hayo riwayah hii inatenguliwa na riwayah zenye nguvu zilizo thabiti katika Ukhalifa wa ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) hivyo rejea tuliyonukuu juu ya hilo katika kurasa zilizo tangulia.

Je, Bi.Fatimah Az-Zahra (A.S.) Alikufa Kifo Cha Kijahiliyyah (Kikafiri)?

Hakika Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) alifariki dunia hali ya kuwa ni mwenye kukasirika juu ya Abubakr, na wala hakumbay’i na aliusia kuwa asimsalie wala asisindikize jeneza lake - tazama Hadith inayokuja chini inayoonyesha ushahidi wenye nguvu juu ya aina ya Uimamu (au amiri) ambaye ni wajibu kumtii na iliyo kusudiwa katika Hadith zinazofuata chini yake.

Binti wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikasirika akamhama Abubakr na hakuacha kuwa ni mwenye kumhama mpaka akafariki, na aliishi miezi sita baada ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kufariki dunia.67 Alipokufa mume wake alimsalia na alimzika usiku na hakumruhusu Abubakr kumsalia.68

Kutoka kwa Ibn ‘Abbas kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) amesema: “Atakayechukia jambo kwa kiongozi wake basi asubiri, kwani atakayetoka kwa kiongozi shubiri moja atakufa kifo cha kikafiri.”69

Na katika Sahih Muslim Atakaye kufa na hana Bay’ia katika shingo yake atakufa kifo cha kikafiri.70 Na katika Musnad Ahmad: Atakaye kufa bila ya Imam atakufa mauti ya kikafiri.71

Hivyo Imam (au amiri) aliyekusudiwa katika Hadith tatu za juu - Hadith hizo ambazo zinabainisha wajibu wa kumtii Imam na kwamba anayekufa bila ya kumbay’i mauti yake yatakuwa ya kikafiri bila shaka sio Abubakr. Kwa nini? kwa sababu kama Abubakr angekuwa ni khalifa na kufa kwa kumkhalifu maana yake ni mauti ya kikafiri, basi lisingetokea hilo kwa ambaye Waislamu wote wanaafikiana kuwa yeye ni bibi wa wanawake wa Jannat, na ambaye Nabii anakasirika kwa hasira yake ambayo bila shaka ina maana ya ghadhabu ya Allah (s.w.t.) kwa anaye mkasirikia kwa sababu Bi, Fatimah az-Zahra (a.s) yeyeni katika Ahlul-Bayt (a.s) ambao Allah (s.w.t) amewaondolea uchafu na akawatakasa kabisa.

Na ambapo Mtume wa Allah (s.a.w.w) amesema juu yake: “Ni pande langu atakaye mkasirisha amenikasirisha mimi.” 72 Bali amesema juu yake vile vile “Ni bibi wa wanawake wa watu wa peponi.”73

Tunasema Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.) mwenye vyeo hivi kwa Mtume na Waislamu hakufa - (Allah (s.w.t.) aepushe mbali) - mauti ya kikafiri, kwa sababu kwa kuchukia kwake msimamo wa Abubakr na muamala wake kwake, kwa kutoka kwake katika utawala wake sio shibiri moja tu bali maili nyingi, kwa kukataa kwake kumbay’i na kumkasirikia na akafariki akiwa katika hali hiyo na kuusia kwake kwamba asimsalie; (yote hayo) ni dalili tosha ya kuonyesha kuwa Abu bakr si miongoni mwa wale viongozi ambao kuwakhalifu kunamsababishia mtu kufa kifo cha kijahiliyyah.

Matokeo

Kwa hiyo Maimamu (viongozi) walio kusudiwa katika Hadith zilizotangulia ambao ni wajibu kuwatii sio aliowakhalifu kamwe Bi.Fatimah az-Zahra (a.s.). Ni nani basi hawa Maimamu (viongozi) ambao ni wajib kuwatii na kutowaba’i ni kuangamia?

Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikwisha jibu swali hili kwa kusema: Amesema: kutakuwa na viongozi kumi na wawili’.74 Na nyinginezo zilizo tangulia katika Hadith za Uimamu.

Nne: ‘Umar Kupewa Ukhalifa Na Bay’ia Yake

Abubakr aliposhikwa na maradhi alimwita ‘Uthman bin ‘Affan na akamwambia: “Andika kwa jina la Allah (s.w.t.) Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu, haya ni aliyoamua Abubakr bin Quhafah kwa Waislamu, ‘amma baad…”, Abubakr akazimia. ‘Uthman bin ‘Affan akaandika, ‘amma baad, mimi nimemfanya ‘Umar bin Al-Khattab kuwa Khalifa wenu na sikuwatawalisheni mtu mwema’, kisha Abubakr akazinduka, ‘Uthman akamsomea alivyoandika. Abubakar akasema: “Na kuona uliogopa watu kukhitalifiana kama ningekufa katika kuzimia kwangu.” akasema: ‘Ndiyo’, akasema: “Mungu akulipe kheri kwa ajili ya Uislamu na watu wake.” Abubakr akaafiki haya.75

Kama ilivyopokelewa kwamba ‘Umar alikuwa na karatasi ambayo humo Abubakr alimteua kuwa khalifa na alikuwa anawaambia watu sikilizeni na tiini kauli ya khalifa wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.), anasema kwamba: “Hakika mimi sikuwatawalishieni mtu mwema.”76

Na inabainika kwamba Abubakr alikuwa anaogopa hitilafu na watu kugombania ukhalifa baada yake na hivyo akauusia uwe kwa ‘Umar na akaandika katika karatasi ili iwe ni hoja kwa watu, na ili kusiwepo na nafasi ya kugombania.
Swali ambalo linajitokeza hapa ni, je, Mtume hakufikiria kama alivyofikiria Abubakr? Au hakuogopa Ikhtilaf na ugomvi katika ‘Ummah juu ya uongozi kama alivyoogopa Abubakr?

Na tofauti ilikuwa kiasi gani baina ya hali ya Waislamu wakati alipofariki Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na hali yao wakati wa kufariki Abubakr? Je, dhana ya kukhitilafiana na kufarakana baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) haikuwa ni kubwa zaidi wakati huo kuliko ule wa Abubakar? (na hiyo ni kwa sababu tulizozitaja mwanzo: hatari ya kuritadi wanafiki, Warumi waliokuwa wanasubiri kuwabadilisha Waislamu wakati watakapo pata fursa, tukiachilia mbali ugomvi wa kikabila baina ya Mabedui) Au Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) hakufahamu hatari zote hizi zinazosubiri Uislamu na watu wake kama alivyo fahamu Abubakr?

Hakika ni ajabu ya maajabu, pamoja na Hadith zote zilizothibiti za Mtume kumfanya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kuwa Khalifa - kama ilivyo tangulia - wote walipinga kwa hoja ya kuwa Mtume alifanya jambo la Ukhalifa liwe Shura baina ya Waislamu - rejea matukio ya Saqifa utaona ni kwa aina gani ya Shura ilitimia Bai’a ya Abubakr- na Abubakr anamfanya ‘Umar kuwa Khalifa wa Waislamu kwa kauli yake bila ya kumshauri yeyote katika Waislamu, iko wapi Shura wanayoidai?

Bila shaka watasingizia msimamo huu kuwa Abubakr ana haki ya kumteua yeyote
amtakae kati ya Waislamu anayeona kuwa anafaa kubeba jukumu la Ukhalifa, pamoja na kwamba alikuwa anaumwa sana wakati wa kuchukua uamuzi huo ambapo alizimia wakati wa kuandika kwake, halafu ‘Uthman akakamilisha badala yake. ‘Uthman ambaye alikuwa anajua kuaminiana kati ya makhalifa wawili, kwa sababu ‘Umar bin Al-Khattab alisimama msimamo mkali ulioshuhudiwa siku ya Saqifa katika kumsaidia Abubakr kupata ukhalifa. La ajabu na la kushangaza ni kwamba hakusema yeyote kati ya Masahaba kuwa Abubakr alikuwa anaweweseka wakati alipoandika wosia, kama ambavyo walimwambia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) neno hilo wakati alipowaamuru wamletee karatasi awaandikie ili wasipotee baada yake, na wakamkataza kuandika wosia wake katika karatasi ambapo ilikuwa inawezekana kumpa Ukhalifa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na kuwaonyesha ushahidi kama alivyoonyesha ‘Umar karatasi hiyo ambayo Abubakr alimwandikia kuwa khalifa.

Tano-Shura Na Bayi’a Ya ‘Uthman Bin ‘Affan.

‘Umar alipochomwa jambia, akaambiwa ungeteua khalifa, akasema: “kama Abu ‘Ubaidatil Jaraha angekuwa hai ningemteua kuwa khalifa na kama Salim mtumwa wa Abi Hudhaifah angekuwa hai ningemteua kuwa Khalifa, kisha akawaambia “Hakika watu wanasema kwamba Bai’a ya Abubakr ilikuwa ghafla, Allah (s.w.t.) ameepusha shari yake na Bai’a ya ‘Umar haikuwa Shura na Ukhalifa baada yangu ni Shura”.77

Kisha akasema nimefanya jambo lenu liwe Shura baina ya watu sita miongoni mwa Muhajirin wa mwanzo, ambapo aliwataja kwa kusema “Niitieni Al- Imam’Ali ibn Abi Talib (a.s.), ‘Uthman, Talha, Zubeir, ‘Abdurahman bin ‘Auf na Sa’ad bin Abi Waqqasi, kama wataafikiana wanne basi wawili wafuate rai ya wanne na kama wataafikiana watatu basi fuateni rai ya ‘‘Abdurahman bin Auf, sikilizeni na tiini...”78

Kutokana na riwayah ya hapo juu inadhihirika kwamba ‘Umar alijaalia jambo la kuteua mikononi mwa ‘Abdurahman bin Auf na hii ni aina ya tatu katika aina za Shura ambayo wanaisema ‘Umar alimwamuru ‘Abdurahman bin ‘Auf aweke sharti la kufuata mwendo wa Masheikh wawili Abubakr na ‘Umar katika bayi’a, tukiongeza kufuata Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.)

Kama alivyotarajia watu sita waligawanyika sehemu mbili na waliopendekezwa ni Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na ‘Uthman bin ‘‘Affan, na Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikataa kufuata mwendo wa masheikh wawili kwa kusema:

“Nitafuata Kitabu cha Allah (s.w.t.), Sunnah za Nabii wake na ijtihadi yangu,79ambapo ‘Uthman aliafiki sharti hilo, hivyo ukhalifa ukamwendea kwa sababu hiyo.

Bukhari ametoa katika Kitabu chake sehemu ya tukio hili kama inavyodhihirika katika Hadith ifuatayo: Akasema (Abdrahman): “Niitieni Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akamwita, akamnong’oneza mpaka usiku ukaingia. Kisha Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akatoka kwake akiwa ana matarajio, na ‘Abdurahman alikuwa anaogopa kitu (fulani) kwa Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kisha akasema: Niitieni ‘Uthman akamwita akamnong’oneza mpaka muadhini wa asubuhi aliwatenganisha, aliposalisha watu sala ya asubuhi na kundi hilo likakusanyika, walipokusanyika ‘Abdurahman akatoa shahada kisha akasema: Ama baad ewe ‘Ali ibn Abi Talib nimetazama jambo la watu sikuwaona kuwa wanamtaka mwingine isipokuwa ‘Uthman bin ‘Affan hivyo usiipe nafsi yako mwanya.

Akasema kumwambia ‘Uthman bin ‘Affan: Nakubay’i kwa kufuata Kitabu cha Allah (s.w.t.), Sunnah za Mtume na mwendo wa makhalifa wawili baada yake, Aburahman akambayii na watu wakambayii.”80

Kuuliwa Kwa ‘Uthman Bin ‘Affan

Maneno mengi yamesemwa kuhusu kuuliwa kwa ‘Uthman, na kauli na mapokezi yamegongana juu ya hilo, hasa kuhusu kundi ambalo lilikuwa linahimiza kuuliwa kwake na sababu ambazo zilikuwa zinawasukuma juu ya jambo hilo na matukio hayo kufikia malengo yake.

Lakini vyovyote mambo yatakavyokuwa, hakika ilikuwa ni kutokana na vitendo vinavyohusiana na utawala na kuteua magavana katika jamaa zake na kuwagawia mali kutoka kwenye hazina ya dola ndiko kulikozua lawama za wenye kufanya Thawrah (mapinduzi).

Na hapa tunanukuu rai ya Khalid bin Muhammad Khalid neno kwa neno, katika yanayohusiana na masuala haya. “Bali tunakaribia kushuku kuwa ‘Uthman alikuwa anafahamu kwamba wengi wa waliofurahi kuchaguliwa kwake kuwa Khalifa badala ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) karamallahu wajhahu... hakika walifanya hivyo kwa kutaka kuondokana na ugumu na ukata wa maisha ambavyo watu wamekuwa wakikabiliwa navyo kwa muda mrefu, na ambavyo vingeleta taabu upya kama Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) angechukua uongozi kwa msimamo wake madhubuti na uadilifu wake ulio makini.81

Hivyo matamanio ya kundi la jamaa zake katika Bani Umayyah yalichezea mwelekeo wa dola, pato lake na mali zake kwa ujumla. Abu Sufian aliingia kwake baada ya Bai’a na kumwambia: “Enyi Banu Umayyah udakeni kama mnavyo daka mpira, kwa yule ambaye Abu Sufian anaapa kwaye sikuacha kuwa natamani liwe kwenu, basi na liwe ni lenye kurithiwa na watoto wenu.82 Na katika mapokezi mengine udakeni kama mnavyodaka mpira kwani hakuna pepo wala moto.83

Yote hayo yamesababisha masahaba watukufu kupinga na kutofautiana kwao na ‘Uthman, kati ya hao ni Abudhar Al-Ghafaariy, ‘Abdallah bin Mas’ud na ‘Ammar bin Yasir ambao Khalifa aliwachukulia msimamo mkali kabisa.

Ama Abudhar alifukuzwa na kwenda katika jangwa la Rabadhah kwa kuadhibiwa na ‘Uthman, kwa Sababu ya kumpinga kwake Mu’awiyah bin Abi Sufian-gavana wa ‘Uthman huko Sham-kwa kulimbikiza kwake dhahabu na ufujaji wake katika hazina ya mali ya Waislamu.

“Nilipitia Rabadhah basi nikamkuta Abudhar nikamwambia: Nani aliyekuleta huku?” Akasema: “Nilikuwa Sham nikakhitalifiana na Mu’awiyah bin Abi Sufian katika wale wanao limbikiza dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allah (s.w.t.) - Mu’awiyah bin Abi Sufian akasema: ‘Imeteremka kwa Ahlul-Kitab’, na nikasema: Imeteremka kwetu na kwao, hivyo ndivyo ilivyokuwa baina yangu na yeye, na akamwandikia ‘Uthman akimlalamikia juu yangu.
‘Uthman akaniandikia: ‘Njoo Madina’, basi nikaja, watu wakanikusanyikia kama kwamba hawajawahi kuniona kabla ya hapo, nikamweleza hayo ‘Uthman, akaniambia ukitaka nyamaza kimya utakuwa karibu yangu. Hayo ndiyo yaliyonileta hapa, na kama wangeamrisha jeshi kwangu ningetii na kusikiliza”.84

Ama ‘‘Abdallah bin Masu’ud mtunza hazina wa Kufah alishavunjwa mbavu zake,85 baada ya kupigwa na kijana wa ‘Uthman, kama adhabu yake kwa kumpinga kwake Al-Walid bin ‘Uqbah bin Abi Muit - ndugu wa ‘Uthman kwa upande wa mama na gavana wake wa Kufah, aloiyechukua nafasi hiyo baada ya kuuzuliwa Sa’ad bin Abi Waqaas - kwa sababu ya kuchukua kwake mali katika Baitul-Maal bila ya kurudisha.

Ama ‘Ammar Yasir alipata mpasuko kutokana na pigo kali kutoka kwa kijana wa ‘Uthman kama adhabu yake kwa sababu ya kufanya kulingana na wosia wa Ibn Mas’ud ya kuwa amsalie na amzike bila ya khalifa kujua ili asimsalie.86

Na mengine mengi yasio kuwa hayo kati ya misimamo ambayo sababu yake ilikuwa ni vitendo vya jamaa wa ‘Uthman katika Bani Umayyah na kufuja kwao mali ya dola, na hasa Marwan bin Al-Hakam ambaye peke yake alichukua khums ya kutoka Afrika, na wala hakuna ajabu kwa hilo, kwani ngawira na mali zilikuwa zinabubujika katika hazina ya dola kama maji yanavyo bubujika, na hiyo ni kwa sababu ushindi ulifikia mbali sana wakati wa ‘Uthman.

Na ghadhabu ya ‘Aisha kwa ‘Uthman ilichangia kuzidi kwa Thawrah (mapinduzi) ya wenye kufanya Thawrah, na kunyanyuka sauti za wapinzani kutokana na kuhimiza kwake juu ya kuuliwa khalifa na kumtuhumu kwa kubadilisha Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kwa kusema “Muuweni Naathala (sanamu) hakika ameshakufuru87 na neno hili lilitoka katika kinywa cha ‘Aisha na kusambaa kwa watu kama vile unavyo sambaa moto katika nyasi kavu, wakakusanyika kwake watu wengi miongoni mwao ni watu wa Madina pamoja na watu ambao waliwasili kutoka Misri, Sham na Kufah na wakamwua.

Bai’a Ya Al-Imam ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.)

Baada ya kuuliwa ‘Uthman watu walimiminika kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) wakitaka kumbay’i wakamwambia: “Hakika huyu mtu ameshauliwa na ni lazima watu wawe na kiongozi na leo hatuoni anayestahiki jambo hili kuliko wewe na Bai’a ikatimia.”

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alipotaka kusimamisha uadilifu baina ya watu; kumfanya mnyonge awe sawa na mwenye nguvu, na wala kusiwe na tofauti baina yao, na kutekeleza adhabu alizo ziteremsha Allah (s.w.t.) katika Kitabu chake, baadhi yao wakampinga na wakawa wakaidi kwake. Wakaeneza fitina na wakaandaa jeshi, huku wakitangaza uasi na ukaidi kwa Khalifa wa Waislamu na Imam wao ambaye ni wajib kumtii na hiyo ilikuwa ni katika matukio mawili mabaya nayo ni Vita vya Jamal na Siffin.

Sita- Tukio La Jamal Na Kutoka Kwa ‘Aisha

‘Aisha alipojua kuuliwa kwa ‘Uthman na watu kumbay’i Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), alimwambia yule aliyempa habari; naye ni ‘Ubaidullah bin Kilab: “Wallahi natamani ningekufa, kama jambo litakuwa kwa sahibu yako, ole wako tazama unayoyasema!” ‘Ubaidullah akamwambia: “Nilivyokuambia ndivyo, Wallahi simjui yeyote aliye bora zaidi yake, basi ni kwa nini unachukia uongozi wake?” ‘Aisha akapiga kelele: “Nirejesheni, nirejesheni”, akaondoka kuelekea Madina huku akiwa anasema: “Wallahi ‘Uthman ameuliwa kwa dhulma, Wallahi nitalipiza kisasi kwa damu yake!” ‘Ubaidullah akamwambia: “Kwa nini? Wallahi wa kwanza kusema auliwe ni wewe, ulikuwa ukisema: muuweni sanamu ameshakufuru.” Akasema: “Wao walimwambia atubu kisha wakamuuwa, nilisema na wao walisema, na kauli yangu ya mwisho ni bora kuliko kauli ya mwanzo.”

Akaondoka kuelekea Makkah akateremka kwenye mlango wa Msikiti, watu wakakusanyika, akasema: “Enyi watu! Hakika ‘Uthman ameuliwa kwa dhulma Wallahi nitalipiza kisasi kwa ajili ya damu yake.”88

Ghadhabu za ‘Aisha ziliafikiana na ghadhabu za Talha na Zubeir. Baada ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kuwaondolea ugavana wa nchi za Yemen na Bahrain, basi wakatengua Bai’a yao kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), na wakaenda Makkah wakimhimiza ‘Aisha kwenda kumpiga vita Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), wakatoka na likaondoka pamoja nao jeshi kubwa chini ya uongozi wa ‘Aisha kuelekea Basra ambapo vilitokea vita vinavyo julikana kwa jina la Vita vya Jamal; na ushindi mkubwa ulikuwa upande wa jeshi la Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na humo akauliwa Talha na Zubeir na Waislamu elfu kumi na tatu, yote hayo ni kwa sababu ‘Aisha anataka kulipiza kisasi kwa waliomwuwa ‘Uthman kama alivyosingizia katika kutoka kwake, na ambao alidai kuwa waliingia katika jeshi la Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.).

Vyovyote mambo yatakavyokuwa je, isingekuwa ni bora kwake kuacha jambo hili kwa kiongozi? Yeye hilo la mhusu nini? ‘Uthman ni mtu katika Bani Umayyah na ‘Aisha ni katika Bani Tamim, isipokuwa kama kutoka kwake kuna sababu nyingine isiyokuwa hiyo! Mtume alishatoa habari juu ya fitina hii ambayo ilitokea kwa sababu ya kutoka ‘Aisha kwake:

Na bakieni katika nyumba zenu na wala....”(Al-Ahzaab 33:32)

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alisema alipohutubia akaashiria kwenye nyumba ya ‘Aisha akasema: “Hapa kutatokea fitina, akakariri mara tatu; kutatokea upembe wa Shetani.”89

Na aliyoyapokea ‘Ammar Yaasir yanaonyesha kuwa aliyemtii ‘Aisha kwa kutoka kwake dhidi ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) hayo yanahesabiwa kuwa ni katika kutomtii Allah (s.w.t.).

“Nilimsikia ‘Ammar anasema: “Hakika ‘Aisha alienda Basra Wallahi hakika yeye ni mke wa Mtume wenu katika dunia na akhera, lakini Allah (s.w.t.) amewapatia mtihani ili ajue mtamtii Allah (s.w.t.) au yeye (Aisha).”90

Na imeshajulikana kwa ‘Aisha gherah yake kubwa kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), kwani alikuwa hawezi hata kutaja jina lake. Amesema ‘Ubaidullah bin ‘‘Abdallah bin ‘Utbah kwamba ‘Aisha amesema: “Alipougua Mtume (s.a.w.w.) na akazidiwa na maradhi yake alitaka ruhusa kwa wake zake augulie katika nyumba yangu basi wakamruhusu Nabii akatoka akiwa baina ya wanaume wawili akikokota miguu yake ardhini, baina ya ‘Abbas na mwanamume mwingine.” ‘Ubaidullahi akasema:”Basi nikamweleza ‘‘Abdallah bin ‘Abbas akasema: “Je, unajua mwanamume mwingine ni nani?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: “Ni Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.)”91

Na huenda aliyo yasikia katika kauli ya Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuhusu yeye katika tukio la ‘Ifki’ yalikuwa ni sababu ya chuki na gherah hii.92

Kiongozi wa washairi Ahmad Shauqi ameelezea gherah ya ‘Aisha katika beti zifuatazo akimhutubia kwayo Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.):

“Ewe jabali, majabali yanashindwa uliyoyabeba, lawama ngapi amekutupia bibi wa Jamal, ni kulipiza kisasi kwa damu ya ‘Uthman kumemhuzunisha au ni wivu ambao huzuni yake bado haijakwisha?
Hiyo ni hila ambayo haikuwa akilini, hila za wanawake zinafanya majabali kuwa mepesi, hakika ‘Aisha ni mwanamke hata kama ametakaswa na kuepushwa na makosa, ameyatoa katika jinsia yake na umri wake ambao yatabaki milele miongoni mwa chuki yake”.

Uzushi Wa ‘‘Abdallah Bin Saba’

Tumetegemea katika tulioyanukuu miongoni mwa Hadith katika kuuliwa kwa Uthman na Vita vya Jamal Hadith zinazoaminiwa na zinazoafikiana na tukio na nyakati ambazo zimezunguka matukio haya mawili. Lakini pamoja na Hadith hizi, kuna Hadith za uongo amabazo ameziweka mpokezi mmoja, na kwake wamechukua waandishi na wana historia wote, aliezua Hadith zote hizo ni “SEIF BIN AMRU AT- TAMIMIY AL-BARJAMI AL-KUUFI. Aliyefariki mwaka 170 Hijriyyah. Huyu mpokezi ameweka uzushi wa uongo, shujaa wake ni ‘Abdallah bin Saba myahudi ambaye nasaba yake ni kutoka Sana’a Yemen, na muhtasari wa uongo huo ni:

Hakika mtu huyu mwongo ‘‘Abdallah bin Saba alidhihirisha Uislamu wake wakati wa ‘Uthman ili kuwahadaa Waislamu, basi akatembea katika miji ya Kiislamu Misri, Sham, Basra na Kufah akibashiri kurejea kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na kwamba Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ndiye wasii wake na kwamba ‘Uthman amenyang’anya haki ya wasii. Basi wakamwamini na likamfuata kundi miongoni mwa Masahaba wakubwa na Tabi’in mfano ‘Ammar bin Yaasir, Abu Dhar, Muhammad bin Hudhaifah na wengineo, na akaweza kuandaa jeshi kwa ajili ya kumwuwa ‘Uthman hadi wakamwua ndani ya nyumba yake.” hivi ndivyo anavyoorodhesha “SEIF BIN AMRU” matukio katika uzushi wake wa uongo mpaka anaishia katika Vita vya Jamal ambapo anaamuru na kuchochea vita, hivi ndivyo ilivyotokea Vita ya Jamal (kwa mujibu wa mzushi huyu).

Uzushi huu wa uongo ameuzua “SEIF BIN AMRU na kutoka kwake wamechukua wanahistoria wote, kisha kisa kikawa mashuhuri na kuenea katika vitabu vya tarekh tangu karne zote hadi leo, mpaka ikawa ni katika matukio mashuhuri ambayo hayaguswi na shaka. Na wamepita (na kukubaliana) waandishi wengi na wana historia wa mashariki na mustashiriqina, kwamba uongo huu ameuzua mpokezi mmoja peke yake, hana mshirika na kwamba mpokezi huyu ni mashuhuri kwa maulamaa wa Hadith waliotangulia kwa uongo anatuhumiwa kwa uzaindiki, Abu Daud amesema juu yake:
“Si chochote, mwongo.”

Na amesema Ibn ‘Abdil-Barri: “Seif ni mwenye kuachwa lakini tumetaja Hadith yake kwa ajili ya kujua”. Na Nisai amesema: “Ni dhaifu, Hadith zake ni zenye kuachwa sio mkweli wala sio mwaminifu”.

Na wamechukua (pokea) kutoka kwa huyu mpokezi: Tabari, Asaakir, na Ibn Abi Bakr na kutoka kwa Tabari wamechukua waandishi na wana historia wengine hadi leo hii, hivi ndivyo ulivyo enea uongo katika vitabu vya tarekh baada ya kupokea Tabari kutoka kwa Seif bin ‘Amru peke yake.

Ni maarufu kuwa Hadith za Ahad hazimaanishi isipokuwa dhana ya kielimu na wala hazimaanishi yakini, sasa itakuwaje ikiwa Hadith hii moja sio ya kweli bali ni mashuhuri kwa uongo wake na uzindiki wake, je Hadith yake itakubaliwa?

Namna gani itakubaliwa kuhukumiwa ‘Ummah mkubwa katika Waislamu kwa kuzingatia Hadith moja ya pweke (Ahad), na kuachwa Hadith mutawatir zilizo thibiti kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kinyume cha aliyo yasema yule mwongo Seif bin ‘Amru At-Tamimiy?

Hakika ni katika upuuzi wa kihistoria Ushi’a kunasibishwa na mtu mwongo naye ni ‘‘Abdallah bin Saba’ na kwamba yeye ndiye aliyesema juu ya wosia wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), pamoja na kuwepo Hadith zote hizo za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ambazo zimethibitisha kwamba Ushi’a haukuwa isipokuwa ni wa Muhammad wala si vinginevyo, rejea Hadith za Uimamu katika kurasa zilizo tangulia ili uone iko wapi nafasi ya ‘‘Abdallah bin Saba’. Je ‘‘Abdallah bin Saba’ ndiye aliyesema: “Nimewaachia Kitabu cha Allah (s.w.t.) na kizazi changu Ahlul-Bayt (a.s.)?”

Je, ‘‘Abdallah bin Saba’ ndiye aliyesema: “Baada yangu kutakuwa na Maimamu kumi na wawili?”
Je, ‘‘Abdallah bin Saba’ ndiye aliyesema: “Ambaye nilikuwa kiongozi wake basi Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni kiongozi wake?”

Na ni upuuzi wa namna gani tunakubali kwamba mwanamume wa kiyahudi amekuja kutoka Yemen na kutangaza Uislamu wake kwa unafiki kisha anafanya kazi zote hizo ambazo zinafikia kuongoza jeshi la Kiislamu dhidi ya baadhi ya Waislsmu bila ya yeyote kumjua? Je, uongozi wa Waislamu na Maimamu walikuwa katika ghafla ya kiasi hiki?
Hakuna shaka kuwa anayesema haya amepotea upotovu ulio wazi na orodha ifuatayo inabainisha msururu wa wapokezi ya uongo wa ‘Abdallah bin Saba’ kutoka kwa mzushi wake wa kwanza “Seif bin ‘Amru At-Tamimiy” hadi kwa wapokezi wake katika wale waliokuja baada yake.

 • 1. Sahih Muslim, Kitabul-fadhail, Babu fadhail ‘Ali j. 5 uk. 272 chapa ya Daru-sh-Sha’b katika sherehe ya An-Nawawi.
 • 2. Sahih At-Tirmidhi J. 2 UK. 308 na Mustadraku-s-Sahihain na Musnad Ahmad.
 • 3. Sahih Muslim, kitabu-l- fadhail, Babu fadhailil-Hasan wal-Husayn j. 5 uk. 287 chapa ya Daru-sh- Sha’b.
 • 4. SahihiSahih At-Tirmidhi j. 2 uk. 209, Mustadrak As- Sahihain j. 2 uk. 416.
 • 5. Musnad Ahmad j. 6 uk 306.
 • 6. Mustadrak As-Sahihain j. 2 uk. 343 zakatul-fitri.
 • 7. Mustadrak As-Sahihain j. 3 uk. 149.
 • 8. Sahih Bukhari j. 3 uk. 171 kitabul-buyu’i, babu maa qiyla fi-s-siwaagh.
 • 9. Sahih Bukhari j. 2 uk. 126, Kitabu Tahajjud
 • 10. Sahih Bukhari j. 4 uk. 486, Kitabu Manaaqib, Babu swifatun- Nabiy (s.a.w.w.).
 • 11. Sahih Bukhari j. 9 uk. 418, Kitabu Tawhid, Babu fil-mashiiat wal-iraadah.
 • 12. Sahih Bukhari j. 8 uk. 245, Kitabu Daawaati, Babu as-swalaat alan-Nabiy.
 • 13. Sahih Bukhari j. 5 uk. 492, Kitabu Maghaaziy, Babu ghaz’wati Taabuk.
 • 14. Sahih Bukhari j. 9 uk. 250, Kitabul ahkaam.
 • 15. Sahihi Muslim j. 4 uk. 482, Kitabul-imaaarah, Babu an-naasu tabaun li Quraish.
 • 16. Sahihi Muslim j. 4 uk. 482, Kitabul-imaaarah, Babu an-naasu tabaun li Quraish.
 • 17. Musnad Ahmad j. 1 uk. 389.
 • 18. Mwanzo 17: 20.
 • 19. Taarikh As-Suyuuti uk. 12.
 • 20. Sahihi Tirmidhi j. 2 uk. 298.
 • 21. Sunan Ibnu Maajah j. 1 uk. 43, babu fadhlu Ali ibn Abi Talib.
 • 22. Musnad Ahmad bin Hambal j. 4 uk. 281.
 • 23. (Sahih Bukhari J: 6 uk:290 Kitabu Tafsir).
 • 24. Al-maidah 67, Al-waahidiy katika As-baabu-n-nuzuul na tafsiri al -kabir ya ar-Raazi.
 • 25. Al--Maaidah 5: 3, As- Suyuuti katika ad-Durrul -manthur, na Taarikh Baghdadi ya Al-khatib al- Baghdadiy
 • 26. Sahihi Tirimidhi j. 2 uk. 297.
 • 27. Tafsir Tabari, Asbaabu-n-Nuzuul ya Al-Waahidiy, Shawahidut-Tanzil ya Al-Hakim na Ansaabul-Ashraaf
 • 28. Sahih Bukhari j. 5 uk. 492, kitabul -maghaazi.
 • 29. Sahih Bukhari j. 6 uk. 10, kitabu-t- tafsiri, babu qawlihi- maa nansakhu aayatan au nunsihaa.
 • 30. Sahih Tirmidhi j. 2 uk. 299
 • 31. Mustadrak as-Sahihayn j. 3 uk. 126.
 • 32. Mustadrak as-Sahihayn j. 3 uk. 122.
 • 33. Sahihi Tirimidhi j. 2 uk 299.
 • 34. Sahih Bukhari j. 5 uk. 43, Kitabu fadhaili -s- sahabah.
 • 35. Mustadrak as-Sahihayn j. 3 uk. 107.
 • 36. Kanzul- umaal j. 13 had. 37753 na Dhakhairul-uqbah.
 • 37. Kunuzul- haqaaiq ya Munawi na pia ameitoa Dailami.
 • 38. Sahih Bukhari j. 5 uk. 511, Kitabul -maghaaziy, Babu maradhu-n-nabiy (s.a.w.w.) wa wafaatuh.
 • 39. Sahih Bukhari j. 5 uk. 512, Kitabul -maghaaziy, Babu maradhu-n-nabiy (s.a.w.w.) wa wafaatuh.
 • 40. Sahih Bukhari j. 7 uk. 389, Kitabu-l-mardhaa, Babu qawlul-maridh -quumuu anniy.
 • 41. Sahihi Muslimu j. 4 uk. 175, Kitabul wasiyyah babu tarki-l- wasiyyah liman laysa lahu shay’un yuuswiy fiyh
 • 42. As-saqifah cha Abubakari Ahmad bin Abdul-Aziz Al- Jauhariy.
 • 43. Musnad Ahmad j. 6 uk. 306.
 • 44. Rijaalun haula -r-Rasuul cha Khalid Muhammad Khalid, uk 548 chapa ya 8, Tarekh Tabari, Ibn al- Athiyr, Tabaqaat cha Ibn Sa’d.
 • 45. Sahih Bukhari j. 5 uk. 387, Kitabul maghaaziy, Babu ghaz’watu Zayd ibn Haarithah.
 • 46. Sahih Bukhari j. 5 uk. 13, Kitabu fadhaili -s- sahaba, Babu in lam tajid nabiy fa inna Aba Bakr.
 • 47. Sahih Bukhari j. 8 uk. 542, Kitabul-muharibina min ahli-l-kufri, Babu rajmi-l-hablaa mina-z-zinaa.
 • 48. Sahih Bukhari j. 5 uk. 14, Kitabu fadhaili- s- sahaba, Babu in lam tajid nabiy fa inna Aba Bakr.
 • 49. Sahih Bukhari j. 5 uk. 14, Kitabu fadhaili- s- sahaba, Babu in lam tajid nabiy fa inna Aba Bakr.
 • 50. Sahih Bukhari. j. 8 uk. 542, Kitabul-muharibina min ahli-l-kufri, Babu rajmi-l-hablaa mina-z-zinaa.
 • 51. Sahih Bukhari j. 5 uk. 14, Kitabu fadhaili- s- sahaba, Babu in lam tajid nabiy fa inna Aba Bakr.
 • 52. Sahih Bukhari j. 5 uk. 14, Kitabu fadhaili- s- sahaba, Babu in lam tajid nabiy fa inna Aba Bakr.
 • 53. Sahih Bukhari j. 8 uk. 542, Kitabul-muharibina min ahli-l-kufri, Babu rajmi-l-hablaa mina-z-zinaa.
 • 54. Sahih Bukhari j. 5 uk. 15, Kitabu fadhaili- s- sahaba, Babu in lam tajid nabiy fa inna Aba Bakr.
 • 55. Sahihi Bukhari j. 8 uk. 542 na j. 5 uk. 14
 • 56. Sahihi Bukhari j. 8 uk. 540, Kitabul-muharibina min ahli-l-kufr, Babu rajmi-l-hablaa mina-z-zinaa.
 • 57. Sahihi Bukhari j. 8 uk. 540, Kitabul-muharibina min ahli-l-kufri, Babu rajmi-l-hablaa mina-z-zinaa.
 • 58. Sahih Bukhari j. 5 uk. 382, Kitabul-maghaziy, Babu ghaz’wati Khaybar.
 • 59. Khulafau-r-Rasuli cha Khalid Muhammad Khalid uk. 418 chapa ya 8.
  * Ndugu msomaji iwapo utafanikiwa kukipata Kitabu ambacho kimetarjumiwa katika Kiswahili Kesi ya
  fadak baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.) cha Amiraly M.H.Datoo
 • 60. Sahih Bukhari j. 4 uk. 208, Kitabul-khumsi, Babul-faraaidh.
 • 61. Sahih Bukhari j. 5 uk. 382, Kitabul Maghaazi, Babu Ghaz’wati Khaybar.
 • 62. Sahih Bukhari j. 5 uk. 75, Kitabu Fadhaili-s- sahaba, Babu manaaqibi Fatwimah radhillahu ‘anha.
 • 63. Sahih Bukhari j. 8 uk. 202, Kitabul Istiidhan, Babu man naajaa bayna yadayi-n-naasi.
 • 64. Sahih Bukhari j. 5 uk. 74, Kitabu Fadhaili-s- sahaba, Babu manaaqibi Fatwimah radhiallahu ‘anha.
 • 65. Manaalu-t-Talib fiy sharhi twiwaalil - gharaib cha Ibn Al-Athir uk. 501, chapa ya Al-madaniy.
 • 66. Ibnul-Jawziy: Kitabu Swaf’watu-s- Swaf’wah.
 • 67. Sahih Bukhari j. 4 uk. 208, Kitabul-Khumsi, Babul-faraaidh.
 • 68. Sahih Bukhari j. 5 uk. 382, Kitabul Maghaazi, Babu ghaz’wati Khaybar.
 • 69. Sahih Bukhari j. 9 uk. 145 kitabul- fitani, Babu satarawna ba’diy umuuran tunkiruunaha.
 • 70. Sahih Muslim j. 4 uk.517, Kitabul-imaarah, Babu wujuubi mulaazamati jamaa’atil-muslimiyna, chapa ya Darush Sha’b.
 • 71. Musnad Ahmad j. 3 uk. 446.
 • 72. Sahih Bukhari j. 5 uk. 75, Kitabu fadhaili-s-sahabah, Babu fadhaaili Fatwimah radhiyallahu ‘anha.
 • 73. Sahih Bukhari j. 5 uk. 74, Kitabu fadhaili-s-sahabah, Babu fadhaaili Fatwimah radhiyallahu ‘anha.
 • 74. Sahih Bukhari j. 9 uk. 250, Kitabul-Ahkam.
 • 75. Tarekh Tabari, Tarekh Dimishqi ya Ibn Asaakir.
 • 76. Tarekh Tabari.
 • 77. Tarekh Tabari.
 • 78. Tarekh Tabari.
 • 79. Khulafau-r-Rasuli cha Khalid Muhammad Khalid uk. 272 chapa ya 8.
 • 80. Sahih Bukhari j. 9 uk. 239, Kitabul-Ahkam, Babu kayfa yubaaya’ul-imamu lin-naas.
 • 81. Khulafau-r-Rasuli uk. 276 chapa ya 8.
 • 82. Tarekh Tabari, Al- Mas’udiy, Ibnul- Athir, Al- Isti’ab.
 • 83. Ibnul-Athir, Al Mas’udiy na Tarekh Tabari.
 • 84. Sahih Bukhari j. 2 uk. 278, Kitabu-z-Zakaah.
 • 85. Baladhuriy katika ansaabul- Ashraaf, Al W aqidi na Tarekh ya Yaaqubi.
 • 86. Sherhe Ibn Abil-hadid.
 • 87. Tabari j. 4 uk. 277, chapa ya Cairo 1357AH. na NihAyah ya Ibnul-Athir na wengineo.
 • 88. Tabari, Juz. 5, uk. 172; Ibnul-Athir na Ibnu Sa’ad.
 • 89. Sahih Bukhari j. 4 uk. 217, Kitabul-khumsi, Babu maa jaa’a fiy buyuuti az’waaji-n-Nabiy.
 • 90. Sahih Bukhari j. 9 uk. 171, Kitabul-fitani, Babu al-fitnati-l-latiy tamuuju kamaujil-bahri.
 • 91. Sahih Bukhari j. 1 uk. 133, Kitabul-wudhui, Babu swabbi-n-Nabiy wudhuu’ahu ‘alal-mughmaa ‘alayhi.
 • 92. Sahih Bukhari j. 6 uk. 252, Kitabu-t-Tafsir, Babu - Lawla idh sami’tumuuhu.

Orodha Ya Wapokezi Wa Uongo Wa Saba’100

Mzushi Wake Ni Seif Bin ‘Amru At-Tamimiy Aliyefariki Mwaka Wa 170 Hijriyyah. Wapokezi Wake:-

JINA MWAKA ALIOFIA
Tabari 310 Hijriyyah
Ibn-Asaakir 571 Hijriyyah
Adh-Dhahabi 748 Hijriyyah
Ibnul-Athir 630 Hijriyyah
Abul-Fidai 733 Hijriyyah
Abi Bakar 741 Hijriyyah
Fan Fulton Nikison
Ibn-Kathir 774 Hijriyyah
Ibn-Khaldun 808 Hijriyyah
Ghiyathu-d-din 940 Hijriyyah
Mir Akhawandi 903 Hijriyyah
Ibn Badaran 1346 Hijriyyah
Rashid Ridhaa 1356 Hijriyyah
Sa’ad Afghani
Farid Wajidi
Ahmad Amini

Saba: Vita Vya Siffin Na Uasi Wa Mu’awiyah Bin Abi Sufian.

Baada ya kutimia nusura kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika vita vya Jamal, Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na jeshi lake aliondoka kwenda kuondoa upinzani ambao aliuongoza Mu’awiyah bin Abi Sufian huko Sham, na majeshi mawili yalikutana katika mto Furat. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alijaribu kusuluhisha jambo hili kwa njia ya mazungumzo, isipokuwa majibu ya Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa ujumbe ambao Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) aliutuma kwake yalikuwa: “Ondokeni kwangu mimi sina njia nyingine isipokuwa vita tu.”1

Hivi ndivyo yalivyokutana majeshi mawili. Na zilipo dhihiri ishara za ushindi kwa jeshi la Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na kundi ovu likakaribia kushindwa, waliandaa hila (`hadaa ya misahafu`), kwani walinyanyua misahafu juu ya ncha za mikuki na panga. Hila hiyo ya udanganyifu ikabadilisha msimamo wa jumla kwa wengi, pamoja na kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alijitahidi kufichua hadaa ya kunyanyua misahafu kwamba huo ni udanganyifu wa kupoteza ushindi ambao umekaribia kwa jeshi la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), isipokuwa wale waliotaka vita visimamishwe hawakukubali wito wake wa mara kwa mara, na wakamlazimisha kukubali suluhu pamoja na kuwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alipinga sana, na pia akapinga kuchaguliwa Abu Musa Al-Ash’ari kuwa mjumbe anayewakilisha jeshi lake katika suluhu, kwa sababu ya udhaifu wake na wepesi wa rai yake pale alipowaambia: “Sikubali mumchague Abu Musa kuwa hakimu kwa sababu yeye ni dhaifu kwa ‘Amr na hila zake.”2

Na hasa baada ya kumwondoa ugavana wa Kufah, ni katika yanayomfanya aone kuwa uaminifu wake kwake ni dhaifu, pamoja na hayo kundi katika jeshi la Imam lilimng’ang’ania Abu Musa tu.

Na kuonyesha kuwepo hila na njama ni utangulizi wa lengo la kunyanyua misahafu, na kutumia utukufu wa Qur’an kwa waumini dhaifu sambamba na hilo, ni pamoja na kuwepo kundi lililomuunga mkono Mu’awiyah bin Abi Sufian lilijipenyeza katika jeshi la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na wakaeneza nguvu zao katika safu ya jeshi la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), mpaka wakamlazimisha suluhu na uteuzi wa mjumbe wake, katika suluhu baadaye ambapo ilifanya matokeo yawe kama alivyo sema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kwa maslahi ya Mu’awiyah bin Abi Sufian ambapo mambo yalianza kumnyookea kidogo kidogo, baada ya kufanya uasi wake mkubwa ambapo alitoka katika utii wa Amirul-Muuminina na Khalifa wa Waislamu ambaye ni wajib kumtii, kwa uasi wake na tamaa ya utajiri wa kidunia ambao ni ndoto yake ya muda mrefu.

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alitoa habari za uovu wa Mu’awiyah bin Abi Sufian, alimwambia ‘Ammar: “Litakuuwa kundi ovu” na yalitokea aliyoyasema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alipokufa shahidi ‘Ammar akiwa anapigana chini ya uongozi wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) huko Siffin. Amesema: “Tulikuwa tunasomba matofali na ‘Ammar alikuwa anasomba matofali mawili mawili, Mtume (s.a.w.w.) akapitia karibu yake na akagusa vumbi kichwani kwake na akasema: “Namhurumia ‘Ammar litamuuwa kundi ovu, ‘Ammar anawalingania kwa Allah (s.w.t.) na wao wanamwita kwenda kwenye moto.”3

Na katika Mustadrak Sahihain kwa sanad ya Khalid Al-’Arabi amesema: “Niliingia mimi na Abu Said Al-Khudhri kwa Hudhaifah tukasema: “Ewe Abu ‘Abdillah! Tusimulie uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) miongoni mwa fitina”.

Hudhaifah akasema: “Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema: “Zungukeni pamoja na Kitabu cha Allah (s.w.t.).” Tukasema watu wakihitalifiana tutakuwa pamoja na nani? Akasema angalieni kundi ambalo lina mtoto wa Sumayyah, liandameni kwani yeye anazunguka pamoja na Kitabu cha Allah (s.w.t.), nimemsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anamwambia ‘Ammar: ‘Ewe Abul-Yaqidhan! Hutokufa mpaka likuue kundi lililo potoka njia.”4

Na uovu wa Mu’awiyah bin Abi Sufian ulikuwa ni jambo lenye kutarajiwa kutokea, kwa sababu ya kuchukua ugavana wa Sham tangu wakati wa ‘Umar na akapata mali, jaha na majumba ya fahari aliyo yajenga.

Na akajijenga wakati wa ‘Uthman, haikuwa rahisi kuyaacha na alikuwa na yakini kuwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kama hatomuuzulu basi atamnyang’anya yote aliyo yamiliki kutoka katika hazina ya Waislamu, na atamfanya awe sawa na watu wengine miongoni mwa Waislamu.

Na kisa chake pamoja na Abudhar wakati wa ‘Uthman kinaonyesha tunayoyasema kupenda kwake dunia na ufujaji wake katika mali za dola kwa ujumla, na upinzani wa Abudhar kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian ulisababisha aamuru kufukuzwa Abudhar kwenda Rabadhah baada ya kuwa alimwita arejee Madina.

“Kutoka kwa Wahhab amesema: “Nilimkuta Abudhar Rabadhah nikamwambia:”Ni kipi kilichokuleta katika ardhi hii?” Akasema: “Tulikuwa Sham, basi nikasoma Ayah: ‘Na wale ambao wanalimbikiza dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allah (s.w.t.), basi wabashirie adhabu iumizayo.’ Mu’awiyah bin Abi Sufian akasema hii haikuteremka kwetu, hii haikuteremka isipokuwa kwa Ahlul-Kitab, akasema; na nikasema: Hakika imeshuka kwetu na kwao.”5

Na Abudhar aliadhibiwa kwa kufukuzwa pamoja na kwamba kuna ushahidi wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) juu ya ukweli wake aliposema: “Haikumfunika mbingu wala hakutembea ardhini (mtu) mkweli wa kauli kuliko Abudhar.”6

Na tabia ya Mu’awiyah bin Abi Sufian katika ugavana na utawala inadhihirika wazi katika kauli ya baba yake Abu Sufian kwa ‘Uthman baada ya kupewa Bai’a: “Enyi Bani Umayyah udakeni kama mnavyodaka mpira, (naapa) kwa ambaye Abu Sufian anaapa kwake sikuacha kuwa nalitamani liwe kwenu na mlirithishe kwa watoto wenu.”7 Na katika mapokezi mengine kuna ziada: “Huko Akherah hakuna Jannat (pepo) wala Jahannam (moto).”8 Na hii inathibitisha ni aina gani ya Uislamu ulioingia katika nyoyo zao hali wao wanauchukia.

“Abu Sufian amesema: “Wallahi sikuacha kuwa dhalili hali ya kuwa na yakini kuwa jambo lake litadhihiri, hadi Allah (s.w.t.) akauingiza moyo wangu katika Uislamu na mimi ni mwenye kuchukia.”9

Na miongoni mwa kauli za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian ni ambayo ameipokea Muslim katika Sahih yake. Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) siku moja alimtuma ‘Abbas kwenda kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian ili aje amwandikie Ibn ‘Abbas akamkuta anakula, Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alimrejesha tena kwenda kumwita akamkuta anakula hadi mara ya tatu, Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) akasema Allah (s.w.t.) asilishibishe tumbo lake”.10 Pia katika Sahih Muslim, amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.); “Amma Mu’awiyah bin Abi Sufian ni fakiri hana mali yoyote.”11

Na katika Musnad Ahmad, amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian na ‘Amr bin ‘Aas: “Ewe Allah (s.w.t.) watie katika fitina kuwatia na waingize motoni kuwaingiza.”12

Na zipo Hadith nyingi zisizokuwa hizo miongoni mwa Hadith zinazo bainisha ukweli wa Mu’awiyah bin Abi Sufian huyu ambaye amehitimisha vitendo vyake katika dunia hii kwa kumtawalisha mwanae Yazid mlevi, fasiki kuwa khalifa wa Waislaam baada yake.

Nane-Kufa Shahid Kwa Al-Imam ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.)

Vita vya mwisho alivyopigana Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni vita vya Nahrawan ambapo alipigana dhidi ya kundi lililo lazimisha suluhu Siffin, lakini likajuta baada ya siku chache, hivyo likatengua ahadi yao na wakatoka katika Bai’a ya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na ambalo baadaye likajulikana kwa jina la Khawarji au Al-Maariqina (waasi). Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) aliwashinda na akawa anajiandaa kurudia mapambano na wapinzani wa Sham baada ya suluhu kushindwa walipokutana wajumbe wawili, lakini Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akawa ameuliwa shahidi na

‘Abdurahman bin Muljim naye ni mmoja wa Makhawariji ambaye alimpiga Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kwa dharuba ya upanga huku akiwa katika sala ya Al-fajiri katika msikiti wa Kufah asubuhi ya kuamkia siku ya kumi na tisa katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan Mwaka wa 40 Hijriyyah baada ya kuongoza kwa muda wa miaka mitano.

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alibakia siku tatu akiumwa kutokana na pigo, ambapo alimwita mtoto wake Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kuja kushika majukumu yake ya Uimamu katika kuongoza ‘Ummah baada yake.

Al Imam Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.) Na Suluhu Ya Mu’awiyah Bin Abi Sufian

Baada ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kufa shahid, Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alipanda Mimbar na watu wa Kufah walinyanyuka na kumbay’i Khalifa wa Nabii na Imam wa Ummah. Lakini hilo halikudumu isipokuwa kwa muda wa miezi sita ambapo habari za Kufah Shahid Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) zilifika Sham, na Mu’awiyah bin Abi Sufian aliondoka na jeshi kubwa kuelekea Kufah kwenda kuchukua hatamu za uongozi wa Waislamu na kumlazimisha Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kufanya suluhu. Imam Hassan hakuwa na njia nyingine isipokuwa kukubali. Na hapa baadhi ya watu wanatia shaka juu ya suluhu ya Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), wakati ambapo ndugu yake Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alichagua njia ya vita na kupigana.

Hakika Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) hakufanya mkataba wa suluhu pamoja na Mu’awiyah bin Abi Sufian bali amelazimishwa. Kulikuwa na mgawanyiko katika jeshi lake na hali ya Iraq kwa ndani haikuwa ni muafaka kwa vita, na ufalme wa Roma ulikuwa unangojea fursa ya kuupiga Uislam, na ulikuwa umejiandaa kwa jeshi kubwa tayari kuwapiga vita Waislamu.

Na kama vingetokea vita baina ya Mu’awiyah bin Abi Sufian na Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), basi ushindi ungekuwa ni wa ufalme wa Roma na sio kwa Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) wala kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian.

Na hivyo kukubali kwa Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kumeondoa hatari kubwa iliyokuwa ikitishia Uislamu. Kwa ujumla hali iliyo kuwepo wakati wa Al-Imam Hassan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), sio hali iliyo kuwepo wakati wa Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), ambaye baadaye alichagua njia ya Thawrah na vita ambavyo ndugu yake Al-Imam Hassan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alivitayarisha kwa udadisi wake kwa kudhihirisha ukweli wa wafalme wa Bani Umayyah katika wakati wake.

Ama misingi ya makubaliano ya suluhu ilikuwa kama ifuatavyo:-

1. Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) asalimishe utawala na hatamu za uongozi kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa sharti, Mu’awiyah bin Abi Sufian ahukumu kulingana na misingi ya Qur’an na Sunnah za Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

2. Baada ya kufa Mu’awiyah bin Abi Sufian Ukhalifa utakuwa ni haki ya Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na kama akifariki basi Ukhalifa utakuwa kwa Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.)

3. Shutuma zote na uovu dhidi ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) uzuiwe, iwe ni kwenye Mimbar au popote (Mu’awiyah bin Abi Sufian alikuwa ana amuru makhatibu katika wilaya zote kumtukana Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), Hassan na Ibn ‘Abbas, katika kila hutuba ya Ijumaa na Iddi, na Mu’awiyah bin Abi Sufian hakutekeleza ahadi yake hii wala nyinginezo ambazo zilikubaliwa).

4. Kutoa kiasi cha dirham milioni tano zilizopo katika hazina ya Kufah ziwe chini ya usimamizi wa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na ni wajibu kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian kutuma kwa kila mwaka dirham milioni moja za pato kwa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ili azigawe kwa familia za wale ambao walikufa shahid katika vita mbili, Jamal na Siffin, katika upande wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.).

4. Mu’awiyah bin Abi Sufian anaahidi kuwaacha watu wote wa aina yeyote kutokana na kusumbuliwa na anaahidi vile vile kuwa atatekeleza misingi ya suluhu hii kwa umakini na anaifanya dini iwe ni shahidi juu yake.

Tisa: Kufa Shahid Kwa Al-Imam Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.)

Mu’awiyah bin Abi Sufian alimshawishi (Ju’udatu binti Al-Ash’ath bin Qais) mke wa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ambaye alikuwa ni wa ukoo wa familia zinazo wapinga Ahlul-Bayt (a.s.), kwa kumtumia dirham laki moja akamwahidi kuwa atamwozesha kwa mtoto wake Yazid kama atampa sumu Al-Imam Hasan bin Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.). Mke mwovu alidanganyika na ahadi za uongo za Mu’awiyah bin Abi Sufian na akampa Imam sumu, na hiyo ilikuwa Mwaka wa 50 Hijriyyah. Mu’awiyah bin Abi Sufian alifurahi sana alipojua kufa shahid kwa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kwa kuwa alikuwa anaona kuwa ni kipingamizi kikubwa katika matakwa yake na hasa katika kuimarisha utawala katika familia ya Mu’awiyah bin Abi Sufian kimekwisha kuondoka.

Kumi: Thawrah (Mapambano) Ya Karbala Na Kufa Shahid Kwa Al Imam Hussein Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.)

Al-Imam Hussein bin ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni Imam wa tatu wa Ahlul- Bayt (a.s.), na tukio muhimu katika historia lilikuwa ni kujitoa muhanga na kufa kwake shahid pamoja na watoto wake Ahlul-Bayt (a.s.) na wafuasi wake pale Karbala. Katika tukio lililotingisha akili na fikira na kuandikwa katika kurasa za historia na litaendelea kuthibiti na kubaki daima.

Hakika sababu zilizowazi za Thawrah ya Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), ni upotovu ambao ulidhihiri wakati huo katika watawala wa Bani Umayyah na ukandamizaji wao kwa watu.

Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa muda wa miaka ishirini alikuwa anaimarisha kumtawalisha mwanae mwovu Yazid na kumpa nguvu ili kumfanya kuwa Amirul-Muuminina na Khalifa wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa Waislamu, na kwa hivyo akakhalifu ahadi zake kwa Al- Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na kutengua ahadi zote alizomwahidi Allah (s.w.t.).

Yazid kwa mtazamo wa makundi yote ya Kiislam, alikuwa anakunywa pombe wazi wazi na anakunywa hata makapi na kukesha, na kuimba mashairi ya kipuuzi tunataja baadhi yake:- “Muziki wa didan umenishughulisha kutosikia adhana, na mwanamke kikongwe asiyejiweza amekuwa ni badala ya hurulain”.

Hakuna ajabu katika hili kwani Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian amelelewa na yaya wa Kikristo, na alikuwa ni kijana mjinga mwovu, tegemezi, mfujaji, hana haya, asiyeona mbali na asiye na maarifa kama walivyosema wanahistoria.

Baada ya kufariki Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika Mwaka wa 50 Hijriyyah, Mashi’a wa Iraq walijaribu kujikomboa na walimwandikia Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) wakitaka amuuzulu Mu’awiyah bin Abi Sufian katika uongozi wa Waislamu. Lakini Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) akawaambia katika jibu lake kuwa ana ahadi na makubaliano na Mu’awiyah bin Abi Sufian hawezi kuyavunja.

Baada ya kufa Mu’awiyah bin Abi Sufian Mwaka wa 60 Hijriyyah, Yazid alichukua utawala, basi utawala wake ukawa ni mwanzo wa upuuzi na madhambi. Katika hali hii Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) aliona sio kwamba wakati ni mwafaka tu, bali ni wajibu kufanya harakati na Thawrah kwa ajili ya kuunusuru Uislamu na misingi ya dini, na sio kwa ajili ya kuchukua Ukhalifa na utawala ambao ndiyo ulikuwa matamanio ya Bani Umayyah, ambapo walipania mno katika kuupata na hasa baada ya watu wa Iraq kukataa kumnusuru Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na hofu yao kwa Bani Umayyah.

Na anabainisha wazi Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika moja ya hotuba zake alipokuwa karibu na Karbala kuhusu sababu ya Thawrah yake, kwa kusema:

“Enyi watu atakayemwona kiongozi mwovu anahalalisha aliyoharamisha Allah (s.w.t.) baada ya kumwahidi, anakhalifu Sunnah za Nabii wake, na anahukumu baina ya waja wa Allah (s.w.t.) kwa ufisadi na ujeuri; na asimpinge kwa ulimi wake na vitendo vyake; basi ni haki kwa Allah (s.w.t.) kumtupa Jahannam.” Vile vile amesema: “Enyi watu, na hakika wao wamemtii Shetani na wamemwasi Allah (s.w.t.) na wamefanya ufisadi katika ardhi, wamevunja Sunnah na wamefuja hazina ya mali ya Waislamu, na wamehalalisha aliyoyaharamisha Allah (s.w.t.), na wakaharamisha aliyoyahalalisha Allah (s.w.t.), na mimi nina haki zaidi kumpinga kuliko watu wengine.” Akakusanya wafuasi wake na Ahlul Bayt wake waliokuwa pamoja naye na akawaeleza wazi kukataa na kusitasita kwa watu wa Kufah, kisha akawaambia: “Wafuasi wetu wametufedhehesha hivyo anayependa kuondoka basi na aondoke na wala hatakuwa na dhima yetu.”

Pamoja na hivyo Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alibaki na msimamo wake na azma ile ile aliyotoka nayo Makkah na hakuwa na yeyote isipokuwa wafuasi, ndugu, watoto na watoto wa Ami zake, na idadi yao haizidi sabini na nane na hapo alitamka tamko lake lenye kudumu; “Kama dini ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) haiwezi kusimama isipokuwa kwa kuuliwa kwangu, basi enyi mapanga niuweni.”

Na alikutana na jeshi la Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian, ambalo idadi yake ilikuwa ni elfu thelathini na mbili, chini ya uongozi wa Hur bin Yazid Ar-Riyaahi. Kwa kawaida kulikuwa na uwezekano mkubwa wa jeshi la Banu Umayyah kuuwa kundi hili lenye idadi ndogo, na hiyo ni kweli. Katika siku hiyo yalitokea mauaji hayo kwa Ahlul-Bayt (a.s.) na kudhulumiwa kwao kunasikitisha, kana kwamba Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian alikuwa analipa malipo ambayo Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimuomba: “Sema siwaombi juu yake malipo isipokuwa kuwapenda jamaa zangu”.

Tarekh imesimulia matukio na mauaji ambayo ni vigumu mno kwa mtu yeyote kuyaelezea. Kati ya hayo ni ya mtoto mchanga, naye ni ‘Abadallah bin Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), ambaye Imam Hussein alimbeba kwenda kumwombea maji baada ya wao kuweka kizuizi baina ya watu wa kambi ya Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), na mto Furati na kiu ikawabana sana. Alimbeba kwenda kumwombea maji na ili kuzitikisa dhamiri zao na kuathiri hisia zao za kibinadamu, hawakumjibu isipokuwa kwa kumlenga mshale mtoto mchanga na wakamwua, na mashahidi katika wafuasi wa Hussein na Ahlul-Bayt (a.s.) waliendelea kuuawa mmoja baada ya mwingine. Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa ni wa mwisho kufa shahid katika vita hivyo vibaya.

Hawakutosheka kwa kumuuwa Bwana wa vijana wa watu wa Jannat (pepo) bali walikata kichwa chake na wakakitenganisha na mwili wake, kichwa cha Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na vichwa vya wafuasi wake vilichukuliwa na kuwa zawadi, wauaji walivigawa na wakavinyanyua huku wakielekea kwa Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian huko Sham ambaye, baadhi ya Waislamu wamempa sifa ya Amirul-Muuminin basi hakuna nguvu wala hila isipokuwa kutoka kwa Allah (s.w.t.)...!

Hakika matukio, mambo na misimamo ambayo tumeieleza na ambayo wameafikiana wapokezi wote wa Kiislamu Sunni na Shi’a, yanabainisha wazi malengo matukufu na ambayo kwa ajili yake Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alifanya Thawrah, pamoja na hayo, ingawa ufisadi, uasherati na upotovu, na uovu ulioenea ambao ni wajibu kuuondoa kwa mkono, ulimi na kuchukia kwa moyo kumepatikana, wanaokosoa Thawrah hii tukufu kwa sababu ya kutumbukia kwao katika propaganda wa upotoshaji wa Bani Umayyah ambao umejaribu kupotosha historia, na vile vile kwa sababu ya kutumbukia kwao katika ta’asub (ushabiki) mbaya za kimadhehebu.

Hivyo zikadhihiri hukumu zenye kutia kasoro na kauli zenye kutuhumu juu ya Thawrah ya ambaye Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) amesema juu yake kwa mapokezi ya Waislamu wote, kwamba yeye ni Bwana wa vijana wa watu wa Jannat; kwa mfano kauli ya Ibn Taymiyyah: “Hakika Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kwa Thawrah yake amekwisha toka katika utii wa kiongozi wa Waislamu na kwamba vile vile amechochea fitina katika ‘Ummah wa Kiislamu!!” Na kama tutamwuliza huyu juu ya kutoka Mu’awiyah bin Abi Sufian katika utii wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) jibu lake lingekuwa hiyo ni fitina iliyotokea baina yao na wala wao hawana dhambi katika hilo.

Na hili si lingine isipokuwa ni hali miongoni mwa hali za kujaribu kupotosha na udanganyifu ambao uko wazi katika historia ya Kiislamu, vinginevyo itatafsiriwaje hali ya baadhi ya Waislamu ya kujifanya kutojua mauaji haya ya kihistoria, ambayo humo wameuliwa watoto wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) katika hali mbaya kabisa ya mauaji na adhabu?

Sio hayo tu, bali watawala wengine wa Bani Umayyah walifuata mwendo wa Mu’awiyah bin Abi Sufian na mtoto wake Yazid; watawala wengine katika kuzima harakati za wapinzani wa utawala wao, na hasa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), walihahikisha kwamba, daima wanakandamizwa, wanafukuzwa, wanaadhibiwa na kuuliwa.

Na udhalimu wao ulikuwa kwa Ahlul-Bayt (a.s.) na wasiokuwa Ahlul-Bayt (a.s.), walikuwa ni shabaha katika kila nyanja ambazo kuna dhana ya kuleta ushindani katika utawala wao wa kidunia na ufalme wa Kisra.
Historia imeandika kwa mfano - tukio la mauaji ambalo alichinjwa ‘Abadallah bin Zubeir, na akachunwa katika eneo takatifu la Makkah ambalo hata makafiri walikuwa wanalitukuza na kuliheshimu, wala hawakuhalalisha kumwagwa humo damu ya mnyama tukiachilia mbali ya binadamu. Al-Ka’abah Tukufu haikumsaidia kitu chochote Ibn Zubeir ambapo aligandamana na pazia yake kwa watawala wa Bani Umayyah.

Vipi nyumba ya Allah (s.w.t.) itakuwa na utukufu kwao na wao ndio ambao waliipiga Al-Ka’abah Tukufu kwa manjanikh (makombeo ya moto), wakati wa utawala wa Abdul-Malik bin Marwan ambaye alitoa mamlaka katika mkono wa mwovu wake Hajjaj ya kuuwa, anauwa na kuchinja watu bila ya haki, na ambao Hassan Al-Basri amesema juu yao: “Kama ‘Abdul-Malik asingekuwa na kosa isipokuwa Hajjaj basi lingemtosha”. Na amesema ‘Umar Abdul-Aziz: “Kama kila ‘Ummah ungekuja na mwovu wao na sisi tukaja na Hajjaj basi tungewashinda”, tukiachilia mbali kisa mashuhuri cha ‘Abdul-Malik cha kuchana Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Je, vitendo hivi vinamfanya mwenye kuvitenda kuwa Mwislamu? Tukiachilia mbali kumuuwa kwake Khalifa wa Waislamu na Amirul- Muuminin?

Hapana shaka kwamba sisi leo tuna haja ya kuangalia historia ya Kiisalmu, na kudadisi katika mengi ya matukio na kuchunguza kwa yale yaliyopo miongoni mwa uhusiano mkubwa na maisha yetu ya kila siku na yawe ndiyo hukumu yetu katika kundi hili au lile, mbali na dhuluma au makosa kwa sababu ya matukio hayo Waislamu wamegawanyika madhehebu na makundi yenye kuzozana, kila moja linadai kuwa ndilo kundi lenye kunusurika na sio kwa yeyote kusubiri wahyi kutoka mbinguni umteremkie na kumwambia jina la kundi hili lenye kunusurika.

Na Allah (s.w.t.) ametujaalia akili ili tutofautishe ovu na jema na akatukataza kuiga kwa upofu na akatutanabahisha: “Bali aliwajia kwa haki na wengi wao ni wenye kuchukia haki.” Na akatuhadharisha kuchukua kutoka kwa kila mtu, “kama akikujieni fasiki kwa habari basi chunguzeni msije mkawadhuru watu kwa ujinga na mkaja juta kwa mliyoyafanya.”

Shura Baina Ya Misingi Na Utekelezaji

Baadhi ya wenye kukhalifu wanajaribu kupinga Ayah za Uimamu wa Ahlul Bayt (a.s) kwa madai kuwa Uimamu wa Waislamu umefanywa kuwa Shura na wametoa ushahidi wa Ayah mbili kutoka katika Kitabu cha Allah (s.w.t.). Ya kwanza ni:

وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ{38}

“Na jambo lao ni Shura baina yao.” (Asy Syuura 42:38)

Ayah hii haionyeshi Shura katika mambo yote ya Waislamu, hiyo ni kwa sababu kushauriana hakusihi katika jambo ambalo kuna Ayah ya Allah (s.w.t.) na kauli ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.):

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا {36}

“Haikuwa kwa Muumini mwanamme wala Muumini mwanamke anapohukumu Allah (s.w.t.) na Mtume wake wawe na hiari katika jambo lao na atakae muasi Allah (s.w.t.) na Mtume wake basi amepotea upotevu ulio wazi.” (Al-Azhaab 33:36)

Vinginevyo, je inajuzu kushauriana katika idadi ya raka’a za sala kwa mfano, au mengineyo katika hukumu ambazo kumeteremka Ayah, na tumebainisha yaliyo pokewa kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) miongoni mwa hadith za Uimamu, hivyo haibaki nafasi ya kushauriana. Ama Ayah ya pili ambayo ni:

وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ{159}

Washauri katika jambo” (Ali-Imran 3:159)

Bali anamwambia: “ukiazimia mtegemee Allah (s.w.t.).” Na fanya kulingana na unavyoona na inadhihiri kuwa nafasi ya kushauriana inayo pendekezwa ni katika vita, na utapata mfano katika ushauriano huu katika sehemu ya nne ya kitabu hiki wakati Mtume lipowashauri Masahaba wake katika vita vya Badr. Na kama tutajaalia uwa hukumu ya Khalifa wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Shura hakika tutajiuliza. Hii Shura ni ya namna gani?

Na ni ipi njia ya kuitekeleza? Na namna gani makhalifa walitekeleza Shura hii? Na nini hukumu ya khalifa ambaye anafikia katika utawala hali amekwishavunja misingi ya Shura?

Na namna gani makhalifa walitekeleza Shura hii kisha tuangalie namna gani kila mmoja katika makhalifa wa mwanzo alivyofika katika utawala.

1. Ukhalifa Wa Abubakr Ibn Abu Quhafa

Hakika njia ambayo ilitimia katika kumtawalisha Abubakr na kupewa Bai’a, amekwisha ieleza ‘Umar ibn Al-Khattab - kama ilivyotangulia - ilikuwa ghafla, lakini Allah (s.w.t.) ameepusha shari yake. Na tumeona kutukanana kwa Muhajirin na Ansar juu ya Ukhalifa, na Ansar walitoa hoja ya kustahiki kwao ukhalifa, tukizingatia asili na nafasi yao katika uongozi wa Madina na kunusuru kwao kukubwa katika Uislamu, na hoja za Muhajirin zilikuwa kwamba wao wanastahiki zaidi, na Abubakr alipendekeza uongozi uwe wa Muhajirin na wasaidizi wawe ni Ansar. Ansar wakamjibu kutokana na mapendekezo yake kuwa kila kundi katika makundi mawili yawe na kiongozi kwa kauli yao: “Kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi.”

Na tumeona namna gani ‘Umar aliokoa msimamo huu kwa kuuchukua kwa nguvu na kumpa Abubakr bay’a. Wakati ambapo Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) pamoja na jamaa wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) hawakuwepo, hivyo Ahlul- Bayt (a.s.) wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) hawakupata fursa katika kuchagua au hata kutoa maoni, iko wapi Shura katika hayo yote?

2. Zama Za ‘Umar

Njia ambayo amefikia ‘Umar katika utawala ni kutokana na wosia aliyo ulioandikwa na Abubakr akiwa katika maradhi yake ya mwisho mbele ya ‘Uthman bin ‘‘Affan tu! Na ‘Umar akachukua wosia huo na kutoa ushahidi kwa watu na akachukua Bai’a kwao kwa sababu hiyo. Je, iko wapi Shura katika hili?

3. Zama Za ‘Uthman Bin ‘‘Affan

Njia ambayo amefikia ‘Uthman bin ‘‘Affan katika utawala, ilitegemea kikao cha Shura na ‘Umar bin Al-Khattab peke yake aliteua wajumbe wake sita, na akajaalia rai ya mwisho mikononi mwa Abdur-Rahman bin ‘Auf katika hali ya kugawanyika wajumbe sita sehemu mbili kama ilivyotokea. Shura iko wapi hapo?

4. Zama Za Mu’awiyah Bin Abi Sufian

Njia ambayo Mu’awiyah bin Abi Sufian alifikia katika utawala, ilikuwa ni kwa kunyanyua upanga dhidi ya Khalifa wa Waislamu na Imam wao aliyepewa Bai’a na wao, baada ya watu kumkimbilia na kumbay’i baada ya kuuliwa ‘Uthman bin ‘Affan kisha, baada ya kumlazimisha Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) kufanya suluhu.

5. Zama Za Yazid Bin Mu’awiyah Bin Abi Sufian.

Njia ambayo Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian amefikia katika utawala ilikuwa ni wosia kutoka kwa baba yake, ambaye alileta njia mpya katika ukhalifa na kuufanya kuwa ni wa kurithiana. Shura iko wapi hapa?

Na Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian alizatiti utawala wake kwa kumwua Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), na watoto wengine wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) pale Karbala. Vivyo hivyo ndivyo watawala wengine wa Waislamu walifikia katika utawala tangu siku hiyo hadi leo hii.

Hivyo njia ambayo ilitumika kuwatawalisha makhalifa katika maelezo tuliyoyataja tunailinganisha na njia ambayo inatumiwa kuwateua watawala wa dola za kimagharibi katika njia ambayo inaitwa Demokrasia.

Basi ni ipi kati ya njia mbili hizi ambayo ni bora kwa mtazamo wa akili sahihi ambayo imeepukana na ta’asub ya dini na madhehebu?

Jamhuri ya Waislamu katika Ahl as-Sunnah wamekataa Hadith zilizopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kuteua Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) kuwa ni Makhalifa wake katika ‘Ummah wa Kiislamu, hivyo wakapinga Hadith katika hilo na wakawapinga wale wanaoziitakidi kwa kusema kwamba jambo hili ni Shura, wakati ambapo Shura haikuwa na athari yoyote katika kutawalisha makhalifa ambao wanawakubali. Wamepinga Hadith za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kuhusu ukhalifa na wakaukubali kutoka kwa asiyekuwa Mtume, na hawakuweka sharti la Shura katika nassi (pokezi) nyingine zisizokuwa hizo bali wamekubali uteuzi wa waliye mchagua.

Wamehukumu uhalali wa Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian, ingawa kulikuwa na Thawrah ya Bwana wa mashahidi, na wakahukumu uhalali wa Mu’awiyah bin Abi Sufian ingawa alimuasi Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na akatoka katika utii wake.

Hakika kosa la wazi ambalo Jamhuri ya Waislamu wanatumbukia kwalo, ni kuchukua Hadith za Nabii katika madhehebu ambayo wanayaamini - yaani wengi wao wanakataa Hadith kwa sababu tu ina khalifu madhehebu yao hata kama Hadith hii imetoka katika vitabu vyao ambavyo wanaamini usahihi wake - pamoja na kwamba hukumu ya akili inawajibisha kuchukua madhehebu kutoka katika nassi na wala si kinyume.

Mwisho Wa Utafiti Wa Uimamu

Tumebainisha katika yaliyotangulia Hadith za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) katika Uimamu ambao unapatikana katika Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na ambao ni maalumu kwa Maimamu kumi na wawili (a.s.), ambao wa kwanza ni Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.). Na tukaweka wazi baadhi ya (mambo) yasiyo eleweka vizuri katika Hadith hizo miongoni mwa dalili, na tukatengua shaka zinazoizunguka. Kisha tukabainisha jinsi Jamhuri ya Masahaba walivyo amiliana na Hadith hizo, kisha Jamhuri ya Waislamu ikaufuata mwendo wao huo hadi leo hii.

Hakika mafhumu ya Uimamu ndiyo ambayo yamewafarakisha Waislamu punde tu baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), isipokuwa Mashi’a ndio wamejulikana kwa kuchukua kwao Sunnah hizi kutoka katika njia ya Ahlul-Bayt (a.s.) na Maimamu wao kumi na wawili; ambapo Ahl as-Sunnah wanachukua Sunnah za Nabii kutoka kwa sahaba yeyote. Aidha wameongezea katika Sunnah ya Nabii, Sunnah ya Makhalifa wawili Abubakr na ‘Umar (na utaona katika sehemu zinazofuatia mengi miongoni mwa ushahidi juu ya ukweli huu).

Na tumebainisha namna gani Jamhuri ya Masahaba walivyofanya ijtihad kati ya Waislamu waliotangulia (na waliosifika zaidi kwa hilo miongoni mwao ni Abubakr, ‘Umar, ‘Aisha na Mu’awiyah bin Abi Sufian); mbele ya Hadith za Mtume kuhusu Uimamu. Jambo ambalo limewaweka mbali Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) katika uongozi wa mambo ya ‘Ummah wa Kiislamu, na hasa baada ya kufa shahidi Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na wakawa ni wenye kupokonywa haki.

Moja kwa moja wamekuwa ni kundi la upinzani ambao hawaoni uhalali wa watawala ambao wameshika uongozi wa Waislamu bila ya haki. Basi wafuasi wa Ahlul Bayt (a.s.) wakawa ni kundi lenye kuchukiwa na watawala wa Waislamu; na hasa Bani ‘Umayyah na Bani ‘Abbas.

Na mgawanyiko wa Waislamu ulikuwa ni makundi mawili yaliyo dhihiri baada ya matukio mawili ya Vita vya Jamal na Siffin, na kufa shahidi kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.). Baada ya kuwa kundi la Ahlul Bayt (a.s.) ni lenye kufichikana katika zama za Makhalifa watatu wa mwanzo kufuatana na siasa ya hekima aliyoifuata Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), kila kundi likawa linadhihirisha dalili na ushahidi walio nao katika haki ya madai yao na kundi lao.

Wakati ambapo wafuasi wa Mu’awiyah bin Abi Sufian, Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian na watawala wengine wa Bani ‘Umayyah walikosa hoja na ushahidi wa kupinga Hadith zenye nguvu za Uimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.), mmoja wao ambaye ni Seif bin ‘Umar At-Tamimiy ambaye amejulikana kwa uongo na uzindiki kwa maulamaa wa Hadith walio tangulia, akazua kwa msaada wa mabwana zake ambao kwayo amejengea Ushi’a kwa huyu mtu wa bandia; na tumebainisha ubatili wa njama hii ya uongo wa ‘Abdillah bin Saba,’ na hata kama ikadhaniwa kuwa alikuwepo kweli, basi hakika yeye siye ambaye alitangaza uwasii wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na kumfanya kuwa Khalifa, bali ni Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kutokana na Hadith tulizozieleza katika sehemu ya kwanza.

 • 1. Fusuulul-muhimmah cha Ibnu Swabbaagh Al-maalikiy uk. 83, chapa ya Dar al-adh’waa’.
 • 2. Tadhkiratul-khawaas cha Sibtwi Ibn Al-Jawziy uk. 79.
 • 3. Sahih Bukhari j. 4 uk. 52, Kitabul-Jihad, Babu mas’hil-ghubaari ‘ani-r-ra’si fiy sabiylillah.
 • 4. Mustadrak Sahihain j.2 uk. 148, chapa ya Dar al-kitaabil-arabiy.
 • 5. Sahih Bukhari j. 6 uk. 146, Kitabu Tafsir, Babu qawlihi - wal-ladhiyna yaknizuna-dh-dhahaba -.
 • 6. Sahih Tirmidhi j.13 uk. 210, Manaaqibu Abiy dharri (r.a.) na Musnad Ahmad j.2 uk.175.
 • 7. Tarekh Tabari.
 • 8. Tarekh Tabari.
 • 9. Sahih Bukhari j. 4 uk. 122, Kitabul-Jihaad.
 • 10. Sahih Muslim j. 5 uk. 462, Kitabul-birri wa-s-swadaqah wal-adab, Babu man la’anahu-n-Nabiy.
 • 11. Sahih Muslim j. 3 uk. 293, Kitabu-t-Talaaq, Babul-mutwallaqatu laa nafaqata laha.
 • 12. Musnad Ahmad j. 4 uk. 421, Ahmad hakutaja majina yao bali amesema”fulani na Fulani”. Majina yao utayakuta katika Tarekh Tabari.

Sehemu Ya Pili: Uadilifu Wa Masahaba

Maneno yamekuwa mengi kuhusu uadilifu wa Masahaba, na watu katika hilo wamekhitalafiana Ikhtilaf kubwa. Ahl as-Sunnah wanaona kuwa Masahaba wote ni waadilifu hawatuhumiwi wala haijuzu kwa yeyote kuwakosoa, au kushuku katika mapokezi yao katika Hadith za Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Na anayefanya hivyo wanatoa Fatwa juu ya ufasiki wake na wanazingatia kuwa ni zandiki, na wao kwa hilo wanajilazimisha kwa kila alicho kipokea Sahaba, kwa mfano inatosha kwao kukubali Hadith iliyopokelewa kwa Sahaba yeyote yule, na Sahaba kwao ni kama alivyoeleza Al-Bukhari: “Ni ambaye alifuatana na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) au aliye mwona miongoni mwa Waislamu.”

Na wala sioni katika hukumu yao hiyo katika ufasiki wa kila anaye mkosoa yeyote miongoni mwa Masahaba, isipokuwa ni israf katika kuamini na ni kupinga Kitabu cha Allah (s.w.t.), Sunnah za Nabii wake na tabia ya binadamu kama tutakavyo thibitisha hayo katika kurasa zinazofuata.

Hakika wanayo singiziwa Shi’a kwamba wao wanakufurisha Masahaba wote, kwa kuongeza kuwatukana kwao na kuwalaani, hayo si kingine isipokuwa ni uongo ulio wazi na wala hauna usahihi wowote. Shi’a hawawakufurishi Masahaba lakini wanaona kuwa wao wanaweza kukosolewa na kurekebishwa na kwamba wote hawakuwa katika daraja moja ya uadilifu, na kumkosoa kwao Sahaba huyu au yule haina maana ya kuwakufurisha, kama wanavyoeneza baadhi ya wapumbavu, na kama ukosoaji wao umesimama juu ya dalili, sasa hasira ni ya nini? Na kelele yote hii ni ya nini?

Katika Masahaba kuna waumini walio wema, Allah (s.w.t.) amewasifu katika Qur’an tukufu kwa kauli yake:

لَقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنْزَلَ السَّكِينَةَ{18}

“Amekwisharidhia Allah (s.w.t.) juu ya waumini wanaokubayi chini ya mti...” (Al-Fath 48:18)

Hivyo Allah (s.w.t.) amewasifu tu waumini mahsusi, kati ya waliohudhuria tukio la Bay’atus-Shajarah na hakuwahusisha wanafiki ambao walihudhuria mfano ‘Abdallah bin ‘Ubay na Aus bin Khauli. Na hakuna dalili katika Ayah juu ya Allah (s.w.t.) kuridhia Masahaba wote waliobay’i - pamoja na kuwa wao wanawahesabia kuwa ni katika Masahaba kwa madai ya Bukhari na mfano wake - bali haionyeshi juu ya mwisho mwema kwa waumini wote walio bay’i.

Ayah haionyeshi zaidi ya kwamba Allah (s.w.t.) ameridhia Bai’a yao hii - yaani ameikubali kutoka kwao - na amewapa thawabu, ridhaa ya Allah (s.w.t.) juu ya watu wa Bai’a hii hailazimu ridhaa yake hii kuwa ni daima, na dalili katika hilo ni kauli ya Allah (s.w.t.) katika jambo lao

إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّهَ يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَنْ نَكَثَ فَإِنَّمَا يَنْكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا {10}

Hakika wale wanaokubayi wanambayi Allah (s.w.t.) mkono wa Allah (s.w.t.) uko juu ya mikono yao na atakaye tengua (Baia yake) basi hakika anatengua kwa ajili ya nafsi yake, na atakaye tekeleza aliyomwahidi Allah (s.w.t.) basi atampa malipo makubwa. (Al-Fath 48:10)

Na miongoni mwa Masahaba kuna ambaye Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ameeleza kuritadi kwake baada ya kufa kwake na kisha kuangamia kwao siku ya Qiyamah kama yanavyo dhihirika wazi hayo katika Hadith mbili zifuatazo chini:-
Sa’ad amesema nimemsikia Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) amesema: “Mimi nitawatangulia katika Hawdh atakaye nifikia atakunywa kwayo na atakaye kunywa hata pata kiu kamwe baada yake, watanijia watu na wajua na wananijua kisha kutawekwa kizuizi baina yangu na wao.”

Akasema nilimsikia akiongezea: Akasema: “Hakika wao ni katika watu wangu, itasemwa: Hakika wewe hujui waliyo yabadilisha baada yako, basi nitasema, awe mbali aliye badilisha baada yangu.”1

Amesema ‘Abdillah kwamba amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.): “Mimi nitawatangulia katika Hawdh, hakika wataletwa wanaume mionngoni mwenu mpaka nitakapo karibia ili niwapatie (maji) watazuiwa dhidhi yangu, basi nitasema: Ewe Allah (s.w.t), Masahaba wangu.’ Atasema: ‘Hujui waliyoyazua baado yako.2

Na mkazo wa Hadith mbili zilizo tangulia ambazo zinaonyesha kuzua na kubadilisha – yaani kuritaddi - hakika Hadith ifuatayo inawalinganisha na ‘Ummah za Kiyahudi na Kinasara ambao walipotosha maneno katika makusudio yake. (Kutoka kwa Nabii amesema: “Hakika mtafuata nyendo za waliokuwa kabla yenu shibr kwa shibr, dhiraa kwa dhiraa hata kama wataingia katika shimo la kenge mtawafuata.” Nikasema: “Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.): “MAyahudi na Manasara?” Akasema: “Ni nani basi?”3

Katika Masahaba kuna miongoni mwa aliowaelezea Allah (s.w.t.) katika Kitabu chake kitukufu:

وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انْفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِنْدَ اللَّهِ خَيْرٌ مِنَ اللَّهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ {11}

“Na wanapoona biashara au upuuzi wanakimbilia huko na wanakuacha umesimama…”
(Al-Juma’a 62:11)

Ayah hii imeteremka kwa Masahaba walioondoka msikitini wakati Mtume (s.a.w.w.) amesimama anawahutubia siku ya Ijumaa ulipowasili msafara kutoka Sham na hawakubaki pamoja na Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa wanaume kumi na mbili kama inavyodhihirika katika Hadith mbili hapa chini.

Amesema Jaabir ibn Abdillahi: Uliwasili msafara wa ngamia siku ya Ijumaa na sisi tuko pamoja na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) basi watu walitoka isipokuwa wanaume kumi na mbili, basi Allah (s.w.t.) akateremsha Ayah; “Na wanapoona biashara au upuuzi wanaenda huko”4

Amesema:”Tulipokuwa tunasali pamoja na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) basi ukawasili msafara wa ngamia umebeba chakula wakauendea na hawakubaki pamoja na Nabii isipokuwa wanaume kumi na wawili basi ikateremka Ayah hii (Na wanapoona biashara au upuuzi wanauendea na wanakuacha umesimama)5

Idadi hiyo hiyo - katika mamia yote hayo miongoni mwa Masahaba - walibaki pamoja na Mtume wakati walipokimbia katika vita vya Uhud kiasi kwamba Mtume (s.a.w.w.) alijiweka mbali nao kutokana na kitendo chao.

Amesema: Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alimpanga ‘Abdallah bin Jubayr katika wapiganaji wanao kwenda kwa miguu siku ya Uhud na wakakimbia waliposhindwa, hivyo Mtume akawa anawaita kwenye Akhera yao, na hawakubaki pamoja na Nabii isipokuwa wanaume kumi na wawili)6
(Kutoka kwa Anas (r.a.) amesema: Alitoweka ami yangu Anasi bin Nadhir katika vita vya Badr akasema: Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.): Nilighibu katika vita vya mwanzo ulivyowapiga washirikina, naapa kama Allah (s.w.t.) atanijaalia kupigana vita na washirikina basi Allah (s.w.t.) ataona nitakavyofanya.

Siku ya Uhud ilipofika na Waislamu wakashindwa na kukimbia, akasema: “Ewe Allah mimi naomba samahani kwako kwa waliofanya hawa watu, yaani Masahaba wake.”7

Na siku ya Hunain kukimbia kwao kulikuwa ni jambo la kushangaza wakati ambapo walikuwa maelfu.

وَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنْكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُمْ مُدْبِرِينَ {25}

ثُمَّ أَنْزَلَ اللَّهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ{26}

“Na siku ya Hunain ulipowashangaza wingi wenu na haukuwasaidia kitu chochote na ardhi ikawa finyu kwenu kutokana na mlivyoshambuliwa kisha mkakimbia kurejea nyuma, halafu Allah akateremsha utulivu wake kwa Mtume wake na waumini.”(At-Taubah 9:25-26)

Na katika masahaba kuna ambao wameteremkiwa na Ayah:

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ {67}

لَوْلَا كِتَابٌ مِنَ اللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ {68}

Haikuwa kwa Nabii awe na mateka hadi apate dhiki katika ardhi, mnataka utajiri wa kidunia na Allah anataka akhera. Allah ni Mtukufu na ni Mwenye nguvu. Kama si Kitabu kitokacho kwa Allah basi ingekufikieni adhabu kubwa kwa yale mliyoyafanya.(Al-Anfaal 8:67-68)

Ayah hii imeteremka siku ya Badr, au baada yake katika kundi miongoni mwa masahaba. Nabii alikuwa amewataka ushauri ili kuona upeo wa kuwa kwao tayari kwa ajili ya vita-basi maoni yao yakawa ni kuteka ngamia na kilichobebwa na msafara wa Abu Sufian na wala wasipigane kama yanavyo dhihirika hayo katika Hadith ifuatayo ambapo inadhihiri ta’assub yao ya kikabila-na wao ni katika masahaba…hata mbele ya Mtume?

‘Amru amesema: “Nilimsikia Jaabir bin ‘Abdillah (r.a.) akisema: ‘Tulikuwa katika vita, Sufian akasema (maneno fulani) katika jeshi, basi mtu mmoja katika Muhajirin akampiga mtu (mwengine) miongoni mwa Ansar, yule mu-Ansar akasema: Enyi Ansar (wenzangu) na (yule mwengine katika) Muhajirin akasema: Enyi Muhajirin (wenzangu), Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akasikia hayo akasema: Huu mwito wa kijahili ni wa nini.”8

Sa’ad bin Ma’adh akasimama na kusema: “Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) nakuomba msamaha kwa hayo kama ni katika Aus tutamkata shingo lake na kama ni katika ndugu zetu wa Khazraj utatuamuru amri yako.” Akasimama Sa’ad bin ‘Ubadah naye ni bwana wa Khazraji na kabla ya hapo alikuwa ni mtu mwema, na alikuwa ameshikwa na ta’assub akasema: “Uongo hutamwua wala hilo huliwezi, akasimama Usiad bin Hadhiri akasema: “Umesema uongo Wallahi tutamuuwa, hakika wewe ni mnafiki unajadili juu ya wanafiki.

Basi ikazuka fujo kati ya Aus na Khazraj mpaka wakataka kupigana na Mtume yuko juu ya mimbar, alishuka akawatuliza hadi wakanyamaza naye akanyamaza9

Na katika Masahaba kuna baadhi yao walikuwa wanamchukia Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.), ambaye kumchukia ni alama ya unafiki kama ilivyoelezwa:

Kutoka kwa Buraydah amesema: Nabii alimtuma ‘Ali kwa Khalidi kuchukua Khums, na nilikuwa namchukia ‘Ali na alikuwa ameshaoga, nikamwambia Khalid, je humwoni huyu? Tulipofika kwa Nabii nikamweleza akasema: “Ewe Buraydah unamchukia ‘Ali?” Nikasema: “Ndiyo,” akasema usimchukie hakika yeye katika Khums ana zaidi ya hayo.”10

Na miongoni mwao kuna walio mkosoa Mtume katika kumpa uongozi Usama bin Zaid juu yao: - Kutoka kwa ‘Abdillah bin ‘Umar amesema Mtume alituma kikosi na akampa Usama bin Zaid uongozi baadhi ya watu wakakosoa katika kumpa uongozi, Nabii akasema kama mnakosoa katika uongozi wake basi mlikwishakosoa katika uongozi wa baba yake kabla yake.11

Na katika Masahaba kuna aliowatoa Nabii katika majilisi yake walipomtuhumu kwa neno baya, naye yuko katika maradhi yake ya mwisho kabla ya kuyaaga maisha ya dunia. Sa’id bin Jubayr alimsikia Ibn ‘Abbas anasema siku ya Alhamisi, ni ipi siku ya Alhamisi, kisha akalia mpaka machozi yake yakaloanisha changarawe nikasema:

“Ewe Ibn ‘‘Abbas ni ipi siku ya Alhamisi?” Akasema: “Mtume alizidiwa na maradhi yake akasema: ‘Nileteeni karatasi niwaandikie maandiko hamtapotea kamwe baada yake’, basi wakazozana na haifai kuzozana mbele ya Mtume, wakasema, ‘ana nini, anaweweseka? Muulizeni’, akasema: ‘Niacheni kwani niliyo nayo ni bora kuliko hayo mnayo niitia.” 12

Na katika Masahaba kuna waliogombania uongozi baada ya kufariki Mtume mpaka ikafikia kutaka kuchaguliwe viongozi wawili mmoja wa Muhajirin na mwingine wa Ansar.

Kisha akasema; ‘amma ba’ad, sisi ni Ansar wa Allah (s.w.t.) na kikosi cha Kiislamu na nyinyi Muhajirin ni kundi na limenyemelea kundi katika kaumu yenu basi wakawa wanataka kututoa katika msingi wetu na kutupokonya uongozi.13

Msemaji wa Ansar akasema: Mimi ni shina lake lenye nguvu na tawi lake lenye matunda akasema: Mimi ni shina lake lenye nguvu na tawi lake lenye matunda kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi, enyi Maquraish. Basi ugomvi ukawa mkubwa na makelele yakawa mengi mpaka nikatoka na kuacha ikhtilafu.”14

Na katika Masahaba kuna Abu Huraira - ambaye tumetenga nafasi yake maalumu katika sehemu ya nne - vile vile kuna Mu’awiyah bin Abi Sufian hivyo rejea tuliyoyataja kuhusiana naye katika sehemu ya kwanza kwa kuongezea hadith nne zifuatazo:-

Kutoka kwa baba yake amesema: Nabii alimtuma Khalid bin Al-Walid kwenda kwa Bani Jadhima akawalinganie Uislamu, basi hawakuweza kusema kwa ufasaha: “Aslamna (tumesilimu) wakawa wanasema: “Sabaana Sabaana” Khalidi akawa anawaua baadhi yao na kuwateka, na kutupa kila mmoja wetu mateka ilipopita siku Khalidi akaturuhusu kila mtu auwe mateka wake: “Nikasema Wallahi sitouwa mateka wangu na wala hatouwa mtu katika wafuasi wangu mateka wake, mpaka tukafika kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) tukamweleza Nabii (s.a.w.w.) akanyanyua mikono yake akasema: Ewe Allah, mimi najikinga kwako na aliyoyafanya Khalidi mara mbili.”15

Tumeona katika siku ya Hudaibiyyah yaani suluhu ambayo ilikuwa baina ya Nabii na washirikina, na kama tungeona vita basi tungepigana, akaja ‘Umar akasema, je hatuko katika haki? Na wao wako katika batili? Je, watu wetu si wataingia Jannat na watu wao wataingia Jahannam? Akasema: “Ndiyo”, akasema kwa nini tuwe wanyonge katika dini yetu na tunarudi, na Allah bado haja hukumu baina yetu?” Akasema: “Ewe mtoto wa Khattab! Mimi ni Mtume wa Allah (s.w.t.) na Allah (s.w.t.) hawezi kunipoteza kamwe.”
Akarejea akiwa na hasira, hakusubiri akamwendea Abubakr akasema: “Ewe Abubakr je, hatuko katika haki na wao wako katika batil?” Akasema: “Ewe mtoto wa Khattab, hakika yeye ni Mtume wa Allah, na allah hatampoteza kamwe.”16

Hivyo ‘Umar bin Al-Khattab hakuridhika na kupata tumaini kwa majibu ya Mtume akaenda kwa Abubakr na akaeleza upinzani wake pamoja na kwamba haijuzu Nabii kupingwa na yeyote katu.

Kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aisha (r.a.) amesema Mtume wa Allah (s.a.w.w.) aliingia kwangu nikiwa na wasichana wawili wakiimba wimbo wa jeshi, akajilaza kitandani na akageuza uso wake, akaingia Abubakr akanikemea na akasema zumari za Shetani mbele ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.), Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akamjia akamwambia waache, alipolala nikawafanyia ishara, wakatoka.”17

Habari hii haisihi kwa hali yeyote, kwa sababu Mtume haiwezekani akasikiliza zumari na muziki ukiachilia mbali hayo kutendeka ndani ya nyumba yake, wakati ambapo Abubakr anajizuia kutokana na hayo na kuyaita zumari za Shetani. Je Abubakr ni mchamungu zaidi ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.)? Na habari hii imepokewa kutoka kwa Sahaba; namna gani tutaafiki uadilifu wao na ukweli wao? Kutoka kwa Mulaikah amesema: “Ilikaribia Wema wawili kuangamia: Abubakr na Umar walinyanyua sauti zao mbele ya Nabii ulipowasili msafara wa Bani Tamim”.18

Hakika kuwa rafiki wa Nabii sio sifa kubwa kuliko utukufu wa kuoa kwa Nabii. Amesema Allah (s.w.t.) kuhusu wanawake:

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَنْ يَأْتِ مِنْكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرًا {30}

“Enyi wake wa Nabii atakayefanya miongoni mwenu uovu ulio wazi basi ataongezewa adhabu mara mbili.” (Al-Azhaab 33:30)

إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِنْ تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّهَ هُوَ مَوْلَاهُ{4}

Tubuni kwa Mwenyezi mungu kwani nyoyo zenu zimeasi na kama mtasaidiana dhidi yake basi Allah (s.w.t.) ni mlinzi wake.” (At-Tahriim 66:04)

ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا لِلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ {10}

Hadi kauli yake Allah (s.w.t.) amepiga mfano kwa wale walio kufuru, mke wa Mtume Nuh (a.s.) na mke wa Mtume Lut (a.s.) walikuwa chini ya waja wawili miongoni mwa waja wetu wema, basi wakafanya hiyana hivyo haikuwasaidia chochote mbele ya Allah (s.w.t.) na ikasemwa ingieni motoni pamoja na wenye kuingia.” (At-Tahriim 66:10)

Tazama Hadith zifuatazo zinazoweka wazi baadhi ya maana ya Ayah zilizotangulia: Kutoka kwa ‘Ubaid bin Hunain kutoka kwa Ibn ‘Abbas amesema: “Nilikaa mwaka na mimi nataka kumwuliza ‘Umar juu ya wanawake wawili ambao wamemuasi Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) basi nikawa namwogopa siku moja aliteremka sehemu akaingia katika mti wa miiba alipotoka nikamwuliza, akasema:

‘Aisha na Hafsa, kisha akasema tulikuwa katika ujahili hatuwahesabu wanawake kuwa ni chochote, ulipokuja Uislamu na Allah (s.w.t.) akawataja tukaona kuwa wana haki kwetu bila ya kuwaingiza kwa chochote katika mambo yetu na kulikuwa na maneno baina yangu na mke wangu akanikasirikia, nikamwambia: hakika wewe uko huko, akasema unaniambia mimi hayo ilihali binti yako anamwudhi Mtume wa Allah (s.a.w.w.)? Basi nikamwendea Hafsa nikamwambia na kumtahadharisha juu ya kumuasi Allah (s.w.t.) na Mtume wake.19
Kutoka kwa ‘Aisha amesema: Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa anakunywa asali kwa Zainab binti Jahshi na kukaa kwake nikaafikiana mimi na Hafsa yeyote kati yetu akiingia kwake basi amwambie, umekula maghaafiir hakika mimi nanusa kutoka kwako harufu ya maghafir, akasema hapana isipokua nilikuwa na kunywa asali kwa Zainab binti Jahshi basi sitokunywa, nimeapa na usimwambie hayo yeyote.20

Kutoka kwa ‘Aisha (r.a.): hakika wake wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) walikuwa makundi mawili kundi ambalo yumo ‘Aisha, Hafswa, Swafiyyah na Sauda na kundi jingine yumo Umm Salamah na wake wengine wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.).21

Kutoka kwa ‘Aisha (r.a.) amesema: “nilikuwa nawaonea gherah wake ambao wametoa nafsi zao hiba kwa Mtume (s.a.w.w.) na nasema: ‘Mwanamke ametoa nafsi yake?’ Basi Allah (s.w.t.) alipoteremsha Ayah isemayo (umuahirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze umtakae.

Na kama ukimtaka yule uliyemtenga basi si vibaya kwako) nikasema naona Mola wako anafanya haraka katika matamanio yako. “22

Kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Sikumwonea gherah mwanamke yeyote kama nilivyomfanyia gherah Khadija, na alikwishakufa kabla ya kunioa mimi kwa miaka mitatu, kwa yale niliyokuwa namsikia akimtaja na Mola wake alikwisha mwamuru ambashirie nyumba ya marumaru Jannat na alikuwa anachinja mbuzi kisha anatoa zawadi kwa marafiki zake.23

Kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Halah binti Khuwailid dada wa Khadija alitaka idhini kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) basi akajua kubisha hodi kwa Khadija akafanya haraka kwa hilo. Akasema (Mtume): “Ee Allah! Ni Halah huyo.” Akasema (‘Aisha): “Nikaona gherah na kusema: “Nini unamtaja kikongwe katika vikongwe wa Kiquraish mwekundu wa mashavu ameshakufa na Allah (s.w.t.) amekubadilishia aliye bora kuliko yeye?”24

Kutoka kwa Hisham kutoka kwa Baba yake kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Sikufanya gherah kwa yeyote kati ya wake wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kama nilivyofanya gherah kwa Khadija na wala sikumwona, lakini Nabii alikuwa akimtaja kwa wingi na huenda alichinja mbuzi kisha anawagawa na kuwapelekea rafiki zake Khadija, na huenda nilimwambia: “Kana kwamba hapakuwa na mwanamke duniani isipokuwa Khadija.” Akasema: “Hakika alikuwa; na nimepata watoto kutoka kwake.”25

Amesema: “Nabii alisimama alihutubia akaashiria upande wa makazi ya ‘Aisha akasema: ‘Hapa kuna fitina mara tatu, ambapo utatokea upembe wa Shetani.”26

Hakika Hadith ya mwisho ya juu inaashiria fitina ambayo ameelekezewa ‘Aisha kwa kutoka kwake kuongoza jeshi ili kumpiga vita Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) Khalifa wa Waislamu katika vita vya Jamal - rejea maelezo zaidi katika sehemu ya kwanza.

Na ambacho wanakitegemea wanaoitakidi uadilifu wa Masahaba wote ni madai yao kuwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema: “Masahaba wangu ni kama nyota yeyote mtakaye mfuata mtaongoka” na katika Hadith nyingine: “Kwa yeyote utakayechukua kauli yake...”.

Tukiachilia kuwa Hadith hii ni sahihi, na kwa kuchukulia Hadith zilizotangulia hiyo itamaanisha kuwa atakayemfuata aliyeondoka msikitini kwa ajili ya maslahi ya kidunia yenye kupita na Mtume (s.a.w.w.) amesimama akihutubia, basi atakuwa ameongoka na kwamba atakayewafuata walioacha sehemu zao ambazo Mtume aliwaamuru wasiziache kwa ajili ya kuchukua baadhi ya ngawira atakuwa ameongoka!

Na kwamba anayemfuata anaye tuhumu uongozi aliouweka Mtume (s.a.w.w.) kwa Usamah basi atakuwa ameongoka! Na kwamba anayemfuata anayepinga na kumuasi Nabii (s.a.w.w.) atakuwa ameongoka!

Hakuna shaka kwamba katika hilo kuna mgongano unao kataliwa na tabia ya kibinadamu na fitra sahihi, tukiachilia mbali kwamba kuitakidi kwetu usahihi wa Hadith hiyo ina maana ya Uma’asum wa Masahaba vile vile, kwa sababu kauli yao hiyo ni dhamana ya amri kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwa Waislamu kufuata Masahaba wote bila ya sharti au pingamizi kulingana na mafhum ya Hadith. Lakini haiwezekani Mtume kuamuru kufuatwa ambaye anaweza kufanya maasi, na kwa sababu hiyo Hadith hizo hazikubaliwi kwa yale yaliyo julikana na ni dhahiri kwamba sahaba sio ma’asum.

Hakika Hadith hizo zimezuliwa ili ziwe badala ya Hadith tukufu za Nabii (s.a.w.w.) ambazo amezitoa Al-Hakim katika Mustadark As-Sahihain kwa Sanad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas: “Amesema Mtume wa Allah (s.a.w.w.) nyota ni tumaini kwa watu wa ardhini kutokana na kughariki na Ahlul-Bayt (a.s.) ni tumaini kwa ‘Ummah wangu kutokana na ikhtilafu, basi kama kabila (lolote) la Kiarabu litawakhalifu, watakhitalifiana na kuwa makundi ya Ibilisi.”27

Na miongoni mwa athari mbaya ambazo ni matokeo ya kuitakidi uadilifu wa Masahaba wote ni kupatikana idadi kubwa ya Hadith hizo potovu katika vitabu vya Hadith kama vile Israiliyyaat, Masihiyyaat *na nyinginezo katika upotovu ambazo ndiyo mianya ya tuhuma katika dini ya Kiislamu, hiyo ni kwa sababu Hadith zimechukuliwa na kuaminiwa kwa kuwa tu zimepokewa kutoka kwa Sahaba pamoja na kuwa kuna uwezekano wa kufanya ambayo tumeyabainisha katika Hadith zilizotangulia.

*Tumeeleza mifano mingi miongoni mwa mifano ya Hadith hizi katika sehemu zilizotangulia.

 • 1. Sahih Bukhari j. 9 uk. 144, Kitabul-fitani, Babu wat-taquu fitnata-l-laa tuswiybanna-l-ladhiyna dhwalamuu minkum khaaswah.
 • 2. Sahih Bukhari j. 9 uk. 144, Kitabul-fitani, Babu wat-taquu fitnata-l-laa tuswiybanna-l-ladhiyna dhwalamuu minkum khaaswah.
 • 3. Sahih Bukhari j. 9 uk. 315, Kitabul- i’tiswaami bil-kitabi wa-s-Sunnah, Babu latat-tabi’anna man kaana qablakum.
 • 4. Sahih Bukhari j. 6 uk. 391, Kitabu-t-Tafsir.
 • 5. Sahih Bukhari j. 6 uk. 28, Kitabul -Imaan.
 • 6. Sahih Bukhari j. 6 uk. 67, Kitabu-t-Tafsir, Babu qawlihi taala - war-rasulu yad’uukum fiy ukhraakum.
 • 7. Sahih Bukhari j. 4 uk. 47, Kitabul -Jihaad, Babu qawlihi - minal-mu’miniyna rijaalun swadaquu-
 • 8. Sahih Bukhari j. 6 uk. 397, Kitabu-t-Tafsir, Babu qawlihi - sawaa’un ‘alayhim astaghfarta lahum-.
 • 9. Sahih Bukhari j. 3 uk. 508, Kitabu-sh-Shahaadaati
 • 10. Sahih Bukhari j. 5 uk. 447, Kitabul-maghaaziy, Babu ba’thi Aliyyin wa Khaalidin (r.a.) ilal-Yaman..
 • 11. Sahih Bukhari j. 5 uk. 57, Kitabu Fadhaili-s-Sahaabah, Babu manaaqibi Zayd.
 • 12. Sahih Bukhari j. 4 uk. 260, Kitabul-khumsi,Babu ikhraajil-yahuudi min jaziyratil-’arab.
 • 13. Sahih Bukhari j. 8 uk. 541, Kitabul-muharibina min ahli-l-kufri, Babu rajmi-l-hablaa mina-z-zinaa.
 • 14. Sahih Bukhari j. 8 uk. 542, Kitabul-muharibiyna min ahlil- kufri, Babu rajmi-l-hablaa mina-z-zinaa.
 • 15. Sahih Bukhari j. 5 uk. 440, Kitabul-maghaaziy.
 • 16. Sahih Bukhari j. 6 uk. 348, Kitabu-t-Tafsir.
 • 17. Sahihi Bukhari j. 4 uk. 100, Kitabul-Jihaad.
 • 18. Sahihi Bukhari j. 6 uk. 349, Kitabu-t-Tafsir.
 • 19. Sahih Bukhari j. 7 uk. 489,Kitabu-l-libaas.
 • 20. Sahih Bukhari j. 6 uk. 404, Kitabu-t-Tafsir, Babu - ayyuha-n-nabiyyu lima tuharrimu -.
 • 21. Sahih Bukhari j. 3 uk. 454, Kitabul-hibah, Babu man ahdaa ilaa swaahibihi.
 • 22. Sahih Bukhari j. 6 uk. 295, Kitabul-t-Tafsir, Babu qawlihi - turjiy maa tashaau minhunna -.
 • 23. Sahih Bukhari j. 5 uk. 104, Kitabu manaaqibil-answar, Babu taz’wiyji-n-Nabiyyi Khadiyjata wa fadhliha.
 • 24. Sahih Bukhari j. 5 uk. 105, Kitabu manaaqibil-answar, Babu taz’wiyji-n-Nabiyyi Khadiyjata wa fadhliha.
 • 25. Sahih Bukhari j. 5 uk. 104, Kitabu manaaqibil-answar, Babu taz’wiyji-n-Nabiyyi Khadiyjata wa fadhliha.
 • 26. Sahih Bukhari j. 4 uk. 217, Kitabul Khumsi, Babu maa jaa’a fiy buyuuti az’waaji-n-Nabiy.
 • 27. Mustadrak As- Sahihain j. 3 uk. 149.

Sehemu Ya Tatu: Shi'a Na Qur'an Tukufu

Shi'a wanaitakidi kuwa (Qur'an ni wahyi wa kimungu ulioteremshwa kutoka kwa Allah -swt- katika ulimi wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kwa kubainisha kila kitu, nayo-Qur'an hiyo-ni muujiza wa milele ambao wanadamu wameshindwa kupambana nao katika balagha, fasaha na katika ukweli na maarifa ya hali ya juu, haiguswi na mabadiliko, mageuzi wala upotovu, na hii ambayo iko mikononi mwetu tunayoisoma ndiyo ile ile Qur'an iliyo teremshwa kwa Nabii (s.a.w.w.) na atakaye dai yasiyokuwa hayo basi ni mwongo au ni mwenye kukosea au amechanganyikiwa na wote -hao- hawako katika uongofu, hakika hayo ni maneno ya Allah-swt- ambayo hayapatwi na upotovu kwa hali yoyote).1

Na amesema Sheikhul Muhadith Muhammad Al-Qummi ambaye amepewa lakabu ya As-Swaduuq: " Itikadi yetu katika Qur'an ambayo ameiteremsha Allah (s.w.t.) kwa Nabii wake Muhammad (s.a.w.w.) ni ambayo iko baina ya majalada mawili na ambayo iko kwa watu na sio zaidi ya hayo na anayetunasibishia kuwa tunasema zaidi ya haya basi ni muongo”2

Na hayo yanatiliwa nguvu na aliyoyasema Al-Bahansawiy naye ni mmoja wa wanafikra wa Ikhwanul-Muslimin: "... hakika Shi'at al-Ja'afariyyah Al- Ithna-'Ashariyyah wanaona kuwa ni ukafiri kwa anayepotosha Qur'an ambayo 'Ummah umekubaliana tangu mwanzo wa Uislam. na kwamba msahafu uliopo baina ya Ahl as-Sunnah ndiyo ule ule uliopo katika misikiti na nyumba za Mashi'a." Na anaendelea katika kumjibu (Dhahir na Khatib) kwa kunukuu rai ya As-Sayyid Al-Khui ambaye ni mmoja wa maraaj'i wakubwa wa Kishi'a katika zama hizi*:

"Iliyo mashuhuri baina ya Waislamu ni kutokuwepo upotoshaji katika Qur'an na iliyopo mikononi mwetu ni Qur'an yote iliyoteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.)".3

Ama Sheikh Muhammad Al-Ghazali anasema katika Kitabu chake Difau anil-'Aqidati wash-shariah dhidu mata'inil-mustash'riqina "Nimesikia kutoka kwa hawa miongoni mwa ambaye anasema katika majlisi za hadhara: "Hakika Shi'a wana Qur'an nyingine ambayo ni zaidi na inapunguza Qur'an yetu iliyo maarufu."

Nikamwambia: "Iko wapi hii Qur'an? na kwa nini majini na wanadamu hawakuona nakala yake kwa muda wote huu mrefu? Huu uongo ni wa nini? Kwa nini kuwasingizia watu na (kuusingizia) wahyi."4

Ama Hadith ambazo sio Sahih ambazo baadhi wanaweza kuzitegemea ambazo zinaeleza kupotoshwa kwa Qur'an na ambazo zipo katika vitabu vya Hadith katika Shi'a, hakika ni dhaifu na hazikubaliwi na mfano wake ni nyingi katika vitabu Sahih vya Ahl as-Sunnah na tutaonyesha mifano ya hayo katika Sahih Bukhari, tunatanguliza Hadith walizozipokea kuhusu kusahau Mtume (s.a.w.w.) katika baadhi ya Ayah:-

Kutoka kwa baba yake kutoka kwa 'Aisha amesema: "Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alimsikia mtu (mmoja) anasoma Surah usiku akasema: 'Allah (s.w.t.) amrehemu kwani amenikumbusha Ayah kadha wa kadha nilikuwa nimezisahau katika sura kadha wa kadha."5

Vile vile katika Sahih Bukhari ni kwamba, walipokuwa wanakusanya Qur'an hawakupata sehemu ya Surah al-Ahzab isipokuwa kwa Khuzaimah Al-Ansar na hii inapingana na ukweli unaosema kuwa Qur'an imepokewa kwa Tawaatur (na watu wengi sana) na wala sio kwa riwayah za ahad (mtu mmoja).

"Tulipokuwa tunanakili karatasi katika misahafu, niliikosa Ayah katika sura ya Ahzaab niliyokuwa namsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anaisoma (na ambayo) sikuikuta kwa yeyote isipokuwa kwa Khuzaimah Al-Ansariy, Khuzaima Al-Ansariy ambaye Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amejaalia ushahidi wake kuwa ni sawa na ushahidi wa waumini wawili".6

Na katika riwayah nyingine kutoka kwa Zayd bin Thaabit alisema: "…Niliifuatilia Qur'an yote kutoka kwenye vipande vya nguo, mifupa, magome na kwa watu waliohifadhi hadi nikakuta Ayah mbili za sura ya Tawbah kwa Khuzaimah Al-Ansariy ambazo sikuzipata kwa yeyote mwengine"7

Na miongoni mwa Hadith ambazo zinasema wazi wazi kupotoshwa kwa Qur'an ni ambayo ameipokea Bukhari, vile vile katika Sahih yake katika Hadith kutoka kwa 'Umar Al-Khattab: Alitoka 'Umar bin Al-Khattab, nilipomwona anakuja nilimwambia Sa'idi bin Zaid bin Amr bin Naufail: "Hakika leo atasema maneno ambayo hajawahi kuyasema tangu akalie ukhalifa."

Akanipinga na akasema: "Ni kipi kimekufanya udhanie kuwa atasema ambayo hajawahi kuyasema kabla yake?" 'Umar alikaa juu ya mimbari, muadh-dhin alipomaliza, alisimama akamshukuru Allah (s.w.t.) kama inavyostahiki kisha akasema: "Ammaa ba'd, hakika mimi nitawaambia maneno nimejaaliwa kuyasema na sijui huenda kifo changu kiko karibu, atakayeyaelewa na kuyafahamu basi ayasimulie pale atakapoishia na ambaye anaogopa kutoyafahamu simruhusu anisingizie.

Hakika Allah (s.w.t.) alimtuma Muhammad (s.a.w.w.) kwa haki na akamteremshia Kitabu na miongoni mwa aliyo yateremsha Allah (s.w.t.) ni Ayah ya Rajm, tulisoma na tukaifahamu.

Mtume alifanya rajm na sisi tuliifanya baada yake, naogopa watu watakapopitiwa na muda mrefu atakuja sema msemaji wao Wallahi hatupati Ayah ya rajm katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) basi wakapotea kwa kuacha faradhi aliyo iteremsha Allah (s.w.t.), na rajm katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) ni haki kwa mwenye kuzini ambaye ameoa kwa wanaume na wanawake kama ushahidi ukithibiti au akiwa mja mzito au akikiri (mwenyewe)."8

Na katika Hadith nyingine: "'Umar anatamani kuongeza Ayah hiyo ambayo ameidai kuwa imeondolewa katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) yeye binafsi. "'Umar amesema lau kama watu wasingesema 'Umar amezidisha katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) basi ningeiandika Ayah ya rajm kwa mkono wangu, alikiri Maa'iz mara nne mbele ya Nabii (s.a.w.w.) kuwa amezini basi akaamuru apigwe mawe.9

Na Ayah iliyodaiwa ni kama ilivyo katika riwayah ya Ibn Majah: "As-shaikhu wa-sh- Shaikha Idha Zanayaa farjumuhumal-battah"10

Na ukweli katika kukaganyikiwa ni kwamba Ayah ya rajm ipo katika Tawrati ya Ahlul-kitab na wala sio katika Qur'an tukufu kama alivyo kanganyikiwa 'Umar ibn al-Khattab.

'Umar amesema: "Mtume aliletewa mwanamume na mwanamke wa kiyahudi wakiwa wamezini akawaambia (wale) wayahudi, Mtawafanyaje?" Wakasema: "(hawa) tunazipaka nyuso zao masizi na tunawafedhehesha", akasema: " Nileteeni Taurati na muisome kama nyinyi ni wakweli.”Walikuja wakamwambia mwanamme katika wanaowaridhia Aa'wari (aliyekuwa na makengeza) soma, akasoma hadi akaishia katika sehemu akaweka mkono wake juu ya sehemu hiyo. Akasema (s.a.w.w.): 'Nyanyua mkono wako', akanyanyua mkono wake basi ikadhihirika Ayah ya rajm. Akasema: “Ewe Muhammad hakika ni juu yake kurujumiwa, lakini sisi tunaficha baina yetu basi akaamuru warujumiwe, basi nilimwona akiwapiga mawe."11

Na kuchanganya kati ya Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Taurati ambako 'Umar alitumbukia humo.

Mtume alimtanabahisha 'Umar alipomuona akiwa na karatasi ya Taurati mkononi mwake, Mtume alikasirika sana na akamwamuru 'Umar kutokuisoma na akasema: "Kama Mtume Musa (a.s.) angekuwepo angenifuata?"12

Pia imepokelewa kauli ya kutoka kwa 'Umar kuwa: "Kisha tulikuwa tunasoma katika Kitabu cha Allah (s.w.t.), msiwachukie baba zenu kwani ni ukafiri kwenu kuwachukia baba zenu au hakika ukafiri wenu ni kuwachukia baba zenu."13 (Yaani kuoa wake walio olewa na baba zenu). Na haifichikani kwa yeyote kuwa Ayah hii ni kama ile iliyotangulia haipatikani katika Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Tunahamia kwa Sahaba Abdallah ibn Masu'ud ambaye imepokewa kutoka kwake kuwa alikuwa anasoma Ayah ya (Wallaili idha yaghsha...) kwa kuongeza wa dhakar wal-untha, kama ambavyo inajulikana vile vile kuwa Ayah hii iliyozidi haipo katika Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Kisha akasema: "Namna gani Abdallah anasoma Wallaili idha yakh'sha, basi nikamsomea - Wallaili idha yakh'sha wannahaari idha tajallaa wadhakari wal-unthaa - akasema Wallahi alinisomea Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kutoka katika kinywa chake hadi kwenye kinywa changu".14 Na hiyo bila shaka inapingana na yaliyo pokewa kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwamba amesema katika Hadith mbili zifuatazo chini ambapo haingii akilini, Mtume (s.a.w.w.) kutuamrisha kujifunza Qur'an kwa mtu asiye na hifdhi nzuri.

Kutoka kwa Abdillahi ibn 'Umar amesema:"Huyo mtu sikuacha kuwa nampenda baada ya kumsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anasema: 'Jifunzeni Qur'an kwa watu wanne: kwa Abdillahi ibn Mas'ud …(akaanza kwaye)’15

Na amesema: "Hakika anaye pendeza kwangu sana miongoni mwenu ni mbora wenu wa tabia na akasema: Jifunzeni Qur'an kwa watu wanne: Abdallah bin Mas'ud, Salim mtumwa wa Abu Hudhaifah, Ubay bin Ka'ab na Ma'adhi bin Jabal."

Na Muslim amepokea katika Sahih yake kutoka kwa 'Aisha kwamba amesema: Ilikuwa katika yaliyo teremshwa katika Qur'an ('Ashara ridha'atim-ma'alumaatin) na Mtume amefariki ingali inasomwa katika Qur'an.16

Pia katika Muslim ni kwamba (Abu Musa Al-Ash'ari aliwatumia wasomaji wa Basra, na walikuwa wanaume mia tatu na akasema katika aliowaambia: hakika tulikuwa tunasoma Surah tuliyokuwa tunaifananisha kwa urefu na ukali na Surahal-Baraat, isipokuwa nimehifadhi baadhi yake "Lau kaana libni aadama waadiyaani min-malin labtaghaa waadiyan thaalithan, wa laa yamla'u jaufa-bni-aadama illa-t-turaab."17

Na katika Kitabu Al-Itiqan fi ulumil Qur'an cha Suyuti anataja baadhi ya riwayah kwamba Qur'an ina sura mia moja kumi na mbili tu au kwa kuongeza sura mbili Al-Hafd na Al-Khal'i...!18

Na Waislamu wote hawajui kitu kinachoitwa Suratul-hafdi wala Al-khal'i, na mengineyo yasiyo kuwa hayo mfano wa riwayah hizo dhaifu zilizopo kwa Ahl as-Sunnah na ambazo tunatosheka kwa kiasi tulichokinukuu.

Na baada ya hayo je, inajuzu kwa Shi'a kusema kuwa Qur'an ya Masunni imepungua au imezidi kwa kuwepo riwayah zinazosema hivyo katika vitabu vyao vya Hadith? Bila shaka laa! Kwa sababu kongamano la Ahl as-Sunnah ni kauli inayosema kutopotoshwa Qur'an.

Na maadamu hali ni hii, basi ni kwa nini tunaona tuhuma kali kutoka katika baadhi ya waandishi wa siku hizi katika kuwatuhumu Shi'a kwa kupotosha Qur'an kwa kupatikana tu baadhi ya riwayah dhaifu zinazosema hayo, ambazo hazikubaliwi kwao na kuna mifano ya riwayah nyingi katika vitabu sahihi vya Hadith vya Ahl as-Sunnah. Basi ambaye nyumba yake ni ya vioo asitupie mawe nyumba za wengine!

 • 1. Aqaidul Imamiyyah cha Muhammad Ridha Al-Mudhaffar uk. 41 chapa ya 3.
 • 2. I'tiqaadaatu-s-Swaduuq.
  *Amefariki mwaka 1992 AD. - 8/Safar/1413 AH.
 • 3. As-sunnatul Muftaraa 'alayhaa uk. 60.
 • 4. Difaa'un 'anil 'aqiydati wa-sh-shari'ati dhidda mataa'ini-l-mustash'riqiyna.
 • 5. Sahih Bukhari j. 6 uk. 508, Kitabu Fadhlil-Qur'an, Babu nis'yaanil-Qur'an.
 • 6. Sahih Bukhari j. 6 uk. 291, Kitabu-t-Tafsir, Babu - fa minhum man qadhaa nahbahu -.
 • 7. Sahih Bukhari j. 6 uk. 162, Kitabu-t-Tafsir, Babu - laqad jaa'akum rasuulun min anfusikum -.
 • 8. Sahih Bukhari j. 8 uk. 539, Kitabul Muhaaribina min Ahlil-kufri, Babu rajmil-hablaa mina-z-zinaa.
 • 9. Sahih Bukhari j. 9 uk. 212, Kitabul Ahkami, Babu-sh-shahaadati takuunu 'indal-haakim.
 • 10. Sunan Abi Daud
 • 11. Sahih Bukhari j..9 uk.476, Kitabu-t-Tawhid, Babu maa yajuuzu min tafsiyri-t-Tawraati.
 • 12. Haadhihi Naswihatiy ilaa kulli shi'iy cha Abi Bakari Al Jazaairiy uk.8.
 • 13. Sahih Bukhari j. 8 uk. 540, Kitabul Muhaaribina min Ahlil-kufri, Babu rajmil-hablaa mina-z-zinaa
 • 14. Sahih Bukhari j..5 uk. 63, Kitabu fadhailis-Sahaba, Babu manaaqibi 'Ammaar wa Hudhayfah.
 • 15. Sahih Bukhari j. 5 uk.70 -71, Kitabu fadhailis-Sahaba, Babu manaaqibi 'Abdillahi bin Mas'uud
 • 16. Sahih Muslim j.2 uk. 1075, Kitabu-r-radhaa', Babu-t-tahrim bikhamsi radha'aat, chapa ya Daru ih'yaai-t-turaathil-'arabiy.
 • 17. Sahih Muslim j. 2 uk.726, Kitabu-z-zakah, Babu lau anna libni Aadama waadiyayni labtaghaa thaalithan.
 • 18. Al-Ittiqaan fiy 'uluumil Qur'an cha Suyuuti.

Sehemu Ya Nne: Shi'a Na Sunnah Tukufu Za Nabii (S.A.W.W.)

Msimamo Wa Shi'a Katika Sunnah Za Mtume (S.A.W.W.) :-

Hakika katika wanayosingiziwa Shi'a kutoka kwa baadhi ya wajinga ni kwamba wao wanakataa Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), huo ni uongo ambao hakuna uongo kama huo.

Na tunanukuu baadhi ya maoni ya maulamaa wa Kisunni katika msimamo wa Shi'a katika Sunnah tukufu za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.):-

Sheikh Abu Zahrah anasema katika Kitabu chake Al-Imamu-s-Sadiq, Sunnah mutawatir ni hoja kwao bila ya kuwa na khitilafu katika kuitolea kwake hoja, na tawaturi kwao inawajibisha kuwa na elimu kamili.

Kwani kupinga hoja ya Sunnah ya Nabii iliyo pokelewa kwa tawatur kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) ni kufuru, kwa sababu ni kupinga ujumbe wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), ama kupinga hoja za kauli za maimamu ni chini ya hapo inahesabika kuwa ni ufasiki na wala sio kufr.1

Na anasema Sheikh Muhammad Al-Ghazali katika Kitabu chake Difaun 'anil -'aqidati wa-sh-shari'ati dhiddu mataa'inul-mustashriqina: "na miongoni mwa hawa waongo ni ambaye ameeneza kuwa Shi'a ni wafuasi wa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) na Sunni ni wafuasi wa Muhammad na kwamba Shi'a wanaona kuwa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ana haki zaidi kupewa utume au umekosewa na kupewa mtu mwingine na huo ni upuuzi, uzushi na uovu."

Kisha anasema: "Hakika Shi'a wanaamini utume wa Muhammad na wanaona utukufu wa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) upo katika kujumuika na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na kushikamana na Sunnah zake, na wao ni kama Waislamu wengine; hawaoni binadamu mtukufu zaidi katika walio tangulia na wanaokuja kuliko As-Sadiq - Al- amin. Vipi wananasibishiwa uongo huu."2

Na vitabu vikubwa vya Hadith kwa Mashi'a ni vinne:

1. Al-Kafi
2. Man laa yah'dhuruhul-faqih
3. Al-istibsaar
4. At-Tahdhib

Na riwayah zote katika vitabu hivi zinakubali kufanyiwa uchunguzi, kwa hiyo kuna Hadith zinazo kubalika na zisizo kubalika, na Shi'a hawasemi kuwa Hadith zote zilizopokewa katika vitabu hivyo ni Sahih, kama halii livyo kwa mashekhe wawili, Bukhari na Muslim katika vitabu vyao Sahih. Na katika Shi'a hakuna Kitabu kinacho linganishwa na Kitabu kitukufu cha Allah (s.w.t.) katika usahihi, na wala kitendo hakitimii kwa riwayah yoyote isipokuwa baada ya kufanyiwa uchunguzi, na hii ni kazi ya Maulamaa wenye jitihada katika kila zama, na kuihakiki riwayah ni kuipima kwanza katika Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Kisha kunatazamwa matin yake na Sanad yake na kulinganisha na riwayah nyingine zilizo thabiti kwa tawatur, mwisho inapimwa kiakili, na riwayah yoyote inayopungukiwa na moja ya masharti haya, basi kufanyia kazi ni mahali pa kutazama na kuidadisi.

Na katika Kitabu cha Masadirul Hadith as-Shi'ah Al-Imamiyyah, cha Allamah-Al-Muhaqiqi As-sayyid Muhammad Hussein Jalali, katika kuzigawa Hadith za al-Kaafi anasema:-

Jumla ya Hadith ambazo zipo humo ni Hadith 16,121, kati ya hizo Hadith 9,485 ni dhaifu, Hadith 114 ni Hasan, Hadith 1,118 ni mauthuq, Hadith 302 ni qawiyu (zenye nguvu) na Hadith 5,102 ni Sahih.

Na hii ina dhihirika wazi namna gani ambavyo Maulaama wa Kishi'a wamezifanya maelfu ya Hadith kuwa dhaifu katika Kitabu cha Al-Kaafi. Uko wapi sasa ukweli wa (yale) waliyoshikamana nayo baadhi ya waongo mfano wa Dhahiriy na Al-Khatib wanaosema kuwa Kitabu cha Al-Kaafi ni kama Sahih Bukhari kwa Masunni, kisha wanadai kuwa jina lake ni Sahih Al- Kaafi, huu ni uongo ulio wazi.

Wengi wanakariri katika vitabu vyao vyenye sumu kwa lengo la kumpoteza msomaji, kwa kuongeza sifa ya usahihi katika riwayah dhaifu walizo zichukua kwenye Al-Kaafi au kwenye vitabu vinginevyo katika vitabu vya Hadith vya Shi'a kwa kusimamisha hoja juu yao na kuwa ni ushahidi kwao.

Na wao hawapingi Hadith zote za Sahih Bukhari na Muslim, kama baadhi wanavyodai, lakini wao wana masharti yao maalumu katika kuikubali riwayah - kama ilivyotangulia - na hiyo ni kwa udadisi wao katika kuamini, kunukuu, na kuthibitisha.

Na kuna Hadith nyingi ambazo wanashirikiana baina yao na Masunni ambazo zimepokelewa katika Sahih mbili na vinginevyo, ambapo matin ni moja ingawa Hadith imepokelewa kwa Sanad tofauti tofauti, na ikhtilafu sio katika hoja yake, bali ni katika kuthibiti kwake au kutothibiti kwake.

Kuondoa Shaka Kuhusu Uma'asum Wa Mtume Muhammad Mustafa (S.A.W.W.)

Hakika Shi'a wanazitukuza Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na wanaona ni ukafiri kwa anayepinga hukumu aliyoitoa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na wanaona kwamba katika shakhsiyyah (utu) ya Nabii kuwa yeye ni bora wa waliotangulia na wajao.

Na wanaona ni lazima kushikamana na Maimamu kumi na wawili wa Ahlul Bayt (a.s.), kwa sababu wao ni njia zinazoaminika zaidi katika kunukuu Sunnah ya Nabii (s.a.w.w.), na wao wanaondoa shaka yoyote ambayo inahusu mas'ala ya Uma'asum wa Nabii na wanakanusha wanayo yaitakidi watu wengine miongoni mwa Waislamu.

Kuhusu uwezekano wa Nabii kusahau, kukosea na kusahau kwake Qur'an na kuathirika na uchawi hadi asijue kuwa amefanya kitu fulani au hakukifanya, na mengineyo yasiyo kuwa hayo miongoni mwa uongo kama utakavyoyaona katika riwayah zifuatazo alizozipokea Bukhari, ambazo tunaanza kwa yale waliyo yapokea kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), kwamba hakuwa anajua kuwa alichoteremshiwa katika pango la Hira ulikuwa ni Utume.

Kama asingekuwa Waraqa bin Naufal (Mnasara) ambaye alimfahamisha hayo: "Mpaka akaingia kwa Bi. Khadija na akasema-: "Nifunikeni, nifunikeni, basi wakamfunika hadi woga ukamtoka akasema: Ewe Khadija nimepatwa na nini?"

Kisha Bi.Khadija akamchukua hadi kwa Waraqah bin Naufal bin Asad bin Abdul-'Uzza bin Qusay naye ni mtoto wa Ami wa Khadija, ndugu wa baba yake na alikuwa ni mtu aliyeingia katika Unasara katika zama za ujahili.

Na alikuwa anajua kuandika maandishi ya Kiarabu na alikuwa anaandika Injili kwa lugha ya Kiarabu ambapo Allah (s.w.t.) amemjaalia na alikuwa ni mzee mkubwa kwa umri na alishapofuka, Bi.Khadija akamwambia:

"Ewe mtoto wa Ami sikiliza kutoka kwa mtoto wa ndugu yako." Waraqah akasema:- "mtoto wa ndugu yangu unaona nini?" Nabii akamweleza aliyoyaona, Waraqah akasema:- "Huyu ni Namusi (Jibraili) ambaye aliteremshwa kwa Mtume Musa (a.s.), natamani ningekuwa kisiki niwe hai wakati watakapo kufukuza Kaumu yako."

Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akasema: "Wao watanifukuza?"3 Riwayah inaendelea kwa yanayoshangaza zaidi kuliko hayo Waraqah bin Naufal alipomkuta Mtume akijaribu kujinyonga kwa sababu ya huzuni yake kwa kukatika Wahyi, kama si Jibrail kumtuliza mara hii baada ya kuwa Waraqah bin Naufal akifanya hivyo.

Kisha Waraqah hakuchukua muda akafariki, na Wahyi ukakatika kwa muda na Nabii akahuzunika. Ambapo katika yaliyo tufikia mara nyingi huzuni ilipelekea kutaka kujirusha kutoka katika vilele vya milima, lakini kila alipopanda mlima ili ajiangushe Jibrail (a.s.) alimtokea na akamwambia; "Ewe Muhammad hakika wewe ni Mtume wa kweli wa Allah (s.w.t.)." Basi kwa hayo inapoa hasira yake na nafsi yake inatulia na anarudi, na unaporefuka muda wa kutopata Wahyi anarudia hayo, na anapofika kwenye kilele cha mlima Jibrail (a.s.) anamtokea na kumwambia mfano wa aliyomwambia.4

Vile vile wamepokea kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakuwa amehifadhi Qur'an yote iliyoteremshwa kwake, vile vile kusahau kwake kusali Sala ya 'Alasiri kwa wakati wake. Nabii alimsikia mtu anasoma msikitini akasema: "Allah (s.w.t.) amrehemu kwani amenikumbusha Ayah kadha nilizozisahau katika Surah kadha wa kadha.5

Abu Salamah anasema: "Jaabir bin Abdullah ametueleza kwamba Nabii alijiwa na 'Umar ibn Al- Khattab siku ya Khandaq akasema:
Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) Wallahi sikusali hadi jua lilipokaribia kuzama na hiyo ni baada ya kufuturu mwenye kufunga, Nabii akasema Wallahi sijasali (laasiri), basi Nabii akateremka jangwani na mimi niko pamoja naye akatawadha kisha akasali sala ya alasiri baada ya kuzama jua kisha akasali magharibi baada yake.6 Pia kutangulia kwake na kuwa Imam wao katika sala hali ana janaba na kusali kwake adhuhuri raka'a mbili.

Kutoka kwa Abu Huraira amesema:- Sala ilikimiwa na safu zikanyooshwa akatutokea Mtume wa Allah (s.a.w.w.) aliposimama katika msala wake akakumbuka kuwa ana janaba, akatuambia simameni hivyo hivyo, kisha akarejea akaoga kisha akatoka na kichwa chake kinadondoka maji akatoa takbira ya kuhirimia sala, basi tukasali pamoja nae.7

Kutoka kwa Abu Huraira amesema: Nabii alitusalisha adhuhuri raka'a mbili, kisha akatoa salamu, kisha akasimama kwenye ubao mbele ya msikiti na akaweka mkono wake juu yake, na miongoni mwa watu waliokuwepo siku hiyo ni Abubakr na 'Umar, wakatoka kumweleza na watu wakatoka haraka wakasema: Je sala imepunguzwa? Na katika watu, alikuwepo mwanamume, Nabii (s.a.w.w.) alikuwa anamwita Dhal-yadayni, akasema:- "Ewe Nabii wa Allah, je umesahau au imepunguzwa?" Akasema:-"Sikusahau wala haikupunguzwa." Wakasema; "bali umesahau Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.)."

Akasema:- "amesema kweli Dhul-yadayni." Basi akasimama akasali raka'a mbili, kisha akatoa salamu, kisha akatoa takbira na akasujudu mfano wa Sajdah yake au alirefusha zaidi, kisha akanyanyua kichwa chake na akatoa takbirah, kisha akasujudu kama anavyosujudu, au alirefusha zaidi, kisha akanyanyua kichwa chake na akatoa takbirah.8

Kisha mambo yanafikia hadi mmoja wa mAyahudi kuweza kumroga Nabii mpaka Nabii akawa anaona kuwa amefanya jambo fulani na hakulifanya na kumuuliza kwake 'Aisha, wahyi umeteremshwa kwake au haukuteremshwa na je amemwingilia mkewe au laa!?

Kutoka kwa 'Aishah (r.a.): " …siku moja Mtume (s.a.w.w.) aliniambia: 'Ewe 'Aisha hakika Allah (s.w.t.) amenitatulia jambo ambalo nilimuuliza; wamenijia wanaume wawili mmoja wao akakaa miguuni mwangu na mwingine kichwani mwangu aliye kuwa miguuni mwangu akamwambia aliye kichwani mwangu:- Mtu (huyu) ana nini? Akasema amerogwa, akasema:- Nani amemroga? Akasema:- Labid bin A'asam.”9

Kutoka kwa 'Aisha amesema: - "Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alilogwa hadi alikuwa anapagawa kuwa amefanya kitu kumbe hakukifanya hadi siku moja alipokuwa kwangu alimwomba Allah (s.w.t.) akamjibu, kisha akasema ewe 'Aisha umehisi kuwa Allah (s.w.t.) amenijibu nilivyomuomba."10

Nabii alibaki siku kadhaa wa kadha amepagawa kuwa amemwingilia mke wake na wala hakumwingilia.11 Sheikh Muhammad Abduh amezipinga riwayah hizi ambazo zinasema kuwa Mtume aliathiriwa na uchawi kwa sababu zinapinga kauli yake Allah (s.w.t.) (Na wamesema madhalimu hawamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa).12

Na kuhusu uhusiano wa Mtume (s.a.w.w.) na wake zake; wamepokea yafuatayo:- "Ametusimulia Abu Usamah kutoka kwa Hisham kutoka kwa baba yake.

'Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alipokuwa katika maradhi yake alikuwa akizunguka kwa zamu kwa wake zake na anasema:- Kesho nitakuwa wapi kisha nitakuwa wapi?' kwa kuipupia nyumba ya 'Aisha. 'Aisha akasema ilipofika zamu yangu akatulia".13
Kutoka kwa Dhahari kutoka kwa Ur'wah kutoka kwa 'Aisha amesema:- "Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa anapotaka kusafiri anapiga kura baina ya wake zake yeyote atakaye bahatika anatoka pamoja naye na alikuwa anagawa kwa kila mke kati yao mchana na usiku wake isipokuwa Sauda bint Zam'ah alitoa hiba (zawadi) ya mchana na usiku wake kwa 'Aisha mke wa Nabii kwa kutaka katika hilo radhi ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.)."14

Tazama mgongano baina ya riwayah mbili za juu na riwayah mbili za chini yake. Amesema Anas ibn Malik: "Nabii alikuwa anazunguka kwa zamu kwa wake zake kwa saa moja wakati wa usiku na kwa saa moja wakati wa mchana na wao walikuwa kumi na moja. Akasema: nikamuuliza Anas, Je, alikuwa anaweza? Akasema (Anas) tulikuwa tunasema kuwa yeye amepewa nguvu za watu thelathini."15

Kutoka kwa Anasi:- "Hakika Nabii alikuwa akizunguka kwa wake zake wote kwa usiku mmoja na alikuwa na wake tisa."16

Kwa kutegemea riwayah zilizo tangulia na mfano wake baadhi ya Waislamu wamechukua itikadi yao kwa kujuzu Nabii kukosea, kusahau na mengineyo yasiokuwa hayo. Vivyo hivyo Mtume kwa mtazamo wao ni maasumu katika mambo ya kidini au tablighi tu, na katika yasiokuwa hayo ni kama watu wengine anakosea na kupatia, na wala sijui mpangilio huu umetoka wapi? Hakika Allah (s.w.t.) ametuamuru sisi kumfuata Mtume katika kila kitu bila ya kuweka sharti wala kikwazo chochote kwa kusema:-

وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ {3}

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ {4}

"Na hatamki kwa matamanio yake isipokuwa ni wahyi unaofunuliwa."(An-Najm 53: 3-4)

Vile vile kauli yake:-

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا ۚ{7}

"Alichowaletea Mtume kichukueni na alichowakataza kiacheni."(Al-Hasyr 59:07)

Inaonyesha amri ya jumla bila ya kuwa ni mahsusi na bila ya kuwa na sharti, kama itajuzu Nabii kukosea, basi Allah (s.w.t.) atakuwa ametuamrisha kukosea; na tunajilinda kwa Allah (s.w.t.) kusema mfano wa hayo. Kwa hiyo Allah (s.w.t.) kutuamrisha sisi kumfuata Mtume kwa ujumla bila ya sharti wala kikwazo, ina maana kwamba, Mtume hakosei kabisa katika kauli zake na vitendo vyake vyote na kukiri kwake.

Sasa umetokea wapi mgawanyo huo ambao wanaudai katika Uma'asum wa Nabii? Je, Mtume kutokujua wahyi ambao umeteremshwa kwake katika pango la Hira ni jambo la kidunia? Je, kusahau kwake Qur'an ni jambo la kidunia? Je baadhi ya watu kumroga Nabii ni jambo la kidunia?

Hakika itikadi yetu kwa Uma'asum wa Nabii kwa jumla ndiyo msingi wetu katika kukataa riwayah zilizo tangulia kwa sababu ni katika yanayopinga Uma'asum wake.

Na Ismah ni kutakasika kutokana na dhambi, maasi madogo, makubwa na kutokana na kukosea na kusahau na kwa kuongezea katika uma'asum wa Nabii baada ya kupewa Utume, hakika ni lazima awe mwaminifu, mkweli na mwenye kuepukana na uovu mkubwa na mdogo na kabla ya kupewa Utume vile vile, ili nyoyo zipate utulivu kwake na nafsi zimwandame na kwa hayo anakuwa ni mwenye kustahiki cheo hiki kitukufu cha Allah (s.w.t.).

Hakika kupenya riwayah ambazo zinagusa Uma'asum wa Nabii (s.a.w.w.) kwa kuongezea kuwa zimewekwa na waongo ambapo zinachukuliwa kuwa ni tuhuma katika dini ya Kiislamu, kuna dhana ya kuwa kuna sababu nyingine kati ya hizo, ni kwa maslahi ya kuunga mkono misimamo ya baadhi ya Masahaba walipomwambia Mtume kuwa anaweweseka - naye yuko katika maradhi yake ya mwisho - alipowataka wamletee karatasi awaandikie ili wasipotee kamwe baada yake - rejea tuliyo yaandika kuhusu huzuni ya siku ya Alhamisi katika sehemu ya kwanza - Hivyo hakuna mshangao baada ya hayo, kuwepo kwa baadhi ya riwayah ambazo zinafanya Sahaba apatie katika mas'ala ambayo Nabii (s.a.w.w.) amekosea; tunajikinga kwa Allah (s.w.t.).

Na miongoni mwa riwayah hizi ni ambazo zimenasibishwa na jambo la kuteremka Ayah ya hijab baada ya 'Umar Al-Khattab kumtanabahisha Mtume wa Allah (s.a.w.w.) juu ya ulazima wa kuvaa hijab.

Kutoka kwa Humaid kutoka kwa Anas: amesema 'Umar (r.a.), Nilisema:- "Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anaingia kwako mwema na mwovu je isingekuwa vyema uwaamuru mama wa waumini kuvaa hijab? Basi Allah (s.w.t.) akateremsha Ayah ya hijab."17

Na katika riwaya nyingine 'Umar Al-Khattab alikuwa anamwambia Mtume wa Allah (s.a.w.w.):- "Wavalishe wake zako hijabu." ('Umar) Akasema:- "Hakufanya hivyo (Mtume s.a.w.w.).

Basi Allah (s.w.t.) akashusha Ayah ya hijab." Na wake wa Nabii (s.a.w.w.) walikuwa wanatoka usiku hadi usiku kwenda kujisaidia, basi alitoka Sauda binti Zam'ah na alikuwa ni mwanamke mrefu, 'Umar bin Khattab akamwona naye yuko katika majlisi, akasema tumekujua ewe Sauda, kwa kupupia hijabu iteremshwe, basi, Allah (s.w.t.) Mtukufu akateremsha Ayah ya hijabu.18

Vile vile yaliyonasibishwa kuhusu Ayah ya kukataza kuwasalia wanafiki kwamba imeteremka kuunga mkono msimamo wa 'Umar, baada ya Mtume (s.a.w.w.) kung'ang'ania kumsalia Ibn 'Ubay mnafiki, na kutosikia kwake upinzani wa 'Umar juu ya hilo kama wanavyopokea.

Amesema:- Alipokufa 'Abdallah bin 'Ubay mtoto wake alikuja kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akasema: "Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) nipe nguo yako nikamvike sanda, msalie na mwombee maghfira", akampa nguo yake, na akamwambia, "ukimaliza tuite," alipomaliza akamwita akaja ili amsalie, 'Umar akamvuta na akasema: "Je, Allah (s.w.t.) si amekukataza kuwasalia wanafiki? Akasema uwaombee maghfira au usiwaombee, kama utawaombea maghfira mara sabini, Allah (s.w.t.) hatawasamehe," Ikateremka Ayah - wala usimsalie yeyote akifa miongoni mwao kabisa wala usisimame katika kaburi lake - basi akaacha kuwasalia.19

Kutoka kwa 'Umar al-Khattab ni kwamba amesema:- "Alipokufa 'Abdallah bin 'Ubay bin Salul, Mtume wa Allah (s.a.w.w.) aliitwa kwenda kumsalia, Mtume (s.a.w.w.) aliposimama nilimrukia nikasema:- "Ewe Mtume wa Allah, unamsalia mtoto wa 'Ubay?" Na siku moja alisema kadha wa kadha nikamtajia kauli yake. Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akatabasamu na akasema niachie ewe 'Umar, nilipozidi kumwambia akasema hakika mimi nimepewa hiari."20

Basi nikachagua, kama ningejua kuwa nikimzidishia mara sabini kuwa atasamehewa ningezidisha. Akasema: Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akamsalia kisha akaondoka hakukaa isipokuwa muda mchache zikateremka Ayah mbili katika Surah ya Baraat; "wala msimsalie yeyote miongoni mwao akifa kamwe hali na wao ni mafasiki."

Akasema:- Nikastaajabu baada ya kumkaripia Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na ukweli ni kwamba katika tukio hilo Mtume alipewa hiari kuwasalia wanafiki na kuwaombea msamaha kwa kauli yake Allah (s.w.t.):

اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِنْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ{80}

" Waombee msamaha au usiwaombee, na hata kama utawaombea mara sabini basi Allah (s.w.t.) hatawasamehe"(At-Taubah 09:80)

Na Mtume alichagua kumsalia mnafiki huyo kwa sababu ya kupatikana faida kubwa na maslahi yanayo patikana kwa kuizoeza kaumu yake ya Khazraj na kwa sababu hiyo walisilimu watu elfu moja, na sala yake kwa mnafiki huyo ilikuwa kabla ya kushuka Ayah ya kukataza hilo na Ayah ya (waombee msamaha au usiwaombee...) haionyeshi kukataza ambako alikufahamu 'Umar na akampinga Mtume, na kwa sababu hiyo akamtia makosani.

Na kuteremka Ayah ya kukataza kuwasalia wanafiki haionyeshi kosa kwa Mtume (s.a.w.w.) kumsalia Abdallah bin 'Ubay – na tunajikinga kwa Allah (s.w.t.) kama walivyo fahamu baadhi.

Sala yake kwa mnafiki itakuwa ni makosa kama angeisali baada ya kuteremka Ayah ya kukataza, na wala sio kabla yake. Wala haifahamiki katika Ayah hii isipokuwa kosa la 'Umar na upinzani wake mkali kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kama ambavyo 'Umar alitambua hilo na akajuta kwa pupa yake ambapo inaonekana kuwa amesema:- "Nimefanya kosa katika Uislamu ambalo sikufanya kamwe kosa mfano wa hilo. Mtume (s.a.w.w.) alitaka kumsalia Abadallah bin ‘Ubay nikamvuta nguo na kumwambia:- Wallahi hakukuamrisha Allah (s.w.t.) kwa hili?"

Allah (s.w.t.) amekwishakuambia 'uwaombee msamaha au usiwaombee...' Akasema Mtume wa Allah (s.a.w.w.):- Allah (s.w.t.) amenipa hiari akasema:- 'waombee msamaha au usiwaombee msamaha…' basi nikachagua (kuwaombea msamaha)21

Na kabla ya hayo ni yale yanayoonekana katika kuchukua fidia kutoka kwa mateka siku ya Badr na kwamba Ayah:

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ {67}

"Haimpasi Nabii kuwa na mateka mpaka apigane na kushinda katika nchi mnataka utajiri wa kidunia na Allah ni Mwenye nguvu Mwenye hekima, isingelikuwa hukumu kutoka kwa Allah basi ingekufikieni kwa yale mliyo yachukua adhabu kubwa."(Al-Anfaal 08:67)

Imeteremka kumlaumu Mtume kama baadhi wanavyodai - kwa sababu ya kuchukua kwake fidia kutoka kwa mateka wa Badr na kutokuwauwa kwake wakati ambapo 'Umar bin Khattab alikuwa anataka wauliwe wote, basi Ayah ikateremka ikiunga mkono rai ya 'Umar na wakapokea riwayah inayounga mkono rai yao, kauli ya uongo waliyoizua kutoka kwao na wakainasibisha kwa Mtume (s.a.w.w.) kulingana na maana ya Ayah iliyotangulia ambayo ina makemeo ya adhabu kali, lakini makemeo hayo ni kwa ajili ya nani? kama ambavyo wanapokea na kunasibisha kwa Mtume (s.a.w.w.)kuwa amesema alipokuwa analia pamoja na Abubakr "ilikaribia kutugusa adhabu kubwa kwa kumkhalifu mtoto wa Khattab na kama ingeteremka adhabu basi asingepona kutokana na adhabu hiyo isipokuwa mtoto wa Khattab."

Na ukweli wa tukio hili ni kwamba Ayah iliyotangulia imeteremka kabla ya vita vya Badr na kuwakemea Masahaba ambao walifadhilisha biashara na kilichobebwa na msafara wa Abu Sufiani kuliko kupigana.

Wakati Mtume alipowataka ushauri kwa ajili ya suala hilo ili aone upeo wa kuwa kwao tayari katika kuwapiga vita washirikina, kukataza katika Ayah sio kukataza moja kwa moja kwa Nabii kuchukua mateka bali ni kukataza kuchukua bila ya kuwapiga vita washirikina kama walivyokuwa wanataka baadhi ya Masahaba, wakati Mtume (s.a.w.w.) alipo washauri kuteka msafara wao au kuwapiga vita kabla ya Badr, namna gani itaingia akilini kuwa Ayah hiyo ambayo ina wakemea wale ambao hawataki vita katika ardhi - kuwa imeteremka kwa kumkemea Mtume (s.a.w.w.) na amekwisha wapiga washirikina na kuwauwa mauwaji makali kabisa! Katika vita hivyo waliuliwa mashujaa sabini wa Kiquraish.

Abu Huraira Na Wingi Wa Riwayah Zake Katika Hadith

Wapokezi wa Hadith wameafikiana kuwa Abu Huraira alikuwa ni Sahaba aliyepokea Hadith nyingi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) wakati ambapo hakuandamana na Nabii isipokuwa mwaka mmoja na miezi tisa-au miaka mitatu kwa riwayah za mbali kabisa-Sahih za Ahl as-Sunnah zimepokea kutoka kwake Hadith elfu tano mia tatu na sabini na nne (5,374) kati ya hizo Bukhari amepokea Hadith 466.

Lakini Abu Huraira mwenyewe anasema hakika 'Abdulah ibn 'Umar alikuwa amepokea Hadith nyingi zaidi kuliko yeye na alikuwa Ibn 'Umar anaandika na yeye (Abu Hurayrah) alikuwa haandiki.

Abu Huraira mwenyewe anasema: "Hakuna yeyote katika Masahaba wa Nabii mwenye kupokea Hadith nyingi kuliko mimi isipokuwa Abdullah ibn 'Umar kwani yeye alikuwa anaandika na mimi siandiki." Anafuatiwa na Ma'amar. Imepokewa kutoka kwa Hammam.22

Isipokuwa Hadith zote alizozipokea Ibn 'Umar ni 722 na Bukhari hakuzitoa isipokuwa
Hadith saba tu na Muslim ameandika Hadith 20 tu. Na Abu Huraira mwenyewe amebainisha sababu ya kuandamana kwake na Mtume kwa wingi.

Kutoka kwa Shihabu kutoka kwa Al-A'aray kutoka kwa Abu Huraira amesema: "Wanasema kuwa Abu Huraira anahudhuria sana na wanasema: Muhajirin na Ansari wana nini mbona hawapokei mfano wa Hadith zake, hakika ndugu zangu katika Muhajirin walikuwa wanashughulishwa na bidhaa katika masoko na ndugu zangu katika Ansari walikuwa wanashughulishwa na kuchunga mali zao na mimi nilikuwa mtu maskini namwandama Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa ajili ya kujaza tumbo langu, hivyo nahudhuria wanapoghibu (wanapokuwa hawapo) na nakumbuka wanaposahau.23

Na yafuatayo yanatia mkazo riwayah ya juu na kukiri Abu Huraira sababu ya kuwasomea Qur'an baadhi ya Masahaba.

"Kutoka kwa Sa'id Al-Maqbariya kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika watu walikuwa wanasema Abu Huraira amepokea Hadith nyingi, hakika mimi nilikuwa namwandama Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa ajili ya kushibisha tumbo langu ili nisile uchafu na nisivae ngozi na wala asije akanihudumia fulani na fulani na nilikuwa nikifunga mawe kwenye tumbo langu kutokana na njaa, na nilikuwa simsomei mtu Ayah na hali niko nayo ili aninyenyekee na kunilisha, na mtu bora kwa masikini alikuwa ni Ja'afar ibn Abu Talib, alikuwa anatuhurumia na kutulisha kile kilichopo katika nyumba yake hadi alikuwa anatutolea chombo ambacho hakina kitu, basi tunakipasua ili tulambe kilichomo humo."24

Na katika kumpenda kwake Ja'afar ibn Abi Talib ambako kumebainishwa katika riwayah ya juu imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kwamba amesema hakuvaa viatu wala kupanda wanyama wala hakutembea juu ya ardhi baada ya Mtume aliye bora kuliko Ja'afar ibn Abi talib25

Na ameipokea Muslim katika Sahih yake kuwa 'Umar al-Khattab alimpiga Abu Huraira aliposikia anasimulia kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.): "Mwenye kusema laa ilaha illallah ataingia Jannat (peponi)26

Na amepokea Abdi bar kutoka kwa Abu Huraira mwenyewe anasema: "Nimewasimulia Hadith kama ningewasimulia zama za 'Umar al- Khattab basi angenipiga 'Umar kwa upanga."27

Na yanayotilia mkazo hayo ni alioyasema Faqihil-Muhadithiin Rashid Ridhaa: "Kama umri wa 'Umar ungekuwa mrefu hadi akafa Abu Huraira basi Hadith hizo nyingi zisingetufikia,"28

Na anasema Mustafa Sadiq Ar- Raafi'i; "basi akawa kwa hilo (yaani Abu Huraira) ni mpokezi wa kwanza kutuhumiwa katika Uislam."29

Wakati vilipotokea vita vya Siffin baina ya Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) na Mu'awiyah bin Abi Sufian, Abu Huraira alikimbilia kwa Mu'awiyah bin Abi Sufian naalilipwa kwa upokezi wake mzuri wa Hadith na kuwanusuru kwake Bani 'Umayyah wakamneemesha. Marwan Al-Hakim alikuwa anamfanya naibu wake katika Ugavana wa mji wa Madina basi hali yake ikabadilika kutoka hali ya umaskini kwenda kwenye hali ya utajiri. Imepokelewa kutoka kwa Ayyub bin Muhammad kuwa amesema:

Tulikuwa kwa Abu Huraira na ana vipande viwili vya nguo vilivyo fumwa kwa kitani akivivaa akasema, 'hongera, hongera, Abu Huraira anavaa katani? Hakika uliniona mimi niko wa mwisho baina ya mimbar ya Mtume (s.a.w.w.) na chumba cha 'Aisha nimezimia anakuja anayeingia anaweka mguu wake juu ya shingo langu na ninaonekana kuwa mimi ni kichaa na wala sina kichaa, sikuwa na kitu isipokuwa njaa”30

Na matokeo ya kujiunga kwake na Bani 'Umayyah ilikuwa ni kwa kuficha kwake baadhi ya Hadith ambazo alikuwa anazisikia kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na hofu yake kwa ajili ya nafsi yake kutokana na kuuliwa katika hali ya kuzisimulia.

Kutoka kwa Abu Huraira amesema:- "Nimehifadhi kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) mikoba miwili, mmoja wapo nimeutoa na mwingine kama ningeutoa ningekatwa hili koo."31

Kukiri huku kunapinga kauli yake nyingine kuwa yeye hakuwa anaficha Hadith kwa ajili ya kumwogopa Allah (s.w.t.). Kutoka kwa A'araji kutoka kwa Abu Huraira amesema:- "Hakika watu wanasema Abu Huraira amepokea kwa wingi kama isingekuwa Ayah mbili katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) nisingesimulia Hadith, kisha akasoma:- Hakika ambao wanaficha tuliyo yateremsha katika ubainifu… Mwingi wa Rehema."32

Na ukamilifu wa Ayah mbili katika riwayah zilizotangulia ambazo Abu Huraira hafichi Hadith kwa sababu yake ni:-

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنْزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِنْ بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ {159}

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ {160}

"Hakika ambao wanaficha tuliyoyateremsha katika ubainifu na uongofu baada ya kuubainisha kwa watu katika Kitabu, basi hao Allah anawalaani na wanawalaani wenye kulaani isipokuwa wale walio tubu na wakafanya wema na wakabainisha hao nitawasamehe na mimi ni Mwenye kusamehe Mwingi wa rehema."(Al-Baqarah 02:159-160)

Baada ya kunukuu mifano ya riwayah hizi, ambazo zinabainisha uhakika wa Abu Huraira na daraja la uadilifu wake na uaminifu wake katika kupokewa Hadith, inadhihirika wazi sababu ya Mashi'a kukataa riwayah zake, jambo ambalo limewafanya baadhi ya watu kuwatuhumu Shi'a kwa sababu hiyo. Na hiyo sio jingine isipokuwa ni kuzidisha kipimo, hatuoni kisingizio kinachokubaliwa hususan pamoja na kuwepo dalili zote hizo ambazo zinathibitisha usahihi wa tuliyoyasema.

Katika Ikhtisaru Ulumil-Hadith amesema Ibn Hambal, Abubakr Al- Humaydiy na Abubakr As-Swayrafiy: " Hatukubali riwayah ya aliyesema uongo katika Hadith za Mtume wa Allah (s.a.w.w.) hata kama atatubu na kuacha uongo wake baada ya hapo."33

Na amesema As-Sam'aaniy:- "Mwenye kusema uongo katika habari moja ni wajibu kuporomoa yaliyo tangulia katika Hadith yake".34

Tunaorodhesha katika yafuatayo baadhi ya riwayah za Abu Huraira ambazo amezipokea Bukhari katika Sahih yake. Tunaanza na Mtume Musa (as) kumng'oa jicho Malaika wa mauti.

Kutoka kwa Ibn Twaus kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abu Huraira amesema: - Malaika wa mauti alitumwa kwa Mtume Musa (a.s.) alipomwendea akampiga na akamng'oa jicho, basi akarejea kwa Mola wake akasema umenituma kwa mja wako asiyetaka mauti, Allah (s.w.t.) akamrudishia jicho lake na akasema: Rudi na mwambie aweke mkono wake juu ya mgongo wa ng'ombe dume, basi atapata - kwa kila unywele utakaofunikwa na mkono - mwaka mmoja, (Musa akasema): Ewe Mola kisha nini? Akasema:- Kisha mauti akasema basi iwe sasa hivi, basi akamwomba Allah (s.w.t.) amkurubishe na ardhi tukufu Baitul Muqaddas kiasi cha umbali wa kutupa jiwe."35

*Kutoka kwa Muhammad kutoka kwa Abu Huraira ni Marfu’u: Jahannam itaambiwa je, umejaa itasema Je? Kuna ziada? Allah (s.w.t.) ataweka mguu wake juu yake, basi itasema: Qatu, qatu; yaani imetosha, imetosha.36

Kutoka kwa Abu Huraira (r.a.): amesema Nabii (s.a.w.w.): " kila binadamu huchomwa na Shetani ubavuni mwake kwa vidole vyake wakati anapozaliwa isipokuwa Mtume 'Isa bin Maryam alienda kumchoma, basi akachoma pazia."37

Kutoka kwa Abu Maryam: kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) amesema: " Allah (s.w.t.) amemuumba Adam kwa sura yake, urefu wake ni dhiraa sitini."38

Kutoka kwa Hawa bin Ya'asir kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) amesema: "Anayesema mimi ni bora kuliko Yunus bin Matta amekwishasema uongo."39

Kutoka kwa Salmah na Abu Abdillah Al-Aghar kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema: 'Mola wetu Mtukufu huteremka kila usiku hadi kwenye mbingu ya dunia inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku anasema: Nani atakayeniita ili nimuitikie? Nani atakayeniomba nimpe? nani atakayenitaka msamaha nimsamehe?”40

Na riwayah hii ya mwisho inafaa tusimame kwayo kidogo, ambao wanaoipokea na wanaitakidi usahihi wake, vile vile wanaitakidi kwamba Allah (s.w.t.) amekaa katika 'arsh na kwamba kuteremka kwake huku, kwa madai yao - inakuwa katika mwisho wa usiku tu, lakini kwa kujua kwetu kuwa ardhi ni duara na kuzunguka kwake, inafanya usiku uwepo ardhini kila pande kwa muda wa kuwepo kwake na kuwepo kwa binadamu juu yake na hii ina maana kuwa Allah (s.w.t.) atabaki daima katika mbingu ya dunia. Na wala sisi hatuitakidi kuwepo kwa mgongano baina ya ukweli wa kielimu na ukweli wa kiuungu.

Tukiachilia mbali mgongano huo na tunayoyaitakidi kukaa kwa Allah (s.w.t.) juu ya ''arsh, Allah (s.w.t.) yuko mbali na wanayoyasema. Allah (s.w.t.) ni Nuru ya mbingu na ardhi hana mpaka wa sehemu wala zama, na kama angekuwa amebebwa juu ya 'arsh ingelazimu mbebaji kuwa na nguvu zaidi kuliko aliyebebwa - kama ilivyopokewa kutoka kwa Ja'afar As-Sadiq (a.s.) na kwa nini ateremke na kupanda naye yuko karibu nasi kuliko mshipa wa moyo?

Na Hadith zilizotangulia ni katika Israiliyyaat ambazo Abu Huraira amezipokea kwa wingi na kutokana na kuandamana kwa wingi na Ka'ab Al-Ahbaar, Myahudi aliejidhihirisha kuamini kwake Uislamu na kwa kuongezea katika riwayah hizo:-

Kutoka kwa Abu Huraira ni kwamba Mtume amesema: "Asitembee mmoja wenu kwa kiatu kimoja hivyo aivalishe miguu yote viatu au yote aivue viatu."41 Kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika amesema Mtume wa Allah (s.a.w.w.) "Kila nabii ana ombi lake analoomba na mimi nataka niache ombi langu kwa ajili ya kuuombea shifaa 'Ummah wangu kesho akhera."42

Kutoka kwa Salamah kwamba Abu Huraira amesema: "Nilimsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anasema sisimizi alimuuma nabii miongoni mwa manabii basi, akaamua kuteketeza kijiji cha sisimizi, Allah (s.w.t.) akampelekea wahyi, sisimizi tu amekuuma ukateketeza ‘Ummah miongoni mwa 'Ummah wanao mtukuza Allah (s.w.t.)?"43

Kutoka kwa Al-A'arij kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema: "Mmoja wenu akitawadha basi aweke maji puani mwake kisha ayasambaze, na mwenye kufanya basi asali witri na akiamka mmoja wenu katika usingizi wake basi, aoshe mkono wake kabla ya kuanza kutawadha kwani mmoja wenu hajui mkono wake umelala wapi."44

Kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Nabii amesema: "Ulipotea 'Ummah katika Bani Israil haujulikani umefanya nini na mimi siuoni 'Ummah huo isipokuwa ni panya akiwekewa maziwa ya ngamia hanywi na akiwekewa maziwa ya mbuzi anakunywa."45

Hakika Abu Huraira amesema: "Sisi tulipokuwa kwa Nabii alisema kuwa wakati nilipokuwa nimelala nimeonyeshwa Jannat, basi nikamwona mwanamke anatawadha kando ya kasri nikasema kasri hii ni ya nani? Wakasema: Ya Umar al-Khattab, basi nikakumbuka gherah yake nikageuka na kurejea. 'Umar akalia na akasema: Je kwa ajili yako naonewa gherah ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.)?"46

Kutoka kwa Ata'i bin Ya'sar kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika Nabii siku moja alikuwa anasimulia na alikuwa na mwanamme katika mabedui, kwamba mtu katika watu wa Jannat alimtaka Mola wake ruhusa ya kulima, akasema: basi akapanda mbegu na ikaota mimea yake ikastawi na kaivuna, ilikuwa kama mfano wa milima, basi Allah (s.w.t.) atasema hutosheki ewe binadamu; hakika hakikushibishi kitu chochote, bedui akasema: Wallahi simwoni isipokuwa ni Mquraish au Ansar kwani wao ni wakulima ama sisi sio wakulima basi Nabii akacheka."47

Kutoka kwa A'awadh kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika Mtume (s.a.w.w.) amesema:Allah (s.w.t.) anawachekea watu wawili, mmoja wao atamuuwa mwingine, wanaingia Jannat , huyu anapigana katika njia ya Allah (s.w.t.) na kuuliwa kisha Allah (s.w.t.) anamsamehe muuwaji na kisha anakufa shahidi."48

Hakika yeye amemsikia Abu Huraira anasema kwamba yeye amemsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anasema sisi ni wa mwisho tuliyotangulia.

Na kwa isnad yake kama akichungulia katika nyumba yako yeyote na bila ya kumruhusu ukamtupia mawe na kumtoa jicho lake basi, hakutakuwa na dhambi kwako.49

Ametusimulia Abdurazaq kutoka kwa Ma'amar kutoka kwa Hamaam bin Munabih kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) amesema: " Bani Israili walikuwa wanaoga uchi baadhi yao wanawaangalia wengine na Mtume Musa (a.s.) alikuwa anaoga peke yake wakasema: Wallahi haimzui Mtume Musa (a.s.) kuoga pamoja na sisi isipokuwa ana aibu (kasoro, mshipa) siku moja alienda kuoga akaweka nguo yake juu ya jiwe, basi jiwe likakimbia na nguo yake, Mtume Musa (a.s.) akawa anakimbia nyuma yake akasema nguo yangu ewe jiwe, nguo yangu ewe jiwe, hadi Bani Israeli wakamwangalia Mtume Musa (a.s.) wakasema:
Wallahi Mtume Musa (a.s.) hana kasoro, na akachukua nguo yake akaanza kulipiga jiwe. Abu Huraira akasema: Wallahi hakika alilipiga jiwe na kulijeruhi majeraha sita au saba.”50

Ametusimulia Abul-yaman Shu'ayba ametupa habari kutoka kwa Zuhri amesema: Ametusimulia Sa'id bin Musayyab: Hakika Abu Huraira amesema: nimemsikia Mtume wa Allah (s.a.w.w.) anasema: Litaingia Jannat katika 'Ummah wangu kundi la watu sabini elfu nyuso zao zinatoa nuru kama unavyo angaza mwezi, Ukasha bin Muhsin Al Asadi akasimama ananyanyua kipande cha nguo yake akasema: "Niombee Allah (s.w.t.) anijaalie miongoni mwao." Akasema: "Ewe Allah (s.w.t.) mjaalie awe miongoni mwao, kisha akasimama mwanamume katika Ansar. Akasema: "Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) niombee Allah (s.w.t.) anijaalie niwe miongoni mwao." Akasema:'Ukasha amekutangulia.”51

Kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Nabii (s.a.w.w) amesema: wakati Ayyub alipokuwa anaoga uchi, panzi wa dhahabu akamwangukia Ayyub akamficha katika nguo yake. Mola wake akamwita: "Ewe Ayyub je sikuwa nimekutosheleza kwa unayoyaona?" Akasema: "Ndiyo kwa utukufu wako lakini sitosheki kwa baraka zako."52

Kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Nabii amesema: Wakati mwanamme alipokuwa amepanda ng'ombe alimgeukia akamwambia sikuumbwa kwa ajili hii, nimeumbwa kwa ajili ya kulima, akasema nilimwamini mimi Abubakr na 'Umar. mbwa mwitu alichukua kondoo, mchungaji akamfuata, mbwa mwitu akasema nani atamchunga siku ya saba? Siku ambayo hakuna wakumchunga isipokuwa mimi? Akasema nilimuamini mimi, Abubakr na 'Umar. Abu Salamah akasema na wao siku hiyo hawakuwa katika kaumu.53

Kutoka kwa Abu Huraira: " hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema: 'Ikiadhiniwa kwa ajili ya sala Shetani anakimbia na kutoa ushuzi ili asisikie adhana, adhana ikimalizika anarudi, sala zinapoanza kulipwa anakimbia zikishalipwa anarudi ili ahadae baina ya mtu na nafsi yake, anasema: kumbuka kadha, kumbuka kadha hataacha kusema mpaka mtu atakuwa hajui amesali raka'a ngapi”54

Kisimamo Pamoja Na Bukhari Katika Sahih Yake

Baada ya kueleza riwayah zilizotangulia ambazo zinagusa Uma'asum wa Nabii na kisha riwayah za Abu Huraira, imekuwa ni dharura kutupia macho juu ya Sahih ya Bukhari kwa sifa yake, ambayo imedhamini riwayah hizo na kwa sifa yake ya kuwa ni kitabu Sahih zaidi katika vitabu vya Hadith kwa Ahl as-Sunnah na ambacho wanakizingatia baada ya kitabu cha Allah (s.w.t.) katika usahihi. Na hapa ni chimbuko la siri ya upinzani wao kwa kila anayekataa Hadith iliyo pokelewa katika Sahih Bukhari, wao wanaamini kabisa usahihi wa yote yaliyopokelewa humo.

Bukhari amepokea Hadith zake Sahih kwa maoni yake Hadith elfu sita kama ilivyopokelewa kwa Bukhari mwenyewe amesema: "Sikupokea katika kitabu hiki isipokuwa Hadith Sahih tu na nilizoziacha miongoni mwa Hadith Sahih ni nyingi zaidi."55

Na tuliyo yachukua kwanza kwa Bukhari ni; kutegemea kwake uadilifu wa mlolongo wa wapokezi wa Hadith kama sharti lake pekee katika kuthibitisha usahihi wa Hadith iliyopokelewa bila ya kuangalia matin na maana iliyobeba. basi pakawa na mgongano mwingi katika riwayah ambazo zinaweza kuchukuliwa kuwa ni tuhuma katika dini.

Mpokezi (wa hadithi) hata kama atakuwa mwadilifu, uadilifu wake hauzuii kusahau kwake kipande cha Hadith aliyoisikia, tukiachilia mbali dhana ya kupokea kwake Hadith kwa maana yake na wala si kwa matamshi halisi aliyoyasikia.
Jambo ambalo linaikosesha Hadith matamko yake ya asili, na ambayo yanaweza kuwa na maana nyingine, na mpokezi akawa hajatambua hivyo akainukuu kwa maana nyingine. Tukiongezea ugumu wa kujua uadilifu wa watu hasa wanafiki kati yao, ambao hakuna anayejua undani wao isipokuwa Mola wa waja, inadhihirika kwetu kasoro kubwa katika sharti la Bukhari katika kuandika kwake Hadith zake Sahih.

Kama alivyosema Ahmad Amin, hakika baadhi ya watu ambao amepokea kutoka kwao sio waaminifu, na amewatia udhaifu karibu wapokezi themanini56 kati ya watu aliopokea kwao Al Bukhari. Na katika yafuatayo tunaeleza zaidi katika riwayah ambazo Bukhari amezihesabu kuwa ni sahih, na baadhi ya Waislamu wakajilazimisha kuzifuata katika muda wote.

Kutoka kwa Abi Sa'id al-Khudriy; ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema kuhusu siku ya Qiyamah: " Hakika sisi tulisikia mwitaji anaita kila watu wakiendee walicho kuwa wanakiabudu na sisi tunamsubiri Mola wetu." akasema: "Basi Allah (s.w.t.) atawajia katika sura isiyokuwa sura yake ambayo walimwona nayo mara ya kwanza na kusema mimi ni Mola wenu watasema wewe ni Mola wetu, basi hawatomsemesha isipokuwa manabii, atasema je, kati yenu na yake kuna alama mtakayomjua? Watasema muundi (mguu), basi atadhihirisha muundi wake; basi kila muumini atamsujudia."57

Amesema Jariyr bin Abdillahi: "Tulikuwa tumekaa usiku mmoja pamoja na Nabii (s.a.w.w.), akatazama mwezi usiku wa kumi na nne akasema: 'Hakika nyinyi mtamwona Mola wenu kama mnavyo uona huu mwezi hamtadhulumiwa katika kumwona kwake.”58

Hakika riwayah mbili hizo hapo juu, ambazo zinafahamika kuwa kuna uwezekano wa kuonekana kwa Allah (s.w.t.), hazikubaliwi kwa sababu walioitakidi uwezekano wa kuonekana Allah (s.w.t.) wamekosea katika ta'awil yao, katika kauli yake Allah (s.w.t.) (nyuso siku hiyo zitang'ara kumwangalia Mola wao) na ta'awil yake sahih ni zikisubiri amri ya Mola wao na vivyo hivyo ta'awil ya Ayah nyingine ambazo dhahiri yake zinaonyesha kuwa Allah (s.w.t.) ni kiwiliwili na yanatiliwa nguvu yale tuliyo yasema na riwayah ambayo Bukhari mwenyewe ameinukuu vile vile.

Kutoka kwa Masruq amesema:- Nilimwambia 'Aisha: "Ewe mama yangu, je, Muhammad amemwona Mola wake?" Akasema: "Hakika nywele zangu zimesisimuka kwa uliyo yasema: uko wapi wewe na mambo matatu atakayekueleza atakuwa anasema uongo? Anayekwambia kuwa Muhammad amemwona Mola wake anasema uongo, kisha akasema macho hayamwoni na yeye anayaona macho Naye ni Mtukufu, Mjuzi na wala hakuwa mwanadamu ni mwenye kusemeshwa na Allah (s.w.t.) isipokuwa kwa wahyi au nyuma ya pazia."59

Na tunafuatilia pamoja na Abu Huraira riwayah zake za ajabu; amesema: “Alikuja mchungaji miongoni mwa wachungaji kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akasema: 'Ewe Muhammad! Hakika tunakuta kwamba Allah (s.w.t.) ataziweka mbingu juu ya kidole na ardhi juu ya kidole na miti juu ya kidole na maji juu ya kidole, na sayari juu ya kidole na viumbe vingine juu ya kidole. Atasema Mimi ni Mfalme,’ Nabii (s.a.w.w.) akacheka mpaka magego yake yakaonekana kwa kuisadikisha kauli ya mchungaji, kisha Mtume wa Allah (s.a.w.w.) akasema: 'Na hawakumtukuza Allah (s.w.t.) kama anavyostahiki kutukuzwa.”60

Watasema: "Ewe Adam Je! huoni watu? Allah (s.w.t.) amekuumba kwa mkono wake na akaamuru Malaika wake wakusujudie?"61

Amesema alitajwa mwanaumme mbele ya Nabii (s.a.w.w.) ikasemwa bado amelala mpaka kumekucha hakuamka kusali, akasema Shetani amekojoa kwenye sikio lake."62

'Umar akasema Je! hukujua kuwa Nabii amesema: "Hakika maiti anaadhibiwa kwa kilio cha aliye hai."63
Na kwa nini maiti ataadhibiwa kwa kumlilia watu wake? Na ilhali Allah (s.w.t.) anasema:

وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۗ{15}

'Haadhibiwi mtu kwa makosa ya mtu mwingine.(Al-Israa 17:15)

Amesema funikeni vyombo na fungeni viriba vya maji na fungeni milango na wakumbatieni vijana wenu wakati wa usiku, kwani majini wanasambaa na kupora. Na zimeni taa wakati wa kulala, kwani mafasiki huenda wakachomoa utambi na kuwaunguza wenye nyumba."64

Amesema Mtume wa Allah (s.a.w.w.): "Jua linapochomoza acheni sala mpaka lichomoze kabisa, na linapoanza kuzama acheni sala mpaka lizame kabisa, wala Sala yenu isiende sambamba na kuchomoza jua wala kuzama kwake, kwani linachomoza baina ya pembe mbili za Shetani." Na Hisham akasema: 'Na sijui ni Shetani (yeyote) au Al- Shaytan (maalum)'.65

Kutoka kwake amesema: "Amesema Nabii kumwambia Abudhar; ‘wakati linapozama jua unajua linaenda wapi?' Akasema: 'Allah (s.w.t.) na Mtume wanajua.'

Akasema: 'Hakika huenda mpaka likasujudu chini ya 'arsh, na linataka ruhusa na linapewa ruhusa na limekaribia kusujudu na lisikubaliwe na litataka ruhusa na lisikubaliwe litaambiwa rejea ulikotoka, basi litatoka magharibi na hiyo ni kauli yake Allah (s.w.t.) (na jua linapita katika njia yake na huu ni mpango wa Mwenye nguvu , Mjuzi).”66

Sijui yako wapi mafungamano ya riwayah mbili za mwisho na elimu? Je! Waislamu na Maulamaa wanakubali mfano wake na hasa ambao wanaamini kuwa Uislamu haupingani na elimu?

Je! kuna njia ya kuzioanisha riwayah mbili za Bukhari zifuatazo:- Ibn Jubair amesema: "Ibn 'Abbas ameniambia Je! umeoa?" Nikasema: "Hapana." Akasema: "Basi oa kwani kheri ya 'Ummah huu iliyo nyingi zaidi ni wanawake."67

Abdullah ibn ‘Umar amesema: "Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema: 'uovu uko kwa mwanamke, nyumba na farasi.”68

Hakika kutokuwa sahihi yote yaliyo pokelewa katika Sahih Bukhari, yanatufanya tuhukumu kwamba, haitoshi kuwa Hadith yeyote iliyopokewa katika kitabu chake ni Sahih, kwa sababu tu ya Bukhari kuipa sifa ya usahihi na kwa kuwa hukumu nyingi zilijengewa juu ya Sahaba huyu au yule, na itikadi nyingi zimechukuliwa kwao.

Mfano wa uwezekano wa kuonekana Allah (s.w.t.) au kutokamilika Uma'asum wa Nabii kwa mfano kwa kutegemea katika Hadith zilizopokelewa katika Sahih Bukhari na nyinginezo miongoni mwa vitabu vya Hadith hakika hiyo inawajibisha kurejea tarikh ya Kiislamu na kufanya uchambuzi wa uadilifu wa wapokezi miongoni mwa Masahaba na tabi'in kwa yale tuliyoyajua miongoni mwa udanganyifu mwingi katika yaliyopokelewa katika Sahih Bukhari na nyinginezo katika Hadith yaliyochukua nafasi na mazingatio na kuaminiwa katika baadhi ya Waislamu pamoja na yaliyomo humo miongoni mwa shaka na upotovu ambayo yanachukuliwa kuwa tuhuma juu ya dini ya Kiislamu.

 • 1. "Al-imaamus Saadiq" cha Abuu Zuhrah.
 • 2. "Difaa'un 'anil 'aqidati wa-sh-shariah dhidda matwaa'inil-mustashriqiyna" cha Al-Ghazaliy.
 • 3. Sahih Bukhari j. 9 uk. 92, Kitabu-t-ta'biyr, Babu awwali maa badaa bihi rasuulullahi (s).
 • 4. Sahih Bukhari j. 9 uk. 93, Kitabu-t-ta'biyr, Babu awwali maa badaa bihi rasuulullahi (s).
 • 5. Sahih Bukhari j. 8 uk. 234, Kitabu-d-da'awaat, Babu qawlihi taala "wa swalli 'alayhim".
 • 6. Sahih Bukhari j. 1 uk. 349, Kitabul-adhaan, Babu qawlu-r-rajuli lin-Nabiy -maa swallaynaa -.
 • 7. Sahih Bukhari j. 1 uk. 168, Kitabul-ghusli, Babu idhaa dhakara fil-masjidi annahu junub.
 • 8. Sahih Bukhari j. 8 uk. 48, Kitabul-adabi, Babu maa yajuuzu min dhikri-n-naasi.
 • 9. Sahih Bukhari j. 8 uk. 57, Kitabul-adabi, Babu innallaha ya'muru bil -'adli wal-ihsaan.
 • 10. Sahih Bukhari j. 7 uk. 444, Kitabu-t-twibbi, Babu-s-sihri.
 • 11. Sahih Bukhari j. 8 uk. 56, Kitabul-adabi.
 • 12. Al-Furqaan: 8.
 • 13. Sahih Bukhari j. 5 uk. 77, Kitabu fadhaailis sahaba, Babu fadhli 'Aaishah.
 • 14. Sahih Bukhari j. 3 uk. 462, Kitabul-hibah, hibatul-mar'ati li ghayri zawjiha.
 • 15. Sahih Bukhari j. 1 uk. 165, Kitabul-ghusli, Babu adhaa jaama'a thumma 'aada wa man daara 'alaa nisaa'ihi fiyghuslin waahid.
 • 16. Sahih Bukhari j. 7 uk. 5, Kitabu-n-nikaah.
 • 17. Sahih Bukhari j. 6 uk. 296, Kitabu-t-tafsir,.
 • 18. Sahih Bukhari j. 8 uk. 170, Kitabul-Isti'dhaan.
 • 19. Sahih Bukhari j. 7 uk. 462, Kitabu-l-libaas.
 • 20. Sahih Bukhari j. 2 uk. 252, Kitabul-janaaiz.
 • 21. Kanzul-Ummaal Hadith Na. 4404.
 • 22. Sahih Bukhari j. 1 uk. 86, Kitabul-Ilmi.
 • 23. Sahih Bukhari j. 3 uk. 313, Kitabul-muzaara'ah, Babu maa jaa'a fil-farasi.
 • 24. Sahih Bukhari j. 5 uk. 47, Kitabu fadhaaili-s-Sahaba, Babu manaaqibi Ja'fari-bni AbiTalib.
 • 25. Ameipokea Tirmidhi j. 13 uk.189, chapa ya Darul-kitabil-arabiy Beirut, na Al-Haakim kwa isnad sahihi.
 • 26. Sahih Muslim j. 1 uk.201, Babu man shahida laa ilaaha illallahu mustayqinan dakhalal-jannah.
 • 27. Fiqhu-s-sirah ya sheikh Muhammad Al ghazaali uk..41 chapa 6.
 • 28. Majallatul-Manaar j. 10 uk. 851.
 • 29. Tarekh Aadaabil-Arab j. 1 uk. 278.
 • 30. Sahih Bukhari j. 9 uk. 317, Kitabul-I'tisaami bil-kitabi wa-s-Sunnah, Babu maa dhakara-n-Nabiyyu 'ala-t-tifaaqi ahlil-'ilm.
 • 31. Sahih Bukhari j. 1 uk. 89, Kitabul-Ilmi, Babu hifdhil-ilmi.
 • 32. Sahih Bukhari j. 1 uk. 88, Kitabul-Ilmi, Babu hifdhil-ilmi.
 • 33. Ikhtisaru Uluumil-hadith uk. 111.
 • 34. At-Taqrib cha An-Nawawi uk. 14.
 • 35. Sahih Bukhari j.2 uk. 236, Kitabul-Janaaiz.
 • 36. Sahih Bukhari j. 6 uk. 353, Kitabu-t-Tafsir, Babu qawlihi - wa hal mim-maziyd -
 • 37. Sahih Bukhari j. 2 uk. 324, Kitabu bid'il-khalq.
 • 38. Sahih Bukhari j. 8 uk. 160, Kitabu-sti'dhaan.
 • 39. Sahih Bukhari j. 6 uk. 311, Kitabu-t-Tafsir.
 • 40. Sahih Bukhari j. 2 uk. 136, Kitabu-t-Tahajjud.
 • 41. Sahih Bukhari j. 7 uk. 496, Kitabu-l-libaas, babu laa yamshiy fiy na'lin waahidah.
 • 42. Sahih Bukhari j. 8 uk. 211, Kitabu-d-Da'awaat.
 • 43. Sahih Bukhari j. 4 uk. 163, Kitabul-jihad.
 • 44. Sahih Bukhari j. 1 uk. 114, Kitabul-wudhui.
 • 45. Sahih Bukhari j. 4 uk. 333, Kitabu bid'il khalq.
 • 46. Sahih Bukhari j. 4 uk. 306, Kitabu bid'il khalq.
 • 47. Sahih Bukhari j. 3 uk. 312, Kitabul-muzaara'ah.
 • 48. Sahih Bukhari j. 4 uk. 60.
 • 49. Sahih Bukhari j. 9 uk. 18, Kitabu-d-Diyyaat, Babu man akhadha haqqahu aw-iqtasswa duuna-s- sultaani.
 • 50. Sahih Bukhari j. 1 uk. 169, Kitabul-ghusli, Babu manightasala 'ur'yaanan wahdahu fiy khal'wah.
 • 51. Sahih Bukhari j. 7 uk. 473, Kitabu-l-libaasi, Babul-buruudi wal-hibri wa-sh-shumlah
 • 52. Sahih Bukhari j.1 uk.170 Kitabul-ghusli
 • 53. Sahih Bukhari j. 3 uk. 297, Kitabul-muzaara'ah, Babu-sti'maalil-baqari lil-hiraathah.
 • 54. Sahih Bukhari j. 1 uk. 336, Kitabul-adhaan, Babu fadhli-t-ta'dhiyn.
 • 55. Ibnu Hajar katika utangulizi wa Shar'hul Baary 'alaa sahihil-Bukhari uk.5, chapa ya Daru ihyaai-t- turaathil-arabiy.
 • 56. Dhuhal - Islam cha Ahmad Amin j. 2 uk. 117-118.
 • 57. Sahih Bukhari j. 9 uk. 396, Kitabu-t-Tawhid, wujuuhun yawma'idhin naadhwirah.
 • 58. Sahih Bukhari j. 6 uk. 355, Kitabu-t-Tafsir, Babu qawlihi - fasabbih bihamdi rabbika -.
 • 59. Sahih Bukhari j. 6 uk. 359, Kitabu-t-Tafsir, Babu suurati-n-Najmi.
 • 60. Sahih Bukhari j. 6 uk. 317, Kitabu-t-Tafsir, Babu - wa maa qadarullaaha haqqa qadrihi -.
 • 61. Sahih Bukhari j. 9 uk. 373, Kitabu-t-Tawhid.
 • 62. Sahih Bukhari j. 2 uk. 135, Kitabu-t-Tahajjud.
 • 63. Sahih Bukhari j. 2 uk. 212, Kitabul-Janaa'iz.
 • 64. Sahih Bukhari j.4 uk.336,Kitabu bid'il-khalqi,Babu idha waqa'a-dh-dhubaabu fi sharaabi ahadikum fal-yaghmis'hu.
 • 65. Sahih Bukhari j. 4 uk. 319, Kitabu bid'il -khalqi, Babu swifati Ibliis wa junuudihi.
 • 66. Sahih Bukhari j. 4 uk. 283, Kitabu bid'il-khalqi, Babu swifati-sh-shamsi wal- qamar bi husbaani.
 • 67. Sahih Bukhari j.7 uk. 5, Kitabu Fadhail-s-Sahaba.
 • 68. Sahih Bukhari j.7 uk. 21, Kitabu-n-Nikah

Sehemu Ya Tano: Ndoa Ya Muda

Ndoa ya muda ambayo inajulikama vile vile kama ndoa ya "Mut'a," nayo ni mwanamke kuozesha nafsi yake kwa mwanamme kwa mahari maalumu na kwa muda maalumu, kwa kufunga ndoa iliyotimiza masharti Sahih ya kishariah. Tamko lake ni mwanamke kumwambia mwanaume baada ya maafikiano na maridhiano juu ya mahari na muda: "Zawwajtuka nafsi bimahri qadruhu kadha ilal-ajalil-maalum" (Nimekuoza nafsi yangu kwa mahari kadha kwa muda maalumu), na muda unabainishwa wazi. Na jibu la mwanaume linakuwa haraka "Qabiltu" (Nimekubali).

Na wakala unajuzu katika ndoa hii kama ilivyo katika mikataba mingine. Na kwa kukamilika masharti ya ndoa, mwanamke anakuwa ni mke wa mwanaume na mwanaume anakuwa ni mume wake hadi mwisho wa muda uliopangwa katika ndoa. Na wanaweza kuongeza muda mwingine, na ni wajibu kwa mke akae 'Iddah baada ya kumalizika muda kwa tohara mbili (hedhi mbili) kama anapatwa na hedhi, vinginevyo ni kwa muda wa siku arobaini na tano. Na mtoto wa mut'a awe ni mvulana au binti ananasibishwa kwa baba yake.

Na Waislamu pamoja na khitilafu za madhehebu yao wanaafikiana na aina hii ya ndoa, ndoa hii ni katika mambo yalioanza tangu mwanzo wa Uislamu na kwayo imeteremka Ayah:

فَمَا اسْتَمْتَعْتُمْ بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ{24}

"Kwa mlio jifurahisha nao miongoni mwao basi wapeni mahari yao.” (An-Nisaa 04:24)

Na wamefasiri wengi wa wafasiri wa Ahl as-Sunnah Al-Istimtai katika Ayah hii kwa ndoa ya Mut'a na Ibn 'Abbas na 'Ubay bin Kaab na Sa'id bin Jubair walikuwa wanasoma Ayah hii "Fama-stamta'atum bihii minhunna ilaa ajalim-musammaa fa'tuuhunna ujuurahunna."1

Amesema Ibn Kathir katika tafsiri yake akielezea hilo "na jambo ambalo liko mbali sana, ni hawa kuamini kupotoshwa kwa Qur'an, hivyo ni lazima kwa lililokusudiwa na wala sio kusoma"2 na kuteremka Ayah hii katika ndoa ya Mut'a ni katika ambayo hayapasi kuwa ni maudhui ya mjadala, bali mjadala ni kuwa Ayah hii ni Mansukh au sio Mansukh? yaani imeharamishwa baada ya kuhalalishwa kwake au imebakia katika hali yake?

Mwanzo tunaeleza baadhi ya yaliopokewa katika Hadith zinazothibitisha ndoa ya Mut'a, kuwa ni ya kisheria katika Uislamu miongoni mwa aliyopokea Bukhari katika Sahih yake.

Kutoka kwa 'Abdillah amesema tulikuwa tukipigana vita pamoja na Nabii (s.a.w.w.) na hatukuwa na wanawake basi tukasema Je tufanye ponyeto (tujichue wenyewe)? Akatukataza hilo, akaturuhusu baada ya hapo kuoa mke kwa kumpa nguo - kisha akasema: "Enyi mlioamini msiharamishe mazuri aliyo wahalalishia Allah (s.w.t.)."3

Na Hadith ifuatayo inathibitisha bila ya shaka yoyote kwamba Mtume amefariki bila ya kuharamisha ndoa ya Mut'a na kwamba aliyekataza ni mtu mwingine baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.). Amesema Ayah ya Mut'a imeteremka katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) na haikuteremka Ayah ya Qur'an ya kuiharamisha na kuikataza mpaka akafariki, Mtu (fulani) akasema kwa maoni yake aliyoyataka.4

Na 'mtu' anaye ashiriwa katika Hadith iliyotangulia, si mwingine isipokuwa ni 'Umar al-Khattab, ambaye imethibitika kuwa yeye ndiye aliyeharamisha ndoa hii kama ilivyokuja katika Sharh ya Al-Baari katika Sahih Bukhari - angalia maelezo yake chini kwa tarjuma ya Kiingereza.

Na imekuja katika Sahih Bukhari vile vile katika Babu al-Tamattu' 'alaa ‘ahdi rasulilah (s.a.w.w): ametusimulia Musa bin Isma’il, ametusimulia Hamaam kutoka kwa Qatadah amesema, amesimulia Mutarifu kutoka kwa Imran amesema: Tulifanya Mut'a wakati wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na Qur'ani ilishuka (juu ya hilo), na mtu (fulani) akasema kwa maoni yake anayoyataka.5

Ni uwazi ulioje wa vipi mtarjum alivyopiga chenga kwa kuifanya kwake kuwa ni mahsusi kwa Tamattu iliyopokewa katika riwayah ya Imran kuwa ni Haji-Tamattu na wala sio Mut'a ya wanawake. Vyovyote iwavyo kilicho muhimu kwetu ni kile kilichopokewa katika Sahih Bukhari tu, na kuashiria kwetu katika tarjuma haikuwa isipokuwa ni kudhihirisha alicho kinukuu mtarjum kutoka sharh ya Al-Baary katika Sahih Bukhari, na hasa kwa mwanamme asiyejulikana katika riwayah. Na yanatiwa nguvu kwa aliyo mwanamme asiyejulikana katika riwayah. Na yanatiwa nguvu kwa aliyo yapokea Muslim katika Sahih yake kwa Isnad ya Ibnun-Nadhar amesema: “Ibn ‘Abbas alikuwa anaamrisha Mut’a na Ibn Zubeir alikuwa anaikataza basi nikaeleza hilo kwa Jabir.”

Akasema:”Tulifanya Mut’a pamoja na Mtume wa Allah (s.aw.w.) na alipotawala ‘Umar akasema: “Hakika Allah (s.w.t) anahalaisha kwa Mtume wake anayoyataka, basi timizeni Hijja na Umra na acheni kuoa hawa wanawake, sitoletewa mwanamme aliyeoza mwanamke kwa mwanamme isipokuwa nitampiga kwa mawe.”6

Na katika Sahih Tirmidhi kutoka kwa 'Abdallah bin 'Umar aliulizwa na mtu kutoka katika watu wa Sham juu ya Mut'a ya wanawake, akasema: "Ni halali", akasema: "Hakika baba yako alikwishaikataza." Ibn 'Umar akasema: "Unaonaje kama baba yangu amekataza na Mtume (s.a.w.w.) ameifanya, utaacha Sunnah na kufuata kauli ya baba yangu?"7

Vile vile katika Sahih Muslim kumepokewa: "Kisha wakataja Mut'a, akasema kweli tulifanya Mut'a wakati wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.), Abubakr na 'Umar."8

Na imekuwa mashuhuri kwa hibril-ummah 'Abdallah bin 'Abbas (r.a.) kwa rai yake kuwa Mut'a haikufutwa kama anavyopokea hayo Al- Zamakh'shariy katika Tafsiri yake Al-Kashaaf, ambapo ananukuu kutoka kwa Ibni 'Abbas kwamba Ayah ya Mut'a ni katika Muhkamaati, na vile vile katika Sahih Bukhari kuna yanayotilia mkazo hayo.

Amesema: "Nilimsikia Ibn 'Abbas anaulizwa kuhusu mtumwa wake akamwambia: 'hakika hiyo ni katika hali ngumu na wanawake wakiwa ni wachache au mfano wa hayo?’. Ibn Abbas akasema: “Ndiyo.”9 Pamoja na uwazi wa dalili hizo ni kama vile uwazi wa jua katikati ya mchana kuhusu kuendelea uhalali wa ndoa ya Mut’a.

Watu wengi katika Ahl as-Sunnah wako kinyume na hayo, lakini Ayah ambayo ni maalumu katika ndoa hii wanadai kuwa imefutwa na wamehitilafiana kuhusu Ayah iliyo ifuta, kati yao wanasema imefutwa na Ayah iliyopo katika Qur'an, na kati yao wanasema iliyofuta ni riwayah zilizopo kati ya Hadith. Tunajibu rai zote mbili kwa Hadith zilizothibiti ambazo zimetangulia, na ambazo zinaonyesha kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.) bila ya kukataza, na wale waliosema iliyofuta ni Ayah katika Qur'an nayo ni:

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ {5}

إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ {6}

"Na wale ambao wanahifadhi tupu zao isipokuwa kwa wake zao au iliyowamiliki mikono yao ya kuume.”(Al-Mu’minun 23:5-6)

Inatosha kujibu rai yao hii kwa kutazama katika Ayah hii ambayo wanadai kuwa imefuta Ayah ya Mut'a, Ayah hii ni Makki (yaani imeshuka Makkah) na Ayah ya Mut'a ni Madani (yaani imeshuka Madina) na hukumu ya kisheria ya ndoa ya Mut'a ni madani (yaani imeshuka baada ya Ayah ya (na ambao wanahifadhi tupu zao...) na Ayah iliyotangulia haifuti inayokuja baada yake.

Ama aliyesema iliyofuta ni Hadith zilizopokewa kwa Mtume (s.a.w.w.), hakika Hadith hizo wanazozidai kuwa zimefuta, zinapingana zenyewe kwa zenyewe, baadhi yake zinasema imefutwa katika Khaibar na nyingine katika Autasi, ya tatu inasema ni katika siku ya Fath Makkah, na ya nne katika vita vya Tabuk na ya tano ni katika Umrah ya Qadhaa, ya sita ni katika Hajjat tul-Wida'a.

Kugongana na kupingana kwa riwayah hizo sio kwengine ila ni kuonyesha dalili ya kutokuwa ni Sahih, hayo ni pamoja na kuongezea kuwa riwayah hizo. Haziepukani na kuwa kwake ni Hadith za Ahaad, ambazo hazifai kuwa ni zenye kufuta hukumu ambayo imeletwa na Qur'an, na Shariah yake imethibiti kwa kongamano la Waislamu wote, kwa sababu Naasikhi haipatikani kwa habari ya mtu mmoja kwa ijmai, na Ayah haifutwi isipokuwa na Ayah kwa dalili ya kauli ya Allah (s.w.t.):

مَا نَنْسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنْسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ{106}

"Hatufuti Ayah au kuisahaulisha isipokuwa tutaleta iliyo bora zaidi au mfano wake.”
(Al-Baqarah 02:106)

Na ambacho kinaweza kuwa ni kisingizio cha ijtihad ya 'Umar katika kuharamisha ndoa ya Mut'a ni kwamba, mmoja wa Waislamu jina lake ni 'Amr bin Harith alitumia vibaya Shariah hii, hivyo akachokoza hasira za 'Umar na ikampelekea kuharamisha huku. Na dalili kuhusu haya ni riwayah ambayo ameipokea Muslim katika Sahih yake kutoka kwa Ja'abir: "Tulikuwa tunafanya mut'a kwa kutoa kiasi cha tende na unga wakati wa Mtume (s.a.w.w.) na Abubakr na Umar, mpaka alipokataza kutokana na jambo la 'Amr bin Hurayth.10

Na ameitoa Tabarani na Tha'alabi katika tafsiri zao kwa isnad ya Al- Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) amesema: "Kama asingekataza 'Umar Mut’a, basi asingezini isipokuwa mwovu.”11

Na katika riwayah nyingine isipokuwa wachache.

Baada ya riwayah zote hizi ambazo zinathibitisha hukumu ya ndoa ya Mut'a, na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kutoikataza, na kubaki kwake halali hadi alipoharamisha 'Umar wakati wa ukhalifa wake, hatupati ufumbuzi wa tatizo hili, isipokuwa 'Umar amefanya ijtihad kwa rai yake kwa ajili ya maslahi aliyoyaona - kwa mtazamo wake - kwa Waislamu katika wakati wake na siku zake, yaliyo sababisha kuzuia kufanya Mut'a.

Kuzuia huko ni kwa kijamii na wala sio kwa kidini kwa ajili ya maslahi ya muda, kwa sababu 'Umar ana cheo kikubwa na alikuwa na daraja kitawala, hawezi kuharamisha alichokihalalisha Allah (s.w.t.) au kuingiza kitu katika dini naye anajua kuwa halali ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni halali hadi siku ya Qiyamah, na haramu ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni haramu hadi siku ya Qiyamah.

Hivyo ni lazima makusudio yake ya kukataza yawe ya muda na ni kuharamisha kwa kijamii na wala siyo kwa kidini. Na msimamo wake huu mkali katika jambo la ndoa ya Mut'a sio wa kwanza katika aina yake kwani amejulikana kwa ukali na ugumu katika mambo yake yote. Anafanya ijtihad katika hilo kwa kutaka kupata maslahi bora zaidi - kwa mtazamo wake - kwa ajili ya Uislamu na kusimamisha Shariah. Na miongoni mwa mifano katika ijtihad ya 'Umar katika hukumu na ukali wake, ni amri yake kwa Waislamu kusali Sala ya Ramadhani (tarawih) katika jamaa baada ya kuwa inasaliwa furada (mmoja mmoja) wakati wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

Kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema mwenye kusali Sunnah ya Ramadhani kwa imani na kutaka thawabu anasamehewa yaliyo tangulia katika dhambi zake." Ibnu Shihab amesema: "Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amefariki na watu wanafanya hivyo, kisha mambo yalikuwa vivyo hivyo katika zama za Abubakr na mwanzo wa zama za 'Umar (r.a.)."

Akasema (Ibn Shihab): "Nilitoka pamoja na 'Umar Al-Khattab usiku wa mwezi wa Ramadhani kwenda msikitini basi tukakuta watu wametapakaa na wametawanyika, kila mtu anasali peke yake na mtu anasali na kundi linasali nyuma yake, 'Umar akasema mimi naona kama nitawakusanya hawa kwa msomaji mmoja ingekuwa ni bora.

Kisha akaazimia, akawakusanya kwa 'Ubay bin Ka'ab, kisha nilitoka pamoja naye usiku mwingine na watu wanasali kwa sala ya msomaji wao, 'Umar akasema: "Bida'a nzuri ni hii na wale wanaolala (wakasali usiku) ni bora kuliko wanaoisali (sasa), amekusudia mwisho wa usiku na watu walikuwa wanasali mwanzo wa usiku.”12

Vile vile amefanya ijtihadi katika Sunnah hiyo ambayo imeitwa sala ya tarawih kwa kuongeza idadi ya raka'a zake hadi kufikia ishirini. Kutoka kwa 'Abdurahman kwamba amempa habari kwamba yeye alimwuliza 'Aisha Sala ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) ilikuwaje katika mwezi wa Ramadhani?" Akasema: "Mtume wa Allah (s.a.w.w.) hakuwa anazidisha katika Ramadhani wala katika mwezi mwingine zaidi ya raka'a kumi na moja."13

Lakini baadhi ya walioishi wakati wa khalifa na walio kuja baada yake baadhi ya muhadithin wajinga, waliona ni jambo kubwa mno kuwa ameharamisha alichokihalalisha Allah (s.w.t.) na wakalazimika kutoa kisingizio kwa ajili ya hilo. Hivyo hawakupata isipokuwa madai ya nasikh kutoka kwa Nabii baada ya kuhalalishwa, basi wakagongana mgongano huo na kauli zao zikapingana mpingano huo.

Tazama riwayah ifuatayo ili uone upeo wa mgongano na mgawanyiko ambao tunauzungumzia, na mshangao ni kwamba wazushi wa riwayah hiyo wameinasibisha kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) na watoto wake.

Kutoka kwa Zuhri kutoka kwa Hassan na 'Abdillah watoto wa Muhammad bin 'Ali kutoka kwa baba yao: Hakika Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) aliambiwa kuwa Ibn 'Abbas haoni ubaya wa Mut'a ya wanawake, akasema: 'Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) ameikataza siku ya Khaibar, pamoja na nyama ya punda wa nyumbani', na baadhi ya watu wakasema na kama atafanya hila hadi akafanya Mut'a basi ndoa itakuwa ni batil na baadhi yao wamesema: "Ndoa inajuzu na sharti litakuwa batili."14

Kama hawa wangefahamu sababu ya khalifa kukataza Mut'a hilo lingewatosha kutokana na mgawanyiko na kutokuendelea.

Hakika mtazamo wa ndoa ya Mut'a uliotangulia ulikuwa ni kwa pande mbili; kidini na kihistoria. Ama mtazamo katika upande wa tabia ya kijamii kuhalalishwa kwake kumekuja kuwa ni rehema kwa wanaadamu na ruhusa kwa walio wengi, na hasa wanaosafiri kwa kutafuta elimu au biashara au wanaopigana jihadi au wanajeshi pamoja na kushindwa kwao kuoa ndoa ya daima, kwa vile mara nyingi kuna vipengele na vitu ambavyo haviendani na hali ya wasafiri, hasa ambao wako katika umri wa ujana na mchemko wa shahawa.

Kwani hali yao haiepukani na mambo mawili, ima subira na kubana nafsi ambako kunasababisha matatizo ambayo yanaleta maradhi ya kudumu na magonjwa ya kinafsi yenye kuangamiza, na mengineyo katika madhara ambayo hayafichikani kwa yeyote, na ima kutumbukia katika zinaa ambayo imejaza dunia kwa ufisadi na madhara. Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbas kuhusu suala hilo; " Mut'a haikuwa isipokuwa ni rehema ya Allah (s.w.t.) ameuhurumia ‘Ummah wa Muhammed na kama sio kukataza kwake (yaani ‘Umar) asingezini isipokuwa mwovu.”15

Na katika yanayotia mkazo dharura ya kitabia na kijamii kwa kuhalalisha aina hii ya ndoa ya muda, ni ambayo baadhi ya Waislamu wametoa Fatwa katika wakati ambao tunao kwa kuruhusu ndoa ya aina nyingine inayomrahisishia msafiri peke yake kutatua matatizo yake katika hali ya kutoweza kuoa ndoa ya daima, na sifa ya ndoa hii ni ya muda kwa upande wa wanaume na ni ya daima kwa upande wa wanawake. Na aliyo kusudia mume katika nafsi yake bila ya yeyote kujua unapomalizika muda, anamshitusha mke wake masikini kwa kumpa talaka.

Hivyo aina hii ya ndoa wameipa jina la "Ndoa kwa nia ya talaka (kuachika)," pamoja na kutambua wale waliozua kuwa huo ni uongo kwa mke na ni udanganyifu na hakuna dalili juu ya hilo katika Kitabu wala Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) lakini wao wanafanya kwa hoja ya kuwa madhara yake yatabaki yamefichikana kuliko ufisadi wa zinaa. Yote ni kwa kuwa wao wameamini kubatilika kwa ndoa ya Mut'a ambao uhalali wake umekuja katika Kitabu kitukufu na Sunnah za Mtume na kwa kufanya hivyo watakuwa wamebadilisha bida'a walioizua na hukumu ya Allah (s.w.t.). "Je mnabadilisha ambacho ni duni kwa kile kilicho bora." Fala haula wala Quwata illa billahi.

Mut'atul Hajj

Mtume amekwisha ifundisha na akaamuru kutokana na kauli ya Allah (s.w.t.) Mtukufu: “Basi atakayefanya umrah ya hijja, hiyo ni kwa ambaye familia yake haiko karibu na Msikiti Mtakatifu wa Makkah.” (Al-Baqarah 02:196)

Na makusudio ya hayo ni 'Umrah katika miezi ya hijja kabla ya hijja, nayo ni faradhi kwa ambaye familia yake iko mbali na Makkah. Na imeitwa Tamattu ya hijja kwa yale yaliyomo humo katika kujifurahisha, (yaani raha ya kuhalalishiwa makatazo ya Ihraam katika muda uliopo baina ya Ihraam mbili - Ihraam ya umrah Tamattu na Ihraam ya hijja. Na hayo ni ambayo 'Umar aliyachukia pia, na akayakataza pamoja na kuwa Mtume (s.a.w.w.) alifariki bila ya kukataza.

Kutoka kwa Sa'id bin Mussayib amesema: "Ali (a.s.) alikhitilafiana na 'Uthman na wao wako katika kuhirimia 'Umrah Tamattu. 'Ali (a.s.) akasema: 'Hataki isipokuwa kukataza jambo alilolifanya Nabii (s.a.w.w.).' 'Ali (a.s.) alipoona hivyo akahirimia zote mbili."16

Kutoka kwa Al-Hakim amesema: "Niliwaona 'Ali (a.s.) na 'Uthman , na (huku) 'Uthman anakataza Mut'a na kuunganisha baina yake, 'Ali (a.s.) alipoona akapaza sauti kwa vyote viwili: " Labayka bi umrati wa hajjati. " Akasema: 'Sikuwa ni mwenye kuacha Sunnah ya Nabii kwa kauli ya yeyote.”17

Ama udhr wa 'Uthman katika rai yake hiyo ni kwa kuwa yeye alikubali sharti kabla ya kupewa bay'a ya kuwa khalifa, Abdulrahman bin 'Auf alitoa sharti kwa wosia kutoka kwa 'Umar, ahukumu kwa Kitabu cha Allah (s.w.t.)

Sunnah za Nabii wake na kwa mwenendo wa masheikh wawili kama ilivyo tangulia katika sehemu iliyo tangulia. Na imepokewa kwa tawatur kauli ya 'Umar: "Mut'a mbili zilizo kuwepo wakati wa Mtume wa Allah (s.a.w.w) mimi nazikataza”18 na anakusudia kwa kauli yako hiyo Mut’a ya wanawake na Mu’ta ya Hijja.

Na maneno ya 'Umar yanadhihirisha uamuzi wa hukumu hizo ni wake,na wala sio wa mwengine, kwani yeye anakiri kuwa Mut'a mbili zilizokuwa katika wakati wa Nabii (s.a.w.w.).

Na hakunasibisha kukataza kwake kwa Mtume bali amekataza yeye mwenyewe kwa kauli yake "na mimi nakataza" na Allah (s.w.t.) amrehemu aliyesema kuhusu Hadith ya mwisho kuhusu 'Umar "Tumekubali ushahidi wake lakini hatujakubali kuharamisha kwake."

 • 1. Tafsir Ibn Kathir, Sahih Muslim kwa Sherehe ya An-Nawawiy j. 3 uk.552, Tafsir Qurtuby.
 • 2. Tafsir Ibn Kathir.
 • 3. Sahih Bukhari j. 6 uk. 110 Kitabu-t-Tafsir, Babu qawlihi - ya ayyuha-l-ladhiyna aamanuu laa tuharrimuu twayyibaati maa ahalla llahu lakum.
 • 4. Sahih Bukhari j. 6 uk. 34, Kitabu-t-Tafsir, Babu faman tamatta'a bil-'umrati illal-hajji.
 • 5. Sahih Bukhari j. 2 uk. 375, Kitabul-hajji.
 • 6. Sahih Muslim j.3 uk. 331, Kitabul-hajji, Babu madhaahibil-'ulamaa' fiy tahallulil-mu'tamiril- mutamatti'
 • 7. Sahih Tirmidhi.
 • 8. Sahih Muslim j. 3 uk. 555 Kitabu-n-nikah, Babul-Mut'ah, ch. ya Daru-sh-Sha'b, katika sherhe ya An-Nawawiy.
 • 9. Sahih Bukhari j. 7 uk. 36, Kitabu-n-Nikah.
 • 10. Sahihi Muslim, j. 3 uk. 556 Kitabu-n-Nikah, Babul-Mut'a, ch. ya Daru-sh-sha'b katika sherhe ya An-Nawawiy.
 • 11. Tafsir Twabraniy (Tabari?), Tafsir Tha'labiy.
 • 12. Sahih Bukhari j. 3 uk. 126, Kitabu-s-swalaati-t-Taraawiyh, Babu fadhlu man qaama Ramadhaan
 • 13. Sahih Bukhari j. 2 uk. 137, Kitabu-t-Tahajjud.
 • 14. Sahih Bukhari j. 9 uk. 76, Kitabul-Ikraahi, Babul-hiylati fi-n-nikaah
 • 15. An-nihaAyah cha Ibnul-Athir.
 • 16. Sahih Bukhari j. 2 uk. 374, Kitabul-Hajj.
 • 17. Sahih Bukhari j. 2 uk. 371, Kitabul-Hajj.
 • 18. At-tafsirul-Kabir cha Ar-Raziy j. 5 uk. 153, ch. ya Daru ih'yaai-t-turaathil-arabiy, At-Tabraniy (Tabari?).

Sehemu Ya Sita: Taqiyyah

Taqiyyah ni mwanadamu kuficha ukweli wa imani yake, ili kujihifadhi katika sehemu za hatari anapohisi kuwa kuna hatari kwa nafsi yake au mali yake, kwa sababu ya kutangaza itikadi (imani) yake au kujidhihirisha nayo. Na kumepatikana baadhi ya watu wanaotuhumu Shi'a kwa itikadi (imani) yao ya Taqiyyah kwa ujahili wao wa kutojua maana yake, nafasi yake na makusudio yake. Na kama wangefanya uchunguzi katika jambo (hili) na kufahamu hukumu, wangejua kuwa Taqiyyah ambayo wanaisema Shi'a haiwahusu wao tu, wala sio wao peke yao wanaosema hivyo, bali ni jambo la dharura la kiakili.

Matakwa ya binadamu na Shariah ya Kiislamu na kila mwanadamu analazimika kutetea nafsi yake na kuhifadhi maisha yake, navyo ni vitu vitukufu mno kwake na anavyo vipenda zaidi. Ni kweli wakati mwingine inakuwa rahisi kuvitoa katika njia ya utukufu na kuhifadhi heshima na kulinda haki.

Lakini katika yasiyokuwa makusudio haya na malengo matukufu, kufanya israf kwayo na kujitumbukiza katika sehemu za hatari ni ujinga na upumbavu, akili hairidhii wala Shariah. Na Uislamu umemruhusu Mwislamu katika sehemu za hofu, kuficha haki na kuifanyia kazi kwa siri mpaka dola ya haki inusurike katika dola ya batili. Kulingana na kauli yake Allah (s.w.t.):

إِلَّا أَنْ تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ{28}

"isipokuwa mkiogopa kwao madhara.”(Ali-Imran 03:28)

Na kauli yake:

إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ{106}

"isipokuwa aliye lazimishwa na moyo wake umetulizana kwa imani". (An-Nahl 16:106)

Na kisa cha 'Ammar na wazazi wake na mateso ya washirikina kwao na baadhi ya Masahaba kwa kuwataka wakubali ushirikina na kudhihirisha kwao ukafiri ni mashuhuri. Na katika kufanya Taqiyyah kuna hukumu tatu:-

1. Wajibu: na hiyo ni ikiwa kuiacha kunasababisha kuangamia nafsi bila ya faida.

2. Ruhusa: ikiwa kuiacha kwake na kudhihirisha haki ni kuipa haki nguvu basi ana hiari kuitoa mhanga nafsi yake.

3. Haramu: na hiyo ni ikiwa kufanya Taqiyyah kunasababisha kueneza batili na kudhalilisha haki na kuihuisha dhulma na ujeuri.

Na ni maarufu kwa wafuasi wa madhehebu ya Shi'a Ithna-'Ashariyyah, na Maimamu wao wamepata balaa na kila aina ya dhiki katika uhuru wao katika zama zote ambazo madhehebu yoyote au 'Ummah wowote ule haujapata. Hivyo walilazimika katika wakati mwingi wa zama zao kutumia Taqiyyah kwa kuwaficha wanao wakhalifu kwa yale ambayo yangeleta madhara katika dini na dunia, na kwa sababu hii wamejulikana sana kwa Taqiyyah kuliko wasiokuwa wao.

Mwisho

Tumekwisha bainisha katika sehemu za utafiti huu yaliyo muhimu zaidi, ambayo kumetokea hitilafu baina ya Sunni na Shi'a, na tukabainisha njia ya sawa humo kwa kueleza dalili nyingi na hoja ambazo nyingine zimechukuliwa katika Sahih Bukhari.

Nayo ni ambayo inazingatiwa kuwa ni Kitabu muhimu cha marejeo na kinachoaminika kwa Ahl as-Sunnah baada ya Kitabu cha Allah (s.w.t.), na haikuwa kuandika kwetu kurasa hizi kwa njia hii ambayo pengine inawaumiza baadhi ya watu, isipokuwa ni wasila (njia).

Tumelazimika kuitumia baada ya waongo kuvuka mpaka kwa upeo wa uongo na upotovu; wamekwisha turushia (sisi Mashi'a) tuhuma, na uongo mbaya zaidi miongoni mwa tuhuma hizo ni ushirikina, umajusi, unasara na uyahudi; mpaka wametoa Fatwa juu ya ukafiri wetu.

Na Mawahhabi wamechukua jukumu la mwelekeo huu mwovu ambao umesababisha kuzuka fitina hii kubwa baina ya Waislamu, na kuwapoteza wasiojua miongoni mwao kwa kutumia kila njia isiyokuwa ya kisheria miongoni mwa uongo na udanganyifu katika mambo ili kufikia malengo yao ya kutenganisha 'Ummah na kuwaridhisha mabwana zao ambao kumewakasirisha kuona Uislamu unameremeta na kuamka tena kutoka katika usingizi wake wa upotofu.

Vinginevyo kwa nini hatukuona aina hii ya fitina inakua na kumea isipokuwa baada ya kufaulu kwa mapinduzi matukufu ya Kiislamu nchini Iran? Mapinduzi hayo ambayo yametikisa utawala wa madhalimu na madikteta na ambayo Waislamu wote walipata matumaini, pamoja na tofauti zao za madhehebu. Baada ya kheri na matumaini ya kuchukua hatamu za haraka, katika njia ya kuwarejesha Waislamu katika nguvu na utukufu wao baada ya kuwa dhalili, 'Ummah zinageuzwa geuzwa kama chakula kinavyogeuzwa geuzwa juu ya sahani.

Maadui wa Uislamu walipokosa njia yenye mafanikio katika kuwaweka mbali Waislamu na mapinduzi haya, wamejaribu kutia shaka katika itikadi ya watu wake baada ya kushindwa vibaya sana kuvunjika hayo kwa Helikopta zao ambazo Allah (s.w.t.) aliuwezesha mchanga wa jangwani kuziharibu na kuzisambaratisha, na kuharibu mbinu zao katika vita vyao ambavyo walipanga kupitia mamluki wao mtiifu ambaye walimvalisha vazi la utaifa hakuvuna isipokuwa hasara na fedheha katika mwito wake mwovu wa utaifa.

Amesema Sheikh mwanajihadi Abdulhamid Kishki, katika mazungumzo yake ya kujibu kauli ya mwovu huyo mwenye kuajiriwa: "Kwamba watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wao ni Wafursi tu, hawajui Uislam wala Qur'an ambayo imeteremka kwa Waarabu na lugha yao, hivyo wao wanajua zaidi kuliko watu wengine wasio kuwa Waarabu kwa kusema kuwa Shi'a wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni Waislamu wenye kumpwekesha Allah (s.w.t.) na Uislamu wao umekuwa mzuri tangu walipoingia katika Uislamu katika zama za 'Umar."1

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alishabashiri tangu karne ya kumi na nne, watu hawa ambao walipokea Uislamu na kuupeleka katika taifa hili la Kiislamu lililopo sasa, katika Hadith ambayo ameitoa Bukhari katika Sahih yake.

Kutoka kwa Thaur kutoka kwa Abu Huraira amesema: "Tulikuwa tumekaa kwa Mtume (s.a.w.w.), basi akateremshiwa Surah al-Jumuah (na wengine miongoni mwao bado hawajajiunga nao) akasema: 'Nilisema nani hawa ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) hakumjibu hadi akauliza mara tatu na alikuwepo pamoja nasi Salman Al-Farsi akaweka mkono wake juu ya Salman, kisha akasema kama imani ingekuwa kwenye sayari basi wangeifikia wanaume au mwanamume katika hawa."2

Na Allah (s.w.t.) ameashiria katika Kitabu chake kitukufu juu ya watu hawa kwa kauli Yake: "Ninyi ndiyo mnalinganiwa ili mtoe katika njia ya Allah (s.w.t.) miongoni mwenu kuna wanaofanya ubakhili na anaefanya ubakhili hakika anafanya ubakhili kwa nafsi yake na Allah (s.w.t.) ni tajiri na nyinyi ni mafakiri na kama mtakataa ataleta watu wengine, kisha hawatakuwa mfano wenu."3

Kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika Mtume (s.a.w.w.) alisoma Ayah hii (na kama mtakataa ataleta watu wengine kisha hawatakuwa mfano wenu)." Wakasema: "Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) nani hao ambao kama tutakataa wataletwa baada yetu kisha hawatakuwa mfano wetu?" Basi akapiga juu ya paja la Salman kisha akasema: "Huyu na watu wake na kama dini ingekuwa katika sayari basi wangeifikia wanaume kutoka Farsi (Jamhuri ya Kiislamu ya Iran)."4

Lakini maadui wa Uislamu hawakukata tamaa baada ya kushindwa kwao katika uwanja wa mapambano na bado wanazo nafasi nyingine wanazopigana na huu ndiyo Uwahhabi umeshika nafasi ile ile.

Lakini kwa mara hii ni kwa silaha tofauti, wameshawavalisha askari wao vazi la Uislamu huenda ukawa unang'ara zaidi kuliko vazi la utaifa ambao umegeuka kuwa majivu katika upande wao wa mashariki.

Hila mpya kwa masikitiko makubwa imewakumba baadhi ya watu wasiojua, na wengi wametumbukia katika mtego wa fitina hii, ambayo hawajui itawapeleka wapi! "siku ambayo haitafaa mali wala watoto isipokuwa yule atakaye mwendea Allah kwa moyo safi."

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alishatahadharisha hadhari kubwa kutokutumbukia kwenye moto wa fitina hii, kama wangekuwa wanajua Sunnah zake katika Hadith nyingi ambazo amebainisha humo hata wale watakao isababisha kama ilivyo katika Hadith aliyoitoa Bukhari katika Sahih kutoka kwa Naf'i kutoka kwa Ibn 'Umar amesema:”

Mtume (s.a.w.w.) alisema: "Ewe Allah! Tubariki sisi katika Sham. Ewe Allah! Tubariki sisi katika Yemen." Wakasema: "Na katika Najd?" Akasema: "Ewe Allah! Tubariki sisi katika Sham. Ewe Allah! Tubariki sisi katika Yemen." Wakasema: "Ewe Mtume wa Allah! Na katika Najd?" Alisema mara tatu: "Huko kuna tetemeko na fitina na huko kutachomoza upembe wa Shetani.”5

Na kundi lililokusudiwa katika Hadith iliyotangulia hatuoni isipokuwa linaafikiana na kundi la Mawahhabi ambalo muasisi wake ni Muhammad bin Abdul-Wahhab amezaliwa katika moja ya vijiji vya Najd kinachoitwa Uyainah. Kundi hili ambalo limekuwa ni tezi la kansa katika jamii ya Kiislamu na kukua kwake na kuendelea kwa juhudi zake za kubomoa katika njia ya kurejea Uislamu mtukufu; kwa hakika si lingine isipokuwa ni fitina nyuma yake umesimama ukoloni mwovu kama ambavyo historia yake inaonyesha hivyo na unalenga kwenye:-

1. Kubomoa shakhsiyyati (watu muhimu) za kidini kwa kuzuia watu kuwa karibu yao na kuwa karibu na athari na misingi yao.

2. Kutoa Uislamu kwa sura ya dini kavu isiyo na maendeleo ambayo haikubali kutekelezeka katika zama mbali mbali.

3. Kutengeneza vikundi na hitilafu katika safu za Waislamu kwa kuzuia umoja na udugu wao.

Na wameichukulia Tawhid kuwa ni uwanja wa malengo yao maovu kwa kutuhumu madhebu mengine kwa ushirikina kwa kudai kwamba tawassul kwa Manabii na watu wema ni chanzo cha ushirikina, wakapinga kwa hilo yaliyo pokewa kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa tawatur kwa kuruhusu hilo.

Na yanatutosha aliyoyatoa Bukhari katika Sahih yake juu Tawassul ya 'Umar kwa 'Abbas. Kutoka kwa Anas: "Hakika 'Umar al-Khattab alikuwa wakipatwa na ukame akimwomba 'Abbas bin 'Abdul-Muttalib awaombee mvua akasema: "

Ewe Allah (s.w.t.) hakika sisi tulikuwa tuna-tawasali kwako kupitia kwa Nabii (s.a.w.w.) wetu na unatunyesheleza, na hakika sisi tuna-tawasali kwako kupitia kwa Ami wa Nabii wetu basi tunyesheleze akasema: 'Basi wanateremshiwa mvua.'"6

Bali inatosha kwa kuwajibu Mawahhabi kwa kauli yake alama zao7 ni kunyoa (wanawake vipara). Kama alivyopokea hayo Bukhari katika Sahih yake, hakika hakufanya hayo yeyote miongoni mwa wazushi isipokuwa wao kama ilivyo julikana hivyo katika historia yao.8

Na katika Hadith nyingine Nabii alibainisha maelekezo yake ya kinabii kwa watu katika yaliyo " wajib kuyafanya wakati zinapotokea fitna " kama hizi; anasema watu walikuwa wanamwuliza Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuhusu kheri na nilikuwa namwuliza kuhusu shari kwa kuogopa isije ikanifika.

Nikasema:"Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Hakika sisi tulikuwa katika ujahili (ujinga) na shari, Allah (s.w.t.) akatuletea kheri hii je baada ya kheri hii kuna shari?"

Akasema: "Ndiyo!"
Nikasema:"Je baada ya shari hiyo kuna kheri?"
Akasema: "Ndiyo na kuna dakhani (wanaoongoza bila ya uongofu)."
Nikasema:"Je dakhani ni nini?"
Akasema: "Ni watu wanaoongoza bila ya uongofu, baadhi yao utawajua na baadhi yao hutawajua."
Nikasema:"Je! baada ya kheri hiyo kuna shari?"
Akasema: "Ndiyo, wenye kulingania katika milango ya Jahannam atakaye waitikia watamtupia humo."
Nikasema:"Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Tupe sifa zao."
Akasema: "Wao ni katika kabila letu, wanazungumza lugha yetu."
Nikasema:"Unaniamuru nini kama hayo yatanifikia?"
Akasema: "Jilazimishe na jamaa ya Waislamu na Imam wao.
Nikasema:"Na kama hawatakuwa na jamaa wala Imam?"
Akasema: "Basi jitenge na kundi hilo lote hata kama ni kung'ang'ania shina la mti hadi mauti yakufikie na wewe uko hapo."9

Na Hadith ya hapo juu inabainisha wazi wajibu wa kujilazimisha kushikamana na jamaa ya Kiislamu na Imam wao, na kwamba katika hali ya mkanganyiko wa mambo kutofahamika na kutowezekana kujua uhakika wake.

Basi maelezo ya Nabii yanatuamuru kunyamaza na vile vile Hadith inabainisha kuwa walinganiaji katika milango ya Jahannam atakaye waitikia watamtupia humo sio katika Waajemi bali ni katika Waarabu, na haya yanatilia mkazo yaliokuja katika Hadith iliyotangulia (kutoka Najd).

Jambo hili lazima limfanye Mwislamu awe katika hali ya uangalifu sana na tahadhari kwa kufuata mwendo unao mpelekea kwenye usalama katika Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), na hasa pamoja na kuwepo makundi mengi ambayo idadi yake ni sabini na tatu, kila moja linadai kuwa kunukuu kwake Sunnah za Nabii (s.a.w.w.) ni sahih na amekwishatupa habari ambaye hatamki kwa matamanio yake kuwa kundi moja tu ndilo Sahihi na mengine sio Sahih.

Hivi ndivyo zilivyo patikana tofauti na Ikhtilaf hadi Waislamu wakawa wanatahayari na wenye kushangaa kwa yote yanayotendeka pembezoni mwao, miongoni mwa zogo hili kubwa na fitina kubwa.

Na mimi sishangai tahayari hii na mshangao huu, kwani Nabii wa Uislam amekwisha ashiria kuhusu jambo hili kwa kauli yake: "Uislamu umeanza katika hali ya ugeni na utarejea kuwa mgeni kama ulivyoanza." Je, ugeni hauko katika Waislamu kumpiga vita yule ambaye ni Mwislamu halisi? Je, sio ugeni! Na mshangao zaidi kwa watoa mawaidha kusimama na vilemba vyao juu ya mimbar na kupaaza sauti na hali wakiwakufurisha ambao ni Waislamu halisi?
Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.) umesema kweli na hawa ndio Waislamu wanawapiga vita na kuwakufurisha Mashi'a (wafuasi wako) ambao wameshikamana na Sunnah zako kupitia katika njia ya viumbe watoharifu zaidi (Ahlul Bayt (a.s.)) baada yako. Hakika wao wanampiga vita huyu mwenye kurejea na watu wake wamekuwa wageni katika kundi la Waislamu na wamepotoshwa na kupelekwa katika njia ya wale ulio tahadharisha kuwa ndiyo machomozo ya upembe wa Shetani, tetemeko na fitina. Na ulishasema kuwa kundi katika 'Ummah wangu halitaacha kudhihirisha haki, hata wadhuru atakaye wakhalifu mpaka itakapokuja amri ya Allah (s.w.t.) kulingana na kauli ya Allah (s.w.t.):

لَقَدْ جِئْنَاكُمْ بِالْحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ {78}

"Tumekwisha wajieni kwa haki, lakini wengi wenu wanaichukia haki.”(Az-Zukhruf 43:78)

Na umekwisha mbashiri Mahdi wa Aali Muhammad mjukuu wako na wasii wako, Imam wa kumi na mbili (Al Imam Muhammad Mahdi Sahib az-Zamaan (a.s.)) ambaye atajaza dunia haki na uadilifu, baada ya kujazwa dhulma na jawr (ujeuri) na umetuamuru kuelekea kwake hata kama ni kwa kutembea juu ya theluji kwa kauli yako: "Hakika sisi ni Ahlul-Bayt; Allah (s.w.t.) ametuchagulia akhera dhidi ya dunia, na hakika watu wa nyumba yangu watapata baada yangu tabu, shida na kufukuzwa katika nchi, mpaka watakuja watu, (kutoka hapa akaashiria kwa mkono wake upande wa mashariki) watu wenye bendera nyeusi, wataombwa haki, lakini hawataitoa watapigana, basi watanusurika na watapewa wayatakayo hawatakubal,i hadi wampe mwanamme katika watu wangu. Basi ataijaza dunia uadilifu kama ilivyojazwa dhuluma, basi atakaye fikiwa na huyo amwendee, hata kama ni kwa kutembea juu ya theluji.10

Mwisho wa ulingano wetu tunamwomba Allah (s.w.t.), atuja'alie kuwa miongoni mwa ambao wanasikiliza kauli, wakafuata mazuri yake. Na shukurani njema ni za Allah (s.w.t.) Mola wa viumbe, sala na salamu zimwendee Bwana wetu Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) na Ahlul Bayt zake watoharifu.

Wassalamu ‘alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
 • 1. Abdul-Hamid Kishki kanda na. 385.
 • 2. Sahih Bukhari j. 6 uk. 390, Kitabu-t-Tafsir, Babu - wa aakhariyna minhum lammaa yal'haquu bihim -; Sahih Muslim j.5 uk. 408, Kitabul-fadhaail, Babu fadhli ahli Faaris, ch. ya Daru-sh-sha'b katika sherhe ya An-Nawawiy.
 • 3. Surat Muhammad 47: 38. 282 Tafsir Ibn Kathir, Qurtubi ,Twabary na Durrul-Manthur.
 • 4. Tafsir Ibn Kathir, Qurtubi ,Twabary na Durrul-Manthur.
 • 5. Sahih Bukhari j. 9 uk. 166, Kitabul-fitan, Babul-fitnati min qibalil-mashriq.
 • 6. Sahih Bukhari j. 2 uk. 66, Kitabul Istisqaa'.
 • 7. Sahih Bukhari j. 9 uk. 489, Kitabu-t-Tawhid, Babu qiraa'atil-faajiri wal-munaafiq.
 • 8. Fitnatul-Wahabiyyah uk. 77, chapa ya Istambul - 1978
 • 9. Sahih Bukhari j. 9 uk. 159, Kitabul-fitani, Babu kayfal-amru idhaa lam yakun jamaa'ah..
 • 10. Tarekh