Ubashiri Wa Kuja Kwa Imam Mahdi A.S.

Wale waliokuwa wakitoa ubashiri walikuwa wakiishi huko Bara la Arabia na walikuwa wakijua vyema kiwango fahamu za watu wenzao na hivyo tutaona kuwa ubashiri mwingi utazungumzia Mashariki ya Kati. Popote pale walipokuwa wakiulizwa maswali, wao walikuwa wakizingatia elimu na fahamu ya mwulizaji. Zipo jumla zingine zilizotumika kijumla kama 'ardhi' n. k. katika mabashiri.

Jambo lingine la kukumbuka ni kwamba kumetokea mabadiliko na hata kamili katika mazingira na kisiasa kuanzia wakati huo. Majina ya miji imebadilika na miji mingi kuangamizwa kabisa na ikatoweka. Na miji mipya kutokezea. Hivyo ni ombi kwa msomaji kujaribu kupitia vitabu vya jiografia vya mambo ya kale ili aweze kupata ufafanuzi zaidi.

IIikuwa ni desturi ya Waarabu kujulikana kwa majina ya baba, familia au ukoo, hivyo ndivyo ilivyo tumika muundo huo huo katika majina humu kitabuni.

Ubashiri wa kuja kwa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. umegawanywa na kuchambuliwa kama ifuatavyo:
(1) Ubashiri wa kawaida,
(2) Ubashiri maalum na
(3) Ubashiri wa lazima.

(1). Ubashiri wa Kawaida.

Abdullah ibn Abbas (r. a. ) amesema kuwa baada ya kumaliza Hajj ya mwisho (mwaka wa 10 Hijriyyah), Mtume Mtukufu s.a.w.w alisimama mbele ya mlango wa Ka'aba Tukufu, akiwa ameshikilia komeo ya mlango, huku akiwauliza ma-Sahaba wake: "Je, nikuambieni dalili za siku ya QayamaError: Reference source not found?" Salman Farsi (r. a. ) ambaye alikuwa karibu naye,alisema: "Ndiyo, Ewe Mtume wa Allah swt. "

Mtume Mtukufu s.a.w.w akasema, "Hakika, miongoni mwa dalili za saa, ni kuwa:
(1) watu watapuuza salaError: Reference source not found,

(2) watafuata matamanio yao wenyewe

(3) wataelekeza kujipendelea wao wenyewe,watawaheshimu matajiri

(4) na watauza Dini yao kwa manufaa ya kidunia

(5) wakati huo roho na moyo wa Muumin itayayuka (kwa huzuni) kama chumvi inavyoyayuka katika maji,kwa sababu ataona mambo yaliyoharamishwa na hataweza kuyabadili. "

Salman akasema: "Haya yatatokea,ewe Mtume wa Allah swt?"
Mtume Mtukufu s.a.w.w akasema: "Ndiyo,naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake. "

"Ewe Salman,:
(6) wakati huo watawala watakuwa wadhalimu

(7) Mawaziri watakuwa waasi,

(8) na wadhamini (wale waliopewa amana kwa kuaminiwa) watafanya hiana

(9) hakika wakati huo maovu yatakuwa mema na mema yatakuwa maovu

(10) wale wafanyao hiana wataaminiwa na waaminifu watafikiriwa kuwa si waaminifu;

(11) na mwongo atasadikiwa,na msema kweli atahesabiwa mwongo

(12) Wakati huo kutakuwapo na utawala wa wanawakeError: Reference source not found

(13) Masuria watashauriwa

(14) na watoto watakaa juu ya mimbarError: Reference source not found

(15) udanganyifu utahesabiwa kuwa ni uerevu

(16) na Zaka itakuwa ni kama kutozwa faini;

(17) na mateka ya vita (yaani mali ya ummahError: Reference source not found) yatakuwa kama ni mali ya mtu binafsi;

(18) na mtu atakuwa mjeuri kwa wazazi wake na atakuwa mwema kwa marafiki zake

(19) na wakati huo kutatokea na nyotaError: Reference source not found zenye mikia (comets). "

Salman akasema: "Haya yatatokea, ewe Mtume wa Allah swt?"

Mtume Mtukufu s.a.w.w akasema: "Ndiyo, naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake. "

"Ewe Salman!:
(20) wakati huo mwanamke atakuwa mshiriki wa mumewe katika biashara,

(21) na mvuaError: Reference source not found itakuwa motoError: Reference source not found sana

(22) na watu wema watabaki katika huzuni;

(23) na masikini hawata heshimiwa;

(24) na wakati huo masoko yatakaribiana,

(25) Tena huyu atasema,"Mimi sikuuza chochote, na yule atasema, "Mimi sikupata faida yoyote. " Kwa hivyo hutamkuta mtu yeyote asiyemlalamikia Allah swt.

"Ewe Salman!
(26) tena itatokea iwapo watu watawazungumzia watawala wao, watawaua, na ikiwa watanyamaza kimya, watanyang'anywa mali yao, watanyimwa heshima zao, watamwaga damuError: Reference source not found yao na mioyo ya watu itajaa woga; kisha hutamwona mtu yeyote ila atakuwa mwoga, mwenye khofu, ametishika na ameshstushwa”

"Ewe Salman!
(27) Bila shaka wakati huo mambo fulani yataletwa kutoka Mashariki

(28) na mambo fulani yataletwa kutoka Magharibi,

(29) Basi ole kwa watu walio dhaifu (wa imani) katika UmmahError: Reference source not found wangu kutokana na hayo; Ole ya Allah swt iwe kwa hayo. Wao hawatakuwa na huruma juu ya wadogo wao, wala hawatamsamehe yeyote aliyefanya kosa. Miili yao itakuwa ya wanadamu, lakini mioyo yao itakuwa ya mashetani. "

"Ewe Salman!
(30) Wakati huo wanaumeError: Reference source not found watawaashiki wanaume,

(31) na wanawakeError: Reference source not found watawaashiki wanawake;

(32) na watoto wa kiume watapambwa kama wanawake;

(33) na wanaume watajifanya kama wanawake

(34) na wanawake wataonekana kama wanaume;

(35) na wanawake watapanda mapando (farasi na ngamia)

(36) Hapo tena patakuwepo laana ya Allah swt juu ya wanawake wa UmmahError: Reference source not found wangu. "

"Ewe Salman!
(37) Bila shaka wakati huo MisikitiError: Reference source not found itapambwa (kwa dhahabu n. k. ) kama inavyofanywa katika masinagogi na makanisa,

(38) na QuranError: Reference source not found zitapambwa (kwa nakshi na rangi za kupendeza n. k. )

(39) na minara ( ya misikiti) itakuwa mirefu; na safu za watu wanaosimama katika salaError: Reference source not found zitazidi, lakini nyoyo zao zitachukiana na maneno yao yatatofautiana. "

"Ewe Salman!
(40) Wakati huo wanaumeError: Reference source not found watatumia mapambo ya dhahabu; kisha watavaa hariri,n a watatumia ngozi za chui. "

"Ewe Salman!
(41) Wakati huo ribaError: Reference source not found itakuwako,

(42) na watu watafanyia biashara kwa kusemana na rushwa

(43) na dini itawekwa chini, na dunia itanyanyuliwa juu. "

"Ewe Salman!
(44) Wakati huo talaqaError: Reference source not found zitazidi

(45) na Sheria ya Allah swt haitasimamishwa. Lakini hayo hayatamdhuru Allah swt. "

"Ewe Salman!
(46) Wakati huo watatokea wanawakeError: Reference source not found waimbaji,

(47) na ala za muziki

(48) na wabaya kabisa watawatawala UmmahError: Reference source not found wangu. "

"Ewe Salman!
(49) Wakati huo matajiri katika UmmahError: Reference source not found wangu watakwenda Kuhiji kwa matembezi, na walio wastani kwa biashara,na masikini kwa kujionyesha.

(50) Hivyo basi wakati huo watakuwapo watu ambao watajifundisha QuranError: Reference source not found si kwa ajili ya Allah swt na wataifanya QuranError: Reference source not found kama ala ya muziki.

(51) Na watakuwapo watu ambao watasoma dini si kwa ajili ya Allah swt

(52) na idadi ya wanaharamu itazidi

(53) watu wataiimba QuranError: Reference source not found,

(54) na watu watavamiana kwa uroho wa kidunia. "

"Ewe Salman!
(55) Haya yatatokea wakati heshima zitakapoondoka, na madhambi yatatendwa

(56) na watu waovu watakuwa na uwezo juu ya watu wema,

(57) na uongo utaenea na mabishano (matusiError: Reference source not found) yatatokea

(58) na umasikini utaenea,

(59) na watu watajivuna kwa mavazi yao

(60) na itakuwepo mvuaError: Reference source not found wakati si wake

(61) na watu watacheza dama, kamari na Ala za muziki,

(62) na hawatapenda kuhimizana mema wala kukatazana maovu

(63) na kwa ajili hali itakavyokuwa hata itafikia wakati huo kuwa Muumin atakuwa na heshima ndogo kuliko hata mjakazi

(64) na wanaosoma na wanaotumia wakati wao katika kumwabudu Allah swt watalaumiana.

(65) Hao ndio watu watakaoitwa wachafu na wanajisi katika Ufalme wa mbinguni. "

"Ewe Salman!
(66) Wakati huo matajiri hawataogopa chochote isipokuwa mtu masikini; hadi kwamba masikini wataendelea kuomba kati ya ijumaa mbili, na hawatamwona mtu yeyote wa kutia chochote mikononi mwao. "

"Ewe Salman!
(67) Wakati huo itazungumzwa Ruwaibidhah. "

Salman akauliza: "Ni nini Ruwaibidhah ? Ewe Mtume wa Allah swt, baba na mama yangu wawe fidia kwako. "

Mtukufu Mtume s.a.w.w akajibu:
(68) "Watu fulani watazungumza kuhusu mambo ya watu ambayo hayakuwahi kuzungumzwa namna hii zamani.

(69) Tena baada ya muda mchache machafuko yatatokea duniani,na kila nchi itafikiri kuwa machafuko yapo katika nchi yao tu. "

(70) "Watabaki katika hali hiyo kwa muda ambao Allah swt atapenda wabaki;

(71) kisha ardhi itatapika vipande vya moyo wake dhahabu, fedha na madini mengineyo;

(Hapo Mtume s.a.w.w ) alinyosha kidole chake penye nguzo, na akasema: "Kama hizi (kwa ukubwa), lakini siku hiyo dhahabu wala fedha hazitamsaidia mtu yeyote. Na hii ndiyo maana ya maneno ya Allah swt 'Hakika dalili Zake zimekuja. '1

Zipo habari zingine zilizoelezwa katika vitabu vinginevyo kwa kupitia Jabir Ibn Abdullah Ansari, ambavyo ninazitaja:

"Ewe Salman! Wakati huo:
(1) Wazee watajitumbukiza katika mambo ya ushirikina na uchawi,

(2) ghiba ndiyo itakuwa mazungumzo yenye kupendeza,

(3) mali iliyopatikana kwa njia za haramu, itachukuliwa kama ndiyo neema,

(4) wazee hawatakuwa na mapenzi ya wadogo na vile vile wadogo hawatawajali wazee na kuwaheshimu

(5) Islam itabakia kwa jina tu kwani wafuasi wake hawatakuwa wakifuata maadili na maamrisho yake,

(6) Kimbunga kikubwa cha rangi nyekundu kitatokezea mbinguni na kutaanguka mawe kutoka mbinguni

(7) nyuso zitakuwa za kuchukiza

(8) kutakuwa na mitetemeko na kuporomoka kwa ardhi kila mara.

Hapo Sahaba walimwuliza Mtume s.a.w.w , "Ewe Mtume wa Allah swt, je lini yatakapotokea hayo yote?" (pamoja na nishani na dalili za hapo juu, baadhi zimeongezeka hapa chini)

Mtume s.a.w.w aliwajibu:
(9) Watu watakuwa watumwa wa shahwa au matamanio yao

(10) watu watakuwa walevi wa kupindukia kwani matumizi ya uleviError: Reference source not found utakithiri na utakuwa ukipatikana kwa udhahiri bila ya watu kuona aibu ya aina yoyote,

(11) Wanaume watakuwa wakiwatii wake zao,

(12) jirani atakuwa wakiwaudhi na kuwatesa majirani wenzake,

(13) Wakubwa hawatakuwa watu wenye huruma, mioyo yao itakuwa imejaa kwa maonevu,

(14) vijana hawatakuwa na heshima

(15) watu watajenga majumba imara na marefu mno,

(16) wafanyakazi watadhulumiwa hakiError: Reference source not found zao,

(17) ushahidi wa kiuongo utachukuliwa kuwa wa kawaida,

(18) ndugu atakuwa akimwonea wivu ndugu yake halisi

(19) watu watakaokuwa wakifanya biashara kwa ushirika, basi watakuwa daima wakifikiriana mbinu za kumdhulumu mwenzake,

(20) mambo ya zinaaError: Reference source not found yatakuwa kama kawaida kwani yatatendeka na kusikika pia.

(21) ile mioyo ya kutaka kusaidia watu wengine itakuwa imetoweka,

(22) Maasi na dhuluma itaongezeka kupita kiasi,

(23) matumbo ya watu itachukuliwa kuwa ndiyo miungu yao, kwani hawatajali kiwevyo, ilimradi wapate chochote kile,

(24) wanawakeError: Reference source not found watakuwa wakitawala akili za wanaumeError: Reference source not found na watakuwa wakiwaendesha wanaume vile watakavyo wao,

(25) kutatokea Maulamaa au wanazuoni waovu kabisa kwani watajionyesha kuwa ni wacha Mungu na wenye elimu, ambapo kwa hakika watakuwa waroho wa mali ya dunia tu. "

Hapo Mtume Mtukufu s.a.w.w aliwaonya: "Kumbukeni, wakati kama huo utakapokuja, basi Allah swt atatumbukiza watu katika balaaError: Reference source not found za aina nne:
(1) kutawaliwa na watawala dhalimu
(2) ukame na vitu vya matumizi ya kila siku kuwa bei ghali yaani kupanda kwa maisha,
(3) dhuluma za watawala
(4) kuabudu miungu. "

Sahaba waliposikia hayo walishtushwa na kuuliza: "Ewe Mtume wa Allah swt ! Je kweli kuwa Mwislamu atakuwa akiabudu miungu na masanamu?"

Mtume s.a.w.w aliwajibu: "Naam! Kwao mapesa yatakuwa kama miungu kwani watakuwa wakiziabudu kupindukia kiasi. "

Kwa hakika sisi tunayashuhudia haya yote yakitokea ambayo Mtume s.a.w.w amekwisha bashiri karibu karne kumi na nne zilizokwishapita. Imam Ali a.s. katika khutba yake ijulikanayo kama Al-Bayan anaelezea ubashiri kwa undani zaidi. Wasomaji wenye kutaka kupata habari zaidi wanaweza kutazama (1) Yanabi-ul-Muwaddah (2) Basharat-ul-Islam, Sayyid Mustafa Ali-Sayyid Haider al-Kazami, chapa ya BaghdadError: Reference source not found.

Ubashiri ya Imam Ja’far As-Sadiq A.S.

Mazungumzo yafuatayo yamefanywa na Imam Jaafer as-Sadiq a.s. ambamo ameripoti ubashiri wa siku za mwisho wa dunia hii. Yametolewa kutoka Darul Islam, Bihar-ul-Anwar na Raudhat-ul-Kafi. Wanaoripoti habari hizo ni Allamah Naraqi na Sheikh Kulaini r. a. kutokea kwa Himran.

Imam a.s. alisema:
(1) "Haki itakuwa imetokomezwa na watu walio katika hakiError: Reference source not found hawatapatikana.
(2) Dhulma na uonevu utaenea katika miji yote.
(3) Kufuata QuranError: Reference source not found kimatendo itajulikana kama tabia ya kizamani.
(4) Zitatolewa maana ya Aya za QuranError: Reference source not found kwa mujibu wa matakwa ya watu, hivyo mafhum ya Quran itakuwa imebadilishwa na kupotoshwa.
(5) Wadhalimu watakuwa wakiwa kandamiza wale walio katika haki.
(6) Uchokozi na uchochezi utatokea kutoka kila pande na pembe.
(7) Matendo maovu na kukosa aibu vitaenea na kuzagaa kila mahala.
(8) UlawitiError: Reference source not found utakuwa ni jambo la kawaida.
(9) Muumin atakuwa akionekana kama mtu dhalili ilhali waovu watakuwa wakiheshimiwa
(10) Vijana hawatakuwa wakiwaheshimu wakubwa wao
(11) Huruma itakuwa imepotea kabisa.
(12) Waovu watakuwa wakitukuzwa kwa udhalimu wao na hakutakuwapo na mtu yeyote wa kuwapinga.
(13) Wanaume watafurahishwa mno kwa kuingiliana na wanaumeError: Reference source not found wenzao.
(14) Wanawake watawaoa wanawakeError: Reference source not found wenzao.
(15) Mapesa yatatumika kwa ajili ya matumizi yale yaliyo haramishwa na Allah swt.
(16) Starehe, anasa na zinaaError: Reference source not found zitashamiri.
(17) ZinaaError: Reference source not found itajulikana kama maadili yaliyopitwa na muda.
(18) Muumin atatengwa kwa sababu ya kufanya ibada za Allah swt.
(19) Jirani mmoja atafurahi mno kwa kumuudhi na kumbughudhi jirani mwenzake.
(20) Wazushi (kama Salman Rushdie wa Uingereza) watatukuzwa na kusifiwa katika kueneza fitina na yale wanayozusha.
(21) Ushauri mzuri utakanwa.
(22) Milango ya wema yatafungwa wakati milango ya maovu yatafunguliwa.
(23) Al-KaabaError: Reference source not found haitatumika au haitafikika kwa sababu ya vikwazo na ugumu utakaowekewa mahujaji.
(24) Watu watalazimishwa kuacha kwenda MakkahError: Reference source not found kuhiji.
(25) Watu hawatakuwa wakitimiza ahadi zao watakazokuwa wakizitoa.
(26) Wanaume watakuwa wakitumia dawa za kuamsha tamaa za kiume kwa ajili kulawiti na wanawakeError: Reference source not found watakuwa wakitumia vyakula vya mafuta ili kujitayarisha kwayo.
(27) Baadhi ya wanaume watakuwa wakiishi kwa kujipatia mapesa kwa kuuza mikundu yao
(28 ) na wanawake watakuwa wakijipatia mapesa kwa kufanyisha biashara uuke wao.
(29) Wanawake wataunda vilabu vyao, mashirika na umoja wao.
(30) Wanaume atajigeuza kama wanawake na watavutia na wanawake.
(31) Wanaume watajirembesha kama wanawake.
(32) Ulawiti utachukuliwa kama ndiyo ustaarabu na starehe ya kweli. Na Banu Abbas watalipia ulawiti.
(33) Wanawake wataona fakhari kwa kuwa na waume nje ya mume mmoja wa ndoa na vivyo hivyo wanaumeError: Reference source not found watakuwa hivyo hivyo.
(34) Heshima itakuwa ikitolewa kwa utajiri wa mtu na wala si ucha Mungu.
(35) ribaError: Reference source not found ndiyo itakayokuwa biashara ya kila siku.
(36) Ushahidi wa uongo utakuwa ukisadikiwa mno.
(37) Kile alichokiharamisha Allah swt kitachukuliwa ni halali na chochote kile alichokihalalisha Allah swt kitachukuliwa ni haramu.
(38) Maamrisho ya Dini yatageuzwa kwa mujibu wa matakwa yao.
(39) Wachokozi na waovu watatenda maovu kwa udhahiri bila ya khofu yoyote ile na Muumin hawataweza kuwazuia vyovyote vile.
(40) Watawala watawapenda mno Makafiri kuliko Muumiin.
(41) RushwaError: Reference source not found ndiyo itakuwa njia ya kujitimizia kazi kutoka maofIssa wanaohusika.
(42) Wanaume wata walawiti wake zao.
(43) Watu watakuwa wakiuawa kwa visingizio vidogo vidogo na magomvi madogo madogo.
(44) Wanawake watawafanyia wanaume dhihaka, nao watashawishiwa kufanya uhusiano na wanawakeError: Reference source not found.
(45) Wanaume wataishi kwa mapato ya wake zao zitakazopatikana kwa zinaaError: Reference source not found.
(46) Wanawake watakuwa wakiendesha hukumu majumbani huku wanaume wakiwatii wake zao kwa sababu wanawake hao ndio watakuwa wenye mapato.
(47) Wanawake watatumiwa katika kupatikana huduma mbalimbali.
(48) Kula kiapo kwa jina la Allah swt litakuwa ni jambo lililowekwa ulimini.
(49) PombeError: Reference source not found na kamari vitapatikana kila mahala na vitakuwa vimezagaa.
(50) wanawakeError: Reference source not found wa Kiislamu wataingiliana na Makafiri, ambapo Waislamu hawataweza kuwazuia na wala hawatakuwa na uwezo kama huo.
(51) Maadui wetu watasaidiwa na watawala na marafiki zetu watadhalilishwa kiasi kwamba hata kiapo chao hakitakubaliwa.
(52) Udanganyifu na hila ndizo zitakuwa desturi miongoni mwa watu.
(53) Usomaji na usikilizaji wa QuranError: Reference source not found utakuwa ni bughudha kwa watu.
(54) Kusikiliza mambo fidhuli ndiyo itakuwa ikipendelewa na watu.
(55) Jirani hatamstahi jirani mwenzake illa kwa khofu ya ulimi mkali na mchafu.
(56) Sheria na kanuni za Allah swt hazitatambuliwa na waovu hawataadhibiwa kwa maamrisho hayo.
(57) Ghiba na kulaghaiana ndivyo vitakuwa vitu vya kawaida.
(58) Madhumuni ya Hajj na Jihad yatakuwa mbali na yale ya Kiislamu.
(59) MisikitiError: Reference source not found itarembeshwa kwa dhahabu.
(60) Watawala watawataka ushauri kwa nia ya Makafiri.
(61) Litakuwa ni jambo la kawaida kuibia katika uzani na vipimo vya biashara.
(62) Kumwaga damuError: Reference source not found ya watu wegine litakuwa ni jambo la kawaida.
(63) Watu watajigamba kwa ndimi zao chafu zenye matusiError: Reference source not found mabaya ili kuwatishia watu wengine.

Imam a.s. aliendelea kusema:
(64) "Watu watakuwa wakipuuzia salaError: Reference source not found na kutojali.
(65) Watu hawatakuwa wakilipa zakaError: Reference source not found ingawaje watakuwa na utajiri mkubwa.
(66) Sanda za maiti zitakuwa zikiibiwa na kuuzwa tena
(67) Mauaji yatakithiri mno kiasi kwamba hata wanyama pia wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.
(68) Watu watakuwa wakisali katika mavazi ya kiajabu.
(69) Macho na mioyo itapoteza nuru zao za heshima na huruma.
(70) Watu watakuwa wamejishughulisha na maswala ya kutafuta mali na mapesa tu.
(71) Watu watasali kwa kuonyesha tu.
(72) Watu watatafuta elimu ya Dini kwa ajili ya kujipatia mali ya dunia.
(73) Ushirika katika makundi yatakuwa ndiyo mambo ya maisha.
(74) Wale watakaojipatia riziki kwa njia ya halali, watasifiwa kwa midomo tu.
(75) Matendo maovu na machafu yataenea hata MakkahError: Reference source not found na MadinaError: Reference source not found.
(76) Watu waliokufa watafanyiwa mizaha na vichekesho.
(77) Mwaka hadi mwaka hali itakuwa ikiendelea kuharibika kuwa mbaya zaidi.
(78) Matajiri wataigwa.
(79) Masikini, mafukara watafanyiwa dhihaka na kufedheheshwa.
(80) Matukio ya kudura kama yale ya mitetemeko, maporomoko n. k. yatakuwapo lakini watu watakuwa hawaviogopi.
(81) Matendo maovu yatakuwa yakitendwa kiwaziwazi.
(82) Wazazi watatupa watoto wao na watoto watawatusi wazazi wao na daima watakuwa wakitaka mali na utajiri wa wazazi wao.
(83) Wanawake hawatawatii na kuwafuata waumeError: Reference source not found wao.
(84) Siku itakayopita bila ya mtu kutenda madhambi, basi itachukuliwa ni siku yenye nuksi.
(85) Watu wenye uwezo wataficha mali muhimu na kuviuza kwa bei ya ulanguzi.
(86) Waombaji na walaghai watajumuika katika kucheza kamari na kulewa.
(87) PombeError: Reference source not found itatumika kama ni kitu chenye kuponya yaani dawa.
(88) Makafiri watatukuzwa juu ya watu wengine na Muumin watadhalilishwa na kupuuzwa.
(89) Kutafanywa malipo kwa ajili ya kutoa Adhan na salaError: Reference source not found.
(90) MisikitiError: Reference source not found itajaa kwa watu wasiokuwa na khofu ya Allah swt.
(91) Watu wenye fahamu na akili kasoro ndio watakaokuwa wakiongoza salaError: Reference source not found za jamaa' na watu kama hao kamwe hawatashutumiwa au kusutwa na badili yake wataheshimiwa. "

(2) Ubashiri Maalum

Mtume Mtukufu s.a.w.w amesema: "Kabla ya kuja kwa QayamaError: Reference source not found, vitu vitatu vitakuwa vya kawaida
(1) ugonjwa wa bawasiri,
(2) vifoError: Reference source not found vya ghafla,
(3) Saratani ya damuError: Reference source not found.

Vile vile Mtukufu Mtume s.a.w.w amesema: "Mojawapo ya sharti kwa kuja Siku ya QayamaError: Reference source not found ni motoError: Reference source not found utakaotanda Mashariki hadi Magharibi. "

Ameendelea kusema, "Idadi ya wanawakeError: Reference source not found itazidi idadi ya wanaumeError: Reference source not found kwa uwiano wa wanawake hamsini kwa mwanamme mmoja. "

Kuangamizwa Kwa Nchi Na Miji Mbalimbali

Mwanachuoni mkuu wa Kisunni Mohiuddin, ameandika katika Muhadherat-ul-Abrar na Muthammerat-ul-Akhyar, riwaya kutoka Ilyas, mtiririko hadi kumalizikia kwa Hudhaifah, kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w alisema:
1. "MisriError: Reference source not found haitaangamizwa hadi hapo BasraError: Reference source not found imeteketezwa, Basra itateketezwa kwa sababu ya IraqError: Reference source not found na Misri itaangamizwa kwa sababu ya mto Nile.

2. MakkahError: Reference source not found itatekwa na Ethiopia.

3. MadinaError: Reference source not found itakumbwa na mafuriko.

4. YemenError: Reference source not found itateketezwa na ndui.

5. Eila itaangamizwa kabisa katika kutekwa.

6. Uajemi utatekwa na Saalik kutoka Dailam na Dailam atatimuliwa na Waarmenia na wao watatekwa na WaturukiError: Reference source not found.

7. Waturuki watakumbwa na kuangamizwa kwa radi.

8. Sind itatolewa na IndiaError: Reference source not found

9. na India itapinduliwa na Wachina.

10. Error: Reference source not foundChinaError: Reference source not found itaharibiwa na mchanga au nzigeError: Reference source not found.

11. Rafdha itaipoteza Ethiopia.

12. SufianiError: Reference source not found atawatilia vikwazo wale wanaokwenda kuzuru makaburi ya Mtume Mtukufu s.a.w.w na Maimamu a.s.

13. Ramla itateketezwa nusu na

14. Iraq itakumbwa na ukame.

Mitume Sitini Bandia

Abdullah ibn Umar anaripoti kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w alisema: "QayamaError: Reference source not found haitakuja hadi MahdiError: Reference source not found atakapodhihiri kutokana na kizazi changu; na yeye pia hatajitambulisha hadi hapo patakapotokea watu sitini watakaodai kuwa wao ni mitume (bandia). "

Vita Pamoja Na Weupe Na Maangamizo

Imeripotiwa katika kitabu cha Aqdud Dur cha Auf Ibn Malik kuwa mimi nilimwijia Mtume s.a.w.w ambapo alipokuwa ameketi katia hema lenye rangi ya udongo. Kwa utaratibu alitawadha na kuniambia, "QayamaError: Reference source not found inasubiri ubashiri sita:
(1)mvuaError: Reference source not found ya changarawe kutoka mbinguni (labda inaweza kumaanisha kuporomoka kwa mabomuError: Reference source not found na matokeo yake). Hili ndilo la kwanza. "

Mimi nilimjibu: "Naam, Bwana wangu!"

Aliendelea Mtume Mtukufu s.a.w.w:
(2) "Ushindi wa kuishinda JerusalemError: Reference source not found.
(3) Mauaji kupindukia kiasi. Watu watakuwa wakiuawa kama ng'ombe na mbuzi.
(4) Kuzidi kwa mali ambayo haitoshelezi kukamilisha matakwa ya mtu.
(5) Yatatokea magomvi na hakuna hata nyumba moja itakayobakia salama bila ya kukumbwa na magomvi hayo.
(6) Watu weupe watawageuka. Wao watakushambulieni katika mabatalioni themanini na kila batalioni litakuwa na askari kumi na mbili elfu.

Kuteketezwa kwa Baadhi ya Miji

Katika Manaqib ya Ibn Shahar Ashub imerekodiwa kutoka kwa Qatada ambaye ameripoti kutoka Saeed Ibn Musayyab: "Imam Ali a.s. aliulizwa juu ya Aya ya QuranError: Reference source not found Tukufu: Na hakuna taifa lolote ila alipita humo Muonyaji.’ Hapo Imam Ali a.s. alitoa tafsiri ndefu mno na humo alitoa ubashiri wa kuangamizwa kwa baadhi ya miji.
1. Samarqand, Jaj, Khwazim, Isfehan na KufaError: Reference source not found vitaharibiwa na WaturukiError: Reference source not found. (Hapa Waturuki wanamaanishwa WarusiError: Reference source not found) .

2. Hamadan na Ray yataangamizwa na watu wa Kazvin.

3. Tabrusa, MadinaError: Reference source not found na sehemu ya Ghuba ya Uajemi yatakumbwa na ukame na njaa.

4. MakkahError: Reference source not found itatekwa na Ethopia.

5. BasraError: Reference source not found na Balkh yatazama majini.

6. Sind itatwaliwa na India.

7. Error: Reference source not foundIndia na Tibet

8. Tibet na ChinaError: Reference source not found.

9. Majeshi yatatetemesha Badakshan, Saani Kirman na baadhi ya sehemu za SyriaError: Reference source not found.

10. YemenError: Reference source not found itaangamizwa na watawala

11. Sijistan na baadhi ya sehemu za Syria zitaangamizwa kwa gesi

12. Saman itaangamizwa na magonjwa na nzigeError: Reference source not found wataiharibu Marv

13. Nyoka watua viumbe katika Hirat

14. Naishapur itateketezwa.

15. Azarbaijan itavamiwa na majeshi na radi kali zitapiga (labda kwa sababu ya mabomuError: Reference source not found)

16. Mto Nile utafurika

17. Bokhara itazama majini

18. Kutakuwapo na ukame na miji ya Salam na BaghdadError: Reference source not found itaangamizwa.

Ubashiri wa Ziada wa Imam Ali A. S.

Abu Abdullah Jafar ibn Muhammad anaripoti kutoka kwa Imam Husain a.s. ambaye alimwuliza baba yake: "Tafadhali sana baba naomba utuambie ni lini Allah s.w.t. ataitakasa ardhi kutokana na watu waovu?"

Imam Ali a.s. alimjibu: "Ardhi haitaweza kamwe kutakasika hadi hapo damuError: Reference source not found ya wazushi itakapokuwa imekwisha mwagika kikamilifu. "
Imam Ali a.s. akizungumzia tawala za Banu Umaya na Bani Abbas, alisema: "Kabla ya kuja kwa Qaim kutatokezea mtu mmoja Sayyid Hasani atakayejiweka huko Khorasan. Yeye ataiteka Kirman na Multan. Na hapo baadaye ataendelea mbele kuelekea BasraError: Reference source not found. Qaim kutokana na sisi, atajitokezea katika Jilan. Watu wa Astrabad na Kazvin watamtii. Baadaye kutatokezea kupandishwa kwa benderaError: Reference source not found za Uturuki. Hapo kutakuja kutokezea vita vikali mno. Hapo ndipo Basra itakapokuja kuangamizwa na makao makuu ya Waarabu itakuja kuwa MisriError: Reference source not found.
Imam Ali a.s. aliendelea kusema hadithi moja iliyokuwa ndefu ya tukio, na alisema: “Mikuki itaimarishwa na kusimamishwa na watu walio dhaifu na wastani watawaua watu walio wema.”

Vifo Vyeupe na Vyekundu

Kuhusu kifo cheupe na chekundu, Imam Ali a.s. alisema: “Kabla ya kudhihiri kwa al-Qaim a.s. kutatokezea kwa aina mbili za vifoError: Reference source not found - nyekundu na nyeupe. Kwa nyekundu kunamaanisha damuError: Reference source not found yaani kumwagika kwa damu nyingi mno kwa sababu za vita na mauaji ya aina mbalimbali. Na kifo cheupe kinamaanisha kuzuka kwa maafaError: Reference source not found ya magonjwa ambayo yatakuwa daima yakienea na kuzuka kila mahala.”
Tanbihi: Kwa vifoError: Reference source not found vyekundu hapo juu tunaelewa kuwa kutakuwapo na vita vya kutisha mno ambapo damuError: Reference source not found itakuwa ikimwagika kutoka kila pembe ya dunia. Tunasikia kila siku katika maredio na televisheni vile dunia yetu hii ilivyokumbwa na mauaji kila pande. Na ama kuhusiana na kifo cheupe, tunasikia vile magonjwa mbalimbali ya saratani, ukimwi n. k. yanayoua watu kwa mamilioni.

Syria na Iraq

Imam Ali a.s. alisema: "Kutazuka vita katika SyriaError: Reference source not found na itashambuliwa kwa mabomuError: Reference source not found. Katika matokeo yake takriban watu laki moja watakuwa wameuawa. Allah swt atabariki Waumin na kuwaadhibu Makafiri. Ole wenu wakati huo!"
Farasi wakiwa na mabendera ya rangi ya njano watatokezea Magharibi. Wao watafika Syria na huko kuna kijiji kimoja kiitwacho Harsa au Kharsa ambacho kitadidimia ardhini. Muwe tahadhari kwa hayo! Ni ubashiri kuwa kutakuwapo na uasi wa SufianiError: Reference source not found ambaye atatokezea kutoka mabonde makavu ya PalestinaError: Reference source not found (vitabu vya zamani vya jiografia vinaelezea kuwa Kharsa au Harsa ipo karibu na Damascus huko Syria).

Kuzingirwa kwa Mji wa Kufa

Asbagh ibn Nabata anaripotiwa kusema: "Sisi tulisikia tafsiri ya Aya ifuatayo ya QuranError: Reference source not found Tukufu kutoka kwa Imam Ali a.s. Kisha tukakurudishieni nguvu zenu juu yao na tukakuongezeeni mali na watoto na tukakufanyeni wenye kundi kubwa kuliko wao' (Sura Bani Israil, 17:6) hapo Imam Ali a.s. alisema: Humo kuna baadhi ya mabashiri na dalili. Kwanza ni kule kuzingirwa na kutekwa kwa mji wa Kufa.

Kutachimbwa mahandaki kuuzunguka mji kwa sababu ya khofu ya maadui. Kutachomwa au kuchanwa mabendera katika mitaa ya mji wa KufaError: Reference source not found. Msikiti Mkuu wa Kufa utabakia tupu kwa siku arobaini kwa sababu hakutakuwapo na mtu wa kuja kusali humo. Wakristo watakuwa na nguvu katika maeneo hayo. Kutapeperushwa kwa mabendera tatu kwa pamoja. Kutamwagika damuError: Reference source not found kwa wingi mno ambamo muuaji na aliyeuawa wote wataingia motoni Jahannam. Mcha-Mungu pamoja na watu sabini watauawa katika kitongoji cha Msikiti wa Kufa. Huko MakkahError: Reference source not found, baina ya Rukn na Maqam atakuja kuuawa mcha -Mungu mwingine. 2

Imam Ali A.S. Aelezea Ubashiri Kumi

1. Katika mitaa ya mji wa KufaError: Reference source not found, kutapeperushwa benderaError: Reference source not found nyingi mbalimbali

2. MisikitiError: Reference source not found haitatumika vile ipasavyo

3. Zitafungwa kila njia zielekeazo kwenda HijjaError: Reference source not found (kwa kila mbinu)

4. Kuzama kwa ardhi huko Khorasan

5. Watu watakuwa wakibadili makazi na maishio yao (watahamahama ovyo ) kwa sababu ya vita na machafuko kila mahala

6. Nyota zenye mikia zitakuwa zikionekana

7. Baadhi ya nyotaError: Reference source not found zitakutanika mahala pamoja

8. Kutatokea na umwagaji wa damuError: Reference source not found kwa wingi na kila upande

9. Mauaji na maangamizi yatatokea kwa kupindukia kiasi

10. Tawala za kikatili na kutisha zitawaghalibu watu kila mahala. Kuna mshangao kwa kila ubashiri na baada ya kutokea kwao Al-Qaim wetu atadhihiri. "

Theluthi Mbili za Binadamu wa Dunia Wataangamizwa

Imerekodiwa katika Oqdatud-Durr kuwa Imam Ali a.s. amesema: “Al- MahdiError: Reference source not found a.s. hatadhihiri hadi hapo theluthi moja ya watu wa dunia hii hawatauawa na theluthi ya pili hawatakufa kwa mauti. Kwa hivyo kutakuwa kumebakia theluthi moja tu walio hai!"

Iran

Imam Husain a.s. ameripotiwa akisema kuwa kutatokezea vita vya makundi mbalimbali katika IranError: Reference source not found na maelfu ya watu watauawa.

Kupatwa kwa Mwezi na Jua

"Kinyume na desturi ya kupatwa kwa mwezi na jua katika mwezi mmoja, kutatokezea kupatwa kwa mwezi tarehe 5 ya mwezi na kutapatwa kwa jua mnamo tarehe 15 ya mwezi huo huo. Jambo kama hilo halijawahi kutokezea kamwe tangia Mtume Adam a. s " Hayo yameripotiwa yakisemwa na Imam Muhammad al-Baquir a.s.

Mitetemeko ya Ardhi

Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema: “al-Qaim a.s. hatadhihiri hadi:
1. Dunia nzima kukumbwa na woga na khofu.

2. Kutakuwa na mitetemeko mingi na watu watakuwa wamejawa kwa woga

3. Kutatokea na kuzagaa kwa magonjwa yenye kuuwa kwa wingi

4. Kutazuka vita vikali mno miongoni mwa Waarabu

5. Kutazuka tabia ya watu kuzozana mno

6. Dini itakuwa dhaifu

7. Hali za jamii zitakuwa mbaya mno kiasi kwamba watu watakuwa wakiomba mauti kila usiku na mchana.

Mahdi Wazushi

Imam Jaafer as-Sadiq a.s. amesema: "Kutatokea wazushi kumi na wawili watakaojiita MahdiError: Reference source not found, kabla ya kudhihiri al-Mahdi wa kweli. "

Siku ya Waarabu Katika Mji wa Kufa

Imam Jaafer Sadiq a.s. siku moja alipokuwa akimwambia kijana mmoja huko KufaError: Reference source not found: "Katika mji wenu wa Kufa, karibu na Msikiti, watu wapatao elfu nne wa kabila la Saabun watauawa na Lango la Tembo katika Siku ya Waarabu.

(3). Ubashiri Wa Lazima

Mabashiri haya yatatokea kwa lazima kabla ya kudhihiri kwa Al Qaim a.s. Katika kitabu hiki ninawakusanyieni baadhi tu, hivyo msomaji mwenye shauku zaidi anaweza kutafuta katika vitabu vingine vya Kiarabu, Kiajemi n. k.

Uasi wa Sufiani

Mtu mwovu mwenye sura isiyopendeza na yenye kuchukiza, mwenye macho - paka na makengeza kutoka kabila la Bani Umayya aitwaye Uthmaan bin Utba au Ushba ataongoza uasi karibu na PalestinaError: Reference source not found. Uasi wake utatokezea baada ya vita vikuu vya dunia. Jeshi lake litakuwa katili mno na wenye kiu cha damuError: Reference source not found. Kiasi cha Wayahudi elfu sabini watajiunga naye. Wanajeshi wake wote watakuwa wanaharamu. Udhihiri wa al-MahdiError: Reference source not found a.s. utakuwa katika miaka hiyo hiyo. SufianiError: Reference source not found atatawala takriban Bara la Arabia zima kwa vitisho na maangamizo. MadinaError: Reference source not found, SyriaError: Reference source not found na IraqError: Reference source not found vitateketezwa. Baada ya hapo yeye atajitayarisha kwa ajili yaMakkahError: Reference source not found. Mahala pamoja panapoitwa Beda, katika jangwa la Madina, ardhi itapasuka na Sufiani pamoja na jeshi lake zima litatumbukia humo na kuangamia.

Sauti Kutoka Mbinguni

Tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, usiku wa Alhamisi, kabla ya Alfajiri, kutasikika sauti moja kubwa mno. Itamfikia kila mtu popote pale alipo na ataielewa. Sauti hiyo nzuri kabisa itakuwa ni ya Bwana JibrailError: Reference source not found a.s. ikitangaza ubashiri mwema wa kudhihiri kwa Al-MahdiError: Reference source not found a.s. Hapo baadaye katika saa za mchana kutasikika sauti nyingine kama hiyo, nayo itakuwa ni sauti ya Ibilisi. Sauti ya kufanana itatosheleza kuwapotosha watu. 3

Kupatwa Kwingi Kwa Jua na Mwezi

Kwa mara ya kwanza yatatokea katika nchi za Mashariki, baadaye katika nchi za Magharibi na baadaye katika bara la Bara la Arabia

Katika baadhi ya riwaya kumeripotiwa kwa mitetemeko ya ardhi yatatokea katika taratibu hizo katika mwaka mmoja. Allah swt ndiye mwenye kujua zaidi!

Kuchomoza Jua Kutoka Magharibi

Baadhi ya wana-Hadith wanasema kuwa hiyo ndiyo dalili mojawapo ya Siku ya Qayama. Kwa kufanyia utafiti zaidi tumeweza kujua kuwa jua litabakia kati kati saa za asubuhi mbele ya macho ya wakazi wa dunia na itabakia hivyo hadi wakati wa mchana na itaanza kupanda kama kwamba inaanza kuchomoza kutokea Magharibi. Kwa hakika ubashiri huu ni mgumu kuusadiki. Katika mabadiliko hayo ya utaratibu wa jua kunaweza kuleta maafaError: Reference source not found na mabadiliko makubwa mno. Ingawaje mimi si bingwa katika mambo ya mahesabu, lakini ni kama wataalamu walivyosema. Lakini hii itatokea kama ni ubashiri wa mwisho.

Dajjal

Ni neno la Kiarabu likimaanisha mhaini mkubwa na mleta balaaError: Reference source not found kubwa mno. Hivyo wale wote walio wahaini na waleta balaa basi wajijue kuwa wao pia na ma-DajjalError: Reference source not found wa zama zetu hizi. Lakini Dajjal anayezungumziwa hapa ni yule ambaye anaitwa Sayyid na utambulisho wake ni Dajjal. Yeye atakuwa ni mchawi mkubwa. Hapo mwanzoni atakapojitokeza atadai kuwa yeye ni mtume na baadaye atajiita kuwa yeye ni mungu. Yeye atatokezea pale ambapo Mashariki ya Kati itakuwa imekwisha dhoofika kwa sababu ya ukame utakaodumu kwa miaka mitatu kwa mfululizo. Katika mwaka wa tatu kutakuwa hakuna dalili ya majani na hakutakuwapo na mvuaError: Reference source not found kabisa.
Hili jitu lenye jicho moja litakuwa na urefu wa mita ishirini. Jicho lake la kulia litakuwa halifanyi kazi na litakuwa kama donge la nyama nyekundu. Jicho lake la kushoto litawaka kutokea paji la uso. Yeye atakuwa akimwendesha punda mwekundu, mwenye manywele ambaye miguu yake itakuwa mieusi kutokea mifupa ya juu hadi magoti na nyeupe kutokea magoti hadi makwata. Kutasikika sauti ya muziki kutokea nywele zake na za punda wake.

Watu wanyonge, wanawakeError: Reference source not found, Mabedui wa Kiarabu na Kiyahudi watamtii na kumfuata. DajjalError: Reference source not found mwenyewe atakuwa Myahudi wa asili ya ukoo wa Qutama na kwa kutokana na udugu wa Abu Yusuf. Kwa hakika watu watamkubalia kama mtume (ingawaje atakuwa ni mzushi) .

Kwa kupatiwa msaada wa wanajeshi sabini elfu wa Kiyahudi na wenye silaha na matayarisho yote, yeye ataeneza kila mahala hali ya dhuluma na uoga. Mioyo ya watu itajawa kwa khofu na hatari. Wakati huo, JerusalemuError: Reference source not found ndio itakapokuwa mahala pa usalama kwa sababu Mtume Issa a.s. atateremkia. Imam MahdiError: Reference source not found a.s. atafika hapo pia. Hapo kutatokea vita vikali na Mtume Issa a.s. atamwua DajjalError: Reference source not found. WayahudiError: Reference source not found wataangamizwa. Ulaji wa nyama ya nguruwe utaachwa. Hakutakuwapo na alama za MsalabaError: Reference source not found. Na hapo kutakuwapo na Dini moja tu duniani -- ISLAM.

Mapokezi yafuatayo yametolewa kutoka Kitabu cha Kamal-ud-Din ambamo Muhammad Ibn Ibrahim anarikodi kama Hadith sahihi iliyopokelewa na Ibn Sabra,anayesema:

"Wakati mmoja Imam Amir-al-Mominiin Ali ibn Abi Talib a.s. alituambia hivi:

Sifa zote ni za Allah swt na Salaam ziwe juu yake Mtume Mtukufu s.a.w.w , na baadaye aliendelea kusema: "Niulizeni kile mukitakacho. . . "

Saasaan ibn Suhan aliinuka na kuuliza "Ewe Mawla wetu! Naomba utuambie ni lini atakapotokezea DajjalError: Reference source not found.

Imam Ali a. s alimwambia aketi na kumjibu. Saasan aliketi na Imam Ali a.s. alianza kuelezea:

"Allah swt amekusikiliza na anajua kile ukitakacho. Zitapita dalili moja baada ya nyingine. Je niwaambieni ?"

Watu waliokuwapo walisema: "Naam tunaomba hivyo, Ewe Abul Hasan ! "

Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake,
(1) watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa.
(2) Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi
(3) Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi
(4) Waislamu wataanza kuchukua ribaError: Reference source not found
(5) Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida
(6) Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa
(7) Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia
(8) Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao 4
(9) Wanaume watawataka wanawakeError: Reference source not found ushauri na uongozi
(10) Hakutapatikana huruma kokote pale, dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu
(11) Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida 5
(12) Mauaji na umwagaji wa damuError: Reference source not found utachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe
(13) Watu wenye elimu watakuwa wadhaifu na wadhalimu watakuwa wenye nguvu.
(14). Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu
(15) Wasufi na wasomaji wa QuranError: Reference source not found watakuwa wapumbavu
(16) Kutakuwa kukitolewa ushahidi wa kughushiwa
(17) Quran Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu
(18) MisikitiError: Reference source not found itakuwa ikijengewa minara mirefu
(19) Watu waovu watakuwa wakiheshimwa
(20) Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao
(21) Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale
(22) Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaumeError: Reference source not found wao kwa uroho wa mali
(23) Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana.
(24). Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu
(25). Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa
(26) Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji
(27). Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi.
(28). wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.
(29). Kuiga, hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke (ajifanye mwanamke)na mwanamke atapenda ajifanye kama mwanamme6.
(30). Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea
(31). Mbwamwitu watakuwa wengi , katika makundi ya kondoo.
(32) Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia .
(33) Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko kitu chochote kile
(34) Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem. Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem.
Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema "Ewe Bwana, naomba utwambie DajjalError: Reference source not found atakuwa ni mtu wa aina gani?"
Imam Ali a.s. alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed . Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia DajjalError: Reference source not found na atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal.
(35). Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia . Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyotaError: Reference source not found ya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damuError: Reference source not found. Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.
(36). Jua litakuwa pamoja naye.
(37). Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.
(38). Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,
(39) Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.
(40) Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye DajjalError: Reference source not found yatakauka hadi siku ya QayamaError: Reference source not found,(41). baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema"Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri, mimi ndiye niliyewaumba, na niliyewafanya nyie mkawa wazuri. Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana. "
(42). Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.
(43) Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaaError: Reference source not found,
(44) wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,
(45) huyo DajjalError: Reference source not found atauawa mahala panapoitwa Aqba huko SyriaError: Reference source not found, atauawa siku ya Ijumaa mchana,
(46) Mtume Issa a.s. atasali nyuma ya Imam MahdiError: Reference source not found a.s.
(47) na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.

Yajuj na Majuj

Allah swt anasema katika Quran,Sura 18 : 92 - 99.

Kisha akaifuata njia.
Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa).
Wakasema: “Ewe Dhulqarnain! Hakika Yajuj na Majuj wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?”
Akasema: “Yale ambayo Mola wangu amenimakinishia ni bora (kuliko ujira wenu. Nitakufanyieni bure);Lakini nIssaidieni kwa nguvu zenu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi chenye imara.”
Nileteeni vipande vya chuma. ”Hata alipoijaza nafasi iliyo katikati ya milima miwili,alisema: “Pulizeni” mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa moto, alisema “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake. ”
Hivyo (Yajuj na Majuj) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa.
Akasema: “Hili ni rehema itokayo kwa Mola wangu. Na itakapofika ahadi ya Mola wangu ya kufika QayamaError: Reference source not found),atauvunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu ni kweli tu. ”

Yajuj na Majuj walikuwa ni viumbe vyenye miguu minne na wakifanana na wanaadamu kisura na wao walikuwa ni wafupi mno mbele ya watu wa zama hizo. Na watoto wao walikuwa wakizaliwa kama watoto wa wanaadamu na walikuwa hawakui zaidi ya shubiri tano na sura zao zilikuwa aina moja na walikuwa wazururaji. Kwa kuwa ngozi zao zilikuwa ngumu kama zile za ngamia, hivyo hawakuathirika kwa baridi wala joto. Walikuwa na makucha makubwa na meno makali na masikio yao yalikuwa marefu kiasi kwamba walikuwa wakitandika moja na kujifunika kwa la pili. Walikuwa wakiingiliana kama wanyama na chakula chao kikubwa kilikuwa ni samaki kwa sababu kulikuwa kukinyesha mvua za samaki, na kama kulikuwa na kasoro ya samaki basi walikuwa wakishambulia miji na kuchafua na kuvuruga kila kitu kiasi kwamba watu walipokuwa wakizisikia sauti zao, walikuwa wakikimbia na kuacha makazi yao kwa sababu ilikuwa ni vigumu mno kuwakabili kwani walipokuwa wakiingia mijini basi miji yote ilikuwa ikijaa wao tu. Idadi yao ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba hakuna mtu mwingine ajuaye isipokuwa Allah swt. Wao walikuwa hawafi hadi wamezaa watoto zaidi ya elfu moja.

Katika vitabu tunapata habari zaidi kuwa Yajuj na Majuj ni makabila mawili yaliyokuwa makubwa kutokana na kizazi cha Yafus, mwana wa Mtume Nuh a.s. Na katika Agano la Kale, Majuj anaelezwa kuwa ni Chifu wa Mashech na Tunal. Kwa sasa Moscow ndio mto unaosimama mji huo, uitwao Moscow, mji mkuu wa Urusi; Tabul ni mto huko Urusi ambapo kuna mji Tobolsk.

Katika eneo la Ulaya ya Kusini na Urusi ya Kiasia, baina ya Wacarpathiani na Don, kulikaliwa katika enzi za zamani na kabila katili kabisa ambao waliiteka Asia ya Magharibi kuanzia karne ya 7 Kabla ya Kristo hadi mwanzoni mwa kipindi cha Kikristo, wakati mashambulizi yao yalipokwisha kwa sababu ya Bwana Dhulqarnain alipoujenga huo ukuta.

Vile vile inasemekana kuwa neno Mongol ni mvurugano wa neno la Kichina Mongog au Manchog Iwapo utafiti huu utakuwa wa kweli, hivyo. Hivyo itamaanisha kuwa eneo la Yajuj na Majuj inaanzia Mto wa Moscow hadi Turkistan ya Kichina na Mangolia.

Maelezo ya ‘kuta’ katika Quran Tukufu yanaonyesha kuwa lazima iwe imejengwa pale penye njia ili kuzuia makabila hayo ya wachochezi na wakatili kuwashambulia majirani wao waliokuwa mafundi stadi katika kazi za kufua vyuma na walikuwa matajiri.

Sheikh Abul-Kalam Azad, katika moja ya makala yake (katika Jannatul-Ma’arif) anaelezea kuwa kuta hizo zimeendelea hadi Uturuki.

Ayatullah Agha Haji Mirza MahdiError: Reference source not found Puya Yazdi (katika hashia ya Tafsiri ya Quran iliyofanywa na S. V. Mir Ahmad Ali) anawanakili wengine wakisema kuwa kuta hizo zipo baina ya milima ya Armenia na Azerbaijan.

Hata hivyo kuna tofauti ya maoni kuhusu utambulisho wa Dhulqarnain. Abdullah Yusuf Ali anadhani kuwa jina hilo linaelezea kuwa ni Alexandar Mkuu wa Misri.

Wengineo, kama Agha Puya, wanafikiri kuwa huyo anatambulishwa kama ni Mfalme wa Kiajemi aliyekuwa akiitwa Darius.

Kwetu sisi hatumaanishi kuingia katika mazungumzo mengi kuhusu mjadala huu lakini inatubidi liwe jambo lililowazi mbele yetu kuwa kwa mujibu wa Quran Tukufu, Dhulqarnain alikuwa ni mcha Mungu hivyo kamwe haiwezekani kumtambulisha Dhulqarnain kama kafiri au mpagani.

Kwa mujibu wa Quran Tukufu, itakapokaribia Siku ya QayamaError: Reference source not found, kabila hizi zitafanikiwa kuvunja kuta, yaani zitaenea zaidi kuliko mipaka yao ya awali. Upanuzi huo unaweza kuwa kimantiki; ambapo inaweza kumaanisha kuwa itikadi zao (ukomunisti na ukafiri) zinaweza kuenezwa nje ya mipaka ya nchi zao. Au itakuwa aina ya kikoloni yaani kukalia maeneo ya mashariki ya Ulaya, Asia ya Kusini na maeneo mengineyo. Au inaweza kumaanisha yote.

Imeandikwa katika Tafsir Majma-ul-Bayan kuwa baada ya kuteka maeneo ya ardhi watajararibu kuiteka mbingu. “Hivyo watatupa mishale yao kuelekea angani, na itawarejea zikiwa na alama kama za damu. Hivyo watasema: ‘Sisi tumekwishawateka wakazi wa dunia na tumewateka wakazi wa angani. ”

Ni dhahiri kuwa mishale inamaanisha maroketi na vyombo vya angani. Maneno itawarejea zikiwa na alama kama za damu inamaanisha kuwa vyombo vya angani vitafikia malengo yao na kurejea duniani.

Kwa mujibu wa Tafsiri hiyo, “wakati watakapokuwa na takabari kubwa kwa sababu ya ‘kushinda anga za juu’, Allah swt atawaumba funza au minyoo ambayo itawaingia masikio yao, na kuwaua wote. Inamaanisha kuwa hatima yao itakuwa kwa kuangamizwa kwa maafa makhsusi, au kwa magonjwa ya kuambukizwa yatakayotokana na vijidudu.

Dabbatul Ardh

Saasaan anaelezea zaidi: "Sisi tulimwuliza Imam Ali a.s. Je ni nini kitakachotokea baadaye?"
Ali a.s. alijibu: “Karibu na mlima Saffa na Marwa, Dabbatul Ardh atakuja. Yeye atakuwa na pete ya Mtume Suleiman na atakuwa na mkongojo wa Mtume Musa a.s. na yeye atakuwa akiiweka hiyo pete juu ya vipaji vya makafiri na loh ! kutatokezea dalili za kuonyesha kuwa huyu mtu ni kafiri, na ukafiri wake utaonekana usoni mwa mtu huyo aliyegusishwa pete ya Mtume Suleiman a.s. Dabbatul ardh pia atakuwa akiwaangalia waumini na ataweza kuwatambulisha kuwa wao ni waumini, yeye kwa amri ya Allah swt atakuwa akiangalia juu ya mbingu na ataweza kuona Mashariki na Magharibi papo hapo. Na tukio hili litatokezea baada ya jua kuchomoza kutoka Magharibi hapo ndipo milango ya tawba itakuwa imefungwa, muda wa kufanya tawba utakuwa umekwisha. Matendo na amali havitasaidia chochote. Ninawaombeni msiniulize baadaye kitakachotokea kwa sababu nimempa ahadi Mtume s.a.w.w kuwa sitaitoboa hii siri isipokuwa kwa yule atakayekuwa mrithi wangu. "
Mpashaji habari wa tukio hili Taran ibn Sabra alimwuliza Saasan ibn Suhan "Je nini maana hili jambo aliloliezea Imam Ali a.s."
Saasan alijibu: "Ewe ibn Sabra, Mtume Issa a.s. atasali nyuma ya Imam wa 12 (kumi na mbili ) katika kizazi cha Imam Ali a.s. na ni mtu wa kizazi cha tisa (9) katika kizazi cha Husein ibn Ali a.s. Huyo atakuwa ni jua litakalo chomoza kutoka Magharibi, yeye ataitakasisha ardhi baina ya Rukn na Msikiti na ataeneza uadilifu duniani kote. Baada ya hapo hakutakuwapo na dhuluma ya aina yoyote. "

Kudhihiri Kwa Mtume Issa A.S. Kutoka Mbinguni

Ni imani ya Waisilamu wote kuwa Mtume Issa a.s. alikuwa hakusulubiwa wala hakuuliwa bali alichukuliwa na Allah swt katika mbingu za juu na yupo hai. Kwa wakati maalum uliowekwa na Allah swt, Mtume Issa a.s. atadhihiri duniani kutoka mbinguni hadi SyriaError: Reference source not found. Wakati huo Imam MahdiError: Reference source not found a.s. atakuwa humu humu duniani na Mtume Issa ataungana naye. Pamoja na Imam Mahdi a.s. wakati wa salaError: Reference source not found Imam Mahdi a.s. atakuwa akiongoza sala na Mtume Issa a.s. atakuwa akisali sala nyuma yake. Wao wote kwa pamoja watatangaza vita dhidi ya DajjalError: Reference source not found ambaye atauawa. Baada ya hapo WayahudiError: Reference source not found wote na Wakristo wote watakuwa Waislamu .
QuranError: Reference source not found Tukufu inatupa habari kwa urefu na mapana kuhusu Mtume Issa a.s. vile vile tunapata habari nyingi sana katika Hadithi tukufu. Vile vile kulitokezea na mtu ambaye alidai kuwa Mtume Issa a.s. amekufa na yeye alikuwa ni masiha mtu huyo anajulikana kwa jina la Mirza Gulam Ahmad KadianiError: Reference source not foundError: Reference source not found, mimi sitapenda kuingilia maswala haya na kuyachambua kwani mambo haya yametobolewa khususani katika nchi ya Pakistani na serikali ya Pakistani imefichua siri za hawa watu na imetangaza kuwa wafuasi wa Kadiani si Waislamu na haya ndiyo yalikuwa maamuzi ya Mahakama yaliyosikiliza kesi zao. Iliyochukua nafasi muhimu katika mahakama ya Pakistani .

Kuzagaa kwa Moto na Moshi Duniani

Allah swt anasema katika Quran, Sura Ad -Dukhan 44:10-16
Basi ingoje siku ambapo mbingu zitakapoleta moshi uliodhahiri.
Utakaowafunika watu; Hii ni adhabu iumizayo.
(Wao watasema) ‘Mola wetu! Tuondolee adhabu hii hakika (sasa) mumin. ’
Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wajia Mtume abainishaye.
Wakampa kisogo na wakasema: ‘Amefunzwa ni mwendawazimu.
Kwa yakini Sisi tutaiondoa adhabu kidogo, nyinyi mtarudia (makosa yenu).
(Na itakuja) siku ambapo tutawateka (wote) kwa mteko mkubwa; Kwa hakika sisi ni wenye kulipiza.

Kwa mujibu wa riwaya nyingi mno, Aya hizi zinabashiria moshi utakaokuwapo karibu na QayamaError: Reference source not found. Moshi huo utaingia katika masikio (na macho), na vichwa vya watu vitaonekana kama yamechomwa. Lakini haitawadhuru waumini; wao watahisi mwasho wa kawaida wa kama baridi. Na dunia nzima itakuwa mfano wa nyumba iliyoshika moto na ambayo haina madirisha wala sehemu za kutokezea moshi. Na sura hii itadumu kwa muda wa siku arobaini.

Dalili hii itakuwa ni ishara ya kuonywa; na kama inavyoonekana katika Aya wanaadamu watapewa muda wa kurejea katika imani na njia iliyo ya haki na wajirekebishe. Maneno ‘Kwa hakika Sisi tutaiondoa adhabu kidogo’ inatudhihirishia kuwa moshi utaondolewa, lakini maneno yanayofuata nyinyi mutarudia (makosa yenu) inatuonyesha kuwa kuondolewa kwa adhabu hiyo tu, basi si watu wengi watakaotafakari juu ya suala hilo. Labda wengi watatafuta visingizio vya kijiografia au zinginezo kwa ajili ya kutokezea kwa adhabu hiyo, na watasahau ahadi zao walizompa Allah swt kuwa Mola wetu !. . . hakika (sasa) muumin.

Kwa hakika si vigumu kukubaliana na mambo yaliyoeelezwa hapo juu:
1. Umande na moshi unakuwapo hata leo hivyo Allah swt anao uwezo wa kuumba moshi utakaotanda duniani kote.
2. Allah swt anaweza kuwaepusha mumin kutokana na athari mbaya kabisa za moshi huo. Kwani hata leo tunaona kuwa si watu wote wanaoathirika na maafa yanapozuka katika maeneo fulani.
3. Na kuna idadi kubwa kabisa isiyohIssabika ya makafiri wanaotubu pale wanapopatwa na adhabu au matatizo,na husahau kwa urahisi ahadi zao kwaAllah swt (za kuwa mumin) za kuomba, mara baada ya kuondokea na matatizo yao.

Ubashiri huu umeelezwa katika vitabu vingi vya Hadith, kutakuwa na moshi mwingi sana katika anga zetu kwa sababu hiyo kutakuwapo kwa motoError: Reference source not found kila mahali.

Inawezekana ubashiri huu unadalilisha utumiaji wa aina nyingi za magesi ambayo yanalipuka yenye hatari na motoError: Reference source not found ndio utakuwa sababu ya gesi hizi, majaribio ya nyukilia vile vile yanatoa gesi nyingi na miale ya radio active vile vile katika ubashiri mwingine imeelezwa kutakuwapo na moto unaotokea ndani mwa ardhi ya AdenError: Reference source not found, nimeelezea maswala haya katika kurasa zilizopita.

Kuangamizwa kwa Baghdad

Kuna mabashiri mengi katika kuelezea kuteketezwa kwa baadhi ya miji khususan kuteketezwa kwa mji wa BaghdadError: Reference source not found ndiyo imeelezwa kwa zaidi na wanazuoni wengi wanasema kuwa ubashiri huo ni wa kweli.
Imam Jaafer Sadiq a.s. alitoa hotuba ndefu sana kuhusiana na swala hilo. Imam Ali a.s. pia ameelezea kwa undani zaidi katika hotuba zake na hapa ninawachambulia machache kutoka hotuba hiyo: “Enyi watu kutabuniwa mji mpya utakaoitwa BaghdadError: Reference source not found (Labda alimaanisha Baghdad mpya) Mji huo utakithiri kwa madhambi na maasi kiasi kwamba adhabu za Allah swt zitakuwa zikilengwa sana huko. Balaa za kila aina zisizojulikana, magonjwa yakuangamiza, ukame, mafuriko ya mto Tigris na mvuaError: Reference source not found zisizo na mpangilio vile vile tufani za kila aina zitakuwa zikitokea kuuangamiza mji huo. Na kuangamizwa kwa mji huu kutatokea baada ya aina tatu za benderaError: Reference source not found kuchomoza katika mji huo. Bendera ya kwanza itakuwa rangi Njano, ya pili aina ya bendera itakuwa kutoka pande za magharibi, na ya tatu itatokezea sehemu za kuizunguka, na labda hii ndiyo dalili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Uasi Kuongozwa na Hasan Sayyid

Kijana huyu atakuwa mzuri na atakuwa ametokana na kizazi cha Imam Hasan a.s. na katika baadhi ya Hadith anapewa jina la Hasan, atatokezea kutoka kijiji cha Dailam (karibu na Kazvin) yeye hatajitangazia uongozi wowote wa kidini bali atakuwa akiwaita watu baada ya kuona hali ya jamii na jumuia imeharibika na kuvurugika, atawaita watu waache maovu na wajirekebishe. Watu wa Taliqan watakuwa ndio watu wa kwanza kuutikia wito wake. Watu watamzunguka na watajiunga kwa wingi katika harakati zake, ujumbe wake utaenea katika sehemu zinazozunguka za karibuni na kufikia hadi Multan kupitia Kirman na vile vile atafika BasraError: Reference source not found. Sehemu zote hizi zitakubaliana na mazungumzo na mambo yake. Baaada ya hapo ataelekea KufaError: Reference source not found na huko atapata habari kuwa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. amedhihiri na Imam a.s. ameondoka kuelekea IraqError: Reference source not found kupitia MakkahError: Reference source not found na MadinaError: Reference source not found.
Wakazi wa KufaError: Reference source not found watakuwa wakiishi maisha yasiyo wafurahisha wao wenyewe. Huyu Hasan Sayyed ataonana na Imam MahdiError: Reference source not found a.s. kutaka kujua miujiza na uthibitisho wa uhalali wake wa kuwa Imam Mahdi a.s. baada ya kuthibitishiwa atakula kiapo kwa Imam Mahdi a.s. pamoja na jeshi lake la utiifu.
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: “Kwa jina la Allah swt, Hasan Sayyed atakuwa akimtambua vyema kabisa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. lakini ili kuwahakikishia watu na kuwathibitishia na kuwatolea shaka watu kuwa huyu ndiye Imam Mahdi a.s. atamuomba Imam amthibitishie kwa miujiza uhalali wake. Wanajeshi elfu nne wa Zaid kutoka YemenError: Reference source not found watakaokuwa katika jeshi la Hasan Sayyed wataaasi. Hapo Imam Mahdi a.s. atamshauri Hasan Sayyed awatulize hao vijana wa kabila la Zaid wajisalimishe. Mazungumzo hayo yataendelea kwa muda wa siku tatu, lakini wanajeshi wa Zaid hawatakubali, hatimaye wote watauawa.

(4). Ubashiri Wa Siku Za Mbeleni

Kwa hakika mabashiri yafuatayo yanahitaji kuzingatiwa mno, hapa chini ninawaleteeni machache na nitawapa maelezo kidogo juu yake:

(1). Uasi wa Shuayb ibn Saleh
Yeye atakuwa ni mtu mwema na ataanzisha uasi wake katika mji wa Samarqand. Mambo mengi ya muhimu yatatokea wakati wake. Hadithi nyingi zinaelezea kuwa ama yeye atakuwa ni kamanda katika jeshi la Hasan Sayyed au Imam MahdiError: Reference source not found a.s.

(2). Uasi wa Aus
Huyu atakuwa ni mtu mwema atakayewaita watu katika mawazo yake baada ya vita vikuu, huyu mtu atakuwa amesimamia mapinduzi kutoka Kuwait hadi Syria ambapo ndipo atakapouawa.

(3). Uasi wa Yamani
Kutatokezea kwa mtu asiyejulikana kutokea huko YemenError: Reference source not found ambapo ataleta maangamizi na ataleta fitina na ugomvi wa hali ya juu sana.

(4). Maghrebi kuilinda MisriError: Reference source not found
Katika lugha ya Kiarabu Algeria,Tunisia,Morocco na Libya, zinaitwa Maghreb kutatokezea mtu katika nchi hizi yaani Maghreb ambaye atakuja MisriError: Reference source not found na atahukumu nchi hizo zote ikiwemo SyriaError: Reference source not found.

(5). Kuuawa kwa Mohammad Hasan Zakiyya
Imam Ja'afer as- Sadiq a.s. amesema: "Siku kumi na tano tokea kudhihiri kwa MahdiError: Reference source not found a.s. mtu mtakatifu sana kwa jina la Muhammad ibn Hasan Zakiyya ambaye atakuwa ni mmoja wa wafuasi wakubwa wa Imam Mahdi a.s. atauawa karibu na Al-Ka'aba baina ya Rukn na Maqam.

(6). Kutokezea kwa Ikhtilafu

Kutatokezea ikhtilafu kubwa sana miongoni mwa Bani Abbas.

(7). Mtu Maarufu sana
Mtu maarufu sana mcha Mungu ajulikanaye kwa jina la nafsi Zakiyyah atauawa pamoja na Sayyid sabini nyuma ya Msikiti wa KufaError: Reference source not found. Ukatili na mauaji haya ya kikatili yatatendwa na jeshi la SufianiError: Reference source not found.

(8). Mji wa MakkahError: Reference source not found
Mtu mmoja kutoka Bani Hashim, mcha Mungu kabisa atauawa katika mji wa MakkahError: Reference source not found.

(9). Mahakama ya KufaError: Reference source not found
Chumba cha Mahakama ya KufaError: Reference source not found kitaharibiwa pamoja na ukuta wa Msikiti wa Kufa.

(10). Theluji ya kushangaza
Kutakuwepo na kuanguka kwa theluji ya kushangaza katika Roma kila kipande cha theluji kitakuwa kama yai.

(11). Nyota ya kustaajabisha sana
Kutachomoza kwa nyotaError: Reference source not found kutoka Mashariki, mwanga wake utakuwa sawa na wa mwezi. Mkia wake utakuwa ukipotea pole pole na hatimaye kupotea. Nyota hizi za kuanguka zimekuwa zikitokea daima lakini hakuna hata moja ambayo imeweza kuwa na nuru kama mwezi.

(12). MotoError: Reference source not found katika anga za juu
Katika anga za juu baina ya anga na ardhi kutatokezea motoError: Reference source not found utakaowaka siku tatu mfululizo au siku saba kwa hakika litakuwa jambo kubwa la kustaajabisha.

(13). Rangi nzito mbinguni.

Rangi nzito nyekundu iliyoiva itazagaa mbinguni.

(14). MotoError: Reference source not found Mashariki ya Kati.
Kutakuwa na mioto ikiwaka kila mahala khususan Mashariki ya Kati. MotoError: Reference source not found utakuwa wa kutisha sana kiasi kwamba watu wataanza kutubu madhambi yao.

(15). Waarabu watakuwa ni watu wasiokuwa na msimamo:
Hakuna hata mmoja atakayeweza kumsaidia mwenzake kwa moyo kwani kila mmoja atakuwa akitenda vile atakavyo kwa masilahi yake mwenyewe.

(16). Mfalme wa IranError: Reference source not found ataanguka:
Yaani ufalme wa IranError: Reference source not found utakwisha na utawala wake utatokomea na utawala mpya utatokezea yaani katika mwaka 1978|79 ubashiri huu umetokezea kuwa kweli wakati Shah Muhammad Riza Pahlawi alipopinduliwa na umma wa Waislam chini ya uongozi shupavu wa marehemu Ayatullah Ruhullah Al-Musawi al- Khomeini (a. r.) utawala wa Shah ulidumu zaidi ya karne mbili na nusu.

(17). Amir wa MisriError: Reference source not found atauawa:
Atakuwa ni mtu mmoja mwenye mamlaka ya utawala na atakuwa ni mtu mashuhuri katika Misri. Error: Reference source not foundKatika Kiarabu hapa neno lililotumiwa ni Amir yaani hakukutumiwa jina la Sultani au Malkia hivyo inatudhihirishia aina ya utawala utakaokuwepo wakati huo.

(18). Kuteketezwa kwa SyriaError: Reference source not found :
Kutakuwa na benderaError: Reference source not found zilizoinuliwa kutokea MisriError: Reference source not found zikielekea SyriaError: Reference source not found na kutatokezea bendera moja kutokezea Khorasan na bendera zote hizi tatu zitadai kumiliki Syria na wote hawa watapigania katika ardhi ya Syria. Vita ambavyo vitaangamiza na kuteketeza Syria.

(19). Majeshi kupitia mipaka ya Magharibi wataingia SyriaError: Reference source not found :
Yaani inawezekana majeshi ya Wazungu na nchi za Magharibi zitaingia SyriaError: Reference source not found kupitia Uturuki ili kuikalia Syria.

(20). Bendera rangi nyeusi
Bendera rangi nyeusi zitachomoza kutoka Khorasan (Labda linamaanisha jeshi la Hasan Sayyid).

(21). Kutajengwa njia za kupita chini ya ardhi kutokea mto wa Furati.
Kipitio hicho kitapitia KufaError: Reference source not found na itauletea utajiri mji huo. Wakazi wake watakuwa idadi kubwa na utashamiri (Ubashiri huu umeshatokea na kukamilika pia).

(22). Watu sitini
Kutatokezea watu sitini, watu wenyewe watakuwa waovu na majangiri ambao watadai kuwa wao ni mitume kwa hakika kutokana na wanavyovutia na wanavyojionyesha wataweza kuwavuta watu wengi upande wao (kiasi cha watu hamsini na nane wameishatokezea kudai utume hadi leo).

(23). Sayyid waongo kumi na wawili :
Kutokana na kizazi cha Abu Talib watu kumi na wawili watadai kuwa wao ni Imam, kizazi cha Imam au warithi wa Imam au wao ni MahdiError: Reference source not found (baadhi ya watu wameshatokezea na wameshapita na wengine bado watatokezea nao pia watapita ).

(24). Mtu atachomwa motoError: Reference source not found
Mtu mwenye heshima sana kutoka Bani Abbas atachomwa motoError: Reference source not found hai baina ya Jehula na Khanqin (tunaweza kusema kuwa huyo mtu ni Abdus Salaam Arif ambaye aliungua moto katika ajali ya ndege )

(25). Kujengwa daraja mpya
Kujengwa daraja mpya katika mto wa Tigris katika upande wa Karkh, kutajengwa daraja huko BaghdadError: Reference source not found (daraja kama hili lilijengwa miaka michache iliyopita labda kunaweza kujengwa daraja lingine jipya).

(26). Kuteketezwa kwa BaghdadError: Reference source not found:
Watu wengi wa mji wa BaghdadError: Reference source not found watauawa kutokana na mitetemeko mingi ya ardhi na kutatokezea maafaError: Reference source not found na tufani nyeusi wakati wa mchana ambapo kutaleta matishio mbalimbali kwa wakazi wa Baghdad.

(27). BasraError: Reference source not found itazama.
BasraError: Reference source not found itazama katika maji kufuatia tufani kubwa ya mawimbi ya maji makubwa (Wasomaji wanashauriwa kusoma Nahjul Balaqgha kwa utabiri huu ).

(28). Magonjwa sugu yataenea duniani
Kutakuja kuangamizwa na magonjwa sugu yataenea duniani kote na itaua watu kwa idadi kubwa sana.

(29). Makundi makubwa mno ya nzigeError: Reference source not found
Kutakuwa na makundi makubwa mno ya nzigeError: Reference source not found duniani kote, vita vya wenyewe kwa wenyewe huko IraqError: Reference source not found, kutakuwa na umwagaji wa damuError: Reference source not found kupindukia duniani kote na kutokezea vita vikali sana huko IranError: Reference source not found baina ya makundi mawili kiasi cha watu elfu themanini watauawa (Au imekamilika mwaka 1978 |79) .

(30). Nyuso za wanadamu zitabadilika
Hali ya nyuso za wanadamu zitabadilika na zitageuka kuwa za nyani na nguruwe.

(31). Kutatokezea mkono karibu na jua
Kutatokezea mkono karibu na jua ambapo wakazi wa duniani wataona pamoja na kustaajabika (jambo hili litatokezea muda mchache kabla ya kudhihiri kwa MahdiError: Reference source not found a.s. ).

(32). Kunyesha mvuaError: Reference source not found yenye fujo
Duniani kote kutaanza kunyesha mvuaError: Reference source not found yenye fujo sana kuanzia tarehe 16 Jamadi us-Thani hadi tarehe 10 Rajab.

Kila Mwislamu mwenye kuwa na imani kamili juu ya Allah swt anaamini kuwa mvua hainyeshi kwa sababu ya misimu tu bali ni kwa sababu za amri na idhini za Allah swt.

Allah swt anatuambia katika Quran Tukufu kuhusu mvua:
Sura 25, Furqan Aya 48
Naye ndiye azitumaye pepo kuwa bashara njema kabla ya rehema
yake ya mvua; na tunayateremsha kutoka mawinguni maji safi.

Sura 35,Fatir Aya 9:
Allah ndiye aliyetuma hewa inayopeleka mawingu.

Sura 6,An-Am Aya 6:
Sisi tumeifanya mbingu kuwa yenye kunyesha mvua iendeleayo.

Sura 15 Al-Hijr Aya 22:
Sisi tumefanya mawingu na kunyesha mvua kutoka mbinguni.

Sura 29 Ankabut,Aya 63:
Na ukiwauliza,’Ni nani ateremshaye maji na kuhuisha ardhi baada ya kufa kwake?’ Bila shaka watasema ‘Allah’ .

Sura 50 Qaf Aya 9:
Na tumeyateremsha kutoka mawinguni maji yaliyobarikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka zivunwazo.

Sura 8 Anfal, Aya 11:
Na anakuteremshieni mani kutoka mawinguni ili kukutakasisheni.

Sura 40 Muminun, Aya 18:
Na tumeteremsha kutoka mawinguni maji kwa kiasi.

Katika Aya hizo Tukufu za Quran kuwa upepo ndio unaosafirisha mawingu kuelekea mashariki, magharibi au kaskazini na kusini. Yaani inachukua kwa amri za Allah swt. Vile vile tumeona waziwazi kuwa kunyesha kwa mvua na kiasi chake kinahusishwa na Allah swt.

Baada ya kusoma hizo Aya tukufu tumeona kuwa mvua imekuwa daima ni rehema na idhini ya Allah swt ndipo inaponyesha juu ya ardhi.

Imeonekana kuwa katika baadhi ya nyakati neema na baraka hii inakuwa imezuiliwa. Na katika sura hii kuna riwaya nyingi kutoka kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w na Maimamu a.s. zinazotuambia tusali sala za Istisqaa.

Tunapata mapokezi kutoka vitabuni kuwa katika zama za Imam Ali a.s. na Maimamu a.s. wamekuwa wakIssali sala za Istisqaa kwa ajili ya kuomba mvua,na mvua zilikuwa zikinyesha.

Mvua hii isiyo na mpangilio itanyesha kabla ya kudhihiri kwa Imam Mahdi Error: Reference source not found a.s. na haijulikani kama itanyesha Mashariki ya Kati tu au mahala penginepo.

(33). Watu waliokufa watakuwa hai
Watu waliokufa watakuwa hai (matukio haya yatatokea muda mchache kabla ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. Baadhi ya vitabu vinataja majina ya watu wataofufuka kupata maisha mara ya pili).

(34). MisikitiError: Reference source not found itarembeshwa
MisikitiError: Reference source not found itarembeshwa kwa mabati ya dhahabu vile vile QuranError: Reference source not found tukufu itarembeshwa kwa nyuzi za dhahabu.

(35). Sehemu tatu duniani zitadidimia
Sehemu tatu duniani zitadidimia ardhini au zitamezwa na ardhi pamoja na wakazi wake,y a kwanza itakuwa katika upande wa Magharibi baadaye katika Mashariki na hatimaye katika Bara la Arabia

(36). Dini ya Islam itakuwa dhaifu.
Islamu itabakia kwa jina tu. Maamrisho ya dini yatapotea. Watu wataingiliana sana kiasi kwamba itakuwa vigumu sana kumwelewa Mwislamu na yule asiye Mwislamu yaani Waislamu watakuwa wamepoteza hata ile sura yao ya Kiislamu.

(37). Kufr itakithiri katika Islam:
Nchi za Kiislamu zitaiga mitindo na maisha ya nchi zile zisizo za Kiislam. Waislamu wataomba misaada kutoka wale wasio Waislamu. Nchi za Kiislamu watauana miongoni mwao, watagombana kwa kutaka urafiki wa nchi zile ambazo zinamkanushaAllah swt (nchi za Kiislamu zitagombana miongoni mwao kwa kushawishiwa na nchi zile zisizo za Kiislamu )7

(38). Utawala wa Bani Hashim:
Imam Ali a.s. amebashiri kuwa utawala wa Bani Hashim utakwisha duniani. Mtawala wa mwisho atakuwa kijana mmoja mdhaifu, asiye na ujuzi wala utaalamu wowote na vile vile atakuwa akifuata ushauri wa watu wengi (katika dunia hii leo kuna utawala wa Bani Hashim nchi moja tu duniani kote nayo ni Jordan ).

(39). Miaka thelathini ya mwisho
Miaka thelathini ya mwisho katika karne atakayodhihiri Imam MahdiError: Reference source not found a.s. kutakuwa na vitu vya ajabu ajabu na vya kustaajabisha mno.

Tanbihi Kuanzia mwaka 1370 A. H. inahitaji uchambuzi hadi siku ya leo, dunia imeona maajabu ya mageuzi ya mapinduzi na mauaji ya kushtusha na mambo mengi ya ajabu ajabu yasiyoweza kusadikiwa na watu kuwa binadamu anaweza kufanya mambo haya maovu kwa binadamu mwenzake.

(41). Kufika kwa WaturukiError: Reference source not found
Kufika kwa WaturukiError: Reference source not found katika pembe la Bara la Arabia katika Hadith maneno ya Turki na Jazira yametumika. Wataalam wa uchambuzi wa maswala haya wanasema: “Neno Turuki linamaanisha WarusiError: Reference source not found na Jazira ni Bara la Arabia, hivyo ni ubashiri mmoja muhimu sana wa kuzingatia kuwa Warusi wataingia Bara la Arabia yaani inawezekana wakaingia kwa mabavu (kwa nguvu) au wanaweza kuingia kwa upole kwa kutumia njia nyinginezo (tunaona Warusi wameingia katika Bara la Arabia ).

(42). WazunguError: Reference source not found kuingia katika PalestinaError: Reference source not found:
Watu wa Roma ni wazungu na Ramla ni PalestinaError: Reference source not found hivyo kutakuwa na mvutano wa hali ya juu katika Bara la Arabia kwa sababu ya kugombania nguvu baina ya Waamerika, WazunguError: Reference source not found na WarusiError: Reference source not found.

(43). Mtu mwenye kuheshimiwa
Mtu mwenye kuheshimiwa mno kutoka Bani Abbas atatoswa majini katika mto Tigiris karibu na daraja jipya huko BaghdadError: Reference source not found.

(44). Kijiji cha Jabiya
Kijiji cha Jabiya karibu na Damascus itadidimia ardhini.

(45). Ziwa Sawa
Ziwa Sawa litajaa kwa maji kwa mara nyingine tena. Ziwa hili liko karibu na mji mtukufu wa Qum lilikauka pale Mtume s. a. w. w alipozaliwa. Wale wote wanaokwenda ziara ya Masuma -i-Qum wanashuhudia ubashiri huu.

(46). Wanawake na watoto
Watoto na wanawake watakuwa watawala.

(47). Taratibu za tawala za nchi
Taratibu za tawala za nchi zitakuwa zikipata sura mpya mpya za kutawala vile vile utawala wa kifalme utatokomea.

(48). Kizingiti baina ya ardhi na mbingu
Kutaonekana kitu kama kizingiti baina ya ardhi na mbingu, kweli litakuwa ni jambo la kustaajabisha kabisa hasa Mashariki ya Kati.

(49). Jumuiya ya wale wasio waumini
Jumuiya ya wale wasio waumini wataenea Bara la Arabia na nchi nyingine za Kiarabu (ama wao ni WarusiError: Reference source not found au WachinaError: Reference source not found kwani Warusi wameishajidhatiti katika nchi nyingi za Kiarabu).

(50). Kuwasili kwa WachinaError: Reference source not found
Kuwasili kwa WachinaError: Reference source not found katika Bara la Arabia ni ubashiri mkubwa wa vita vikubwa hali mbaya kabisa isiyoelezeka itatokea baada ya wao kuwasili huko.

(51). Michafuko ya kila aina
Kutakuwa na michafuko ya aina mbalimbali kuanzia Azarbaijan na Armenia. Machafuko haya yataenea hadi mlima mwekundu. Matokeo haya na hatima yake yatakuwa mabaya kiasi kwamba watoto watakuwa kama wamezeeka na wazee watatamani mauti. Machafuko haya yatafika mpaka mji wa KufaError: Reference source not found kupitia Wast na vita hatari kabisa vitatokea karibu na mji wa Najaf. Kwa hakika maovu na matisho haya hayaelezeki. Vile vile vita vitatokezea karibu na Teheran.

(52). Kuzuia kizazi
Kutakuwa na mipango mbalimbali ya kuzuia kizazi na mbinu hizo zitashurutishwa kwa njia mbalimbali.

  • 1. Habari hizi tazama Day of Judgement ,Sayyid Saeed Akhtar Rizvi,Bilal Muslim Mission of Tanzani,DSM,chapa ya pili,1978,uk. 44. ,naye amenakili kutoka Bihar-ul- Anwar,j. III.
  • 2. Kwa msomaji atakayependa kufanya utafiti zaidi juu ya swala hili juu ya Ubashiri,anaweza kusoma Hotuba ya Imam Ali a.s. Al-Makhzun katika kitabu kiitwacho Basharatul-Islam,chapa ya Baghdad.
  • 3. Leo duniani tunaona kuwa maendeleo ya sayansi yametudhihirishia kuwa kuna uwezekano wa kufikisha Sauti na sura duniani kote hasa kwa kupitia satellites. Sasa jee kuna ugumu gani kwake Allah swt kufanya kudra zake?
  • 4. Mambo kama haya ndivyo yanavyotokea katika kupiga kura za kidemokrasia!
  • 5. Kwa utumwa hapa kunamaanisha mbinu za kumfanya mtu asiweze kusema dhidi ya mambo ya mfadhili wake kama vile tunavyoona na kusikia kuhusu masharti ya misaada itolewayo na nchi na watu wafadhili.
  • 6. Nimesikia katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC mnamo tarehe 17 Novemba 1995 saa 6. 30 jioni kuwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar University cha huko Misri kimetoa fatwa kuwa mwanamme anaweza kujigeuza k,uwa mwanamke na vile vile mwanamke anaweza kugeuzwa kuwa mwanamme kwa njia za operesheni ati kwa sababu ni maumbile yake ndivyo yalivyo.
    Vile vile nimesikia katika idhaa ya Kiingereza ya BBC hivi majuzi (wiki moja kabla ya Fatwa kutoka Al-Azhar) kuwa kumefanywa uchunguzi na utafiti huko Amerika na kutolewa ripoti kuwa mtu khanisi na anayelawiti na kulawitiwa aachwe awe hivyo na wala asilaumiwe na jamii kwa sababu ndivyo yalivyo maumbile yake.
  • 7. Tunajionea vile nchi za Kiarabu zinavyopingana na kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya ushawishi wa nchi za Magharibi. Utengano miongoni mwao unatokana na kulaghaiwa na nchi za Magharibi ambavyo ni vyema kwa maslahi yao.