Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho International Jew. Sisi tumekiita, Myahudi wa Kimataifa.

Kitabu hiki, Myahudi wa Kimataifa ni matokea ya tume iliyoundwa na Henry Ford wa Kwanza na kuchapishwa kwa mara ya kwanza baina ya miaka 1919-1920. Henry Ford I alikuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa viwanda; yeye alikuwa na kiwanda chake maarufu sana kati­ka miaka ya 1900 kilichojulikana kwa jina la Ford Motor Company.

Mtasinia huyu alitishiwa na jinsi wahamiaji wa Kiyahudi walivyokuwa wakiendesha biashara na mambo yao kwa kuhodhi nchini Marekani na sehemu nyinginezo ulimwengu. Kwa hiyo, uzalendo ukamsukuma na akaamua kuunda tume ya wataalamu waliobobea katika shughuli za utafi­ti ili wafanye utafiti kuhusu shughuli za Wayahudi nchini Marekani na katika nchi za Magharibi, na matokeo ya utafiti wao ni kitabu hiki ulicho nacho mikononi mwako.

Sote tunajua uharibifu na ukaidi wa Wayahudi kuanzia wakati wa Nabii Musa (a.s.) mpaka sasa. Katika kitabu hiki utaona jinsi walivyopanga mbinu na mikakati ya kutawala kwa hila, mikakati ambayo waliipanga kabla na baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, na ambayo wanaen­delea kuitekeleza mpaka sasa. Watafiti hawa waligundua mambo mengi ya uovu uliokuwa ukifanywa na Wayahudi.

Kwa kweli kitabu hiki ni kifumbua macho kwa wale wote ambao wanawaona Wayahudi kama taifa teule la Mungu. Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kuwazindua wasomaji wetu wa Kiswahili kutokana na njama za Wazayuni.

Tunamshukuru ndugu yetu, Salman Shou kwa kukubali kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es-Salaam, Tanzania.