67 - Na miongoni mwa semi zake (A.S)

Na miongoni mwa semi zake (a.s) - Ameieleza An-Nuweiry mwanzo wake katika kitabu Nihayatul-Irbi, Jz. 8, uk. 168.

Wamesema: Na zilipomfika Amirul-Mu’minin habari za Saqiifah,1 baada ya kutawafu Mtume (s.a.w.w.) alisema Ali (a.s):

“Wamesema nini Ansar?” Wakasema: Wamesema: Sisi tuwe na amiri na ninyi muwe na amiri; akasema (a.s.): “Je hamkuhoji dhidi yao kuwa Mtume ameusia atendewe mema aliye mwema miongoni mwao na asame- hewe muovu wao!?”

Wakasema: Katika hili hakuna hoja yoyote dhidi yao? Akasema (a.s): “Lau uimamu ungekuwa katika wao, wasingeusiwa.” Kisha akasema (a.s): “Basi nini walisema maquraishi?” Wakasema: Wametoa hoja kuwa wao ni mti wa Mtume (s.a.w.w.). Akasema (a.s): “Wameutolea hoja mti na wamelipoteza tunda.”2

  • 1. Saqifa Bani Sa’idah masahaba walijikusanya humo baada ya kutawafu Nabii (s.a.w.w.), ili kumchagua khalifa wake.
  • 2. Tunda anawakusudia Ahlil-Bayt Rasuul (s.a.w.w.)