68 - Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Na Miongoni Mwa Maneno Yake (a.s) - * Tabariy ameieleza khutba hii ndani ya matukio ya mwaka wa 36, na Al’Baladhuuriy ndani ya Ansabul-Ashrafi, uk. 404, chapa ya Al’aalamiy. Alipomteua Muhammad bin Abi Bakr kuwa Gavana wa Misri, alizidiwa na kuuliwa: 1

“Nilitaka kumtawaza Hashim bin Utba huko Misri; 2 lau ningemtawaza yeye Misri pasingebakia eneo, na wasingepata fursa, bila ya kumlaumu Muhammad bin Abi Bakr, kwa kweli alikuwa mpenzi kwangu na kwangu alikuwa (rabiiba).” * Rabiiba - mtoto wa kamsbo.

  • 1. Muhammad bin Abi Bakr: Mama yake ni Asma bint Umays bin An-Nu’man, alikuwa chini ya Ja’far bin Abi Talib, na katika hij’ra ya kwanza alihama na Ja’far mpaka Uhabeshi. Huko alimzalia Abdullah bin Ja’far Al-Jawadi, baada ya hivyo (Ja’far) aliuawa katika siku ya Mu’uta. Alichukuliwa na Abu Bakr, akamzalia Muhammad, kisha (Abubakar) alikufa na kumwacha Asma akiwa hai, baadae alichukuliwa na Ali bin Abi Talibi ndipo Muhammad alipokuwa mtoto wake wakulea, na alikuwa akimchukulia kama mwanawe. Alinyonya upendo na ufuasi toka zama za utoto, kwa hiyo alikulia kwake, ilikuwa hajulikani baba yake ila Ali (a.s) kiasi kwamba Ali alisema: Muhammad ni mwanangu kutoka mgongo wa Abu Bakar.
  • 2. Hashim bin Utba bin Abi Waqqaas, ami yake ni Sa’ad bin Abi Waqqaas, na baba yake ni Utba bin Abii Waqqaas, ndiye ambaye alivunja jino la Mtume (s.a.w.w.) siku ya Uhud, na Hashim ndiyo Al-Mirqalu: Ameitwa Al-Mirqalu kwa kuwa alikuwa anaharakia katika vita, naye ni miongoni mwa Mashi’a wa Ali.