96 - Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

“Shukrani ni za Mungu ni wa mwanzo hapakuwa na kitu kabla yake, na ni wa mwisho hapatokuwa na kitu baada yake, na ni wa dhahiri hapana kitu juu yake, na ni wa batwini hapana kitu chini yake.”
Na miongoni mwake katika kumsifu Mtume (s.a.w.w.): Mahali pa makazi yake ni mahali bora, na asili yake ni asili iliyo bora mno kuliko asili zote, ni asili ya heshima na susu iliyo salama.1 Nyoyo za watu wema zimeelekezwa kwake, na hatamu za macho zimegeuzwa kumuelekea yeye. Mungu (swt) amezizika chuki kupitia yeye,2 na kwa yeye amezima mashambulizi ya kulipiza kisasi,3 kwa yeye ameunganisha udugu, na kuwatenganisha walioungana4 na kwa yeye amewatukuza waliokuwa dhalili,5 maneno yake ni ubainifu na kunyamaza kwake ni hekima.”

  • 1. Yaani anatokana na nasaba iliyo tohara mbali na aibu, kwani yeye amezaliwa mahali palipo salama mno mbali na aibu ya uzinzi.
  • 2. Kuizika chuki: Yaani kuizuia kwa kuwa yeye ni Mtume wa utangamano na wana dini yake ni watu wa mtangamano wenye kusaidiana katika mambo ya kheri, na ambaye hayuko ndani ya tanzi la mtangamano miongoni mwao basi Yeye - Mungu swt. ndiye ajuaye - yuko nje mbali nao.
  • 3. Uadui wa kushambuliana: Yaani uadui wa mtu kumshambulia ndugu yake, ili amdhu- ru, ikiwa hatomuuwa.
  • 4. Amewatangamanisha kwa uislamu wakawa ndugu na amewafarikisha kwa Uislamu waliokuwa karibu, ni kwa sababu Uislamu umewatangamanisha waliokuwa mbali kwa nasaba, mfano wa Ali na Ammar, na kuwafarikisha waliokurubiana kwa nasaba, mfano wa Hamza na Abu Lahab, na kuwafarikisha waliokurubiana kwa mtangamano wa kishirikina. Amesema (swt): “fa asbah’tum biniimatihi ikh’wanan” (kwa neema yake mkawa ndugu 3:103).
  • 5. Udhalili wa wanyonge miongoni mwa watu bora waliositirika na stara ya kutotajika, na wamedhalilishwa na enzi ya ushirikina na dhulma na uadui.