Maelezo Ya Nyongeza (Post Script)

Mheshimiwa Mwandishi (wa kitabu hiki) aliandika nyongeza ya maelezo katika mwaka wa 1987 wakati Afrika ya Kusini ilikuwa bado ni Taifa la kibaguzi (ubaguzi wa rangi) na shirikisho la Urusi (Sovieti Union) ilikuwa bado ni taifa lenye nguvu sana.

Licha ya mabadiliko haya muhimu katika uwanja wa kisiasa ulimwenguni, maelezo ya mwandishi kuhusu utumwa wa kitaifa (taifa moja kutumikishwa na lingine) bado ni halali wakati huu wa mwanzo wa karne mpya.

Ukoloni mambo leo bado upo katika mifumo mbalimbali tofauti na sasa Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO) linatumiwa kama mhuri wa kibali cha kuendelezwa zaidi shabaha na malengo ya mataifa yenye nguvu sana yaliyobaki katika ulimwengu huu.

Nchi ya Marekani (USA) na washirika wake wa Ulaya walitumia “Kadi ya demokrasia,” demokrasi ya kuteuliwa katika Ulimwengu wa Tatu inavumilika tu kama itahakikisha faida na maslahi ya nchi za Magaribi, kama ilivyoonekana katika suala la Algeria na Uturuki.

Baraza la Usalama, Baraza pekee lishughulikalo na maamuzi ya Baraza la Umoja wa Mataifa (UNO), linaendesha shughuli zake katika misimamo isiyokuwa ya kidemokrasia. Inatumika kwa kuchaguliwa tu au kuteuliwa katika kuhalalisha maslahi ya matajiri na wenye nguvu juu ya mataifa yaliyo dhaifu ya ulimwengu.

Nchi ambayo iko ndani ya ‘vitabu vibaya’ vya nchi za Magharibi kamwe nchi hiyo haiwezi kupatiwa uamuzi ulio sawa na haki wakati nchi ya Iraq ilipoivamia Iran, hakukuwepo na dhoruba kali la jangwani, lakini wakati nchi hiyo hiyo, yaani Iraq ilipoivamia Kuwait na kuitishia Saudia (Saudi Arabia) na washirika wengine katika eneo hilo. “majeshi ya ushirika huo” yaliungana kwa kibali cha ridhaa ya Umoja wa Mataifa (UNO).

Jinai hiyo katika hali zote lilikuwa sawasawa na kutendwa na mhalifu yule yule, lakini bado hali iliyooneshwa kwa mhalifu ilikuwa tofauti kwa sababu tu muathirika wa pili (yaani Kuwait) alikuwa mshirika wa upande wa nchi za Magharibi wakati ambapo huyo muathirika a kwanza (Iran) hakuwemo ndani ya vitabu vizuri vya nchi ya Marekani (USA).

The New World Order (mpango wa Marikani) kwa hakika ni zama ya unafiki: Mataifa yenye nguvu za kijeshi bado yanaendelea kulundika na kutengeneza zaidi silaha za kisasa zenye maangamizi makubwa na wakati huo huo wanaendelea kuhubiri kwa mataifa dhaifu kuhusu kujizuia wasitengeneze silaha kama hizo!

Wakiwa mbele kwa masuala ya mazingira; wachafuzi wakubwa kabisa wa mazingira ni mataifa yenye viwanda vingi: lakini bado ni nchi ya Marekani (USA) ambayo ndiyo inakataa kutia sahihi mkataba wa kuzuia momonyoko wa ukanda wa hewa safi katika angahewa.

Kanuni ya uadilifu ya haki kwa wote siyo kawaida katika mpango huu wa Marikani (New World Order). Maslahi binafsi ya matajiri na nchi zenye nguvu, katika istilahi yake zaidi ya kistaarabu ya “maslahi ya kitaifa” bado ndio ufunguo unaofanya kazi katika mchezo huu. Pengo lililopo kati ya nchi za Kaskazini na Kusini linakuwa kwa haraka sana. Serikali za nchi masikini haziko huru kutekeleza sera zao wenyewe; ni Benki ya Ulimwengu, chombo kingine cha Ukoloni mambo leo, ambayo ndiyo inayowaundia sera za kiuchumi watu wan chi hizo. Sera hizi haziboreshi wengi wa watu katika nchi za Afrika na Asia.
Kwa masikitiko sana, hata katika suala la utambuzi wa misiba ya watu inaonyesha kunakuwepo na ubaguzi; msiba wa kundi moja la watu ambao waliteseka katika mikono ya Wanazi unafahamika kwa mapana sana (na Pia wakazawadiwa kuwa na “Nchi ya kuishi” ambayo baadaye inageuka kuwa “taifa”) wakati ambapo utambuzi wa msiba wa mamilioni ya Waafrika ambao walichukuliwa na kupelekwa katika nchi za Amerika na kunyang’anywa jina lao, utambulisho, dini, lugha na haki za msingi za kibinadamu bado ni jambo lilioko katika kujadiliwa.

Na tukiwa pamoja na mwandishi, tunamwomba Muumba Mwenye Nguvu Zote aharakishe kudhihiri kwa Mahdi, aliye Masihi, ambaye atauondolea ulimwengu na uonevu na kuieneza haki na amani katika ulimwengu.

Amin.

Back cover

“Enyi watu! Hakika Adamu hakuzaa mtumwa mwanaume au mtumwa mwanamke, wanadamu wote wako huru.” Imamu Ali (as)

Maoni ya watu kuhusu utumwa ni kwamba umetupwa kwenye mapipa ya takataka ya historia, wakati bado athari za ushenzi huu wa kuchukiza ambao mwanzo wake ulikuwa dhidi ya Waafrika, unajitokeza wenyewe kwa sura mpya na mbaya zaidi kwenye karne ya 21. Tangu kupigwa marufuku kwake rasmi katika mwaka wa 1863, utumwa umechukuwa sura ya uovu na ya kuchukiza zaidi, katika muundo wa utumwa uliopakazwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za kuzalisha unaofanywa na “Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba” (Multi National Cartels) ni muundo mpya wa utumwa.

Allamah Rizvi anaelezea suala hili la biashara ya utumwa kwa muktadha wake halisi. Allamah Sayyid Saeed Akhtar amekiandika kitabu hiki kwa uwezo mkubwa na jitihada. Kama ilivyo kwa msomi mtafiti kama yeye, ameshuhgulikia mada ya kitabu hiki bila upendeleo, Ameupanga ukweli baada ya ukweli kutoka kwenye historia; amenukuu kutoka kwenye Qur’an, Hadithi na waandishi wa zama za leo kuhusu somo hili, na ameonyesha sheria za Kiislamu na zile zilizotumika kabla ya Uislam. Ameonyesha waziwazi kwamba ustaarabu wa Kimagharibi sio bingwa mkubwa kiasi hicho wa kuwaokoa watumwa kama unavyojionyesha na kujigamba. Kwa kweli kitabu hiki kitathibitisha kuwa kifungua macho kwa wale ambao hukubali bila kuchunguza kuhusu propaganda ya ubinadamu wa Kimagharibi.

Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640/ 2127555
Barua Pepe: alitrah@raha.com
Tovuti: www.ibn-tv.com