Mkakati Wa 6: Kujiamini

Katika kitabu chake, Self Building, al-Amini anashauri sehemu iliyojitenga, kuondoa vizuizi vyote, uimarishaji wa imani, kukumbuka kifo, na kuwa tayari, kama njia kuu nne za kujenga na kudumisha mazingatio ya mtu katika Swala. Yeye pia anamaliza kwa kusema kwamba:
Kama mtu hakufanikiwa katika jaribio la awali haswa, badala ya kukata tamaa, anapaswa kujizatiti zaidi na makini katika kujaribu tena, mpaka upatikane utawala juu ya nafsi polepole. Akili lazima isafike kabisa kutoka na mawazo yaliyotawanyika na ihamasishwe kufanya mazingatio kwa Mwenyezi Mungu.

Kama kupata mazingatio ya namna hiyo kutakuwa hakuwezekani ndani ya siku moja, majuma machache au hata miezi michache, asiwe mwenye kukata tamaa kwa sababu, hata hivyo, namna kama hiyo ya mazingatio ya kujizatiti yanawezekana.

Kuwa na nia na imani madhubuti kwamba kwa hali yoyote ile, hutapotoshwa kamwe katika Swala, unahitaji kujiamini na kukubali kwa moyo wote kwamba nguvu za shetani ni dhaifu zaidi kuliko yale uliyojaaliwa nayo na Mola wako mpendwa, Aliye Mkuu. Allah (s.w.t.) anasema katika Qur’an tukufu kwamba

إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا {76}

“Hakika! Hila za shetani ni dhaifu mno. (Sura 4: 76)

Zaidi ya hayo, ni wewe utakayekuwa kwenye msukosuko katika Siku ya Kiyama wakati Shetani atakaposema:

إِلَّا أَنْ دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنْفُسَكُمْ ۖ{22}

“...bali niliwaiteni (kwenye maovu) nanyi mkaniitika. Hivyo (Siku hii ya Hukumu) msinilaumu mimi bali zilaumuniNafsi zenu wenyewe ...” (Sura 14: 22)

Kujiamini binafsi labda ni moja ya tabia muhimu sana unayoweza kuwa nayo. Kujiamini kunaakisi tathmini yako ya hali yako halisi. Kutachukua nafasi kubwa katika kukitambua kiwango chako cha mazingatio na umakini katika Swala.

Kujenga kujiamini na kuyashinda mawazo yanayopotosha katika swala kunachukua muda na juhudi. Kuweka malengo yamkini ndio njia yenye nguvu zaidi ya kujijengea kujiamini. Kwa kuweka malengo yenye vipimo, kuyafikia, na kuweka malengo mapya, kuyafikia na kadhalika, unajithibitishia uwezo wako wewe mwenyewe.

Unaweza kujithibitishia mwenyewe kwamba unao uwezo wa kutenda na kufanikisha vizuri sana. Unaweza kuona, kutambua na kufurahia mafanikio yako, na kujihisi mwenye thamani hasa katika mafanikio hayo. Tafadhali rejea kwenye Kitabu cha Mazoezi ya Siku 30 kwa maelezo zaidi.