Hitimisho

Maelezo ya Imam al-Khumeini (r.a.) juu ya ukamilifu wa Swala yanafaa kabisa kuwa hitimisho la hiki kitabu kifupi juu Swala. Tunawatarajia wasomaji kukisoma na kukichunguza kitabu hiki ili kupata manufaa yake, na tunatumaini kwamba mazoezi na kitabu cha mazoezi ya siku 30 vimekuwa na msaada.

“Pale unapoitamka takbir – ALLAH-U-AKBAR, uvione viumbe vyote kuwa ni vidogo kulinganisha na ukubwa wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Uchunguze moyo wako wakati wa Swala. Kama uliuhisi utamu wa Swala hiyo, na kama moyo wako ulisikia raha kutokana nayo, na moyo wako ulifurahia du’a kwa Allah (s.w.t.) na kuzungumza Naye, weka kwamba Allah (s.w.t.) amezikubali Takbir zako. Vinginevyo, bila ya kuhisi furaha juu ya du’a zako, na kunyimwa uonjaji wa utamu wa ibada, unapaswa ujue kwamba Allah (s.w.t.) amekukataa na kukuondoa kwenye Mlango Wake.”(Mustadrak al-Wasa’il; Kitabu cha Swala, Mlango wa Matendo ya Swala, Sura ya 2, Hadithi ya 9)

Ewe Mola Wangu, tujaalie kujishughulisha zaidi juu Yako na uyatilie mwanga mawazo ya mioyo yetu kwa mwanga wa nuru Yako, mpaka kuona kwa mioyo yetu kuweze kupenya mapazia ya nuru na kufikia kiini cha ukubwa na mpaka nafsi zetu ziwe zimeshikilia kwenye lango la hifadhi Yako. (Munajat-u-Sha’baniyyah – Mafatih al-Jinaan)

Kujifunza namna ya Fokasi na Kumakinika katika Swala Yako ya kila siku