Kundi La Kwanza: Elimu Na Ufahamu

1. Je! nimeelewa na kuridhika juu ya kuwepo kwa Allah (s.w.t.)?

2. Je! mimi ninatambua kwamba nimesimama mbele ya Allah (s.w.t.)?

3. Ninakielewa kile ninachokisoma?

4. Je! ninatoa matamshi sahihi kwa kiarabu?

5. Je! Mimi ninafahamu na kutekeleza zile Kanuni za usomaji wa Qur’an tukufu?

6. Hivi nimezielewa sababu kuu za msingi zilizoko nyuma ya Swala Tano za kila Siku?

7. Je! Ninayo hamasa na nguvu ya kuendeleza usikivu wangu?

8. Hivi ninao uhakika wa kutosha kwamba Allah (s.w.t.) yuko pamoja nami na kwamba ananisaidia katika Swala yangu?

9. Je! Nimejizuia mwenyewe kutokana na mazungumzo yasiyo na maana?

10. Je! Ninakikumbuka kifo mara kwa mara?

11. Je! Ninafunga mara kwa mara ili kuongeza uwazi wangu wa kiakili?

12. Nimejiaminisha mimi mwenyewe kwamba Swala ninayoswali inaweza kuwa ya mwisho?

Kama umejibu “NDIYO” kwa maswali 6 kati ya hayo 12 hapo juu, unaweza kuendelea na ratiba. Hata hivyo, hata jibu moja la kinyume lina maana kwamba lazima urudi nyuma na kutumia muda mwingi zaidi na fikira katika kipengele hicho mahususi. Vinginevyo, zoezi hili halitakuwa lenye manufaa sana.