Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
Mtoto wake Husseini

Jambo jengine ni hili

La majonzi ikhiwani

Hiki si kisa cha pili

Ambacho ni cha huzuni

Ni cha kijana rijali

Mtoto wake Husseini

   

Kadhulumiwa Husseini

Na wake mwana mchanga

   

Naye kafa madhulumu

Kijana wa mikononi

Muovu huyo Khasimu

Adui aso imani

Bure kaimwaga damu

Ya kijana maskini

   

Kadhulumiwa Husseini

Na wake mwana mchanga

   

Kifo chake ni dhuluma

Kijana huyu yakini

Adui aso huruma

Aso Imani moyoni

Kwa mshale kamfuma

Ukamwingia mwilini

   

Kadhulumiwa Husseini

Na wake mwana mchanga

   

Mshale ulimdunga

Mtoto wake Husseini

Ikawa hapana kinga

Ya kuiyepuka zani

Akafa mwana mchanga

Kiumbe cha Rahamani

   

Kadhulumiwa Husseini

Na wake mwana mchanga

   

Ovu liso wezekana

Kupata chake kifani

Kiumbe chake rabana

Kilo safi cha peponi

Walimu-uwa kijana

Bila kosa asilani

   

Kadhulumiwa Husseini

Na wake mwana mchanga

   

Huyo ni wake uwele

Alo mughuri shetani

Alomdunga mshale

Kipenzi chake amini

Naye piya vile vile

Ataingia motoni

   

Kadhulumiwa Husseini

Na wake mwana mchanga

   

Kwa kumuuwa kijana

Malaika kwa yakini

Hata akatubu sana

Haipati samahani

Adhabu yake ragana

Kwake haiwezekani

   

Kadhulumiwa Husseini

Na wake mwana mchanga

 

IMAM HUSAIN (A.S.) ASEMA:

"Kufa kwa heshima ni bora kuliko kuishi kwa aibu".