Sura Ya Kumi Na Sita

Kama tulivoeleza kwa ufupi kwenye kurasa za nyuma, Uthman, alikua anagawa fedha ya Waislamu miongoni mwa ndugu zake tu huku anawanyima haki watu masikini. Abu Dharr, kwa ajili ya ushupavu wake wa kidini katika kufuatilia mafundisho matukufu ya Mtume, alilazimika kupiga kelele kukemea maovu hayo. Matokeo yake alipelekwa Syria. Halafu aliitwa kutoka Syria na kurudi Madina kwa namna ya kuadhibiwa. Akawekwa katika taabu nyingi. Kwa kuwa Abu Dharr alikuwa mtu mwenye msimamo na alikuwa makini katika kutimiza ahadi yake ya kuwa mkweli ambayo alimwahidi Mtukufu Mtume, aliendelea na kazi yake bila kujali mamlaka yoyote au shutuma kutoka popote pale. kamwe hakujali ama alikuwa anazungumza kwa mfalme au kwa mtu wa kawaida. Hakujali kama pale alipokuwa anasema ni mtaani, sokoni, msikitini au baraza. Mzigo na aina ya kilio chake cha ukweli ulikuwa ni ule ule.

Sasa tunataka kuandika kwa kina jinsi Uthman alivyofungua mlango wa Hazina ya Taifa kwa ajili ya washirika wake na jinsi ndugu wa wafuasi wake walivyotajirika kupindukia. Hapa tunaorodhesha majina ya watu waliohusika ile iwe rahisi wewe msomaji kuamua jinsi wale waliofuata nyayo za Mtume (s.a.w) yaani Ali, Abu Dharr, Salman, Miqdadi, Ammar, na masahaba wengineo wa Mtume, walivyokuwa wakijinyima na hawa waolifanya upinzani dhidi ya utendaji wa aina hiyo.

Tunanukuu mifano michache ya ubadhirifu na upendeleo wa Uthman. Lakini, kabla ya hapo tunataka kuelezea jinsi fikra ya kuionesha upendeleo kwa uzao wa Umayyah ilivyoanza akilini mwake na jinsi alivyovuka mipaka ya mwenendo mwema. Bin Asakir, mwandishi wa historia na mtoa maoni wa labda karne ya pili ya A.H ameandika:

“Kwa mujibu wa simulizi za Anas bin Malik, siku moja Abu Sufyani bin Harb, ambaye alikwishapofuka, alikwenda kwa Uthman na akauliza kama palikuwepo na mtu mwingine pale. Masahaba wake wakasema, ‘hapana.” halafu akasema, “Ewe Uthman! Ifanye serikali hii ya Kiislamu iwe ya kabla ya Uislamu; iache inchi iwe kama ile iliyonyakuliwa kutoka kwa mtu na uitunze iwe ya kudumu kwa ajili ya uzao wa Umayyah.” (Tarikh bin Kathir, Juz. 6, uk. 407).

Waheshimiwa wasomaji! Ni Abu Sufyani yule yule aliyemfanyia Mtukufu Mtume karaha zisizo na mfano kabla ya Uislamu, halafu akaingia kwenye Uislamu bila kupenda. Hakuheshimu Uislamu katika yakini ya moyo wake.

Uthman alikubali ushauri wake akawaunga mkono kwa ukamilifu Bani Umayyah, akawafanya kuwa matajiri na kufanya serikali kuwa nchi iliyonyakuliwa kutoka kwa mtu, akaanza kuwatendea matendo mabaya na kuwadharau wenyewe wa mwanzo. Ni dhahiri kwamba haki ya kumiliki utawala ulitakiwa uende kwa Ali na uzao wake. Kwa hiyo, Uthman kuwatendea uonevu kama alivyoshauriwa na Abu Sufyani haiendani na utaratibu uliowekwa.

Inathibitika kutoka kwenye maelezo ya kihistoria kwamba usiku huo alipofariki Umm Kulthum, Uthman alifanya tendo la ndoa na mwanamke mwingine bila kumjali yule anayeugua kwa sababu ya kwamba alikuwa na uhusiano wa kindugu na Mtume. (Tajul Urus Juz. 6, uk. 220, Tabaqat bin Sad Juz. 8, uk. 31; Musnad Almad Juz. 3, uk. 126; Mustadirak Juz. 4, uk. 47; Sunan al-Kubra Bayhaqi, Juz. 4, uk. 53, Nihaya bin Athir, Juz. 3, uk. 286; ilichapishwa Misri, Lisanul Arab, Juz. 11, uk. 8809, Isabah, Juz. 4, uk. 489).

Maelezo kuhusu sababu ya watu kuwa wapinzani wa Uthman waandishi wa historia wameandika kwamba Uthman alimpa Marwani bin Hakam, Fadak (Kiunga kilichoporwa kutoka kwa Fatimah wakati wa utawala wa Abu Bakr –Khalifa wa Kwanza).

Fadak ni rasilimali iliyobakia kwenye miliki ya Marwani na wazao wake hadi hapo Umar bin Abdul Aziz aliichukua kutoka kwake na akawarudishia Ahlul Bait ambao ndio walikua na haki ya kumiliki. (Maarif cha bin Qutayba, uk. 84, Tarikh Abul Fida, Juz. 1, uk. 168; Sunan al-Kubra Bayhaqi, Juz. 6, uk. 301, Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 261).

Uthman hakumpa tu Marwan bin Hakam alikuwa binamu yake na mume wa bint yake, Umme Aban, umilikaji wa Fadak lakini alimpa pia sehemu ya tano (1/5) ya ngawira iliyopokelewa kutoka Afrika yaani dinari laki tano ambazo Abdul Rahman bin Hanbal al-Jamai al-Kindi wakati anazungumza na Khalifa alikariri aya za kejeli. Kwenye mojawapo ya Aya hizi anasema;

Ewe Khalifa! Ulimleta Marwan aliyelaaniwa karibu sana na wewe kinyume na walivyofanya wale waliokutangulia na ukamfanya kuwa mkwe wako, na halafu ukampa moja ya tano ya ngawira ya Afrika ukawadhulumu masikini.” (Maaeij uk. 84; Abul Fida, Juz. 1, uk. 160) Waandishi wa historia bin Kathir na Waqidi wanasimulia kwamba jumla ya thamani ya ngawira ya Afrika aliyopewa Marwan ilikuwa sarafu za dhahabu elfu ishirini. (Tarikh bin Kathir, Juz. 7, uk. 152) Tabari anasema kwamba ilikuwa dinari laki tano, sarafu aza dhahabu elfu ishirini (Tarikh Tabari, Juz. 5, uk. 50 Zaidi ya haya pia alipewa moja ya tano ya ngawira kutoka Misri. (Ansab al-Ashraf Balazari, Juz. 5, uk. 25; Tabari bin Sad, Juz. ya 3, uk. 44, ilichapishwa London)

Bin Abil Hadid ameandika, halafu alipomuoza mwanae kwa Marwan pia alimpa dinari laki moja kutoka kwenye Hazina ya Taifa. Kwa kitendo hiki, Zayd bin Arqam alimtupia Uthman funguo za hazina na akasema kwamba Marwan hakustahili kupewa hata dinari mia moja (Sharah bin Abil hadid, Juz. 1, uk. 67).

Waandishi wa historia wote, watoa maoni, wahadithi na wasimulizi miongoni mwao, Aishah anashika nafasi ya kutambulikana, wanasema wazi kwamba wote wawili Marwan na baba yake Hakam na pia uzao wao walilaaniwa na walichukiwa na Mtume. Aishah anasema kwamba Marwan alizaliwa kutokana na mbegu ya kiume iliyolaaniwa na Mtume ambaye hakuvumilia kuishi kwao hapa duniani. Mwenyezi Mungu aliwatangaza wao, wahenga wao na wazao wao mti wa nasaba iliyolaaniwa, na Mtume wa Mwenyezi Mungu alimhamisha Hakam kutoka Madina. Abu Bakr na Umar pia hawakuwaruhusu kurudi. Lakini Uthman aliwarudisha, akawapa zawadi na akamwoza binti yake Umm Aban kwa Marwan.

Kwa maelezo ya kina angalia kwenye Mustadrak Hakam, Juz. 4, 481, Tafsir Qurtabi, Juz. 16, uk. 197, Tafsir Khashashaf Juz. 3, uk. 99, ilichapishwa Misri.

Marwan bin Hakam aliporudi kwa kuitwa na Uthman alivaa matambaa na alipotoka ndani ya baraza lake alivaa nguo za hariri na josho. Khalifa alimpa laki tatu kutoka kwenye sadak ya Yemen. (Tarikh Yaqubi, Juz. 2, uk. 41) Ni mtu ambaye alihamishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu na Abu Bakr na Umar pia hawakumruhusu kuingia Madina. Lakini Uthman alimwita akampa zawadi ya dinari laki moja. (Maarif bin Qutaibah, uk. 83, Iqdul Farid, Juz. 2, uk 261, na Mahizirat al-Jinan Yafei, Juz. 1, uk 85).

Harith bin Hakim alikuwa ndugu yake Marwan na mume wa Ayesha bint yake Uthman. Uthman alimpa dinari laki tatu kutoka kwenye rasilimali ya Waislamu. Pia kama sadaka (Ansabul Ashraf Balazaqi, Juz. 5, uk 52). Uthman pia alimpa soko “Mahzuni, ambalo liliasisiwa na Mtume hapo Madina. (Maarif, uk. 84, Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 261; Mahazarat Raghib Isafahan, Juz. 2, uk. 212). Zaidi ya hii, sehemu ya kumi (1/10) ya pato lililopokelewa kutoka kwenye masoko ya Madina pia ikitengwa kwa ajili ya Harith. (Sirat Halaabian, Juz.2).

Uthman alimpa Said bin Aas bin Umayyah dinari laki moja. (Abu Makhnaf na Waqidi) Aas baba yake na Said alikuwa mtu aliyekuwa na tabia ya kumtesa sana Mtume Ali alimua kwenye vita ya Badr. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 301). Said mtu ambaye wakati moja alimwita Hashim bin Utabah mtu mwenye jicho moja kwa dharau wakati wa kuangalia mwezi. Mtu huyu alipoteza jicho moja katika vita ya Siffin. Matokeo ya kejeli ya Said masahaba waheshimiwa wa Mtume wakampiga na kuichoma nyumba yake. (Tabaqat bin Sad). Inaeleweka kwamba Ali, Talha, Zubayr na Abdul Rabman bin Auf alipinga kitendo cha Uthman kumpa Said dinari laki moja, lakini khalifa hakujali. (Ansabul Ashraf Balazari, Juz. 5, uk. 28).

Uthman alimpa kaka yake wa kambo Walid bin Uqbah bin Abi Muit bin Abi Umar bin Umayyah mkopo wa dinari laki moja kutoka kwa Abdullah bin Masud, mweka hazina wa Kufah. Baadaye, bin Masud alimwambia arudishe fedha hizo za Hazina ya taifa, alimwandikia barua Khalifa kwamba bin Masud alimwambia arudishe deni la fedha za Hazina ya Taifa ambazo yeye Uthman alimpa. Tukio hili lilimfanya Khalifa Uthman aandike barua kwa Abdullah bin Masud, “Wewe ni mweka hazina wangu. Ninakuamuru usimwambie Walid kurudisha deni ambalo amekopa kutoka Hazina ya Taifa, wala usikatae kutekeleza amri hii.”

Alipoona hali hii, Abdullah bin Masud alikwenda kwenye msikiti wa Kufah siku ya Ijumaa na akawaambia watu tukio hili la Walid na Uthman bila kuficha. Walid akamtaarifu Uthman kuhusu jambo hili ambapo matokeo yake Abdullah bin Masud alifukuzwa kazi. (Ansabul Ashraf Balazari, Juz. 5, uk. 30 na Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 272).

Huyu Walid ni mtu ambaye baba yake, Uqbah alikuwa adui mbaya sana wa Mtukufu Mtume. Kwa mujibu wa simulizi ya Aishah, Mtukufu Mtume mara nyingi alikuwa akisema; “Nimechoshwa na majirani zangu wawili. Mmojawapo ni Abu Lahab na mwingine ni Uqbah bin Abi Muit. Wote wawili, zaidi ya fitina zingine, huacha lundo la uchafu na takataka, mlangoni mwangu.” (Tabaqat bin Sad, Juz. 1, uk. 186, chapa Misri). Waandishi wa historia wametengeneza orodha ya watu kama hawa ambamo majina ya Abu Lahab, Uqbah Abu Jahl, Hakam bin Abil, Aas bin Umayyah ni maarufu. (Tabaqat bin Sad, Juz. 1, uk. 186; na Sirah bin Hisham, Juz. 2, uk 25).

Watoa maoni na waandishi wa historia wanayomaoni kwamba Uqbah ni mtu aliye laaniwa ambaye alikwenda asi baada ya kuingia kwenye Uislamu. Aya hii iliteremshwa kwa ajili yake;

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ{27}

“Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake.” (Surah al-Furqan, 25:27).

Kwenye Aya hii dhalimu maana yake ni huyu Uqbad aliye laaniwa kama ambavyo imeelezwa kwenye Tafsir, Juz. 9, uk. 25; Tafsir Baizawi, Juz. 2, uk. 161; Tafsir bin Kathir, Juz. 3, uk. 317; Tafsir Naishapuri kwenye maandishi ya pembeni Tabari, Juz. 19, uk 10; Tafsir Kabir Razi, Juz. 6, uk. 369).

Kwa ufupi, yapo maandishi mengi sana kwenye vitabu vya historia na hadith kuhusu tabia mbaya ya Walid na baba yake kwamba kitabu cha pekee yake kinaweza kuandika kuhusu watu hawa. Kwa ufupi ni kwamba Walid alikuwa mwasherati, mzinifu, fisadi, na mlevi ambaye alinajisi imani, hapa chini tunaorodhesha baadhi ya matukio muhimu ambayo yana dhihirisha tabia yake:

Kwenye Msikiti wa Kufah, Walid asali Swala ya rakaa nne wakati wa Swala ya alfajiri badala ya rakaa mbili kwa sababu alilewa.

Kwa amri ya Imamu Ali, Abdullah bin Jafar alimwadhibu Walid kwa kumchapa viboko thelathini kwa sababu ya kunywa mvinyo.

Walid bin Aas aliposhikanafasi ya Ugavana wa Kufah baada yake, alihakikisha mimbari ilisafishwa na alisema, “Ondoeni uchafu wa Walid kutoka humo.” (al-Ghadir na Allamah Amini, Juz. 1, uk 274).

Khalifa Uthman alimpa Abdullah bin Khalid bin Usayd bin Aas bin Umayah dinari laki tatu na dinari elfu moja kwa kila mtu wa kabila lake. (Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 26) na Maarif cha bin Qutayba, uk. 84), Bin Abil hadid ameandika tarakimu ya laki nne (Sharah Nahju balaghah Juz. 1, uk. 66).

Yaqubi ameandika kwamba Uthman alimuoza binti yake kwa Abdullah bin Khalid na Usayd na akaamuru apewe dinari laki sita na kuhusu jambo hili alimwandikia Abdullah bin Aamir kwamba kiasi hicho cha fedha kichotwe kutoka kwenye Hazina ya Taifa ya Basrah (Tarikh bin Wazih Yaqubi, Juz. 2, uk. 45).

Kila mtu anajua tabia ya Abu Sufyani bin Harb, Uthman pia alimpa mtu huyu dinari laki mbili kutoka kwenye Hazina ya taifa fedha hii ilitolewa siku moja alipopewa Marwan bin Hakam dinari laki moja (Sharah Nahju Balagha, Juz. 1, uk. 67).

Khalifa Uthman alimpa Abdullah bin Sad bin Abi Sarah kaka yake wa kuchangia ziwa sehemu ya tano ya ngawira kutoka Afrika. Kwa mujibu wa Abul Fida thamani ya ngawira hiyo ilikuwa dinari laki moja (Usudul Ghaba, Juz. 3, uk. 173; na Tarikh bin Khathir, Juz. 7, uk. 152).

Bin Abil Hadid ameandika kwamba Uthman alimpa Abdullah bin Sad ngawira yote iliyopokewa kutoka Afrika ya Magharibi bila kupunguza hata sehemu ndogo kumpa Muislamu yeyote. (Sharah Nahju Balaghah, Juz. 1, uk. 67).

Sad bin Abi Sarah ndiye mtu aliyeingia kwenye Uislamu kabla Makkah haijatekwa. Halafu akahamia Madina na akaasi imani ya Uislamu.

Baada ya uasi wake, Mtume wa Mwenyezi Mungu akatangaza kwamba Sad bin Abi Sarah lazima auawe popote pale atakapoonekana hata kama alikuwa chini ya kifuniko cha Ka’abah takatifu. Katika kuangalia mambo haya, Uthman alimficha na akamwombea msamaha akasamehewa. (Sunan Abu Daud na Mustadrak Hakim).

Uthman alimpa Talha bin Abdullah dinari laki mbili (Sarafu za dhahabu). (Balazari, Juz. 5, uk. 7) na alimpa mifuko kadhaa ya dhahabu na fedha.

Mifano iliyotajwa hapo ju imeonesha upendeleo wa Uthman na jinsi alivyo watengeneza Bani Umayyah wanagalagala kwenye utajiri wa Waislamu. Sasa tunataka kueleza jinsi watu wengine ambao si masahaba walivyoanza kutafuta dunia baada ya kifo cha Mtume na sasa dunia imewashinda. Lakini kabla ya hapo tunataka kuonesha kwamba msukumo waliopewa ani Umayyah na Uthman ilikuwa kinyume na radhi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Mwenyezi Mungu amewaita ‘mti uliolaaniwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu amewaita watu walioapizwa na umma. Wasomi wanakubaliana kwa pamoja kwamba Bani Umayyah walikuwa na chuki dhidi ya Mtume.

Ali anasema kwamba kila umma ulikuwa na shida za namna moja au nyingine Balaa la uma huu ni Bani umayyah (Tathir al-Jinan kwenye maandishi ya pembeni Sawaiq Muhriqah, uk. 143, na Kanzul Ummah, Juz. 6, uk. 91).

Kwa mujibu wa maoni yaliyothibitishwa ya Mtume na uzao wake, Bani Ummayah walikuwa balaa la uma lakini msimamo wa Uthman kwao ni kwamba alijivunia kitendo cha kufungua hazina ya Taifa kwa ajili yao. Khalifa Uthman alikuwa akisema; “Hazina ya Taifa ni yetu. Tutatumia kama tupendavyo na hatutakubali ushauri wa mtu yeyote.” (Sahuh Bukhari, Juz. 5, uk 17 na Tarihut Tashrib, Juz. 7).

Sasa tutatoa maelezo kuhusu urithi kwa baba wa masahaba. Itahakikishw utajiri mkubwa wa Waislamu ulifujwa na Uthman na jinsi alivyowatajirisha ndugu zake.

Zubayr bin Awam alikuwa mkwe wa khalifa wa kwanza. Alichoacha baada ya kifo chake ni:

    • Nyumba kumi na moja –Madina

    • Nyumba mbili –Basrah Nyumba moja- Kufah.

    • Nyumba moja Misri. Alioa wanawake wanne.

Baada ya kutoa theluthi moja (1/3) ya utajiri wake, kila mke alipata robo (1/4) ya thamani ya utajiri wa rasilimali yake yote ilikuwa dinari laki nane. (Sahih Bukhari, Kitabul Jihad Baab Barakar al-Ghifani Fi-Malih, Juz. 5, uk 17 na 21; Irshad al-sare Undat al-Qari Shazarat Dhahab Juz. 1, uk 43, Tarikh bin Kathir Juz. 7 uk. 249 na Tarikh Khsanus, Juz. 2, uk 311).

Muhammad bin Sad al-Dhahri al-Basri, Kitab al-Abbasi al-Qaqidi (Alifariki mwaka 230 A.H), ameandika kwamba alikuwa na mashamba huko Alexandria, Misri na Kufah na nyumba kadhaa Basrah. Alipokea magunia mengi sana ya nafaka kutoka Madina (Tabaqat bin Sad Waqidi; Juz. 3, uk. 77 chapa –London) Abul Has Ali bin Husain bin Ali Masud alikufa mwaka 346 A.H) ameandika kwamba zaidi ya vitu hivi aliacha farasi elfu moja, watumishi elfu moja, watumishi wa kike elfu moja na sehemu kubwa ya ardhi. (Murujuz Zahab uk, 434).

Talha bin Ubaydullah Tamim pia alikuwa mkwe wa Khalifa wa kwanza. Alikuwa na nyumba Kufah iliyojulikana kwa jina la Kanaas. Pato lake la kila siku kutokana na mauzo ya nafaka ilikuwa dinari elfu moja. Alikuwa na nyumba za kulala wageni kadhaa ambazo zilikuwa kati ya Tahama na Taif. Alimiliki ikulu ya hali ya juu sana Madina. Alikuwa na rasilimali Iraq ambayo ilikuwa inazalisha pato la dinari 10,000 kila mwezi Musa bin Talha anasema kwamba aliacha dinari laki mbili fedha taslim. Pia aliacha ardhi ya kilimo. Zaidi ya hayo, aliacha magunia ya ngozi mia tatu yaliyojaa dhahabu na fedha. Bin Jauzi anasema magunia hayo yalitengenezwa kwa ngozi ya ngamia na yalikuwa makubwa sana (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 158, Ansabul Ashraf Balazari, Juz. 5, uk 7; Murujuz Zahab, Juz. 1, uk. 434, Iqbdul Farid, Juz. 2, uk 258, Duwalul Islam Zahabi, Juz. 1, uk 18 na Al-Khulasah Khazraji, uk. 152).

Abdur Rahman bin Auf alikuwa shemeji yake Uthman na ni mtu huyu ndiye wakati Umar alimfanya Uthman kuwa Khalifa badala ya Ali, kama ambavyo imekwisha simuliwa. Aliacha ngamia elfu moja, mbuzi elfu themanini na farasi mia moja na aliacha dhahabu nyingi sana hivyo kwamba ilibidi ikatwe kwa shoka ili igawanyike. Alikuwa na wanawake wanne wa ndoa. Kila mmojawao alikuwa na dinari 83,000. Alimtaliki mke mmoja wakati anaugua na alimpa dinari 83,000. Aliacha kondoo 10,000, wenye thamani ya dinari 84,000. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 96, Murujuz Zahab, Juz. 1, uk 434; Tarikh Yaqubi Juz, 2, uk. 146; Safwatus Safwah bin Jauzi Juz. 1, uk. 138, Riazun Nazrah, Juz. 2, uk. 291; Istiab Abdul Barr Makki, Juz. 2, uk. 404 na Tuhfah Ithna Ashariyah na Muahadithi Dehlavi). Sasa kutokana na urithi aliooacha tunapata sababu iliyomfanya amweke Uthman kwenye Ukhalifa badala ya Ali bin Abi Talib.

Sad bibn Abi Waqqas aliacha dinari 250,000 na nyumba iliyojengwa mahali paitwapo Aqiq. Nyumba hii ilikuwa nzuri, kubwa yenye nafasi ndefu kwenda juu. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 105, na Murujuz Zahab, uk 120 wa Tafsir ya kitabu cha Abdul Hamid Jaudatus Sahar kwamba Sad bin Abi Waqqas alikuwa amenakshi sehemu ya ndani ya ikulu yake kwa mawe magumu.

Yala bin Ummayah ambaye alikuwa gavana wa Yemen aliacha dinari 500,000, wadeni wake wengi na ardhi kubwa. Zaidi yake, aliacha rasilimali yenye thamani ya Dinari 100,000. (Murujuz Zahab, Juz. 1, uk 432).

Zaid bin Thabit ni mtu aliye msaidia Uthman kwa kila njia na alikuwa mnyenyekevu kwake. Alipokufa, aliacha dhahabu na fedha katika hali ambayo haingegawika isipokuwa kuikata kwa shoka na kishoka. Zaidi ya hayo, aliacha mali nyingine iliyokuwa na thamani ya dinari laki moja. (Murujuz Zahab Masud).

Huu ulikuwa ukarimu, upendeleo na fadhila za Uthman, Khalifa wa tatu kwa watu wake waliokuwa wanamtakia mema. Hakuna mfuasi wa Mtume ambaye angevumilia namna yake ya kugawa utajiri wa Waislamu miongoni mwa watu wake. Ndio sababu Ali, Salman, Abu Dharr, Miqdadi na Ammar walikuwa wanampinga wakati wote kuhusu tabia yake.

Inawezekana watu wakasema kwamba lolote alilofanya Uthman ilikuwa kwa ajili ya ndugu zake kama alivyosema yeye mwenyewe kwamba aliwafikiria kwamba walistahili na hakufanya lolote kwa maslahi yake. Jibu la maoni ya Uthman linaweza kuwa mtu asiyezingatia sharia ya dini katika masuala yahusuyo ndugu zake, kwa hakika hatakuwa muangalifu hata kwa mambo yanayomhusu yeye mwenyewe. Uthman alikuwa na meno kadhaa yaliyotengenezwa kwa dhahabu. Kivazi chake kilikuwa joho la hariri na manyoya ambalo thamani yake ilikuwa dinari mia moja.

Vazi la mkewe Nailah pia liligharimu dinari mia moja. (Tabaqat bin Sad Juz. 3, uk. 40; Ansad, Balazari Juz. 3, uk. 4, Istiab, Juz. 4, uk. 476).

Palikuwepo kasha kwenye Hazina ya Taifa huko Madina ambalo lilijaa dhahabu na fedha. Alitengenezesha urembo kwa ajili ya familia yake kutokana na madini hayo. Watu walimpinga sana kuhusu suala hilo, na alizozana na Ali pia, lakini hakujali lolote. (Ansah, Balaziri juz, 3, uk. 4). Alijenga ikulu Madina; jengo hilo liliimarishwa kwa mawe na marumaru na milango yake ilitengenezwa kwa mbao za mvule zenye ubapa unaoteleza. Alihodhi utajiri mwingi sana. Alimiliki chemchem kadhaa Madina. Waandishi wa historia wanasema kwamba baada ya kuuawa, aliacha dinari laki hamsini. Miongoni mwa mali zake na vitu vingine vilivyokuwa kwenye miliki yake, vile vilivyokuwa kwenye bonde la Qura na Hunayn peke yake thamani yake ilifika dinari laki moja. Zaidi ya hayo aliacha farasi na ngamia wengi. Kwa mujibu wa bin Sad thamani urith wa bonde la Qura na Khaybar ulikuwa dinari laki mbili. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 53 na Masudi, Juz. 1, uk 433). Na kwa mujibu wa Jovji Zaydan uriti huo ulikuwa dinari laki 10. (Tamaddume Islam, Juz 1, uk 22, chapa Misri) Zaidi yake, aliacha watumishi elfu moja; (Bin Sad, Juz. 3, uk. 53).

Umar khalifa wa pili pia hakuweza kuepuka ladha ya ukabaila. Alikuwa na bustani Hijaz iliyokuwa inaingiza pato la dinari elfu 40 kwa mwaka ambalo alitumia yeye binafsi na familia yake Bani Adi. (Tarikh Tabari, Juz. 2, uk. 82, chapa Misri) kwa mujibu wa hadith ilioko sahih Bukhari, Umar aliuliza kiasi cha deni lake alilotakiwa kulipa Hazina ya Taifa. Watu walifanya hesabu na wakamwambia deni lake lilikuwa dinari elfu themanini na sita. Akawaamuru walipe deni hilo kutoka kwenye fedha ya ndugu zake mwenyewe. Ni kwamba, aliwaambia walipe deni hilo kutoka kwenye rasilimali yake. (Tarikh Tabari, Juz. 2, uk. 382). Naafe mtumishi wa bin Umar, amekanusha kwamba Umar hakuwa na deni na amesema ingewezekanaje Umar kuwa na deni ambapo mmojawapo wa warithi wake aliuza mgawo wa rasilimali kwa dinari laki moja. (Kitab Madina Umar bin Shaybah).

Akitoa maoni kuhusu usemi wa Naafe bin Hajaz alisema kwamba wakati mwingine hutokea kwamba mtu anakuwa na deni licha ya utajiri wake. (Tarikh Tabari, Juz. 3, uk. 383). Ndugu alimuomba Umar fedha. Mara ya kwanza alimdharau lakini baadaye alimpelekea dinari elfu kumi. (Tarikh Tabari, Juz. 5, uk. 19) Yakiwepo mambo kama haya tunapoangalia uzao wa Mtume na jinsi walivyoteseka, tunawasikitikia na tunashtuka sana tunapoona kwamba watu hawa waliwanyang’anya Ahlul-Bait hata ile haki yao ya khumus (Izatul Khifa, Juz. 2, uk. 256) na kuwapora fadak.