Sura Ya Kumi Na Saba

Ni ukweli ulio thabiti kwamba Abu Dharr alikuwa karibu sana na Mtukufu Mtume na Ahlul Bait wake na aliendelea kuwa msiri wao mkubwa. Aliona kwa uangalifu sana kila kipengele cha maisha yao, na alijifunza mengi kutokana nao. Ameona kwa macho yake si mara moja lakini mara nyingi kwamba Mtukufu Mtume alikuwa anajilaza msikitini akiwa na njaa na watoto wake nyumbani walikuwa na njaa. (Alaimun Nubuwwah, al-Mawardi, uk. 146 chapa Misri).

Abu Dharr pia alimuona Ali bin Abi Talib akifanya kazi ya kupokea ujira akiwa amevaa nguo zakukwaruza. Aliona majani ya mtende kwenye joho la bint yake Mtume.

Pia aliusikia Ali akimnasihi mtumishi wake wa kike wa Kiafrika Fizzah; “Ewe Fizah! Sisi Ahlul Bait hatukuumbwa kwa ajili ya dunia au kutafuta faida ya kidunia. Badala yake tumeumbwa kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu, Uislamu. Ni kazi yetu kuongoza thamani ya uadilifu wa mtu, kuwasha mwanga wa Upweke wa Mwenyezi Mungu kwenye mioyo ya watu na kuwapa njia na namna ya kuendesha na kustawisha maisha yao.”

Abu Dharr pia aliona kwamba Ali alikuwa na kawaida ya kula mkate mkavu wa shayiri na alificha mifuko unga wa Shayiri yake kwa ustadi mkubwa hivyo kwamba haingewezekana mtu kuweka samli. (Allamah Kashif al-Ghita, The Shia Origin and Faith, ISP 1982). Pia alimuona Ali kwamba alikuwa na desturi ya kubeba mfuko ya unga yeye mwenyewe kuwapelekea wajane masikini na mayatima. Pia alimuona Ali akiiambia dunia, “Ewe Dunia! Nenda ukawadanganye wengine. Nimekutaliki mara tatu!.” Pia alishuhudia kwa macho yake kwamba wazawa wa Muhammad walikuwa na tabia ya kula chakula pamoja na watumishi na watumwa wao. Alikumbuka vizuri kwamba wakati fulani ambapo dinari nne zilibaki baada ya Mtume kugawa fedha aliyokuwa nayo na kiasi hiki hakingemfikia mtu anayestahili, alisikitika sana. Alikuwa bado anakumbuka maneno haya ya Mtume aliyomwambia yeye, Ewe Abu Dharr! Hata kama nina miliki dhahabu yenye ukubwa sawa na Mlima Uhud sipendi ibakiea kwangu hata chembe.”

Katika hali kama hii, ingewezekanaje Abu Dharr anyamaze wakati Uislamu ulikuwa unageuzwa na mafundisho ya viongozi wa Uislamu yalikuwa yanadharauliwa? Mara tu Mtukufu Mtume alipofariki kila kitu kilibadilishwa. Dhuluma na udikteta ilishamiri, watu walilazimishwa kutoa kiapo cha uaminifu, nyumba ya Ahlul Bait ilichomwa moto, na mlango ulivunjwa na kumwangusha Fatimah, bint yake Mtukufu Mtume.(al-Milal wan Nahl Juz. 1, uk. 25 chapa ya Bombay).

Ali alifungwa kwamba shingoni na masahaba mashuhuri waliishi maisha ya upweke majumbani mwao. Katika kulazimishwa na hali halisi Abu Dharr alistahamili kwa kipindi fulani. Hatimaye akaondoka Madina na kwenda Syria na akakaa huko. Baada ya muda alipokwenda tena Madina aliona kwamba viongozi walifika kwenye kilele cha kuendelea mambo ya dunia.

Fahari na maonesho ya kifalme yalishika nafasi ya ucha Mungu aliyoishi Mtukufu Mtume. Fadhila na upendeleo ni tabia ambazo zilishamiri, na uaminifu na uchaji Mungu vilionekana kuwa vitu vya zamani. Utajiri wa Hazina ya Taifa ulikuwa unafujwa. Utajiri wa Waislamu ulikuwa unatumiwa kwa maslahi ya binafsi. Kila ndugu na anayemtakia mema khalifa alipata umilionea. Ukabaila ulipanuka. Palikuwepo na utajiri mwingi sana. Hakuna mtu aliyejali Zaka. Hakuna Mtu aliyejali mayatima na wajane.

Alipoona mambo mengi yasiyo na idadi kama haya, Abu Dharr alijaribu kumwonya Khalifa Uthman kwa ajili ya kuulinda umma wa Kiislamu na serikali ya Kiislamu na akamshauri kadiri alivyoweza, lakini Khatifa hakutilia maanani ushauri wake. Hatimaye kwa kuzingatia ahadi aliyoahidi kwa Mtukufu Mtume na ule uzio wa imani ambao Mwenyezi Mungu alihifadhi moyoni mwake, alijitokeza uwanjani na akaanza kutangaza dosari za Uthman. kuunganisha na hayo, pia alikemea tabia ya kuhodhi utajiri na ukabaila na alianza hotuba yake na zile aya za Qurani zinazokosoa kuhodhi utajiri.

Kwa kuwa Abu Dharr hakuvumilia kuona utajiri wa rasilimali ya taifa inatumika kwa kuwagawia ndugu zake khalifa tu na mayatima na wajane wanakufa kwa njaa, aliongeza kazi ya mahubiri yake, na kwa hiyo alikwenda sehemu nyingi mbali mbali.
Alihamishwa kutoka Madina na kupelekwa Syria na wakati mwingine alilazimishwa kuishi kwenye sehemu iliyokuwa tupu kama Rabzah.

Ni dhahiri kwamba kugawa utajiri miongoni mwa fukara ni muhinu, lakini pia ni muhimu kufikiria utajiri huo ugawiwe kwa kanuni gani kwa masikini na watu wengine wanaostahili. Ilikuwa ni kanuni ya Mtume kwamba aligawa utajiri bila upendeleo. Kuhusu ngawira ya kivita, alisema kwamba moja ya tano (1/5) ilikuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na sehemu nne ya tano (4/5) kwa ajili ya jeshi la Uislamu ambamo mashujaa wote wanapata mgawo sawa. Hakuna anayestahili kupata zaid ya mwingine (Sunan Baihaqi).

Inajulikana kutoka kwenye vitabu vya hadithi kwamba alikuwa na kawaida ya kugawa pato la ushuru miongoni mwa Waislamu siku hiyo hiyo ya kupokea pato hilo. Watu waliooa aliwapa mgawo mara mbili na mgawo moja kwa mseja. (Sunan Abi Daud, Juz. 1, uk 25; Musnad Ahmad bin Hanbal, Juz. 2, uk. 29 na Sunan Baihaqi Juz. 6, uk. 346).

Utaratibu huo huo ulifuatwa na Imamu Ali. Hafidh Baihaqi anasema kwamba wakati fulani alipata fedha na rasilimali kutoka Isfahan. Aligawa fedha na rasilimali hiyo katika sehemu saba za mgawo zilizo saw, mkate wa boflo moja ulibaki lakini aliugawa pia katika vipande saba vilivyo sawa na kuweka kipande kimoja kwenye kila mgawo katika hiyo migawo saba. Aliandika majina na alimpa mtu mgawo ambaye jina lake lilitokea kwenye kura. (Sunan Baihaqi juz, 6, uk 438).

Wakati fulani wanawake wawili walimwomba. Mmojawao alikuwa huru na mwingine alikuwa na asili ya utumwa. Alimpa kila mmoja ngano kidogo na dinari arobaini.

Mwanamke mwenye asili ya utumwa alikwenda na mgawo wake lakini yule mwanamke huru akasema, “Umenipa mgawo sawa na ule wa mtumwa, ingawa mimi ni mwanamke huru wa Kiarabu ambapo mwenzangu ni mtumwa na si Mwarabu.” Amiri wa Waumini akasema, Nimepekua kwa uangalifu mkubwa Kitabu cha Mungu lakini sikuona sababu yoyote ya ubora wako.”

Muhammad Razi Zangipuri ameandika kwamba wakati wa utawala wa Ali ambapo utaratibu wa Mtume alifuatwa na fedha iligawanywa katika misingi ya usawa, hali ya kutokuridhika chuki na kero ilionea miongoni mwa masahaba wa Mtume walio mashuhuri wakipinga mbinu hiyo. Ali akasema kuhusu kuonesha kwao chuki na kero; “Mtakuwa mnaniamuru mimi kwamba nitafute msaada wenu na kuniunga mkono kwa kufanya udhalimu kwa watu ambao kuwa ajili yao mimi nimewafanywa mtawala? Ni kwamba, niwapunje stahili yao ili nyingi niwazidishe mgawo na kwa hiyo kuwafanyeni nyinyi kuwa watu wanao niunga mkono?

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu hadi hapo ambapo hadithi za usiku zinaendelea kusimuliwa na nyota inafuata nyingine yaani nyota zinakuwa kwenye mwendo, sitakaribia utaratibu kama huo. Hata kama ingekuwa rasilimali yangu binafsi, ningeigawa sawa kwa sawa miongoni mwa watu, lakini sasa inapokuwa hii ni mali ya Mwenyezi Mungu, kwa nini nisizingatie usawa. Lazima mtambue kwamba kugawa fedha na wema bila kuzingatia usawa ni ubadhilifu na ufujaji ambao unamnyanyua mgawaji juu hapa duniani na kumteremsha chini na kumfedhehesha huko akhera.” (Islam ka Maashi Nizam, toleo la lugha ya Urdu, uk 154).

Ni wazi kwamba kutokana na kanuni iliyotajwa kwenye kurasa za nyuma ya kugawa utajiri kwamba rasilimali zitagawanywa bila upendeleo miongoni mwa masikini, wasiojiweza na aina zote za watu wanaostahili. Mara tu Ali alipokalia kiti cha Ukhalifa alitangaza, “Nyingi ni waja wake Mwenyezi Mungu. Utajiri utagawanywa sawa sawa miongoni mwenu bila ubaguzi au kutofautisha.” (Nasikhut tawarikh, Juz. 2, uk. 21).

Endapo Waislamu wanafuata njia za Kiislamu, maisha ya umasikini hayatakuwa mzigo kwao.