Maneno Machache

Kwa jina la Allah swt.

Watu walio hodari humu duniani wanakubali kuwa akili/busara ni mwongozo na mtoa ushauri wa mwanadamu. Huwa inamwongoza kuelekea mema na kumzuia na mabaya. Ni busara hiyo ambayo ndiyo inayomtofautisha mtu na mnyama na kumfanya awe kiumbe bora kuliko wote.

Allah swt anawaamrisha watu watumie busara katika kutatua matatizo yao. Allah swt anatuambia katika Qurani Tukufu kuwa 'aya zake kwa ajili ya wale wanaofikiri. ' Maneno machache kiasi gani lakini hayakosi hekima ndani yake. Iwapo tutafuata mambo kama vipofu basi hatutakuwa na tofauti na wanyama na labda tutakuwa dhalili kuliko hao kwa sababu mtu kama huyo inavyoonekana hajijali.

Busara bila ya elimu pia ni bure kwa sababu elimu ni nuru ya busara. Lakini elimu ni kiasi kidogo sana kwa kulinganisha na ukubwa wa ulimwengu. Allah swt anatuambia kuwa hatukupewa isipokuwa elimu kidogo tu, rejea 17:85. Hivyo ni ujahili mtupu iwapo sisi tutajigamba kwa elimu yetu kwa kutaka kukanusha sharia za Allah swt ambapo jambo la msingi ni kutokuelewa kwetu vyema masuala hayo.

Hivyo ni dhahiri kuwa yale yote ambayo yameelezwa na kubashiriwa katia Kitabu cha asili na kudura na yale ambayo yamesemwa na Mtume Mtukufu s.a.w.w hayawezi kamwe kuwa uongo ati kwa sababu sisi hatuelewi. Kila mmoja atakubaliana nasi iwapo tutasema kuwa kazi za kubuni na kufikiri hazina uhakika wowote mbele ya uchunguzi na matendo.

Kujitumbukiza katika mambo ya kubuni na uzushi ni tabia ya Shaitani kwani yeye alijitakabarisha kiasi cha kumuasi Allah swt. Kufuata elimu kwa njia sahihi ni kule kufanya uchunguzi na utafiti juu yake kabla ya kutekeleza. Mtume Muhammad s.a.w.w alisema kuwa "Mimi ni mji wa elimu na Ali ni mlango wake" na vile vile alisema kuwa "Mimi ni hazina ya elimu na Ali ni ufunguo wake". Kwa hivyo tumepata ushahidi wa Mtume Mtukufu s.a.w.w kuwa kuna shakhsiya waliobarikiwa elimu kwa kudura za Allah swt. Hivyo elimu yake Imam Ali a.s. haiwezi kupimika au kuelezeka.

Kwa hivyo ni faradhi kwetu sote kuamini na kusadiki yale yaliyoelezwa katika Qurani Tukufu na marejeo ya Qurani katika Ahadith za Mtume Mtukufu s.a.w.w na Mrithi wake Imam Ali a.s. na Ahali yake a.s. Haitupasi sisi kamwe kuzikataa semi zao ambazo sisi hatuzielewi kikamilifu. Kutoamini na kutosadiki huku katika Islam kunamfanya mtu akufuru.

Na mojawapo ya maudhui hayo ni kuhusu QayamaError: Reference source not found - ambayo ni mojawapo ya misingi ya Dini ya Islam. Hivyo kuna mabashiri mengi kabla ya kufikia Qayamah. Mambo yaliyobashiriwa yanapatikana katika QuranError: Reference source not found Tukufu na katika Ahadith. Katika mabashiri yote hayo kuna ubashiri mmoja muhimu kabisa wa kuja kwa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. Na ubashiri huu upo unapatikana katika Aya za Qurani Tukufu, Ahadith, misemo ya Wanazuoni wakuu na Mafuqahaa. Hivyo litakuwa ni jambo la kuaibisha iwapo atatokezea mtu kupinga ubashiri huo ati kwa sababu ya ujahili wake. Jee huyo mtu ataweza kukabiliana na Qurani, Ahadith na wanazuoni?

Waislamu wote kwa ujumla wanaamini kudhihiri kwa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. ingawaje kuna tofauti kidogo. Mashiah wanaamini kuwa Imam Mahdi a.s. yu hai na yupo ghaibu (mafichoni) kama vile walivyo Mtume Issa a.s. , Ilyas, Khizr n. k. Kwa upande wa Masunni wao wanaamini kuwa yeye bado hajazaliwa na atajidhihirisha atakapofikia umri wa miaka arobaini. Kwa mukhtasari, Masunni wanaamini kuwa atakuwa ghaibu kwa kipindi cha miaka arobaini ambapo wanazuoni wakubwa wanaungana na Mashiah katika masuala hayo.

Kukanusha kuwapo kwa MahdiError: Reference source not found ni uthibitisho wa kufr, kwa sababu Mtume s.a.w.w amesema kuwa yeyote atakaye kataa kuwapo kwa Mahdi basi ni Kafiri. Jambo dogo kabisa linalo tuhakikishia kuwapo kwa Mahdi a.s. ni kule kutokezea kwa Mahdi-bandia ambao wapo wanapatikana katika historia. Kwa hivyo iwapo utataka nakala basi itatokana na nakala asilia, kama hakuna nakala asilia basi huwezi kupata nakala yake. Vile vile kuna habari kamili katika vitabu vya kale kuhusu Imam Mahdi a.s. , nasaba yake n. k. hivyo inatuwia rahisi kwetu sisi kuweza kutofautisha baina ya Mahid wa kweli na wale bandia. .

Hao MahdiError: Reference source not found bandia wameweza daima kuwazuzua wale wote waliokuwa majahili na wasio zijua sifa za Imam a.s. na ambao hawajui kuhusu ubashiri wa kuja kwa Imam Mahdi a.s. Hivyo ni faradhi kwetu sote kufahamu na kujua elimu na maarifa ya Imam a.s. hasa katika kipindi hiki kilichojaa kwa uovu na dhuluma za kila aina za Shaitani. Watu wengi hawana mapenzi na Dini, na hapa ndipo Shaitani anapopata nguvu na wafuasi wake katika mambo ya maasi. Dunia yetu inakaribia kuangamia kwani dalili za Qayama zipo mbele yetu hivyo kunakaribia kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s.

Nimejaribu kuzikusanya mabashiri yote ya kuja kwa Imam Mahdi a.s. ambayo bado hayajatokea katika kitabu hiki na kukipa jina la Qayamat-i-Sughra ambapo ni matumaini yangu kuwa wasomaji wote watafaidika na kuifanya imani yetu kuwa madhubuti katika Dini na kujitayarisha kumpokea na kukutana na Imam Mahdi a.s. Mwokozi na mkombozi wetu sote !

Sababu ya kukipa jina hili la Qayamat-i-Sughra ni kwamba Imam MahdiError: Reference source not found a.s. hatadhihiri hadi hapo dunia nzima ichafuke kwa maonevu na dhuluma kwa kiasi cha kupindukia. Hivyo jina hili linamaanisha 'kipindi kitakachotangulia QayamaError: Reference source not found'

Kitabu hiki kimezungumzia na kugusia mambo mengi mno zikiwemo itikadi za watu, dini zao, mila na desturi, utamaduni, elimu,mawazo na fikara zao. Hivyo ninawaombeni nyote kunitumia maoni yenu kwa kukubalia maandiko au kuyapinga au kuyafafanua zaidi ili yanisaidie katika kuendeleza kazi hii iwe vyema zaidi hapo siku za mbeleni. Yote mutakayonitumia lazima ziwe na hoja na ufafanuzi mzuri kwani zitaweza kuingizwa katika chapa zitakazokuja.

Hatimaye ninatoa shukrani zangu za dhati kwa wote.

5 Januay 1996
Amiraly M. H. Datoo
P. O. Box 838,
Bukoba, Tanzania (E. Africa)