Sehemu ya Tatu : Kadiani : Madhehebu Ya Maahmadiya

Miaka1 150 iliyopita katika mji wa Kadyan, katika jimbo la Punjab, India, alizuka Gulam Ahmed KadianiError: Reference source not found ambaye alijitangazia Utume na Umahdi. Wafuasi wake hata leo wako IndiaError: Reference source not foundna kwingineko. Baada ya kifo cha Gulam Ahmed wafuasi wake waligawanyika katika makundi mawili: Kadiani na Mirzai. Gulam Ahmed alifanya daawa kubwa ya Umahdi. Vitabu vingi vimeandikwa na wanazuoni wa madhehebu yote, Shia na Sunni, kubatilisha dai lake na majadiliano yalifanywa kudhihirisha ubatili wa nadharia yake na madai yake ambayo yalikuwa kinyume cha dini. Kitabu hiki hakina lengo la kueleza marefu na mapana juu ya jambo hilo, lakini kuthibitisha ukweli wa Uimamu wa Hadhrat MahdiError: Reference source not found (A.S. ) suala limeguswa tu ili kuthibitisha ubatili wa dai la Makadiani na maamrisho ya dini juu yake.

Gulam Ahmed Gulam Murtaza Atta Mohamed alifariki duniani 1908 akiwa na umri wa miaka 65. Yeye alikuwa Moghul kutoka Samarkand mwenye asili ya Kiajemi. Alifanya daawa nyingi; kwanza alitangaza kuwa yeye ni mwongozi wa dini, baadaye akawa MahdiError: Reference source not found na hatimaye kajidai kuwa Mtume.

Kwa kufanya daawa ya Utume yeye na wafuasi wake wameondoka katika Imani ya Islam kwa sababu Waislamu wote hukubaliana kwa kauli moja kwamba Mtume Muhammad s.a.w.w ni Mtume wa mwisho. Katika 1898, Mirza aliwauliza maswali wanazuoni wa Kisunni na kutokana na majibu ya Uimamu wa kughibu na kutokeza kwa Imani MahdiError: Reference source not found yalithibitishwa pasipo shaka. Hata hivyo, Mirza bado aliendelea kudai kuwa yeye ni Mahdi, Mtume Issa, Krishna na Mtume.

Munshi Mohamed Abdalla katika kitabu chake Shahadate Qur’any amechapisha maswali aliyoulizwa Mirza Gulam Ahmed KadianiError: Reference source not found na majibu aliyopokea kutoka wanazuoni wa Kisunni.

Suala: Kutokana na hadithi, wafuasi wa madhehebu ya Sunni huamini kwamba katika siku za mwisho wa dunia atatokeza MahdiError: Reference source not found ambaye atatokana na dhuria ya Fatima (a.s. ) binti wa Mtume s.a.w.w na ambaye atakuwa mrithi wa kweli wa Mtume s.a.w.w Ikiwa mfuasi yeyote haamini hayo afikiriwe namna gani ? Suala hili lazima lijibiwe na wanazuoni na ulamaa wa dini. Tarehe 29 Desemba 1898, 15 Shaaban 1316 A. H. Mirza Gulam Ahmed”.

Jibu: “ Masunni wote hukubaliana katika imani yao kwamba katika siku za mwisho za dunia kutokana na dhuria ya Fatima (a.s. ) binti wa Mtume s.a.w.w atatokeza MahdiError: Reference source not found. Yeye ataeneza Islam duniani kote na kuitawala dunia katika mambo yote ya kidini na kiulimwengu. Yeyote asiyeamini hayo atastahiki adhabu kufuatana na aya ya Quran isemayo: “Na atakayemwasi Mtume ataingizwa Jahannam. . . ”(4:115)Mtu huyo atakuwa amepotea njia, bila shaka amepotea njia kabisa.

Imetiwa saini na Abdul Haq Gazanwy (Mwanazuoni wa Kisunni) na baada ya hapo wanazuoni 19 wa Kisunni wakatuma majibu yao na baadhi yao walieleza bayana kwamba mtu asiyekuwa na “Imani hiyo” ataishia motoni.

Mwanazuoni wa Kisheria Janab Molvi Seyyid Ali Hainy amethibitishia ukweli wa jibu hilo kwamba mtu asiyekuwa na “Imani hiyo” ni kafiri.

Gulam Ahmed mwenyewe alikuwa Sunni na aliamini kwamba Mtume Muhammad s.a.w.w alikuwa ni Mtume wa mwisho. Kama vile Waislam wote wanavyoamini kwamba Mtume Issa yupo hai mbinguni yeye vile vile aliamini na hata kuandika hivyo katika kitabu chake Barahine Ahmadia baada ya kujitangazia Umahdi. Hatuna haja ya kuendeleza mada hayo, bali nia ni kueleza maneno machafu aliyotumia dhidi ya Islam, Quran na Imani za Kiislamu na vipi bishara zake alizotoa zikaonekana za uwongo.

Imani za Mirza Gulam Ahmed

1. Baada ya kutoa ilani kuwa yeye ni Imam MahdiError: Reference source not found, Mirza akachapisha kitabu kiitwacho Baharine Ahmadia na katika maelezo katika ukurasa 498 amearidhiwa kwamba: “Aya hii ni kwa ajili ya Mtume Issa ambaye atakuja mara ya pili duniani”.

Zaidi ya hayo mwanae wa mrithi wake Mirza Mahmoud, katika gazeti la Kiurdu Afzal” la tarehe 27 Juni 1916 amenakili kwamba: “Zamani ilikuwa itikadi ya Waislamu wote pamoja na viongozi wakuu kwamba Mtume Issa bado yu hai. Hata hivyo baba yangu Mirza Gulam Ahmed alikuwa na itikadi hiyo kwa muda wa miaka 10 hata baada ya (kudai) MahdiError: Reference source not found na aliamini hivyo na kusisitiza kwamba Mtume Issa yu hai na yuko mbinguni. ”

1. Kwa muda wa miaka 1300 Waislamu wote hata Mtume s.a.w.w mwenyewe pamoja na Maimamu wote na Wanazuoni walikubali itikadi hii ya kwamba Mtume Issa yu hai. Lakini baada ya miaka kumi na kujitangaza kuwa MahdiError: Reference source not found Mirza alipokea Wahyi kwamba Mtume Issa amefariki dunia na yeye amekuwa Mtume Issa ( kwa utanasukhi?) Amesema kuwa Mungu amemteremshia Wahyi: Yule Mtume Issa amefariki dunia wala hatarudi tena duniani na kwa hivyo yeye (Mirza) ni Mtume Issa, mwana wa Maria, alijitokeza. ” Mirza mwenyewe alikuwa mwanazuoni na alifahamu hadithi vizuri sana. Baada ya kufahamu kote huko akadharau imani iliyokubaliwa kwa makini na Waislamu kwa miaka 1300 hata na yeye mwenyewe kwa muda mrefu na kujitangazia kuwa yeye ni Mtume Issa kinyume cha aya za Quran Tukufu na hadithi, bila kuwa na ushahidi au dalili ya aina yoyote ya kuthibitisha daawa yake.

2. Mirza aliaridhia katika gazeti la “Badar” katika toleo la 5 March 1908, kuwa: “Ni daawa yetu kwamba sisi ni Rasul au Mtume. Yeyote anayeteuliwa na Mungu lazima awe bora kuliko wengine kutokana na nasaba yake na sifa zake na awe mtu mwenye kutabiri mambo mengi na sisi tunazo sifa hizo. ”

Katika kitabu cha Shahadate Quran ala kidhbe Krishna Kadiani kilichochapishwa Lahore Pakistan na Islamiyya Steam Press yafuatayo ni maoni yaliyotolewa na Mirza:

1. Mirza ameandika katika Izale Awham, ukurasa 689 kuwa: “Baadhi ya bishara zilizotolewa na Mtume Muhammad s.a.w.w pia yamethibitika kuwa ni uwongo”.

2. Katika Barahine Ahmadia, Ukurasa 556 ameandika, “Mungu amemweka Hadhrat Muhammad s.a.w.w chini ya uongozi wangu na kwa hivyo Mungu huniteremshia Wahyi kupitia kwake. ”

3. Katika kitabu cha Izala ukurasa 25, aliandika kuwa,“Mwenyezi Mungu ameteremsha Quran lakini kuna baadhi za aya ambazo ni kinyume cha ustaarabu na msikilizaji yeyote anayeweza kufahamu hizo aya atasema kuwa kauli ya aya hizo ni mbaya. Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri katika aya hizo. Maneno machafu yasiyoweza kutumika yamezungumzwa juu ya Walid bin Mugheira. ”

4. Katika kitabu cha Anjame Atham:, ukurasa 51, ameandika kuwa: Bibi Maryam (Bikira Maria) na mwane Mtume Issa hawawezi kuwa bora kuliko Kaushalya (mama yake mfalme Ramchandra)”.

5. Katika kitabu hicho hicho, ukurasa 80, ameandika kuwa: Waislamu wanaamini kwamba Mtume Issa atarudi duniani lakini Mungu amenijulisha kwamba Mtume Issa amefariki dunia na mimi ndiye Mtume Issa:.

6. Kwenye ukurasa 691, katika Izalae Awhad amewataja kuwa: “Mimi ni Mtume Issa mwana wa Maria, Wakristo ni DajjalError: Reference source not found na gari moshi ni punda wa Dajjal. ”

7. Katika gazeti la kila mwezi la Al Hakam, Juzuu la iv, la 17 Juni 1900, amedai kuwa: “Baina yenu mimi ndiye Ali aliye hai na nyinyi mnaamini Ali aliyekufa.

8. Anaendelea kusema katika Aine Kamalati Islam, kurasa 564-65 kuwa: “Nimejipatia maongozi ya Mungu kwamba mimi ni Mungu mwenyewe. Nafsi Mungu imeingia kwangu. Kwa sababu Nafsi Mungu imeingia mwilini mwangu mimi ndiye niliyeumba dunia na mbingu”.

9. Kuhusu Imam Hussein (A.S. ) amesema: “Ninao Hussein kama hao kiasi cha elfu moja mfukoni mwangu”.

Bishara za Mirza Kadiani Zimethibitika kuwa ni za Uwongo

Mirza amechapisha bishara nyingi katika kitabu chake Ilhame Mirza na karibu zote zimethibitika kuwa ni uwongo.

1. “ Mimi ninabashiri kwa ukweli kwamba Mungu amenisimulia kwamba nitamwoa binti mkubwa wa Mirza Ahmed Beg. Ubashiri huu ukithibitika idadi maalum ya makafiri watageuka kuwa Waislam na wengi waliopotoka watarudi kwenye njia ya haki”. (Amed Beg alikuwa mtoto wa mjomba wake Mirza KadianiError: Reference source not found).

Alituma ushenga kwa Beg amwoe binti yake, na kutishia kwamba ombi lake likikataliwa bidhaa yake itakuwa mbaya kwa ajili ya binti huyo na kama akiolewa na mwanamme mwingine, huyo mwanamme atafariki dunia katika muda wa miaka miwili na nusu na katika muda wa miaka mitatu baba mkwe vile vile atafariki. Zaidi ya hayo maafa makubwa yatakabili jamii ya Ahmed Beg. Hata hivyo Ahmed Bag hakujali vitisho hivyo; alimwoza binti yake kwa mtu mwingine.

Mirza alipoona ubashiri wake umekuwa udanganyifu tu akatoa ubashiri mwingine: “Mwenye Enzi Mungu amenijulisha kuwa: Hatimaye mimi nitamwoa Binti na hakuna hata mmoja ataweza kuzuia jambo atakalo Mungu na yeyote atakayekukashifu atadhalilika. ”

Imetiwa saini na mnyenyekevu Gulam Ahmed, Gordapur, tarehe 10 Julai 1888 A. D.

Aliendelea kubashiri mengi juu ya jambo la ndoa na mwishowe katika kitabu chake Shahadatul Quran ukurasa wa 4, alitamka kwamba Ahmed Beg na mkwewe hawatakuwa hai baada ya 21 Agosti 1894. Mirza aliendelea kutoa vitisho dhidi ya huyo binti kwa muda wa miaka 20 eti kutokana na habari alizopewa na Mungu. Hatimaye Mirza mwenyewe alifariki dunia. Licha ya kumkosa huyo binti lakini yeye mwenyewe alifariki dunia, na huyo binti, babake na mumewe wote walikuwa hai wakiishi raha mustarehe.

2. Katika Ubashiri mwingine katika Jange Mukadas aliandika kwamba “Ikiwa Atham Shakhs hakufa na kuingia motoni katika miezi 15 mimi nipo tayari kupewa adhabu yoyote; mnidhalilishe, mnidharau, mnifunge kamba shingoni mwangu, mpake masizi usoni mwangu na mnilaani kuliko mashetani”. Hata hivyo, muda huo ulipita bila Atham Shakhs kufa.

3. Katika Kitabu chake Dafeul Bala amearidhia kwamba: KadianiError: Reference source not found haiwezi kukabiliwa na ugonjwa wa tauni kwa sababu Mtume wa Mungu huishi huko. Baada ya muda mfupi ugonjwa wa tauni ukaenea huko KadianiError: Reference source not found na kusababisha vifo vya watu kwa maelfu wakiwemo na wafuasi wa Mirza.

4. Tarehe 15 Aprili 1907 Mirza akatoa kitabu ambamo anadai kuwa ikiwa daawa yake itathibitika basi mtu mmoja Mirza Sonullah (wa Amritsar) atakabiliwa na laana ya Mungu na atakufa katika uhai wake (Mirza) kutokana na tauni au balaa nyingine. Akanadi kwamba Mweye Enzi Mungu atathibitisha ukweli wa daawa yake. Hata hivyo, Mirza mwenyewe akafa 26 April 1908 na wakati huo Molvi Sonullah alikuwa hai na licha ya kuwa na afya njema lakini hakupata hata kuugua. Bishara nyingi za Mirza zimethibitika kuwa ni udanganyifu tu lakini hatuwezi kuandika yote hapa.

Mirza Kadiani kama Mungu, Mke wa Mungu, na Mwana wa Mungu (Mungu apishie Mbali)

1. “Mungu anatamani kukuona unaingia mwezini, au unanajisika. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu atakujulisha alama zake ambazo zitaendelea kukufikia. Wewe hupati hedhi lakini umezaa mtoto ambaye atakuwa na hedhi ya mwana wa Mungu”. (Hakikatul Wahyi, ukurasa 143, na Arbaeen, uk,12).

2. Mmoja wa wafuasi wake mwaminifu, Kadhi Yar Mohamed B. O. L. Pleader, ameandika katika chapisho lake “Islami Kurbani” Juzuu la 24/Riaz Hind Press, Amritsar: “wakati mmoja Masihi anayesubiriwa (Mirza) alisimulia kwamba anapoteremshiwa Wahyi (ufunuo) na Mungu hali yake hugeuka kuwa kama mwanamke na Mungu hutumia nguvu zake za kiume juu yake”. (Audhubillahi).

3. “Roho yake ilipulizwa mwilini mwangu kama alivyofanyiwa Mariyam na kwa mfano mimi nimekuwa mja mzito. Baada ya muda usiozidi miezi kumi mimi niligeuzwa kwa njia ya ufunulio, kutoka Maria kuwa Mtume Issa (Kishtie Nooh ukurasa 47).

4. “Eh Mirza umetokana na maji yetu (manii) na wengine ni wa vitu vikavu. ” (Arbaeen,toleo 2, ukurasa 390).

5. “Baadaye maumivu yakamkokota Mariyam, yaani miye, kwenye mti wa tende. ” (Kishtie Nooh, ukurasa 47).

6. “Wakati wa ufunulio mwumbaji huniita “sikiliza mwanangu” (Hakikatul Wahyi, ukurasa 79, na Arbaeen, uk. 22).

7. “Niliota ndoto kwamba mimi ni Mungu na nina hakika kwamba mimi ni Mungu” (Hakikatul Wahyi, ukurasa 64).

8. “Mungu ameniambia, “Wewe unatokana na mimi na mimi (Mungu) natokana na wewe”. (Hakikatul Wahyi, ukurasa 74).

Kwa hivyo Mirza amekuwa mwanamke Mariyam - baadaye mja mzito - tena mwana wa Mungu - baba wa Mungu na hatimaye Mungu mwenyewe. Ni mtu wa kushangaza mno! Hawezi kueleweka.

Babi, Azali, Bahai

Kama vile huko Punjab, Mirza alifanya daawa ya Utume na Umahdi, huko Iran, kabla ya miaka 100, yalizuka Madhehebu mapya ya Babi, AzaliError: Reference source not found na BahaiError: Reference source not found. Wafuasi wa madhehebu hayo hadi leo wako Iran na India.

Katika kitabu kidogo kama hiki hayamkiniki kueleleza maisha ya Babi AzaliError: Reference source not found na BahaiError: Reference source not found na ubatilisho wa madai yao. Hata hivyo, tutaeleza kwa muhtasari historia ya madhehebu haya.

Mwanzilishi wa Ubabi alikuwa Mirza Ali Mohammed Mirza Raza Shirazi. Vichepuko vya madhehebu ya Babi vikawa madhehebu ya AzaliError: Reference source not found na BahaiError: Reference source not found yakimhesabu BaabError: Reference source not found kuwa Mtume na ishara ya habari njema kwa sababu alibashiria juu ya ndugu hao wawili.

Katika Mabahai, BaabError: Reference source not found hujulikana kuwa ni mtu mmoja tu aliyebaki hai kutokana na dhuria ya Mtume s.a.w.w na Mirza Husseinali ni Mtume Issa wa pili anayesubiriwa.

Baada ya kifo ya Mirza Mohammed BaabError: Reference source not found, wafuasi wake hawakutambua au kumkubali Mirza Yahya Subhe Azal au Mirza Husseinali kama walivyomkubali Baah. Mirza alidai kwamba Baab alitangaza kuja kwake (Mirza Yahya). Mirza Husseinali BahaiError: Reference source not found mwanzoni alimkubali ndugu yake na kueneza madhehebu yake kwa niaba ya nduguye lakini baadaye akageuka na kutangaza kuwa madhehebu ya nduguye ni udanganyifu na kubatilisha madai yake kuwa ni ya uongo kuanza kueneza madhehebu yake mwenyewe ya Ubahai.

Kutoka na mafarakano baina ya ndugu wawili hao, damu nyingi ilimwagika. Wafuasi wa Mirza Yahya wakajitambulisha kuwa Maazali na wa Mirza Husseinali kuwa Mabahai.

Siku hizi Wamisionari wa Kibahai wameenea kote katika mabara ya Asia ,Ulaya na Afrika. Vipi mtu anaweza kuwa na daawa ya kuteremshiwa Wahyi wakati yeye mwenyewe amebadilisha dini yake mara tatu ! kwanza alikuwa Shia Ithnaasheri, baadaye akaungana na madhehebu ya Ubabi na baadaye kuwa misionari wa madhehebu ya nduguye Mirza Yahya AzaliError: Reference source not found. Hatimaye akawa mwanzilishi wa madhehebu yake na kujitangazia kuwa yeye ni MahdiError: Reference source not found anayesubiriwa. Madhehebu yake ni mchapuo wa madhehebu ya Ubabi.

Al-Bayan husemekana ni kitabu alichoteremshiwa mwanzilishi wa madhehebu ya BaabError: Reference source not found. Maadili kadhaa kutoka kitabu hicho yanaorodheshwa hapa. Itadhihiri kwamba maadili yote ni kinyume cha maagizo ya Quran na Hadith.

1. Sala ya jamaa hukatazwa.

2. Baada ya raka 17 za kila siku mtu asali rakaa tisa tu na kuna mabadiliko mengi katika hizo sala.

3. Kufunga katika mwezi wa Ramadhan kumekatazwa na badala yake mtu afunge siku 19 tu kuanzia tarehe 1 Machi (Asrarul Akaid, uk. 830.

4. Kuoga tohara baada ya mtu kujamiiana na mwanamke au kutoka manii usingizini sio lazima.

5. Mwanamke yeyote, ila mama mzazi, huweza kufungwa naye ndoa.

Mwanzoni, mwanzilishi wa madhehebu ya Babi Mirza Mohammedali BaabError: Reference source not found alikuwa Shia Ithnaasheri. Alikuwa mwanazuoni wa kidini huko Najaf-Iraq. Baadaye alikwenda Iran na akaanza uombezi. Alikuwa akisimama kichwa wazi juani kwa muda mrefu. Mwishowe, akapotelewa na akili na kujitangazia kila daawa.

Katika 1844 A. D. Mirza Ali Muhamad akaanza kutangaza dini yake. Akatangaza yeye ni mlango wa Mungu (huwezi kumfikia Mungu bila kupitia kwake), Mti wa Toor, MahdiError: Reference source not found anayesubiriwa na mwishowe Mtume.

Katika majadiliano bayana na mwanazuoni wa Shia Ithnaasheri akatangaza “Kauli zangu ni bora na zenye ufasaha kuliko Quran. Madhehebu yangu hubatilisha Islam. Tahadharini mimi nitawaua wapinzani wangu wote”.

Aliwaamuru wafuasi wake kuongeza katika Adhana kauli ya kuwa: “Nitatoa ushahidi kwamba Ali Mohammed ni dalili ya Mungu na vile vile natoa shahada kwamba Ali Mohammed ni mlango wa Mungu”

Katika washabiki wakuu wa kueneza na kukubali madhehebu ya Babi alikuwa mwanamke mmoja, Kurratul Ayn, ambaye alikuwa binti wa mwanazuoni naye aliolewa na mwanazuoni. Alikuwa mwanamke mjanja, aliyeelimika na msemaji hodari. Jina lake la mwanzo lilikuwa Zarrin Taj na alikuwa mwanamke mwenye sura nzuri sana. Kutokana na mafarakano na mumewe akaungana na madhehebu ya Babi ili alipize kIssasi dhidi ya mumewe. Kila alipopata fursa alionyesha umbo na uzuri wake kwa kuvua buibui lake hadharani. Siku moja alipanda juu ya mimbar mbele ya watu wengi, akavua buibui na kutangaza: “Marafiki na maadui! Kutokeza kwa madhehebu ya Babi kumebatilisha Islam. Amri zote kuhusu sala, saumu, kutoa sadaka na kadhalika zimetenguliwa. Tahadharini. Hadhrat BaabError: Reference source not found akaiteka dunia nzima na karibu hakutakuwa na dini yoyote duniani ila Ubabi na kwa hivyo kila mtu anawajibika kuungana nasi kwa wingi kadri iwezekanavyo. “Achilieni mbali baibui ambalo lawatenganisheni na wanawake. Mkumbuke kuwa mwanamke ni ua linalonukia la bustani la dunia hii. Hivyo, lichume na kulistaladhi. Ua huzawadiwa kwa marafiki. Tamaa mbele giza nyuma. Msikose kuwapa marafiki zenu, wake zenu na maana vikwazo kama hivyo vimekwishaondolewa katika madhehebu ya Ubabi. Staladhi raha zote za dunia maana hakuna lolote baada ya kifo. ”

Mwenye akili hahitaji maelezo zaidi kuhusu imani ya madhehebu hayo.

Ubahai

Ubahai ulianzishwa 1853 B.K. na mwanzilishi wake Husseinali ambaye hujulikana kama Bahaullah, huko Mazinderan Iran baadaya kuacha madhehebu ya Ubabi. Watu wengi waliuawa.

Mwishowe kwa amri ya Shah wa Iran, Nasiruddin, Bahaullah akafungwa jela na kufia huko gerezani 1886. Alirithiwa na mwanawe Abbas Effendi ambaye alistakimu katika jiji la Akka huko Palestina.

Professa Browne aandika kwamba Ubahai ni muundo mpya wa Ubabi. Kama vile Mababi humtukuza Ali Mohammed (BaabError: Reference source not found) kuwa mtukufu mno vivyo hivyo Mabahai vile vile humfikiria Mirza Husseinali Bahauddin kuwa mtukufu mno.

Mabahai huamini kwamba Ali Mohammed BaabError: Reference source not found alibashiri tu juu ya kutokeza kikamilifu kwa amri ya Mungu na hilo likafuatwa na kuzaliwa kwa Bahauddin kwa sababu Mirza Hussein Ali alikuwa kiwiliwili cha Mungu. Hata Bahaullah mwenyewe alipokuwa gerezani alitangaza kwamba “hakuna Mungu ila mimi mwenyewe aliyefungwa na kukandamizwa”. Mtu atamfikilia nini huyo Mungu aliyefungwa gerezani na anayekandamizwa? Madhehebu hayo vipi huweza kuhesabiwa kuwa na uhusiano wowote na Islam ?

Kitabu cha kwanza cha Mabahai kilikuwa Aykan Baada ya kujitangazia kama yeye mwenyewe ndiye Mungu akachapisha kitabu cha pili kiitwacho Aqdas ambacho kinadaiwa kuwa ni bora kuliko vitabu vyote vya dini. Katika humo imearidhiwa: “Mama zenu tu hamwezi kulala nao na ustaarabu tu tunakataza kutoa kanuni kuhusu kumfeli (Mwanume kulala na) mtoto mwanamume mwenye sura ya kupendeza”. Hivyo, inamaanisha kwamba mtu anaruhusiwa kuingiliana na kila mwanamke ila mama yake mzazi na vile vile kufeliana na mwanamume mwenzie.

Uchochezi wa Babi-BahaiError: Reference source not found ulisababisha umwagaji mkubwa wa damu huko Iran. Wanazuoni, Mawaziri na mwishowe Shah wa Iran Nasirrudin Shah waliuawa. Idadi kubwa ya Mababi na Mabahai waliokuwa Iran na Mayahudi wa Hamadan, Kashan na Yazd waliokubali madhehebu hayo, na vile vile Maparisi wa Iran na India . Waislamu wachache mno walikubali madhehebu hayo.

Mmisionari Mkuu wa madhehebu ya BahaiError: Reference source not found, Mirza Hassan Niku, alikuwa mwanzilishi wa Abbas Effendi, mwana wa Bahaullah. Abbas ambaye alitunukiwa jina kuu la “Jibrael” na Mabahai. Jina lake la Kiislam lilikuwa Abdulhussein Ayni naye alikuwa mfuasi mkuu wa madhehebu hayo. Hao wote pamoja na wamisionari wakuu wa madhehebu hayo wakatubu na kuandika vitabu dhidi ya Ubahai na kufichua mabaya ya madhehebu hayo.

Avarah katika kitabu cha Kashful Hiyal amechapisha kibayana picha zinazofichua siri za madhehebu hayo. Kwa sababu tu kuimarisha upinzani dhidi ya Islam huko Iran ndiyo Mayahudi na Maparisi walijiunga na madhehebu hayo.

Mdai Umahdi katika karne ya 13 na 14, Mirza KadianiError: Reference source not found mwanzoni alikuwa mubalighi wa Kisunni. Pole pole, akaanza kudai Umahdi, Utume na mwishowe Uungu. Vile vile, Mirza Mohammed Ali BaabError: Reference source not found wa Ubaabi na Husseinali Bahaullah wa Ubahai mwanzoni walikuwa Mashia-kila mmoja akaanzisha madhehebu mapya na wakadai kuwa ni wawakilishi wa Baab, MahdiError: Reference source not found, Mtume na mwishowe Mungu.

Babu zake His Highness AgakhanError: Reference source not found walikuja India kutoka Iran wakiwa Shia Ithnaasheri na kuamini Maimam kumi na wawili, watukufu kumi na wanne na wakifuata sheria za kusali, kufunga Ramadhani na kanuni zote za madhehebu ya Shia. Siku za mwanzoni viongozi wa dini ya AgakhanError: Reference source not found walijulikana kwa jina la “Peer”. Jamatini watu wakiswali na kufunga Ramadhani. Quran ikisomwa na watu wakiamini Maimam kumi na wawili. Pole pole katika karne hii Maagakhani wakaanza daawa ya Umahdi, utume na hatimaye kiwiliwili cha Mungu. Mwanzoni, wafuasi wa Agakhan wakijulikana kwa jina la Bhagat na Mashia Ithnaasheri Subhanya. Baadaye Wa-AgakhanError: Reference source not found wakajigeuza kuwa Maismaili na kitambo kidogo wamekuwa wakijitambulisha kama Shia Imami Ismailia
Kwa upande mwingine, kwa mujibu wa itikadi ya Shia Ithnaasheri, tangu kuja kwa Islam, Imani katika Quran, Maimam kumi na wawili, kuzaliwa kwa Hadhrat MahdiError: Reference source not found(A.S. ), kughibu kwake na kutokeza mara ya pili kumethibitishwa kutokana na Quran, Hadith na historia. Dalili madhubuti za uhakika huo na ufununuzi wake umeelezwa kikamilifu katika kitabu hiki.

Waliodai Umahdi ulijitokeza mmoja baada ya mwingine,na kueleza nadharia zilizokuwa kinyume na tofauti na maadili ya Islam kama ilivyoelezwa katika Quran na Hadith. Hapana shaka wadai wote hao hawawezi kuwa wakweli kwa sababu ubashiri uliopo ni wa MahdiError: Reference source not found mmoja tu.

Hadithi maarufu ya Mtume Mtukufu s.a.w.w kwamba watakuwa Maimam kumi na wawili baada yake na mwisho ni Hadhrat MahdiError: Reference source not found (A.S. ) imenakiliwa na wanazuoni maarufu wa Kisunni katika vitabu vifuatavyo:-

1. Kanzul Ammal, Juzuu la 6, uk. 198

2. Sunan Abi Daud uk. 558

3. Jama-e-Tirmizi uk. 269

4. Sahih Muslim, Juzuu la pili, uk. 119

5. Sahihih Bukhari, Kitabul Fitan, Babul Istikhlaf, Juzuu la 29, uk. 629

Bila shaka Mume Mtukufu s.a.w.w alitangaza Hadith hiyo kuhusu Maimam kumi na wawili kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo, lazima wawe warithi 12 wa Mtume s.a.w.w Basi imani yoyote kuamini warithi zaidi ya kumi na wawili wa Mtume s.a.w.w haiwezi kuwa na ridhaa ya Allah swt na Mtume s.a.w.w

Ifuatayo ni orodha ya madai ya warithi wa Mtume s.a.w.w :

1. Msururu wa kwanza ni wa Khulafa-ul-Rashiden ambao walikuwa wanne tu na sio kumi na wawili.

2. Msururu wa pili wa daawa ya urithi ni kutoka nasaba ya Bani Umayyah ambao walikuwa kumi na wanne.

3. Msururu wa tatu ulikuwa wa Bani Abbasi ambao walikuwa 37 (thelathini na saba).

4. Msururu wa nne ulikuwa mchanganyiko wa watu wa Misri na Bani Abbas ambao walikuwa kumi na wanane. Halaku Khan alikomesha ukhalifa wa Bani Abbas huko Baghdad, na mfalme wa Misri alimtawaza mwana wa mfalme wa Bani Abbas kuwa Khalifa na kufanya idadi yao iwe kumi na wanane.

5. Msururu wa tano unatokana na Makhalifa wa Kituruki. Khalifa wa kwanza wa Kituruki Salim Sultan aliiteka Misri na kuanzisha ukhalifa wa Kituruki. Idadi ya Makhalifa hao ilikuwa thelathini, lakini alipokuja Mustafa kamal Pasha akakomesha ukhalifa huo; kwa hivyo, duniani sasa hayupo Khalifa wa Kusinni.

Madai ya Madhehebu Mengine

1. Madhehebu ya Bab AzaliError: Reference source not found bna BahaiError: Reference source not found, ambayo yamejitenga mbali na itikadi ya Islam, hayawezi kufikiriwa kwamba ni madhehebu ya Kiislam.

2. Vile vile U-Kadiani hupinga moja kwa moja imani ya Islam na kwa hivyo madhehebu hayo pia siyo ya Kiislam.

3. Hata hivyo waumini wa madhehebu ya Dawoodi Bohora ni Waislamu lakini huamini Maimam ishirini na mmoja na vile vile huamini hadi leo kuwa Imam wao wa mwisho, Imam Tayab amejificha hivyo, daawa yao huzidi idadi ya Imam kumi na wawili.

4. Waismailia, wafuasi wa AgakhanError: Reference source not found, huamini imam wao wa kipindi hiki ni wa 49; kwa hivyo idadi yao huzidi idadi iliyotajwa na Mtume s.a.w.w zaidi ya mara nne.

5. Ni Shia Ithnaasheri pekee yao tu ndio wanawaamini Maimamu kumi na wawili, kama ilivyosimuliwa na Hadith ya Mtume s.a.w.w . Imam wa kwanza ni Hadhrat Ali (A.S. ) na wa kumi na mbili Hadhrat MahdiError: Reference source not found (A.S. ) kama ilivyoridhiwa katika vitabu vitano mashuhuri vya madhehebu ya Kusunni na kutajwa katika vitabu vingi vingine . Jina maalum la kila Imam (A.S. ) lilitajwa na mwenyewe Mtume s.a.w.w . Ukweli huu vile vile umethibitishwa katika vitabu maarufu vya Kisunni, k. m.

i. Mawaddatul Qurba uk 34, kilichoandikwa na Allamah Seyyid Ali Hamdan, kilichochapishwa Bombay Press.

ii. Arjahul Matalib , uk. 402, Lahore Press.

iii. “Yanabiul Mawaddah”, uk. 445, kilichoandikwa na Allama Sheikh Suleiman Kanduzi, Sheikh wa Istanbul. Istambul Turkish Press.

iv. Tarikhul Rawzatul Ahbab, Yanabiul Muwaddah Juzuu 3, uk. 27. Licha ya hivyo, kuna vitabu vingi vimetaja majina halisi ya Imam MahdiError: Reference source not found a.s.

v. Babu zake AgakhanError: Reference source not found wa siku hizo wakiamini Maimamu Kumi na Wawili kama ilivyoelezwa katika vitabu vyao ambavyo tumekwishavitaja.

  • 1. Makala haya katika sura hii ya tatu yametolewa kutoka Imam Zaman Hadhrat Mahdi a.s. kilichoandikwa na Mulla Muhammadjaffer Sherif Dewji na kutarjumiwa na Alhaj Zakirhussein M. S. Lakha, kilichotolewa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, P. O. Box 20033 Dar Es Salaam, Toleo la kwanza 1991.