Na mwisho wa dua yetu ni kumshukuru Allah Bwana Mlezi wa walimwengu

Bila shaka kipindi cha ujana ndio fursa muhimu inayompa mwanadamu uwezo wa kutimiza vipaji na uwezo binafsi, kama ambavyo vijana ni haz- ina kubwa yenye thamani ndani ya jamii mbalimbali za wanadamu. Kuanzia hapa ndipo maendeleo yote ya nchi yoyote ile yakategemea jinsi vipaji vya vijana vitakavyotunzwa, na jinsi watakavyoelimishwa na vipaji vyao kukuzwa. Kwa ajili hiyo daima wanaharakati, viongozi wa kidini na wa kisiasa wametilia sana umuhimu wa harakati za vijana ndani ya zama zote za historia ya mwanadamu.

Kwa hakika kitabu hiki kinazungumzia maadili ya vijana kwa mtazamo wa Kiislamu. Kama tujuavyo Uislamu ni dini na mfumo wa maisha, kwa hiyo, haukuacha chochote kinachomhusu mwanadamu katika maisha yake ya hapa duniani na ya kesho Akhera.

Mwandishi wa kitabu hiki amejaribu kwa uwezo wake kuwakumbusha vijana juu ya wajibu wao katika jamii na kuwarejesha katika maadili mema. Na katika kuikamilisha kazi yake hii amerejea sana kwenye mafunzo ya Uislamu ambayo chimbuko lake ni Qur’ani na Sunna. Hivyo basi, huu ni mwongozo halisi kwa vijana unaolenga kuwaokoa katika harakati zao za maisha na hatimaye wawe ni wenye kufuzu kesho Akhera.

Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640 / 2127555
Barua Pepe: alitrah@raha.com
Tovuti: www.ibn-tv.org