Neno La Mchapishaji

Kijitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahihi kutoka Kiingereza.

Maandishi ya asili ya Kiingereza yaliandikwa na mwanachuoni wetu mashuhuri wa Kiislamu Sayyid Muhammad Rizvi.

Ni maelezo mafupi ya wasifu wa Mtukufu Mtume wa Mungu mwenye nguvu sana, Muhammad (s.a.w.), ambaye kuhusu yeye Qur’an Tukufu inasema:

“Bila shaka amekufikieni Mtume kutoka miongoni mwenu, yanamhuzunisha yanayokutabisheni, anakuhangaikieni, kwa waumini ni mpole, mwenye kurehemu.”(9:128)

“Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu.” (21:107)

Wakati ambapo jukumu la kuelezea haiba hii kubwa mno ingechukua mijalada mingi, tuna imani kwamba msomaji asiye na upendeleo kwa hakika atanufaika kutokana na toleo hili nyenyekevu.

Tarjuma yake ya Kiswahili inafanywa ipatikane kwa ajili ya faida ya ndugu zetu wazungumzaji wa Kiswahili katika Afriuka ya Mashariki na pengine popote.

Tunawashukuru wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wamechangia katika utoaji wa tarjuma hii ya Kiswahili ambayo inawasilishwa hapa.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es- Salaam, Tanzania.