read

1. Khutba Ya Kwanza

Ameieleza khutba hii Al’Waasiti ndani ya Kitabu chake (Uyunul’Mawaaidhi wal’Hikami), na Az-Zamakhshari ndani ya (Rabiiul’Abrari) mlango wa mbingu na nyota. Na Ibun Shu’uba Al’Halabi ndani ya (Tuhaful’Uquli), na Al’Qaadhi Al’Qadhaa-i ndani ya (Dusturu maalimil’Hikamis), na Ibnu Tal’ha Ash Shaafi’i ndani ya (Matalibus Su’ul) na Al’Fakh’rur Raazi ndani ya juzu ya pili ya Tafsyri yake.

Ndani ya khutba hii anaelezea kuumbwa kwa ardhi, mbingu, na kuumbwa kwa Adam (a.s)

Anayestahiki sifa njema ni Allah (s.w.t) ambaye ubora wa sifa zake hawa ufikii wasemaji. Ambaye neema zake wahasibu hawawezi kuzihisabu. Wenye juhudi hawawezi kutekeleza haki ya utii wake.

Ambaye fahamu ya hali ya juu ya wenye akili haiwezi kumfikia kumtambua,1 wala, utambuzi wa kina hauwezi kumuelewa 2 ambaye sifa zake hazina mpaka wenye kikomo,3 wala hana sifa.
Wala wakati uhisabiwao, wala muda uliowekwa.4 Ameumba viumbe kwa uwezo wake, na ameutawanya upepo kwa rehema zake; kwa milima ameimarisha uyumbaji wa ardhi yake.

La kwanza katika dini ni kumtambua yeye,5 na ukamilifu wa kumtambua ni kumsadiki, na ukamilifu wa kumsadiki ni kumpwekesha.6

Na ukamilifu wa kumpwekesha ni kumtakasa na ukamilifu wa kumtakasa ni kumuepusha mbali na sifa. Na mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu swt. Atakuwa amemuambatanisha,7 na mwenye kumuambatanisha amemfanya kuwa wawili,8 na mwenye kumfanya kuwa wawili atakuwa amemfanya kuwa mwenye sehemu sehemu, na mwenye kumfanya kuwa mwenye sehemu sehemu atakuwa hamjui (s.w.t.), na asiyemjua atakuwa amemuonyesha, na mwenye kumuonyesha atakuwa amemwekea mipaka,9 na mwenye kumuwekea mipaka atakuwa amemuhisabu.10 Na mwenye kusema yuko ndani ya nini? Anakuwa amemwingiza (s.w.t) ndani ya kitu.11

Na mwenye kusema yuko juu ya nini? Atakuwa amemtoa humo.12 Amekuwa yupo sio kwa kutukia, yupo lakini sio kwa maana ya hakuwapo hapo kabla. Yuko pamoja na kila kitu si kwa mwambatano wa kimwili.13 Yutafauti na kila kitu si utafauti wa kimwili, mtendaji sio kwa maana ya harakati za kimwili na vyombo, mwenye kuona pindi hakuna wakuonwa kati ya viumbe wake. Yu pweke pindi hakuna mkazi analiwazika naye wala haoni ukiwa kwa kukosekana kwake.

A. Kuumbwa Kwa Ulimwengu.

Alianza kuumba viumbe mwanzo, na kuvibuni kwa ubunifu, bila ya kupitisha fikra, wala kufaidika na uzoefu wowote, wala hakufanya harakati yeyote, wala kusumbuliwa na azma ya ndani ya nafsi, amevitoa viumbe (kutoka hakuna kitu na kuviingiza) kwenye ulimwengu wa kuwepo kwa wakati wake.
Akaviunganisha viumbe pamoja na tofauti zao. Akaweka silika zao, na akaziambatanisha hizo silika na wenyewe. Akiwa mjuzi (s.w.t) kabla hajabuni (viumbe) akiwa mwenye kuelewa kwa ukamilifu, mipaka yao na mwisho wao, akiwa mwenye kutambua utashi wao na sehemu zao nyingi.

Kisha aliumba (s.w.t.) mwanya wa anga na eneo la mbingu na utando wa upepo, alimimina humo maji ambayo mawimbi yake yalikuwa makali na mawimbi yalilundikana moja juu ya jingine, aliyabebesha kwenye upepo uendao kwa kasi, na mtikisiko mkali, na kimbunga kinachovunja. Aliyaamrisha yamwage (mvua) aliufanya upepo uwe na uwezo wa kuzuia nguvu za mvua na kuijulisha mipaka yake. Upepo ulivuma chini hali maji yalibubujika kwa kasi kwa upande wa juu.

Kisha (s.w.t.) aliumba upepo ambao ulifanya mvumo wake uwe tasa. Yaani mvumo wa hewa ulifanywa usioweza kurutubisha kizazi, kwa kuwa kuna upepo urutubishao mimea na kuifanya itoe mazao. Na upepo huu uli- umbwa ili kuyatikisa maji tu. Na akadumisha kubaki kwake, mwendo wake ulishika kasi na akayatawanya kwa umbali na kwa upana.

Kisha aliuamrisha upepo kuyanyanyua maji yalio kwenye kina, na kuongeza kasi ya mawimbi ya bahari. Yakatikisa mtikiso kama ule ufanywao kwa kinywaji cha maziwa. Na kuvuma nayo angani. (Anakusudia kueleza kuwa upepo ukivuma angani anga ambazo ziko tupu huwa mvumo wake mkali kwa sababu ya kutozuilika na kitu chochote, na upepo huu ulivuma na maji mengi mvumo mkali sana).

Wayarudisha ya mwanzo nyuma na yaliyotulia kuyapeleka kwa yaliyo kwenye mtikisiko, mpaka yakainuka mwinuko. Na sehemu ya chini ilijaa povu. Baadaye Mungu (s.w.t.) aliinua povu lile juu ya upepo ulio wazi kutoka humo aliumba mbingu Saba. Na sehemu ya mawimbi ya chini aliyazuia na kuwa kituo, na ya juu kuwa kama dari inayo zuia na jumba lililoinuka bila ya nguzo zenye kulikinga, wala misumari inayo imarisha, kisha alizipamba (mbingu) kwa mapambo ya nyota na mianga yenye nuru. Na alipitisha humo jua lenye taa yenye kuenea mwanga wake. Na mwezi wenye nuru katika sayari zinazozunguka. Na dari inayokwenda, na ubao uendao.14

B. Kuumba Malaika.

Kisha aliumba mwanya kati ya mbingu za juu na kuzijaza malaika wake wenye daraja tofauti.15

Malaika amewafanya wa aina tatu:

a. Mabingwa wa ibada, miongoni mwao kuna ambao wamesujudu na wala hawarukuu, na kuna waliorukuu na wala hawasimami, kuna waliosimama katika safu na wala hawatawanyiki kuna wanaosabihi na wala hawachoki, hawasinzii, wala hapitiwi, wala hawanyong’onyei, wala kughafilika kwa kusahau.

b. Miongoni mwao kuna waaminifu wa wahyi wa Mungu, na ni ndimi zitamkazo ndani ya vinywa vya mitume Wake, na wanaopokezana kwa hukumu na amri zake (kupitia wao Mungu hupitisha hukumu kwa amtakae kwa apendacho).

c. Malaika wahifadhi wa waja Wake (swt), kana kwamba wao ni nguvu iliyowekwa ndani ya miili ya wanadamu na nafsini mwao. Na miongoni mwao wamo ambao miguu yao imeimarika katika ardhi ya chini, na shingo zao zimechomoza kwenye mbingu ya juu, na nguzo zao zimezidi kwenye peo (horizon), na mabega yamelingana na nguzo za Arshi, wenye kuinamisha macho yao mbali na Arshi, wenye kuizingira kwa mbawa zao, imepigwa pazia ya utukufu kati yao na wasiokuwa wao na stara ya uwezo, hawamfanyii taswira Mola wao, wala hawampitishii sifa za viumbe, wala hawamuwekei mipaka ya mahali, wala hawamuashirii kwa mifano.

C. Maelezo Ya Kuumbwa Kwa Adam (A.S.)

Kisha (s.w.t.) alikusanya aina za udongo: Ngumu, laini, tamu, chachu, udongo ambao aliumwagia maji mpaka ukalowana, na aliukanda kwa unyevunyevu mpaka ukaganda, kutoka humo aliumba sura yenye pande tofauti, na viungo tanzu, sehemu ya pingili aliigandisha na ikashikamana, akaifanya kuwa ngumu mpaka ikawa ngumu, kiasi cha kusikika sauti, kwa wakati uliowekwa kwa muda ujulikanao.

Baadaye alipulizia humo roho, akawa mtu mwenye akili imsukumayo, na fikra aitumikishayo, na viungo vya mwili avitumiavyo, na ala zimsaidiazo kubadilisha hali yake, na maarifa ambayo kwayo anatofautisha kati ya haki na batili, akiwa na uwezo wa kuonja, na kunusa, kupambanua rangi, na jinsi yenye mchanganyiko wa udongo wa rangi tofauti, na vitu vyenye kufanana na kuafikiana, vitu vilivyo kinyume na visivyoafikiana. Aina tofauti za mchanganyiko: kama vile joto, baridi, hali ya chepe, ugumu, chuki, furaha.

Mungu (s.w.t.) aliwataka malaika watekeleze ahadi aliyowekeana nao, na kutimiza agizo lake la kuwataka wamsujudie Adamu, na kunyenyekea ili kumpa heshima, akasema (s.w.t): “Msujudiyeni Adamu, walisujudu isipokuwa iblisi”. Quran 2:34. Yeye alijiona, akazidiwa na uovu, akajitukuza na kufanya kibri kwa sababu ya kuumbwa kutokana na moto. Alikebehi asili ya umbo la Adamu, yaani udongo.

Mungu (s.w.t.) alimpa (Ibilisi) muda ili ghadhabu ithibiti kwake. Na kukamilisha mtihani ( kwa mwanadamu) na kutekeleza ahadi, akasema: “Basi kwa hakika umekwisha kuwa mingoni mwa waliopewa muhula mpaka ya siku ya wakati maalum” (15:38, 38:81)

Baadaye Mungu (s.w.t.) alimuweka Adamu peponi ambapo aliyafanya maisha yake yakuridhisha, na kubaki kwa amani. Alimtahadharisha na Ibilisi na uadui wake. Adui yake (ambae ni Ibilisi) alimghuri. Akimwonea wivu kubaki kwake milele Peponi akiwa na watendao mema. Akauza yakini kwa shaka yake, na azma kwa unyonge wake, na furaha aliibadilisha kwa woga. Na kuhadaika ikawa ni majuto.

Kisha Mungu s.w.t. alimpa Adamu fursa ya kutubia. Alimfundisha neno la rehema Zake. Na alimuahidi kumrudisha kwenye Pepo yake. Alimteremsha duniani kwenye makazi ya mtihani, nyumba ya majaribu, na kuzaa watoto.

D. Kuteuliwa Kwa Manabii

Mungu (s.w.t.) aliwateua manabii katika kizazi chake - watoto wa Adamu (a.s) - akachukuwa kwao ahadi kwa ajili ya wahyi, na kuchukuwa dhamana kwao kwa ajili ya kuifikisha risala - Ujumbe - lakini wengi katika viumbe Wake walivyobadili ahadi ya Mungu walipotosha agizo lake (s.w.t.) kwao wakapuuza haki yake wakamfanyia washirika pamoja naye. Shetani aliwapotosha mbali na kumtambua Yeye. Na aliwaweka mbali na ibada yake.

Aliwatuma kwao Mitume wake, aliwapeleka manabii wake kwao kwa vipindi: Ili watekeleze ahadi ya kuumba kwao, na wakumbushe neema zake zilizosahauliwa, na ili watoe hoja kwao kwa kufikisha ujumbe. Ili kuamsha vipaji vya hikima vilivyofichikana. Na kuwaonesha alama za uwezo wake wa kila kitu kama vile mbingu zilizoinuliwa na ardhi iliotandikwa chini yao, na sababu za maisha zinazowapa uhai, na ajali zinazowamaliza, na taabu zinazowazeesha na matukio yanayofululiza kwao.

Mungu (s.w.t.) hakuwaacha viumbe wake bila ya nabii mwenye kutumwa, au bila ya Kitabu kilichoteremshwa, au bila ya hoja ya lazima, au bila ya njia iliyonyooka.
Hawa wajumbe, hawakujihisi kuwa wachache kwa udogo wa idadi yao wala kwa ukubwa wa idadi ya wanaowakadhibisha. Miongoni mwao aliyetangulia humtaja anayefuata baada yake au mfuasi aliyetambulishwa na mtangulizi wake.

Kwa utaratibu huo karne baada ya karne zilipita, vilizaliwa vizazi. Miaka ikapita, mababa walipita na watoto walichukua nafasi.

E. Kutumwa Kwa Muhammad (S.A.W.W.)

Hali iliendelea hivyo mpaka Allah (s.w.t) alipomtuma Muhammad (s.a.w.w.), mjumbe Wake ili kutimiza idadi Yake, na kukamilisha unabii Wake. Akiwa mwenye kuchukua ahadi Yake kutoka kwa manabii, alama zake (s.a.w.w.) zilikuwa mashuhuri, uzao wake ni wa heshima.

Watu wa dunia hii wakati huo walikuwa kwenye itikadi zinazotofautiana, tamaa za nafsi zimeenea, na njia zikiwa tofauti, wakiwemo waliomshabihisha Mungu (s.w.t.) na viumbe Wake au wenye kupotosha jina lake (s.w.t.) au wenye kumshirikisha na viumbe.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwaongoza kupitia kwake kutokana na upotovu, na kwa nafasi yake (s.a.w.w.) aliwaokoa mbali na ujahili.

Kisha Mungu (s.w.t) alimhitari Muhamamd (s.a.w.w.) kukutana naye na alimridhia ili awe karibu Yake (s.w.t), na alimzidishia heshima kwa kumwondoa duniani mahali pa majaribu, kwa hiyo alimchukuwa Kwake kwa heshima (s.a.w.w).

Na aliacha kwenu ambayo manabii waliacha katika Umma zao.16 Kwani hawakuwaacha wamepuuzwa, bila ya kuwaeleza njia iliyowazi, wala watakayoongoka kwayo.

D. Kitabu Cha Mwenyezi Mungu Na Sunnah

Amekuachieni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mola wenu: kibainishacho halali yake na haramu yake.17 Faradhi zake na fadhila zake. Batilisho (nasikh) zake na zilizobatilishwa (mansukh) zake, ruhusa zake na azma zake, hukumu ambazo ni makhsusi, na ambazo zipo katika sura ya jumla, na ambazo zina mafunzo ndani yake na mithali, ndefu na fupi, thabiti zake na mutashabih zake: zilizo wazi na ambazo ni ngumu kueleweka maana yake, zenye kufasiri aya zilizokuja kwa maana ya jumla, na zenye kubainisha maana zake ngumu. Humo kuna aya ambazo kuzijua ni lazima, na kuna ambazo watu wanaruhusiwa kutozijua.

Na ambazo imethibiti Kitabuni faradhi yake, na zajulikana kutenguliwa katika sunnah, na ambazo ni wajibu katika sunnah kuzitekeleza, na ambazo katika kitabu zaruhusiwa kuziacha.

Na kuna ambazo ni wajibu kwa wakati wake, na wenye kuondoka wakati ujao, uharamu wake pia watofautiana, kuna ambazo ni kubwa ametishia kwa (kosa hilo) moto wake, au ndogo zenye ghofrani yake, na kati ya yanayokubalika uchache wake na yenye wasaa katika umbali wake.

Kuna ambazo uchache wake wakubaliwa (kwa Mungu) na zenye uwezekano wa kutanuliwa (hukumu yake)18

E. Ndani Ya Khutba Hii Aelezea Hijja

Na amewajibisha juu yenu kuhiji nyumba yake tukufu, ambayo ameifanya Qibla kwa wanadamu, wanaiendea kama wanyama walazimikapo kuyaendea manyweo ya maji wanayahamanikia uhamanikaji wa njiwa.

Mungu (s.w.t.) ameifanya (Kaaba) iwe ndio alama ya unyenyekevu wao kuunyenyekea utukufu Wake, na utii wao kwa enzi Yake. Amechagua kutoka kwa viumbe Wake watiifu walioitikia wito wake. Na wamesadikisha neno Lake. Na wakasimama msimamo wa manabii Wake. Wakashabihiana na malaika wake wazungukao Arshi Yake. Wanafaidika na biashara ya ibada yake. Wakiharakia kwenye ahadi ya msamaha Wake. Mungu (s.w.t.) ameifanya (nyumba hii) kuwa ni alama ya Uislamu na ni lengo la heshima kwa wanaojikinga nayo.

Amefaradhisha haki yake, na kulazimisha kuihiji. Na amefanya faradhi juu yenu kuiendea aliposema (s.w.t.): “Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awazae njia ya kwendea. Na atakayekanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. (3:97)

 • 1. Anakusudia hima ya wenye uoni na wanafikra japo iwe ya hali ya juu haiwezi kumdiriki yaani kumtambua (swt) kama kitambuliwavyo kiumbe, wala kumzunguka.
 • 2. ni wingi wa yaani kutambua kuzama mbizi, na hapa maana inakuwa: kuzama mbizi ndani ya bahari ya mambo yazingatiwayo kiakili ili kudondoa lulu za ukweli wa mambo, nazo japo ziende mbali katika mbizi haziwezi kuipata hakika ya dhati yake (swt).
 • 3. Ambaye sifa zake hazina mpaka ujulikanao: yaani sifa hapa yakusudiwa dhati yake na hakika yake (s.w.t.) na jinsi alivyo yaani dhati yake (swt) haina mpaka uwezao kutambuliwa. Amemaliza maneno kuihusu dhati yake (swt) na kuzuilika kwa akili ya mwanadamu kuidiriki, baada ya hapo anazitakasa sifa zake (swt) kuwa hazifanani na sifa za vizushi yaani viumbe vilivyo zuka (hapo kabla havikuwa na baada ya kuumbwa vikawa ndio maana ya kuzuka hapa) kwa hiyo kila sifa za kiumbe kwa kawaida kiumbe huwa na sifa ya (imkaanu) kwa maana ya kuwa kwa kiumbe si wajibu bali ni mumkinul wujudu (kupo ndani ya uwezekano) na Mungu ni wajibul'wujud. Hivyo basi kila sifa za kizushi ina kikomo kama tunavyojiona ndani ya uwezo wetu, ilimu yetu kwa mfano. Kwa kuwa kila moja ina kikomo haiwezi kukivuka, lakini uwezo wa Mungu, ilimu yake haina mpaka kwa uene- vu wake. Hivyo hivyo husemwa kukhusu sifa nyingine za ukamilifu. Na (naat) huwa sifa zinazokubali kubadilika, na sifa zetu zina (naat). Kama vile uhai wetu kwa mfano una daraja kutokea daraja ya mtoto mchanga mtoto wa makamo na daraja baada ya hapo, kama vile wakati wa nguvu, udhaifu, na hali ya wastani, na uwezo wetu pia ni kama hivyo. Na ilimu yetu ina duru ya upungufu na ukamilifu, hali ya undani, na ya uwazi. Lakini sifa zake (swt) zimetakasika mbali na (nautu) kama hizi na -mfano wake, kisha hizi sifa zake (swt) ni azaliza milele hazina hisabu ya wakati wa kuwa kwake na yeye kusifika kwa dhati yake nazo, wala haziwekewi muda.
 • 4. . Wala muda uliowekwa, ni ishara ya kanusho kwa wanaodai kuwa Mungu (s.w.t.) atajuli kana alivyo atakapoonekana siku ya Kiyama kwa hiyo asema (a.s): Hapana wakati kamwe Mungu atakuwa ajulikana dhati yake.
 • 5. Mwanzo wa dini ni kumtambua Mungu (swt): kwa sababu taq'liid ni batili, la kwanza katika wajibu za kidini ni kutambua. Msingi wa dini ni kumtambua Mungu, na Yeye anaweza kutambuliwa kuwa muumba wa ulimwengu, bila ya kumtakasa, kwa hiyo huo ni utambuzi pungufu, na ukamilifu wake ni kumsadiki dhati Yake kwa sifa makhsusi ambazo yeyote hashirikiani Naye, nayo ni sifa ya wajibu wa kuwepo kwake (wajibul'wu-jud). Na kusadiki huku hakukamiliki mpaka kuwe na lazima yake, nayo ni Tawheed kwa kuwa ambaye kuwepo kwake ni wajibu hana idadi, kama ijulikanavyo katika fani ya Ilahiya na ilmul’kalam (scholasticism). Na Tawheed haikamiliki ila kwa kumtakasia siri kuwa ni yake bila ya kumuambatanisha na kitu chochote miongoni mwa mambo ya matukio katika kumuelekea na kutarajia mwanga wa nuru Yake. Utakaso huu hauwi kamili mpaka uwe pamoja na kumuepushia sifa za dhahiri katika ainisho zionekanazo katika vitu. Kwa sababu kuitambua dhati iliyo takasika ndani ya sifa hizo ni kuizingatia dhati na kitu kingine mbali nayo. Kwa hiyo ametambuliwa (Allah) mwenye viungo na siye Aliye kamili bila ya viungo. Kwa hivyo inakuwa sifa zinazo kanushwa na kutoambatanishwa Naye (swt) ni sifa za viumbe, vinginevyo maneno ya Imamu yamejaa sifa Zake swt. Bali katika maelezo haya amsifu kwa sifa kamilifu mno.
 • 6. Ukamilifu wa kumsadiki ni kumpwekesha: Kwa sababu kujua kuwa Yeye kuwepo kwake ni wajibu peke yake ni kusadiki kupungufu, na kusadiki kamili ni kujua Upweke Wake swt.
 • 7. Na mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu atakuwa amemuambatanisha: Kwa sababu mwenye kusifiwa huambatana na sifa, na sifa inamuambata yeye.
 • 8. Na mwenye kumuambatanisha amemfanya wawili kwa hakika, kwa kuwa ame- wathibitisha wa zamani wawilina kufanya hivyo ni kuwafanya wa milele wawili.
 • 9. Kwa kuwa kila chenye kuoneshwa ni chenye mipaka, kwa kuwa wakionyesha kitu kikiwa kipo upande mwingine mbali na ule uliokuwapo, kwa hiyo wewe wakielekea kwa ishara yako. Na ambaye yuko upande fulani anakuwa amejitenga na mwingine, na anakuwa ndani ya mipaka maalumu, yaani kuna ncha anayoishia. Hivyo basi mwenye kumwonesha amemuwekea mipaka.
 • 10. Na mwenye kumwekea mipaka atakuwa amamhesabu: Yaani, amemfanya miongoni mwa vitu vinavyotukia.
 • 11. Kwa sababu mwenye kufanya tasuwira kuwa yupo ndani ya kitu atakuwa amemfanya kuwa ni mwili uliojificha mahali, au kitu miongoni mwa vitu visivyo kuwa mwili, (incorporeal)
 • 12. Na mwenye kusema: Yupo juu ya nini? Atakuwa amemtoa nje yake: Kwa sababu mwenye kufanya taswira kwamba Mungu (swt) yuko juu ya Arshi au yuko juu ya Kursiy amemfanya hayupo katika sehemu zisizokuwa hizo.
 • 13. Yuko pamoja na kila kitu, si kwa mwambatano: Yaani anajuwa vitu sehemu sehemu zake kama avijuavyo katika hali ya ukamilifu wake, kama alivyosema (swt): yaani hawawi katika siri watu watatu ile Yeye ni wanne wao. (Suratul-Mujadillah:7).
 • 14. Sayari zimeitwa ubao kwa kuzifananisha na ubao kwa sababu zipo katika umbo la ubapa.
 • 15. Malaika wabeba Arshi, wao ni kama nguvu ya jumla ambayo Mungu ameikabidhi kwa ulimwengu wote, hiyo ni nguvu inayoushika ulimwengu, na ya uhifadhi sehemu zake zote na makao makuu yake na mipaka ya mwendo wake ni katika mzunguko wake, kwa hiyo nguvu hiyo yapenya na yenye kuingia humo, yenye kuchukuwa kutokea juu yake mpaka chini yake, na kutoka chini yake mpaka juu yake. Na kauli yake: Al’maariqatu minas samaai, al’muruqu: Al’khuruju - kutoka - Na kauli yake: Al’khaarijatu minal’aq’tari arkanuhum: Arkaanu ni viungo vya miili yao, na maneno hayo ni aina ya mfano ulio wazi kwa waelewao.
 • 16. Anakusudia kubainisha kuwa manabii wa Mungu (s.w.t.) hawakuwaacha watu wao bila ya kitakacho waongoza baada ya umauti wao. Kwa hiyo hivyo hivyo ilikuwa kwa Muhammad (s.a.w.w.) yeye aliuachia Umma wake Kitabu cha Mungu (s.w.t.) kikiwa na kila wahitajialo katika dini yao.
 • 17. Halali yake: kama kula vitu vizuri yaani vya halali, na haramu kama kula mali ya watu wengine kwa njia ya batili. Na faradhi zake: Kama zaka dada wa sala. Na fadhila zake: kama vile sunna zake za sadaka ambazo ujira huwa mkubwa kwa kuzitekeleza, wala si vibaya akizembea mwenye kuzembea, na naasikh zake: zilizokuja kutoa hukumu zaondoa waliokuwanayo wapotovu miongoni mwa itikadi, au kuondoa hukumu zilizokuwa hapo kabla, mfano wa kauli yake (swt):
  na mansukhah: Iliyokuwa maelezo ya hukumu hizo, mfano wa kauli yake
  na aliyoruhusu: mfano wa kauli yake
  na ambazo ni lazima: mfano wa kauli yake
  na khaaswa mfano wa kauli yake
  na aamah: mfano wa kauli yake: Na mafunzo kama aya ambazo zinatoa habari za umma zilizopita miongoni mwa adhabu: “Tumewateremshia adhabu kwa sababu ya kupinga haki na wakafanya dhulma na uadui”. Na mifano: Kama kauli yake: “Mwenyezi Mungu ametoa mfano wa mja mmilikiwa” (16:75). na “Mfano wa ambaye amekoka moto ......” (2: 17). Na vinavyoshabihiana na hayo mengi.
 • 18. Kurejea kwenye mgawanyiko wa hukumu Kitabuni, al-maq'bulu fii adnaahu al'- muwassau fii aqswaahu,: mfano wa kafara ya kiapo Hukubaliwa uchache wake kuwalisha masikini kumi, na ina wasaa katika kuwavika na kumuacha mtumwa huru.