read

3. Katika Jumla Ya Khutba Zake Alayhis-Salaam:

Nayo ni ile maarufu kuwa ni khutba ya Shaqshaqiyah.1 “Amma! Wallahi fulani, ameuvaa (Ukhalifa)2 hali akiwa yuajuwa kuwa nafasi yangu kuhu- siana nao ni sawa na mahala pa muhimili wa jiwe la kusagia, maji ya mafuriko huniporomokea wala ndege hawezi kunirukia.

Nilijikinga nao kwa nguo na nikajiweka kando nao. Nikajifikiria, je! Nishambulie na mkono butu, au nilivumilie giza la upofu,3 mtu mkubwa humo huzeeka, na mdogo humo huwa kijana, muumini anataabika humo mpaka akutane na Mola wake, nikaona kuivumilia hali hii ni busara, basi nikasubiri hali jichoni mwangu muna utongotongo, na kooni kuna kitu kilichokwama.

Naiona mirathi yangu imepokonywa,4 wa kwanza akapita katika njia yake, - yaani alikufa - akampasia (ukhalifa) fulani baada yake. Alinakili ubeti wa kauli ya Al-A’asha - maana yake: kuna tofauti kubwa kati ya siku yangu nikiwa juu ya ngamia na siku ya Hayyani nduguye Jabir: (yaanni siku ya Hayyani ilikuwa ya raha).

Ajabu ilioje! Alikuwa anaomba wamuuzulu wakati wa uhai wake, punde si punde akaagiza uende kwa mwingine baada ya kifo chake!

Kwa hakika wameshirikiana viwele vyake viwili wao kwa wao tu, huyu mmoja ameuweka (ukhalifa) katika upande ulio mgumu, mguso wake wakwaruza, kujikwaa kunakithiri na kuomba udhuru, aliyekuwa nao ni kama aliyepanda ngamia machachari asiyepandika: akimvuta hatamu atamkaba na akimlegezea atamtupa kweye maangamizi, hapo wallahi watu watapatwa na myumbo, uovu na kupotoka, Nilivumilia kwa muda mrefu wote huo, ingawaje ulikuwa mtihani mgumu: Na alipofikia muda wake akauweka chini ya uchaguzi wa kundi la watu sita akadai akinidhania mimi ni mmoja kati yao. Eee Mungu! Nahusika nini mimi na Shuura!5

Lini ameingiwa na shaka na mimi wa kwanza katika wao kiasi niwe naambatanishwa na mfano wa hawa! Lakini nilitua walipotua, na niliruka waliporuka, mtu miongoni mwao alinigeuka kwa sababu ya kunichukia kwake,6 na mwingine alielemea upande wa shemeji yake.7

Pakiwa na hili na lile, mpaka akasimama watatu wao hali ameinua kifua chake mbele kati ya kinyesi chake na chakula chake - chakula cha mifugo - walisimama pamoja naye watoto wa babu yake, wakawa wanazitafuna mali za Mungu kama anavyotafuna ngamia majani ya msimu wa kuchipua (spring season), mpaka kamba yake ikakatika, na matendo yake yakammaliza, na ulafi wake ukamtupa chini kifudifudi.

Nilishitushwa na kundi la watu likimiminika kuja kwangu mfano wa manyoya ya shingoni mwa fisi toka kila upande, kiasi kwamba Hasan na Husayn walikanyagwa, na sehemu za ncha za mabega ya vazi langu zikararuriwa, wakiwa wamejikusanya kunizunguka kama kundi la kondoo na mbuzi.

Nilipochukua hatamu za uongozi, kundi moja lilivunja ahadi na jingine liliasi, na lililobaki lilifanya uovu na dhulma8 kana kwamba hawakusikia neno la Mungu aliposema: “Hayo ndiyo makazi ya akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujitukuza duniani wala ufisadi, na mwisho mwema ni wa wachamungu.” (28:83).

Ndio wallahi waliyasikia na waliyaelewa lakini machoni mwao dunia ilijipamba na kuliwapendeza kujiremba kwake. Angalia! naapa kwa yule ambaye ameatua mbegu na kumuumba binadamu, lau si kufika kwa watu na kulazimu hoja kwa kuwepo wasaidizi - yaani askari wa kumnusuru - na ahadi iliyochukuliwa na Mungu kwa wanachuoni, kuwa wasiridhike kimya kimya na ulafi wa madhalimu na kusagwa kwa haki ya mdhulumiwa, ningeitupa kamba ya ukhalifa kwenye bega lake - yaani ninge tupilia mbali suala la ukhalifa bila kujali - na ningemtendea wa mwisho kama wa kwanza. Na mungeona kwa maoni yangu huu ulimwengu wenu si bora kuliko chafya ya mbuzi”.

Walisema kuwa: Amirul-Mu’minina alipofikia hapa katika KHUTBA hii, mtu mmoja katika watu wa Iraqi alisimama na kumkabidhi karatasi yenye maandishi, akawa anaiangalia, alipomaliza kuisoma, ibn Abbas alimwambia: Ewe Amirul-Mu’minina ungeendelea na KHUTBA yako ulipoachia!

Hivyo basi alijibu: “Ewe ibn Abbas hilo ni povu la ngamia, ameunguruma kisha akanyamaza”.

Ibn Abbas akasema: “Wallahi sikuwahi kuhuzunikia maneno kamwe, kama huzuni yangu juu ya maneno haya kwamba awe Amirul-Mu’minin hakufikia alipotaka”.

Amesema Sharifu (r.a), kauli yake (a.s): “Ni kama mfano wa aliyepanda ngamia mkorofi”: Anakusudia kuwa, ikiwa atakaza kuvuta hatamu hali akimkinza kichwa chake atararua pua yake, na endapo atamlegezea kitu kidogo na ugumu wake atamuendesha mbio ovyo, na wala hatomdhibiti, husemwa: Ashnaka naakata akikivuta kichwa chake kwa hatamu na kukiinua, na Washanakahaa aidhwan, pia hutumika kwa maana hiyo, hilo limesemwa na ibn Sakiit katika kitabu Islahu al-Mantiq. Na sababu ya kusema (a.s) (Ashanaka laha) na wala hakusema Ashnaakaha kwa kuwa amelijaalia liwe mkabala wa kauli yake: (Aslasalaha) hivyo inakuwa kama kwamba amesema: In raf ’a laha rasaha bizimami: yaani ameishika.
Na katika hadithi imekuja kuwa Mtume wa Mungu (s.a.w.w) alihutubia akiwa juu ya ngamia aliyemvuta hatamu kwa kuinua kichwa chake. Na miongo- ni mwa ushahidi kuwa (ashnaka) maana yake (Shaanaka) ni kauli ya Adiyyu bin Zayd al-Abadiyy: Sa’a aha maa tabaiyyana fil aidi wa ish- nakuhaa ilal-a’anaaqi.

 • 1. Kwa ajili ya kauli yake: (hiyo ni Shaqshaqa hadarat thumma karrat) kama inavyokuja.
 • 2. Fulani ni kinaya ya khalifa wa Kwanza Abu Bakr, (na katika nakala ya Ibn Abi-Hadid: Hakika mwana wa Abi Quhafa ameuvaa). Na ameuvaa: yaani ameufanya kama kanzu naye ameingia humo.
 • 3. Yaani nilivumilia katika giza kwa uchungu kama avumiliavyo mgonjwa wa macho.
 • 4. . Naiona mirathi yangu imepokonywa, ametumia kinaya ukhalifa kuwa ni mirathi, nayo ni mali inayo milikiwa.
 • 5. Msingi wa Shuraa ni kutaka ushauri. Na kisa hiki kwa sura ya jumla ni kwamba: Umar bin Al’Khatab ulipotimia muda wake wa kuiaga dunia, aliwataka ushauri waliokuwa karibu naye kuhusu ni nani amtawaze ukhalifa baada yake! Alishauriwa amtawaze mwanawe Abdullah, akasema:
  Hawatotawalia – yaani ukhalifa - wawili katika wana wa al’Khatab, yamtosha Umari aliy- oyabeba. Halafu aliona kuwa aliwakilishe jambo hili kwa watu sita, alisema: (hakika Mtume s.a.w.w. alikufa akiwa radhi nao, na juu yao baada ya mashauriano wamuainishe mmoja miongoni mwao asimamie jambo la Waislam), na watu sita wa Shuura nao ni: Ali bin Abi Talib, Uthman bin Affan, Talha bin Ubaidullah, Zubeir bin Awwam, Abdur-Rahman bin Auf na Sa’d bin Abi Waqqas.
  Saadu alikuwa mtoto wa Ami yake Abdur Rah'man wote wawili kutoka bani Zuh'ra, na naf- sini mwake kulikuwa na jambo dhidi ya Ali Karramal llahu Waj'hahu kwa upande wa wajomba zake, kwani mama yake ni Hamnatu binti Sufyani bin Umayyah bin Abdi'Shaamsi. Na Ali ni maarufu mashuhuri kwa kuwa uwa mashujaa wao wa kishiriki- na.Na Abdur Rah'man alikuwa shemejiye Oth'man, kwa kuwa mkewe alikuwa Ummu Kulthum bint Uq'bah bin Abi Muiyt alikuwa dada wa Oth'man bin Affan upande wa mama yake.
  Na Tal'ha alikuwa aelemea sana upande wa Oth'man kwa sababu ya mawasiliano yao mema, kulingana na yaliotajwa na baadhi ya wasimulizi wa mambo ya kale. Kwa hiyo kuelemea kwake kwa Oth'man kunatosha kumtupilia mbali Ali, kwani yeye pia ni katika Bani Taymi. Na kati ya Bani Hashim na Bani Taymi kulikuwa na ghadhabu kwa sababu ya ukhalifa wa Abubakar.
  Na baada ya kifo cha Omar bin Khattab walikusanyika na kushauriana. Walitofautiana, Talha katika rai yake aliungana na Oth'man, na Zubair akawa upande wa Ali na Saad upande wa Abdur Rah'man.
  Inaendelea uk. 19
  Na Omar bin Khattab ali usia kuwa muda wa Shuraa usiwe mrefu zaidi ya siku tatu, na kwamba isifike siku ya nne illa tayari wawe na amiri, na alisema Omar: "Ikitokea tofauti munapaswa muwe upande ule wa kundi la Abdur Rah'man." Abdur rah'man Alimkabili Ali na kumwambia : "Ni juu yako ahadi ya Mungu na makubaliano yake utafanya kulingana na Kitabu cha Mungu na Sunnah ya Mtume na makhalifa wawili waliokuwa baada yake" Ali alisema: "Nataraji nifanye kulingana Kitabu, sunna na upeo wa ilimu yangu na uwezo wangu. Kisha alimwita Uthman na akamwambia mfano wa aliyomwambia Ali. (Yeye) Alimwitikia kwa: Naam, kisha Abdur'rah'man aliinua kichwa chake kuielekea dari ya msik- iti - mahali ambapo Shuraa ilikuwa inafanyika - na akasema: (Ewe Mungu Wangu sikia na shuhudia, hakika mimi nimejaalia lililokuwa shingoni mwangu katika shingo ya Uthman) alipiga mkono wake kwenye mkono wa Uthman na akasema: (As-salaam alayka yaa Amiral-Mu'minin) na akamfanyia bai'a.
  Wakasema: (Akatoka Imam Ali bin Abi Talib hali amekasirika) Mikdadi bin Al'Aswad akamwambia Abdur'rah'man: (Wallahi umemwacha Ali naye ni miongoni mwa ambao wanahukumu kwa haki na wanafanya uadilifu katika hukumu) akasema: (Ewe Mikdadi kwa kweli nimefuatilia kwa juhudi zangu kwa ajili ya waislamu) Mikdadi akasema: (Wallahi kwa kweli mimi nawashangaa maquraishi kuwa wao wamemuacha mtu ambaye, sisemi wala simjui kuwa kuna mtu anahukumu kwa haki wala mjuzi zaidi kuliko yeye) Abdur'rah'man akasema: (Ewe Mikdadi, mimi nahofia fitna, kwa hiyo mche Mungu).

  Kisha yalipotokea katika utawala wa Uthman, yaliyotokea kupatikana kwa matukio toka kwa watu wa karibu yake, wakiwa magavanaa wa mikoa, masahaba wakubwa wakubwa walimchukia. Imeelezwa kuwa yeye alimwambia Abdur'rah'man: (Haya ni matendo ya mkono wako) Akasema: (sikuwa namdhania huyu kuyafanya haya, Lakini namuapa Mungu sitosema naye abadan). Kisha Abdur'rah'mani alifariki akiwa haongei na Uthman, mpaka yasemekana: (kuwa Uthman aliingia kwa Abdur'rah'man wakati yu mgonjwa akimzuru, akageukia ukutani bila kusema naye) Mungu ndiye ajuaye, na hukumu ni ya Mungu, anafanya atakayo. Mwisho wa Tanbihi 31

 • 6. Mtu miongoni mwao hapa anamkusudia Talha.
 • 7. Mwingine alielemea kwa shemeji yake anamkusudia Abdur-Rahman ambaye alielemea kwa Uthmani; kwa sababu Ummu Kulthum bint Ukbah bin Abii Mu’iti alikuwa mke wake Abdur-Rahman. Na huyu Ummu-Kulthumu ni dada wa Uthmani upande wa mama yake Urwa binti Kuraizi.
 • 8. An-Nakithu: Watu wa ngamia, na al-Mariqatu: Watu wa Nahrawan, na al-Qasituna: Wadhalimu, watu wa Siffin, na Maraqat: Kharajat, na katika maana ya kidini: Fasaqat.