read

4. Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Hotuba hii ameitoa baada ya kuuliwa Talha na Zubair ili kuwaongoza watu na (kuwabainishia) ukamilifu wa yakini ya ustahiki wa uongozi wake:-

“Kupitia sisi mumeongoka kutoka gizani1 na mumepanda daraja ya juu. Na kupitia sisi mumepambazukiwa na alfajiri mkiwa mbali na giza la usiku.

Asiyenisikia, basi lizibe sikio lisilosikia mawaidha. Vipi ataisikia sauti dhaifu na aizingatie aliyefanywa kiziwi (hakuweza kusikia) na ukelele wa sauti kubwa? (Atasikia sauti yangu dhaifu?). Uimarike moyo ulioendelea kumwogopa Allah.

Siku zote nilikuwa natazamia kutoka kwenu usaliti, na nimekuoneni ndani ya pambo la walioghurika, pazia ya dini imewaficheni mbali na mimi. Lakini nia yangu ya kweli imenionesha mlivyo. Nilizisimamisha kwa ajili yenu njia za haki kati ya njia za upotovu, hali ikiwa mlikuwa mnakutana lakini hapakuwa na kiongozi, na mlichimba bila ya kupatikana maji.

Leo navifanya hivi vitu bubu2vyenye ubainifu viwasemesheni.

Hana rai mwenye kuwa kinyume na mimi. Sikuwa na shaka na haki toka nilipoonyeshwa! Musa (a.s) hakujihofia binafsi,3 bali alihofia ushindi wa majahili na zamu ya upotovu! Leo tumesimama njia panda kati ya haki na batili.4

Mwenye kuwa na hakika ya kupata maji hawezi kuhisi kiu.5

Maelezo: Maneno haya na mifano yamedondolewa kutoka KHUTBA ndefu iliyonasibishwa kwake (a.s), kaumu ya watu fulani imezidisha humo vitu, kilichowafanya wafanye hivyo ni utashi wa nafsi zao.

Matamshi hayo hayaafikiani na utaratibu wake (a.s) katika KHUTBA, wala ufasaha wa hayo hauendani na ufasaha wake. Wala hapana haja ya kutaja kwa kuwa ni mashuhuri.

Na sisi tutafafanua matamko haya, kwa kuwa ni maneno yake (a.s), hawi na shaka na hilo mwenye dhouqu na naqdu na kuwa na maarifa na mwenendo wa watoa khutba na wenye ufasaha katika khutba zao na risala zao. Na kwa sababu Ar-Radhiyy (r.a) ameidondoa na ameinasibisha kwake (a.s) na ameisahihisha na kuondoa yasiyo yake.

  • 1. Ama kukhusu usemi wake(a.s): (kupitia sisi mumeongoka katika giza): Akusudia giza la ujinga na kupanda kilele: mumepanda daraja. Na ibara hizi ni Istiara-methali.
  • 2. Vitu bubu alikusudia alama na ishara, kwani hizo japokuwa ni bubu kwa asiyeelewa, lakini ziko wazi kwa mwenye moyo wa uelewa (li man kaana lahu kalbu au alqas-sam’a wa huwa shahid) kwa ajili hiyo ameviita vyenye ubainifu ingawaje ni bubu na bubu ni mnyama
  • 3. Anafuata nyayo za Musa pale walipomzulia woga, na anabainisha ukweli wa mambo mbali na wanayoyadhania, hakujihofia nafsi yake, bali alihofia fitna kuingia kwa watu wenye akili timamu pindi walipotupa wachawi fimbo zao, hivyo hivyo mimi sijihofii maadui binafsi ambapo wamenitegea mitego, bali nahofia wasije wakadanganyika wenye akali timamu kwa utata wao, hivyo dola ya upotovu itakuwa na nguvu, neno la wajinga lisije likashinda.
  • 4. Yaani, leo haki na batili zimekuwa wazi na tumezijua sisi na ninyi.
  • 5. Anasema: Mkiniamini mtakuwa mbali na upotovu, na karibu na yakini, kama ambaye ana uhakika na maji katika chombo chake anavyokuwa mbali na kiu, kuliko asiyekuwa na uhakika.