read

6. Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Aliposhauriwa kuwa asimfuatilie Talha na Zubair wala - asijiandae kwa vita na wao, pia humo anabainisha sifa yake kuwa yeye (a.s) - hawezi kuhadaiwa, ndipo aliposema:

“Wallahi siwi kama fisi anayelala muda wote wa mdundo mpaka amfike anayemtafuta, na amhadae muwindaji wake.

Lakini mimi nitampiga aigeuziaye mgongo haki kwa msaada wa anayeikubali, na kwa msaada wa msikivu mtii nitampiga, nitampiga muasi mwenye shaka daima, mpaka nijiwe na siku yangu (ya mauti); Wallahi ningali nasukumwa mbali na haki yangu, imetwaliwa kinyume nami toka siku Mwenyezi Mungu (swt) alipomfisha Nabii wake (s.a.w.w.) mpaka siku hii ya leo.1

  • 1. Anasema; kwa kweli kutwaa ukhalifa na kujitenga nao dhidi yangu na kuuhodhi si jambo jipya lililotokea hivi sasa, bali lilianzia mara tu alipofishwa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.).