read

7. Miongoni Mwa Khutba Zake (Amani Imfikie)

Katika kuwalaumu wafuasi wa Shetani:

“Wamemfanya shetani kuwa ndio kiini cha mambo yao, na yeye amewafanya washirika wake.

Hivyo basi ametaga na kutotoa vifuani mwao,1 na ametambaa na kujiburuza mapajani mwao,2kwa hiyo aliangalia kwa macho yao, na alitamka kwa ndimi zao, hivyo basi aliwapotosha, na kuwapambia kauli ovu, na makosa mabaya ni kitendo cha ambaye shetani ameshirikiana naye katika mamlaka yake na akatamka ya batili ulimini mwake.”

  • 1. Ametaga na kutotoa: ni kinaya (metaphoric), inamaanisha kuchukua nafasi kwake vifuani mwao na kubaki kwake muda mrefu humo; kwa kuwa ndege hatagi isipokuwa ndani ya kiota chake. Na kutotoa kwa shetani ni ule utiaji wake wasiwasi.
  • 2. Kuburuzika mapajani mwao: yaani wao wameilea batili kama wazazi wawili wamleavyo mtoto mapajani, hiyo ni kuonyesha kiwango cha kuambatana kwake nao na kuchanganyika kwake pamoja nao na kuwa kama ambaye anaangalia kwa macho yao, na yuatamka kwa ndimi zao, yaani wawili wamekuwa kama mtu mmoja.