read

8. Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Kwayo anamkusudia Zubair katika hali ambayo ilibidi iwe hivyo:

“Anadhani kuwa amekula kiapo cha utii kwa mkono wake, wala hakula kiapo kwa moyo wake, kwa hiyo amekiri kula kiapo cha utii, na anadai yaliyojificha ndani ya dhamira yake, basi na alete hoja ya kuthibitisha hilo, kama sivyo yampasa aingie alikotoka.”1

  • 1. Katika usemi wa Imam: waidda’aa al’waliijah: Al’waliijah: ni jambo lililositiriwa lililofanywa kwa kufichwa. Na Bw. Zubair alikuwa akisema: “Nimefanya bai’a - kiapo cha utii”. Nimekula kiapo cha utii kwa mkono wangu si kwa moyo wangu, au pengine anadai kuwa alilishwa kiapo bila ya ridhaa yake, na pengine anadai kuwa alikula kiapo kwa kujionesha tu kuwa yu ala kiapo, lakini alikuwa hali kiapo halisi. Kwa mantiki hiyo akasema (a.s): Usemi huu ni kukiri Zubair kuwa alikula kiapo cha utii, na yu adai jambo jingine ambalo halina ushahidi, hivyo basi alete dalili ya kuthibitisha kubatilika kwa kiapo alichokula dhahiri, au arejee kwenye utii wake.