read

9. Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Miongoni mwa maneno yake (a.s) - Sheikh Al-Mufiid ameieleza hii ndani ya Kitabu chake (Al-Jamalu) kutoka kwa Al- Waaqidiy.

Maelezo yanayomhusu (a.s.) na maelezo ya mahasimu wake, na pengine husemwa kuwa: yanawahusu watu wa Vita vya Jamal (Ngamia): “Kwa kweli waliunguruma na kumulika,1 pamoja na mambo mawili haya ni woga. Sisi hatuungurumi mpaka tushambulie adui na hatutiririki mpaka tunyeshe.2

  • 1. Maneno yake sana yalikuwa ya methali. Kwa hiyo kuunguruma na kumulika hapa ni methali ya mtu anayetaka kumshambulia adui, huanza na kelele za vitisho, kabla hajasham- bulia ili kuingiza hofu moyoni.
  • 2. Sisi hatuungurumi mpaka tufanye: yaani hatumtishii adui ila baada ya kipigo, kwa sababu sisi tukishampiga adui tunamtishia mwingine kuwa atasibiwa na lililomsibu wa kwanza. Tukinyesha twatiririka, ama hao ambao wanasema: (tutafanya, tutafanya) wala sio wafanyaji, wao wako sawa na anayetiririka kabla ya mvua, na hivyo ni muhali haupo.