read

10. Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Miongoni mwa maneno yake (a.s)- Al wahihiy ameieleza hii ndani ya Kitabu chake (Al jamaalu).

Katika khutba hii huenda anamkusudia shetani wa kweli, na inawezekana awe anamkusudia Mu’awiya. Ikiwa anamkusudia Mu’awiya basi kauli yake: (qadjama’a ...) ni maneno yapitayo juu ya ukweli wake, na ikiwa anamkusudia Shetani huo utakuwa ni mlango wa istiara.

Au kinaya - mfano wa maneno, anawakusudia watu fulani wafanyao yanayofanana na yafanywayo na shetani:

“Angalia! Kwa hakika shetani amekusanya kundi lake, na amewaleta wapanda farasi wake na askari waendao kwa miguu. Nami nina busara yangu. Sijajidanganya wala sijadanganywa. Nitawajazia hodhi la maji ambalo mimi ndiye mfutaji wake, hawarudi baada ya kunywa wala hawatolirudia.”1

  • 1. Yaani hilo hodhi la maji ni mfano wa vita; hawarudi baada ya kunywa, yaani wakija kwenye mapambano hayo watakufa na hawatorudi walikotoka, na watakaonusurika na kifo hawatorudi tena kuchochea vita vingine.