read

11. Na Katika Maneno Yake (A.S)

Kwa mwanawe Muhammad ibnul-Hanafiyya alipokuwa akimpa bendera siku ya Jamal:

“Milima huenda ikaondoka na ikatoweka (mahali pake) wewe usiondoke! Uma meno yako.1 Mwazime Mungu fuvu lako la kichwa chako. Imarisha nyayo zako ardhini, mtazame adui wa mbali, fumba macho yako.2 (Yaani usiogope adui kwa kujali wingi wao na kutishika), jua kuwa ushindi ni kutoka mwa Mwenyezi Mungu swt.

  • 1. Kauli yake: Uma meno yako, yasemekana mwenye kuuma meno yake mshale hauathiri ubongo wake, kwa sababu mifupa ya kichwa hukomaa na kuwa migumu. Na kauli yake: Air’llaha jum jumataka maana yake litumie hilo katika utii wa Mungu.
  • 2. Tupa macho yako; yaani, zizunguke harakati zao zote, na yafumbie macho yale yanayokutisha kutokana nao, yaani lisikutishe la kutisha bali lifumbie macho.