read

12. Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Mwenyezi Mungu alipompa ushindi dhidi ya watu wa Jamal (Ngamia). Mmoja kati ya Sahaba wake alisema: “Natamani lau ndugu yangu fulani angekuwa yupo, ili aone ushindi Mungu aliokusaidia kuupata dhidi ya maadui zako.” Hapo akasema (a.s):

“Je, mwelemeo na upendo wa ndugu yako u pamoja nasi?” Akasema: “Ndiyo,” akasema (a.s): “Basi itakuwa kwamba alikuwa pamoja nasi katika kikosi cha askari wetu hawa, kwa hakika walikuwa wapo hata wale ambao bado wapo viunoni mwa wanaume na mifuko ya uzazi ya wanawake, punde tu wakati utawatoa, na kwa wao imani itakuwa na nguvu”.