read

13. Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Kuwalaumu watu wa Basra baada ya vita vya Jamal (Ngamia):

Mlikuwa askari wa mwanamke, na wafuasi wa mnyama;1 amepiga kelele mkamwitika, na akajeruhiwa mkakimbia. Tabia zenu ni mbaya na ahadi zenu ni khiyana na dini yenu ni unafiki, maji yenu ya chumvi.2 Mwenye kuishi kati yenu yuko rehani kwa dhambi zake, mwenye kuondoka kwenu atapata amani ya rehema kutoka kwa Mola wake Mlezi. Kama nauona msikiti wenu wafanana na sehemu ya mbele ya Safina (boti), Mungu ameipeleka adhabu kutoka juu na kutoka chini yake, na waliomo humo wamezama.”

Na katika riwaya nyingine: “Wallahi mji wenu utazama, kana kwamba nauona msikiti wenu ukiwa kama sehemu ya mbele ya boti au mbuni aliyeanguka kwa kifua chake.”

Na katika usemi wake mwingine: “Kama kifua cha ndege katika kilindi cha bahari.”

Na katika usemi wake mwingine: “Mji wenu ni miongoni mwa miji ya Mungu ambayo udongo wake unanuka sana, ukaribu mno na maji, na umbali mno na mbingu, na una sehemu tisa katika kumi ya maovu, aingiaye humo huzungukwa na dhambi zake na atokaye humo huneemeka na msamaha wa Mungu. Naona mji wenu kama kwamba umefunikwa na maji kiasi kwamba hakuna kinachoonekana isipokuwa sehemu ya juu ya msikiti, ukiwa kama kifua cha ndege katika kilindi cha bahari.”

  • 1. Atba’ul-bahima: Wafuasi wa mnyama, yaani ngamia, na ngamia wa Aisha alikuwa ni bendera ya kikosi cha Basra, waliuawa kwa ajili yake kama watu wanavyouliwa chini ya bendera yake.
  • 2. Maji yenu ya chumvi, waweza kuduwaa vipi washutumiwe maji kuwa ya chumvi hiyo si miongoni mwa sifa za matendo yao! Jibu: Hilo japo si katika matendo yao, ila ni mion- goni mwa lawama za mji. Kisha ameeleza mkazi wake ni mtu aliye rehani kwa dhambi yake, kwa kuwa yawezekana awe ashiriki nao katika dhambi au aiona dhambi yatendwa na hakanushi; Na madh’habu ya sahiba zetu ni kuwa haijuzu kuishi katika nchi ya kifasiqi, kama ambavyo haijuzu kuishi katika nchi ya kikafiri.