read

14. Na Miongoni Mwa Usemi Wake (A.S)

Katika mfano kama huo:

Ardhi yenu ipo karibu na maji. Iko mbali na mbingu.1 Akili zenu ziko nyepesi, pia zimejaa upuuzi. Kwa hiyo ninyi ni kilengwa cha mtupa mshale, na cha mlaji, na ni windo la mwindaji.

  • 1. Karibu na maji: Yaani karibu na kuzama kwa maji na iko mbali na mbingu; kwa kuwa watu wa ilmu ya anga na wajishughulishao na sayari wanaeleza: (kuwa sehemu iliyo mbali zaidi na mbingu ardhini ni Ubla nayo ni sehemu karibu na Basra; na hilo linaafikiana na kauli yake (a.s). Na Basra ni mkoa katika nchi ya Iraqi na ndio mkoa wenye bandari.