read

15. Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Kuhusiana na ardhi alizozirudisha kwa Waislamu kutoka Qata’iu za Uthman:1

“Wallahi hata ningezikuta (mali) zimetumika zikiwa mahari kwa kuolea wake, na vijakazi wamemilikiwa kwazo, ningezirudisha, kwa sababu kuwa katika uadilifu kuna wasaa.

Na ambaye umemuwia dhiki uadilifu, udhalimu kwake utakuwa dhiki mno.2

  • 1. Qata'iu: Ni mali huikata Imam kuwapa baadhi ya raia kutoka ardhi ya Baitul'mali yenye kodi na huondoa kodi yake kisha anaifanya ilipiwe kiasi kidogo badala ya kodi. Na Uthman Affan aliwakatia ardhi nyingi Bani Umayah na watu wengine katika wapenzi wake na sahibu zake. Mfano wa kipande cha ardhi alichompa Mu’awiyah na Marwan. Na ilikuwa kwa kawaida mavuno yake hupewa wasafiri, na walio mfano wake.
  • 2. Yaani ambaye atashindwa kupanga mambo yake kwa uadilifu hivyo yeye kuyapanga kwa udhalimu ni mwenye kushindwa zaidi, kwa sababu katika udhalimu kunadhaniwa kukabiliwa na upinzani na kuzuiwa. Na hotuba hii imeelezwa na al-Kalbiy yenyewe ni riwaya mar’fu’u - iliyorushiwa - kwa Abi Swaleh kutoka kwa ibn Abbas: Kuwa Ali alihutubia siku ya pili baada ya Ba’ia yake huko Madina; alisema: ‘Alaa kila kipande alichokikata Uthman na kila mali ambayo amempa mtu kutoka kwenye mali ya Mungu itarejeshwa Ba’itul-Mal, kwa sababu haki ya zamani haibatilishwi na kitu, japo ningeikuta imetumika kwa kuolea...’