read

17. Miongoni Mwa Semi Wake (A.S.)

Maelezo kuhusu wanaotoa hukumu kati ya watu hali wakiwa hawastahiki: Pia katika usemi huo amewaainisha viumbe wenye kuchukiza mno kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) wa aina mbili.

Aina ya kwanza: “Kwa kweli viumbe wenye kuchukiza sana mbele ya Mwenyezi Mungu ni watu (aina) wawili: Mtu ambaye Mungu (s.w.t) amemtelekeza yeye na nafsi yake. Huyu amepotoka mbali na njia ya kweli, 1anapenda sana kusema maneno ya bida’a na kuwaitia kwenye upotovu, kwa hiyo huyu ni fitna kwa wenye kudanganyika naye. Amepotea mbali na mwongozo wa waliokuwa wa kabla yake. Mwenye kuwapotosha wamfuatao maishani mwake na baada ya kufa kwake, mwenye kubeba makosa ya wengine, amekuwa rehani wa makosa yake.

Aina ya pili: “Mtu aliyekusanya ujinga, yu aharakisha kati ya umma wak- ijahili kuwaghushi na kuwadanganya. Haraka haraka afaidika na giza la fitna. Haoni faida iliyo katika utulivu. Walio mfano wa watu wamemwita mjuzi wala hayuko hivyo. Amefanya juhudi mapema asubuhi, na amekithirisha kukusanya vitu ambavyo uchache wake ni bora kuliko wingi wake, mpaka aondoapo kiu kwa maji machafu, na kukithirisha yasiyokuwa na maana, akaketi kati ya watu kama hakimu akichukua jukumu la kutatua yaliyowatatiza watu wengine, na endapo atafikwa na suala lenye maana isiyo dhahiri; ataliongelea kwa maneno mengi yasiyo kuwa na maana na kwa rai yake chakavu, kisha atalitolea maamuzi, kwa hiyo yeye katika kupanga mambo yenye utata ni kama utando wa buibui, hatambui amefanya sawa au amekosea; akifanya sawa yuahofia huenda amekosea, na akikosea huwa na matumaini ya kuwa amefanya sawa. Yu mjinga, anatangatanga bila ya mwongozo, haoni vizuri, mwenye kuyazamia mambo bila ya mwongozo.

Hakuishika ilimu kwa jino lenye makali. Riwaya anazipeperusha kama upepo upeperushavyo majani makavu.2

Wallahi hawezi kuyatatua vyema matatizo yaliyoletwa kwake, wala hafai kwa jukumu alilopewa.

Hajali kutojuwa asiyoyajuwa. Hatambui kuwa asilolijua yeye kuna ambao wanalijua. Na jambo lisipokuwa wazi kwake hulificha, kwa kuwa anajua kuwa mwenyewe ni mjinga. Damu zapiga kelele kutokana na hukumu zake zisizo za uadilifu, na mali zilizorithishwa vibaya zinamnung’unikia.

Ninalalamika kwa Mungu (s.w.t) kuwahusu watu wanaoishi ujingani na wanakufa katika hali ya upotovu, kwao wao hakuna kisicho na thamani zaidi kuliko Kitabu (Qur’ani) endapo kitasomwa ipasavyo,3 na wala hapana biashara yenye thamani zaidi kwa mauzo kuliko Kitabu (Qur’ani) endapo kitapotoshwa mbali na maeneo yake.

Wala hapana kiovu zaidi kwao kuliko mema, na hapana mema zaidi kuliko maovu!”

  • 1. Al-Jai’ru: Mwenye kupotoka mbali na njia, na hiyo ni kinaya cha kwenda kwake nyuma ya nafsi yake katika itikadi yake, harejei kwenye ukweli wa dini, wala haongoki kwa dalili kutoka kitabuni, huyu ndiye aliyepotoka mbali na njia ya sawa, na amekwenda kombo.
  • 2. Na katika riwaya nyingine: yadh’ruu riwayati kamaa tadhru riihul’hashiima, nayo ndiyo fasaha, Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesema: (Fa asbah hashiiman tadhruuhur- riyaahu): - (mimea) ikawa vibua vinavyo peperushwa na upepo; 18:45). Hivyo basi, kama ulivyo upepo haujali katika kubeba majani makavu na kuyaparaganya, haujali kwa kuy- achanachana na kutawanyika mpango wake, vivyo hivyo kwa huyu jahili huzifanyia riwaya kama upepo ufanyavyo kwa majani makavu.
  • 3. Tuliya haqa tilawatihi: Ikisomwa ipasavyo; yaani ikichukuliwa kama inavyobidi na kama jumla zake zinavyojulisha, na ikafahamika kama alivyokuwa anaifahamu Nabii (s.a.w.w.) na masahaba zake walivyokuwa wanaifahamu.