read

18. Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Katika kulaumu tofauti za wanachuoni kwenye utoaji fatwa:
“Lamfikia mmojawao suala kuhusu hukumu mojawapo miongoni mwa hukumu, yeye analitolea hukumu kwa rai yake, kisha lamfikia tatizo lile lile mwanachuoni mwingine, yeye naye hulitolea hukumu tofauti na yule wa kwanza, kisha huwa makadhi au mahakimu wanakusanyika kwa

Khalifa aliyewatawaza ukadhi na hukumu zile, naye anazipitisha kuwa ziko sahihi rai zao zote, hali Mungu wao ni mmoja! Nabii wao ni mmoja! na Kitabu chao ni kimoja! Je Mungu (s.w.t) aliwaamuru watofautiane na wao wakamtii!? Au aliwakataza kutofautiana wakamuasi! Au Mungu (s.w.t) aliteremsha dini yenye upungufu akaomba msaada kwao ili kuikamilisha!? Au walikuwa washirika Wake, kwa hiyo wao waseme watakalo na Yeye (s.w.t) apaswe kuridhika!?

Au Mungu (s.w.t) aliteremsha dini iliyo kamili na Mtume (s.a.w.w.) alizembea kuifikisha na kuitekeleza!, hali Mungu (s.w.t) anasema: “Hatujapuuza kitabuni kitu chochote” (6:38) “Ndani yake muna ubainifu wa kila kitu” na amesema kuwa Kitabu baadhi yake kinaisadikisha baadhi nyingine na yakuwa hakuna hitilafu humo kama alivyosema (s.w.t): “Lau ingekuwa imetoka kwa asiye Mwenyezi Mungu, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi”. (An-Nisaa:82). Na yakuwa Qur’ani dhahiri yake nzuri yastaajabisha na sehemu yake ya ndani imekwenda kwa kina sana. Maajabu yake hayaishi wala mageni yake hayamaliziki wala mafum- bo yake hayatofumbuliwa isipokuwa kwayo.