read

20. Katika Usemi Wake (A.S.)

Katika kukhofisha juu ya hali ya mambo itakavyokuwa baada ya mauti:
“Kwa hakika ninyi lau mungeyaona waliyoyaona waliokufa katika ninyi, mngefadhaishwa na kutishika, na mngesikiliza na kutii. Lakini yamefichika kwenu yale waliyoyaona, hivi punde pazia litaondolewa.1

Mmeoneshwa isipokuwa kama hamkuona, na mmesikilizishwa, isipokuwa kama hamkusikia, na mumeongozwa isipokuwa kama hamkuongoka. Kwa haki nakuambieni mazingatio yamekudhihirikieni, na mumeonywa na ambayo (mtu) anaweza kuonyeka. Baada ya wajumbe wa mbingu (malaika) ni mwanadamu tu ndiye awezaye kufikisha ujumbe kutoka kwa Mungu.2

  • 1. Hivi punde pazia litaondolewa, na hilo litakuwa mwisho wa umri, na mtu kufika nyumba ya kwanza miongoni mwa nyumba za akhera, na maneno haya yanajulisha usahihi wa kauli ya adhabu ya kaburi.
  • 2. Wajumbe wa mbinguni: Malaika, yaani endapo mutasema hakijatujia kitu kutoka kwa Mungu; jibu ni, hoja imesimamishwa dhidi yenu kwa tablighi ya Mtume wa Mungu na mwongozo wa khalifa wake. Yashabihiana na kauli yake (a.s.): “Lau mungeyaona bayana waliyoyaona waliokufa kabla yenu.” Na kauli ya Abu Haazim akimwambia Sulaiman bin Abdil’Maliki katika maneno aliyokuwa anamuwaidhi nayo: “Kwa hakika baba zako wamelifanya suala hili ovyo ovyo bila ya ushauri, kisha wamekufa, lau ungejua waliyosema na waliyoambiwa!” Imeelezwa kuwa: “Alilia mpaka alianguka.”