read

21. Na Katika Jumla Ya Semi Zake (A.S.)

Ili kuwawaidhi watu:-

“Kwa kweli lengo liko mbele yenu.1 Na kwa kweli nyuma yenu kuna (saa) kiyama kinakupelekeni munakoelekea. Jifanyeni wepesi mutawakuta,2 bali tu, wa kwanza wenu wanawangoja wa mwisho wenu.”3

Maelezo: Sharif Ar-Radii (r.a) alisema: “Nasema kwa kweli maneno haya ya Ali lau yangewekwa kwenye mizani upande mmoja na maneno mengine upande mwingine mbali na maneno ya Mungu na maneno ya Mtume wake Mizani ingekuja chini kwa uzito wa maneno ya Ali, na yangethibiti kuwa na ushindi katika nyanja zote. Na usemi wake: “Takhaffafu tal’haqu” Kuweni wepesi mtashinda’ ni ibara fupi sana kupata kusikika iliyo na maana kubwa mno! Ina maana pana iliyoje! Bubujiko la hikima. Tumeishiria ukubwa wa maana yake katika Kitabu “Al-Khasa’is.”

  • 1. Lengo la mukalafiina: Imma ni matokeo ya malipo mema, au adhabu, kwa hiyo inawezekana iwe alikusudia hilo, na inawezekana iwe alikusudia kwa neno lengo - umauti, ila tu amejaalia hilo mbele yetu; kwa sababu mwanadamu ni kama mwenye kwenda kuuelekea umauti, au anakwenda kuyaelekea malipo, hivyo basi hayo mawili yako mbele yake.
  • 2. Takhaffafu talhaqu: Asili yake, mtu anakwenda mbio naye hana uzito wa akibebacho, anastahili kuwakuta waliomtangulia, na wametangulia waliotangulia na matendo yao kwenye wema, basi mwenye kutaka kuwakuta ni juu yake ajifanye mwepesi mbali na uzito wa matamanio, na mzigo wa taabu katika kuzipata ladha, na akimbie binafsi mbali na haya yanayoisha, hivyo basi atawakuta ambao waliofuzu kwa nyumba ya baadae.
  • 3. Yaani waliotangulia kufa hawatofufuka, watafanywa wangojee mpaka watakapofika waliobaki hai, wote na iishe duru ya mwanadamu hapa duniani. Wala hatobaki juu ya uso ya ardhi yeyote, hapo ndio sasa itakuwa imewadia, nayo ndio siku watafufuka.